Hotuba Ya Waziri Wa Mambo Ya Nje Na

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Hotuba Ya Waziri Wa Mambo Ya Nje Na HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MHESHIMIWA BERNARD KAMILLIUS MEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuliongoza kwa umahiri mkubwa Bunge hili la Bajeti la mwaka 2012/2013. Napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb.), Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wanaokusaidia kuongoza Bunge hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. 3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya Nne. Chini ya uongozi wake Taifa letu limeendeleza utamaduni wetu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano. Nawaomba Watanzania wote tuendelee kudumisha hali hiyo ili kuimarisha umoja wetu ambao ni tunu isiyopatikana kwa bei yoyote. 4. Mheshimiwa Spika, niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge wengine wote walionitangulia kuwapongeza kwa dhati kabisa Waheshimiwa Wabunge wapya, Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei 2012. Nawapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge waliochaguliwa kipindi hiki kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye nafasi mbalimbali humu Bungeni na ndani ya Serikali. Nampongeza pia Mheshimiwa Mussa Zungu Azzan, Mbunge wa Ilala, kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge. 5. Mheshimiwa Spika, kwa njia ya kipekee kabisa, niruhusu niwapongeze Waheshimiwa Wabunge waliochaguliwa na Bunge lako Tukufu kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Wizara yangu kwa kuwa ndiyo inayosimamia masuala yote ya mambo ya nje, nawaahidi Waheshimiwa Wabunge ushirikiano wangu binafsi na ule wa Wizara nzima kwa kufanya kazi kwa karibu na kushirikiana na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 6. Mheshimiwa Spika, naomba niwashukuru pia Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa William A. Mgimwa (Mb.), Waziri wa Fedha; pamoja na Mheshimiwa Stephen Masatu Wasira (Mb.), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu kwa hotuba zao za kina ambazo zimetoa ufafanuzi na miongozo kwa masuala mbalimbali muhimu ya Taifa letu kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Kwa ujumla wake, naomba kuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri wote waliotangulia kuwasilisha bajeti zao kwa kazi nzuri walizozifanya. Hotuba zao zote zimefafanua kwa kina masuala ya uchumi, siasa na jamii yanayohusu nchi yetu na hivyo kuigusa pia Wizara yangu kwa njia moja au nyingine. 7. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati na za uongozi mzima wa Wizara kwa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati kwa ushauri wao mzuri ambao wamekuwa wakiutoa mara kwa mara kwa Wizara yangu. Kamati hii imetoa mchango mkubwa sana katika kuiwezesha Wizara kukabiliana na changamoto zinazoikabili katika kutekeleza majukumu yake. Ninaamini ziara walizozifanya kwenye nchi mbalimbali kutembelea Balozi zetu zimewapa fursa ya kujionea wenyewe na kusikia kutoka kwa maafisa wetu changamoto mbalimbali zinazotukabili kama Wizara. Aidha, kwa ujumla, napenda kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yao wanayoitoa Bungeni katika kuishauri Serikali. 8. Mheshimiwa Spika, natoa shukrani na pongezi maalum kwa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ushirikiano anaonipa katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Vilevile, nawapongeza na kuwashukuru Bwana John M. Haule, Katibu Mkuu, Mheshimiwa Balozi Rajabu H. Gamaha, Naibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi, Mabalozi na wafanyakazi wote kwa msaada mkubwa wanaonipa katika kuiongoza Wizara hii. Pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao, nawashukuru kwa kazi nzuri na ya kizalendo ya kutetea maslahi ya Taifa letu. 9. Mheshimiwa Spika, shukrani za pekee ziwaendee wananchi na viongozi wa Mkoa wa Lindi, Wilaya ya Lindi na hasa wana-Mtama wote. Napenda pia nimshukuru mke wangu Mrs. Membe na watoto wangu kwa upendo na uvumilivu waliouonesha kwangu. 10. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanza kueleza kwa kina kuhusu hotuba yangu, niruhusu niungane na Viongozi wote, Wazanzibari na Watanzania kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya meli ya MV Skagit iliyotokea Zanzibar. Kwa wale wote walioumia na wanaoendelea kujiuguza, namwomba Mwenyezi Mungu awape nguvu waweze kupona haraka. 11. Mheshimiwa Spika, vilevile, natoa salamu za pole kwa wale Wabunge wote waliopatwa na misiba ya wapendwa wao. Kwa wote, namwomba Mwenyezi Mungu awape faraja na azilaze Roho za Marehemu mahali pema peponi. Amina. TATHMINI YA HALI YA DUNIA KWA KIPINDI CHA 2011/2012 HALI YA DUNIA ULAYA NA MAREKANI 12. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla, hali ya dunia kiuchumi, kisiasa na kijamii katika mwaka wa fedha 2011/2012 imekuwa ya mashaka makubwa na hivyo kuathiri utulivu katika nchi nyingi duniani. Hali hiyo imechochewa na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali duniani. 13. Mheshimiwa Spika, eneo la Ulaya limeathirika sana kiuchumi kutokana na madeni pamoja na mdororo wa uchumi ulioikumba dunia katika kipindi cha mwaka 2008. Hali hii pia iliathiri kwa kiasi kikubwa sarafu ya Euro, uchumi wa nchi zilizo katika ukanda wa sarafu hiyo ujulikanao kama “Eurozone” pamoja na nchi ambazo zinafanya biashara na nchi za Umoja wa Ulaya. Hali hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa Viongozi katika baadhi ya nchi hizo kama vile; Ufaransa, Ugiriki, Italia, Hispania na Ireland kushindwa katika Chaguzi Kuu au kushinikizwa kujiuzulu. Kwa upande wa Marekani nayo ilikumbwa na misukosuko ya uchumi iliyosababishwa pia na mdororo wa uchumi wa mwaka 2008. Hata hivyo, uchumi wake umeanza kutengemaa baada ya mdororo huo. 14. Mheshimiwa Spika, kutokana na mdororo huo, nchi hizo zimelazimika kuchukua hatua kadhaa kunusuru uchumi wao ikiwa ni pamoja na kubana matumizi, kukopa zaidi ili kuwekeza katika sekta zenye kutoa ajira na kupunguza kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kulingana na ahadi zao za awali. Kuna kila kiashiria kuwa uchumi wa Ulaya na Marekani hautapata utulivu kwa muda mrefu na hivyo uwezo wao wa kutoa misaada kupungua kadiri siku zinavyokwenda. Wizara na Balozi zetu za nje zinaendelea kufuatilia kwa makini hali ya uchumi inavyoendelea duniani na kuishauri Serikali kutekeleza mikakati ya kukabiliana na changamoto zitokanazo na hali hiyo ili kuimarisha uchumi wa Taifa letu na kuondokana na utegemezi. ASIA Mashariki ya Kati 15. Mheshimiwa Spika, eneo la Mashariki ya Kati bado liko katika hali ya tahadhari. Nchini Syria hali imeendelea kuwa tete kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo ambako waasi wanapigana dhidi ya Serikali ya Rais Bashar al – Assad tangu Januari mwaka 2011 na tayari wameshaingia kwenye Mji Mkuu wa Nchi hiyo. Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) zikiongozwa na Msuluhishi wa Mgogoro huo, Dkt. Kofi Annan wameshindwa hadi sasa kufanikisha kusitishwa kwa mapigano. Aidha, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limegawanyika ambapo wajumbe wa kudumu wenye kura ya turufu wametofautiana juu ya uamuzi wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Serikali ya Syria. Tanzania inaunga mkono jitihada za Msuluhishi Kofi Annan na kuwaomba wadau wote kutoingilia na kushinikiza matakwa yao nchini Syria na badala yake kumuunga mkono Msuluhishi ili kumaliza mgogoro huo kwa njia ya amani. 16. Mheshimiwa Spika, aidha, kuendelea kukua kwa uhasama baina ya Iran na nchi za Magharibi kunaleta changamoto ya ustawi wa amani katika ukanda huo. Uhasama huo unaletwa na hofu kuwa nchi ya Iran inarutubisha madini ya urani yanayotumika kutengeneza silaha za nyuklia. Tayari, Iran imewekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani ikishirikiana na nchi za Umoja wa Ulaya. Iran nayo imetishia kujibu mapigo kwa kufunga mlango wa Bahari ya Hormuz ambao hupitisha asilimia ishirini 20 ya mafuta yote ulimwenguni. Iwapo Iran itatekeleza uamuzi huo inaweza kuzusha vita ambayo italeta madhara makubwa kwa uchumi wa dunia. Hali hii ya mtafaruku baina ya Iran na nchi za Magharibi inaathiri pia mustakabali wa ukanda mzima wa Mashariki ya Kati kwa kuwa Iran ina ushawishi mkubwa kwenye siasa za nchi nyingine zenye machafuko kama vile Syria. Kuendelea kwa migogoro na machafuko katika ukanda wa Mashariki ya Kati kunaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa dunia kwa sababu asilimia kubwa ya mafuta yanayotumika duniani hutoka katika ukanda huo. Pamoja na changamoto hizo, habari njema ni kwamba tayari Irani, Marekani, Nchi za Ulaya pamoja na wadau wengine wameshakubaliana kurejea kwenye meza ya mazungumzo na tayari mzunguko wa kwanza wa mazungumzo haya umeshafanyika. Imani yetu kama nchi ni kwamba wahusika wote kwenye mazungumzo hayo wataonesha utashi wa kweli wa kumaliza tatizo hilo kwa njia ya mazungumzo na si vinginevyo. Mashariki ya Mbali 17. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mashariki ya Mbali hali ni tulivu ukiachilia majanga ya asili yaliyozikumba nchi za Japan, Ufilipino na Thailand na kusababisha athari za kijamii
Recommended publications
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 7 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA KIKAO CHA NNE – 7 NOVEMBA, 2014 Kikao kilianza saa 3:00 Asubuhi kikiongozwa na Mhe. Job Y. Ndigai, Mb Naibu Spika ambaye alisoma Dua. MAKATIBU MEZANI 1. Ndg. Charles Mloka 2. Ndg. Lina Kitosi 3. Ndg. Hellen Mbeba I. MASWALI YA KAWAIDA Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge na kupitia majibu Bungeni:- 1. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 38 la Mhe. Anne Kilango 2. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 39 la Mhe. Salum Khalfan Barwary 3. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 40 la Mhe. Moses Joseph Machali 4. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – swali na. 41. La Mhe. Omar Rashid Nundu 5. Wizara ya Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi – swali na. 42. La Mhe. Hilda Ngoye 6. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – swali na. 43. La Mhe. Zitto Kabwe Zuberi 7. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tecknolojia – swali na. 44 –la Mhe. Murtaza Mangungu 8. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - swali na. 45-la Mhe. Godfrey Mgimwa 9. Wizara ya Katiba na Sheria - swali na. 46 – la Mhe. Neema Mgaya Hamid 2 10. Wizara ya Katiba na Sheria- swali na. 47 – la Mhe. Assumpter Mshana 11. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo – swali na. 48 la Mhe. Khatib Said Hji. 12. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - swali na. 49 la Mhe.
    [Show full text]
  • Hotuba Ya Bajeti Ya Wizara Ya Mambo Ya Nje 2012/2013 Posted: Monday August 06, 2012 1:06 PM BT
    Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje 2012/2013 Posted: Monday August 06, 2012 1:06 PM BT HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MHESHIMIWA BERNARD KAMILLIUS MEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO W A KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuliongoza kwa umahiri mkubwa Bunge hili la Bajeti la mwaka 2012/2013. Napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb.), Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wanaokusaidia kuongoza Bunge hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. 3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya Nne. Chini ya uongozi wake Taifa letu limeendeleza utamaduni wetu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano. Nawaomba Watanzania wote tuendelee kudumisha hali hiyo ili kuimarisha umoja wetu ambao ni tunu isiyopatikana kwa bei yoyote. 4. Mheshimiwa Spika, niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge wengine wote walionitangulia kuwapongeza kwa dhati kabisa Waheshimiwa Wabunge wapya, Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei 2012. Nawapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge waliochaguliwa kipindi hiki kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye nafasi mbalimbali humu Bungeni na ndani ya Serikali.
    [Show full text]
  • Akiwasilisha Bungeni Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Ya Wizara Ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo Ya Makazi Kwa Mwaka Wa Fedha 2013/2014
    HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, MHESHIMIWA PROF. ANNA KAJUMULO TIBAIJUKA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 DIRA YA WIZARA: Kuwa na uhakika wa miliki za ardhi, nyumba bora na makazi endelevu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. DHIMA: Kuweka mazingira yanayofaa kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma za ardhi, nyumba na makazi. MAJUKUMU: Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayo majukumu yafuatayo:- i. Kuandaa sera na mikakati ya uendelezaji wa sekta ya ardhi; ii. Kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi; iii. Kusimamia upangaji wa miji na vijiji; iv. Kupima ardhi na kutayarisha ramani; v. Kutoa hati za kumiliki ardhi na hatimiliki za kimila; vi. Kusajili hati za umiliki ardhi na nyaraka za kisheria; vii. Kuthamini mali; viii. Kuhamasisha na kuwezesha wananchi kuwa na nyumba bora; ix. Kutatua migogoro ya ardhi na nyumba; i x. Kusimamia upatikanaji na utunzaji wa kumbukumbu za ardhi; xi. Kusimamia ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na huduma za sekta ya ardhi; xii. Kusimamia Shirika la Nyumba la Taifa, Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba na Vifaa vya Ujenzi na Wakala wa Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni; xiii. Kusimamia uendeshaji wa Vyuo vya Ardhi vya Tabora na Morogoro; na, xiv. Kusimamia maslahi na utendaji kazi wa watumishi wa sekta ya ardhi. Katika kutekeleza majukumu hayo, Wizara inaongozwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA II), Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16), Malengo ya Milenia, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010, Mpango Mkakati wa Wizara (2012/13- 2016/17), Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Sera ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 na miongozo mbalimbali ya Serikali.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA TATU Kikao Cha
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Arobaini na Tatu – Tarehe 3 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Arobaini na Tatu. Katibu NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, aah sasa hivi unavaa sketi ndefu, hataki ugomvi na Mgogo. (Kicheko) Tunaendelea, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri Mkuu karibu sana. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, nawakumbusha tena kuhusu maswali ya kisera sio matukio, sio nini, ni ya kisera. Tunaanza na Mheshimiwa Mbunge wa Liwale, Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka, maswali kwa kifupi. MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kwanza kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Spika, swali langu litahusu sekta ya korosho. Mwaka huu tumepata taarifa kwamba Serikali ilijipanga kutupatia pembejeo wakulima wa zao la korosho kwa maana kwamba waje kuzilipa baadaye kwenye mjengeko wa bei. Hata hivyo, kuna taharuki kubwa kwa wakulima wetu wa korosho baada ya Bodi ya Korosho kuleta waraka kwenye Halmashauri zetu, wakiwaambia kila mkulima akipeleka zao lile kwenye mnada kila kilo moja itakatwa shilingi 110 bila kujali kwamba mkulima yule amechukua pembejeo kwa kiwango gani.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Arobaini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 15 Juni, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, tunaendelea na Mkutano wetu wa 19, Kikao cha 46, bado kimoja tu cha kesho. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na: NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 (Monetary Policy Statement for the Financial Year 2020/2021). MHE. ALBERT N. OBAMA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI:Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. RHODA E. KUNCHELA - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). MHE. DKT. TULIA ACKSON - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KANUNI ZA BUNGE: Azimio la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Bunge SPIKA: Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika, Katibu MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 426 Migogoro ya Mipaka MHE.
    [Show full text]
  • Ofisi Ya Bunge S.L.P 941 Dodoma 27 Juni, 2013
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA MOJA YATOKANAYO NA KIKAO CHA HAMSINI NA NANE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) OFISI YA BUNGE S.L.P 941 DODOMA 27 JUNI, 2013 YATOKANAYO NA KIKAO CHA HAMSINI NA NANE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS – FIFITY EIGTHTH SITTING) TAREHE 27 Juni, 2013 MAKATIBU MEZANI: (1) Ndg. Justina Shauri (2) Ndg. Charles Mloka (4) Ndg. Lawrence Makigi I. DUA: Dua ilisomwa saa 3.00 asubuhi na Kikao kilianza kikiongozwa na Mhe. Spika Anne S. Makinda, (Mb). II. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI: WAZIRI MKUU: Utekelezaji Wa Taarifa ya Ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2012. WAZIRI WA FEDHA: Taarifa ya Majumuisho ya Mpango Mkakati wa kujibu Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Wizara, Idara za Serikali na Mikoa (Vol. I na II) kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. III. MASWALI: Maswali ya yafuatayo yaliulizwa na kujibiwa:- (I) WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI – SWALI NA. 478, (II) WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI – SWALI NA. – 479, NA. 480 2 IV. MATANGAZO: Mheshimiwa Spika aliwatangazia Wabunge matangazo kama ifuatavyo:- - Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kutakuwa na kikao saa 7.00 mchana katika Ukumbi Na. 133. - Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira watakuwa na kikao leo saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa Basement. - Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali kutakuwa na kikao leo saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa Msekwa. - Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii watakuwa na kikao leo saa 7.00 mchana katika Ukumbi Msekwa C.
    [Show full text]
  • Tarehe 28 Aprili, 2017
    NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Nne – Tarehe 28 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Ester Michael Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum, kwa niaba yake Mheshimiwa Stanslaus Mabula. Na.110 Vigezo vya Kurasimisha Vibali vya Ajira na Kuishi Nchini MHE. STANSLAUS S. MABULA (K.n.y. MHE. ESTER M. MMASI) aliuliza:- Pamoja na juhudi za Serikali katika kulinda ajira za vijana wa Kitanzania, Serikali kupitia Sheria ya Ajira ya Wageni Na. 1 ya mwaka 2015 ilirasimisha vibali vya kuishi na ajira kwa wageni batili wapatao 317 kati ya 779. Je, ni vigezo gani vilivyotumika katika urasimishaji wa vibali hivyo wakati vijana wengi wa Kitanzania hususan 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wahitimu wa vyuo vikuu wanahangaika katika kupata ajira ili wafurahie faida ya taaluma zao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ester Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Kuratibu Ajira kwa Wageni Nchini Na.1 ya mwaka 2015 ilianza kutumika tangu tarehe 15/9/2015. Sheria hii imeweka utaratibu maalum kwa mtu anayetaka kumuajiri raia wa kigeni kuomba kibali cha ajira kwa Kamishna wa Kazi ambaye ndiye mwenye mamlaka pekee ya utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni nchini.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Nane
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Nane – Tarehe 24 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Mwaka 2019/2020. NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Ndanda sasa aulize swali lake. Na. 485 Utoaji wa Namba Vijiji vya Jimbo la Ndanda MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itasaidia na kufanikisha kutoa Namba kwa Vijiji vya Chipunda, Mkalinda na Sululu ya Leo vyenye wakazi zaidi ya elfu kumi katika Jimbo la Ndanda? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mheshimiwa David Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Jimbo la Ndanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Vijiji vya Chipunda na Sululu ni vijiji halali ambavyo vimeendelea pia kutambulika kupitia Matangazo ya Serikali Namba 536 Mamlaka za Miji na 537 Mamlaka za Wilaya ya tarehe 19/07/2019.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA 18 TAREHE 4 FEBRUARI, 2015 MREMA 1.Pmd
    4 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA __________________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Nane - Tarehe 4 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu tuanze. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na :- MHE. RIZIKI OMARI JUMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII): Taarifa ya Mwaka ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Katika Kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Katika Kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. 1 4 FEBRUARI, 2015 MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, Maswali yetu kama kawaida yanaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. David Malole, kwa niaba yake Mheshimiwa Hezekiah Chilibunje. MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, jina langu ninaitwa Hezekiah Chibulunje. Na. 83 Ujenzi wa Barabara za Dodoma Mjini MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE (K.n.y. MHE. DKT. DAVID M. MALOLE) aliuliza:- Serikali imefanya kazi nzuri ya kutengeneza barabara za Dodoma Mjini kupitia fedha za mfuko wa World Bank awamu ya kwanza:- Je, ni lini fedha za awamu ya Pili za World Bank zitatoka ili kukamilisha ujenzi wa barabara ambazo bado hazijawekewa lami katikati ya Mji wa Dodoma. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. David Mciwa Malole, Mbunge wa Dodoma Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2011 Mkoa wa Dodoma kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania (TSCP) ulitengewa kiasi cha dola za Kimarekani 2 4 FEBRUARI, 2015 milioni 32 kutoka Benki ya Dunia na Serikali ya Denmark kwa ajili ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita zipatazo 42 katika Mji wa Dodoma.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 21 Juni, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri. Tunaendelea na nifafanue tu hapa kwa kuwa Wizara hii au Ofisi ya Makamu ina masuala ya Muungano na Masuala ya Mazingira. Kwa hiyo watakuwa wanakuja Wenyeviti wawili na pengine kwenye Wasemaji Wakuu wa Upinzani pia wawili. Kwa hiyo, namwita sasa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala. Kwa niaba yake Mheshimiwa Paul Lwanji. MHE. JOHN P. LWANJI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Taarifa ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ukamilifu zaidi jina lake ni Mheshimiwa John Paul Lwanji. Sasa upande huo sasa mwakilishi wa Mwenyekiti wa Ardhi, Maliasili na Mazingira. MHE. ALI KHAMIS SEIF – MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ilikuwa taarifa yetu hatujaimaliza kidogo, labda tutaiwasilisha baadaye. 1 SPIKA: Lakini basi iwahi kabla ya saa saa tano, saa 4.30 MHE. ALI KHAMIS SEIF – MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Sawa sawa.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 17 Julai, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda ) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, leo ni siku ya alhamisi, kwa hiyo tuna kipindi kile cha Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kawaida yetu. Katibu tuendelee na Order Paper. MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Mgana Msindai. MHE. MGANA I. MSINDAI: Mheshimiwa Naibu Spika……! MHE. HAMAD RASHID MOHAMED: Mwongozo wa Spika. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mgana Msindai samahani naomba ukae. Nilikuwa sijamwangalia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Kwa kawaida utaratibu wetu hapa akiwepo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni inabidi yeye apewe nafasi ya kwanza ya kuuliza swali. Sasa nilikuwa nimepitiwa. Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. MHE. HAMAD R. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu mwaka 1992 Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Seif Sharrif Hamad, Waziri Kiongozi wa SMZ ilibaini kuwa kuna utata mkubwa katika 1 vifungu vingi vya Katiba na Mahakama ya Rufaa ikapendekeza kwa Mamlaka mbili kwamba zikae kitako ili kutatua matatizo hayo pamoja na vifungu vingine vya Katiba ambavyo vina utata. Tokea wakati huo mpaka leo Mamlaka hizo mbili hazijachukua hatua yoyote mpaka tumefikia leo kuna matatizo. Je, Mheshimiwa
    [Show full text]
  • UNDP TANZANIA MID-TERM EVALUATION of the LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT PHASE II (2017-2021) November 2019
    UNDP TANZANIA MID-TERM EVALUATION OF THE LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT PHASE II (2017-2021) November 2019 Disclaimer The Mid-term Evaluation of “UNDP TANZANIA LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT PHASE II 2017-2021” has been drafted by Tim Baker and Chris Awinia. The views expressed in this document are those of the authors and do not necessarily represent the views of these institutions. Project Title Legislative Support Project (LSP), Phase II Atlas ID Award 00095419, Project 0009425 Corporate Outcome Citizen expectations for voice, development, the rule of law and accountability are met by stronger systems of democratic governance Corporate Outputs Output 1: Increase the capacity of the National Assembly to effectively scrutinise legislation and its implementation and to monitor government performance in a participatory manner Output 2: More effective parliamentary scrutiny of government budget and expenditure, including monitoring of the Sustainable Development Goals (SDGs) Output 3: Enhance the capacity of the National Assembly to engage citizens and represent their interests in the work of the parliament Output 4: The National Assembly is more effectively engaged in strategic leadership, transparency and external engagement Output 5: Gender is mainstreamed in all functions of the National Assembly Country Tanzania Project Dates Start: 01 January 2017 Planned end: 31 December 2021 Project Budget USD $12,765,600 Funding Source DFID, Royal Danish Embassy, One Fund, Embassy of Ireland, TRAC Implementing party National Assembly Tanzania 2 Table
    [Show full text]