Tarehe 4 Aprili, 2019
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 4 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Leo ni kikao cha tatu cha Mkutano wetu wa Kumi na Tano. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, AJIRA, KAZI VIJANA NA WAZEE NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. HASNA S.K. MWILIMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tume ya Uratibu na Udhibiti wa UKIMWI) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. RAPHAEL J. MICHAEL – MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YA WAZIRI MKUU: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE: Taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu shauri la Mheshimiwa Godbless Jonathan Lema la kudharau na kulidhalilisha Bunge. SPIKA: Katibu! 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. STEPHEN KIGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali, swali la kwanza linakwenda ofisi ya Rais, TAMISEMI, tunaanza na Mheshimiwa Alfredina Apolinary Kahigi, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 19 Posho za Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa MHE. ALFREDINA A. KAHIGI aliuliza:- Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa hupata posho shilingi elfu ishirini kwa mwezi kiasi ambacho ni kidogo ikilinganishwa na kazi kubwa wanayoifanya:- Je, ni lini Serikali itaongeza posho kwa Wenyeviti hao? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Mwita Mwikabe Waitara, tafadhali. MHE. MWITA M. WAITARA-NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS- TAMISEMI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alfredina Apolinary Kahigi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji katika shughuli za maendeleo. Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji, Mitaa, vitongoji na Wajumbe wa Serikali za Vijiji pamoja na Wajumbe wa Mitaa za mwaka 2014 zilizotolewa kupitia Tangazo la Serikali Na. 322 na Na. 323, sifa zinazomwezesha mkazi wa 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mtaa, Kijiji na Kitongoji kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti au mjumbe wa Serikali za Mitaa ni pamoja na kuwa na shughuli halali inayomwingizia kipato. Mheshimiwa Spika, Serikali inalipa posho ya Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa kwa kutumia asilimia 20 ya mapato ya ndani inayorejeshwa na Halmashauri kwenye ngazi za Serikali za Mitaa. Hata hivyo, kiasi hicho kinategemea hali ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri yanayokusanywa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290. Mkakati uliopo ni kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha makusanyo katika vyanzo vya mapato vilivyopo kwa kutumia mifumo ya kielektroniki ili kujenga uwezo wa kulipa posho kwa viongozi hao. Aidha, viwango vya posho inayolipwa vinatofautiana kati ya Halmashauri moja na nyingine kulingana na uwezo wa kifedha uliopo. SPIKA: Mheshimiwa Apolinary, swali la nyongeza. MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi mara ya pili kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji hawana ofisi za kufanyia kazi. Je, ni lini Serikali itawajengea ofisi za kufanyia kazi? Mheshimiwa Spika, Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa wana wajumbe wanaosaidiana nao katika kazi za utendaji wa kazi za kila siku. Je, ni lini Serikali itawapa posho wale wajumbe? SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba ku-declare kwamba mimi pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa mstaafu. Naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, swali la kwanza anaulizia kuhusu Ofisi za Serikali za Mitaa. Sasa hivi tunaenda kwenye Bunge la Bajeti na mpango wa kujenga ofisi za mitaa, vijiji na vitongoji ni mpango wa halmashauri husika. Kwa hiyo kama kuna upungufu mkubwa, tunatarajia kwamba halmashauri hizo na vijiji watakuwa wameweka kwenye bajeti yao ili waweze kuleta kwenye Bunge lako Tukufu iweze kupitishwa na waweze kujenga ofisi hizo. Mheshimiwa Spika, swali la pili anaulizia juu ya posho, kama nilivyojibu kwenye swali langu la msingi ni kwamba posho za wenyeviti na wajumbe wao zinapatikana kwenye halmashauri husika kulingana na vipato vyao. Kwa hiyo kama kuna sababu ya kulipa posho tofauti na ilivyo kwa Wenyeviti wa Mitaa hili nalo pia lilifanyiwa kazi kwenye ngazi ya chini ya halmashauri husika kulingana na mapato yao, kama wana uwezo wataendelea kuwalipa. Hata hivyo, sifa ya msingi ya kugombea kama ilivyo kwenye uchaguzi mwezi wa Kumi wajumbe hawa na Wenyeviti wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji wanajua wanapaswa kufanya kazi ya kujitolea. Kwa hiyo tunatarajia kwamba watafanya kazi kama ambavyo waliamua kugombea na kupata nafasi hizo kama kuna uwezo wa posho watalipana, kama haupo wafanye kazi kama ambavyo waliamua kugombea nafasi hizo. SPIKA: Wizara ya Maji, swali linaulizwa na Mheshimiwa Allan Joseph Kiula. Na. 20 Utafiti wa Vyanzo vya Maji Jimbo la Mkalama MHE. ALLAN J. KIULA aliuliza:- Pamoja na mambo mengine, Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano imelenga kuongeza asilimia za upatikanaji wa maji vijijini. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (a) Je, lini Serikali itafanya utafiti wa vyanzo vya maji katika Jimbo la Mkalama ili kuwa na uhakika wa rasilimali hiyo? (b) Je, lini Serikali itatoa fedha za kutosha kuwapatia maji safi wananchi wa Jimbo la Mkalama? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji, Mheshiimwa Jumaa Hamidu Aweso, tafadhali. NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Allan Joseph Kiula, Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, lenye kipengele (a) na (b), kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/ 2019, Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga kiasi cha shilingi milioni 450 kwa ajili ya kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi katika maeneo kame ya Mikoa ya Singida, Mwanza, Tabora na Shinyanga. Utafiti huo utahusisha pia Wilaya ya Mkalama ambapo shilingi milioni 50 zitatumia. Mheshimiwa Spika, pamoja na utafiti unaotarajiwa kufanyika, Serikali imekua ikitekeleza miradi mbalimbali yamaji katika Vijiji vya Ndunguti, Kinyangiri, Ipuli na pia inatekeleza miradi ya uchimbaji wa visima 24 katika maeneo mengine tofauti. Ili kuhakikisha miradi hii inakamilika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 1.36 kwa mwaka wa fedha 2018/2019. SPIKA: Mheshimiwa Kiula, tafadhali. MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa tena nafasi. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza ikiwemo kushukuru ziara ya Makamu wa Rais ambaye alibaini ubadhirifu wa mradi wa Nyahaa, natumaini Wizara inaendelea kulifanyia kazi suala hilo. Swali la kwanza, je, Serikali iko tayari kuongeza fedha za utafiti hususan katika 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) maeneo yasiyo na miradi mikubwa kama ile iliyopitiwa na maji ya Ziwa Victoria au mkopo wa India ikiwemo Mkalama ili kuweza kupata vyanzo vya uhakika vya maji? (Makofi) Mheshimiwa Spika, swali la pili je, ni kweli Serikali inatekeleza miradi hiyo na pesa hizo zilitengwa, je ni lini certificate za wakandarasi zitalipwa ili kazi iweze kuendelea kwa sababu kazi kule imesimama kutokana na wakandarasi kutokulipwa? SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Aweso, tafadhali. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza nimpongeze Mheshimiwa Allan Kiula Mbunge wa Jimbo la Mkalama kwa kazi nzuri sana anayoifanya katika jimbo lake. Kubwa ni kuhusu suala zima la utafiti, sisi kama Serikali tunautambua umuhimu wa suala zima la utafiti hasa katika sekta ya maji kwa sababu italeta mapinduzi makubwa. Nataka nimhakikishie sisi kama Serikali hatutokuwa kikwazo kuongeza fedha za utafiti kadiri bajeti itakavyokuwa imeruhusu katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na tafiti ambazo zitaruhusu kufanya mapinduzi katika sekta ya maji. Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu suala zima la madai ya wakandarasi hususan katika miradi ya jimbo lake. Utekelezaji wa miradi ya maji unategemeana na fedha, tukubali tulikuwa na madai zaidi ya bilioni 88 ya wakandarasi lakini tunashukuru Wizara ya Fedha ijumaa imetupa zaidi ya bilioni 44 kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi certificate zao na wametupa commitment ndani ya mwezi huu wa nne watatupa bilioni 44 zingine kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi fedha zao. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge apate nafasi ya kuwasiliana na sisi katika kuhakikisha tunamlipa mkandarasi wake ili aweze kuendeleza miradi ya maji katika Jimbo lake la Mkalama.