Tarehe 5 Aprili, 2019
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _______ MAJADILIANO YA BUNGE _______ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Nne -Tarehe 5 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu! NDG. ATHUMANI HUSSEIN – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Maulid Said Mtulia, Mbunge wa Kinondoni, sasa aulize swali lake. Na 24 Idadi ya Watu Wenye Ulemavu Nchini MHE. MAULID S. MTULIA aliuliza:- Walemavu wana mahitaji maalum ukilinganisha na watu wasiokuwa na Ulemavu na idadi ya walemavu imekua ikiongezeka siku hadi siku kutokana na ajali za barabarani hasa zitokanazo na usafiri wa bodaboda:- (a) Je, Serikali inaweza kutoa orodha ya idadi ya watu wenye ulemavu nchini kwa kuzingatia makundi yao kwa asilimia? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (b) Je, Serikali ina mpango gani mahususi wa kuwajengea uwezo wa kujitegemea watu wenye ulemavu hasa Vijana, Watoto na Wanawake ili kuondoa utamaduni wa kuendesha maisha yao kwa kuombaomba? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maulid Said Mtulia, Mbunge wa Kinondoni lenye kipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, idadi ya Watu wenye Ulemavu kwa kuzingatia makundi yao na kwa asilimia ni kama ifuatavyo:- Watu wenye Ualbino ni 16,477 sawa na 0.04%; walemavu wasioona ni 848,530, sawa na 1.93%; walemavu ambao ni viziwi ni 425,322, swan a 0.97%; walemavu wa viungo ni 525,019, sawa na 1.19%; walemavu wa kumbukumbu ni 401,931, sawa na 0.91%; walemavu wa kujihudumia ni 324,725, sawa na 0.74%; na Ulemavu mwingine, yaani kwa ujumla wake ni 99,798, sawa na 0.23%.
[Show full text]