Majadiliano Ya Bunge

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Majadiliano Ya Bunge Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 24 Juni, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 111 Malipo ya Likizo za Watumishi MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Ni haki ya Mtumishi kulipwa likizo yake ya mwaka hata kama muda wa likizo hiyo unaangukia muda wake wa kustaafu:- Je, Serikali inatoa kauli gani kwa Watumishi ambao wamenyimwa likizo zao kwa kisingizio kuwa muda wao wa kustaafu umefika na kunyimwa kulipwa likizo zao. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pauline Gekul, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni H. I ya Kanuni za Kudumu ( Standing Orders) likizo ni haki ya mtumishi. Endapo mwajiri ataona kuwa hawezi kumruhusu mtumishi kuchukua likizo yake, analazimika kumlipa mshahara wa mwezi mmoja mtumishi huyo. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni H.5 (a) ya Kanuni hizi, mtumishi hulipiwa nauli ya likizo kila baada ya miaka miwili. 1 Mheshimiwa Spika, kutokana na miongozo niliyoitaja, ni makosa kutomlipa mtumishi stahili yake ya likizo kabla ya kustaafu. MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi hii ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya msingi ya Waziri amesema kwamba ni haki ya watumishi wa Umma kulipwa likizo zao pale wanapostaafu. (a) Je, Serikali haioni kwamba sasa ni wakati mwafaka wa kulipa likizo za wastaafu hao ambao wamestaafu lakini hawakulipwa likizo zao? (b) Kwa kuwa mtumishi anapostaafu anahitaji kurudi katika eneo ambalo ametoka, na kwa kuwa katika shule za msingi katika Halmashauri ya mji wa Babati walimu wapatao watano (5) hawakuweza kulipwa likizo zao walipostaafu tangu mwaka jana mwezi wa kwanza mpaka leo, lakini pia walimu hao hawakuweza kupewa fedha za kusafirishia mizigo yao. Je, Serikali haioni kwamba imewatesa walimu hao kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa hawapewi fedha za kusafirishia mizigo yao makwao na wakati huo huo hawajalipwa likizo. Je, Serikali inasema nini kuhusu wastaafu hao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA):- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Pauline Gekul, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, hapa tunazungumzia sheria hata kama mtu amekaa miaka mitano au mingapi, sheria ikisema kwamba ni haki yake alipwe na kama hakulipwa hatuwezi kukaa tuna-debate hapa, debate ya sheria iliishamalizika. Kwa hiyo hapa kama Mheshimiwa Mbunge anafikiri kwamba kuna watumishi waliondoka bila kulipwa kwa misingi hii ya sheria niliyoitaja hapa atuletee mara moja tutamwona Mheshimiwa Hawa Ghasia na kuzungumza naye na kumwambia hawa walipwe haki yao. Hatuwezi ku-debate hapa habari hiyo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge uwe na amani moyoni mwako, wewe katuletee na huyo unayesema kwamba alistaafu hapo akaenda bila kulipwa tuelewane kabisa. Mheshimiwa Spika, lakini nataka ni-quotion kitu kimoja. Haki inayozungumzwa hapa ni haki ya mshahara kwa sababu usije ukasema kwamba nipe mshahara halafu 2 useme nipatie pia na nauli yangu ya kwenda Muleba, akikulipa mshahara ndiyo habari imeishia hapo kwa maana ya mshahara aliokulipa. Kwa hiyo, mimi nataka nitahadharishe tu, lakini sisi tuko tayari kusikia hilo tutazungumza nao. Nimeita watu wangu wa human resources, tumezungumza na bwana Paraga amenieleza kwamba utaratibu ndiyo huo, lakini mimi niko tayari kumsikiliza tuasaidiane. MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Manispaa ya Kigoma Ujiji kuna walimu wengi sana ambao wamekuwa wanaenda likizo hawajapata stahili zao ni zaidi ya miaka miwili, mitatu. Pamoja na kwamba amesema hilo ni suala la sheria, lakini sheria isiyotekelezwa maana yake ni nini sasa? Naomba Mheshimiwa Waziri aniambie kuhusu jambo hili. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Peter J. Serukamba, Mbunge wa Kigoma Mjini, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, mimi hapa nazungumzia matukio na sheria kwa maana ya nchi nzima. Mheshimiwa Serukamba anasema kwamba kuna watu ambao hawakupewa haki yao. Mimi nimekwenda Morogoro pale nika- head delegation pale na nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ambayo ili-review madai ya watumishi wote ukiacha hata na walimu wanaozungumzwa hapa. Tukasema tufanye mahesabu tuangalie kila kitu kinachodaiwa pale, baadaye tukaambiwa kwamba tupeleke madai yale kwa CAG’s Office aangalie na ahakiki aseme anaonaje kuhusu hayo madai. Taarifa ya CAG ikatoka ikasema kwamba hawa haki zao ni hizi, hawa haki zao ni hizi. Mheshimiwa Spika, hapa tuna-deal na nchi nzima, inawezekana kabisa kama anavyosema Mheshimiwa Serukamba kwamba katika hali hiyo bado kuna walioponyoka pale wakawa hawakulipwa haki zao. Mimi namuomba atuletee majina ya wale walimu anaowasema hapa sisi kama Serikali tutashughulikia jambo hilo. Na. 112 Matokeo Mabaya ya Kidato cha Nne MHE. VINCENT J. NYERERE aliuliza:- Matokeo ya mtihani wa kidato cha Nne mwaka 2010 hayakuwa mazuri na yameacha vijana wengi mitaani na vijijini, vijana ambao ni tegemeo la nguvu kazi ya Taifa lakini wamebaki bila elimu wala matarajio yoyote. 3 Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya vijana hao wengi waliobaki mitaani kutokana na kufeli katika mitihani yao. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA YA UFUNDI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vicent Josephat Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, matokeo ya mtihani wa kidato cha Nne mwaka 2010 hayakuwa mazuri na vijana wengi walishindwa mtihani huo. Kufuatia hali hiyo na kwa kuzingatia maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Seriakli za Mitaa(TAMISEMI) tumefanya utafiti ili kubaini sababu za ufaulu duni, na nini kifanyike kwa wanafunzi walioshindwa mtihani huo. Mheshimiwa Spika, kazi hii ya utafiti wa ufaulu duni imekamilika na Serikali itatoa tamko juu ya hilo katika mkutano huu wa Nne wa Bunge lako Tukufu. Aidha, wakati tunasubiri tamko hilo la Serikali, namwomba Mheshimiwa Mbunge pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote wawe na subira. MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mabaya ya kukatisha tamaa ya Mheshimiwa Waziri, naomba kumwuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa mojawapo ya majibu ya tafiti itakuwa ni ukosefu wa walimu, vifaa vya kufundishia na maabara na si kosa la wazazi na wanafunzi bali ni kosa la Serikali. (a) Je, Serikali haioni sasa ni muda mwafaka wa kuhakikisha watoto hao wanarudi shuleni ili wasome na wafanye mitihani na washinde ili wasiharibikiwe na maisha hapo baadae? (b) Je, Serikali haioni sasa ni muda mwafaka wa kufundisha stadi za kazi katika shule za sekondari kwa vitendo ili watoto wanaoshindwa kuingia kidato cha tano waweze kwenda katika soko la ajira moja kwa moja? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, ningependa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Vicent Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, moja ni kuhusu sababu za ufaulu duni wa Kidato cha Nne. Kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge ni kweli michango yake ni mingi na hatuwezi tukawachukulia wanafunzi wale kwamba wao wenyewe tu peke yao ndiyo walikuwa wana makosa kwa ufaulu huu duni. 4 mSerikali imefanya utafiti imegundua, lakini kwa lile ambalo Mheshimiwa Mbunge amelipendekeza halitakuwa rahisi kulitekeleza kwa nchi nzima, kwa maana ya kuwarudisha wanafunzi wale wa kidato cha nne wote shuleni katika shule zetu hizi kwa sababu sisi sote tunafahamu kwamba katika shule zetu za Sekondari bado tuna mapungufu ambayo Serikali inahangaika kuweza kuyaweka vizuri ili tuweze kupata elimu bora. Mheshimiwa Spika, tuna uhaba wa madarasa na vitendeakazi. Sasa hivi kuna vijana tayari ni Form Four pamoja na kwamba kuna mapungufu kule madarasani, utakapowaleta tena wengine waingie humo humo kwenye Form Four ile bila shaka ni kwamba uwezo hautakuwepo wa kuwahudumia nao kwa lengo la kuweza kufanya mtihani kama wanafunzi wenzao wanaosoma full time. Kwa hiyo, hilo bahati mbaya hatutaweza kumudu kulifanya. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la pili kwamba Serikali ibadilishe mitaala ili iwe na mafunzo ya vitendo ili kumwezesha mwanafunzi awe na uwezo mkubwa zaidi anapomaliza shule. Hilo tutalizingatia, tumeanza kulifanyiakazi na tutaendelea kuhakikisha kwamba tunalifanyiakazi vizuri zaidi. (Makofi) MHE. AGNESS E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona, naomba niulize swali la nyongeza kama ifuatavyo. Kwa kuwa Wizara imetoa mwongozo kwa maswali katika shule za msingi kujibiwa kwa njia ya multiple choise au kwa kutikii. Je, Serikali haioni kwamba kwa kuendelea kufanya hivyo tunatengeneza watoto ambao wanafaulu kwa njia ya kubuni kwa kuwa watakuwa wanatiki tu kwa ku-guess hali ambayo itaendeleza watoto kufeli kama ilivyojitokeza
Recommended publications
  • Process in Tanzania the Political, Civil and Economic Society
    Tanzania has been independent in 2011 for 50 years. While most neighbouring states have Jonas gone through violent conflicts, Tanzania has managed to implement extensive reforms with- out armed political conflicts. Hence, Tanzania is an interesting case for Peace and Develop- ment research. E Challenges for the This dissertation analyses the political development in Tanzania since the introduction of wald the multiparty system in 1992, with a focus on the challenges for the democratisation process democratisation in connection with the 2000 and 2005 elections. The question of to what extent Tanzania has moved towards a consolidation of democracy, is analysed through an analysis of nine different institutions of importance for democratisation, grouped in four spheres, the state, Challenges for the process in Tanzania the political, civil and economic society. Focus is on the development of the political society, and the role of the opposition in particular. The analysis is based on secondary and primary Moving towards consolidation 50 years material collected in the period September 2000 to April 2010. after indepencence? The main conclusion is that even if the institutions of liberal democracy have gradually developed, in practice single-party rule has continued, manifested in the 2005 election when the CCM won 92% of the seats in the parliament. Despite an impressive economic growth, poverty remains deep and has not been substantially reduced. On a theoretical level this brings the old debate between liberal and substantive democracy back to the fore. Neither the economic nor the political reforms have apparently brought about a transformation of the political and economic system resulting in the poor majority gaining substantially more political influence and improved economic conditions.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA NANE Kikao Cha Kumi Na Tano
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 3 Julai, 2007 (Kikao Kilianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI:- Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mkiangalia Order Paper yetu ya leo, hati za kuwasilisha Mezani iko, Ofisi ya Makamu wa Rais, yuko Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Mazingira, tumemruka Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria na Utawala, halafu atakuja Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA): Hotuba ya Bajeti ya Wizari wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha wa 2007/2008. MWENYEKITI WA KAMATI YA MALIASILI NA MAZINGIRA: Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA (MHE. RAMADHAN A. MANENO): Tarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano kwa mwaka wa Fedha 2006/2007 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2007/2008. MHE. RIZIKI OMARI JUMA (k.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): 1 Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja Maoni ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • 16 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd
    16 MEI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Saba – Tarehe 16 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Waheshimiwa Wabunge Kikao cha Ishirini na Saba kinaanza. Mkutano wetu wa Kumi na Moja. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI:- Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 16 MEI, 2013 MHE. PROF. JUMA A. KAPUYA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. PAULINE P. GEKUL (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA UCHUKUZI): Taaqrifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Uchukuzi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kama kawaida yetu siku ya Alhamisi tunakuwa na Kipindi cha Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu na swali la kwanza la siku ya leo linaulizwa na Mheshimiwa Stephen Hilary Ngonyani. MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kunipa chakula cha msaada kule kwenye jimbo langu. Swali linalokuja ni hivi. Mheshimiwa Naibu Spika, Kitengo cha Maafa ni Kitengo ambacho kiko chini ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, nchi nzima kinajua jinsi unavyosaidia wananchi.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 18 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita muuliza swali la kwanza nina matangazo kuhusu wageni, kwanza wale vijana wanafunzi kutoka shule ya sekondari, naona tangazo halisomeki vizuri, naomba tu wanafunzi na walimu msimame ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwatambua. Tunafurahi sana walimu na wanafunzi wa shule zetu za hapa nchini Tanzania mnapokuja hapa Bungeni kujionea wenyewe demokrasia ya nchi yetu inavyofanya kazi. Karibuni sana. Wapo Makatibu 26 wa UWT, ambao wamekuja kwenye Semina ya Utetezi na Ushawishi kwa Harakati za Wanawake inayofanyika Dodoma CCT wale pale mkono wangu wakulia karibuni sana kina mama tunawatakia mema katika semina yenu, ili ilete mafanikio na ipige hatua mbele katika kumkomboa mwanamke wa Tanzania, ahsanteni sana. Hawa ni wageni ambao tumetaarifiwa na Mheshimiwa Shamsa Selengia Mwangunga, Naibu Waziri wa Maji. Wageni wengine nitawatamka kadri nitakavyopata taarifa, kwa sababu wamechelewa kuleta taarifa. Na. 223 Barabara Toka KIA – Mererani MHE. DORA H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa, Mererani ni Controlled Area na ipo kwenye mpango wa Special Economic Zone na kwa kuwa Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani na inajulikana kote ulimwenguni kutokana na madini hayo, lakini barabara inayotoka KIA kwenda Mererani ni mbaya sana
    [Show full text]
  • MKUTANO WA 18 TAREHE 5 FEBRUARI, 2015 MREMA 1.Pmd
    5 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Tisa – Tarehe 5 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, leo sijamwona. Kwa hiyo tunaendelea na Maswali kwa Waziri Mkuu na atakayeanza ni Mheshimiwa Murtaza A. Mangungu. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa vipindi tofauti vya Bunge Mheshimiwa Peter Msigwa, Mheshimiwa Mussa Zungu na hata Mheshimiwa Murtaza A. Mangungu wamekuwa wakiuliza swali kuhusiana na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara Wadogo Wadogo pamoja na Mamalishe. Kwa kipindi hicho chote umekuwa ukitoa maagizo na maelekezo, inavyoonekana mamlaka zinazosimamia hili jambo haziko tayari kutii amri yako. 1 5 FEBRUARI, 2015 Je, unawaambia nini Watanzania na Bunge hili kwa ujumla? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Murtaza Mangungu swali lake kama ifuatavyo:- Suala hili la vijana wetu ambao tunawajua kama Wamachinga, kwanza nataka nikiri kwamba ni suala kubwa na ni tatizo kubwa na si la Jiji la Dar es Salaam tu, bali lipo karibu katika miji mingi. Kwa hiyo, ni jambo ambalo lazima twende nalo kwa kiwango ambacho tutakuwa na uhakika kwamba tunalipatia ufumbuzi wa kudumu. Kwa hiyo, ni kweli kwamba mara kadhaa kuna maelekezo yametolewa yakatekelezwa sehemu na sehemu nyingine hayakutekelezwa kikamilifu kulingana na mazingira ya jambo lenyewe lilivyo. Lakini dhamira ya kutaka kumaliza tatizo hili la Wamachinga bado ipo palepale na kwa bahati nzuri umeuliza wakati mzuri kwa sababu jana tu nimepata taarifa ambayo nimeandikiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ambayo wanaleta mapendekezo kwangu juu ya utaratibu ambao wanafikiri unaweza ukatatua tatizo hili ambalo lipo sehemu nyingi.
    [Show full text]
  • Consequences for Women's Leadership
    The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures by Christie Marie Arendt B.A. in Interdisciplinary Studies in Social Science, May 2004, Michigan State University M.A. in International Affairs, May 2006, The George Washington University A Dissertation submitted to The Faculty of The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University in partial fulfillment of the requirements for the degree of Doctor of Philosophy January 31, 2017 Dissertation directed by Kimberly J. Morgan Professor of Political Science and International Affairs The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University certifies that Christie Marie Arendt has passed the Final Examination for the degree of Doctor of Philosophy as of December 16, 2016. This is the final and approved form of the dissertation. The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures Christie Marie Arendt Dissertation Research Committee: Kimberly J. Morgan, Professor of Political Science and International Affairs, Dissertation Director Jennifer Brinkerhoff, Professor of International Affairs, International Business, and Public Policy & Public Administration Eric Kramon, Assistant Professor of Political Science and International Affairs, Committee Member ii © Copyright 2017 by Christie Marie Arendt All rights reserved iii Dedication To my parents, Anne and Steve Arendt, none of this was possible without your enduring love and support. iv Acknowledgments This dissertation benefitted from the encouragement and guidance of a number of people. As an alumna of The George Washington University’s Elliott School of International Affairs, I knew that GW would provide a perfect environment to pursue my doctoral studies.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA NANE Kikao Cha
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 29 Juni, 2007 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa Kuwasilisha Hati. Naomba niwashukuru nyote jinsi tulivyoshirikiana kwa pamoja kuweza kumsindikiza mwenzetu Marehemu Amina Chifupa Mpakanjia, katika safari yake ya mwisho. Waheshimiwa Wabunge, napenda niwashukuru Kamati ya Uongozi na Tume ya Huduma za Bunge, lakini pia TWPG kwa kushirikiana vizuri sana kuweza kumsindikiza mwenzetu kwa heshima; na kipekee naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu atutolee salamu za shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais alivyokuwa karibu nasi kila dakika kwa mawasiliano hadi hapo jana kule Njombe. Waheshimiwa Wabunge, narejea tena Mungu ailaze roho ya Marehemu Mheshimiwa Amina Chifupa Mpakanjia, mahali pema peponi. Amin. Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa mwaka 2005/2006 (The Annual Report and Accounts of the Tanzania National Parks for the Year 2005/2006). MASWALI NA MAJIBU Na. 106 Ubovu wa Barabara za Jiji la Dar es Salaam MHE. MUSSA A. ZUNGU aliuliza:- 1 Kwa kuwa sura ya nchi yetu iko katika Jimbo la Ilala; na kwa kuwa barabara nyingi za Jiji la Dar es Salaam ni mbovu sana hali inayosababisha msongamano wa magari na
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA NANE Kikao
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 28 Juni, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo ni siku nyingine ya Alhamisi ambayo tunakuwa na nusu saa kwa maswali ya Waziri Mkuu na baadaye maswali mengine ya kawaida. Namwona Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kwamba yupo leo, kama kanuni yetu inavyoruhusu yeye ndiye ataanza kuuliza swali la kwanza. MHE. FREEMAN A. MBOWE – KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la kwanza kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. 1 Mheshimiwa Waziri Mkuu, wewe ni Kiongozi Mkuu na Kiongozi muhimu katika Serikali na kauli yako ni kauli nzito sana. Siku ya jana ulitoa kauli ambayo kama mzazi ama kama baba imetia hofu kubwa sana katika Taifa, pale ulipokuwa unazungumzia mgomo wa Madaktari na hatimaye ukasema na linalokuwa na liwe. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuanzia jana baada ya kauli yako vilevile zilipatikana taarifa zingine kwamba Rais wa Madaktari Dkt. Ulimboka ametekwa juzi usiku, ameteswa, amevunjwa meno, ameng’olewa kucha na mateso mengine mengi sana na kwa sababu uliahidi Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba mtatoa kauli ya Serikali leo. Jambo hili sasa limechukua sura mpya na katika maeneo mbalimbali ya nchi, tayari Madaktari wengine wako kwenye migomo. Wewe kama Waziri Mkuu unalieleza nini Taifa kuhusu kauli yako ya litakalokuwa na liwe na Serikali inafanya nini cha ziada ku-address tatizo hili? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijaribu kutoa ufafanuzi kwenye maeneo mawili ambayo Mheshimiwa Mbowe ameyazungumza.
    [Show full text]
  • Bulombora Jkt- Kigoma
    BULOMBORA JKT- KIGOMA NA SHULE JINSI JINA KIKOSI 1 AFRICAN TABATA HIGH SCHOOL M MARTINUS EUSTACE SOSPETER 821KJ 2 AGAPE LUTHERAN J SEMINARY M ERICK ELLY MGONJA 821KJ 3 AGAPE LUTHERAN J SEMINARY M JAMES JACOB MUSHI 821KJ 4 AGAPE MBAGALA SECONDARY SCHOOL M JAMES JOSEPH CHACHAGE 821KJ 5 AHMES SECONDARY SCHOOL M EDWIN DOUGLAS SAKIBU 821KJ 6 AHMES SECONDARY SCHOOL M FLAVIAN P LUGONGO 821KJ 7 AHMES SECONDARY SCHOOL M FREDY NYAKUNGA 821KJ 8 AILANGA LUTHERAN JUNIOR SEMINARY M BENJOHNSON B BEJUMLA 821KJ 9 AILANGA LUTHERAN JUNIOR SEMINARY M KELVIN MICHAEL KIPUYO 821KJ 10 ALLIANCE BOYS SECONDARY SCHOOL M EMMANUEL KISIBA 821KJ 11 ALLIANCE BOYS SECONDARY SCHOOL M FAISON F MAFWELE 821KJ 12 ALLIANCE BOYS SECONDARY SCHOOL M FRANK NYANTARILA 821KJ 13 ALLIANCE BOYS SECONDARY SCHOOL M KUBINGWA RAMADHAN OMARY 821KJ 14 ALLIANCE BOYS SECONDARY SCHOOL M MORICE BOAZ KIMORI 821KJ 15 AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY M ABDALLAH ABDUL-QADIR MOHAMED 821KJ 16 AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY M ABDALLAH I CHAUREMBO 821KJ 17 AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY M FAHAD KHALEF MOHAMED 821KJ 18 AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY M HASSAN ABBAS RUMBONA 821KJ 19 AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY M KHALIFA ALLY 821KJ 20 AL-MUNTAZIR ISLAMIC SEMINARY M MOHAMEDAKRAM GAFUR ISSA 821KJ 21 ALPHA SECONDARY SCHOOL M ABDULKADIR M SHIENGO 821KJ 22 ALPHA SECONDARY SCHOOL M AHMED S KAJIRU 821KJ 23 ALPHA SECONDARY SCHOOL M DANIEL E SANGA 821KJ 24 ALPHA SECONDARY SCHOOL M EMMANUEL DICKSON KABUDI 821KJ 25 ALPHA SECONDARY SCHOOL M FRANCIS S MDAKI 821KJ 26 ALPHA SECONDARY SCHOOL M FRANCISCO XAVERY SITTA 821KJ 27 ALPHA
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Nane
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao Cha Tano - Tarehe 30 Januari, 2010 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI Muswada wa Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa wa Mwaka 2009 (The National Security Council Bill, 2009) (Kusomwa Mara ya Pili) NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama tulivyosema, leo Siku ya Jumamosi hatutaanza na kipindi cha maswali kwa sababu tumetengua Kanuni ili tuweze kukamilisha kazi nyingine ambazo zimezidi; kwa hiyo, tunakwenda moja kwa moja kwenye Muswada. Sasa namwita mtoa hoja awasilishe Muswada. Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora). WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Muswada wa Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa wa Mwaka 2009 (The National Security Council Bill, 2009), sasa usomwe mara ya pili. Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, napenda kuungana na wenzangu waliotangulia kutoa pole kwa Mheshimiwa Vita Kawawa na Familia ya Marehemu Mheshimiwa Mzee Rashid Mfaume Kawawa, kwa kuondokewa na baba yao, Mzee wetu Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa. Pole hizo pia nazitoa kwa Watanzania wote kwa sababu Marehemu Mzee Kawawa ni mmoja wa Viongozi Waasisi la Taifa letu. Aidha, napenda pia kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wote wa Jimbo la Ruangwa kwa kuondokewa na mpendwa wao na Mbunge wao, Marehemu Sigfrid Ng’itu. Naomba Mwenyezi Mungu, aziweke roho za Marehemu pahala pema peponi na awajalie ndugu wa Marehemu moyo wa subira.
    [Show full text]