Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Nakala Ya Mtandao (Online Document) NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Nne - Tarehe 31 Januari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) Spika (Mhe.Job Y. Ndugai) Alikalia Kiti D U A Spika (Mhe.Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Nane, Kikao cha leo ni Kikao cha Nne. Katibu! NDG. LAWRENCE MAKIGI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MHE. MIRAJI J. MTATURU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2019. SPIKA: Ahsante sana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Wenyeviti mnaowasilisha muwe mnakuwa karibu ili tuokoe muda na anayefuata awe karibu pia. Karibu sana Mwenyekiti kwa niaba ya! MHE. JULIUS K. LAIZER (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kanati kwa mwaka 2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Kalanga. Katibu! 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NDG.LAWRENCE MAKIGI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Mhehsimiwa Waziri Mkuu, swali la kwanza litauliza na Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa, Senator, Mbunge wa Sumve Na. 37 Ujenzi wa Kiwanda cha Pamba-Kwimba MHE. RICHARD M. NDASSA aliuliza:- Kupitia Mifuko ya Jamii tayari tathmini ya kukijenga Kiwanda cha kuchambua pamba Nyambiti Ginnery kilichopo Kwimba umeshafanyika, kilichobaki ni uamuzi wa Serikali kuliongezea thamani zao la pamba. Je, ni lini Kiwanda hicho kitaanza kujengwa? SPIKA: Ahsante majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Wziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Anthony Mavunde tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri napenda kujibu swali la Mheshimiwa Richard Mganga Ndasa Mbunge wa Sumve kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini inayoundwa na Mifuko ya NSSF, PSSSF, NHIF, WCF na ZSSF imekamilisha mapitio mapya ya upembuzi yakinifu ya ufufuaji wa vinu vya kuchambulia pamba vya Ngasamo, Nyambiti na Kasamwa vilivyoko Mkoani Simiyu, Mwanza na Geita baada ya takwimu za uzalishaji wa kilimo cha pamba kuongezeka hususan katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa. Mheshimiwa Spika, kwa sasa Mifuko inakamilisha taratibu muhimu zinazohusiana na Miongozo ya Uwekezaji kwa kushirikiana na Vyama vya Ushirika vya Mwanza, Simiyu na Geita ili kuwezesha uwekezaji wenye ufanisi na tija taratibu zitakapokamilika. Mheshimiwa Spika, Utaratibu maalum wa namna ya kuwezesha ufufuaji wa viwanda hivyo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi Februari, 2020. SPIKA: Mhehsimiwa Ndassa. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba uniruhuru niipongeze sana Serikali kwa hatua ambayo sasa imefikia kwa sababu kilio kikubwa kwa wakulima wapamba ni kwamba pamba hiyo inatakiwa iongezewe thamani. Sasa swali langu nimesema kwamba upembuzi tayari umeshakamilisha na viongozi wakuu wa mifuko hii wako Mwanza nasikia, sasa ni lini sasa baada ya hiyo Februari kwa sababu majibu haya yanaweza kusema kwamba ni Februari kumbe ni mwezi mwingine, ni lini sasa hasa ujenzi wa vinu hivi vitatu kwa maana ya hii Nyambiti Ginnery, Ngasamo Ginnery pamoja Kasamwa Ginnery. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Lini vitaanza kujengwa ili zao la pamba lipate thamani zaidi? Nakushuru. SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri tafadhali, ni lini. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, niruhusu kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anawapigania wakulima wa pamba wa Kanda ya Ziwa na amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba zao hili linaongezwa thamani. Kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema leo wakurugenzi wote wa uwekezaji wa mifuko hii wako Mwanza na kesho kuna kikao cha Wakurugenzi Wakuu ambao kupitia kikao hicho tutapata way forward ya lini taratibu hizi zitaanza kwa sababu kesho wanakutaka kwa ajili ya mambo ya kitaalam, hivyo nimuombe Mheshimiwa Ndasa awe mvumilivu tusubiri taarifa ya Wakurugenzi Wakuu kesho ili tujue way forward ni nini. Nashukuru. SPIKA: Ahsante sana, tunaendelea wengine hamtoki kwenye pamba, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Sixtus Raphael Mapunda Mbinga Mjini Mariam ndiyo kwa niaba haya endelea. Na. 38 Kuboresha Huduma za Afya – Hospitali ya Mbinga MHE. MARIAM N. KISANGI (K.n.y. MHE. SIXTUS R. MAPUNDA) aliuliza:- Tangu mwaka 2016, Serikali iliahidi kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga ikiwa ni pamoja na kujenga wodi ya watoto, chumba cha upasuaji na gari la wagonjwa:- Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hizo. SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sixtus Raphael Mapunda, Mbunge wa Mbinga Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga ambapo kupitia mapato yake ya ndani Halmashauri ya Mji Mbinga imefanya ukarabati wa jengo la „Grade A‟ kwa gharama ya Shilingi milioni 45 na kununua jokofu la kuhifadhia maiti lenye thamani ya Shilingi milioni 29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetoa kiasi cha Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kalembo ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga, ahsante. SPIKA: Mheshimiwa Mariam Kisangi nilikuona. 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri, kwa kuwa Wilaya ya Mbinga ni Walaya ambao iko pembezoni sana na wananchi wake wnachangamoto nyingi sana pamoja na majibu mazuri bado kuna tatizo kubwa la kuwa gari la wagonjwa katika hospitali hiyo. Je, Serikali ina mkakati saa wa kuhakikisha wanawapelekea gari la wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga? Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa matatizo ya hospitali haya yanaendana kabisa na hali ya hospitali Zakiemu Mbagala. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongezea hospitali ya Zakiem Mbagala ambayo imezidiwa wagonjwa ni wengi lakini majengo ni machache na wahudumu ni wachache, nakushukuru. SPIKA: Majibu ya maswali hayo kwa kifupi Mheshimwia Naibu Waziri TAMISEMI tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kusimamia Mkoa wa Dar es Salama, pia ni Tanzania kwa ujumla wake hususan jambo la afya ya akinamama na watoto na wazee. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba unapokua unajenga kuboresha huduma za afya ni muhimu kuwa na gari la wagonjwa ili inapokea dharura iwe ni rahisi kumuwaisha katika huduma nyingine ya ziara ya pale alipokuwa, lakini naomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba kadri kwa uwezo wa Serikali uwezo ukipatikana basi eneo hilo la Mheshimiwa Raphaeri Mapunda litapata gari la wagonjwa kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameulizia hapa. Mheshimiwa Spika, naomba niseme tu kwamba mpango wa Serikali ni kuboresha huduma zaafya na kupeleka hufuma karibu na wananchi, tumepokea hoja Mheshimiwa Mbunge bahati nzuri tunaenda kwenye mwaka wa bajeti 2020/2021 basi tuangalie uwezekano wa kupatikana ili tuweze kupeleka fedha katika eneo hili kuboresha huduma ya pale Mbagala pia Mkoa wa Dar es Salam kwa ujumla wake. Na natambua kwamba wnanchi wangu wa Jimbo la Ukonga pia wanaweza wakapata huduma pale Mbagala Zakiemu, ahsante sana. SPIKA: Ahsante nilikuwa mnadhimu wa upinzani Bungeni uliza swali lako. MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza, wnanchi wa Jimbo la Bunda Mjini na Wilaya ya Bunda kwa ujumla walikubaliana kwamba hospitali ya Manyamanyama iwe hospitali ya Wilaya. Lakini kuna baadhi ya mambo ambayo hospitali hiyo haina pamoja jokofu la kuhifazia maiti. Wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini wanapata tabu kupeleka maiti Nyamswa Jimbo la Bunda. Sasa ningependa kujua ni lini Serikali itapeleka jokofu katika hospitali ya Manyamanyama? SPIKA: Ahsante sana swlai kutoka Mkoa wa Mara hilo, kuna baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Mara siwaoni oni hapa na sina taarifa zao kwa mfano Mheshimiwa Heche simuoni kabisa hapa sijui yuko wapi, Mheshimiwa Naibu jibu swali hilo la Manyamanyama. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli maneno yako yako ya utangulizi yanafaa sana ndiyo 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) maana tufanye mabadiliko makubwa katika eneo hili ikiwa na Wabunge wanaopatikana wakatI wote Bungeni kusemea watu wao kama Mheshimiwa Ester Bulaya. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwanza Bunge imepata Kituo cha Afya ni suala la kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli tumepata hospitali pale inajenga katika eneo hili lengo ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hii. Mheshimiwa sema Mheshimiwa hoja yako imepokelewa tuangalie uwezo wa Serikali tupeleke jokofu katika eneo hili ili maiti ikipatikana pale basi iweze kuhifadhimiwa eneo la karibu na kupunguza gharama zausafirishaji wa ndugu wa marehemu, ahsante sana. SPIKA: Ahsante sana kwa
Recommended publications
  • Hotuba Ya Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Katika Ufunguzi Wa Mkuta
    HOTUBA YA MGENI RASMI MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB) WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MWAKA WA WADAU WA LISHE, SEPTEMBA 10, 2019 Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Suleiman Jafo (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Mheshimiwa Prof. Joyce Ndalichako (Mb), Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango. Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (Mb), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Mheshimiwa Doto Biteko (Mb), Waziri wa Madini, Waheshimiwa Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge; pamoja na viongozi wengine wa ngazi za Mkoa na Halmashauri mliopo, Waheshimiwa Wabunge na viongozi wa Vyama vya Siasa, Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali, Ndugu Viongozi waandamizi wa Idara, Taasisi, Wakala za Serikali, Wakuu wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Wadau wa Maendeleo na Asasi za Kiraia, 1 Ndugu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Ndugu Wageni Waalikwa, Waandishi wa habari na wadau wote wa Lishe, Mabibi na Mabwana. Habari za asubuhi Kwa mara nyingine tena nina furaha kubwa sana kujumuika na wadau wa lishe siku hii ya leo. Hii ni mara yangu ya tatu kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wadau wa lishe nchini na hivyo nahisi kuwa mwanafamilia wa wadau waliohamasika katika masuala ya lishe.
    [Show full text]
  • Madini News Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Toleo Na.2 Wa Tanzania Machi, 2020 HALIUZWI
    Toleo Na.2 // Machi 2020 Yaliyomo // Biteko - Nitasimama na Mzee Tume ya Leseni ya TanzaniteOne Imefutwa na Kisangani mpaka “asimame” Kurudishwa Serikalini - Biteko... Uk.04 ... Uk.08 Madini Bilioni 66.5 zapatikana tangu Wanawake Tume ya Madini kuanzishwa kwa masoko Wawakumbuka ya madini ... Uk.10 Yatima ... Uk.18 www.tumemadini.go.tz Tume ya Madini 2020 www.tumemadini.go.tz /TAHARIRI Salamu Kutoka kwa Waziri wa Madini Maoni ya Mhariri SEKTA YA MADINI INAIMARIKA, MAFANIKIO MASOKO TUENDELEZE USHIRIKIANO YA MADINI TUMEWEZA! Katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Wizara ya Madini ilipanga kutekeleza majukumu yake kupitia miradi Katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mbalimbali ikilenga katika kuimarisha Sekta ya Madini, hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa, Serikali kupitia uchumi wa nchi. Tume ya Madini kuanzia Machi, 2019 ilifungua masoko ya madini Katika Toleo lililopita nilielezea kwa kifupi kuhusu yale ambayo yamesimamiwa na kutekelezwa na Wizara na vituo vya ununuzi wa madini lengo likiwa ni kudhibiti utorosh- kwa kipindi cha takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. waji wa madini kwa kuwapatia wachimbaji wa madini nchini Katika Toleo hili nitaelezea kwa kifupi mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha sehemu ya kuuzia madini yao huku wakilipa kodi mbalimbali kuanzia Julai, 2019 hadi Februari, 2020. Kama ambavyo nilieleza Bungeni katika Hotuba yangu wakati Serikalini. nikiwasilisha Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2019/2020, nilieleza kuwa, Wizara imepangiwa kukusanya Shilingi 470,897,011,000.00 katika Mwaka wa Fedha 2019/2020. Uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa Napenda kuwataarifu wasomaji wa Jarida hili kuwa, hadi kufikia Februari, 2020 jumla ya Shilingi madini ni sehemu ya maelekezo yaliyotolewa kwenye mkutano wa 319,025,339,704.73 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la makusanyo ya nusu mwaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Dkt.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Sita – Tarehe 9 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Sita – Tarehe 9 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2019/2020. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka ulioisha tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual Report and Audited Accounts of Mzumbe University for the year ended 30th June, 2017). MWENYEKITI: Katibu! NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza leo linaelekezwa Ofisi ya Waziri Mkuu na linaulizwa na Mheshimiwa Dkt. Raphael Masunga Chegeni, Mbunge wa Busega. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo hapa kwa niaba. MWENYEKITI: Wewe unatoka Busega? MHE. RASHID A. SHANGAZI: Hapana, ila hili ni la kitaifa. MWENYEKITI: Aaa, sawa, kwa niaba. Na. 43 Kauli Mbiu ya Kuvutia Wawekezaji Nchini MHE. RASHID A. SHANGAZI (K.n.y. MHE. DKT.
    [Show full text]
  • Ofisi Ya Rais, Menejimenti Ya Utumishi Wa Umma Na Utawala Bora Kwa Mwaka Wa Fedha Wa 2019/20
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI – OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA. KAPT (MST) GEORGE H. MKUCHIKA (Mb.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20 APRILI, 2019 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyochambua bajeti ya Ofisi ya Rais, Ikulu (Fungu 20 na 30), Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Fungu 33), Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Fungu 32), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (Fungu 67), Tume ya Utumishi wa Umma (Fungu 94), Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (Fungu 09), na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (Fungu 04). Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Mpango wa Utekelezaji na Makadirio ya Fedha kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/20. 2. Mheshimiwa Spika, Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia uwezo wa kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi. Pia namshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kuendelea kuniamini katika nafasi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Ninamuahidi kuwa nitatekeleza wajibu wangu kwa ufanisi na uadilifu wa hali ya juu. Aidha, nawashukuru wapiga kura wa Jimbo la Newala Mjini kwa ujumla kwa kuendelea kunipa ushirikiano wakati wote ninapoe ndelea kuwawakilisha.
    [Show full text]
  • Tarehe 30 Juni, 2017
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Saba – Tarehe 30 Juni, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Saba, leo ni Kikao cha Hamsini na Saba. Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Mheshimiwa Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Swali la kwanza linaulizwa na Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki. Mheshimiwa Nyongo. Na. 468 Mikopo kwa Walimu Kwa Ajili ya Ujenzi wa Nyumba MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza:- Walimu Wilayani Maswa wana uhaba wa nyumba za kuishi; pamoja na juhudi za wananchi kujenga nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari lakini walimu hao bado wanahitaji kujenga nyumba zao wenyewe za kudumu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni lini Serikali itaweka utaratibu maalum wa kutoa mikopo kwa walimu hao ili wajenge nyumba zao binafsi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina uhitaji wa nyumba za walimu 1,358. Nyumba zilizopo ni 479 na hivyo upungufu ni nyumba 879. Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu huu Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina mpango wa kujenga nyumba 16 katika mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, kati ya nyumba hizo, nyumba nane zitajengwa kwa bajeti ya 2017/2018 (CDG) na nyumba nyingine nane zitajengwa kwa kutumia mapato ya ndani y (own source) ya Halmashauri.
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania Mkutano Wa Tatu Yatokanayo Na Kikao Cha Arobaini Na Saba 21 Juni, 2016
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA TATU YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA 21 JUNI, 2016 MKUTANO WA TATU - YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA TAREHE 21 JUNI, 2016 I. DUA: Saa 3.00 Asubuhi Naibu Spika (Mhe. Dkt.Tulia Ackson) alisoma Dua na Kuongoza Bunge. Makatibu Mezani: 1. Ndg. Theonest Ruhilabake 2. Ndg. Zainab Issa Wabunge wa Kambi ya Upinzani walitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya dua kusomwa na Mhe. Naibu Spika. II. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali:- OFISI YA WAZIRI MKUU: Swali Na.399 – Mhe. Raphael Masunga Chegeni [kny. Mhe. Salome Makamba] Swali la nyongeza: (i) Mhe. Raphael Masunga Chegeni (ii) Mhe. Abdallah Hamisi Ulega (iii) Mhe. Joseph Kasheku Musukuma (iv) Mhe. Mariam Nassoro Kisangi OFISI YA RAIS (TAMISEMI): Swali Na.400 Mhe. Oran Manase Njeza Swali la nyongeza: (i) Mhe. Oran Manase Njeza (ii) Mhe. Desderius John Mipata (iii) Mhe. Goodluck Asaph Mlinga Swali Na.401 – Mhe. Boniventura Destery Kiswaga Swali la nyongeza: (i) Mhe. Boniventura Destery Kiswaga (ii) Mhe. Augustino Manyanda Maselle (iii) Mhe. Richard Mganga Ndassa (iv) Mhe. Dkt. Dalali Peter Kafumu Swali Na. 402 – Mhe. Fredy Atupele Mwakibete Swali la Nyongeza: (i) Mhe. Fredy Atupele Mwakibete (ii) Mhe. Njalu Daudi Silanga (iii) Mhe. Halima Abdallah Bulembo (iv) Mhe. Azza Hilal Hamad 2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Swali Na.403 – Mhe Joseph Kakunda. kny Mhe. Ally Saleh Ally Swali la nyongeza: (i) Mhe. Joseph George Kakunda (ii) Mhe. Mussa Azzan Zungu (iii) Mhe. Cosato David Chumi (iv) Mhe.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ___Mkutano Wa Kumi Na Moja
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Saba– Tarehe 25 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU WA MEZANI: HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/2019. NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimazi wa Udhibiti wa Nishati na Maji kwa Mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2017 [The Annual Report of Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) for the Year Ended 30th June, 2017]. MWENYEKITI: ahsante, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaanza na maswali yetu ya kawaida, tunaanza Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza Mbunge wa Chumbuni, kwa niaba ya Mheshimiwa Machano. Na. 135 Kuwakamata Wafanyabiashara Wakubwa wa Dawa za Kulevya MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itachukua hatua dhidi ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya wanaoingiza na kuuza badala ya kuakamata waathirika ambao wanahitaji misaada na ushauri nasaha wa kuachana na matumizi ya dawa hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejipanga na inaendelea kukabiliana na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa dawa za kulevya ambao wote wanasababisha madhara kwa jamii kwa kufanya biashara hiyo.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Thelathini
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini na Tano - Tarehe 2 Juni, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua (Hapa Waheshimiwa Wabunge wa Kambi ya Upinzani Walitoka Nje) NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. MBUNGE FULANI: Hamna posho ninyi. NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: Maswali. MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge wa Viti Maalum swali lake litaulizwa na Mheshimiwa Ally Keissy. Na. 284 Unyanyasaji Unaofanywa na Mgambo/Askari Kwa Wafanyabiashara Wadogo Wadogo MHE. ALLY K. MOHAMED (K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI) aliuliza:- Kumekuwa na hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na mgambo na askari polisi wanapotekeleza maagizo ya Serikali dhidi ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) wafanyabiashara wadogo wadogo hususan mama lishe, bodaboda pamoja na machinga. Je, Serikali inatoa tamko gani juu ya hali hiyo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, mgambo wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya polisi wasaidizi ya mwaka 1969 kwa kuzingatia sheria hiyo, Halmashauri zimeruhusiwa kuajiri askari ngambo kwa ajili ya kusaidia usimamizi wa Sheria Ndogondogo za Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya. Mheshimiwa Naibu Spika, askari mgambo anayefanya kazi katika Halmashauri anawajibika kuzingatia sheria za nchi pamoja na sheria ndogo ndogo zilizotungwa na Halmashauri.
    [Show full text]
  • Briefing on “Business & Human Rights in Tanzania” – 2020
    photo courtesy of HakiArdhi BRIEFING ON “BUSINESS & HUMAN RIGHTS IN TANZANIA” – 2020 QUARTER 1: JANUARY – MARCH In March 2020, key stakeholders from civil society, the business community and various government agencies from Tanzania mainland and Zanzibar met in Dar es Salaam to discuss the topics of “land rights and environment” during the second Annual Multi-stakeholder Dialogue on Business and Human Rights (Ref.E1). “Land rights and environment” were identified as cross-cutting issues that affect the rights of many in various ways in Tanzania. Sustainable solutions for addressing the country’s many conflicts related to land are therefore essential to guarantee basic rights for all. During the multi-stakeholder meeting, four case studies on current issues of “land rights and envi- ronment” (Ref.E2) were presented by Tanzanian civil society organisations (Ref.E1). Their studies focussed on initiatives to increase land tenure security and on the tensions between conservation and rights of local communities. The studies confirm that land is indeed a critical socio-economic resource in Tan- zania, but a frequent source of tensions in rural areas due to competing needs of different land users, such as communities versus (tourism) investors or local communities versus conservation authorities (Ref. E2, E3). Women face a number of additional barriers acquiring land rights which affect their livelihoods (Ref.E4, E5). The absence of formalized land rights and land use plans in many regions of the country aids in sus- taining land-related challenges. Therefore, initiatives to address land tenure security (Ref.E5) can have positive effects on local communities (Ref.E6).
    [Show full text]
  • For Personal Use Only Use Personal for Sider All New Mining and Special Mining Licence Applications
    Quarterly Activities Report and Appendix 5B March 2018 HIGHLIGHTS: The company was pleased to announce during the Quarter, strong progress made in a num- ber of important areas towards the successful development of its 75% owned Ngualla Rare Developing the Ngualla Earth Project including: Project into an – ethically sustainable • Oversubscribed Placement of A$6.3M announced post Quarter end – long term – high quality supplier • Recruitment of highly experienced investment banker, Peter Meurer, as of choice to the global Non-Executive Chairman high technology rare earth market • In April 2018, the Tanzanian government announced the appointments to the Mining Commission, paving the way for Peak's SML to be granted • Peak continues to proactively engage with key Tanzanian Ministers and DIRECTORS officials: Non-Executive Chairman: • Positive meeting with the Tanzanian Minister of Constitutional Peter Meurer and Legal Affairs Non-Executive Directors: John Jetter • Visit to Songwe by Deputy Minister for Minerals, Hon. Doto Biteko Jonathan Murray and the MP for Songwe, Hon. Philipo Mulugo Darren Townsend Chief Executive Officer: • Meetings with the Deputy Minister for Minerals, Hon. Stanslaus Rocky Smith Nyongo and the Commissioner for Minerals, Prof. Manya Company Secretary: Graeme Scott • Teesside Planning Application and Environmental Certificate Application submitted CORPORATE Progress on the Special Mining Licence (“SML”) DETAILS Application AS AT 31 MAR 2018: On 17 April 2018, President Magafuli announced the remaining appoint- Ordinary Shares on issue: ments to the Mining Commission. This is a key development for which615.9m Peak has been awaiting and paves the way for the assessment and grant ofListed Peak’s Options SML. PEKOB $0.06 1 November 2018: The SML application was lodged with the Ministry of Minerals in -August 81.2m2017 (ASX An nouncement 6 September 2017 titled “Peak Lodges Special Mining Licence application for Ngualla”).
    [Show full text]
  • Tarehe 12 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tisa – Tarehe 12 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza asubuhi ya leo linaelekezwa kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na linaulizwa na Mheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto. Na. 68 Kukarabati Shule za Msingi na Sekondari - Lushoto MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:- Serikali imekuwa na utaratibu wa kukarabati shule zake za msingi na sekondari nchini:- Je, ni lini Serikali itazifanyia ukarabati Shule za Msingi Kwemashai, Bandi, Milungui, Kilole na Shule za Sekondari za Ntambwe, Ngulwi - Mazashai na Mdando? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2018/2019, Serikali kupitia Program ya Lipa Kulingana na Matokeo (EPforR) imepeleka jumla ya shilingi milioni 467 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili, matundu sita ya vyoo na madarasa mawili katika Shule ya Msingi Shukilai (Shule ya Elimu Maalum) na ujenzi wa mabweni mawili Shule ya Sekondari Magamba, ujenzi wa bweni moja na madarasa mawili Shule ya Sekondari Umba. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika mwaka wa Fedha 2018/2019, Serikali imetoa shilingi bilioni 29.9 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma 2,392 ya madarasa nchi nzima ambapo kati ya fedha hizo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imepewa kiasi cha Sh.512,500,000 kwa ajili ya kukamilisha maboma 46 ya madarasa shule za sekondari.
    [Show full text]
  • Tarehe 7 Februari, 2017
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA SITA Kikao cha Saba – Tarehe 7 Februari, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: MHE. PROF. NORMAN A. S. KING – MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2016 hadi Januari, 2017. MHE. DOTO M. BITEKO -MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kipindi cha kuanzia Januari 2016 hadi Januari 2017. NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na maswali, Ofisi ya Rais - TAMISEMI. Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Na. 69 Tatizo la Ulevi MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Ulevi wa kupita kiasi hasa wa pombe za kienyeji umekuwa na athari kubwa za kiafya na kiakili kwa Watanzania wenye tabia ya ulevi wa kukithiri:- Je, Serikali imejipanga vipi kukabiliana na tatizo hilo hasa ikizingatiwa kuwa Sheria ya Vileo ya mwaka 1969 ni ya zamani sana kiasi kwamba inawezekana kabisa haikidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo kwa wakati huu. NAIBUWAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, pombe za kienyeji zimeainishwa katika Kifungu cha pili (2) cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77.
    [Show full text]