NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 8 Julai, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali na tunaanza na ofisi ya Waziri, Mheshimiwa Kayombo, kwa niaba yake Mheshimiwa Rage. Na. 321 Ofisi kwa ajili ya Tarafa-Mbinga MHE. ISMAIL A. RAGE (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuliza:- Wilaya ya Mbinga ina tarafa sita lakini tarafa zote hazina ofisi rasmi zilizojengwa:- Je, ni lini Serikali itajenga ofisi kwa Makatibu Tarafa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence Cassian Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Ruvuma una jumla ya tarafa 24 yaani Tunduru wako saba, Mbinga wana tarafa sita, Nyasa wana tarafa tatu, Namtumbo wana tarafa tatu na Songea wana tarafa tano. Ni kweli tarafa za Wilaya ya Mbinga hazina ofisi rasmi zilizojengwa na Serikali. Ujenzi wa hizo ofisi unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa Mkoa wa Ruvuma umeweka kipaumbele katika ujenzi wa ofisi nne za tarafa katika Wilaya ya Nyasa na Tunduru. Tarafa hizo ni Luhuhu (Lituhi-Nyasa), Ruhekei (Mbamba bay-Nyasa), Mpepo (Tinga-Nyasa) na Nampungu (Nandembo-Tunduru). Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Mkoa ulitenga shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Tarafa ya Luhuhu (Lituhi), Ruhekei (Mbamba bay), Mpepo (Tingi) na Nampungu (Nandembo). Mpaka sasa mkoa umeshapokea kiasi cha shilingi milioni mia moja na hamsini ili kuendelea na ujenzi wa miradi hiyo. Ofisi za Tarafa ya Ruhekei, Luhuhu na Nandembo zimekamilika. Katika mwaka wa fedha wa 2015/2016, Mkoa umetenga kiasi cha shilingi 140, 337,239 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi za tarafa. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 75 zitatumika kukamilisha ofisi ya tarafa ya Mpepo na shilingi 65,337,000 zitatumika kukamilisha kulipa deni la mkandarasi aliyejenga ofisi ya tarafa ya Nandembo katika Wilaya ya Tunduru. Mheshimiwa Mwenyekiti, azma ya Serikali ni kuhakikisha tarafa zote zinakuwa na ofisi. Mkoa umejipanga kutekeleza ujenzi wa ofisi hizo kwa awamu kutokana na ufinyu wa bajeti ikilinganishwa na mahitaji makubwa yaliyopo ya ujenzi wa ofisi hizo na majengo mengine ya Serikali. Serikali inaendelea kuwasisitizia wananchi na wadau mbalimbali kushiriki katika ujenzi wa mjengo mbalimbali ili kuharakisha ukamilishaji wa majengo hayo ikiwemo ujenzi wa ofisi za tarafa. MWENYEKITI: Mheshimiwa Rage. MHE. ISMAIL A. RAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi namheshimu sana rafiki yangu Naibu Waziri lakini leo majibu yake hayakuniridhisha hata kidogo. Mimi nauliza swali linalohusu Wilaya ya Mbinga, yeye ananieleza Wilaya za Nyasa na Tunduru. Interest yangu mimi ni kutaka kujua tarafa sita ambazo ziko Mbinga lini ofisi zake zitaanza kujengwa basi ni hilo tu. Naomba maelezo hayo Mheshimiwa Naibu Waziri. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niliweke hili jambo vizuri kwa sababu najua kwa nini anasema ananishangaa. Ofisi za halmashauri zinajengwa na halmashauri. Ofisi hizi nazozitaja hapa si za Halmashauri ni za Serikali Kuu. Afisa Tarafa anawajibika kwa Mkuu wa Wilaya. Kwa hiyo, napozungumza habari ya mkoa, hela zote tunazozungumza hapa zinapita kwa Katibu Tawala wa mkoa ndipo zinakwenda pale Mbinga. Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme kweli tu, anachosema Mheshimiwa Gaudence Kayombo hapa kwamba hakuna ofisi ambayo imejengwa pale ni kweli. Mimi ninayo orodha hapa ngoja niwaeleze vizuri ili nieleweke nachozungumza na nisome. Mbinga mjini wako katika ofisi ya jengo la ushirika, Kigonsera wako katika ofisi ya VEO(Village Executive Officer), Luanda wako katika ofisi ya kijiji, Mkumbi wako katika ofisi za kijiji, Mbuji wako katika ofisi za kijiji, ofisi hiyo ni ya zamani sana na mikakati iko hapo. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi nikizungumza habari za halmashauri kwamba wamejenga hapa si atatoka Rage tena ataniambia umesema uongo hapa. Ofisi zote nazokuambia hapa haziingii katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga zinapita kwa Katibu Tawala wa Mkoa na jitihada nilizozionyesha hapa ni hizo tunazozungumza hapa. Kwa hiyo, napoeleza hela zilizokwenda nikataja mimi Nandembo, Tunduru, ni kwa sababu hela zote zinafikia Mkoani pale kwa Katibu Tawala wa Mkoa. Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, sisi tunatambua kwamba kuna tatizo kubwa hapa na ndiyo maana tumejibu kuhusu jitihada tunazozifanya hapa, ni pamoja na kuhamasisha wananchi kupitia ofisi za Wakuu wetu wa Wilaya watusaidie kuchangia ofisi hizi kama ambavyo tumekuwa tunafanya katika maeneo mengine. Kusema Wilaya zile nyingine nilisema kwa sababu ofisi inayohusika ni ya Katibu Tawala wa Mkoa. MWENYEKITI: Mheshimiwa Ndassa. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na maelezo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameeleza, niseme tu kwamba tatizo la nyumba za Maafisa Tarafa ni kubwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali langu kwa sababu Afisa Tarafa wa Tarafa ya Ibindo, Wilaya ya Kwimba ana kata nane na Maafisa Tarafa wengine lakini hawana usafiri ili waweze kuwafikia wananchi. Mtu mmoja anazungukia tarafa saba, nane au tisa lakini hana usafiri. Serikali ina utaratibu gani kama ilivyokuwa zamani kwa hawa Maafisa Tarafa kuwapelekea pikipiki ili waweze kufika kwenye maeneo yao ya kazi bila kuchelewa? 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ametaja Tarafa ya Ibindo na anazungumza habari ya kata. Kwa upande wa kata, ni kweli kata hizi ziko chini yetu katika maana ya halmashauri. Kwa maana ya tarafa inabidi niende nikaiangalie hiyo lakini ni kweli pia kama anavyosema Mheshimiwa Richard Ndassa tumekuwa na utaratibu wa kusaidia ofisi zetu za Maafisa Tarafa kupata pikipiki. Kwa hiyo, nitakwenda kufuatilia kwanza kuijua hii Ibindo iko katika utaratibu gani lakini ni jambo ambalo linazungumzika. Kwa upande wa pikipiki ni kweli kabisa kwamba tumekuwa na utaratibu wa kusaidia Maafisa wetu wa Tarafa wafanye kazi hiyo. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Hilda. MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na maelezo mazuri yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri, napenda kumuuliza swali moja dogo tu la nyongeza kwamba yapo majengo mengine ambayo yalijengwa wakati wa mkoloni, majengo ya Makatibu Tarafa ambayo yako katika Makao Makuu ya Tarafa. Kwa mfano, kuna jengo kubwa sana la Tarafa ya Ukukwe, Wilayani Rungwe, Tarafa ya Pakati na Busokelo, majengo haya yamechakaa na hayafanyiwi matengenezo yoyote lakini yangeweza kufaa kabisa kwa kazi za Maafisa Tarafa. Je, Serikali ina mpango gani basi wa kuweza kuyakarabati majengo haya ili yaweze kurudi tena katika upya uleule wa zamani? Ahsante sana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, naelewa anachozungumza hapa ni kwamba kuna majengo haya ambayo yanaonekana yamechakaa na kama tulivyofanya katika Halmashauri ile ya Wilaya ya Mbinga ambayo nimeulizwa mara ya kwanza ni jambo ambalo tunaweza tukafanya lakini watakao- coordinate hii habari itakuwa ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia Katibu Tawala na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Katibu Tawala wa Wilaya, tutakwenda kuangalia hali yake. Tatizo letu ni bajeti kwa sababu katika Regional Secretariat hakuna mahali popote ambapo tunazalisha mali wanategemea zaidi ruzuku ya Serikali na kama nilivyoeleza hapa hela zilizokuwa zimekwenda pale zilikuwa ni shilingi milioni mia tatu. Sasa nitakwenda kuangalia pia kama hizi hela zinaweza zika-spread over zikaangalia pia katika maeneo haya anayosema ya Ukukwe katika Wilaya ile ya Busokelo. MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea na swali la Mheshimiwa Bungara kwa niaba yake Mheshimiwa Shah. 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Na. 322 Tatizo la Maji Hospitali ya Wilaya ya Kilwa MHE. ABDULKARIM E. H. SHAH (K.n.y. MHE. SELEMANI S. BUNGARA) aliuliza:- Kila mwezi Juni hadi Desemba kila mwaka Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) hukabiliwa na tatizo kubwa la maji kutokana na visima kushindwa kutoa maji kunakosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na wakati mwingine hukauka kabisa na kusababisha adha kubwa hospitalini hapo kwa magonjwa ya mlipuko:- Je, Serikali haioni haja ya kutenga bajeti kwa ajili ya kujenga mfumo rasmi wa kuvuna maji ya mvua kama njia sahihi ya kutatua tatizo hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mku, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Said Bungara, Mbunge wa Kilwa Kusini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) kwa sasa inapata maji kiasi cha mita za ujazo kumi na tano sawa na asilimia 32 ya mahitaji yake halisi kutoka katika chemchem ya Kitumba pamoja na kisima kirefu kilichochimbwa kupitia mradi wa TASAF ambacho kinatumiwa pia na wananchi wa Kivinje. Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukabiliana na tatizo la maji katika Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) mwezi Aprili, 2015 Halmashauri imenunua pampu ya kuendeshwa kwa umeme na kuifunga kwenye kisima kilichochimbwa na Kampuni ya
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages136 Page
-
File Size-