Ofisi Ya Bunge S.L.P 941 Dodoma 27 Juni, 2013
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA MOJA YATOKANAYO NA KIKAO CHA HAMSINI NA NANE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) OFISI YA BUNGE S.L.P 941 DODOMA 27 JUNI, 2013 YATOKANAYO NA KIKAO CHA HAMSINI NA NANE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS – FIFITY EIGTHTH SITTING) TAREHE 27 Juni, 2013 MAKATIBU MEZANI: (1) Ndg. Justina Shauri (2) Ndg. Charles Mloka (4) Ndg. Lawrence Makigi I. DUA: Dua ilisomwa saa 3.00 asubuhi na Kikao kilianza kikiongozwa na Mhe. Spika Anne S. Makinda, (Mb). II. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI: WAZIRI MKUU: Utekelezaji Wa Taarifa ya Ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2012. WAZIRI WA FEDHA: Taarifa ya Majumuisho ya Mpango Mkakati wa kujibu Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Wizara, Idara za Serikali na Mikoa (Vol. I na II) kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. III. MASWALI: Maswali ya yafuatayo yaliulizwa na kujibiwa:- (I) WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI – SWALI NA. 478, (II) WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI – SWALI NA. – 479, NA. 480 2 IV. MATANGAZO: Mheshimiwa Spika aliwatangazia Wabunge matangazo kama ifuatavyo:- - Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kutakuwa na kikao saa 7.00 mchana katika Ukumbi Na. 133. - Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira watakuwa na kikao leo saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa Basement. - Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali kutakuwa na kikao leo saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa Msekwa. - Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii watakuwa na kikao leo saa 7.00 mchana katika Ukumbi Msekwa C. - Wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) watakuwa na kikao saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa Msekwa. - Wajumbe wa TAPAC watakuwa na kikao saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa Msekwa. - Ofisi ya Bunge inawatangazia Wah. Wabunge waende kuchukua makabrasa yao katika Pigeon Holes ili kutoa nafasi ya kugawa nyaraka nyingine. V. MISWADA WA SHERIA YA SERIKALI: Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2013 (The Finance Bill, 2013). Mhe. Spika alimwita Mtoa Hoja Mhe. Dkt. William Mgimwa kuwasilisha hoja yake. Baada ya Mtoa Hoja kuwasilisha Mhe. Spika alimwita:- 3 (1)Mhe. Andrew Chenge, (Mb) Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kuwasilisha Maoni ya Kamati ya Bajeti. (2)Mhe. Christina Lissu Munghwai, (Mb) kuwasilisha Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Waheshimiwa Wabunge wafuatao waliendelea kuchangia hoja ya Waziri wa Fedha. (3)Mhe. Eng. Stella Manyanya, (Mb) (4)Mhe. Peter Serukamba, (Mb) (5)Mhe. James Mbatia, (Mb) (6)Mhe. Luhaga Joelson Mpina, (Mb) (7)Mhe. John J. Mnyika, (Mb) (8)Mhe. Halima Mdee, (Mb) (9)Mhe. Godfrey Zambi, (Mb) VI. KUSITISHA SHUGHULI ZA BUNGE: Shughuli za Bunge zilisitishwa saa 7.00 mchan hadi saa 11.00 jioni. VII. SHUGHULI ZA BUNGE KURUDIA: Baada ya mapumziko ya mchana Shughuli za Bunge zilirudia saa 11.00 jioni zikiongozwa na Mheshimiwa Anne S. Makinda, Spika. VIII. MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI: Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2013 (The Finance Bill, 2013). Mheshimiwa Spika aliwaita Wabunge kuchangia hoja kama ifuatavyo:- 4 (10) Mhe. Christina Lissu Mughwai (Mb) (11) Mhe. Mussa Zungu Azzan, (Mb) (12) Mhe. Amina A. Amour, (Mb) (13) Mhe. Mbarouk Rajab, (Mb) (14) Mhe. Esther Bulaya, (Mb) (15) Mhe. John M. Cheyo, (Mb) IX. MAELEZO YA SPIKA: Mhe. Spika alitoa ufafanuzi kuwa utaratibu wa kupitisha Bajeti umeelezwa katika sehemu ya 9 ya Kanuni za Bunge na kufafanuliwa katika Kanuni 109 (1) kuhusu kupitishwa Muswada kwa kuzingatia Masharti ya sehemu ya 8 ya Kanuni. Kanuni ya 84 (3) (4) zinatoa masharti ya jumla ya mchakato wa kupitisha Bajeti. Aidha, 109 (2) inakataza kufanya marekebisho ya kupunguza kodi bila kutoa mapendekezo mbadala kwa mujibu wa kanuni 72(1) kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati ya Bajeti na mapendekezo yaliyowasilishwa na Wabunge kwenye Bajeti, Spika aliagiza Kamati ya Bajeti ikutane na Wizara ya Fedha na Wabunge wanaohusika kujadiliana namna ya kupata mapendekezo mbadala. Wabunge wafuatao waliendelea kuchangia hoja ya Waziri wa Fedha: (16) Mhe. Jitu Vrajlal Soni (Mb) (17) Mhe. Christopher Ole Sendeka, (Mb) (18) Mhe. Magdalena Sakaya, (Mb) (19) Mhe. Dkt. Khamisi Kigwangala, (Mb) (20) Mhe. Tundu Lissu, (Mb) (21) Mhe. Murtaza Ally Mangungu, (Mb) (22) Mhe. Ally Keissy Mohamed, (Mb) (23) Mhe. Seleman Jafo, (Mb) (24) Mhe. Magale John Shibuda, (Mb) (25) Mhe. Salim Hassan Abdullah Turky, (Mb) (26) Mhe. Dkt. Kebwe S. Kebwe. 5 X. KUAHIRISHA SHUGHULI ZA BUNGE: Shughuli za Bunge ziliahirishwa saa 2.45 usiku hadi kesho saa 3.00 asubuhi. DODOMA DKT. T. D. KASHILILAH 27 Juni, 2013 KATIBU WA BUNGE 6.