Majadiliano Ya Bunge ______

Majadiliano Ya Bunge ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Kumi na Nane - Tarehe 28 Juni, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani:- NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 pamoja na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. NAIBU WAZIRI WAZIRI WA MIUONDOMBINU: Randama za Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MASWALI NA MAJIBU Na. 121 1 Matatizo Katika Hospitali ya Wilaya - Geita MHE. ESTHER K. NYAWAZWA aliuliza:- Kwa kuwa, Hospitali ya Wilaya ya Geita inahudumia Kata 33 na madaktari Bingwa ni wawili (2) tu, na kwa kuwa upanuzi unasuasua na utawala ni mbovu:- Je, ni lini Serikali itarekebisha matatizo hayo? NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Kabadi Nyawazwa, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo. Hospitali ya Wilaya ya Geita ilijengwa mwaka 1957 kwa lengo la kuwahudumia wakazi wapatao 100,000 kwa kipindi hicho. Hadi kufikia Mei, 2010 Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina jumla ya Vijiji 191, Kata 33, Tarafa 7, Majimbo matatu ya Uchaguzi na wakazi wapatao 899,614. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina jumla ya vituo vya huduma ya Afya 61 ambavyo ni: - Hospitali 1 ya Wilaya, vituo vya Afya 9, Zahanati 39 za Serikali, Zahanati 8 za Mashirika yasiyo ya Kiserikali, na vinne (4) za watu binafsi. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Wilaya ya Geita ina watumishi wenye taaluma mbali mbali 218 kati ya watumishi 504 wanaohitajika sawa na asilimai 56.7 ya mahitaji. Kati ya watumishi hao madaktari wa magonjwa ya kawaida ni wawili (2) na Daktari mmoja wa kinywa na afya (DO). Suala la upungufu wa madaktari bingwa sio la hospitali ya wilaya ya Geita peke yake bali ni tatizo la Nchi nzima. Hata hivyo Serikali kupitia Mpango wa MMAM inachukua juhudi za makusudi kuimarisha vituovya kutolea huduma za afya vilivyopo kwa kuviboresha na kuongeza idadi ya watumishi wa kada mbalimbali. Katika mwaka 2010/2011 hospitali ya wilaya ya Geita inatarajia kupata madaktari wawili (2) na madaktari wasaidizi watatu (3). Mheshimiwa Spika, ili kuboresha huduma za afya ziendane na ongezeko la idadi ya watu na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya, halmashauri ya wilaya ya Geita imejenga kituo cha Afya cha Nyankumbu kilichopo mjini Geita na kimeanza kutoa huduma za afya. Vituo viwili vya Kharumwa na Nzera vinaendelea kufanyiwa ukarabati ili kuvipanua viweze kuhudumia wagonjwa wengi zaidi. 2 Mheshimiwa Spika, kuhusu utawala mbovu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, Serikali itafuatilia ili kuhakikisha kwamba watumishi wanafanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa. MHE. ESTHER K. NYAWAZWA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo ya nyongeza. Naomba kuchukua nafasi hii kuipongeza Serikali sana kuona umuhimu wa wilaya ya Geita kuiweka katika mkoa wa Geita. Mheshimiwa Spika, Waziri yeye amekiri kabisa kwamba wananchi wa Wilaya ya Geita ambao sasa wako kwenye mkoa wa Geita walikuwa watu wengi sana na huduma wanayoipata si ndogo sasa imekuwa Mkoa wa Geita. Je, Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha kwamba sasa hospitali ya Mkoa wa Geita inaleta wataalam wengi ambao wanaweza kuhudumia hasa akinamama wenye magonjwa yanayokidhi haja yao na watoto? NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Spika, kama alivyozungumza mwenyewe Mheshimiwa Mbunge ni kwamba sasa Geita imekuwa Mkoa, kwa hiyo tunasubiri ili iweze kutolewa katika Government Notice ili shughuli ziendelee. Naamini kabisa kwamba kwa sababu ni Mkoa basi Geita itapata hadhi yake, Bajeti itatengwa ili iweze kupata huduma zote kama mkoa. Lakini wakati huo huo zile wilaya nyingine tutakuwa tunaziendeleza kuzishauri ziweze kujenga ili hata hivyo ikiwa mkoa isiwe inaleta tena msongamano kwa kutegemea hospitali ya mkoa. (Makofi) Na. 122 Ukosefu wa Maabara Shuleni MHE. HAFIDHI ALI TAHIR aliuliza:- Kwa kuwa, moja kati ya sababu zinazosababisha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani yao ni ukosefu wa maabara mashuleni. (a)Je, ni asilimia ngapi ya shule za Serikali (za Sekondari na msingi) zenye maabara na ngapi hazina maabara? (b)Je, ni asilimia ngapi ya shule za Seminari zina maabara na ngapi zisizo na maabara ambazo Serikali imezisaidia? 3 NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA) alijibu:- (a) Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir, Mbunge wa Dimani, kama ifuatavyo. Mheshimiwa Spika, maabara ni muhimili wa masomo ya sayansi shuleni hasa shule za sekondari. Kukosekana kwa maabara kunasababisha kufeli masomo ya Sayansi. Serikali kwa kuliona hilo, inasisitiza sana kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwa shule zote za Sekondari sharti ziwe na maabara za Sayansi, kwa madhumuni ya kuwa na wanasayansi. Mheshimiwa Spika, Serikali imejitahidi sana kujenga maabara mpya katika shule mpya zinazoanzishwa pamoja na kuimarisha zilizopo na hivyo kuwa na idadi ifuatayo. Shule za skondari za Serikali zilizopo hadi Desemba 2009 ni 3,283, kati ya shule hizo zenye maabara ni 728 na zisizo na maabara ni 2,555 ambazo ni zile zilizojengwa na Serikali pamoja na kwa nguvu za wananchi. Kiasilimia shule zenye maabara ni asilimia 22 na zisizo na maabara ni aslimia 78. Shule za msingi za Serikali katika kujifunza somo la Sayansi kwa vitendo zina vivunge vya Sayansi ambavyo zina vifaa muhimu vya kufanyiwa majaribio ya sayansi kwa vitendo. (Makofi) Mkazo kwa hivi sasa ni kuimarisha shule za Sekondari zilizojengwa kwa mchango mkubwa wa wananchi ili ziwe na miundombinu kamilifu ikiwemo maabara za sayansi. Katika mpango wa maendeleo ya elimu ya Sekondari awamu ya pili (MMES) miundombinu muhimu kama maabara na nyumba za walimu imetiliwa mkazo. (b) Mheshimiwa Spika, shule Seminari zilizopo ni 104 na kati ya shule hizo 103 zina maabara ambayo ni asilimia 99% ya shule za semiari. Shule moja ya seminari ya Kipata iliyoko katika Manispaa ya Ilala haina maabara na hadi sasa ina kidato cha tatu. Aidha, Serikali haina mpango wowote wa kuisaidia Seminari hiyo. MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu lakini kama Serikali inafahamu kuwa kuwepo kwa maabara katika shule zetu za sekondari kunasaidia sana watoto kutokufeli na kutokuwepo watoto wengi wanafeli. Sasa Serikali ina mpango gani basi mbadala ambao utawafanya wanafunzi katika shule zetu hizi waweze kufaulu katika somo hili la Sayansi ambalo ni muhimu sana ukizingatia zaidi kwamba sasa hivi kuna shule 2,555 ambazo hazina maabara hivyo wanafunzi watapelekwa wapi katika suala hili? Serikali ina mpango gani mbadala? Mheshimiwa Spika, anaweza kuliambia Bunge hili ni sababu gani kubwa iliyopelekea shule za Seminari kufikia katika kiwango cha asilimia 99? Kwa kutokuwa na 4 maabara katika shule hizo lakini anaweza kuniambia ni kada gani inayosoma katika shule hizo za Seminari? SPIKA: Ni nini, kada sikuelewa. MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Ni kada gani ya kipato inayosoma katika shule hizo za Seminari? NAIBU WAZIRI WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA): Mheshimiwa Spika, naomba kutoa mpango mkakati ambao katika hotuba ya bajeti mwaka 2009/2010 Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya elimu aliuelezea kwamba baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga madara kwa kushiriana na wananchi katika awamu inayofuata ya mpango wa elimu ya sekondari kipaumbele cha kwanza ni maabara hivi sasa tunavyozungumza andiko limekamilika limegawanywa katika awamu tatu na kwamba maabara zitaanza kujengwa mara baada ya hotuba ya bajeti ya 2010/2011 kwa kushirikiana na TAMISEMI. Mheshimiwa Spika, suala la mbadala walimu wamepewa mbinu za kutumia badala ya maabara kamilifu. Hivi ninavyozungumza Mheshimiwa Spika Serikali imeanzisha mpango maalum wa kufufua maabara na kuimarisha mbinu za ufundishaji kwa walimu wa sayansi kambi kubwa iko mkoani Iringa inaendelea na kazi. Mheshimiwa Spika, suala la kada gani wanaosoma kwenye shule za sekondari za wamisionari nadhani anafahamu kwamba hizo ni shule binafsi mwenye uwezo anakwenda. MHE. MUDHIHIR M. MUDHIHIR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuwa pamoja na uhaba wa maabara sababu nyingine inayofelisha vijana kwa wingi ni uhaba wa mwalimu na kwa kuwa Serikali sasa hivi inafanya jitihada kubwa za kutengeneza walimu zaidi. Je, wakati tunasubiri matunda hayo mazuri isingekuwa jambo zuri kwa Serikali kuwaruhusu vijana wa form four wanaofeli mitihani yao kwa sababu ya uhaba wa walimu labda mmoja wa sekondari wafanye mitihani ya marudio kama school candidates, kwa sababu sio kosa lao wala si kosa la wazazi wao? NAIBU WAZIRI WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA): Mheshimiwa Spika, tunakiri kwamba idadi kubwa ya wanafunzi hawafanyi vizuri katika mitihani yao kutokana na kukosa walimu na masuala mengi muhimu. Suala la kurudia kama wanafunzi shuleni ni la kisheria, sheria tulizonazo

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    196 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us