NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Saba – Tarehe 23 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya mwaka 2020. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2021 (The Finance Bill, 2021). MHE. MARIAMU M. NYOKA - K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Maoni ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2021 (The Finance Bill, 2021) 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Tunaanza na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Makete. Na. 475 Ujenzi wa Kituo cha Afya Ikuwo – Makete MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Ikuwo? MWENYEKITI: Hili ndiyo swali la Kibunge, swali short and clear. Mtu anauliza swali page nane? Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makete, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Makete, Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 400 katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ipelele. Ujenzi wa Kituo hicho umekamilika na kinatoa huduma zikiwemo huduma za dharura za upasuaji. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 150 kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati za Usungilo, Nungu na Matenga. Vilevile, Mei 2021, Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kitulo. Aidha, ombi la Kituo cha Afya Ikuwo limepokelewa na linafanyiwa tathimini. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaipitia na kuiboresha Sera ya Ujenzi wa Zahanati kila Kijiji na Kituo cha Afya kila Kata ili ujenzi ufanyike kimkakati na kwa tija zaidi badala ya kila Kijiji na kila Kata. Ahsante. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Sanga. MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri lakini pia niipongeze Serikali kwa fedha zote ambazo imetuletea kwa ajili ya maendeleo ya Makete. Niseme wazi kwamba sitakuwa na haja ya kuwa na maswali ya nyongeza ila niiombe tu Serikali inavyofanya tathmini kwa ajili ya kituo hiki ikumbuke pia usafiri wa ambulance kwa sababu ni kilometa 70 kutoka pale kwenda Makete Mjini kwa ajili ya wananchi wangu. Ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante na mabilioni ya hela jana Waziri wa Fedha ameyatoa. Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu. Na. 476 Kujenga Vituo vya Afya – Ikungi MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:- (a) Je, ni lini Serikali itajenga Vituo vya Afya vya Issuna, Ikungi, Makiungu, Ntuntu na Misughaa ili kurahisisha huduma za dharura Wilayani Ikungi kwa kuwa Wilaya hii inapitiwa na Barabara ya Dodoma – Mwanza ambayo imekuwa na ajali za mara kwa mara? 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (b) Je, ni lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa ili kuwahisha majeruhi na wagonjwa katika Hospitali za Rufaa? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshmiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi iliyoanza kujengwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo hadi mwezi Mei 2021 ilikuwa imepatiwa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga shilingi milioni 800 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali hiyo. Hospitali hiyo itasaidia kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali zitakazotokea eneo la Ikungi katika barabara ya Dodoma hadi Mwanza. Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018 hadi Mei 2021 Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya Ihanja na Sepuka. Ujenzi wa Vituo hivyo umekamilika na vinatoa huduma ikiwemo huduma za dharura za upasuaji. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inapitia Sera ya Zahanati katika kila Kijiji na Kituo cha Afya katika kila Kata na itafanyiwa maboresho yenye tija zaidi ili ili ujenzi uwe wa kimkakati badala ya kila Kijiji au kila Kata. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya Ikungi ina magari matatu ya kubebea wagonjwa ambayo yapo katika Vituo vya Afya Ikungi, Sepuka na Ihanja ambayo yote yanaendelea kutoa huduma za rufaa za dharura ndani na nje ya wilaya ya Ikungi. Ahsante. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mtaturu. MHE. MIRAJI J MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake lakini katika swali langu la msingi mpango wa Serikali ni kujenga Kituo cha Afya kila Kata na katika Jimbo la Singida Mashariki tuna Kata 13 na tunacho Kituo cha Afya kimoja tu ambacho pia hakina huduma nzuri. Kwa sababu Kata hizi hazina Kituo cha Afya, naomba kujua Serikali ina mpango gani wa kujenga Vituo vya Afya katika Kata zingine ikiwemo Kata za Makiungu na Ntuntu ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni? Swali la kwanza. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, namshukuru sana Mheshimiwa, ni kweli ametuletea fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya. Fedha hizo zilirudishwa kama ambavyo tulisema baada ya kuwa mwaka wa fedha umepita. Hivi tunavyoongea zaidi ya miezi sita, fedha hizo hazipo na ujenzi umesimama. Je, ni lini sasa Serikali italeta fedha hizo ikiwemo kuleta vifaa tiba katika hospitali hiyo ili iweze kuanza kutoa huduma? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimetangulia kutoa ufafanuzi katika majibu yangu ya msingi kwamba Sera ya Maendeleo ya Afya ya Msingi inakwenda kuboreshwa ili iwe na tija na uhalisia na ufanisi mkubwa zaidi kwa sababu tuna vijiji karibu 12,000 na mitaa karibu 16,000 na tuna kata 3,956. Kwa hivyo, tunataka kwenda kimkakati zaidi kujenga vituo vya afya katika maeneo ya kimkakati ambavyo vitakuwa fully equipped na vitatoa tija zaidi badala ya kujenga kila kata na kila Kijiji. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika jimbo lake, vituo hivi vya afya ikiwemo kituo hiki ambacho ni ahadi ya Mheshimiwa Rais lakini na vituo vile vingine vyote tutafanya tathmini na kama tutaona tija ya kuvijenga vitakwenda kujengwa. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie kwamba mpango huo utaendelea kutekelezwa kwa utaratibu huo. Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, fedha za hospitali ya halmashauri zilizorejeshwa, kwa kipindi hicho zilirejeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 lakini Serikali imeshafanya maboresho. Waheshimiwa Wabunge wote tumesikia hapa wakati wa bajeti ya Wizara ya Fedha kwamba kuanzia Mwaka ujao wa Fedha, fedha zinazopelekwa kwenye miradi ya maendeleo hazitarejeshwa baada ya tarehe 30 Juni. Kufuatia hilo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba fedha hizo tutafanya utaratibu kuzipeleka ili kuendelea na ujenzi wa hospitali kama ulivyopangwa. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Gwajima. MHE. ASK. JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tatizo la Singida Mashariki linafanana kabisa na tatizo la Kata ya Mabwepande katika Jimbo la Kawe, ni lini sasa Serikali itamalizia ile Hospitali ya Jimbo la Kawe katika Kata ya Mabwepande? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi. Jiandae Mheshimiwa Bulaya. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inajenga Hospitali ya Manispaa katika eneo la Mabwepande na mwezi wa tatu 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tulifanya ziara pale, tulishirikiana na Mheshimiwa Mbunge, iko hatua za mwisho za ukamilishaji na tulishatoa maelekezo kupitia mapato ya ndani wahakikishe hospitali ile inaanza kufanya kazi ndani ya mwaka huu wa fedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia katika mwaka ujao wa fedha tumetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya vifaatiba lakini pia kwa ajili ya kumalizia baadhi ya shughuli za ujenzi. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Manispaa ya Kinondoni. Ahsante. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Bulaya. MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages240 Page
-
File Size-