Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania Mkutano Wa Tatu Yatokanayo Na Kikao Cha Kumi Na Sita 10 Mei, 2016
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA TATU YATOKANAYO NA KIKAO CHA KUMI NA SITA 10 MEI, 2016 MKUTANO WA TATU YATOKANAYO NA KIKAO CHA KUMI NA SITA TAREHE 10 MEI, 2016 I. DUA: Saa 3.00 asubuhi Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) alisoma Dua na Kuongoza Bunge. Makatibu Mezani 1. Ndg. Ramadhani Issa 2. Ndg. Asia Minja II. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani. 1. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto aliwasilisha Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. 2. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aliwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017. 3. Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama aliwasilisha Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. 4. Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara aliwasilisha taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. III. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa; OFISI YA WAZIRI MKUU: Swali Na.130 – Mhe. Flatei Gregory Massay [Kny. Mhe. Ester Alexander Mahawe] Swali la nyongeza: Mhe. Flatei Gregory Massay OFISI YA RAIS (TAMISEMI): Swali Na.131 – Mhe. Augustino Manyanda Masele Swali la nyongeza: Mhe. Augustino Manyanda Masele 2 Swali Na.132 – Mhe. Bonnah Moses Kaluwa Swali la nyongeza: (i) Mhe. Bonnah Moses Kaluwa (ii) Mhe. Anatropia Theonest Lwehikila Swali Na.133 – Mhe. Ally Seif Ungando Swali la nyongeza: (i) Mhe. Ally Seif Ungando (ii) Mhe. Esther Amos Bulaya WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Swali Na.134 – Mhe. Susan Anselm Lyimo [kny. Naghenjwa Kaboyoka] Swali la nyongeza: (i) Mhe. Susan Anselm Lyimo (ii) Mhe. Rashid Abdallah Shangazi Swali Na.135 – Mhe. George Malima Lubeleje Swali la nyongeza: Mhe. George Malima Lubeleje WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Swali Na.136 – Mhe. Ali Hassan Omar King Swali la nyongeza: (i) Mhe. Ali Hassan Omar King (ii) Raisa Abdallah Mussa WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Swali Na.137 – Mhe. Muhammed Amour Muhammed Swali la nyongeza: Mhe. Muhammed Amour Muhammed WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Swali Na.138 – Mhe. Gimbi Dotto Masaba Swali la nyongeza: (i) Mhe. Gimbi Dotto Masaba (ii) Mhe. Andrew John Chenge WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Swali Na.139 – Mhe. Venance Mwamoto [kny. Mhe. Hafidh Ali Tahir] Swali la nyongeza: (i) Mhe. Venance Mwamoto MATANGAZO: - Wageni wote waliokuwepo Bungeni walitambulishwa. - Kamati zifuatazo zilitangazwa kuwa na vikao mchana:- i) Kamati ya Uongozi ii) Kamati ya Sheria Ndogo iii) Chama cha Wabunge Wanawake (TPWG) 3 IV. HOJA ZA SERIKALI: - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aliwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 ; - Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama aliwasilisha maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka 2016/17; - Mhe Juma Hamad Omar, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani aliwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Uchangiaji wa jumla ulianza na Wabunge wafuatao walipata nafasi ya kuchangia:- 1) Mhe. Shamsi Vuai Nahodha - CCM 2) Mhe. Halima James Mdee - CHADEMA Taarifa: Mhe. Suleiman Masoud Nchambi alimpa taarifa mzungumzaji kwamba Hospitali za Jeshi hazichomi watu sindano za sumu vinginevyo atoe ushahidi. Mwenyekiti alitoa mwongozo kwamba mzungumzaji alisema kuna hisia na kumruhusu kuendelea kuchangia. 3) Mhe. Mussa Azzan Zungu - CCM 4) Mhe. Yussuf Salim Hussein - CUF MWONGOZO WA SPIKA: Mhe. Jenista Mhagama aliomba mwongozo kuhusu kauli ya Mhe. Yussuf Salim Hussein kwamba Zanzibar Jeshi lilifanya Mapinduzi ya uchaguzi ambayo kiti kilimtaka aifute na hakufanya hivyo. Hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 68(1) (a) kauli hiyo ni ya uongo na ni hatua gani sasa ichukuliwe baada ya kukataa kufuta kauli. Kiti kilimtaka afute kauli hiyo mwanzoni alikataa kufuta na baada ya ufafanuzi wa kiti alifuta kauli hiyo. Kiti kiliagiza kauli hiyo kutoonekana kabisa kwenye kumbukumbu za Bunge (Hansard). 5) Mhe. Allan Joseph Kiula - CCM 6) Kanali Mst. Masoud Ali Salum - CCM 7) Mhe. Maryam Salum Msabaha - CHADEMA 4 V. KUSITISHA BUNGE: Saa 7.00 mchana Bunge lilisitishwa hadi saa 10.00 jioni. VI. BUNGE KUREJEA: Saa 10.00 Bunge lilirejea na kuongozwa na Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson. VII. UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA BUNGE: Katibu wa Bunge alitoa maelezo ya awali ya uchaguzi kwamba Kamati ya Uongozi imemteua Mhe. Mussa Azzan Zungu kuwa Mwenyekiti wa Bunge na kwa mujibu wa taratibu kwa vile ni jina moja hivyo amepita bila kupingwa hivyo Naibu Spika alimtangaza Mhe. Mussa Azzan Zungu kuwa Mwenyekiti wa Bunge. Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa uliendelea kwa wafuatao kuchangia. 8) Mhe. Mattar Ali Salum - CCM 9) Mhe. Mwantumu Dau Haji - CCM 10) Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda - CHADEMA Mhe. Mattar Ali Salum alimtaka mzungumzaji kufuta maneno yake ya kumdhalilisha Mhe. Mwantumu Dau Haji kwamba hajui alichoongea. Kiti kilisema alichosema Mbunge ni kwamba amekosea siyo kama alivyosema. Mhe. Sophia Mwakagenda alikataa taarifa hiyo. 11) Mhe. Hajji Khatib Kai - CUF 12) Mhe. Fakharia Shomar Khamis - CCM 13) Mhe. Khadija Hassan Aboud - CCM Taarifa: Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara alitumia Kanuni ya 68(7) kumpa taarifa Mhe. Khadija Hassan Aboud kwamba kwa maelezo yake anakubali Jeshi lilikwenda Zanzibar. Mhe. Khadija alikataa taarifa hiyo. 14) Mhe. Saed Ahmed Kubenea - CHADEMA Taarifa: Mhe. Suleiman Masoud Nchambi alitoa taarifa kwamba mzungumzaji ametoa taarifa za uongo kwa kuzungumzia hekari 26,000 kwa eneo la Masaki jambo ambalo siyo kweli kwani Masaki ni ndogo. Mhe. Kubenea alikataa taarifa hiyo akisema amesema mita za mraba. 5 15) Mhe. Ali Hassan Omar King - CCM 16) Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo - CCM 17) Mhe. Suleiman Masoud Nchambi - CCM Taarifa: Mhe. Mchungaji Peter Msigwa alisema mzungumzaji anatugombanisha Jeshi na Kambi Rasmi ya Upinzani wao kama Kambi wanaliheshimu Jeshi tofauti na anavyosema, Mchangiaji alikataa taarifa hiyo. Mwongozo wa Spika: Mhe. Jenista Mhagama alitumia Kanuni ya 68(7) akitaka mwongozo wa kiti kwani Wabunge hawachangii kuboresha Hoja iliyopo mezani na kwamba imezuka tabia Wabunge wa CCM wanapochangia hukatishwa na Wabunge kusema mambo yasiyo ya kweli kama Mhe. Halima Mdee alivyosema kwamba yeye chief Whip anawaambia wana CCM nini cha kusema na kusisitiza vitendo hivyo ni kupoteza muda wa Bunge. Kiti kielekeze Wabunge kuzingatia utaratibu. 18) Mhe. Daniel Edward Mtuka - CCM 19) Mhe. Sadifa Juma Hamis - CCM Taarifa: Mhe. Maftaha Abdallah Nachuma alitumia kanuni ya 68(8) kwamba maneno aliyotumia mzungumzaji kwamba viongozi wahuni walijitangazia matokeo na kwamba ndiyo maana Jeshi halikuingilia kati siyo ya kweli kwa vile ni watulivu bali kitendo hicho hakikuwepo. 20) Mhe. Angelina Adam Malembeka - CCM Naibu Spika alitumia Kanuni ya 72(1) na 64(1)(a) alimtaka Mhe. Angelina Adam Malembeka kufuta kauli yake kwamba jeshini kuna ukabila. Mhe. Malembeka alikubali kufuta kauli hiyo. Mawaziri wafuatao walichangia:- 21) Mhe. January Makamba 22) Mhe. Nape Moses Nnauye. Taarifa: Mhe. Mch. Peter Simon Msigwa alitumia K.64 (1) (a) amesema uongo Ma-DC na Ma – RC ni wana CCM siyo kama anavyosema kwani wanahudhuria vikao vya chama. Kiti kilitoa mwongozo kwamba Mhe. Nape Nnauye ameeleza kwa mujibu 6 wa katiba ya CCM kwamba kuna Ma-DC au Ma –RC ambao siyo wana CCM na hawahudhurii vikao vya chama. 23) Mhe. Jenista Joakim Mhagama 24) Mwanasheria Mkuu wa Serikali 25) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa KAMATI YA MATUMIZI: Bunge liliingia katika hatua ya Kamati ya Matumizi ili kupitia Vifungu vya Wizara na hatimaye kupitisha Bajeti husika baada ya kuhojiwa. Mwongozo wa spika: Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara alitumia kanuni ya 68(7) na kusema kwamba Mhe. Nape Nnauye amelidanganya Bunge kwa kueleza kwamba Wakuu wa Mikoa na Wilaya si Wajumbe wa Kamati za Siasa za CCM kitu ambacho siyo cha kweli kwa kuwa Wakuu hao huingia kwenye Vikao hivyo; Kiti kilieleza kuwa alichosema Mhe. Nape Nnauye ni kwamba Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Wanachama wa CCM ndio huingia kwenye Vikao hivyo na wale ambao si Wanachama hawaingii. Mhe. Nape Nnauye – aiomba mwongozo kwa kutumia Kanuni ya 68(7) kwamba tabia ya kuzomea wakati wengine wakiongea hasa Wapinzani inavuruga Bunge, kiti kinavumilia, alitaka kujua kama vitendo hivyo vinaruhusiwa. Kiti kilielekeza kuvumiliana na Wabunge wafuate taratibu na kiti kitazingatia hilo. Mhe. Suleiman Maosud Nchambi – alitumia Kanuni ya 64(1)(a) na (68(1) kueleza kuhusu kauli ya Mhe. Saed Kubenea kwamba Jeshi lilitaka kununua Silaha feki athibitishe au afute kauli. Kiti kiliahidi kutoa maelezo baadaye pamoja na hoja ya Waziri aliyoomba kuhusu Mhe. Saed Kubenea alichosema kuhusu ujenzi wa nyumba yake kama Waziri. VIII. KUAHIRISHA SHUGHULI ZA BUNGE Saa 2.30 Usiku Bunge liliahirishwa hadi tarehe 11/5/2016 siku ya Jumatano saa 3.00 asubuhi. 7 DODOMA DKT. T. D. KASHILILAH 10 MEI, 2015 KATIBU WA BUNGE 8 .