Tarehe 15 Aprili, 2019

Tarehe 15 Aprili, 2019

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi – Tarehe 15 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA):- Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU SPIKA: Ahsante, Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 78 Malipo Stahiki Kwa Walimu Waliopanda Daraja MHE. KIZA H. MAYEYE aliuliza:- Serikali imekuwa ikiwapandisha madaraja walimu lakini haitoi malipo stahiki kwa madaraja hayo mapya kwa kipindi kirefu tangu walipopandishwa madaraja yao:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba walimu wanapata stahiki zao mara wanapopandishwa madaraja? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilisitisha kupandisha walimu na watumishi wengine madaraja katika mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017 kutokana na uhakiki wa watumishi uliohusisha uhalali wa vyeti, elimu na ngazi za mishahara. Lengo la uhakiki ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Serikali inabaki na watumishi wenye sifa na wanaostahili kulipwa mishahara. Kutokana na sababu hiyo, ni kweli wapo watumishi ambao walipandishwa madaraja ambao hawajalipwa mishahara mipya, wapo waliopata mishahara mipya na baadaye kuondolewa na wapo ambao hawakupandishwa kabisa pamoja na kwamba walikuwa na sifa. Mheshimiwa Naibu Spika, ili kurekebisha changamoto hizo, Serikali ilitoa maelekezo kuanzia Novemba, 2017 kwa 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) waajiri wote wakiwemo Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhuisha barua za kupandisha madaraja watumishi hao ili waweze kulipwa stahiki zao. Aidha, kwa wale ambao walikuwa na barua lakini taarifa zao zilikuwa hazijaingizwa kwenye mfumo, waajiri walielekezwa kuhuisha barua zao kuanzia tarehe 1 Aprili, 2018 ili waanze kulipwa stahiki zao. Serikali itaendelea kuweka kipaumbele na kutenga bajeti kwa ajili ya kuhakikisha watumishi wenye sifa na kupanda madaraja wanalipwa stahiki zao. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kiza Hussein Mayeye, swali la nyongeza. MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali ya nyongeza. Nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri lakini naomba kuuliza maswali mawili, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, wapo walimu ambao mpaka wanastaafu walikuwa wako katika daraja jipya lakini mlipokuja ku-calculate mafao yao mka- calculate kwa kikokotoo cha mshahara wa zamani. Je, ni lini sasa Serikali mtaona umuhimu wa kuwalipa wastaafu hawa mapunjo yao ya mafao? (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, pesa ya likizo na matibabu kwa walimu hawa ni takwa la kisheria kwa mujibu wa sheria za kazi lakini walimu hawa wamekuwa wakienda likizo au kwenye matibabu pasipo kupewa pesa zao kwa wakati. Je, ni lini sasa Serikali mtaona umuhimu wa kuwalipa walimu hawa pesa kwa wakati mara wanapokwenda likizo au kutibiwa? Ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Kiza maswali yake ya nyongeza mawili, kama ifuatavyo:- 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza Mheshimiwa Mbunge ametaka kujua wale waliolipwa mafao yao kwa kikokotoo cha zamani, naomba nitoe maelekezo kwa waajiri wao na Maafisa Utumishi kwenye Halmashauri zetu, twende case by case walifanyie kazi halafu sisi tutashauriana namna bora ya kulishughulikia ili kuondoa changamoto na malalamiko kwa watumishi hawa. Swali la pili, ni nia ya Serikali kuendelea kulipa watumishi wake na kuwapandisha madaraja kwa wakati. Sasa hivi tumeshafanya calculation na tumejiridhisha kwamba tuna walimu zaidi 86,000 ambao wanaidai Serikali zaidi ya shilingi bilioni 43, tuna walimu wa sekondari zaidi ya 18,000 ambao wanadai karibu zaidi ya shilingi bilioni 18. Jumla ya madai ya walimu wote ya madaraja, likizo na malimbikizo mbalimbali kwa maana ya areas zao ni jumla ya zaidi ya shilingi bilioni moja. Kwa hiyo, Serikali imefanya utafiti na uhakiki sasa tunafanya mchakato wa kutafuta fedha ili walimu wetu waweze kulipwa madai yao na kupunguza malalamiko ambayo kwa kweli ni mengi sana. Ahsante. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na swali linalofuata la Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mheshimiwa Daniel Nicodemus Nsanzugwanko, Mbunge wa Kasulu Mjini sasa aulize swali lake. MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako, naomba kwanza kuipongeza Serikali kwa kuzindua Mji wa Serikali Dodoma, hongereni sana. (Makofi) Na. 79 TAKUKURU Kuendesha Mashauri Mahakamani Moja kwa Moja MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO aliuliza:- Tatizo la ufisadi na wizi nchini limeachwa likaendelea kwa muda mrefu sana:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Je, ni kwa nini TAKUKURU wasiachiwe kuendesha mashauri makubwa ya ufisadi na wizi Mahakamani moja kwa moja bila ya kuomba kibali cha DPP? (b) Je, DPP amezuia majalada mangapi ya uchunguzi kufikishwa Mahakamani na ni kwa nini? (c) Je, Serikali haioni kwamba DPP anaweza kutumika kulinda maslahi ya viongozi ambao kwa kiwango kikubwa wanajihusisha na vitendo vya wizi na ufisadi pamoja na matumizi mabaya ya madaraka? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora) majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Nicodemus Nsanzugwanko, Mbunge wa Kasulu Mjini, lenye sehemu (a),(b) na (c), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, TAKUKURU wanayo mamlaka ya kufikisha watuhumiwa waliotenda makosa ya hongo kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria Na.11 ya mwaka 2007 moja kwa moja Mahakamani bila kupitia kwa Mkurugenzi wa Mastaka (DPP). Makosa mengine yaliyosalia yanapaswa kupata kibali cha DPP kabla ya kupelekwa Mahakamani kama ilivyoelekezwa kwenye kifungu cha 57(1) cha Sheria Na.11 ya mwaka 2007. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 57(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, DPP anapaswa kutoa au kutotoa kibali kuwafikisha watuhumiwa Mahakamani ndani ya siku 60 tangu Jalada la Uchunguzi kumfikia. Hata hivyo, 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) DPP anapokea majalada ya uchunguzi kutoka vyombo mbalimbali vya uchunguzi vikiwemo TAKUKURU, Polisi, na Uhamiaji. Kwa siku DPP hupokea takribani majalada 10 kutoka TAKUKURU. Hivyo, kuna kila sababu DPP akaongezewa rasilimali watu na fedha ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa wakati. Dhana ya kuwa DPP anazuia Majalada ya Uchunguzi yasifikishwe Mahakamani siyo sahihi. (c) Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba DPP ni Ofisi inayojitegemea na mamlaka yake yako kwa mujibu wa Katiba. Hata hivyo, sote tumeshuhudia kwamba viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri wakifikishwa Mahakamani na kuhukumiwa kwenda jela. Naomba nitumie fursa hii kuwaasa watumishi na viongozi wote wa umma mkiwemo ninyi Waheshimiwa Wabunge kutojihusisha na vitendo vyovyote vile vya rushwa. Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Daniel Nsanzugwanko swali la nyongeza. MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na maelezo mazuri ya Naibu Waziri, napenda niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, swali langu la (b) linauliza ni kesi ngapi DPP amezuia majalada hayo ya watuhumiwa, ndiyo msingi wa swali. Kwa maoni yangu swali hilo naomba lijibiwe sasa kwa sababu halikujibiwa katika maelezo yake. Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, Halmashauri ya Mji wa Kasulu tuliibiwa fedha takribani shilingi bilioni 5.9 ingawa baadaye nasikia uhakiki ulibainisha kwamba takribani shilingi bilioni 2 zilikuwa zimeibiwa. Washtakiwa wale walisimamishwa kazi, wakahojiwa na TAKUKURU lakini cha ajabu ni kwamba watuhumiwa hawa hawajafikishwa Mahakamani eti kwa sababu DPP hajatoa kibali. Ni kitu gani hicho? 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali madogo mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa kaka yangu Nsanzugwanko, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba nimpongeze sana kwa jinsi ambavyo anafuatilia sana masuala ya watumishi wa Jimbo lake la Kasulu ambao wanategemewa kutoa huduma kwa wapiga kura wake ambao pia ni wapiga kura wake. Jambo la kwanza, kwenye majibu yangu ya msingi hapa nimesema DPP ni Ofisi inayojitegemea na ipo kwa mujibu wa Katiba.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    226 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us