Majadiliano Ya Bunge ______
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Load more
Recommended publications
-
Online Document)
NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 8 Julai, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali na tunaanza na ofisi ya Waziri, Mheshimiwa Kayombo, kwa niaba yake Mheshimiwa Rage. Na. 321 Ofisi kwa ajili ya Tarafa-Mbinga MHE. ISMAIL A. RAGE (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuliza:- Wilaya ya Mbinga ina tarafa sita lakini tarafa zote hazina ofisi rasmi zilizojengwa:- Je, ni lini Serikali itajenga ofisi kwa Makatibu Tarafa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence Cassian Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Ruvuma una jumla ya tarafa 24 yaani Tunduru wako saba, Mbinga wana tarafa sita, Nyasa wana tarafa tatu, Namtumbo wana tarafa tatu na Songea wana tarafa tano. Ni kweli tarafa za Wilaya ya Mbinga hazina ofisi rasmi zilizojengwa na Serikali. Ujenzi wa hizo ofisi unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa Mkoa wa Ruvuma umeweka kipaumbele katika ujenzi wa ofisi nne za tarafa katika Wilaya ya Nyasa na Tunduru. Tarafa hizo ni Luhuhu (Lituhi-Nyasa), Ruhekei (Mbamba bay-Nyasa), Mpepo (Tinga-Nyasa) na Nampungu (Nandembo-Tunduru). Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Mkoa ulitenga shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Tarafa ya Luhuhu (Lituhi), Ruhekei (Mbamba bay), Mpepo (Tingi) na Nampungu (Nandembo). -
Majadiliano Ya Bunge ______
NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ BUNGE LA KUMI NA MOJA ___________ MKUTANO WA KWANZA Kikao cha Kwanza - Tarehe 17 Novemba, 2015 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Naomba tukae. TANGAZO LA RAIS LA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa masharti ya Katiba, Mkutano huu wa Kwanza unaanza kwa Rais kuuitisha. Naomba kuchukua nafasi hii kusoma Tangazo la Rais kama ambavyo tumelipokea. Tangazo la Serikali Na. 513 la tarehe 6 Novemba, 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sura ya Pili, hati iliyotolewa kwa mujibu wa Ibara ya 90(1). Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya. KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; NA KWA KUWA, masharti ya Ibara ndogo ya kwanza ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, yanamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu; NA KWA KUWA, matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 yalitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2015; HIVYO BASI, mimi John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyonayo chini ya Ibara ya 90(1) ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, naitisha Mkutano wa Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ufanyike katika ukumbi wa Bunge uliopo Mjini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi. -
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 7 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA KIKAO CHA NNE – 7 NOVEMBA, 2014 Kikao kilianza saa 3:00 Asubuhi kikiongozwa na Mhe. Job Y. Ndigai, Mb Naibu Spika ambaye alisoma Dua. MAKATIBU MEZANI 1. Ndg. Charles Mloka 2. Ndg. Lina Kitosi 3. Ndg. Hellen Mbeba I. MASWALI YA KAWAIDA Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge na kupitia majibu Bungeni:- 1. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 38 la Mhe. Anne Kilango 2. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 39 la Mhe. Salum Khalfan Barwary 3. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 40 la Mhe. Moses Joseph Machali 4. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – swali na. 41. La Mhe. Omar Rashid Nundu 5. Wizara ya Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi – swali na. 42. La Mhe. Hilda Ngoye 6. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – swali na. 43. La Mhe. Zitto Kabwe Zuberi 7. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tecknolojia – swali na. 44 –la Mhe. Murtaza Mangungu 8. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - swali na. 45-la Mhe. Godfrey Mgimwa 9. Wizara ya Katiba na Sheria - swali na. 46 – la Mhe. Neema Mgaya Hamid 2 10. Wizara ya Katiba na Sheria- swali na. 47 – la Mhe. Assumpter Mshana 11. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo – swali na. 48 la Mhe. Khatib Said Hji. 12. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - swali na. 49 la Mhe. -
Bunge Newsletter
BungeNe ewsletter Issue No 008 June 2013 New Budget Cycle Shows Relavance For the first time in recent Tanzania history the engage the government and influence it make sev- Parliament has managed to pass the next financial eral tangible changes in its initial budget proposals. year budget before the onset of that particular year. This has been made possible by the Budget Commit- This has been made possi- tee, another new innovation by Speaker Makinda. ble by adoption of new budget cycle. Under the old cycle, it was not possible to influence According to the new budget cycle, the Parliament the government to make changes in budgetary allo- starts discussing the budget in April as opposed to cations. That was because the main budget was read, old cycle where debate on the new budget started on debated and passed before the sectoral plans. After June and ends in the first or second week of August. the main budget was passed, it was impossible for the MPs and government to make changes in the When the decision was taken to implement the new sectoral budgets since they were supposed to reflect budget cycle and Speaker Anne Makinda announced the main budget which had already been passed. the new modalities many people, including Mem- bers of Parliament, were skeptical. Many stakehold- These and many other changes have been made possi- ers were not so sure that the new cycle would work. ble through the five components implemented under the Parliament five years development plan. “Govern- But Ms Makinda has managed to prove the doubt- ment and Budget Oversight and Accountability is one ers wrong. -
Majadiliano Ya Bunge ______
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Tatu – Tarehe 15 APRILI, 2010 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Maswali kwa Waziri Mkuu leo kiongozi wa Upinzani Bungeni hayupo kwa hiyo nitaenda na orodha za wachangiaji na nitakuwa ninakwenda kufuatana na itikadi ya chama, upande, gender na vitu kama hivyo. Kwa hiyo, walioko hapa wasidhani watakwenda kama ilivyoorodheshwa. Kwa hiyo, nitaanza na msemaji wa kwanza Mheshimiwa Dr. Willibrod Slaa. MHE. DR. WILLIBROD P. SLAA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kunipa nafasi, Mheshimiwa Waziri Mkuu sasa ni takribani mwaka mzima tangu nilipoanza kuhoji, mimi na Wabunge wenzangu, tulipoanza kuhoji kuhusu ubadhirifu na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinakabili matumizi ya fedha za umma zilizofanywa na makampuni kama Mwananchi Gold Company, Tan Gold, Kagoda, Deep Green na mengine mengi ambayo yalitajwa ndani ya ukumbi huu. Kwa nyakati tofauti maelezo mbalimbali yametolewa ndani ya Bunge. Mpaka leo hatujapata taarifa ya kinachoendelea. Bunge hili lenye jukumu la kuisimamia Serikali halijui au wananchi hawajui kama kuna kitu kinaendelea je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu ubadhirifu huo? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naamini kabisa Dr. Slaa, hutegemei kwamba kweli nitaweza kujibu maswali hayo uliyoyauliza kwamba mimi nina maelezo juu ya Kagoda, maelezo juu ya nani, is not possible nadhani si sahihi kabisa. (Makofi) Mimi ninachoweza kusema ni kwamba jitihada za Serikali zipo zimekuwa zikionekana katika maeneo ambayo yameshaanza kufanyiwa kazi. Sasa kama kuna maeneo ambayo bado hayajafanyiwa kazi jitihada za Serikali zitaendelea kwa kadri itakavyowezekana. -
-
Hotuba Ya Waziri Wa Mambo Ya Nje Na
HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MHESHIMIWA BERNARD KAMILLIUS MEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuliongoza kwa umahiri mkubwa Bunge hili la Bajeti la mwaka 2012/2013. Napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb.), Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wanaokusaidia kuongoza Bunge hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. 3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya Nne. Chini ya uongozi wake Taifa letu limeendeleza utamaduni wetu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano. Nawaomba Watanzania wote tuendelee kudumisha hali hiyo ili kuimarisha umoja wetu ambao ni tunu isiyopatikana kwa bei yoyote. 4. Mheshimiwa Spika, niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge wengine wote walionitangulia kuwapongeza kwa dhati kabisa Waheshimiwa Wabunge wapya, Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei 2012. Nawapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge waliochaguliwa kipindi hiki kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye nafasi mbalimbali humu Bungeni na ndani ya Serikali. -
Majadiliano Ya Bunge ______
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Ishirini na Tano – Tarehe 17 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO:- Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa Fedha 2012/2013. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:- Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. EUGEN E. MWAIPOSA (K.n.y. MHE. EDWARD LOWASSA - MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA):- Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. VINCENT J. NYERERE – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza maswali kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, atakayeuliza swali letu la kwanza ni Mheshimiwa Beatrice Matumbo Shellukindo kwa niaba yake Mheshimiwa Herbert Mntangi. -
Majadiliano Ya Bunge ______
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Saba – Tarehe 6 Februari, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita Katibu kwa orodha ya shughuli za leo, ninapenda kwanza nimpongeze Corporal Fauster. Napenda niwafahamisheni, ni mara ya kwanza katika historia ya Bunge letu Spika kutanguliwa na Sergeant-At-Arms ambaye ni mwanamke. Tulikwishasema awali Bunge hili litaendeshwa kwa viwango na viwango ni pamoja na kuzingatia jinsia. Hakuna kazi ambazo ni za wanaume tu peke yao. Ahsante sana Corporal Fauster. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, nimerejea, nimesitisha safari ya Marekani. Nalazimika kutoa maelezo kwa sababu ya maneno mengi tu. Safari ile kwenda kule ilipangwa kwa kuzingatia mambo mawili :- Moja, ni umuhimu tu wake. Wenzetu Amerika, wiki ya pili ya Mwezi Februari kila mwaka mihimili yote mitatu ya Dola wanakaa pamoja kwa mlo wa asubuhi, inaitwa National Prayer Breakfast. Pamoja na mambo mengi yatakayofanyika, Rais wao ataongea pale kwenye Prayers Breakfast. Lakini wanawatambua baadhi ya viongozi mashuhuri ambao wana ushirikiano mwema nao. Mimi kama Spika wa Bunge hili, nilialikwa kwa msingi huo. Kwa hiyo, hoja kwamba labda ningeweza kumtuma mtu mwingine, haipo kwa sababu ni mwaliko wa heshima kwa jina. (Makofi) La pili ni kwamba, nikitazama ratiba na Kanuni ya 24 ya Bunge, ilikuwa ni kwamba Miswada inaendelea na kwa hiyo, nilidhani mambo mengine kama vile taarifa za Kamati yangekuja kama ilivyo kawaida katika wiki ya mwisho, na mimi nilikuwa narudi Ijumaa asubuhi. Kwa hiyo, yote yangewezekana. Sasa hilo lilishindikana, niliwaarifu wenyeji wetu kule Marekani na wamesikitika, lakini wamesema kama wanasiasa, wameelewa,kwa sababu niliwaeleza mazingira ambayo yalinifanya nisiende. -
Bunge La Tanzania
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Kwanza – Tarehe 9 Juni, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta ) Alisoma Dua KIAPO CHA UAMINIFU Mbunge afuataye aliapa Kiapo cha Uaminifu na kukaa katika nafasi yake Bungeni:- Mheshimiwa Lolensia Jeremiah Maselle Bukwimba SPIKA: Ahsante sana, leo shamrashamra zimepita kiasi; nimetafuta ushauri wa sheria bado sijapewa kuhusu shamrashamra hizi kwa kiwango hiki kama inaruhusiwa kwa kanuni lakini hayo sasa ni ya baadaye. (Kicheko) T A A R I F A Y A S P I K A SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge hili, tulipitisha Miswada mitano ya sheria iitwayo The Human DNA Regulation Bill, 2009, The Fertilizers Bill, 2009, The Insurance Bill, 2009, The Water Resources Management Bill, 2009 na The Water Supply and Sanitation Bill, 2009. Mara baada ya kupitishwa na Bunge na baadae kupita katika hatua zake zote za uchapishaji, Miswada hiyo ilipelekwa kwa Mheshimiwa Rais ili kupata kibali chake kwa mujibu wa Katiba. Kwa taarifa hii, nafurahi kuwaarifu Wabunge wote na Bunge hili Tukufu kwamba, tayari Mheshimiwa Rais amekwishatoa kibali kwa Miswada yote hiyo mitano na sasa ni sheria za nchi, ambapo The Human DNA Regulation Act, 2009 inakuwa ni Sheria Namba Nane ya Mwaka 2009; The Fertilizers Act, 2009 ni Sheria Namba Tisa ya 1 Mwaka 2009; The Insurance Act, 2009 ni Namba Kumi ya Mwaka 2009; The Water Resources Management, Act 2009 ni Namba Kumi na Moja ya Mwaka 2009; na Sheria Namba Kumi na Mbili ya Mwaka 2009 ni ile ya Water Supply and Sanitation Act, 2009. -
Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tano - Tarehe 16 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU: Hotuba ya Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MHE. MARGARETH A. MKANGA (k.n.y. MHE. OMAR S. KWAANGW’ - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 239 Majimbo ya Uchaguzi MHE. JAMES P. MUSALIKA (k.n.y. MHE. DR. WILLIAM F. SHIJA) aliuliza:- Kwa kuwa baadhi ya Majimbo ya Uchaguzi ni makubwa sana kijiografia na kwa wingi wa watu; je, Serikali itashauriana na Tume ya Uchaguzi ili kuongeza Majimbo ya Uchaguzi katika baadhi ya maeneo nchini katika Uchaguzi wa mwaka 2005? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (MHE. MUHAMMED SEIF KHATIB) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Dr. William Shija, Mbunge wa Sengerema, naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, lilipokuwa linajibiwa swali la Mheshimiwa Ireneus Ngwatura, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na pia swali la Mheshimiwa Sophia Simba, Mbunge wa Viti Maalum, CCM 1 katika Mikutano ya Saba na Kumi na Moja sawia ya Bungeni, nilieleza kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 75(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungao wa Tanzania 1977, Jamhuri ya Muungano inaweza kugawanywa katika Majimbo ya Uchaguzi kwa idadi na namna itakavyoamuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kupata kibali cha Mheshimiwa Rais. -
Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Sita
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Tano – Tarehe 15 Juni, 2009 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI: Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha Mezani Taarifa ya Kamati ya Fedha na Uchumi Kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2008/2009 na Mwelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2009/2010. MHE. MWADINI ABBAS JECHA K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Fedha na Uchumi, naomba kuwasilisha Mezani Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha na Uchumi juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2009/2010. MASWALI NA MAJIBU Na. 33 Athari za Milipuko ya Mabomu - Mbagala MHE. KHADIJA SALUM ALI AL-QASSMY K.n.y. MHE. ANIA S. CHAUREMBO aliuliza:- Kwa kuwa, tukio la tarehe 29 Aprili, 2009 la milipuko ya mabomu kwenye Kambi ya Jeshi la Wananchi – JWTZ, Mbagala Kizuiani, limesababisha hasara kubwa kama vile, watu kupoteza maisha, watu wengi kujeruhiwa, uharibifu mkubwa wa mali na 1 nyumba za wananchi, kuharibika kwa miundombinu na kadhalika. Na kwa kuwa, kuna Kamati maalum inayoshughulikia majanga yanapotokea ambayo iko chini ya Ofisi ya waziri Mkuu:- Je, ni sababu zipi zilizofanya Kamati hiyo isifike kwa haraka kwenye eneo la tukio na kutoa msaada wa haraka uliotakiwa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla sijajibu swali hili naomba kutoa mkono wa pole sana kwa Mheshimiwa Ania Chaurembo, kwa msiba wa Mama yake Mzazi.