Mkutano Wa Tatu

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Mkutano Wa Tatu NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Saba – Tarehe 23 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya mwaka 2020. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2021 (The Finance Bill, 2021). MHE. MARIAMU M. NYOKA - K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Maoni ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2021 (The Finance Bill, 2021) 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Tunaanza na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Makete. Na. 475 Ujenzi wa Kituo cha Afya Ikuwo – Makete MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Ikuwo? MWENYEKITI: Hili ndiyo swali la Kibunge, swali short and clear. Mtu anauliza swali page nane? Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makete, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Makete, Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 400 katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ipelele. Ujenzi wa Kituo hicho umekamilika na kinatoa huduma zikiwemo huduma za dharura za upasuaji. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 150 kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati za Usungilo, Nungu na Matenga. Vilevile, Mei 2021, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kitulo. Aidha, ombi la Kituo cha Afya Ikuwo limepokelewa na linafanyiwa tathimini. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaipitia na kuiboresha Sera ya Ujenzi wa Zahanati kila Kijiji na Kituo cha Afya kila Kata ili ujenzi ufanyike kimkakati na kwa tija zaidi badala ya kila Kijiji na kila Kata. Ahsante. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Sanga. MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri lakini pia niipongeze Serikali kwa fedha zote ambazo imetuletea kwa ajili ya maendeleo ya Makete. Niseme wazi kwamba sitakuwa na haja ya kuwa na maswali ya nyongeza ila niiombe tu Serikali inavyofanya tathmini kwa ajili ya kituo hiki ikumbuke pia usafiri wa ambulance kwa sababu ni kilometa 70 kutoka pale kwenda Makete Mjini kwa ajili ya wananchi wangu. Ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante na mabilioni ya hela jana Waziri wa Fedha ameyatoa. Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu. Na. 476 Kujenga Vituo vya Afya – Ikungi MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya Issuna, Ikungi, Makiungu, Ntuntu na Misughaa ili kurahisisha huduma za dharura Wilayani Ikungi kwa kuwa Wilaya hii inapitiwa na Barabara ya Dodoma – Mwanza ambayo imekuwa na ajali za mara kwa mara? 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (b) Je, ni lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa ili kuwahisha majeruhi na wagonjwa katika Hospitali za Rufaa? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshmiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi iliyoanza kujengwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo hadi mwezi Mei 2021 ilikuwa imepatiwa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga shilingi milioni 800 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo. Hospitali hiyo itasaidia kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali zitakazotokea eneo la Ikungi katika barabara ya Dodoma hadi Mwanza. Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Mei 2021 Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya Ihanja na Sepuka. Ujenzi wa Vituo hivyo umekamilika na vinatoa huduma ikiwemo huduma za dharura za upasuaji. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inapitia Sera ya Zahanati katika kila Kijiji na Kituo cha Afya katika kila Kata na itafanyiwa maboresho yenye tija zaidi ili ili ujenzi uwe wa kimkakati badala ya kila Kijiji au kila Kata. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya Ikungi ina magari matatu ya kubebea wagonjwa ambayo yapo katika Vituo vya Afya Ikungi, Sepuka na Ihanja ambayo yote yanaendelea kutoa huduma za rufaa za dharura ndani na nje ya wilaya ya Ikungi. Ahsante. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mtaturu. MHE. MIRAJI J MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake lakini katika swali langu la msingi mpango wa Serikali ni kujenga Kituo cha Afya kila Kata na katika Jimbo la Singida Mashariki tuna Kata 13 na tunacho Kituo cha Afya kimoja tu ambacho pia hakina huduma nzuri. Kwa sababu Kata hizi hazina Kituo cha Afya, naomba kujua Serikali ina mpango gani wa kujenga Vituo vya Afya katika Kata zingine ikiwemo Kata za Makiungu na Ntuntu ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni? Swali la kwanza. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, namshukuru sana Mheshimiwa, ni kweli ametuletea fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya. Fedha hizo zilirudishwa kama ambavyo tulisema baada ya kuwa mwaka wa fedha umepita. Hivi tunavyoongea zaidi ya miezi sita, fedha hizo hazipo na ujenzi umesimama. Je, ni lini sasa Serikali italeta fedha hizo ikiwemo kuleta vifaa tiba katika hospitali hiyo ili iweze kuanza kutoa huduma? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimetangulia kutoa ufafanuzi katika majibu yangu ya msingi kwamba Sera ya Maendeleo ya Afya ya Msingi inakwenda kuboreshwa ili iwe na tija na uhalisia na ufanisi mkubwa zaidi kwa sababu tuna vijiji karibu 12,000 na mitaa karibu 16,000 na tuna kata 3,956. Kwa hivyo, tunataka kwenda kimkakati zaidi kujenga vituo vya afya katika maeneo ya kimkakati ambavyo vitakuwa fully equipped na vitatoa tija zaidi badala ya kujenga kila kata na kila Kijiji. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika jimbo lake, vituo hivi vya afya ikiwemo kituo hiki ambacho ni ahadi ya Mheshimiwa Rais lakini na vituo vile vingine vyote tutafanya tathmini na kama tutaona tija ya kuvijenga vitakwenda kujengwa. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie kwamba mpango huo utaendelea kutekelezwa kwa utaratibu huo. Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, fedha za hospitali ya halmashauri zilizorejeshwa, kwa kipindi hicho zilirejeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 lakini Serikali imeshafanya maboresho. Waheshimiwa Wabunge wote tumesikia hapa wakati wa bajeti ya Wizara ya Fedha kwamba kuanzia Mwaka ujao wa Fedha, fedha zinazopelekwa kwenye miradi ya maendeleo hazitarejeshwa baada ya tarehe 30 Juni. Kufuatia hilo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba fedha hizo tutafanya utaratibu kuzipeleka ili kuendelea na ujenzi wa hospitali kama ulivyopangwa. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Gwajima. MHE. ASK. JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tatizo la Singida Mashariki linafanana kabisa na tatizo la Kata ya Mabwepande katika Jimbo la Kawe, ni lini sasa Serikali itamalizia ile Hospitali ya Jimbo la Kawe katika Kata ya Mabwepande? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi. Jiandae Mheshimiwa Bulaya. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inajenga Hospitali ya Manispaa katika eneo la Mabwepande na mwezi wa tatu 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tulifanya ziara pale, tulishirikiana na Mheshimiwa Mbunge, iko hatua za mwisho za ukamilishaji na tulishatoa maelekezo kupitia mapato ya ndani wahakikishe hospitali ile inaanza kufanya kazi ndani ya mwaka huu wa fedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia katika mwaka ujao wa fedha tumetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya vifaatiba lakini pia kwa ajili ya kumalizia baadhi ya shughuli za ujenzi. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Manispaa ya Kinondoni. Ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Bulaya. MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.
Recommended publications
  • Hotuba Ya Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Katika Ufunguzi Wa Mkuta
    HOTUBA YA MGENI RASMI MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB) WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MWAKA WA WADAU WA LISHE, SEPTEMBA 10, 2019 Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Suleiman Jafo (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Mheshimiwa Prof. Joyce Ndalichako (Mb), Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango. Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (Mb), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Mheshimiwa Doto Biteko (Mb), Waziri wa Madini, Waheshimiwa Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge; pamoja na viongozi wengine wa ngazi za Mkoa na Halmashauri mliopo, Waheshimiwa Wabunge na viongozi wa Vyama vya Siasa, Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali, Ndugu Viongozi waandamizi wa Idara, Taasisi, Wakala za Serikali, Wakuu wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Wadau wa Maendeleo na Asasi za Kiraia, 1 Ndugu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Ndugu Wageni Waalikwa, Waandishi wa habari na wadau wote wa Lishe, Mabibi na Mabwana. Habari za asubuhi Kwa mara nyingine tena nina furaha kubwa sana kujumuika na wadau wa lishe siku hii ya leo. Hii ni mara yangu ya tatu kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wadau wa lishe nchini na hivyo nahisi kuwa mwanafamilia wa wadau waliohamasika katika masuala ya lishe.
    [Show full text]
  • Tarehe 30 Juni, 2017
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Saba – Tarehe 30 Juni, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Saba, leo ni Kikao cha Hamsini na Saba. Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Mheshimiwa Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Swali la kwanza linaulizwa na Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki. Mheshimiwa Nyongo. Na. 468 Mikopo kwa Walimu Kwa Ajili ya Ujenzi wa Nyumba MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza:- Walimu Wilayani Maswa wana uhaba wa nyumba za kuishi; pamoja na juhudi za wananchi kujenga nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari lakini walimu hao bado wanahitaji kujenga nyumba zao wenyewe za kudumu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni lini Serikali itaweka utaratibu maalum wa kutoa mikopo kwa walimu hao ili wajenge nyumba zao binafsi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina uhitaji wa nyumba za walimu 1,358. Nyumba zilizopo ni 479 na hivyo upungufu ni nyumba 879. Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu huu Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina mpango wa kujenga nyumba 16 katika mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, kati ya nyumba hizo, nyumba nane zitajengwa kwa bajeti ya 2017/2018 (CDG) na nyumba nyingine nane zitajengwa kwa kutumia mapato ya ndani y (own source) ya Halmashauri.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 22 Juni, 2021 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Hamsini na Sita na kabla hatujaendelea nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wasaidizi wangu wote wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa David Kihenzile, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Najma kwa kazi nzuri ambayo wameifanya wiki nzima kutuendeshea mjadala wetu wa bajeti. (Makofi) Sasa leo hapa ndio siku ya maamuzi ambayo kila Mbunge anapaswa kuwa humu ndani, kwa Mbunge ambaye Spika hana taarifa yake na hatapiga kura hapa leo hilo la kwake yeye. (Makofi) Katibu. NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali na tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 465 Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri Katika Mji wa Laela MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Sumbawanga katika Mji wa Laela baada ya agizo la Serikali la kuhamisha Makao Makuu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu la watu wa Kwela, Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 30 zilizohamia kwenye maeneo mapya ya utawala mwaka 2019.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Kumi Na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, sasa aulize swali lake. Na. 158 Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Zahanati – Busega MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Imalamate Wilayani Busega wamejenga zahanati na kumaliza maboma manne kwa maana ya zahanati moja kila kijiji:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi hao kuezeka maboma hayo ili waweze kupata huduma za afya kwenye zahanati hizo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 4 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Leo ni kikao cha tatu cha Mkutano wetu wa Kumi na Tano. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, AJIRA, KAZI VIJANA NA WAZEE NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. HASNA S.K. MWILIMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tume ya Uratibu na Udhibiti wa UKIMWI) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
    [Show full text]
  • Tarehe 3 Februari, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Pili – Tarehe 3 Februari, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Tukae. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na maswali Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, sasa aulize swali lake. Na. 16 Ujenzi wa Barabara za Lami - Mji wa Mafinga MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza Ujenzi wa Barabara za lami na kufunga taa za barabarani katika Mji wa Mafinga chini ya Mpango wa Uendelezaji Miji nchini? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu, kwanza naomba nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenijalia mimi na Waheshimiwa Wabunge wote afya njema na kutuwezesha kuwa wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge lako Tukufu. Mheshimiwa Naibu Spika, pili, naomba nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani kubwa aliyonipa kwa kuniteua kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, nawashukuru sana wananchi wa Jimbo la Wanging’ombe kwa kunichagua na kuchagua mafiga
    [Show full text]
  • Online Document)
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini – Tarehe 10 Juni, 2014 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge Maswali tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Josephat Kandege. Na. 216 Kugawa Jimbo la Kalambo MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Wilaya ya Kalambo ni Jimbo moja lenye eneo kubwa sana la Kiutawala ikipakana na nchi za Zambia na Congo DRC:- Je, Serikali haioni kuwa ipo haja ya kuligawa Jimbo hilo ili kupunguza eneo la uwakilishi wa wananchi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Ibara ya 75(1) – (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano a Tanzania ya Mwaka 1977 imeainisha utaratibu na vigezo vinavyotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kufikia uamuzi wa kugawa mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi angalau kila baada ya kipindi cha miaka kumi (10). Vigezo vinavyozingatiwa na Tume ni pamoja na ukubwa wa eneo la utawala; upatikanaji wa njia ya mawasiliano; Idadi ya Watu na hali ya kijiografia katika jimbo linalokusudiwa kugawanywa. Vigezo vingine vinavyotumika ni hali ya uchumi; mipaka ya kiutawala; jimbo moja lisiwe ndani ya Wilaya/Halmashauri mbili, Kata moja isiwe ndani ya Majimbo mawili; Mazingira ya Muungano, Mgawanyo wa Wastani wa Idadi ya Watu; uwezo wa Ukumbi wa Bunge; Idadi ya Viti Maalum vya Wanawake na mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yaliyopo.
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI YATOKANAYO NA KIKAO CHA NANE 08 FEBRUARI, 2018 MKUTANO WA KUMI KIKAO CHA NANE TAREHE 08 FEBRUARI, 2018 I. DUA Saa 3:00 Asubuhi Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), Naibu Spika alisoma Dua na kuongoza Bunge. MAKATIBU MEZANI: 1. Ndg. Stephen Kagaigai 2. Ndg. Nenelwa Wankanga 3. Ndg. Lawrence Makigi II. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI: (a) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) - Mhe. Jenista J. Mhagama aliwasilisha Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2016; (b) Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria - Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa aliwasilisha Mezani Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017; (c) Mhe. Esther Mmasi K.n.y Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo aliwasilisha Mezani Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017; (d) Mhe. Maidah Abdallah K.ny Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa aliwasilisha Mezani Taarifa ya Kamati hiyo kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. 1 III. MASWALI KWA WAZIRI MKUU: Waheshimiwa Wabunge wafuatao waliuliza maswali:- (a) Mhe. Richard Mganga Ndassa - CCM (b) Mhe. Margareth Simwanza Sitta - CCM (c) Mhe. Devota Methew Minja - CHADEMA (d) Mhe. Zubeir Mohamed Kuchauka - CUF (e) Mhe. Balozi Diodorus Kamala - CCM IV. MASWALI YA KAWAIDA: Maswali yafuatayo yaliulizwa na kujibiwa kama ifuatavyo:- OFISI YA RAIS (TAMISEMI): Swali Na. 99 Mhe. Flatei Gregory Massay Nyongeza (i) Mhe. Flatei Gregory Massay (ii) Mhe.
    [Show full text]
  • (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Sita – Tarehe 18 Mei, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kutokana na maagizo yaliyotolewa humu wiki iliyopita kuhusu Hati za kuwasilisha Mezani. Kama kuna kundi lolote, Kamati, Serikali au Upinzani hawajaleta Hati hazisomwi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais! Mheshimiwa Naibu Waziri! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO): Randama za Makadirio ya Matumizi kwa Ofisi ya Makamu wa Rais na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) pamoja na (Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU): Hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. JASSON S. RWEIKIZA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA: 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu) kwa mwaka wa fedha 2014/2015 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. ESTHER N. MATIKO - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA MAHUSIANO NA URATIBU: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza maswali Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Engineer Athumani Mfutakamba.
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Tatu - Tarehe 16 Juni, 2014 (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na :- MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI: Taarifa ya Kamati ya Bajeti Juu ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2014/2015 Pamoja na Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2013/2014 na Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Juu ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. CHRISTINA LISSU MUGHWAI (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA FEDHA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. Na. 240 Ukosefu wa Hati Miliki MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE aliuliza:- Ukosefu wa Hatimiliki za Kimila Vijijini unasababisha migogoro mingi ya ardhi baina ya Kaya, Kijiji na Koo na kupelekea kutoweka kwa amani kwa wananchi kama inavyotokea huko Tarime. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) (a) Je, ni kwa nini Serikali haitoi
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kwanza – Tarehe 6 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua KIAPO CHA UTII Wajumbe wafuatao waliapa Kiapo cha Utii na kukaa katika nafasi zao Bungeni:- Mhe. Godfrey William Mgimwa Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Ninapenda kuchukua nafasi hii, kuwapongeza Mheshimiwa Godfrey Mgimwa na Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, kwa kuchaguliwa na kujiunga na sisi katika Bunge hili. Tunaamini kwamba, tutapata ushirikiano unaostahili. (Makofi) Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa Kumi na Nne, Bunge lilipitisha Miswada ya Sheria minne iitwayo; Muswada wa Sheria wa GEPF ya Mfuko wa Mafao ya Wastaafu wa Mwaka 2013 (The GEPF Retirement Benefit Fund Bill, 2013); Muswada Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba Tatu wa Mwaka 2013 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Number Three Bill, 2013); Muswada Sheria ya Kura ya Maoni (The Referendum Bill, 2013); na Muswada wa Sheria ya Marekebisho Kodi ya Ushuru wa Mwaka 2013 (The Excise Management and Tariffs (Ammendment Bill), 2013). Kwa Taarifa hii, ninapenda kuliarifu Bunge hili Tukufu kwamba, Miswada hiyo imekwishapata kibali cha Mheshimiwa Rais na kuwa Sheria za nchi ziitwazo; Sheria ya Kwanza ni Sheria ya GEPF ya Mafao ya Mfuko wa Mafao ya Wastaafu Namba Saba ya Mwaka 2013 (The GEPF Retirement Benefit Fund Act Number Seven of 2013); Sheria ya pili ni Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba Nane ya Mwaka 2013 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Number Three Act Number 8 of 2013); Sheria ya Tatu ni Sheria ya Kura ya Maoni Namba Kumi ya Mwaka 2013 (The Referendum Act Number 10 of 2013); na Sheria ya nne ni 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Sheria ya Marekebisho ya Kodi ya Ushuru Namba Kumi na Moja ya Mwaka 2013 (The Excise Management and Tariff Amendment Act Number 11 of 2013).
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA ISHIRINI NA TISA 19 MEI, 2017 MKUTANO WA SABA KIKAO CHA ISHIRINI NA TISA TAREHE 19 MEI, 2017 I. DUA: Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson alisoma Dua na kuongoza Bunge Saa 3:00 asubuhi. Makatibu mezani: 1. Ndugu Theonest Ruhilabake 2. Ndugu Neema Msangi II. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani:- (1) Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliwasilisha:- Hotuba za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. (2) Mhe. Mattar Ali Salum – (Kny. Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji aliwasilisha Mezani: Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. (3) Mhe. Susan A. J. Lyimo – Msemaji Mkuu wa Upinzani kwa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliwasilisha Mezani:- 1 Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, juu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. III. MASWALI OFISI YA RAIS (TAMISEMI) Swali Na. 234: Mhe. Cosato D. Chumi Nyongeza: Mhe. Cosato D. Chumi Mhe. Kasuku S. Bilago Mhe. Daimu I. Mpakate WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO Swali Na. 235: Mhe. Dr. Mary M. Mwanjelwa Nyongeza: Mhe. Dr. Mary M. Mwanjelwa Mhe. Susan A. J. Lyimo Mhe.
    [Show full text]