Tarehe 15 Aprili, 2019

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Tarehe 15 Aprili, 2019 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi – Tarehe 15 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA):- Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU SPIKA: Ahsante, Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 78 Malipo Stahiki Kwa Walimu Waliopanda Daraja MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza:- Serikali imekuwa ikiwapandisha madaraja walimu lakini haitoi malipo stahiki kwa madaraja hayo mapya kwa kipindi kirefu tangu walipopandishwa madaraja yao:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba walimu wanapata stahiki zao mara wanapopandishwa madaraja? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilisitisha kupandisha walimu na watumishi wengine madaraja katika mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017 kutokana na uhakiki wa watumishi uliohusisha uhalali wa vyeti, elimu na ngazi za mishahara. Lengo la uhakiki ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Serikali inabaki na watumishi wenye sifa na wanaostahili kulipwa mishahara. Kutokana na sababu hiyo, ni kweli wapo watumishi ambao walipandishwa madaraja ambao hawajalipwa mishahara mipya, wapo waliopata mishahara mipya na baadaye kuondolewa na wapo ambao hawakupandishwa kabisa pamoja na kwamba walikuwa na sifa. Mheshimiwa Naibu Spika, ili kurekebisha changamoto hizo, Serikali ilitoa maelekezo kuanzia Novemba, 2017 kwa 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) waajiri wote wakiwemo Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhuisha barua za kupandisha madaraja watumishi hao ili waweze kulipwa stahiki zao. Aidha, kwa wale ambao walikuwa na barua lakini taarifa zao zilikuwa hazijaingizwa kwenye mfumo, waajiri walielekezwa kuhuisha barua zao kuanzia tarehe 1 Aprili, 2018 ili waanze kulipwa stahiki zao. Serikali itaendelea kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kwa ajili ya kuhakikisha watumishi wenye sifa na kupanda madaraja wanalipwa stahiki zao. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, swali la nyongeza. MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali ya nyongeza. Nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri lakini naomba kuuliza maswali mawili, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, wapo walimu ambao mpaka wanastaafu walikuwa wako katika daraja jipya lakini mlipokuja ku-calculate mafao yao mka- calculate kwa kikokotoo cha mshahara wa zamani. Je, ni lini sasa Serikali mtaona umuhimu wa kuwalipa wastaafu hawa mapunjo yao ya mafao? (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, pesa ya likizo na matibabu kwa walimu hawa ni takwa la kisheria kwa mujibu wa sheria za kazi lakini walimu hawa wamekuwa wakienda likizo au kwenye matibabu pasipo kupewa pesa zao kwa wakati. Je, ni lini sasa Serikali mtaona umuhimu wa kuwalipa walimu hawa pesa kwa wakati mara wanapokwenda likizo au kutibiwa? Ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Kiza maswali yake ya nyongeza mawili, kama ifuatavyo:- 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza Mheshimiwa Mbunge ametaka kujua wale waliolipwa mafao yao kwa kikokotoo cha zamani, naomba nitoe maelekezo kwa waajiri wao na Maafisa Utumishi kwenye Halmashauri zetu, twende case by case walifanyie kazi halafu sisi tutashauriana namna bora ya kulishughulikia ili kuondoa changamoto na malalamiko kwa watumishi hawa. Swali la pili, ni nia ya Serikali kuendelea kulipa watumishi wake na kuwapandisha madaraja kwa wakati. Sasa hivi tumeshafanya calculation na tumejiridhisha kwamba tuna walimu zaidi 86,000 ambao wanaidai Serikali zaidi ya shilingi bilioni 43, tuna walimu wa sekondari zaidi ya 18,000 ambao wanadai karibu zaidi ya shilingi bilioni 18. Jumla ya madai ya walimu wote ya madaraja, likizo na malimbikizo mbalimbali kwa maana ya areas zao ni jumla ya zaidi ya shilingi bilioni moja. Kwa hiyo, Serikali imefanya utafiti na uhakiki sasa tunafanya mchakato wa kutafuta fedha ili walimu wetu waweze kulipwa madai yao na kupunguza malalamiko ambayo kwa kweli ni mengi sana. Ahsante. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na swali linalofuata la Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mheshimiwa Daniel Nicodemus Nsanzugwanko, Mbunge wa Kasulu Mjini sasa aulize swali lake. MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako, naomba kwanza kuipongeza Serikali kwa kuzindua Mji wa Serikali Dodoma, hongereni sana. (Makofi) Na. 79 TAKUKURU Kuendesha Mashauri Mahakamani Moja kwa Moja MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO aliuliza:- Tatizo la ufisadi na wizi nchini limeachwa likaendelea kwa muda mrefu sana:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Je, ni kwa nini TAKUKURU wasiachiwe kuendesha mashauri makubwa ya ufisadi na wizi Mahakamani moja kwa moja bila ya kuomba kibali cha DPP? (b) Je, DPP amezuia majalada mangapi ya uchunguzi kufikishwa Mahakamani na ni kwa nini? (c) Je, Serikali haioni kwamba DPP anaweza kutumika kulinda maslahi ya viongozi ambao kwa kiwango kikubwa wanajihusisha na vitendo vya wizi na ufisadi pamoja na matumizi mabaya ya madaraka? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora) majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Nicodemus Nsanzugwanko, Mbunge wa Kasulu Mjini, lenye sehemu (a),(b) na (c), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, TAKUKURU wanayo mamlaka ya kufikisha watuhumiwa waliotenda makosa ya hongo kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria Na.11 ya mwaka 2007 moja kwa moja Mahakamani bila kupitia kwa Mkurugenzi wa Mastaka (DPP). Makosa mengine yaliyosalia yanapaswa kupata kibali cha DPP kabla ya kupelekwa Mahakamani kama ilivyoelekezwa kwenye kifungu cha 57(1) cha Sheria Na.11 ya mwaka 2007. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 57(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, DPP anapaswa kutoa au kutotoa kibali kuwafikisha watuhumiwa Mahakamani ndani ya siku 60 tangu Jalada la Uchunguzi kumfikia. Hata hivyo, 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) DPP anapokea majalada ya uchunguzi kutoka vyombo mbalimbali vya uchunguzi vikiwemo TAKUKURU, Polisi, na Uhamiaji. Kwa siku DPP hupokea takribani majalada 10 kutoka TAKUKURU. Hivyo, kuna kila sababu DPP akaongezewa rasilimali watu na fedha ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa wakati. Dhana ya kuwa DPP anazuia Majalada ya Uchunguzi yasifikishwe Mahakamani siyo sahihi. (c) Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba DPP ni Ofisi inayojitegemea na mamlaka yake yako kwa mujibu wa Katiba. Hata hivyo, sote tumeshuhudia kwamba viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri wakifikishwa Mahakamani na kuhukumiwa kwenda jela. Naomba nitumie fursa hii kuwaasa watumishi na viongozi wote wa umma mkiwemo ninyi Waheshimiwa Wabunge kutojihusisha na vitendo vyovyote vile vya rushwa. Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Daniel Nsanzugwanko swali la nyongeza. MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na maelezo mazuri ya Naibu Waziri, napenda niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, swali langu la (b) linauliza ni kesi ngapi DPP amezuia majalada hayo ya watuhumiwa, ndiyo msingi wa swali. Kwa maoni yangu swali hilo naomba lijibiwe sasa kwa sababu halikujibiwa katika maelezo yake. Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, Halmashauri ya Mji wa Kasulu tuliibiwa fedha takribani shilingi bilioni 5.9 ingawa baadaye nasikia uhakiki ulibainisha kwamba takribani shilingi bilioni 2 zilikuwa zimeibiwa. Washtakiwa wale walisimamishwa kazi, wakahojiwa na TAKUKURU lakini cha ajabu ni kwamba watuhumiwa hawa hawajafikishwa Mahakamani eti kwa sababu DPP hajatoa kibali. Ni kitu gani hicho? 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa kaka yangu Nsanzugwanko, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba nimpongeze sana kwa jinsi ambavyo anafuatilia sana masuala ya watumishi wa Jimbo lake la Kasulu ambao wanategemewa kutoa huduma kwa wapiga kura wake ambao pia ni wapiga kura wake. Jambo la kwanza, kwenye majibu yangu ya msingi hapa nimesema DPP ni Ofisi inayojitegemea na ipo kwa mujibu wa Katiba.
Recommended publications
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ BUNGE LA KUMI NA MOJA ___________ MKUTANO WA KWANZA Kikao cha Kwanza - Tarehe 17 Novemba, 2015 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Naomba tukae. TANGAZO LA RAIS LA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa masharti ya Katiba, Mkutano huu wa Kwanza unaanza kwa Rais kuuitisha. Naomba kuchukua nafasi hii kusoma Tangazo la Rais kama ambavyo tumelipokea. Tangazo la Serikali Na. 513 la tarehe 6 Novemba, 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sura ya Pili, hati iliyotolewa kwa mujibu wa Ibara ya 90(1). Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya. KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; NA KWA KUWA, masharti ya Ibara ndogo ya kwanza ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, yanamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu; NA KWA KUWA, matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 yalitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2015; HIVYO BASI, mimi John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyonayo chini ya Ibara ya 90(1) ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, naitisha Mkutano wa Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ufanyike katika ukumbi wa Bunge uliopo Mjini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi.
    [Show full text]
  • Bunge Newsletter
    BungeNe ewsletter Issue No 008 June 2013 New Budget Cycle Shows Relavance For the first time in recent Tanzania history the engage the government and influence it make sev- Parliament has managed to pass the next financial eral tangible changes in its initial budget proposals. year budget before the onset of that particular year. This has been made possible by the Budget Commit- This has been made possi- tee, another new innovation by Speaker Makinda. ble by adoption of new budget cycle. Under the old cycle, it was not possible to influence According to the new budget cycle, the Parliament the government to make changes in budgetary allo- starts discussing the budget in April as opposed to cations. That was because the main budget was read, old cycle where debate on the new budget started on debated and passed before the sectoral plans. After June and ends in the first or second week of August. the main budget was passed, it was impossible for the MPs and government to make changes in the When the decision was taken to implement the new sectoral budgets since they were supposed to reflect budget cycle and Speaker Anne Makinda announced the main budget which had already been passed. the new modalities many people, including Mem- bers of Parliament, were skeptical. Many stakehold- These and many other changes have been made possi- ers were not so sure that the new cycle would work. ble through the five components implemented under the Parliament five years development plan. “Govern- But Ms Makinda has managed to prove the doubt- ment and Budget Oversight and Accountability is one ers wrong.
    [Show full text]
  • Hotuba Ya Bajeti Ya Wizara Ya Mambo Ya Nje 2012/2013 Posted: Monday August 06, 2012 1:06 PM BT
    Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje 2012/2013 Posted: Monday August 06, 2012 1:06 PM BT HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MHESHIMIWA BERNARD KAMILLIUS MEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO W A KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuliongoza kwa umahiri mkubwa Bunge hili la Bajeti la mwaka 2012/2013. Napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb.), Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wanaokusaidia kuongoza Bunge hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. 3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya Nne. Chini ya uongozi wake Taifa letu limeendeleza utamaduni wetu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano. Nawaomba Watanzania wote tuendelee kudumisha hali hiyo ili kuimarisha umoja wetu ambao ni tunu isiyopatikana kwa bei yoyote. 4. Mheshimiwa Spika, niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge wengine wote walionitangulia kuwapongeza kwa dhati kabisa Waheshimiwa Wabunge wapya, Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei 2012. Nawapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge waliochaguliwa kipindi hiki kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye nafasi mbalimbali humu Bungeni na ndani ya Serikali.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Sita – Tarehe 9 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Sita – Tarehe 9 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2019/2020. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka ulioisha tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual Report and Audited Accounts of Mzumbe University for the year ended 30th June, 2017). MWENYEKITI: Katibu! NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza leo linaelekezwa Ofisi ya Waziri Mkuu na linaulizwa na Mheshimiwa Dkt. Raphael Masunga Chegeni, Mbunge wa Busega. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo hapa kwa niaba. MWENYEKITI: Wewe unatoka Busega? MHE. RASHID A. SHANGAZI: Hapana, ila hili ni la kitaifa. MWENYEKITI: Aaa, sawa, kwa niaba. Na. 43 Kauli Mbiu ya Kuvutia Wawekezaji Nchini MHE. RASHID A. SHANGAZI (K.n.y. MHE. DKT.
    [Show full text]
  • Ofisi Ya Rais, Menejimenti Ya Utumishi Wa Umma Na Utawala Bora Kwa Mwaka Wa Fedha Wa 2019/20
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI – OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA. KAPT (MST) GEORGE H. MKUCHIKA (Mb.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20 APRILI, 2019 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyochambua bajeti ya Ofisi ya Rais, Ikulu (Fungu 20 na 30), Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Fungu 33), Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Fungu 32), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (Fungu 67), Tume ya Utumishi wa Umma (Fungu 94), Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (Fungu 09), na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (Fungu 04). Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Mpango wa Utekelezaji na Makadirio ya Fedha kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/20. 2. Mheshimiwa Spika, Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupatia uwezo wa kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wananchi. Pia namshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kuendelea kuniamini katika nafasi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Ninamuahidi kuwa nitatekeleza wajibu wangu kwa ufanisi na uadilifu wa hali ya juu. Aidha, nawashukuru wapiga kura wa Jimbo la Newala Mjini kwa ujumla kwa kuendelea kunipa ushirikiano wakati wote ninapoe ndelea kuwawakilisha.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Sita – Tarehe 27 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo ni Kikao cha 36. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CATHERINE V. MAGIGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI) Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu utekelezaji na Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. TUNZA I. MALAPO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA MADINI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza Malapo, tunakushukuru. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Azza Hilal, Mbunge wa Viti Maalum - Shinyanga.
    [Show full text]
  • Joint Declaration by Non Governmental Organisations on the Ongoing Human Rights Violations in Loliondo
    JOINT DECLARATION BY NON GOVERNMENTAL ORGANISATIONS ON THE ONGOING HUMAN RIGHTS VIOLATIONS IN LOLIONDO Background For several weeks now there has been an alarming situation and mistreatments to residents of Loliondo in Ngorongoro District along with the claim that most of them are not citizens of Tanzania. Some citizens living Loliondo area have been arrested by police, tortured, humiliated, intimidated and detained on the grounds that they are not citizens of Tanzania. Our joint declaration aims at condemning and making a call to the government in Loliondo to immidiately stop violations foisted to the people of Loliondo asserting on the issue of citizenship. It should be noted that various operations in the country such as Tokomeza, have been conducted with hidden agendas and without respect to laws and human rights. These incidents of arrest of citizens in Loliondo is a continuation of a longlived conflict between Loliondo, Sale villagers and investors associated with the government’s intention of giving away an area of square kilometers 1,500 to Otterlo Business Corporation from Dubai (OBC) The History of the Area of Conflict: Loliondo Gate Scandal Loliondo area which is known today as the Division of Loliondo and Sale is an area that has been domiciled by pastoralist since time immemorial. In 1993 the government illegally issued a wildlife hunting permit to Prince Brigadier Mohamad Al-Ali illegally for only companies ought to be issued with a hunting permit and not an individual. Since then conflicts between citizens and the government have persisted with the government using its power and resources to protect its taxpayers, OBC.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019 Feathers Ruffled in CCM Plastic Bag Ban TSh 33 trillion annual budget Ben Taylor: FEATHERS RUFFLED IN CCM Two former Secretary Generals of the ruling party, CCM, Abdulrahman Kinana and Yusuf Makamba, stirred up a very public argument at the highest levels of the party in July. They wrote a letter to the Elders’ Council, an advisory body within the party, warning of the dangers that “unfounded allegations” in a tabloid newspaper pose to the party’s “unity, solidarity and tranquillity.” Selection of newspaper covers from July featuring the devloping story cover photo: President Magufuli visits the fish market in Dar-es-Salaam following the plastic bag ban (see page 5) - photo State House Politics 3 This refers to the frequent allegations by publisher, Mr Cyprian Musiba, in his newspapers and on social media, that several senior figures within the party were involved in a plot to undermine the leadership of President John Magufuli. The supposed plotters named by Mr Musiba include Kinana and Makamba, as well as former Foreign Affairs Minister, Bernard Membe, various opposition leaders, government officials and civil society activists. Mr Musiba has styled himself as a “media activist” seeking to “defend the President against a plot to sabotage him.” His publications have consistently backed President Magufuli and ferociously attacked many within the party and outside, on the basis of little or no evidence. Mr Makamba and Mr Kinana, who served as CCM’s secretary generals between 2009 to 2011 and 2012-2018 respectively, called on the party’s elders to intervene.
    [Show full text]
  • Muhtasari Wa Hotuba Ya Waziri Wa Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto, Mhe
    MUHTASARI WA HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2021/22. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lako Tukufu, iliyochambua Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ninaomba kutoa hoja Bunge lako likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Wizara yangu kwa mwaka 2020/21 na Vipaumbele vyake kwa mwaka 2021/22. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida pamoja na Miradi ya Maendeleo ya Wizara kwa mwaka 2021/22. 2. Mheshimiwa Spika, Namshukuru Mungu kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu na kuwasilisha hotuba yangu. Aidha, kwa masikitiko makubwa, natoa pole kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge Wote, Chama Cha Mapinduzi pamoja na Watanzania wote kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 3. Mheshimiwa Spika, Vilevile, natoa pole kwa Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuondokewa na Viongozi Wakuu, Hayati Benjamin William Mkapa, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na Balozi Mhandisi John Herbert Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kazi ya Mungu haina makosa, Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. 4. Mheshimiwa Spika, Vilevile, naomba kutoa pole kwako, Bunge lako Tukufu, familia na wananchi wa Mkoa wa Manyara kwa kifo cha Mheshimiwa Martha Umbulla, Mbunge wa Viti Maalum (CCM).
    [Show full text]
  • Did They Perform? Assessing fi Ve Years of Bunge 2005-2010
    Policy Brief: TZ.11/2010E Did they perform? Assessing fi ve years of Bunge 2005-2010 1. Introducti on On July 16th 2010, following the completi on of the 20th session of the Bunge, the President of Tanzania dissolved the 9th Parliament. This event marked the end of the term for Members of Parliament who were elected during the 2005 general electi ons. Now that the last session has been completed it allows us to look back and to consider how MPs performed during their tenure. Did they parti cipate acti vely and represent their consti tuencies by asking questi ons and making interventi ons, or were they silent backbenchers? The Bunge is the Supreme Legislature of Tanzania. The Bunge grants money for running the administrati on and oversees government programs and plans. The Bunge oversees the acti ons of the Executi ve and serves as watchdog to ensure that government is accountable to its citi zens. To achieve all this, Members of Parliament pass laws, authorize taxati on and scruti nize government policies including proposal for expenditure; and debate major issues of the day. For the Bunge to eff ecti vely carry out its oversight role, acti ve parti cipati on by Members of Parliament is criti cal. MPs can be acti ve by making three kinds of interventi ons: they can ask basic questi ons, they can ask supplementary questi ons and they can make contributi ons during debates. This brief follows earlier briefs, the last of which was released in August 2010. It presents seven facts on the performance of MPs, including rati ng who were the most acti ve and least acti ve MPs.
    [Show full text]
  • 20 MAY 2019.Pmd
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Moja – Tarehe 20 Mei, 2019 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo kikao cha 31. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nasikitika kuwatangazia kifo cha mwanasiasa mkongwe na kiongozi aliyepata kuhudumia kwa muda mrefu hasa kule kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Ally Juma Shamhuna. Waheshimiwa Wabunge, katika uhai wake, marehemu Ally Juma Shamhuma amepata kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo hizi zifuatazo; amepata kuwa Mkurugenzi wa Mifugo, amewahi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, amewahi kuwa Katibu Mkuu, Export Processing Zone Zanzibar, amewahi kuwa Waziri wa Mipango, amekuwa Waziri wa Nchi, Afisi ya Waziri Kiongozi, aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na wakati huo huo akiwa ni 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Naibu Waziri Kiongozi, katika uhai wake amekuwa Waziri wa Ardhi, Maji na Nishati na alipata kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali. Aidha, Marehemu Mheshimiwa Shamhuna kwa muda mrefu alikuwa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kutokea Zanzibar na baadhi yenu humu Wabunge mtamkumbuka marehemu Mheshimiwa Shamhuna kama Mbunge wa Bunge la Katiba na alikuwa Mjumbe wa Kamati namba 8 kwenye Bunge la Katiba, Kamati ambayo nilikuwa Mwenyekiti wake. Kwa niaba yenu Waheshimiwa Wabunge, tunatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Tunatoa pole kwa Wazanzibari wote na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia kifo hicho na tunamuomba Mwenyezi Mungu aihifadhi roho yake mahali pema peponi, amina.
    [Show full text]
  • Tarehe 12 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tisa – Tarehe 12 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza asubuhi ya leo linaelekezwa kwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na linaulizwa na Mheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto. Na. 68 Kukarabati Shule za Msingi na Sekondari - Lushoto MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:- Serikali imekuwa na utaratibu wa kukarabati shule zake za msingi na sekondari nchini:- Je, ni lini Serikali itazifanyia ukarabati Shule za Msingi Kwemashai, Bandi, Milungui, Kilole na Shule za Sekondari za Ntambwe, Ngulwi - Mazashai na Mdando? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2018/2019, Serikali kupitia Program ya Lipa Kulingana na Matokeo (EPforR) imepeleka jumla ya shilingi milioni 467 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili, matundu sita ya vyoo na madarasa mawili katika Shule ya Msingi Shukilai (Shule ya Elimu Maalum) na ujenzi wa mabweni mawili Shule ya Sekondari Magamba, ujenzi wa bweni moja na madarasa mawili Shule ya Sekondari Umba. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika mwaka wa Fedha 2018/2019, Serikali imetoa shilingi bilioni 29.9 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma 2,392 ya madarasa nchi nzima ambapo kati ya fedha hizo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imepewa kiasi cha Sh.512,500,000 kwa ajili ya kukamilisha maboma 46 ya madarasa shule za sekondari.
    [Show full text]