MKUTANO WA SABA Kikao Cha Kumi Na Tatu – Tarehe 27 Aprili, 2
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 27 Aprili, 2017 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. RAMADHANI ABDALLAH ISSA - KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MHE. RITA E. KABATI (K.n.y. MHE. DKT. NORMAN A.S. KING - MWENYEKITI KAMATI YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. QAMBALO W. QULWI (K.n.y. MHE. JAMES F. MBATIA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu. NDG. RAMADHANI ABDALLAH ISSA - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali tutaanza na Ofisi na Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa John P. Kadutu, Mbunge wa Ulyankulu, swali lake litaulizwa kwa niaba na Mheshimiwa Constatine Kanyasu, Mbunge wa Geita. Na. 105 Ukiukwaji wa Sheria unaofanywa na Makampuni ya Migodi MHE. CONSTATINE J. KANYASU (K.n.y JOHN P. KADUTU) Aliuliza:- Kampuni binafsi ya migodi zimekuwa zikikiuka mikataba ya kazi na pia zikikandamiza na kuwanyanyasa wafanyakazi:- (a) Je, ni lini Serikali itafanya ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofamya kazi migodini? (b) Je, kwa nini Serikali isiamue kuwaondoa nchini waajiri wakorofi kwa unyanyasaji wanaoufanya? 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) Alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa John Peter Kadutu, Mbunge wa Ulyankulu, kama ifutavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, waajiri wote nchini yakiwemo na makampuni ya madini wanapaswa kutekeleza matakwa ya Sheria za Kazi kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi, kupunguza migogoro isiyo ya lazima sehemu za kazi na kuongeza tija na uzalishaji mahala pa kazi. Ofisi yangu imeendelea kutekeleza majukumu yake ya usimamizi wa sheria kwa kufanya kaguzi sehemu za kazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa waajiri wanazingatia matakwa ya sheria. Pia elimu ya sheria za kazi zinatolewa kwa waajiri, wafanyakazi na vyama vyao ili kuongeza uelewa wao katika kutekeleza sheria. Aidha, hatua zinachukuliwa kwa kuwafikisha Mahakamani waajiri wanaokiuka masharti ya sheria za kazi. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ukaguzi wa mikataba wa kampuni zinazofanya kazi migodini, Serikali iliunda kikosi kazi ambacho kilishirikisha Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, NSSF, SSRA, OSHA, Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wakala wa Ukaguzi wa Madini. Kikosi hiki kilipewa jukumu la kufanya ukaguzi wa kina kwenye migodi iliyopo kanda ya Ziwa na Kaskazini kwa lengo la kuangalia hali halisi ya utekelezaji wa sheria za kazi, afya na usalama mahali pa kazi, masuala ya hifadhi ya jamii, fedha na kodi. Mheshimiwa Naibu Spika, aidha Serikali inatambua umuhimu wa uwekezaji katika kukuza fursa za ajira kwa Watanzania na kuchangia kukua kwa uchumi. Serikali itaendelea kusimamia sheria za kazi ili kuhakikisha kuwa waajiri wote nchini wanatimiza wajibu wao na wawekezaji wanapata nafasi ya kuwekezana kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi yetu kwa kufuata sheria zilizoko nchini. 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Constantine Kanyasu swali la nyongeza. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa pamekuwepo na unyanyasaji mkubwa sana wa wafanyakazi katika migodi, ikiwepo tabia ya ku-blacklist wafanyakazi na mfanyakazi anapokuwa blacklisted hawezi kuajiriwa sehemu yoyote katika mgodi, mara nyingi wanapokuwa blacklisted hawapewi nafasi ya kusikilizwa. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri ni kwa kiwango gani vyama vya vya wafanyakazi vina uwezo wa kuwatetea wafanyakazi linapoteka tukio kama hili? (Makofi) Swali langu la pili, migodi mingi imekuwa ikiwashirikisha wananchi wanaozunguka migodi kwa ajili ya ulinzi lakini wananchi hao wamekuwa wakipwewa mikataba ya mwaka mmoja na miezi sita, hawana bima na hawana mikataba ya aina yoyote, hili linafanyika ili kukwepa sheria ya kuwalipia NSSF na faida zao zingine. Je, ni lini migodi hii itaelekezwa kuhakikisha kwamba wananchi hawa wanapewa mikataba na wanalipwa haki zao kama wafanyakazi? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la kwanza la unyanyashaji na blacklisting ambayo imekuwa ikifanyika, kama Wizara tumeshapata malalamiko hayo kutoka kwa wafanyakazi wengi walioko katika migodi, ambao wamekuwa wakilalamika kwamba waajiri wengi katika migodi hii hasa baada ya kuwa wafanyakazi hawa wametoka katika maeneo yao, wamekuwa wakiwa- blacklist ili wasipate nafasi yakuweza kuajiriwa katika migodi mingine na makampuni zingine. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tumeshachukua hatua na tayari katika ukaguzi wetu huu ambao tumeufanya 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) katika migodi yote, moja kati ya taarifa ambayo tunaisubiri ambayo itafanyiwa utekelezaji ni pamoja na jambo hilo na Serikali itatoa maelekezo kwa waajiri wote kwamba wanachokifanya ni kinyume na utaratibu wa sheria za nchi na hairuhusiwi kwa mwajiri yeyote kum-blacklist mfanyakazi. Kwa hiyo, tutaendelea kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaoendelea kufanya jambo hili, ambalo linawaondolea haki ya kimsingi kabisa wafanyakazi wa Kitanzania. Mheshimiwa Naibu Spika, pili kuhusu mikataba, kwa mujibu wa Sheria Na. 6 ya mwaka 2004 imeanisha vema katika Kifungu Na. 14 aina ya mikataba ambayo mwajiri anapaswa kumpatia mfanyakazi. Kama Mwajiri anakiuka katika eneo hilo, anashindwa kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria inavyosema, Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie kwamba kwa sababu umeleta lalamiko hili rasmi tutalifanyia kazi na tutachukua dhidi ya wale waajiri wote ambao wanashindwa kukidhi matakwa ya Kifungu Na. 14 cha Sheria za Kazi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mukya, swali la nyongeza. MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kumekuwa na tabia mbaya na chafu ya udhalilishaji wa hawa waajiri wa madini ya kuwapekua wafanyakazi sehemu za siri. Hii imefanyika katika Kampuni ya Tanzanite one kule wanapovuna madini ya Tanzanite, wanawapekua sehemu za siri hasa sehemu za kujisaidia haja kubwa. Je, hakuna njia mbadala ya kufanya zoezi hilo zaidi ya kuwadhalilisha hawa wafanyakazi (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Antony Mavunde, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI,VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, anachokisema Mheshimiwa Mbunge, mimi mwenyewe nilikwenda pale Tanzanite one katika mgodi huo, nilikutana na changamoto hiyo kubwa ambayo wafanyakazi waliieleza mbele yangu. 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa ziara ile nilitoa maelekezo na taratibu zote za namna ya ukaguzi unavyopaswa kufanyika ili usidhalilishe utu wa wafanyakazi ambao wanafanya kazi katika migodi hiyo. Maelekezo yalitolewa ya kwamba zipo taratibu za kufuata katika ukaguzi lakini siyo za kumdhalilisha mtu. Mheshimiwa Naibu Spika, nimuondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba maelekezo tayari yapo, kama vitendo hivi vinaendelea basi niwaombe wafanyakazi wale waripoti tuchukue hatua stahiki zaidi. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rita Kabati, swali la nyongeza. MHE. RITA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa huu udhalilishaji ambao umekuwa ukifanyika na hao wawekezaji siyo katika migodi tu, upo hata katika viwanda vyetu. Nimeshuhudia mara nyingi sana Mheshimiwa Naibu Waziri akienda kusuluhisha migogoro hasa ikihusiana na unyanyasaji wa wafanyakazi. Je, ni adhabu gani kubwa kabisa ambao wamekuwa wakipatiwa hawa waajiri au wawekezaji ambao wamekuwa wakiwanyanyasa hawa wafanyakazi. Kwa sababu nimeona jambo hili limekuwa likijirudia mara kwa mara. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Antony Mavunde majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI,VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kila mwekezaji anayekuja kuwekeza hapa nchini hasa wale ambao wanapitia TIC na wale ambao wamejisajili katika Vyama vya Waajiri. Wamekuwa wakipewa sheria za nchi hii na utaratibu ambao unapaswa kufuatwa na jambo lolote linalojitokeza kinyume chake hapo sisi kama Serikali tumeendelea kuchukua hatua stahiki. Mheshimiwa Naibu Spika, tuna changamoto kubwa sana kwa wawekezaji raia wa China ambao wengi 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wamekuwa wakiingia nchini na taratibu za kisheria zimekuwa hazifuatwi, lakini wale ambao wamesajiliwa wako chini ya ATE. ATE wamefanya kazi kubwa ya tafsiri sheria za kazi za nchi yetu kwenda katika lugha ya Kichina. Maana mwanzoni wao walikuwa wanatumia excuse ya kutofahamu sheria, ingawa katika principle zile za sheria katika ile maxim inayosema ignorantia juris non excusat, ambayo inasema muhimu kabisa kwamba hakuna excuse kwa mtu ambaye hafahamu sheria. Kwa hiyo walichokifanya hawa waajiri wametafsiri sheria zile, lakini bado kuna watu