MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA TATU Kikao Cha
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Arobaini na Tatu – Tarehe 3 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Arobaini na Tatu. Katibu NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, aah sasa hivi unavaa sketi ndefu, hataki ugomvi na Mgogo. (Kicheko) Tunaendelea, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri Mkuu karibu sana. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, nawakumbusha tena kuhusu maswali ya kisera sio matukio, sio nini, ni ya kisera. Tunaanza na Mheshimiwa Mbunge wa Liwale, Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka, maswali kwa kifupi. MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kwanza kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Spika, swali langu litahusu sekta ya korosho. Mwaka huu tumepata taarifa kwamba Serikali ilijipanga kutupatia pembejeo wakulima wa zao la korosho kwa maana kwamba waje kuzilipa baadaye kwenye mjengeko wa bei. Hata hivyo, kuna taharuki kubwa kwa wakulima wetu wa korosho baada ya Bodi ya Korosho kuleta waraka kwenye Halmashauri zetu, wakiwaambia kila mkulima akipeleka zao lile kwenye mnada kila kilo moja itakatwa shilingi 110 bila kujali kwamba mkulima yule amechukua pembejeo kwa kiwango gani.
[Show full text]