Majadiliano Ya Bunge ___Mkutano Wa Kumi Na Moja

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Majadiliano Ya Bunge ___Mkutano Wa Kumi Na Moja NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Saba– Tarehe 25 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU WA MEZANI: HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/2019. NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimazi wa Udhibiti wa Nishati na Maji kwa Mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2017 [The Annual Report of Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) for the Year Ended 30th June, 2017]. MWENYEKITI: ahsante, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaanza na maswali yetu ya kawaida, tunaanza Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza Mbunge wa Chumbuni, kwa niaba ya Mheshimiwa Machano. Na. 135 Kuwakamata Wafanyabiashara Wakubwa wa Dawa za Kulevya MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itachukua hatua dhidi ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya wanaoingiza na kuuza badala ya kuakamata waathirika ambao wanahitaji misaada na ushauri nasaha wa kuachana na matumizi ya dawa hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejipanga na inaendelea kukabiliana na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa dawa za kulevya ambao wote wanasababisha madhara kwa jamii kwa kufanya biashara hiyo. Hadi kufikia Februari, 2018 jumla ya wanyabiashara 3,486 wa dawa za kulevya walikamatwa na kufikishwa mahakamani. Kati ya hao zaidi ya asilimia 30 ni wafanyabiashara wakubwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wamekimbia nchini kutokana na ukali wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Tano ya mwaka 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2017 pamoja na udhibiti unaofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola. Aidha, Serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya kwa kutoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya kwa watumiaji na jamii kwa ujumla. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa wale walioathirika kwa kutumia dawa za kulevya, wanapopatikana Serikalini imekuwa ikijikita zaidi kutoa ushauri nasaha, tiba na kuwahamasisha kupata tiba hiyo kwani hutolewa bure. Hadi kufikia mwezi Februari, 2018 zaidi ya warahibu 5,560 wamendelea kupata tiba katika vituo vya Serikali, mpango wa Serikali ni kusambaza huduma hii nchi nzima ili kuwafikia waathirika wengi wenye uhitaji. MWENYEKITI: Mheshimiwa Machano. MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa jibu lake. Lakini pamoja na jibu hilo naomba kuuliza maswala mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara hii ya dawa za kulevya ina mtandao mrefu, na katika mtandao huo wapo baadhi ya raia ya wa kigeni ambao wanaishi Tanzania wanajishirikisha na dawa hizi. Miaka miwili, mitatu, minne nyuma kuna mwanamke mmoja kutoka nchi jirani alikamatwa maeneo ya Mbezi beach na alikuwa akitumia passport nyingi na majina tofauti. Je, Serikali ina mpango gani wa kukabiliana na wageni ambao wanaitumia Tanzania kwa uuzaji wa madawa ya kulevya? Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, miongoni mwa waathirika wakubwa watumiaji wa dawa za kulevya ni wasanii wetu. Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wasanii 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) hawa kuondokana na tatizo hili la utumiaji wa dawa za kulevya? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la kwanza, sheria yetu haibagui wenyeji na ugeni. Inapotokea mtu yeyote anajihusisha na dawa za kulevya sheria yetu imekuwa ikitumika kwa kuhakikisha kwamba hatua stahiki zinachukuliwa na kufanya kitu ambacho kinaitwa deterrence ili kuwazuia watu wengine wasifanye biashara hii ya dawa za kulevya. Adhabu kali kali hutolewa na hatua stahiki huchukuliwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu kuwasaidia wasanii; katika mpango tulionao wa kuhakikisha kwamba tunatatua changamo hii ya dawa za kulevya ambayo inawaathiri vijana wengi ikiwemo nguvu kazi ya taifa hili, moja kati ya kazi kubwa tunayofanya ni kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya. Vilevile katika mpango mmoja wapo ni kuhakikisha kwamba tunafanya kitu kinaitwa supply reduction kuhakikisha kwamba madawa hawa hayapatikani na hivyo kutokuwalazimu vijana wengi zaidi kuweza kuyatumia. Tume imefanya kazi kubwa mpaka hivi sasa na wameendelea kukamata na kuteketeza dawa nyingi na hivi sasa kuna upungufu mkubwa sana wa dawa za kulevya katika viunga vya miji yetu mingi ya Tanzania kutokana na kazi kubwa ambayo inafanywa na tume. MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Bulembo Halima. MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuku kwa kuniona. Kumekuwa na malalamiko mengi ya waathirika wa dawa za kulevya wanapokuwa rehab (rehabilitation) wanakaribia kupona wahusika wanawachoma tena dawa ya kulevya ili wasiweze kutoka na lengo limekuwa ili waendelee kujipatia fedha. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha rehab zao wenyewe ili kuweza kuwasaidia waathirka hawa dawa za kulevya? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, kwa kifupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia kubwa ya sober house zinamilikiwa na watu binafsi na hilo lililolalamikiwa na Mheshimiwa Mbunge hatujapata malalamiko rasmi. Hata hivyo niseme tu kwamba kwa kuzingati hizi sober house nyingi ziko chini ya watu binafsi tumeamua sasa kutengeneza miongozo ambayo itasaidia namna bora ya management ya hizi sober house ili inapotokea mazingira ya namna hiyo tuwe tuna sehemu ya kuweza kukabiliana nao, kwa sababu miongozo ile itakuwa inaeleza mtu ambaye ni muathirika wa madawa ya kulevya awe treated vipi. Mpango wa Serikali, katika swali lake, ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na sober house nyingi za Serikali ili kuondokana na changamo hii ambayo wananchi wengi wanaipata hasa kutokana na gharama kubwa ya kulipia katika hiyo sober house. MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa suala la madawa ya kulevya ni suala ambalo walinzi wake ni wananchi wote, hatuwezi kuiachia Mamlaka na Serikali peke yake. Mbunge, mwananchi unapouona kuna athari kama hiyo unatakiwa useme, utoe taarifa kwa mamlaka zinazohusika, Mheshimiwa Waziri Jenista. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Tumepokea hii taarifa sasa mara kadhaa na hata wakati wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Waheshimiwa Wabunge wametuarifu kwamba uko mchezo mbaya unaoendelea kwenye sober house; badala kuwasaidia vijana wetu wapone na waondoke ndani ya sober house, lakini taarifa ambazo tumekuwa tukizipokea ni kwamba wamiliki 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wa sober house wanataka kuendelea kuwaweka vijana wetu pale kwa faida binafsi. Naomba sasa nitoe tena agizo kwa wamiliki wa sober house wote ambao wana mchezo huo ambao umekuwa ukisemekana wauache haraka. Mheshimiwa Mwenyekiti, na ninatumia muda huu pia kuiagiza mamlaka sasa kuanza kufanya uchunguzi wa kina na atakaye bainika ana tabia hiyo aweze kuchukuliwa hatua haraka sana na hiyo itatusai kuwaokoa vijana wetu kutokuendea kutumia dawa za kulevya katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi) MWENYEKITI: ahsante, Waheshimiwa tunaendelea, Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha. Na. 136 Mafanikio ya Mradi wa MIVARF MHE. ASHA MSHIMBA JECHA aliuliza:- Mradi wa Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi Vijijini (MIVARF) katika Mkoa wetu wa Kusini Unguja umeweza kuwakomboa wananchi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na kuboresha mawasiliano ya barabara na kuweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi. Kwa kuwa mradi huu umeonesha mafanikio na wananchi wamehamasika. Je, Serikali ipo tayari kuwaongezea mitaji na mafunzo wananchi hao ili waweze kufikia malengo yao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni azma ya Serikali kuhakikisha inaunga mkono juhudi za wananchi kushiriki katika uchumi wa kilimo kwa kusaidia upatikanaji wa mitaji na kuwapatia mafunzo stahiki. Hatua za kuwawezesha wananchi wa Zanzibar kimtaji zilianza kwa kuvijengea uwezo wa kiutawala na kiutendaji Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) na vikundi vingine vya uzalishaji ili viweze kuratibu na kusimamia kwa ufanisi matumizi ya mitaji itakayopatikana kupitia mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, matayarisho yanaendelea ili kuvipatia vikundi vya wazalishaji ambavyo tayari vimehakikiwa na uwezo wao baada ya ziara ya uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutembelea Zanzibar mwezi
Recommended publications
  • Tarehe 7 Februari, 2017
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA SITA Kikao cha Saba – Tarehe 7 Februari, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: MHE. PROF. NORMAN A. S. KING – MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2016 hadi Januari, 2017. MHE. DOTO M. BITEKO -MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kipindi cha kuanzia Januari 2016 hadi Januari 2017. NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na maswali, Ofisi ya Rais - TAMISEMI. Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Na. 69 Tatizo la Ulevi MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Ulevi wa kupita kiasi hasa wa pombe za kienyeji umekuwa na athari kubwa za kiafya na kiakili kwa Watanzania wenye tabia ya ulevi wa kukithiri:- Je, Serikali imejipanga vipi kukabiliana na tatizo hilo hasa ikizingatiwa kuwa Sheria ya Vileo ya mwaka 1969 ni ya zamani sana kiasi kwamba inawezekana kabisa haikidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo kwa wakati huu. NAIBUWAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, pombe za kienyeji zimeainishwa katika Kifungu cha pili (2) cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77.
    [Show full text]
  • Tarehe 12 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Saba – Tarehe 12 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Saba. Natumaini mlikuwa na weekend njema Waheshimiwa Wabunge, ingawaje weekend ilikuwa na mambo yake hii. Jana nilimtafuta Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba kwa mambo yetu haya ya Bunge kuhusiana na uchangiaji wa Mpango wa Maendeleo akaniambia Mheshimiwa Spika tafadhali niache. Aah! Sasa nakuacha kuna nini tena? Anasema nina stress. Kumbe matokeo ya juzi yamempa stress. (Makofi/Kicheko) Pole sana Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, na Wanayanga wote poleni sana. Taarifa tulizonazo ni kwamba wachezaji wana njaa, hali yao kidogo, maana yake wamelegealegea hivi. Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge baadaye tunaweza tukafanya mchango kidogo tuwasaidie Yanga ili wachezaji… (Kicheko) Katibu, tuendelee. (Kicheko) NDG. EMMANUEL MPANDA – KATIBU MEZANI: 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA NA VIJANA) (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu. Katibu! NDG. EMMANUEL MPANDA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali la kwanza linaelekea TAMISEMI na litaulizwa na Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, Mbunge kutoka kule Ruvuma. Na. 49 Hitaji la Vituo vya Afya – Tunduru MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga vituo vya afya katika Kata za Tinginya, Muhimba, Kalulu, Mindu, Nalasi Magharibi na Nalasi Mashariki Wilayani Tunduru? SPIKA: Majibu ya Serikali kuhusu ujenzi wa vituo vya afya Ruvuma na nchi nzima, Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI, Mheshimiwa David Silinde, tafadhali.
    [Show full text]
  • Annual Report 2013/14 Highlights
    H E KI RU MA NI UHU UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM ANNUAL REPORT 2013 - 2014 University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 VISION STATEMENT A leading centre of intellectual wealth spearheading the quest for sustainable and inclusive development. MISSION STATEMENT To advance the economic, social and technological development of Tanzania and beyond through excellent teaching and learning, research and knowledge exchange. GUIDING THEME The focus of the University of Dar es Salaam activities during the reporting period, continued to be guided by the following theme: “Enhanced quality outputs in teaching, research and public service”. Multi-media Laboratory at CoICT – Kijitonyama Campus University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 i ANNUAL REPORT 2013/14 HIGHLIGHTS ii University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 ANNUAL REPORT 2013/14 HIGHLIGHTS University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 iii ANNUAL REPORT 2013/14 HIGHLIGHTS iv University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 ANNUAL REPORT 2013/14 HIGHLIGHTS 7 University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 University of Dar es Salaam ANNUAL REPORT 2013-14 v TABLE OF CONTENTS Vision Statement ........................................................................................................................ i Mission Statement ...................................................................................................................
    [Show full text]
  • 1 Bunge La Tanzania
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Tano – Tarehe 5 Februari, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae, Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: KIAPO CHA UAMINIFU Mhe. Dkt. Adelardus Lubango Kilangi NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MHE. MOSHI S. KAKOSO - K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA - K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2017. NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 55 Changamoto Zinazowakabili Walemavu MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:- Watanzania wenye ulemavu wanakabiliwa na kero mbalimbali za kimaisha ikiwemo ukosefu wa ajira kama ilivyo kwa Watanzania wengine, aidha, zipo changamoto za jumla kama vile kijana mwenye ulemavu wa ngozi asiye na ajira ana changamoto ya mahitaji ya kujikimu na pia ana changamoto za kipekee za mahitaji ya kiafya na kiusalama. Je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu umuhimu wa kuwatazama vijana wenye ulemavu mbalimbali kwa namna ya pekee na kama zipo sera na mikakati ya kiujumla kwa vijana wote nchini? NAIBU SPIKA: Ofisi ya Waziri Mkuu sijui nani anayejibu maswali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, niko hapa.
    [Show full text]
  • THEME “Science, Technology, Engineering and Mathematics For
    UNITED REPUBLIC OF TANZANIA ENGINEERS REGISTRATION BOARD 15TH ANNUAL ENGINEERS DAY Dr. Jakaya Kikwete Convection Centre - DODOMA September 7– 8, 2017 CONFERENCE PROCEEDINGS THEME “Science, Technology, Engineering and Mathematics for Industrialization towards Socio-economic Development” TABLE OF CONTENTS Contents TABLE OF CONTENTS ................................................................................................................................ I PREFACE ...................................................................................................................................................... II 1.0 OPENING SESSION ................................................................................................................................ 1 1.1 INTRODUCTION .............................................................................................................................................. 1 1.1.1 Greetings from the Dodoma Regional Commissioner .......................................................................... 1 1.1.2 Introduction from the ERB Acting Registrar......................................................................................... 1 1.2 INTRODUCTORY REMARKS ............................................................................................................................ 2 1.3 STATEMENT FROM ONE OF THE FOREIGN DELEGATES ................................................................................... 4 1.4 OATH TAKING CEREMONY ...........................................................................................................................
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Nne - Tarehe 31 Januari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) Spika (Mhe.Job Y. Ndugai) Alikalia Kiti D U A Spika (Mhe.Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Nane, Kikao cha leo ni Kikao cha Nne. Katibu! NDG. LAWRENCE MAKIGI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MHE. MIRAJI J. MTATURU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2019. SPIKA: Ahsante sana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Wenyeviti mnaowasilisha muwe mnakuwa karibu ili tuokoe muda na anayefuata awe karibu pia. Karibu sana Mwenyekiti kwa niaba ya! MHE. JULIUS K. LAIZER (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kanati kwa mwaka 2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Kalanga. Katibu! 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NDG.LAWRENCE MAKIGI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Mhehsimiwa Waziri Mkuu, swali la kwanza litauliza na Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa, Senator, Mbunge wa Sumve Na. 37 Ujenzi wa Kiwanda cha Pamba-Kwimba MHE. RICHARD M. NDASSA aliuliza:- Kupitia Mifuko ya Jamii tayari tathmini ya kukijenga Kiwanda cha kuchambua pamba Nyambiti Ginnery kilichopo Kwimba umeshafanyika, kilichobaki ni uamuzi wa Serikali kuliongezea thamani zao la pamba.
    [Show full text]
  • 4 FEBRUARI, 2019.Pmd
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Sita – Tarehe 4 Februari, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Nne, Kikao cha Sita. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- MHE. AGNESS M. MARWA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018. MHE. KANALI (MST) MASOUD ALI KHAMIS – (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 53 Ombi la Halmashauri ya Geita DC Kugawanywa MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza:- Halmashari ya Geita DC ina Majimbo mawili ya Geita Viijini na Busanda ambayo kiutawala husababisha usumbufu na hali tete kwa wananchi kijiografia na mkoa ulishapitisha kuomba Serikali iigawe kuwa na Halmashauri ya Busanda:- Je, ni lini Serikali itaridhia ombi hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Kasheku Musukuma, Mbunge wa Geita Vijijini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura Na.
    [Show full text]
  • Dreamliner: Ndoto Iliyotimia Rais Magufuli: Itaongeza Mapato, Heshima Ya Nchi Vyombo Vya Habari Kimataifa Vyaisifu Tanzania Tabasamu La Obama Serengeti
    Jarida la NchiUtamaduni, Yetu Sanaa na Michezo Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO JARIDA LA MTANDAONI TOLEO LA Juni-Julai 2018 Dreamliner: Ndoto Iliyotimia Rais Magufuli: Itaongeza Mapato, Heshima ya Nchi Vyombo vya Habari Kimataifa Vyaisifu Tanzania Tabasamu la Obama Serengeti www.maelezo.go.tz i Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO Bodi ya Uhariri Mwenyekiti Dkt. Hassan Abbasi Mkurugenzi-Idara ya Habari-MAELEZO Wajumbe Rodney Thadeus Jonas Kamaleki John Lukuwi Elias Malima Casmir Ndambalilo Msanifu Jarida Hassan Silayo Huduma zitolewazo MAELEZO 1.Kutangaza Utekelezaji wa Serikali. 2.Kuuza Picha za Viongozi wa Taifa na Matukio Muhimu ya Serikali. 3.Kusajili Magazeti na Majarida 4.Kukodisha Ukumbi kwa Ajili ya Mikutano na Waandishi wa Habari. 5.Rejea ya Magazeti na Picha za Zamani 6.Kupokea Kero Mbalimbali za Wananchi. Jarida hili hutolewa na: Idara ya Habari-MAELEZO S.L.P 25 Dodoma-Tanzania Baruapepe:[email protected] Blogu: blog.maelezo.go.tz Website: www.maelezo.go.tz Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO ii TAHARIRI NI BAJETI ILIYOLENGA KUINUA MAISHA YA WANANCHI Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa na kupitishwa Bungeni hivi karibuni ni bajeti inayolenga kuwainua wananchi na kuboresha maisha yao. Tumeona jinsi Wabunge wa Chama Tawala na Vyama vya Upinzani wakiiunga mkono kwa namna ilivyoondoa kero zilizokuwa zikiwasumbua wananchi hasa wa kipato cha chini. Kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka takribani 57 ya uhuru, Bajeti Kuu ya Serikali haikupandisha bei za vinywaji na sigara zinazotengenezwa nchini ili kulinda viwanda vya hapa nchini. Kwa jinsi hii wananchi wa kipato cha chini wataweza kupata bidhaa hizi bila ongezeko la bei.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Ishirini Na Mbili – Tarehe 18 Mei, 2
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 18 Mei, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe.Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa Fedha 2016/2017. NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. NEEMA MSANGI - KATIBU MEZANI: Maswali! MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Amina Nassoro Makilagi, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Kwa niaba yake, Mheshimiwa Bura. Na. 184 Umuhimu wa Rasilimali Watu Katika Kukuza Uchumi wa Taifa MHE. FELISTER A. BURA (K.n.y. AMINA N. MAKILAGI) aliuliza:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali ina mkakati gani wa kutumia rasilimali watu katika kukuza uchumi wa Taifa, hasa ikizingatiwa kuwa rasilimali hiyo ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa Taifa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Amina Nassoro Makilagi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua kuwa ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini, matumizi ya rasilimali watu ni muhimu sana. Ili kuhakikisha kuwa rasilimali watu inawezeshwa na kutumika kukuza uchumi wa Taifa, Serikali imeweka mikakati ifuatayo:- (i) Serikali imeandaa mkakati wa Kitaifa wa kukuza ujuzi nchini ambao umelenga kutoa mafunzo ya vitendo yatakayofanyika maeneo ya kazi (apprenticeship and internship programs).
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA TATU Kikao Cha Ishirini Na Tisa
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Tisa – Tarehe 17 Mei, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Mtaturu. MHE. MIRAJI J. MTATURU K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea, Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Maswali tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Mheshimiwa Bryceson Magessa Tumaini Mbunge wa Busanda sasa aulize swali lake. Na. 243 Uhitaji wa Vituo vya Afya katika Jimbo la Busanda MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza:- Je, ni lini Serikali italipatia Jimbo la Busanda Vituo vya Afya hususan Tarafa ya Butundu na Tarafa ya Busanda? NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mheshimiwa Silinde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA SABA Kikao Cha Kumi Na Tatu – Tarehe 27 Aprili, 2
    NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 27 Aprili, 2017 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. RAMADHANI ABDALLAH ISSA - KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MHE. RITA E. KABATI (K.n.y. MHE. DKT. NORMAN A.S. KING - MWENYEKITI KAMATI YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. QAMBALO W. QULWI (K.n.y. MHE. JAMES F. MBATIA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu. NDG. RAMADHANI ABDALLAH ISSA - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali tutaanza na Ofisi na Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa John P. Kadutu, Mbunge wa Ulyankulu, swali lake litaulizwa kwa niaba na Mheshimiwa Constatine Kanyasu, Mbunge wa Geita. Na. 105 Ukiukwaji wa Sheria unaofanywa na Makampuni ya Migodi MHE.
    [Show full text]
  • Tarehe 13 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Nane – Tarehe 13 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu Tatu, leo ni Kikao cha Nane. Katibu NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI SPIKA: Hati za kuwasilisha Mezani, Mheshimiwa Waziri Mkuu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2021/2022. MHE. JOSEPH K. MHAGAMA K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, baadaye tutakapokuwa tunaisoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni muhimu vilevile kupitia Hotuba za Kamati, zinasaidia kutoa picha pana zaidi kuhusiana na Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Sasa nimuite Mwenyekiti wa Kudumu ya Bajeti na wale Wenyeviti wengine wasogee karibu karibu. Mheshimiwa Shally J. Raymond, karibu sana. MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
    [Show full text]