MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Arobaini Na Sita

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Arobaini Na Sita NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 15 Juni, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, tunaendelea na Mkutano wetu wa 19, Kikao cha 46, bado kimoja tu cha kesho. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na: NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 (Monetary Policy Statement for the Financial Year 2020/2021). MHE. ALBERT N. OBAMA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI:Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. RHODA E. KUNCHELA - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). MHE. DKT. TULIA ACKSON - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KANUNI ZA BUNGE: Azimio la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Bunge SPIKA: Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika, Katibu MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 426 Migogoro ya Mipaka MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:- Kumekuwepo na migogoro mingi ya mipaka katika ngazi za Mitaa, Kijiji, Kata, Wilaya na hata Mkoa hali inayosababisha maeneo husika kutotambua vizuri wakazi wake:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo hilo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Nassor Kisangi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura 288 na Sheria ya Mipango Miji, Na.8 ya mwaka 2007 zimeweka utaratibu wa kuzingatia wakati wa kuanzisha na kusimamia Maeneo ya Utawala (Mitaa, Vijiji, Kata, Wilaya na hata Mikoa). Utaratibu huo, pamoja na mambo mengine, unahusisha kuandaa Matangazo ya Serikali (Government Notice-GN) yenye maelezo ya mipaka ya ardhi ya kila eneo la utawala hasa wakati wa uanzishaji wa mamlaka hizo. Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kumekuwepo na changamoto kadhaa ikiwemo: Kutotafsiriwa vyema matangazo hayo ya Serikalini ardhini jambo linalosababisha wananchi kutotambua vizuri mipaka hiyo na hivyo kuleta migogoro na wananchi kutozingatia ipasavyo mipaka kama ilivyobainishwa kwenye Matangazo ya Serikali. Ili kukabiliana na changamoto hizo, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inapitia na kuboresha Mwongozo wa Uanzishwaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wa mwaka 2014 ambao utapaswa kuzingatiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zote wakati wa kuanzisha maeneo mapya au kupandisha hadhi maeneo ya utawala. Mheshimiwa Spika, katika utaratibu huo, kusudio la kuanzisha eneo jipya la utawala (Kiijiji, Kata, Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji) lililojadiliwa na vikao stahiki lazima liambatane na Rasimu ya Ramani inayoainisha mipaka ya kijiografia ya mamlaka inayopendekezwa kuanzishwa pamoja na rasimu ya ramani ya mamlaka inazopakana nazo. Aidha, ili kuondoa migogoro, uhakiki wa ramani hizo uwandani utafanyika kabla ya Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa kutoa kibali cha uanzishaji wa mamlaka hizo. Mheshimiwa Spika, katika Mamlaka za zamani (zisizo mpya), Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeendelea kutatua migogoro ya mipaka kwa kupitia na kutafsiri ardhini Matangazo mbalimbali ya Serikali yaliyoanzisha Wilaya na Mikoa husika na kuondoa mkanganyiko wa mipaka. Pia, Ofisi ya Rais, TAMISEMI 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) inaandaa mfumo wa usajili wa maeneo ya utawala kwa njia ya kielektroni unaoitwa Administrative Areas Registration System-AReS ambao utazuia mwingiliano (overallaping) wa mipaka na hivyo kupunguza migogoro. Na. 427 Hitaji la Gari la Wagonjwa Kituo cha Afya Bwisya MHE. KEMILEMBE J. LWOTA aliuliza:- Kituo cha Afya cha Bwisya kilichoko Kisiwani Ukara kimekarabatiwa kwa kiwango kikubwa na kuwa na hadhi ya hospitali; Serikali iliahidi kupeleka gari la wagonjwa toka mwaka juzi lakini bado gari hilo halijapelekwa:- Je, ni lini gari la wagonjwa litapelekwa katika Kituo hiki? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kamilembe Julius Lwota, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kulingana na mazingira ya kituo hiki, kuna hitaji la usafiri kwa ajili ya wagonjwa kutoka kisiwa cha Ukara kwenda maeneo mengine hususan Hospitali ya Nansio ambayo iko kwenye Kisiwa cha Ukerewe. Kwa kuwa visiwa hivi vimetanganishwa na maji, Serikali imeona umuhimu wa kutengeneza boat ambulance mpya kwa ajili ya Kisiwa cha Ukara badala ya kununua gari. Boti hiyo imekamilika na inatumika. Na. 428 Mradi wa Maji wa Lwakajungu – Karagwe MHE. ALFREDINA A. KAHIGI aliuliza:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mradi wa maji Ziwa Lwakajungu uliopo Wilayani Karagwe, Mkoani Kagera unaoanzia Kata ya Bweranyange mpaka Nyaishozi ulianza tangu mwaka 2005 lakini mpaka sasa hakuna jitihada zinazoonekana:- Je, ni lini Serikali itawapatia wananchi hao maji ya uhakika na kuwatua ndoo kichwani wanawake wa wilaya hiyo? WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alfredina Apolinary Kahigi, Mbunge wa Viti Maalum, Kagera, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya India imeingia Mkataba wa Mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maji na Usafi wa Mazingira katika miji 28 ukiwemo Mji wa Kayanga/Omurushaka ambao ni Makao Makuu ya Wilaya ya Karagwe. Mwezi Mei, 2019 Wizara ya Maji iliingia Mkataba na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa miradi katika miji hiyo ukiwemo Mji wa Kayanga. Mheshimiwa Spika, kwa sasa taratibu za manunuzi ya Wakandarasi zinaendelea ambapo ujenzi wa miradi unatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2020. Mradi huu utakapokamilika unatarajiwa kunufaisha wananchi wapatao milioni nne kwa kuanzia na wananchi milioni sita ifikapo mwaka 2040 katika miji 28. Na.429 Uchakavu wa Mitambo – Skimu ya Maji Makonde MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Skimu ya Maji ya Makonde inakabiliwa na tatizo kubwa la uchakavu wa mitambo na umeme usio wa uhakika na hivyo kushindwa kusambaza maji hadi Mji wa Nanyamba. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo hilo? WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, eneo la Mamlaka ya Maji Makonde ina jumla ya watu 510,975 wenye mahitaji ya maji mita za ujazo 766,462 kwa mwezi. Maeneo yaliyofikiwa na miundombinu ya maji yana wakazi wapatao 275,928.00 wenye mahitaji ya maji mita za ujazo 413,892 kwa mwezi sawa na asilimia 54 ya mahitaji ya wakazi wote wa Mamlaka ya Maji Makonde. Miundombinu iliyopo inaweza kuzalisha maji mita za ujazo 482,400 kwa mwezi kiasi ambacho kinakidhi mahitaji ya watu wote waliofikiwa na mtandao wa maji. Mheshimiwa Spika, kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji na matengenezo, uwekezaji umepangwa kuelekezwa kwenye chanzo cha Mitema kwani chanzo hicho kina gharama za umeme nafuu zaidi katika uzalishaji maji na uwezo wa chanzo hiki ni mkubwa kuliko vyanzo vingine na unaotosheleza mahitaji ya wakazi wote na kijiografia kiko katikati ya eneo la Mamlaka ya Maji Makonde. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha wananchi wanaoishi maeneo yanayohudumiwa na Mamlaka ya Maji Makonde wanapata huduma ya maji, Serikali kupitia Wizara ya Maji ikishirikiana na Wadau wa Maendeleo imetoa kipaumbele katika uboreshaji wa huduma ya maji katika Mamlaka hiyo. Katika kipindi kilichoanzia mwaka 2015 hadi 2020, miradi yenye thamani ya Shilingi 13,436,000,000 imetekelezwa na miradi mingine inaendelea kujengwa. Aidha, Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tatizo la uchakavu wa mitambo, miundombinu na umeme usio wa uhakika kwa kufanya marekebisho ya mitambo iliyopo pamoja na kutoa kipaumbele katika matumizi ya nishati jadilifu na hatimaye kupunguza gharama za uendeshaji kwa wananchi. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 430 Hitaji la Baraza la Ardhi la Wilaya MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI aliuliza:- Wilaya ya Busega haina Baraza la Ardhi na hivyo kupelekea kesi za ardhi za wilaya hiyo kupelekwa wilaya za jirani: - Je, ni lini Busega watapatiwa Baraza la Ardhi la Wilaya? WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Raphael Masunga Chegeni, Mbunge wa Busega, kama ifuatavyo: - Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi sasa imeunda jumla ya Mabaraza 111 ambapo kati ya hayo, Mabaraza 55 yanatoa huduma na Mabaraza 56 hayajaanza kutoa huduma kutokana na changamoto za uhaba wa rasilimali watu na majengo ya ofisi. Ili Baraza liweze kutoa huduma linahitaji kuwa na jengo la ofisi pamoja na watumishi, yaani angalau Mwenyekiti wa Baraza mmoja, Katibu Muhtasi, Msaidizi wa Kumbukumbu, Msaidizi wa Ofisi, Dereva na Mlinzi. Mheshimiwa Spika, taratibu za ajira kupata watumishi zitakapokamilika, wananchi wa Wilaya ya Busega watapewa kipaumbele kwa kufungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ili kuondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya lililopo Maswa. Aidha, natoa rai kwa uongozi wa Wilaya ya Busega waweze kuandaa na kutoa jengo litakalofaa kutumika kwa matumizi ya Ofisi ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, tukiwa tunasubiri upatikanaji wa watumishi wa kuhudumia Baraza hilo. 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 431 Upatikanaji wa Chanjo ya Mama na Mtoto – Katavi MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Katavi ni Mkoa wa mwisho katika upatikanaji wa chanjo kwa mama na mtoto:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha akinamama na watoto wa Mkoa wa Katavi wanapata chanjo.
Recommended publications
  • 9Aprili,2013
    9 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kwanza - Tarehe 9 Aprili, 2013 WIMBO WA TAIFA (Hapa Waheshimiwa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa) (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa msimame tena. Mtakumbuka kwamba wakati wa Vikao vyetu vya Kamati, kwa bahati mbaya sana tulimpoteza mpenzi wetu Mheshimiwa Salim Hemed Khamis. Kwa hiyo, tumkumbuke kwa dakika moja. (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa Dakika moja kumkumbuka Mheshimiwa Salim Hemed Khamis aliyekuwa Mbunge wa Chambani Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amin. Ahsanteni sana na karibuni tukae. 1 9 APRILI, 2013 Waheshimiwa Wanbunge, katika Mkutano wa Tisa, Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya Serikali uitwao The Plant Breeders` Rights Bill, 2012, kwa taarifa hii napenda kulialifu Bunge hili Tukufu kwamba, Mswada huo umekwisha pata kibali cha Mheshimiwa Rais na kuwa Sheria ya nchi iitwayo: The Plant Breeders` Rights Act, 2012 Na. 9 ya mwaka 2012. Kwa hiyo, ule sasa ni sheria ya Nchi. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kuwasilisha mezani Taarifa ya Matoleo yote ya Gazeti la Serikali pamoja na nyongeza zake zilizochapishwa tangu Kikao cha mwisho cha Mkutano wa Bunge uliopita. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. MASWALI NA MAJIBU Na. 1 Kujenga Barabara ya Old Moshi kwa Lami MHE. GODFREY W. ZAMBI (K.n.y. MHE. DKT. CYRIL A. CHAMI) aliuliza:- Je, Serikali itatekeleza lini ahadi ya kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Old Moshi inayoanzia Kiboriloni kupitia Kikarara, Tsuduni hadi Kidia? 2 9 APRILI, 2013 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015 ELECTION EDITION: MAGUFULI vs LOWASSA Profiles of Key Candidates Petroleum Bills Ruaha’s “Missing” Elephants ta112 - final.indd 1 8/25/2015 12:04:37 PM David Brewin: SURPRISING CHANGES ON THE POLITICAL SCENE As the elections approached, during the last two weeks of July and the first two weeks of August 2015, Tanzanians witnessed some very dra- matic changes on the political scene. Some sections of the media were even calling the events “Tanzania’s Tsunami!” President Kikwete addessing the CCM congress in Dodoma What happened? A summary 1. In July as all the political parties were having difficulty in choosing their candidates for the presidency, the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) party decided to steal a march on the others by bringing forward their own selection process and forcing the other parties to do the same. 2. It seemed as though almost everyone who is anyone wanted to become president. A total of no less than 42 CCM leaders, an unprec- edented number, registered their desire to be the party’s presidential candidate. They included former prime ministers and ministers and many other prominent CCM officials. 3. Meanwhile, members of the CCM hierarchy were gathering in cover photos: CCM presidential candidate, John Magufuli (left), and CHADEMA / UKAWA candidate, Edward Lowassa (right). ta112 - final.indd 2 8/25/2015 12:04:37 PM Surprising Changes on the Political Scene 3 Dodoma to begin the lengthy and highly competitive selection process. 4. The person who appeared to have the best chance of winning for the CCM was former Prime Minister Edward Lowassa MP, who was popular in the party and had been campaigning hard.
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 7 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA KIKAO CHA NNE – 7 NOVEMBA, 2014 Kikao kilianza saa 3:00 Asubuhi kikiongozwa na Mhe. Job Y. Ndigai, Mb Naibu Spika ambaye alisoma Dua. MAKATIBU MEZANI 1. Ndg. Charles Mloka 2. Ndg. Lina Kitosi 3. Ndg. Hellen Mbeba I. MASWALI YA KAWAIDA Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge na kupitia majibu Bungeni:- 1. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 38 la Mhe. Anne Kilango 2. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 39 la Mhe. Salum Khalfan Barwary 3. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 40 la Mhe. Moses Joseph Machali 4. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – swali na. 41. La Mhe. Omar Rashid Nundu 5. Wizara ya Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi – swali na. 42. La Mhe. Hilda Ngoye 6. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – swali na. 43. La Mhe. Zitto Kabwe Zuberi 7. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tecknolojia – swali na. 44 –la Mhe. Murtaza Mangungu 8. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - swali na. 45-la Mhe. Godfrey Mgimwa 9. Wizara ya Katiba na Sheria - swali na. 46 – la Mhe. Neema Mgaya Hamid 2 10. Wizara ya Katiba na Sheria- swali na. 47 – la Mhe. Assumpter Mshana 11. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo – swali na. 48 la Mhe. Khatib Said Hji. 12. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - swali na. 49 la Mhe.
    [Show full text]
  • Tanzania Budget Speech 2021
    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA SPEECH BY THE MINISTER FOR FINANCE AND PLANNING, HON. DR. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU (MP), PRESENTING TO THE NATIONAL ASSEMBLY, THE ESTIMATES OF GOVERNMENT REVENUE AND EXPENDITURE 10thJune2021 Dodoma 0 “I urge businessmen to pay taxes. It is neither right nor fair for them to evade taxes. Evading taxes will make our Government fail to provide essential services for the people. Our hospitals will run out of medicines that may lead to deaths, Government employees will not get salaries and other statutory benefits and students will be denied fee free education which is granted to them” Her Excellency Samia Suluhu Hassan The President of the United Republic of Tanzania 14th May 2021 1 I. INTRODUCTION 1. Honourable Speaker, I beg to move that your esteemed House resolves to receive, debate and approve the Government’s Revenue and Expenditure Estimates for the financial year 2021/22. This speech presents the first national budget of the Sixth Phase Government under the leadership of Her Excellency Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania. The Estimates of the Government Revenue and Expenditure are submitted to your esteemed House in accordance with Article 137 of the Constitution of the United Republic of Tanzania of 1977; Section 23 (3) of the Budget Act, CAP 439; and Article 124 (4) of the Standing Orders of Parliament, June 2020 Edition. 2. Honourable Speaker, together with this speech, I submit four volumes of budget books: Volume I provides Revenue Estimates; Volume II provides Recurrent Expenditure Estimates for Ministries, Independent Departments and Agencies; Volume III covers Recurrent Expenditure Estimates for Regional Secretariats and Local Government Authorities; and Volume IV is for Development Expenditure 2 Estimates for Ministries, Independent Departments, Agencies, Regional (ii (MPRU) Reserves Marine (i) follows: as shall be distribution percentage The Act.
    [Show full text]
  • Hotuba Ya Waziri Wa Mambo Ya Nje Na
    HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MHESHIMIWA BERNARD KAMILLIUS MEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuliongoza kwa umahiri mkubwa Bunge hili la Bajeti la mwaka 2012/2013. Napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb.), Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wanaokusaidia kuongoza Bunge hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. 3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya Nne. Chini ya uongozi wake Taifa letu limeendeleza utamaduni wetu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano. Nawaomba Watanzania wote tuendelee kudumisha hali hiyo ili kuimarisha umoja wetu ambao ni tunu isiyopatikana kwa bei yoyote. 4. Mheshimiwa Spika, niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge wengine wote walionitangulia kuwapongeza kwa dhati kabisa Waheshimiwa Wabunge wapya, Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei 2012. Nawapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge waliochaguliwa kipindi hiki kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye nafasi mbalimbali humu Bungeni na ndani ya Serikali.
    [Show full text]
  • Election Violence in Zanzibar – Ongoing Risk of Violence in Zanzibar 15 March 2011
    Country Advice Tanzania Tanzania – TZA38321 – Revolutionary State Party (CCM) – Civic United Front (CUF) – Election violence in Zanzibar – Ongoing risk of violence in Zanzibar 15 March 2011 1. Please provide a background of the major political parties in Tanzania focusing on the party in power and the CUF. The United Republic of Tanzania was formed in 1964 as a union between mainland Tanganyika and the islands of Unguja and Pemba, which together comprise Zanzibar. Since 1977, it has been ruled by the Revolutionary State Party (Chama Cha Mapinduzi or CCM). In 1992 the government legislated for multiparty democracy, and the country is now a presidential democratic republic with a multiparty system. The first multiparty national elections were held in 1995, and concurrent presidential and parliamentary elections have since been held every 5 years. The CCM has won all elections to date. The CUF, founded in 1991, constituted the main opposition party following the 1995 multiparty elections.1 At the most recent elections in October 2010, the CCM‟s Jakaua Kikwete was re-elected President with 61.7% of the vote (as compared to 80% of the vote in 2005) and the CCM secured almost 80% of the seats. Most of the opposition votes went to the Chadema party, which displaced the Civic United Front (CUF) for the first time as the official opposition. The opposition leader is Chadema‟s Chairman, Freeman Mbowe. Chadema‟s presidential candidate, Willibrod Slaa, took 27% of the vote, while CUF‟s Ibrahim Lipumba received 8%.2 Notwithstanding the CCM‟s election success, the BBC reports that Kikwete‟s “political legitimacy has been seen by some to have been somewhat dented in the 2010 elections”, given the decline in his percent of the vote, and a total election turnout of only 42%, down from 72% in 2005.
    [Show full text]
  • Tanzanian State
    THE PRICE WE PAY TARGETED FOR DISSENT BY THE TANZANIAN STATE Amnesty International is a global movement of more than 7 million people who campaign for a world where human rights are enjoyed by all. Our vision is for every person to enjoy all the rights enshrined in the Universal Declaration of Human Rights and other international human rights standards. We are independent of any government, political ideology, economic interest or religion and are funded mainly by our membership and public donations. © Amnesty International 2019 Except where otherwise noted, content in this document is licensed under a Creative Commons Cover photo: © Amnesty International (Illustration: Victor Ndula) (attribution, non-commercial, no derivatives, international 4.0) licence. https://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/4.0/legalcode For more information please visit the permissions page on our website: www.amnesty.org Where material is attributed to a copyright owner other than Amnesty International this material is not subject to the Creative Commons licence. First published in 2019 by Amnesty International Ltd Peter Benenson House, 1 Easton Street London WC1X 0DW, UK Index: AFR 56/0301/2019 Original language: English amnesty.org CONTENTS EXECUTIVE SUMMARY 6 METHODOLOGY 8 1. BACKGROUND 9 2. REPRESSION OF FREEDOM OF EXPRESSION AND INFORMATION 11 2.1 REPRESSIVE MEDIA LAW 11 2.2 FAILURE TO IMPLEMENT EAST AFRICAN COURT OF JUSTICE RULINGS 17 2.3 CURBING ONLINE EXPRESSION, CRIMINALIZATION AND ARBITRARY REGULATION 18 2.3.1 ENFORCEMENT OF THE CYBERCRIMES ACT 20 2.3.2 REGULATING BLOGGING 21 2.3.3 CYBERCAFÉ SURVEILLANCE 22 3. EXCESSIVE INTERFERENCE WITH FACT-CHECKING OFFICIAL STATISTICS 25 4.
    [Show full text]
  • Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Sita – Tarehe 4 Februari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Katibu tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na Mkutano wetu wa Kumi na Nane, kikao cha leo ni kikao cha tano, Katibu NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazi Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- (i) Toleo Namba 46 la tarehe 8 Novemba, 2019 (ii) Toleo Namba 47 la tarehe 15 Novemba, 2019 (iii) Toleo Namba 48 la tarehe 22 Novemba, 2019 (iv) Toleo Namba 49 la tarehe 29 Novemba, 2019 (v) Toleo Namba 51 la tarehe 13 Desemba, 2019 (vi) Toleo Namba 52 la tarehe 20 Desemba, 2019 (vii) Toleo Namba 53 la tarehe 27 Desemba, 2019 (viii) Toleo Namba 1 la tarehe 3 Januari, 2020 (ix) Toleo Namba 2 la terehe 10 Januari, 2020 (x) Toleo Namba 3 la tarehe 17 Januari, 2020 (xi) Toleo Namba 4 la terehe 24 Januari, 2020 MHE. JASSON S. RWEIKIZA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za MItaa kuhuus shughuli za Kamati hii kwa Mwaka 2019. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Kmaati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu shughuli zilizotekelezwa na Kamati hiyo kwa kipindi cha kuanzia Februari, 2019 hadi Januari, 2020.
    [Show full text]
  • In the High Court of the United Republic of Tanzania
    IN THE HIGH COURT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA (MAIN REGISTRY) AT PAR ES SALAAM (MAIGE, MAGOIGA AND KULITA, JJJ) MISC CIVIL CAUSE NO. 10 OF 2020 IN THE MATTER OF THE CONSTITUTION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND IN THE MATTER OF THE ENFORCEMENT OF ARTICLE 71(1) (f) OF THE CONSTITUTION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 1977 (AS AMENDED FROM TIME TO TIME) AND IN THE MATTER OF THE ALLEGED CONTRAVENTION OF ARTICLE 71(1) (f) OF THE CONSTITUTION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA (AS AMENDED FROM TIME TO TIME) AND IN THE MATTER OF A PETITION TO CHALLENGE THE STATEMENT OF THE SPEAKER OF THE NATIONAL ASSEMBLY TO RECOGNIZE MR. CECIL MWAMBE AS STILL A MEMBER OF PARLIAMENT WHILST HE HAS ALREADY CROSSED THE FLOOR FROM CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) TO CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) AS BEING UNCONSTITUTIONAL PAUL REVOCATUS KAUNDA PETITIONER VERSUS THE SPEAKER OF THE NATIONAL ASSEMBLY 1st RESPONDENT MR. CECIL DAVID MWAMBE 2 nd RESPONDENT THE ATTORNEY GENERAL 3 rd RESPONDENT I. MAIGE, J RULING Under article 71(1) (f) of the Constitution of the United Republic of Tanzania, 77 [Cap. 2, R.E., 2002], as amended from time to time, (herein after referred to as “the Constitution”), a member of the Parliament he who denounces his/her membership in or ceases to be a member of a political party in whose sponsorship he or she was elected into Parliament, loses, by operation of the law, a qualification of being a member of the Parliament. The second respondent was, in 2015 General Elections, elected a member of Parliament for Ndanda Constituency under the sponsorship of Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (herein after referred to as “CHADEMA”).
    [Show full text]
  • Discussion Paper
    View metadata, citation and similar papers at core.ac.uk brought to you by CORE provided by Stellenbosch University SUNScholar Repository Discussion Paper TANZANIA-CHINA ALL-WEATHER FRIENDSHIP FROM SOCIALISM TO GLOBALIZATION: A CASE OF RELATIVE DECLINE Jean-Pierre Cabestan and Jean-Raphaël Chaponnière Stellenbosch | May 2016 1/2016 1 ABSTRACT How close is the Tanzanian-Chinese partnership today? Bi-lateral trade and Chinese economic activity in Tanzania today is far more significant than in the 1970s; China’s “no strings attached” policy is still attractive and political solidarities and military co-operation have remained relatively strong. However, this bi-lateral relationship does not have the importance, nor the exclusiveness it enjoyed in the heydays of socialism. Today, China must compete economically, politically and culturally with the activism and soft power of a larger group of countries, particularly the United States. Although both in Dar es Salaam and in Beijing this relationship is still presented as “special”, it has lost the structural role that it had until the late 1970s in shaping Sino-African relations. Growing Sino-American and Sino-Western competition in Africa has increased Tanzania’s option and helped it, to some extent, to better defend its own interests. This paper examines Tanzanian-Chinese relations over the past half century and more particularly since 2005, highlighting how global political, strategic and economic shifts have affected and on the whole reduced, in relative terms, the importance of this bi-lateral relationship. The authors: Jean-Pierre Cabestan is Professor and Head, Department of Government and International Studies, Hong Kong Baptist University; Jean-Raphaël Chaponnière is Associate Researcher at Asia Centre, Paris.
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania Mkutano Wa Tatu Yatokanayo Na Kikao Cha Arobaini Na Saba 21 Juni, 2016
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA TATU YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA 21 JUNI, 2016 MKUTANO WA TATU - YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA TAREHE 21 JUNI, 2016 I. DUA: Saa 3.00 Asubuhi Naibu Spika (Mhe. Dkt.Tulia Ackson) alisoma Dua na Kuongoza Bunge. Makatibu Mezani: 1. Ndg. Theonest Ruhilabake 2. Ndg. Zainab Issa Wabunge wa Kambi ya Upinzani walitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya dua kusomwa na Mhe. Naibu Spika. II. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali:- OFISI YA WAZIRI MKUU: Swali Na.399 – Mhe. Raphael Masunga Chegeni [kny. Mhe. Salome Makamba] Swali la nyongeza: (i) Mhe. Raphael Masunga Chegeni (ii) Mhe. Abdallah Hamisi Ulega (iii) Mhe. Joseph Kasheku Musukuma (iv) Mhe. Mariam Nassoro Kisangi OFISI YA RAIS (TAMISEMI): Swali Na.400 Mhe. Oran Manase Njeza Swali la nyongeza: (i) Mhe. Oran Manase Njeza (ii) Mhe. Desderius John Mipata (iii) Mhe. Goodluck Asaph Mlinga Swali Na.401 – Mhe. Boniventura Destery Kiswaga Swali la nyongeza: (i) Mhe. Boniventura Destery Kiswaga (ii) Mhe. Augustino Manyanda Maselle (iii) Mhe. Richard Mganga Ndassa (iv) Mhe. Dkt. Dalali Peter Kafumu Swali Na. 402 – Mhe. Fredy Atupele Mwakibete Swali la Nyongeza: (i) Mhe. Fredy Atupele Mwakibete (ii) Mhe. Njalu Daudi Silanga (iii) Mhe. Halima Abdallah Bulembo (iv) Mhe. Azza Hilal Hamad 2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Swali Na.403 – Mhe Joseph Kakunda. kny Mhe. Ally Saleh Ally Swali la nyongeza: (i) Mhe. Joseph George Kakunda (ii) Mhe. Mussa Azzan Zungu (iii) Mhe. Cosato David Chumi (iv) Mhe.
    [Show full text]
  • Hotuba Ya Wizara Ya Viwanda Na
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA HOTUBA YA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA, MHE. PROF. KITILA ALEXANDER MKUMBO (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2021/2022 Dodoma. Mei, 2021. YALIYOMO ORODHA YA VIFUPISHO ........................................ vi DIRA, DHIMA NA MAJUKUMU YA WIZARA ................x 1. UTANGULIZI ..................................................... 1 2. UMUHIMU WA VIWANDA NA BIASHARA KATIKA UCHUMI WA TAIFA .............................. 7 3. MCHANGO WA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA KATIKA UCHUMI ........................... 10 3.1. Sekta ya Viwanda ......................................... 10 3.2. Sekta ya Biashara ........................................ 11 4. TATHMINI YA MPANGO NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2020/2021 12 Bajeti Iliyoidhinishwa na Kupokelewa kwa Mwaka 2020/2021 ......................................... 12 4.1. Tathmini ya Utekelezaji wa Malengo ya Bajeti kwa Mwaka 2020/2021 ............................... 12 4.1.1. Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara- BLUEPRINT ..............................................12 4.1.2. Mapitio na Utungaji wa Sera na Marekebisho ya Sheria na Kanuni ........ 14 4.1.3. Sekta ya Viwanda .................................. 19 4.1.4. Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo .................................................... 41 4.1.5. Sekta ya Biashara .................................. 48 4.1.6. Sekta ya Masoko .................................... 69 4.1.7. Maendeleo
    [Show full text]