Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 24 Juni, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 111 Malipo ya Likizo za Watumishi MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Ni haki ya Mtumishi kulipwa likizo yake ya mwaka hata kama muda wa likizo hiyo unaangukia muda wake wa kustaafu:- Je, Serikali inatoa kauli gani kwa Watumishi ambao wamenyimwa likizo zao kwa kisingizio kuwa muda wao wa kustaafu umefika na kunyimwa kulipwa likizo zao. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Pauline Gekul, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni H. I ya Kanuni za Kudumu ( Standing Orders) likizo ni haki ya mtumishi. Endapo mwajiri ataona kuwa hawezi kumruhusu mtumishi kuchukua likizo yake, analazimika kumlipa mshahara wa mwezi mmoja mtumishi huyo. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni H.5 (a) ya Kanuni hizi, mtumishi hulipiwa nauli ya likizo kila baada ya miaka miwili. 1 Mheshimiwa Spika, kutokana na miongozo niliyoitaja, ni makosa kutomlipa mtumishi stahili yake ya likizo kabla ya kustaafu. MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi hii ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya msingi ya Waziri amesema kwamba ni haki ya watumishi wa Umma kulipwa likizo zao pale wanapostaafu. (a) Je, Serikali haioni kwamba sasa ni wakati mwafaka wa kulipa likizo za wastaafu hao ambao wamestaafu lakini hawakulipwa likizo zao? (b) Kwa kuwa mtumishi anapostaafu anahitaji kurudi katika eneo ambalo ametoka, na kwa kuwa katika shule za msingi katika Halmashauri ya mji wa Babati walimu wapatao watano (5) hawakuweza kulipwa likizo zao walipostaafu tangu mwaka jana mwezi wa kwanza mpaka leo, lakini pia walimu hao hawakuweza kupewa fedha za kusafirishia mizigo yao. Je, Serikali haioni kwamba imewatesa walimu hao kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka sasa hawapewi fedha za kusafirishia mizigo yao makwao na wakati huo huo hawajalipwa likizo. Je, Serikali inasema nini kuhusu wastaafu hao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA):- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Pauline Gekul, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, hapa tunazungumzia sheria hata kama mtu amekaa miaka mitano au mingapi, sheria ikisema kwamba ni haki yake alipwe na kama hakulipwa hatuwezi kukaa tuna-debate hapa, debate ya sheria iliishamalizika. Kwa hiyo hapa kama Mheshimiwa Mbunge anafikiri kwamba kuna watumishi waliondoka bila kulipwa kwa misingi hii ya sheria niliyoitaja hapa atuletee mara moja tutamwona Mheshimiwa Hawa Ghasia na kuzungumza naye na kumwambia hawa walipwe haki yao. Hatuwezi ku-debate hapa habari hiyo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge uwe na amani moyoni mwako, wewe katuletee na huyo unayesema kwamba alistaafu hapo akaenda bila kulipwa tuelewane kabisa. Mheshimiwa Spika, lakini nataka ni-quotion kitu kimoja. Haki inayozungumzwa hapa ni haki ya mshahara kwa sababu usije ukasema kwamba nipe mshahara halafu 2 useme nipatie pia na nauli yangu ya kwenda Muleba, akikulipa mshahara ndiyo habari imeishia hapo kwa maana ya mshahara aliokulipa. Kwa hiyo, mimi nataka nitahadharishe tu, lakini sisi tuko tayari kusikia hilo tutazungumza nao. Nimeita watu wangu wa human resources, tumezungumza na bwana Paraga amenieleza kwamba utaratibu ndiyo huo, lakini mimi niko tayari kumsikiliza tuasaidiane. MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Manispaa ya Kigoma Ujiji kuna walimu wengi sana ambao wamekuwa wanaenda likizo hawajapata stahili zao ni zaidi ya miaka miwili, mitatu. Pamoja na kwamba amesema hilo ni suala la sheria, lakini sheria isiyotekelezwa maana yake ni nini sasa? Naomba Mheshimiwa Waziri aniambie kuhusu jambo hili. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejementi ya Utumishi wa Umma, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Peter J. Serukamba, Mbunge wa Kigoma Mjini, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, mimi hapa nazungumzia matukio na sheria kwa maana ya nchi nzima. Mheshimiwa Serukamba anasema kwamba kuna watu ambao hawakupewa haki yao. Mimi nimekwenda Morogoro pale nika- head delegation pale na nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ambayo ili-review madai ya watumishi wote ukiacha hata na walimu wanaozungumzwa hapa. Tukasema tufanye mahesabu tuangalie kila kitu kinachodaiwa pale, baadaye tukaambiwa kwamba tupeleke madai yale kwa CAG’s Office aangalie na ahakiki aseme anaonaje kuhusu hayo madai. Taarifa ya CAG ikatoka ikasema kwamba hawa haki zao ni hizi, hawa haki zao ni hizi. Mheshimiwa Spika, hapa tuna-deal na nchi nzima, inawezekana kabisa kama anavyosema Mheshimiwa Serukamba kwamba katika hali hiyo bado kuna walioponyoka pale wakawa hawakulipwa haki zao. Mimi namuomba atuletee majina ya wale walimu anaowasema hapa sisi kama Serikali tutashughulikia jambo hilo. Na. 112 Matokeo Mabaya ya Kidato cha Nne MHE. VINCENT J. NYERERE aliuliza:- Matokeo ya mtihani wa kidato cha Nne mwaka 2010 hayakuwa mazuri na yameacha vijana wengi mitaani na vijijini, vijana ambao ni tegemeo la nguvu kazi ya Taifa lakini wamebaki bila elimu wala matarajio yoyote. 3 Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya vijana hao wengi waliobaki mitaani kutokana na kufeli katika mitihani yao. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA YA UFUNDI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vicent Josephat Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, matokeo ya mtihani wa kidato cha Nne mwaka 2010 hayakuwa mazuri na vijana wengi walishindwa mtihani huo. Kufuatia hali hiyo na kwa kuzingatia maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Seriakli za Mitaa(TAMISEMI) tumefanya utafiti ili kubaini sababu za ufaulu duni, na nini kifanyike kwa wanafunzi walioshindwa mtihani huo. Mheshimiwa Spika, kazi hii ya utafiti wa ufaulu duni imekamilika na Serikali itatoa tamko juu ya hilo katika mkutano huu wa Nne wa Bunge lako Tukufu. Aidha, wakati tunasubiri tamko hilo la Serikali, namwomba Mheshimiwa Mbunge pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote wawe na subira. MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mabaya ya kukatisha tamaa ya Mheshimiwa Waziri, naomba kumwuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa mojawapo ya majibu ya tafiti itakuwa ni ukosefu wa walimu, vifaa vya kufundishia na maabara na si kosa la wazazi na wanafunzi bali ni kosa la Serikali. (a) Je, Serikali haioni sasa ni muda mwafaka wa kuhakikisha watoto hao wanarudi shuleni ili wasome na wafanye mitihani na washinde ili wasiharibikiwe na maisha hapo baadae? (b) Je, Serikali haioni sasa ni muda mwafaka wa kufundisha stadi za kazi katika shule za sekondari kwa vitendo ili watoto wanaoshindwa kuingia kidato cha tano waweze kwenda katika soko la ajira moja kwa moja? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, ningependa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Vicent Nyerere, Mbunge wa Musoma Mjini, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, moja ni kuhusu sababu za ufaulu duni wa Kidato cha Nne. Kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge ni kweli michango yake ni mingi na hatuwezi tukawachukulia wanafunzi wale kwamba wao wenyewe tu peke yao ndiyo walikuwa wana makosa kwa ufaulu huu duni. 4 mSerikali imefanya utafiti imegundua, lakini kwa lile ambalo Mheshimiwa Mbunge amelipendekeza halitakuwa rahisi kulitekeleza kwa nchi nzima, kwa maana ya kuwarudisha wanafunzi wale wa kidato cha nne wote shuleni katika shule zetu hizi kwa sababu sisi sote tunafahamu kwamba katika shule zetu za Sekondari bado tuna mapungufu ambayo Serikali inahangaika kuweza kuyaweka vizuri ili tuweze kupata elimu bora. Mheshimiwa Spika, tuna uhaba wa madarasa na vitendeakazi. Sasa hivi kuna vijana tayari ni Form Four pamoja na kwamba kuna mapungufu kule madarasani, utakapowaleta tena wengine waingie humo humo kwenye Form Four ile bila shaka ni kwamba uwezo hautakuwepo wa kuwahudumia nao kwa lengo la kuweza kufanya mtihani kama wanafunzi wenzao wanaosoma full time. Kwa hiyo, hilo bahati mbaya hatutaweza kumudu kulifanya. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la pili kwamba Serikali ibadilishe mitaala ili iwe na mafunzo ya vitendo ili kumwezesha mwanafunzi awe na uwezo mkubwa zaidi anapomaliza shule. Hilo tutalizingatia, tumeanza kulifanyiakazi na tutaendelea kuhakikisha kwamba tunalifanyiakazi vizuri zaidi. (Makofi) MHE. AGNESS E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona, naomba niulize swali la nyongeza kama ifuatavyo. Kwa kuwa Wizara imetoa mwongozo kwa maswali katika shule za msingi kujibiwa kwa njia ya multiple choise au kwa kutikii. Je, Serikali haioni kwamba kwa kuendelea kufanya hivyo tunatengeneza watoto ambao wanafaulu kwa njia ya kubuni kwa kuwa watakuwa wanatiki tu kwa ku-guess hali ambayo itaendeleza watoto kufeli kama ilivyojitokeza
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages106 Page
-
File Size-