SUMAJKT Ili Kuwa Vya Kisasa Na Imara Katika Kutekeleza Majukumu Yake

SUMAJKT Ili Kuwa Vya Kisasa Na Imara Katika Kutekeleza Majukumu Yake

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MKUTANO WA NANE _______________ Kikao cha Ishirini na Nane – Tarehe 16 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:- Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:- Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. BETTY E. MACHANGU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA):- Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza maswali Ofisi ya Waziri na Mheshimiwa Ramadhani Haji Saleh ndio atakayeuliza swali la kwanza. Na. 196 Uwekezaji Katika Sekta ya Uvuvi MHE RAMADHAN HAJI SALEH aliuliza:- Sekta ya Bahari ni chanzo cha pili cha Mapato katika nchi ukiacha Madini kama itatumika vizuri lakini bado Serikali haijawekeza katika sekta hiyo:- Je, ni lini sasa Serikali itawekeza katika Sekta ya Bahari? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ramadhani Haji Saleh, Mbunge wa Bumbwini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inakubali kwa Sekta ya Bahari na hususan uvuvi ni muhimu kwa mapato ya nchi yetu. Hivyo, Serikali imeendelea kuboresha mazingira kwenye Sekta ya Bahari na hasa uvuvi ili kuwezesha wadau wa sekta hiyo, ikiwemo sekta binafsi kuwekeza ipasavyo. Baadhi ya mazingira hayo ni kuwepo kwa Sera ya Uwekezaji Nchini, Sera ya Taifa ya Uvuvi (1997), Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Sheria ya Kuanzisha Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi kwenye Bahari Kuu Na. 17 ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007. Aidha, Serikali imeandaa programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi ambayo tayari imeingizwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambayo itatekelezwa na Taifa, Halmashauri zote nchini zenye maji. Sekta ya Bahari, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge inapewa umuhimu mkubwa. Mheshimiwa Mbunge miundombinu mbalimbali imejengwa na kuboreshwa. Kwa mfano, Mialo 25 ya kupokelea samaki katika Ziwa Victoria imeboreshwa na Mialo mitatu (3) inajengwa katika ukanda wa Pwani. Aidha, kwa kushirikiana na Mradi wa Uwiano wa Bonde la Ziwa Tanganyika, Serikali itajenga Mialo minne (4) katika ukanda wa Ziwa Tanganyika. Serikali pia imekamilisha ujenzi wa masoko makubwa ya kupokelea samaki ya Ferry, Dar es Salaam na Kirumba, Mwanza, pamoja na soko la Kasanga, Rukwa. Vile vile, Serikali imehamasisha sekta binafsi kuongeza thamani ya mazao kwa kuanzisha viwanda vya kisasa 17 vya kuchakata samaki na mazao ya uvuvi, viwanda vidogo 17 na maghala 84. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika maeneo mbalimbali katika Sekta ya uvuvi. Aidha, Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye zana za uvuvi ikiwa ni pamoja na injini za kupachika, vifungashio, nyuzi za kutengeneza nyavu na kufuta kodi ya zuio kwa usafirishaji wa samaki nje ya nchi. MHE. RAMADHANI HAJI SALEH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri, lakini naomba nimwulize swali moja la nyongeza. Kutokana na utafiti uliofanywa katika Bahari yetu ya Hindi kumegunduliwa samaki wengi sana na kutokana na meli nyingi kutoka nje kuja kuvua katika bahari yetu. Je, Serikali hili imeliona vipi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa na ni jambo la kufurahisha kwamba utafiti umeonyesha kwamba bahari yetu ina samaki wengi na wa kuvutia meli kufika kwenye eneo la bahari yetu kutaka kuvua ili na wao wanufaike. Serikali imeliona hilo itaongeza kwanza uwekezaji ili sisi wenyewe tunufaike na rasilimali samaki kwenye eneo letu la bahari. Lakini vilevile kuongeza ulinzi ili meli kutoka nje zisiweze kuvua samaki wetu bali sisi wenyewe tunufaike nao. Pamoja na hivyo kama nilivyosema sera inaeleza kwamba lazima tushirikiane na sekta binafsi kuona kwamba uvuvi na teknolojia bora zaidi inatumika katika kuvua rasilimali kutoka bahari yetu. MHE. ALPHAXARD K. N. LUGOLA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika jibu la msingi Mheshimiwa Waziri amejaribu kuonyesha kwamba uwekezaji katika sekta ya Bahari ni suala la uvuvi tu. Lakini kuna suala hili la uzalishaji wa mabaharia hasa katika ngazi ya digrii na elimu zaidi ya hiyo. Sasa Chuo chetu cha DMI ilikuwa kiingie ubia na Wachina na kujaribu kujenga chuo ambacho kitazalisha Mabaharia. Waziri anasema nini katika sekta hii ya Bahari katika uzalishaji wa mabaharia kuliko tu alichozungumzia uvuvi wakati swali zima linazungumzia sekta ya Bahari? SPIKA: Sina uhakika kama ni uzalishaji wa mabaharia au ufundishaji wa mabaharia waliohusika. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Lugola kama alirejea majibu yangu ya msingi, nilisema sekta ya Bahari nikasema hususan uvuvi. Kwa hivyo sekta ya Bahari inahusisha na kuwafunza mabaharia au kuwanoa mabaharia kusudi basi tuwe na watu ambao wataendesha meli kwenda kuvua kwenye bahari yetu. Kwa hivyo na uvuvi nao unahitaji mabaharia hao wawe na uwezo, wawe na ujuzi na wawe ni majasiri kwenda kuvua hasa kwenye deep sea au bahari ya mbali. MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi ili niweze kumwuliza Waziri swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amekubali kabisa kwamba bahari yetu ina samaki wengi sana. Je, ni jambo gani au ni sababu gani inayopelekea nchi yetu kuruhusu samaki kuingia nchini kutoka nje ya nchi ikiwepo nchi ya Japan wakati ambapo tuna samaki wengi sana? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa mujibu wa utafiti kwamba tuna samaki wengi. Lakini ni kweli vilevile kwamba katika enzi hizi za utandawazi huwezi ukazuia soko lako jambo lililo muhimu ni kwamba sisi Watanzania tupende vya kwetu zaidi hata pale ambapo watu wanakuwa na choice au wanaweza kuchagua kitu kutoka nje. Lakini pam oja na uzalendo vilevile tuongeze uwezo wetu wa kuvua ili tuwe na samaki wa kutosha ili Watanzania waweze kuchagua samaki wa kwao badala ya wale wanaotoka nje wanaokaa kwenye barafu muda mrefu kwanza na usalama wake ukilinganisha na samaki wa kwetu watakuwa salama zaidi kwa sababu ni karibu na sisi. Na. 197 Gharama Kubwa za Kuendesha Chaguzi Ndogo MHE. PINDI H. CHANA aliuliza:- Zoezi la kuendesha Chaguzi Ndogo nchini limekuwa ni gharama kubwa sana kwa vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla:- Je, Serikali haioni kuna haja ya kulitafakari upya jambo hili na kuja na mpango wa gharama ndogo ya kuendesha Chaguzi Ndogo ama kwa kutumia “Proportional Representation” au Uchaguzi kufanyika baada ya miaka miwili na nusu (2 ½ )? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Pindi Hazara Chana, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba zoezi la kuendesha Chaguzi Ndogo limekuwa la gharama kubwa kwa Serikali, Vyama vya Siasa na Wananchi kwa ujumla. Katika hilo naomba nimpe mifano miwili inayothibitisha ukweli wa kauli hiyo Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 - 2010 zilifanyika Chaguzi Ndogo za Wabunge sita (6) katika Majimbo ya Wilaya ya Tunduru, Kiteto, Tarime, Mbeya Vijijini na Busanda. Wastani wa gharama zilizotumika katika Chaguzi Ndogo 2005-2010 kwa Ubunge peke yake ilikuwa ni shilingi 9,261,810,000/=. Lakini kwa Madiwani katika kipindi hicho zilifanyika Chaguzi Ndogo 75 nazo ziligharimu shilingi bilioni 9,555,000,000/=. Lakini kipindi hiki baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 zimefanyika Chaguzi Ndogo mbili katika Majimbo ya Igunga na Arumeru Mashariki, fedha zilizotumika kuendeshea uchaguzi huu ni shs. 3,087,270,000/=. Lakini pia zimefanyika Chaguzi Ndogo 30 za Madiwani ambazo Serikali imetumia shs. 3,822,000,000/= na hizi fedha zote huwa kwa kweli ni za dharura. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba umeshaanza, suala hili linaweza kujadiliwa kwa kina katika mchakato huo ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya Mheshimiwa Mbunge. Napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa wananchi wote, kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali, likiwemo hili la namna bora ya kujaza nafasi wazi za Ubunge na Udiwani wakati Tume ya Mabadiliko ya Katika itakapotembelea maeneo yao. MHE. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante. pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge. Kwa kuwa fedha hizi tunazotumia kwenye Chaguzi Ndogo kwa kweli ni nyingi zingeweza kujenga madarasa, maji na kadhalika. Na kwa kuwa zoezi la Katiba linaloendelea ambalo ni matarajio yetu mwaka 2014 ndio liwe limekamilika haliathiri majukumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ambayo ni kutunga sheria na kurekebisha sheria. Je, Serikali haioni ni wakati muafaka watuletee humu ndani Sheria ya Uchaguzi sisi Wabunge kwa pamoja tuijadili, tuitafakari ifanye kazi hadi Uchaguzi wa mwaka 2015 na baadaye maoni yatakapokuja kwenye Katiba basi maoni yale yatachukua nafasi yake? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kama nilivyosema jambo hili lina gharama kubwa na imethibitisha hivyo. Lakini mapendekezo aliyotoa Mheshimiwa Mbunge ni mazuri sana ya kurekebisha sheria, lakini lazima uanzie kwenye Katiba.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    372 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us