SUMAJKT Ili Kuwa Vya Kisasa Na Imara Katika Kutekeleza Majukumu Yake

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

SUMAJKT Ili Kuwa Vya Kisasa Na Imara Katika Kutekeleza Majukumu Yake Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MKUTANO WA NANE _______________ Kikao cha Ishirini na Nane – Tarehe 16 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:- Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:- Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. BETTY E. MACHANGU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA):- Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza maswali Ofisi ya Waziri na Mheshimiwa Ramadhani Haji Saleh ndio atakayeuliza swali la kwanza. Na. 196 Uwekezaji Katika Sekta ya Uvuvi MHE RAMADHAN HAJI SALEH aliuliza:- Sekta ya Bahari ni chanzo cha pili cha Mapato katika nchi ukiacha Madini kama itatumika vizuri lakini bado Serikali haijawekeza katika sekta hiyo:- Je, ni lini sasa Serikali itawekeza katika Sekta ya Bahari? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ramadhani Haji Saleh, Mbunge wa Bumbwini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inakubali kwa Sekta ya Bahari na hususan uvuvi ni muhimu kwa mapato ya nchi yetu. Hivyo, Serikali imeendelea kuboresha mazingira kwenye Sekta ya Bahari na hasa uvuvi ili kuwezesha wadau wa sekta hiyo, ikiwemo sekta binafsi kuwekeza ipasavyo. Baadhi ya mazingira hayo ni kuwepo kwa Sera ya Uwekezaji Nchini, Sera ya Taifa ya Uvuvi (1997), Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Sheria ya Kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi kwenye Bahari Kuu Na. 17 ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007. Aidha, Serikali imeandaa programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi ambayo tayari imeingizwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambayo itatekelezwa na Taifa, Halmashauri zote nchini zenye maji. Sekta ya Bahari, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge inapewa umuhimu mkubwa. Mheshimiwa Mbunge miundombinu mbalimbali imejengwa na kuboreshwa. Kwa mfano, Mialo 25 ya kupokelea samaki katika Ziwa Victoria imeboreshwa na Mialo mitatu (3) inajengwa katika ukanda wa Pwani. Aidha, kwa kushirikiana na Mradi wa Uwiano wa Bonde la Ziwa Tanganyika, Serikali itajenga Mialo minne (4) katika ukanda wa Ziwa Tanganyika. Serikali pia imekamilisha ujenzi wa masoko makubwa ya kupokelea samaki ya Ferry, Dar es Salaam na Kirumba, Mwanza, pamoja na soko la Kasanga, Rukwa. Vile vile, Serikali imehamasisha sekta binafsi kuongeza thamani ya mazao kwa kuanzisha viwanda vya kisasa 17 vya kuchakata samaki na mazao ya uvuvi, viwanda vidogo 17 na maghala 84. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika maeneo mbalimbali katika Sekta ya uvuvi. Aidha, Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye zana za uvuvi ikiwa ni pamoja na injini za kupachika, vifungashio, nyuzi za kutengeneza nyavu na kufuta kodi ya zuio kwa usafirishaji wa samaki nje ya nchi. MHE. RAMADHANI HAJI SALEH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri, lakini naomba nimwulize swali moja la nyongeza. Kutokana na utafiti uliofanywa katika Bahari yetu ya Hindi kumegunduliwa samaki wengi sana na kutokana na meli nyingi kutoka nje kuja kuvua katika bahari yetu. Je, Serikali hili imeliona vipi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa na ni jambo la kufurahisha kwamba utafiti umeonyesha kwamba bahari yetu ina samaki wengi na wa kuvutia meli kufika kwenye eneo la bahari yetu kutaka kuvua ili na wao wanufaike. Serikali imeliona hilo itaongeza kwanza uwekezaji ili sisi wenyewe tunufaike na rasilimali samaki kwenye eneo letu la bahari. Lakini vilevile kuongeza ulinzi ili meli kutoka nje zisiweze kuvua samaki wetu bali sisi wenyewe tunufaike nao. Pamoja na hivyo kama nilivyosema sera inaeleza kwamba lazima tushirikiane na sekta binafsi kuona kwamba uvuvi na teknolojia bora zaidi inatumika katika kuvua rasilimali kutoka bahari yetu. MHE. ALPHAXARD K. N. LUGOLA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika jibu la msingi Mheshimiwa Waziri amejaribu kuonyesha kwamba uwekezaji katika sekta ya Bahari ni suala la uvuvi tu. Lakini kuna suala hili la uzalishaji wa mabaharia hasa katika ngazi ya digrii na elimu zaidi ya hiyo. Sasa Chuo chetu cha DMI ilikuwa kiingie ubia na Wachina na kujaribu kujenga chuo ambacho kitazalisha Mabaharia. Waziri anasema nini katika sekta hii ya Bahari katika uzalishaji wa mabaharia kuliko tu alichozungumzia uvuvi wakati swali zima linazungumzia sekta ya Bahari? SPIKA: Sina uhakika kama ni uzalishaji wa mabaharia au ufundishaji wa mabaharia waliohusika. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Lugola kama alirejea majibu yangu ya msingi, nilisema sekta ya Bahari nikasema hususan uvuvi. Kwa hivyo sekta ya Bahari inahusisha na kuwafunza mabaharia au kuwanoa mabaharia kusudi basi tuwe na watu ambao wataendesha meli kwenda kuvua kwenye bahari yetu. Kwa hivyo na uvuvi nao unahitaji mabaharia hao wawe na uwezo, wawe na ujuzi na wawe ni majasiri kwenda kuvua hasa kwenye deep sea au bahari ya mbali. MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi ili niweze kumwuliza Waziri swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amekubali kabisa kwamba bahari yetu ina samaki wengi sana. Je, ni jambo gani au ni sababu gani inayopelekea nchi yetu kuruhusu samaki kuingia nchini kutoka nje ya nchi ikiwepo nchi ya Japan wakati ambapo tuna samaki wengi sana? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa mujibu wa utafiti kwamba tuna samaki wengi. Lakini ni kweli vilevile kwamba katika enzi hizi za utandawazi huwezi ukazuia soko lako jambo lililo muhimu ni kwamba sisi Watanzania tupende vya kwetu zaidi hata pale ambapo watu wanakuwa na choice au wanaweza kuchagua kitu kutoka nje. Lakini pam oja na uzalendo vilevile tuongeze uwezo wetu wa kuvua ili tuwe na samaki wa kutosha ili Watanzania waweze kuchagua samaki wa kwao badala ya wale wanaotoka nje wanaokaa kwenye barafu muda mrefu kwanza na usalama wake ukilinganisha na samaki wa kwetu watakuwa salama zaidi kwa sababu ni karibu na sisi. Na. 197 Gharama Kubwa za Kuendesha Chaguzi Ndogo MHE. PINDI H. CHANA aliuliza:- Zoezi la kuendesha Chaguzi Ndogo nchini limekuwa ni gharama kubwa sana kwa vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla:- Je, Serikali haioni kuna haja ya kulitafakari upya jambo hili na kuja na mpango wa gharama ndogo ya kuendesha Chaguzi Ndogo ama kwa kutumia “Proportional Representation” au Uchaguzi kufanyika baada ya miaka miwili na nusu (2 ½ )? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Pindi Hazara Chana, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba zoezi la kuendesha Chaguzi Ndogo limekuwa la gharama kubwa kwa Serikali, Vyama vya Siasa na Wananchi kwa ujumla. Katika hilo naomba nimpe mifano miwili inayothibitisha ukweli wa kauli hiyo Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 - 2010 zilifanyika Chaguzi Ndogo za Wabunge sita (6) katika Majimbo ya Wilaya ya Tunduru, Kiteto, Tarime, Mbeya Vijijini na Busanda. Wastani wa gharama zilizotumika katika Chaguzi Ndogo 2005-2010 kwa Ubunge peke yake ilikuwa ni shilingi 9,261,810,000/=. Lakini kwa Madiwani katika kipindi hicho zilifanyika Chaguzi Ndogo 75 nazo ziligharimu shilingi bilioni 9,555,000,000/=. Lakini kipindi hiki baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 zimefanyika Chaguzi Ndogo mbili katika Majimbo ya Igunga na Arumeru Mashariki, fedha zilizotumika kuendeshea uchaguzi huu ni shs. 3,087,270,000/=. Lakini pia zimefanyika Chaguzi Ndogo 30 za Madiwani ambazo Serikali imetumia shs. 3,822,000,000/= na hizi fedha zote huwa kwa kweli ni za dharura. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba umeshaanza, suala hili linaweza kujadiliwa kwa kina katika mchakato huo ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya Mheshimiwa Mbunge. Napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa wananchi wote, kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali, likiwemo hili la namna bora ya kujaza nafasi wazi za Ubunge na Udiwani wakati Tume ya Mabadiliko ya Katika itakapotembelea maeneo yao. MHE. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante. pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge. Kwa kuwa fedha hizi tunazotumia kwenye Chaguzi Ndogo kwa kweli ni nyingi zingeweza kujenga madarasa, maji na kadhalika. Na kwa kuwa zoezi la Katiba linaloendelea ambalo ni matarajio yetu mwaka 2014 ndio liwe limekamilika haliathiri majukumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ambayo ni kutunga sheria na kurekebisha sheria. Je, Serikali haioni ni wakati muafaka watuletee humu ndani Sheria ya Uchaguzi sisi Wabunge kwa pamoja tuijadili, tuitafakari ifanye kazi hadi Uchaguzi wa mwaka 2015 na baadaye maoni yatakapokuja kwenye Katiba basi maoni yale yatachukua nafasi yake? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kama nilivyosema jambo hili lina gharama kubwa na imethibitisha hivyo. Lakini mapendekezo aliyotoa Mheshimiwa Mbunge ni mazuri sana ya kurekebisha sheria, lakini lazima uanzie kwenye Katiba.
Recommended publications
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA KUMI NA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 21 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI SABA KIKAO CHA KUMI NA NNE – 21 NOVEMBA, 2014 I. DUA Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu alisoma Dua saa 3.00 Asubuhi na kuliongoza Bunge. MAKATIBU MEZANI – i. Ndg. Asia Minja ii. Ndg. Joshua Chamwela II. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge:- 1. OFISI YA WAZIRI MKUU Swali Na. 161 – Mhe. Betty Eliezer Machangu [KNY: Mhe. Dkt. Cyril Chami] Nyongeza i. Mhe. Betty E. Machangu, mb ii. Mhe. Michael Lekule Laizer, mb iii. Mhe. Prof. Peter Msolla, mb Swali Na. 162 - Mhe. Richard Mganga Ndassa, mb Nyongeza (i) Mhe Richard Mganga Ndassa, mb Swali Na. 163 - Mhe. Anne Kilango Malecela, mb Nyongeza : i. Mhe. Anne Kilango Malecela, mb ii. Mhe. John John Mnyika, mb iii. Mhe. Mariam Nassor Kisangi iv. Mhe. Iddi Mohammed Azzan, mb 2 2. OFISI YA RAIS (UTUMISHI) Swali Na. 164 – Mhe. Ritta Enespher Kabati, mb Nyongeza i. Mhe. Ritta Enespher Kabati, mb ii. Mhe. Vita Rashid Kawawa, mb iii. Mhe. Mch. Reter Msingwa, mb 3. WIZARA YA UJENZI Swali Na. 165 – Mhe. Betty Eliezer Machangu, mb Nyongeza :- i. Mhe. Betty Eliezer Machangu, mb ii. Mhe. Halima James Mdee, mb iii. Mhe. Maryam Salum Msabaha, mb Swali Na. 166 – Mhe. Peter Simon Msingwa [KNY: Mhe. Joseph O. Mbilinyi] Nyongeza :- i. Mhe. Peter Simon Msigwa, Mb ii. Mhe. Assumpter Nshunju Mshama, Mb iii. Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa 4.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015 ELECTION EDITION: MAGUFULI vs LOWASSA Profiles of Key Candidates Petroleum Bills Ruaha’s “Missing” Elephants ta112 - final.indd 1 8/25/2015 12:04:37 PM David Brewin: SURPRISING CHANGES ON THE POLITICAL SCENE As the elections approached, during the last two weeks of July and the first two weeks of August 2015, Tanzanians witnessed some very dra- matic changes on the political scene. Some sections of the media were even calling the events “Tanzania’s Tsunami!” President Kikwete addessing the CCM congress in Dodoma What happened? A summary 1. In July as all the political parties were having difficulty in choosing their candidates for the presidency, the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) party decided to steal a march on the others by bringing forward their own selection process and forcing the other parties to do the same. 2. It seemed as though almost everyone who is anyone wanted to become president. A total of no less than 42 CCM leaders, an unprec- edented number, registered their desire to be the party’s presidential candidate. They included former prime ministers and ministers and many other prominent CCM officials. 3. Meanwhile, members of the CCM hierarchy were gathering in cover photos: CCM presidential candidate, John Magufuli (left), and CHADEMA / UKAWA candidate, Edward Lowassa (right). ta112 - final.indd 2 8/25/2015 12:04:37 PM Surprising Changes on the Political Scene 3 Dodoma to begin the lengthy and highly competitive selection process. 4. The person who appeared to have the best chance of winning for the CCM was former Prime Minister Edward Lowassa MP, who was popular in the party and had been campaigning hard.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA NANE Kikao Cha Kumi Na Tano
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 3 Julai, 2007 (Kikao Kilianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI:- Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mkiangalia Order Paper yetu ya leo, hati za kuwasilisha Mezani iko, Ofisi ya Makamu wa Rais, yuko Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Mazingira, tumemruka Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria na Utawala, halafu atakuja Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA): Hotuba ya Bajeti ya Wizari wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha wa 2007/2008. MWENYEKITI WA KAMATI YA MALIASILI NA MAZINGIRA: Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA (MHE. RAMADHAN A. MANENO): Tarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano kwa mwaka wa Fedha 2006/2007 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2007/2008. MHE. RIZIKI OMARI JUMA (k.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): 1 Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja Maoni ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 22 Juni, 2021 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Hamsini na Sita na kabla hatujaendelea nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wasaidizi wangu wote wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa David Kihenzile, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Najma kwa kazi nzuri ambayo wameifanya wiki nzima kutuendeshea mjadala wetu wa bajeti. (Makofi) Sasa leo hapa ndio siku ya maamuzi ambayo kila Mbunge anapaswa kuwa humu ndani, kwa Mbunge ambaye Spika hana taarifa yake na hatapiga kura hapa leo hilo la kwake yeye. (Makofi) Katibu. NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali na tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 465 Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri Katika Mji wa Laela MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Sumbawanga katika Mji wa Laela baada ya agizo la Serikali la kuhamisha Makao Makuu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu la watu wa Kwela, Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 30 zilizohamia kwenye maeneo mapya ya utawala mwaka 2019.
    [Show full text]
  • Tanzania Human Rights Report 2008
    Legal and Human Rights Centre Tanzania Human Rights Report 2008: Progress through Human Rights Funded By; Embassy of Finland Embassy of Norway Embassy of Sweden Ford Foundation Oxfam-Novib Trocaire Foundation for Civil Society i Tanzania Human Rights Report 2008 Editorial Board Francis Kiwanga (Adv.) Helen Kijo-Bisimba Prof. Chris Maina Peter Richard Shilamba Harold Sungusia Rodrick Maro Felista Mauya Researchers Godfrey Mpandikizi Stephen Axwesso Laetitia Petro Writers Clarence Kipobota Sarah Louw Publisher Legal and Human Rights Centre LHRC, April 2009 ISBN: 978-9987-432-74-5 ii Acknowledgements We would like to recognize the immense contribution of several individuals, institutions, governmental departments, and non-governmental organisations. The information they provided to us was invaluable to the preparation of this report. We are also grateful for the great work done by LHRC employees Laetitia Petro, Richard Shilamba, Godfrey Mpandikizi, Stephen Axwesso, Mashauri Jeremiah, Ally Mwashongo, Abuu Adballah and Charles Luther who facilitated the distribution, collection and analysis of information gathered from different areas of Tanzania. Our 131 field human rights monitors and paralegals also played an important role in preparing this report by providing us with current information about the human rights’ situation at the grass roots’ level. We greatly appreciate the assistance we received from the members of the editorial board, who are: Helen Kijo-Bisimba, Francis Kiwanga, Rodrick Maro, Felista Mauya, Professor Chris Maina Peter, and Harold Sungusia for their invaluable input on the content and form of this report. Their contributions helped us to create a better report. We would like to recognize the financial support we received from various partners to prepare and publish this report.
    [Show full text]
  • Strategic Maneuvering in the 2015 Tanzanian Presidential Election Campaign Speeches: a Pragma-Dialectical Perspective
    STRATEGIC MANEUVERING IN THE 2015 TANZANIAN PRESIDENTIAL ELECTION CAMPAIGN SPEECHES: A PRAGMA-DIALECTICAL PERSPECTIVE BY GASPARDUS MWOMBEKI Dissertation presented for the degree of Doctor of Philosophy in the Faculty of Arts and Social Sciences at Stellenbosch University Supervisor: Professor Marianna W. Visser April 2019 Stellenbosch University https://scholar.sun.ac.za DECLARATION By submitting this dissertation electronically, I declare that the entirety of the work contained therein is my own, original work, that I am the sole author thereof (save to the extent explicitly otherwise stated), that reproduction and publication thereof by Stellenbosch University will not infringe any third party rights and that I have not previously in its entirety or in part submitted it for obtaining any qualification. April 2019 Copyright © 2019 Stellenbosch University All rights reserved i Stellenbosch University https://scholar.sun.ac.za ABSTRACT The study investigates strategic maneuvering in the 2015 Tanzanian presidential campaign speeches of Chama Cha Mapinduzi (CCM) and Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)/Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) in the Extended pragma-dialectical theory of argumentation. The study employs the Extended pragma-dialectical theory of argumentation to analyse two inaugural speeches conducted in Kiswahili language. It also analyses a part of the CCM closing campaign, that is, a response to some argumentations of the CHADEMA/UKAWA. The study evaluates argumentation structures, argument schemes, presentational devices, successful observation of rules, identification of derailments of rules, and effectiveness and reasonableness in argumentative discourse as objectives of the study. The data were collected from the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) and from other online sources.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 4 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Leo ni kikao cha tatu cha Mkutano wetu wa Kumi na Tano. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, AJIRA, KAZI VIJANA NA WAZEE NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. HASNA S.K. MWILIMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tume ya Uratibu na Udhibiti wa UKIMWI) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 24 Juni, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 111 Malipo ya Likizo za Watumishi MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Ni haki ya Mtumishi kulipwa likizo yake ya mwaka hata kama muda wa likizo hiyo unaangukia muda wake wa kustaafu:- Je, Serikali inatoa kauli gani kwa Watumishi ambao wamenyimwa likizo zao kwa kisingizio kuwa muda wao wa kustaafu umefika na kunyimwa kulipwa likizo zao. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pauline Gekul, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni H. I ya Kanuni za Kudumu ( Standing Orders) likizo ni haki ya mtumishi. Endapo mwajiri ataona kuwa hawezi kumruhusu mtumishi kuchukua likizo yake, analazimika kumlipa mshahara wa mwezi mmoja mtumishi huyo. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni H.5 (a) ya Kanuni hizi, mtumishi hulipiwa nauli ya likizo kila baada ya miaka miwili. 1 Mheshimiwa Spika, kutokana na miongozo niliyoitaja, ni makosa kutomlipa mtumishi stahili yake ya likizo kabla ya kustaafu. MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi hii ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya msingi ya Waziri amesema kwamba ni haki ya watumishi wa Umma kulipwa likizo zao pale wanapostaafu.
    [Show full text]
  • Tarehe 3 Februari, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Pili – Tarehe 3 Februari, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Tukae. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na maswali Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, sasa aulize swali lake. Na. 16 Ujenzi wa Barabara za Lami - Mji wa Mafinga MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza Ujenzi wa Barabara za lami na kufunga taa za barabarani katika Mji wa Mafinga chini ya Mpango wa Uendelezaji Miji nchini? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu, kwanza naomba nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenijalia mimi na Waheshimiwa Wabunge wote afya njema na kutuwezesha kuwa wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge lako Tukufu. Mheshimiwa Naibu Spika, pili, naomba nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani kubwa aliyonipa kwa kuniteua kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, nawashukuru sana wananchi wa Jimbo la Wanging’ombe kwa kunichagua na kuchagua mafiga
    [Show full text]