Mkutano Wa Tatu
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Saba – Tarehe 23 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya mwaka 2020. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2021 (The Finance Bill, 2021). MHE. MARIAMU M. NYOKA - K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Maoni ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2021 (The Finance Bill, 2021) 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Tunaanza na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Makete. Na. 475 Ujenzi wa Kituo cha Afya Ikuwo – Makete MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Ikuwo? MWENYEKITI: Hili ndiyo swali la Kibunge, swali short and clear. Mtu anauliza swali page nane? Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makete, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Makete, Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 400 katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ipelele.
[Show full text]