Online Document)

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Online Document) NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 8 Julai, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali na tunaanza na ofisi ya Waziri, Mheshimiwa Kayombo, kwa niaba yake Mheshimiwa Rage. Na. 321 Ofisi kwa ajili ya Tarafa-Mbinga MHE. ISMAIL A. RAGE (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuliza:- Wilaya ya Mbinga ina tarafa sita lakini tarafa zote hazina ofisi rasmi zilizojengwa:- Je, ni lini Serikali itajenga ofisi kwa Makatibu Tarafa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence Cassian Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Ruvuma una jumla ya tarafa 24 yaani Tunduru wako saba, Mbinga wana tarafa sita, Nyasa wana tarafa tatu, Namtumbo wana tarafa tatu na Songea wana tarafa tano. Ni kweli tarafa za Wilaya ya Mbinga hazina ofisi rasmi zilizojengwa na Serikali. Ujenzi wa hizo ofisi unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa Mkoa wa Ruvuma umeweka kipaumbele katika ujenzi wa ofisi nne za tarafa katika Wilaya ya Nyasa na Tunduru. Tarafa hizo ni Luhuhu (Lituhi-Nyasa), Ruhekei (Mbamba bay-Nyasa), Mpepo (Tinga-Nyasa) na Nampungu (Nandembo-Tunduru). Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Mkoa ulitenga shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Tarafa ya Luhuhu (Lituhi), Ruhekei (Mbamba bay), Mpepo (Tingi) na Nampungu (Nandembo). Mpaka sasa mkoa umeshapokea kiasi cha shilingi milioni mia moja na hamsini ili kuendelea na ujenzi wa miradi hiyo. Ofisi za Tarafa ya Ruhekei, Luhuhu na Nandembo zimekamilika. Katika mwaka wa fedha wa 2015/2016, Mkoa umetenga kiasi cha shilingi 140, 337,239 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi za tarafa. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 75 zitatumika kukamilisha ofisi ya tarafa ya Mpepo na shilingi 65,337,000 zitatumika kukamilisha kulipa deni la mkandarasi aliyejenga ofisi ya tarafa ya Nandembo katika Wilaya ya Tunduru. Mheshimiwa Mwenyekiti, azma ya Serikali ni kuhakikisha tarafa zote zinakuwa na ofisi. Mkoa umejipanga kutekeleza ujenzi wa ofisi hizo kwa awamu kutokana na ufinyu wa bajeti ikilinganishwa na mahitaji makubwa yaliyopo ya ujenzi wa ofisi hizo na majengo mengine ya Serikali. Serikali inaendelea kuwasisitizia wananchi na wadau mbalimbali kushiriki katika ujenzi wa mjengo mbalimbali ili kuharakisha ukamilishaji wa majengo hayo ikiwemo ujenzi wa ofisi za tarafa. MWENYEKITI: Mheshimiwa Rage. MHE. ISMAIL A. RAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi namheshimu sana rafiki yangu Naibu Waziri lakini leo majibu yake hayakuniridhisha hata kidogo. Mimi nauliza swali linalohusu Wilaya ya Mbinga, yeye ananieleza Wilaya za Nyasa na Tunduru. Interest yangu mimi ni kutaka kujua tarafa sita ambazo ziko Mbinga lini ofisi zake zitaanza kujengwa basi ni hilo tu. Naomba maelezo hayo Mheshimiwa Naibu Waziri. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niliweke hili jambo vizuri kwa sababu najua kwa nini anasema ananishangaa. Ofisi za halmashauri zinajengwa na halmashauri. Ofisi hizi nazozitaja hapa si za Halmashauri ni za Serikali Kuu. Afisa Tarafa anawajibika kwa Mkuu wa Wilaya. Kwa hiyo, napozungumza habari ya mkoa, hela zote tunazozungumza hapa zinapita kwa Katibu Tawala wa mkoa ndipo zinakwenda pale Mbinga. Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme kweli tu, anachosema Mheshimiwa Gaudence Kayombo hapa kwamba hakuna ofisi ambayo imejengwa pale ni kweli. Mimi ninayo orodha hapa ngoja niwaeleze vizuri ili nieleweke nachozungumza na nisome. Mbinga mjini wako katika ofisi ya jengo la ushirika, Kigonsera wako katika ofisi ya VEO(Village Executive Officer), Luanda wako katika ofisi ya kijiji, Mkumbi wako katika ofisi za kijiji, Mbuji wako katika ofisi za kijiji, ofisi hiyo ni ya zamani sana na mikakati iko hapo. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi nikizungumza habari za halmashauri kwamba wamejenga hapa si atatoka Rage tena ataniambia umesema uongo hapa. Ofisi zote nazokuambia hapa haziingii katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga zinapita kwa Katibu Tawala wa Mkoa na jitihada nilizozionyesha hapa ni hizo tunazozungumza hapa. Kwa hiyo, napoeleza hela zilizokwenda nikataja mimi Nandembo, Tunduru, ni kwa sababu hela zote zinafikia Mkoani pale kwa Katibu Tawala wa Mkoa. Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, sisi tunatambua kwamba kuna tatizo kubwa hapa na ndiyo maana tumejibu kuhusu jitihada tunazozifanya hapa, ni pamoja na kuhamasisha wananchi kupitia ofisi za Wakuu wetu wa Wilaya watusaidie kuchangia ofisi hizi kama ambavyo tumekuwa tunafanya katika maeneo mengine. Kusema Wilaya zile nyingine nilisema kwa sababu ofisi inayohusika ni ya Katibu Tawala wa Mkoa. MWENYEKITI: Mheshimiwa Ndassa. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na maelezo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameeleza, niseme tu kwamba tatizo la nyumba za Maafisa Tarafa ni kubwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali langu kwa sababu Afisa Tarafa wa Tarafa ya Ibindo, Wilaya ya Kwimba ana kata nane na Maafisa Tarafa wengine lakini hawana usafiri ili waweze kuwafikia wananchi. Mtu mmoja anazungukia tarafa saba, nane au tisa lakini hana usafiri. Serikali ina utaratibu gani kama ilivyokuwa zamani kwa hawa Maafisa Tarafa kuwapelekea pikipiki ili waweze kufika kwenye maeneo yao ya kazi bila kuchelewa? 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ametaja Tarafa ya Ibindo na anazungumza habari ya kata. Kwa upande wa kata, ni kweli kata hizi ziko chini yetu katika maana ya halmashauri. Kwa maana ya tarafa inabidi niende nikaiangalie hiyo lakini ni kweli pia kama anavyosema Mheshimiwa Richard Ndassa tumekuwa na utaratibu wa kusaidia ofisi zetu za Maafisa Tarafa kupata pikipiki. Kwa hiyo, nitakwenda kufuatilia kwanza kuijua hii Ibindo iko katika utaratibu gani lakini ni jambo ambalo linazungumzika. Kwa upande wa pikipiki ni kweli kabisa kwamba tumekuwa na utaratibu wa kusaidia Maafisa wetu wa Tarafa wafanye kazi hiyo. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Hilda. MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na maelezo mazuri yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri, napenda kumuuliza swali moja dogo tu la nyongeza kwamba yapo majengo mengine ambayo yalijengwa wakati wa mkoloni, majengo ya Makatibu Tarafa ambayo yako katika Makao Makuu ya Tarafa. Kwa mfano, kuna jengo kubwa sana la Tarafa ya Ukukwe, Wilayani Rungwe, Tarafa ya Pakati na Busokelo, majengo haya yamechakaa na hayafanyiwi matengenezo yoyote lakini yangeweza kufaa kabisa kwa kazi za Maafisa Tarafa. Je, Serikali ina mpango gani basi wa kuweza kuyakarabati majengo haya ili yaweze kurudi tena katika upya uleule wa zamani? Ahsante sana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, naelewa anachozungumza hapa ni kwamba kuna majengo haya ambayo yanaonekana yamechakaa na kama tulivyofanya katika Halmashauri ile ya Wilaya ya Mbinga ambayo nimeulizwa mara ya kwanza ni jambo ambalo tunaweza tukafanya lakini watakao- coordinate hii habari itakuwa ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia Katibu Tawala na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Katibu Tawala wa Wilaya, tutakwenda kuangalia hali yake. Tatizo letu ni bajeti kwa sababu katika Regional Secretariat hakuna mahali popote ambapo tunazalisha mali wanategemea zaidi ruzuku ya Serikali na kama nilivyoeleza hapa hela zilizokuwa zimekwenda pale zilikuwa ni shilingi milioni mia tatu. Sasa nitakwenda kuangalia pia kama hizi hela zinaweza zika-spread over zikaangalia pia katika maeneo haya anayosema ya Ukukwe katika Wilaya ile ya Busokelo. MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea na swali la Mheshimiwa Bungara kwa niaba yake Mheshimiwa Shah. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Na. 322 Tatizo la Maji Hospitali ya Wilaya ya Kilwa MHE. ABDULKARIM E. H. SHAH (K.n.y. MHE. SELEMANI S. BUNGARA) aliuliza:- Kila mwezi Juni hadi Desemba kila mwaka Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) hukabiliwa na tatizo kubwa la maji kutokana na visima kushindwa kutoa maji kunakosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na wakati mwingine hukauka kabisa na kusababisha adha kubwa hospitalini hapo kwa magonjwa ya mlipuko:- Je, Serikali haioni haja ya kutenga bajeti kwa ajili ya kujenga mfumo rasmi wa kuvuna maji ya mvua kama njia sahihi ya kutatua tatizo hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mku, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Said Bungara, Mbunge wa Kilwa Kusini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) kwa sasa inapata maji kiasi cha mita za ujazo kumi na tano sawa na asilimia 32 ya mahitaji yake halisi kutoka katika chemchem ya Kitumba pamoja na kisima kirefu kilichochimbwa kupitia mradi wa TASAF ambacho kinatumiwa pia na wananchi wa Kivinje. Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukabiliana na tatizo la maji katika Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) mwezi Aprili, 2015 Halmashauri imenunua pampu ya kuendeshwa kwa umeme na kuifunga kwenye kisima kilichochimbwa na Kampuni ya
Recommended publications
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 1 Julai, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 132 Kuimarisha Ulinzi na Usalama Jiji Dar es Salaam MHE. CHARLES N. KEENJA : Kwa kuwa, Serikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua madhubuti za kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye Jiji la Dar es Salaam kwa kuligawa Jiji kwenye Mikoa na Wilaya za Ki-ulinzi ; na kwa kuwa, hatua hiyo haikwenda sanjari na ile ya kuigawa Mikoa ya Kiutawala:- (a) Je, ni lini Serikali itachukua hatua za kuligawa eneo la Jiji la Dar es Salaam kwenye Mkoa/Wilaya zinazokwenda sanjari na zile za Ulinzi na Usalama ? (b) Je, Serikali haioni kwamba Viongozi kwenye eneo lenye hadhi zinazotofautiana kunaleta matatizo ya ushirikiano na mawasiliano hatimaye kukwamisha utendaji kazi ? (c) Kwa kuwa, zaidi ya 10% ya wananchi wa Tanzania wanaishi Dar es Salaam. Je, Serikali haioni kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuweka utaratibu mzuri zaidi wa Uongozi kwenye Jiji hilo ? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 1 Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Charles Keenja, Mbunge wa Ubungo, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa katika hatua za kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye Jiji la Dar es Salaam Serikali iliamua kuligawa eneo katika ngazi ya Mikoa ambapo Wilaya zote tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala ni Mikoa ya Kiulinzi na ngazi ya Mkoa kupewa hadhi ya Kanda Maalum ya Ulinzi na Usalama.
    [Show full text]
  • Bunge La Tanzania
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Kwanza – Tarehe 9 Juni, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta ) Alisoma Dua KIAPO CHA UAMINIFU Mbunge afuataye aliapa Kiapo cha Uaminifu na kukaa katika nafasi yake Bungeni:- Mheshimiwa Lolensia Jeremiah Maselle Bukwimba SPIKA: Ahsante sana, leo shamrashamra zimepita kiasi; nimetafuta ushauri wa sheria bado sijapewa kuhusu shamrashamra hizi kwa kiwango hiki kama inaruhusiwa kwa kanuni lakini hayo sasa ni ya baadaye. (Kicheko) T A A R I F A Y A S P I K A SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge hili, tulipitisha Miswada mitano ya sheria iitwayo The Human DNA Regulation Bill, 2009, The Fertilizers Bill, 2009, The Insurance Bill, 2009, The Water Resources Management Bill, 2009 na The Water Supply and Sanitation Bill, 2009. Mara baada ya kupitishwa na Bunge na baadae kupita katika hatua zake zote za uchapishaji, Miswada hiyo ilipelekwa kwa Mheshimiwa Rais ili kupata kibali chake kwa mujibu wa Katiba. Kwa taarifa hii, nafurahi kuwaarifu Wabunge wote na Bunge hili Tukufu kwamba, tayari Mheshimiwa Rais amekwishatoa kibali kwa Miswada yote hiyo mitano na sasa ni sheria za nchi, ambapo The Human DNA Regulation Act, 2009 inakuwa ni Sheria Namba Nane ya Mwaka 2009; The Fertilizers Act, 2009 ni Sheria Namba Tisa ya 1 Mwaka 2009; The Insurance Act, 2009 ni Namba Kumi ya Mwaka 2009; The Water Resources Management, Act 2009 ni Namba Kumi na Moja ya Mwaka 2009; na Sheria Namba Kumi na Mbili ya Mwaka 2009 ni ile ya Water Supply and Sanitation Act, 2009.
    [Show full text]
  • Check Against Delivery HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA
    Check Against Delivery HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA, (MB), WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA SITA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DODOMA, TAREHE 9 FEBRUARI, 2007 Mheshimiwa Spika, Mkutano wa sita wa Bunge lako Tukufu umehitimisha shughuli zote zilizokuwa zimepangwa. Mkutano huu ni wa kwanza baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kutimiza mwaka mmoja madarakani. Taarifa za mafanikio na changamoto zilizojitokeza zimewasilishwa kupitia mikutano mbalimbali ya Chama Tawala, Serikali na vyombo mbalimbali vya habari. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa, nachukua nafasi hii tena kwa niaba ya Serikali na wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa rambirambi kwako wewe Mheshimiwa Spika, kwa Waheshimiwa Wabunge wote, kwa familia, jamaa na marafiki kwa msiba uliotokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tunduru, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Bunge na Uratibu) Marehemu Juma Jamaldin Akukweti. Wote tulimfahamu Marehemu Akukweti kwa umakini na umahiri wake hapa Bungeni. Marehemu Akukweti alifariki kutokana na ajali ya ndege iliyokuwa inamrejesha Dar es Salaam baada ya kumaliza kazi ya kukagua soko la Mwanjelwa lililoteketea kwa moto mkoani Mbeya. Katika ajali hiyo Watumishi wa Serikali walipoteza maisha. Watumishi hao ni Bibi Theresia Nyantori, Mwandishi wa Habari wa Idara ya Habari; Bwana Nathaniel Katinila, Mratibu wa Mradi wa Masoko; na Bwana George Bendera, Afisa Habari Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu. Majeruhi katika ajali hiyo ambao bado wanapata matibabu lakini wametoka hosptali ni Bw. Nisetas Kanje, Katibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Bunge na Uratibu); na rubani wa ndege hiyo Bw. Martin Sumari. Tunamwomba Mwenyezi Mungu awasaidie majeruhi wote waweze kupona haraka na kurudia katika afya zao.
    [Show full text]
  • Majina Ya Walimu Wa Ajira Mbadala Shule Za Msingi Na Sekondari
    OFISI YA RAIS - TAMISEMI MAJINA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WA AJIRA MBADALA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI APRILI, 2019 NAMBA YA KIDATO CHA DARAJA/ SOMO LA Na. MAJINA KAMILI JINSI SOMO LA 2 MKOA HALMASHAURI SHULE KIWANGO CHA ELIMU IDARA NNE 1 1 ABAS MATAKA AHMAD S0197-0015/2005 M PHYSICS MATHEMATICS MTWARA MTWARA NDUMBWE SHAHADA SEKONDARI 2 ABAS NDIMUKANWA MATHAYO S0320-0001/2010 M BIOLOGY CHEMISTRY KIGOMA KASULU NYAKITONTO SHAHADA SEKONDARI 3 ABASI RUGA KISHOMI S1192-0053/2013 M MATHEMATICS PHYSICS PWANI KISARAWE KURUI STASHAHADA SEKONDARI 4 ABBAKARI SHIJA S2996-0012/2012 M GRADE IIIA MOROGORO MALINYI MBALINYI ASTASHAHADA MSINGI 5 ABDALLA S DAUDI S0346-0069/2012 M GRADE IIIA SIMIYU BARIADI IKINABUSHU ASTASHAHADA MSINGI 6 ABDALLAH ABDUL S0104-0001/2006 M GRADE IIIA MOROGORO GAIRO KINYOLISI ASTASHAHADA MSINGI 7 ABDALLAH ABDULRAHMAN MWENDA S1483-0064/2009 M MATHEMATICS KAGERA BUKOBA BUJUNANGOMA SHAHADA SEKONDARI 8 ABDALLAH HAMIS ABDALLAH S0769-0059/2011 M GRADE IIIA KIGOMA KASULU ASANTE NYERERE ASTASHAHADA MSINGI 9 ABDALLAH JOHN ZUAKUU S0580-0094/2010 M ACCOUNTING GEOGRAPHY TANGA MUHEZA MLINGANO SHAHADA SEKONDARI 10 ABDALLAH JUMANNE MLEWA S2636-0013/2013 M GRADE IIIA SINGIDA MANYONI KINANGALI ASTASHAHADA MSINGI 11 ABDALLAH MHANDO SAMPIZA S0747-0102/2012 M GRADE IIIA DODOMA KONDOA MKONGA ASTASHAHADA MSINGI 12 ABDALLAH MMUKA S0147-0001/2010 M MATHEMATICS PHYSICS SINGIDA MKALAMA KINAMPUNDU STASHAHADA SEKONDARI 13 ABDALLAH RAMADHANI S0465-0103/2009 M GRADE IIIA SIMIYU MEATU MWAFUGUJI ASTASHAHADA MSINGI 14 ABDALLAH SAIDI ABDALLAH
    [Show full text]
  • Case of Railway Concession in Tanzania
    Lund University Lund University Master of International Development and Management June, 2009 PERFORMANCE OF THE CONTRACTUAL ARRANGEMENTS OF PUBLIC-PRIVATE PARTNERSHIPS: CASE OF RAILWAY CONCESSION IN TANZANIA. Author: Alexander Shlyk Supervisor: Ellen Hillbom Table of Contents: List of Abbreviations................................................................................................. 2 Abstract..................................................................................................................... 3 1. Introduction........................................................................................................... 4 1.1. The Aim ......................................................................................................... 5 1.2. Outline of the Thesis....................................................................................... 6 2. Background........................................................................................................... 7 2.1. Tanzania: Political Transformations................................................................ 7 2.2. Tanzania: Privatization Agenda. ..................................................................... 9 2.3. Transport Corridors in East Africa. ............................................................... 10 3. Theory................................................................................................................. 13 3.1. PPP: a Particular Kind of a Contractual Arrangement. .................................. 13 3.2.
    [Show full text]
  • TANZANIA OIL and GAS ALMANAC TANZANIA OIL and GAS ALMANAC Print Edition June 2015
    TANZANIA OIL AND GAS ALMANAC TANZANIA TANZANIA OIL AND GAS ALMANAC Print edition June 2015 A Reference Guide published by the Friedrich-Ebert-Stiftung Tanzania and OpenOil Tanzania Oil and Gas Almanac A Reference Guide published by the Friedrich-Ebert-Stiftung Tanzania and OpenOil EDITORIAL Abdallah Katunzi – Chief Editor Marius Siebert – Deputy Editor PUBLISHED BY Friedrich-Ebert-Stiftung P.O Box 4472 Mwai Kibaki Road Plot No. 397 Dar es Salaam, Tanzania Telephone: 255-22-2668575/2668786 Email: [email protected] PRINTED BY FGD Tanzania Ltd P.O. Box 40331 Dar es Salaam Disclaimer While all efforts have been made to ensure that the information contained in this book has been obtained from reliable sources, FES (Tanzania) bears no responsibility for oversights or omissions. ©Friedrich-Ebert-Stiftung, 2015 ISBN: 978-9987-483-36-5 A commercial resale of this publication is strictly prohibited unless the Friedrich-Ebert-Stiftung gives explicit and written approval beforehand. PREFACE With an estimated gas reserve of more than 55 trillion cubic feet (Tcf), Tanzania readies itself to join the gas economy. Large multinational oil companies are currently exploring natural gas and oil in various parts of Tanzania – both offshore and onshore. Despite these huge discoveries, there is little publicly available information on natural gas on a wide range of issues. Consequently, the Friedrich-Ebert-Stiftung (FES), Tanzania, with the technical support of OpenOil– a Berlin based organisation – created the Tanzania Oil and Gas Almanac as a living database for publicly available information around the country’s Oil and Gas sector. It has been created to significantly increase the stock of information available in local contexts among extractive stakeholders including civil society organizations, government, journalists and companies.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA SITA ______________ Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 27 Julai, 2009) (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita anayeuliza swali la kwanza, karibuni tena baada ya mapumziko ya weekend, nadhani mna nguvu ya kutosha kwa ajili ya shughuli za wiki hii ya mwisho ya Bunge hili la 16. Swali la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Waziri Mkuu na linauliza na Mheshimiwa Shoka, kwa niaba yake Mheshimiwa Khalifa. Na.281 Kiwanja kwa Ajili ya Kujenga Ofisi ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI MHE KHALIFA SULEIMAN KHALIFA (K.n.y. MHE. SHOKA KHAMIS JUMA) aliuliza:- Kwa kuwa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa Ofisi; na kwa kuwa Tume hiyo imepata fedha kutoka DANIDA kwa ajili ya kujenga jengo la Ofisi lakini inakabiliwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa kiwanja:- Je, Serikali itasaidia vipi Tume hiyo kupata kiwanja cha kujenga Ofisi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Shoka Khamis Juma, Mbunge wa Micheweni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, tatizo la kiwanja cha kujenga Ofisi za TACAIDS limepatiwa ufumbuzi na ofisi yangu imewaonesha Maafisa wa DANIDA kiwanja hicho Ijumaa tarehe 17 Julai, 2009. Kiwanja hicho kipo Mtaa wa Luthuli Na. 73, Dar es Salaam ama kwa lugha nyingine Makutano ya Mtaa wa Samora na Luthuli. MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri, naomba kumuuliza swali moja la nyongeza.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 18 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita muuliza swali la kwanza nina matangazo kuhusu wageni, kwanza wale vijana wanafunzi kutoka shule ya sekondari, naona tangazo halisomeki vizuri, naomba tu wanafunzi na walimu msimame ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwatambua. Tunafurahi sana walimu na wanafunzi wa shule zetu za hapa nchini Tanzania mnapokuja hapa Bungeni kujionea wenyewe demokrasia ya nchi yetu inavyofanya kazi. Karibuni sana. Wapo Makatibu 26 wa UWT, ambao wamekuja kwenye Semina ya Utetezi na Ushawishi kwa Harakati za Wanawake inayofanyika Dodoma CCT wale pale mkono wangu wakulia karibuni sana kina mama tunawatakia mema katika semina yenu, ili ilete mafanikio na ipige hatua mbele katika kumkomboa mwanamke wa Tanzania, ahsanteni sana. Hawa ni wageni ambao tumetaarifiwa na Mheshimiwa Shamsa Selengia Mwangunga, Naibu Waziri wa Maji. Wageni wengine nitawatamka kadri nitakavyopata taarifa, kwa sababu wamechelewa kuleta taarifa. Na. 223 Barabara Toka KIA – Mererani MHE. DORA H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa, Mererani ni Controlled Area na ipo kwenye mpango wa Special Economic Zone na kwa kuwa Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani na inajulikana kote ulimwenguni kutokana na madini hayo, lakini barabara inayotoka KIA kwenda Mererani ni mbaya sana
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 107 Jan - Apr 2014
    Tanzanian Affairs Text 1 Issued by the Britain-Tanzania Society No 107 Jan - Apr 2014 British Aid - New Direction Mandela and Tanzania Chadema’s Crisis Transport in Dar es Salaam Visiting Kilwa Kisiwani AN APOLOGY-TO RICHARD BEATTY OBE Publishing an obituary of someone who is very much alive is the kind of nightmare editors greatly fear. I have been editing Tanzanian Affairs for 28 years and this is the only time that this has happened. When I realised what had happened I did what governments do when they are in trouble. We launched an investigation! Firstly, I came to the conclusion that this document must have passed through my hands at some stage – at present we are juggling with about 80 different stories for our next issue – but my memory is not what it used to be and I can’t remember. Another quite plausible pos- sibility has been suggested. Someone might have sent us an article about your OBE award in the hope that we would publish it and the document might have got into the wrong file i.e. OBIT file instead of OBE file. But we still really don’t know how it happened. I hope you have already received short apologies from members of our editorial team. We have removed the obituary from our online edition. I am feeling very guilty about the distress that this has caused and must add my apologies as humbly as I can. Am relieved to hear from you that there has also been lots of mirth about it. I have found your exhilarating twitter column (@afrenv – highly recommended reading) and realise how much the world would have been a poorer place if the worst had happened.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Tatu – Tarehe 30 Oktoba, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kama kawaida yetu siku ya Alhamisi kazi zetu zinaanza kwa maswali kwa Waziri Mkuu kwa muda wa dakika 30. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu mwulizaji wa swali la kwanza leo ni Mheshimiwa Mzee John Samwel Malecela. MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la kwanza. Mheshimiwa Waziri Mkuu hivi sasa kuna tatizo la uandikishaji wa vijiji vipya, vijiji ambavyo zamani vilikuwa kama vitongoji lakini sasa vimekuwa vijiji vingi na vikubwa na pia kuna tatizo la ugawaji wa kata. Sasa mambo yote haya yanashughulikiwa na TAMISEMI. Je, Serikali haingeona uwezekano wa kukasimu madaraka ya uandikishaji wa vijiji yaende kwenye Halmashauri za Wilaya na suala la uandikishaji wa ugawaji wa kata liende kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo kuondoa msongamano ambao sasa hivi uko TAMISEMI kiasi kwamba viko vijiji ambavyo vimependekezwa na Halmashauri zaidi ya miaka 10 iliyopita lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Mzee Malecela swali lake zuri sana kama ifuatavyo. Mheshimiwa Naibu Spika, sababu ya kuendeleza utaratibu huu wa kutaka jambo hili liwe linaamuliwa katika ngazi hii ni kwamba kuna masuala ya kifedha ambayo yanaendana sambamba na uanzishwaji wa vijiji, kata na maeneo mengine mapya. Kwa hiyo, kwa msingi huo Serikali bado inaona ni vizuri uamuzi kama huo ukaendelea kubaki 1 mikononi mwetu ili hilo liweze kuwa ni jambo ambalo linatu-guide katika kuamua vijiji vingapi safari hii turuhusu itakuwa na component ya Watendaji na kata ngapi kwa sababu utaongeza mambo mengine ndani ya kata.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Tano - Tarehe 4 Novemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Gaudence Kayombo, kwa niaba yake naona Mheshimiwa Mwambalaswa unaweza kumwulizia! Na. 53 Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga Kuwa Mamlaka Kamili MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuza:- Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga umekamilisha vigezo vyote kuwa Mamlaka kamili ya Mji:- Je, ni lini Serikali itaridhia na kutekeleza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence C. Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki, kama ifuatavyo:- 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI)] Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, mwaka 2010, Mheshimiwa Rais, aliahidi kupandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga kuwa Halmashauri ya Mji. Ahadi hii ilitokana na ukweli kwamba, Mamlaka hii imeonekana kukua kwa kasi, kwa maana ya ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi na kijamii na hivyo Serikali inaona ipo haja ya kuipandisha hadhi ili kuingiza dhana ya Mpango Miji kwa lengo la kuzuia ukuaji holela, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za jamii. Mheshimiwa Spika, hata hivyo, mchakato wa kuupandisha hadhi Mji wa Mbinga bado unaendelea na ofisi yangu bado haijapokea maombi kutoka Mkoa wa Ruvuma.
    [Show full text]