MKUTANO WA 18 TAREHE 3 FEBRUARI, 2015 MREMA 1.Pmd
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
3 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Saba - Tarehe 3 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- SPIKA: Hati za kuwasilisha mezani, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama au kwa niaba yake Mheshimiwa Capt. John Chiligati. MHE. CAPT. JOHN Z. CHILIGATI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Katika Kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. MHE. SELEMANI S. JAFO (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA): Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Katika kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. 1 3 FEBRUARI, 2015 MHE. DUNSTAN L. KITANDULA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara Katika Kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tumeletewa taarifa kwamba kwa sababu mgeni tulionao ndani ya nchi hii Rais wa Ujerumani vipindi vya TBC asubuhi hii vitakuwa kwenye TBC 2 na siyo TBC1, kwa sababu kule kuna mapokezi huko uwanja wa Taifa kule. Kwa hiyo, tutarudia tena baada ya mapokezi hayo kumalizika. Lakini pia jioni kwa sababu kutakuwa na dhifa ya kitaifa, pia matangazo hayatakuwa kwenye TBC1 na siyo vinginevyo. Kwa hiyo, hayo ni maelezo wazi sana. Maswali Waheshimiwa Wabunge tunaingia Ofisi ya Waziri Mkuu na Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe anauliza swali hilo, kwa niaba yake Mheshimiwa Grace Kiwelu. Na. 68 Ahadi ya Ujenzi wa Daraja la Mnepo Kijiji cha Mijongweni MHE. GRACE S. KIWELU (K.n.y. MHE. FREEMAN A. MBOWE) aliuliza:- Daraja la mnepo lililopo kijiji cha Mijongweni Kata ya Machame Weruweru, Wilayani Hai limekuwa kero ya muda mrefu inayohatarisha maisha na hata kufifisha uchumi na wananchi wa kata hiyo. Kwa zaidi ya miaka ishirini (20) Serikali imekuwa ikitoa ahadi mbalimbali za ujenzi wa daraja la kudumu bila utekelezaji:- 2 3 FEBRUARI, 2015 (a) Je, kwa mara nyingine tena, Serikali inatoa jibu gani la utatuzi wa tatizo hilo? (b) Je, ni sababu gani zinazosababisha jambo hili lisitekelezwe kwa vitendo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe, Mbunge wa Hai, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/2015 Halmashauri ya Wilaya Hai imeidhinishiwa shilingi bilioni 1,026,433,120.50 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za barabara, kati ya fedha hizo shilingi milioni 353 ni kwa ajili ya utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa daraja la Mnepo katika kijiji cha Mijongweni. Mheshimiwa Spika, hadi sasa Halmashauri ya Wilaya ya Hai ilishapelekewa shilingi milioni 266,959,192 ambapo shilingi milioni 210 zimeshatumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo. Kazi ya ujenzi wa nguzo za daraja umekamilika na ujenzi wa sehemu ya juu yaani deki unaendelea. Ujenzi wa daraja umefikia asilimia 65 na kazi inategemewa kukamilika mwisho mwa mwezi Machi, 2015. (b) Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa ahadi za Serikali umekuwa ukifanyika kwa awamu katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuzingatia upatikanaji wa rasilimali fedha. Hivyo hakuna sababu za makusudi za Serikali kuchelewa kutekeleza ahadi hiyo. Azma ya Serikali ni kuhakikisha hadi zote zinazotekelezwa ili kuimarisha huduma kwa wananchi. 3 3 FEBRUARI, 2015 Mheshimiwa Spik, Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa jimbo la Hai kuwa daraja hilo linajengwa na kukamilika ili kuondoa kero ya usafiri mahali hapo. MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza nishukuru kwa niaba ya Halmashauri yetu ya Hai kwa kupokea fedha hizo lakini ningependa kumwuliza Mheshimiwa Naibu Waziri amesema fedha zimeweza kukamilisha ujenzi wa daraja kwa asilimia 65 fedha zilizobaki zinaweza kukamilisha asilimia 35 iliyobaki? Kwa kukizingatia tunakwenda kipindi cha mvua ambapo daraja hilo limekuwa likisababisha vifo kwa wananchi wetu wa jimbo la Hai? Nashukuru sana. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru ameshukuru kwa jitihada hizo ambazo zimefanyika mimi hili eneo labda ni declare interest Siha ile inatokana na Hai kwa hiyo, mimi nalifahamu hilo daraja linalozungumzwa na nimekwenda kule, nimeliona nafahamu kinachozungumzwa hapa. Wakati tunaanza kujenga daraja hili tuliona hilo tatizo ambalo Mheshimiwa Grace Kiwelu analizungumzia. Kwa hiyo, kazi ya kwanza inayofanyika pale ni kuhakikisha kwamba tunaanza kujenga kutoka kule chini ili kuanza kuja kutengeneza sasa hii runway ambapo ndipo magari yatakapopita pale. Kwa hiyo, tatizo la kwamba mvua zitakuja zitatukuta huko tumeshapita look at my eyes and look at my lips nenda kaangalie kule utakuta hilo jambo linafanyika pale. Lakini kiasi cha pesa ambacho kimebaki ni shilingi milioni 147 ambazo nataka nimthibitishie Mheshimiwa kwamba kufikia mwezi Machi tena mwezi Machi nimekwenda mbali tu najaribu kuwa mwangalifu maana yake najua watakuja kunikandamizia hapo chini. 4 3 FEBRUARI, 2015 Lakini nataka nimthibitishie kwamba kazi hii inafanyika nimezungumza mimi hapa na engineer wa wilaya Bwana Kweka, asubuhi hii nikamwambia una hakika mkandarasi yuko kwenye site na amenithibishia kwamba kazi hii inaendelea. Uwe na amani moyoni mwako na Mheshimiwa Mbowe mwambie home boy wangu asiwe na wasiwasi, kazi inaendelea. (Makofi) SPIKA: Haya macho na lips hatuzionagi, Mheshimiwa Cynthia Ngoye swali linalofuata. Na. 69 Uchafu Kwenye Miji Nchini MHE. CYNTHIA HILDA NGOYE aliuliza:- Miji mingi hapa nchini ni michafu sana yakiwemo maeneo ya mitaa, Taasisi za Umma na za binafsi:- (a) Je, ni hatua zipi za muda mfupi na za muda mrefu zimewekwa ili kuhakikisha miji yetu ina usafi endelevu? (b) Je, ni utaratibu gani umewekwa na TAMISEMI kuhakikisha utekelezaji wa sheria, kanuni na maagizo yanayohusu uhifadhi wa mazingira yanatekelezwa kwa ukamilifu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cynthia Hilda Ngoye, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- 5 3 FEBRUARI, 2015 Mheshimiwa Spika, suala la usafi wa miji hapa nchini linasimamiwa na sheria mbalimbali zikiwemo sheria za mazingira ya mwaka 2004, sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009 pamoja na sheria ndogo za Halmashauri. Serikali inazingatia sheria hii katika kuhakikisha miji inakuwa safi ili kutunza mazingira na kuepuka magonjwa yanayosababishwa na uchafu. Usimamizi wa sheria kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo mamlaka za Serikali za Mitaa umekuwa siyo wa kuridhisha hali ambayo imesababisha baadhi kuwa na uchafu uliokithiri. Mheshimiwa Spika, pamoja na usimamizi usioridhisha wa sheria changamoto nyingine ni uhaba wa vifaa vya kufanyia usafi pamoja na baadhi ya wananchi kutothamini vifaa vya kufanyia usafi pamoja na baadhi ya wananchi kutothamini usafi wa mazingira kama sehemu ya maisha yao. Kwa kuzingatia hali hiyo Halmashauri zimekuwa zikitenga Bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufanyia usafiri. Mfano jiji la Mbeya, limenunua vifaa vya kuhifadhia na kusafirishia taka zinaitwa skip containers, magari manne ya kubeba makasha ya taka skip loaders trucks, makasha 83 ya kuhifadhia taka, mitambo miwili ya kuhudumia dampo la kisasa nak ukamilisha ujenzi wa dampo la kisasa yaani Sanitary landfill. Kazi zote hizi zimegharimu jumla ya shilingi bilioni 3.8. Aidha, Halmashauri kupitia sheria ndogo zimeweka adhabu kwa yoyote atakayesababisha uchafu ambayo ni kati ya shilingi 10,000 hadi shilingi 50,000 kama inavyofanyika katika Jiji la Mbeya. Manispaa ya Moshi na Jiji la Dar es Salaam. Hatua nyingine zinazochukuliwa ni kushirikisha Kamati za Maendeleo za Kata na Mitaa, vikundi vya kijamii na makampuni binafsi kushiriki moja kwa moja katika kupanga na kusimamia suala la usafi wa maeneo yao. ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imekuwa ikikumbusha Halmashauri na Mikoa kupitia vikao pamoja na kuhakikisha usimamizi wa Sheria na Kanuni za usafi unaimarishwa ili kufanya miji yake iweze kuwa safi. 6 3 FEBRUARI, 2015 Vilevile ofisi imekuwa ikifanya ufuatiliaji na kuchukua hatua kwa watendaji wanaoshindwa kusimamia usafi kwenye maeneo yao. Hivi sasa Serikali imeanzisha Idara ya Usafi na Mazingira katika Halmashauri kwa lengo la kuimarisha huduma ya usafi na usafishaji wa miji nchini. Utaratibu mwingine unaotumika ni kushindanisha Majiji, Manispaa, Miji na Halmashauri za Wilaya kila mwaka ili kutoa motisha kwa Halmashauri zinazofanya vizuri. Serikali itaendelea kusimamia Halmashauri kupitia mikoa ili kuhakikisha kazi ya usafi inatekelezwa kikamilifu. (Makofi) MHE. CYNTHIA HILDA NGOYE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na nimshukuru kwa majibu yake mazuri na fasaha. Nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Kwa kuwa ni kweli kwamba Serikali imekuwa ikiratibu masuala ya Usafi wa Mazingira katika Halmashauri za Wilaya na katika Miji na Majiji. Je, Waziri anaweza kutuambia hapa Bungeni ameweka mtu maalum katika ofisi yake au dirisha maalum ambaye anashughulikia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa Sheria Kanuni na Taratibu katika mikoa, wilaya na maeneo mengine hapa nchini? Swali