MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA TATU Kikao Cha
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Arobaini na Tatu – Tarehe 3 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Arobaini na Tatu. Katibu NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, aah sasa hivi unavaa sketi ndefu, hataki ugomvi na Mgogo. (Kicheko) Tunaendelea, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. NENELWA MWIHAMBI, ndc – KATIBU WA BUNGE: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri Mkuu karibu sana. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, nawakumbusha tena kuhusu maswali ya kisera sio matukio, sio nini, ni ya kisera. Tunaanza na Mheshimiwa Mbunge wa Liwale, Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka, maswali kwa kifupi. MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kwanza kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Spika, swali langu litahusu sekta ya korosho. Mwaka huu tumepata taarifa kwamba Serikali ilijipanga kutupatia pembejeo wakulima wa zao la korosho kwa maana kwamba waje kuzilipa baadaye kwenye mjengeko wa bei. Hata hivyo, kuna taharuki kubwa kwa wakulima wetu wa korosho baada ya Bodi ya Korosho kuleta waraka kwenye Halmashauri zetu, wakiwaambia kila mkulima akipeleka zao lile kwenye mnada kila kilo moja itakatwa shilingi 110 bila kujali kwamba mkulima yule amechukua pembejeo kwa kiwango gani. Barua ile inasema kwamba jambo hili hata sisi Wabunge tumeliridhia. Mheshimiwa Spika, sasa kuna taharuki kubwa sana kiasi kwamba mpaka… SPIKA: Swali lako ni nini katika jambo hilo? MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, kutokana na mkanganyiko huu ni nini kauli ya Serikali ili wakulima wetu waendelee kuchukua zile pembejeo maana sasa hivi wanaziogopa. SPIKA: Ahsante sana. Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuu, tafadhali. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Wizara yetu ya Kilimo imetoa miongozo kadhaa ya kuboresha masoko ya mazao nchini ili kuwanufaisha wakulima kwenye mazao wanayoyalima ikiwemo na kuwarahisishia namna nzuri ya kupata pembejeo. Zao la korosho ni miongoni mwa mazao ambayo Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kufanya mapitio ya maboresho ya namna nzuri ambayo wakulima ambao kwa sasa ndiyo wapo kwenye msimu wa kutumia pembejeo ili waweze kupata pembejeo wakulima wote na waweze kushiriki vizuri kwenye kilimo hiki. Mheshimiwa Spika, nakiri kwamba ipo taharuki kwa sababu na mimi ni mdau pia wa zao hilo lakini taharuki hii imetokana na vikao vya awali vya majadiliano ya mfumo mzuri ambao pia wakulima nao wanaweza kushiriki vizuri kupata pembejeo. Si kwamba Wabunge wameshiriki katika kutoa maamuzi, hapana, bali Wizara inaendelea kuwa na vikao vya mara kwa mara ili kufikia hatua nzuri ya kuwezesha kila mkulima kupata pembejeo. Vikao hivi bado havijakamilika na kikao kikubwa kabisa kipo tarehe 6 ambacho kinaalika wakulima, viongozi wa ushirika, viongozi wa Serikali na Waheshimiwa Wabunge pia mtaalikwa ambacho sasa tutajadili namna nzuri ya kumwezesha mkulima kupata pembejeo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, maelekezo ya awali ya kwamba kila mkulima atakatwa shilingi 110 yamesitishwa kwa muda ila wakulima wote waende kupata pembejeo zile ambazo zimepelekwa kwenye maeneo yale. Kiwango cha pembejeo kilichoagizwa kinatosha kabisa kwa kila mkulima kutokana na takwimu zilizopatikana kutoka vyama vyetu vya ushirika ili kila mkulima apate pembejeo ya kutosha kupuliza awamu zote nne kufikia kipindi cha uzalishaji. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kikao kile cha tarehe 6 ndicho kitakachotoa mwelekeo mzuri wa nini kitafanyika kwa 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) pembejeo ambazo zimetolewa na wala haitakuwa kumkata kila mkulima kwa kilo aliyoipeleka sokoni kwa sababu wapo wengine wana kilo mbili, wengine kilo 10 lakini wapo wamezalisha zaidi ya tani 20, sasa huwezi kukata kwa kila kilo. Kwa hiyo, hilo linafanyiwa kazi na Wizara na ufafanuzi utatolewa siku ya tarehe 6 ambapo wadau wa zao la korosho kila mmoja atashiriki kwenye eneo hili. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niwasihi wakulima wa zao la korosho waendelee kupokea pembejeo zile. Serikali inaendelea kuangalia namna bora ya kumfanya mkulima aweze kupata pembejeo kwa gharama nafuu ili aweze kuendelea kulima zao hilo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nataka niongezee eneo lingine ambalo pia limeleta mkanganyiko kwamba mabenki ambayo miaka yote yamekuwa yakitoa mikopo kwa wakulima, mwaka huu walisimama kutoa mikopo yao kwa hofu kwamba wakulima watakapopata pembejeo huku Serikalini hawataweza kulipa gharama ya mikopo ambayo wameikopa kwenye mabenki. Tumeruhusu mabenki yaendelee kukopesha wakulima kwa sababu bado kwenye zao la korosho kuna shughuli nyingi za kufanya; pamoja na kupilizia dawa lakini pia kuna kupalilia, kuokota na kuhakikisha zao linakwenda sokoni, yote inahitaji mtaji ambapo mkulima ambaye amelima, anajiamini kwamba atakopa na kurejesha, bado mabenki yaendelee kukopesha. Tumeshawapa maelezo hayo mabenki na wanaendelea na kukopesha. Kwa hiyo, wakulima waende wakakope kulingana na mahitaji yake ili alihudumie zao na hatimaye aweze kurejesha. (Makofi) Mheshimiwa Spika, napenda kuwaambia Waheshimiwa Wabunge wote wanaotoka kwenye majimbo yanayolima zao la korosho muendelee kuiamini Serikali na mifumo ambayo inaendelea kuipanga. Mifumo hii haiamuliwi tu moja kwa moja na Serikali bali inashirikisha wadau na kwa zao la korosho wadau tutakutana siku ya tarehe 6. Kwa hiyo, siku hiyo tutatoa mwelekeo wa zao hilo sote kwa Pamoja. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Kwa hiyo, wawe na amani na waendelee na uratibu wa zao hili la korosho, ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde, uliza swali lako kwa kifupi. MHE. ANTHONY P. MAVUNDE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwa mujibu wa kifungu cha 64(2)(c) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2016, sambamba na Tangazo la Serikali Na.30 la mwaka 2013 inazitaka taasisi nunuzi (procuring entity) zitenge asilimia 30 ya zabuni zake kwa mwaka kwa ajili ya vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kumekuwa na ulegelege katika utekelezaji wa takwa hili ambalo linawanyima fursa vikundi hivi muhimu, je, ni mkakati gani sasa ambao Serikali unauweka kuhakikisha kwamba takwa hili la kisheria linazingatiwa ili kuweza kuwapa fursa hizi vikundi vya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu? (Makofi) SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuu, tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mavunde, Mbunge wetu wa Dodoma Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli tumeweka sheria inayowezesha kila taasisi kutenga kiwango cha fedha kwa ajili ya kukopesha makundi kama alivyoyataja Mheshimiwa Mbunge lakini tunatambua zipo changamoto kwa baadhi ya taasisi kutotekeleza sheria hiyo huku wakitakiwa kutekeleza sheria hiyo. Serikali inaendelea kusisitiza na kuhamasisha taasisi zetu kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na hasa kwenye eneo hili la mikopo kwa sababu tunahitaji sasa Watanzania wanaotaka kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi au masuala ya kijamii wapate uwezesho wa kumudu kutekeleza wajibu huo. Maelekezo 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ambayo tunayo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba kila mtumishi wa umma aliyepo kwenye kitengo ambacho kimetakiwa kutoa mikopo hii, lazima afanye hivyo kwa sababu tayari pia Serikali huwa inatenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali na wale wote ambao wanatakiwa kupewa mikopo hiyo ikiwemo wanawake, vijana na walemavu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, msisitizo wa Serikali kwa kila mmoja kujishughulisha na masuala ya kiuchumi ni msisitizo ambao unatokana na malengo yaliyowekwa na utekelezaji ambao upo kwa taasisi hizo. Kwa hiyo, bado nitoe wito kila taasisi ambayo imetenga fedha hizo na sheria inamtaka kutoa mikopo hiyo bado waendelee kutoa mikopo kwa wahitaji ili kila mkopaji aweze kupata fedha hizo na aweze kuendesha miradi yake kadiri alivyojipanga. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nachotaka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kusisitiza kuhakikisha kwamba kila mmoja anatekeleza sheria ili wanufaika waweze kunufaika kwa utaratibu ambao tumejiwekea. Ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, Mbunge wa Msalala. MHE. IDDI S. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Tunatambua kwamba Serikali yetu ilizuia kabisa usafirishwaji wa makinikia nje ya nchi na kwa sasa tumeshuhudia makontena ya makinikia yakisafirishwa kupitia barabara ya Bulyanhulu – Kahama na Bandari yetu ya Dar es salaam hivyo kupelekea taharuki kwa Watanzania na kwa wananchi wa Jimbo la Msalala. Nini sasa kauli ya Serikali juu ya jambo hili? Ahsante. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu tafadhali WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Iddi, Mbunge wa Msalala, kama ifuatavyo: - 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, nami nimeona pia kwenye mitandao watu wakionesha kwamba wanaona makontena ya makinikia yakisafirishwa kwenda nje. Nataka niwakumbushe Watanzania