NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Saba– Tarehe 25 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU WA MEZANI: HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/2019. NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimazi wa Udhibiti wa Nishati na Maji kwa Mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2017 [The Annual Report of Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) for the Year Ended 30th June, 2017]. MWENYEKITI: ahsante, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaanza na maswali yetu ya kawaida, tunaanza Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza Mbunge wa Chumbuni, kwa niaba ya Mheshimiwa Machano. Na. 135 Kuwakamata Wafanyabiashara Wakubwa wa Dawa za Kulevya MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itachukua hatua dhidi ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya wanaoingiza na kuuza badala ya kuakamata waathirika ambao wanahitaji misaada na ushauri nasaha wa kuachana na matumizi ya dawa hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejipanga na inaendelea kukabiliana na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa dawa za kulevya ambao wote wanasababisha madhara kwa jamii kwa kufanya biashara hiyo. Hadi kufikia Februari, 2018 jumla ya wanyabiashara 3,486 wa dawa za kulevya walikamatwa na kufikishwa mahakamani. Kati ya hao zaidi ya asilimia 30 ni wafanyabiashara wakubwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wamekimbia nchini kutokana na ukali wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Tano ya mwaka 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2017 pamoja na udhibiti unaofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola. Aidha, Serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya kwa kutoa elimu ya madhara ya dawa za kulevya kwa watumiaji na jamii kwa ujumla. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa wale walioathirika kwa kutumia dawa za kulevya, wanapopatikana Serikalini imekuwa ikijikita zaidi kutoa ushauri nasaha, tiba na kuwahamasisha kupata tiba hiyo kwani hutolewa bure. Hadi kufikia mwezi Februari, 2018 zaidi ya warahibu 5,560 wamendelea kupata tiba katika vituo vya Serikali, mpango wa Serikali ni kusambaza huduma hii nchi nzima ili kuwafikia waathirika wengi wenye uhitaji. MWENYEKITI: Mheshimiwa Machano. MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa jibu lake. Lakini pamoja na jibu hilo naomba kuuliza maswala mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara hii ya dawa za kulevya ina mtandao mrefu, na katika mtandao huo wapo baadhi ya raia ya wa kigeni ambao wanaishi Tanzania wanajishirikisha na dawa hizi. Miaka miwili, mitatu, minne nyuma kuna mwanamke mmoja kutoka nchi jirani alikamatwa maeneo ya Mbezi beach na alikuwa akitumia passport nyingi na majina tofauti. Je, Serikali ina mpango gani wa kukabiliana na wageni ambao wanaitumia Tanzania kwa uuzaji wa madawa ya kulevya? Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, miongoni mwa waathirika wakubwa watumiaji wa dawa za kulevya ni wasanii wetu. Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wasanii 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) hawa kuondokana na tatizo hili la utumiaji wa dawa za kulevya? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la kwanza, sheria yetu haibagui wenyeji na ugeni. Inapotokea mtu yeyote anajihusisha na dawa za kulevya sheria yetu imekuwa ikitumika kwa kuhakikisha kwamba hatua stahiki zinachukuliwa na kufanya kitu ambacho kinaitwa deterrence ili kuwazuia watu wengine wasifanye biashara hii ya dawa za kulevya. Adhabu kali kali hutolewa na hatua stahiki huchukuliwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu kuwasaidia wasanii; katika mpango tulionao wa kuhakikisha kwamba tunatatua changamo hii ya dawa za kulevya ambayo inawaathiri vijana wengi ikiwemo nguvu kazi ya taifa hili, moja kati ya kazi kubwa tunayofanya ni kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya. Vilevile katika mpango mmoja wapo ni kuhakikisha kwamba tunafanya kitu kinaitwa supply reduction kuhakikisha kwamba madawa hawa hayapatikani na hivyo kutokuwalazimu vijana wengi zaidi kuweza kuyatumia. Tume imefanya kazi kubwa mpaka hivi sasa na wameendelea kukamata na kuteketeza dawa nyingi na hivi sasa kuna upungufu mkubwa sana wa dawa za kulevya katika viunga vya miji yetu mingi ya Tanzania kutokana na kazi kubwa ambayo inafanywa na tume. MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Bulembo Halima. MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuku kwa kuniona. Kumekuwa na malalamiko mengi ya waathirika wa dawa za kulevya wanapokuwa rehab (rehabilitation) wanakaribia kupona wahusika wanawachoma tena dawa ya kulevya ili wasiweze kutoka na lengo limekuwa ili waendelee kujipatia fedha. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha rehab zao wenyewe ili kuweza kuwasaidia waathirka hawa dawa za kulevya? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, kwa kifupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia kubwa ya sober house zinamilikiwa na watu binafsi na hilo lililolalamikiwa na Mheshimiwa Mbunge hatujapata malalamiko rasmi. Hata hivyo niseme tu kwamba kwa kuzingati hizi sober house nyingi ziko chini ya watu binafsi tumeamua sasa kutengeneza miongozo ambayo itasaidia namna bora ya management ya hizi sober house ili inapotokea mazingira ya namna hiyo tuwe tuna sehemu ya kuweza kukabiliana nao, kwa sababu miongozo ile itakuwa inaeleza mtu ambaye ni muathirika wa madawa ya kulevya awe treated vipi. Mpango wa Serikali, katika swali lake, ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na sober house nyingi za Serikali ili kuondokana na changamo hii ambayo wananchi wengi wanaipata hasa kutokana na gharama kubwa ya kulipia katika hiyo sober house. MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa suala la madawa ya kulevya ni suala ambalo walinzi wake ni wananchi wote, hatuwezi kuiachia Mamlaka na Serikali peke yake. Mbunge, mwananchi unapouona kuna athari kama hiyo unatakiwa useme, utoe taarifa kwa mamlaka zinazohusika, Mheshimiwa Waziri Jenista. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Tumepokea hii taarifa sasa mara kadhaa na hata wakati wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Waheshimiwa Wabunge wametuarifu kwamba uko mchezo mbaya unaoendelea kwenye sober house; badala kuwasaidia vijana wetu wapone na waondoke ndani ya sober house, lakini taarifa ambazo tumekuwa tukizipokea ni kwamba wamiliki 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wa sober house wanataka kuendelea kuwaweka vijana wetu pale kwa faida binafsi. Naomba sasa nitoe tena agizo kwa wamiliki wa sober house wote ambao wana mchezo huo ambao umekuwa ukisemekana wauache haraka. Mheshimiwa Mwenyekiti, na ninatumia muda huu pia kuiagiza mamlaka sasa kuanza kufanya uchunguzi wa kina na atakaye bainika ana tabia hiyo aweze kuchukuliwa hatua haraka sana na hiyo itatusai kuwaokoa vijana wetu kutokuendea kutumia dawa za kulevya katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi) MWENYEKITI: ahsante, Waheshimiwa tunaendelea, Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha. Na. 136 Mafanikio ya Mradi wa MIVARF MHE. ASHA MSHIMBA JECHA aliuliza:- Mradi wa Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi Vijijini (MIVARF) katika Mkoa wetu wa Kusini Unguja umeweza kuwakomboa wananchi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na kuboresha mawasiliano ya barabara na kuweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi. Kwa kuwa mradi huu umeonesha mafanikio na wananchi wamehamasika. Je, Serikali ipo tayari kuwaongezea mitaji na mafunzo wananchi hao ili waweze kufikia malengo yao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni azma ya Serikali kuhakikisha inaunga mkono juhudi za wananchi kushiriki katika uchumi wa kilimo kwa kusaidia upatikanaji wa mitaji na kuwapatia mafunzo stahiki. Hatua za kuwawezesha wananchi wa Zanzibar kimtaji zilianza kwa kuvijengea uwezo wa kiutawala na kiutendaji Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) na vikundi vingine vya uzalishaji ili viweze kuratibu na kusimamia kwa ufanisi matumizi ya mitaji itakayopatikana kupitia mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, matayarisho yanaendelea ili kuvipatia vikundi vya wazalishaji ambavyo tayari vimehakikiwa na uwezo wao baada ya ziara ya uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutembelea Zanzibar mwezi
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages281 Page
-
File Size-