NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Nne - Tarehe 31 Januari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) Spika (Mhe.Job Y. Ndugai) Alikalia Kiti D U A Spika (Mhe.Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Nane, Kikao cha leo ni Kikao cha Nne. Katibu! NDG. LAWRENCE MAKIGI - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MHE. MIRAJI J. MTATURU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2019. SPIKA: Ahsante sana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Wenyeviti mnaowasilisha muwe mnakuwa karibu ili tuokoe muda na anayefuata awe karibu pia. Karibu sana Mwenyekiti kwa niaba ya! MHE. JULIUS K. LAIZER (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kanati kwa mwaka 2019. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Kalanga. Katibu! 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NDG.LAWRENCE MAKIGI - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Mhehsimiwa Waziri Mkuu, swali la kwanza litauliza na Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa, Senator, Mbunge wa Sumve Na. 37 Ujenzi wa Kiwanda cha Pamba-Kwimba MHE. RICHARD M. NDASSA aliuliza:- Kupitia Mifuko ya Jamii tayari tathmini ya kukijenga Kiwanda cha kuchambua pamba Nyambiti Ginnery kilichopo Kwimba umeshafanyika, kilichobaki ni uamuzi wa Serikali kuliongezea thamani zao la pamba. Je, ni lini Kiwanda hicho kitaanza kujengwa? SPIKA: Ahsante majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Wziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Anthony Mavunde tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri napenda kujibu swali la Mheshimiwa Richard Mganga Ndasa Mbunge wa Sumve kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini inayoundwa na Mifuko ya NSSF, PSSSF, NHIF, WCF na ZSSF imekamilisha mapitio mapya ya upembuzi yakinifu ya ufufuaji wa vinu vya kuchambulia pamba vya Ngasamo, Nyambiti na Kasamwa vilivyoko Mkoani Simiyu, Mwanza na Geita baada ya takwimu za uzalishaji wa kilimo cha pamba kuongezeka hususan katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa. Mheshimiwa Spika, kwa sasa Mifuko inakamilisha taratibu muhimu zinazohusiana na Miongozo ya Uwekezaji kwa kushirikiana na Vyama vya Ushirika vya Mwanza, Simiyu na Geita ili kuwezesha uwekezaji wenye ufanisi na tija taratibu zitakapokamilika. Mheshimiwa Spika, Utaratibu maalum wa namna ya kuwezesha ufufuaji wa viwanda hivyo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi Februari, 2020. SPIKA: Mhehsimiwa Ndassa. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba uniruhuru niipongeze sana Serikali kwa hatua ambayo sasa imefikia kwa sababu kilio kikubwa kwa wakulima wapamba ni kwamba pamba hiyo inatakiwa iongezewe thamani. Sasa swali langu nimesema kwamba upembuzi tayari umeshakamilisha na viongozi wakuu wa mifuko hii wako Mwanza nasikia, sasa ni lini sasa baada ya hiyo Februari kwa sababu majibu haya yanaweza kusema kwamba ni Februari kumbe ni mwezi mwingine, ni lini sasa hasa ujenzi wa vinu hivi vitatu kwa maana ya hii Nyambiti Ginnery, Ngasamo Ginnery pamoja Kasamwa Ginnery. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Lini vitaanza kujengwa ili zao la pamba lipate thamani zaidi? Nakushuru. SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri tafadhali, ni lini. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, niruhusu kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anawapigania wakulima wa pamba wa Kanda ya Ziwa na amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba zao hili linaongezwa thamani. Kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema leo wakurugenzi wote wa uwekezaji wa mifuko hii wako Mwanza na kesho kuna kikao cha Wakurugenzi Wakuu ambao kupitia kikao hicho tutapata way forward ya lini taratibu hizi zitaanza kwa sababu kesho wanakutaka kwa ajili ya mambo ya kitaalam, hivyo nimuombe Mheshimiwa Ndasa awe mvumilivu tusubiri taarifa ya Wakurugenzi Wakuu kesho ili tujue way forward ni nini. Nashukuru. SPIKA: Ahsante sana, tunaendelea wengine hamtoki kwenye pamba, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Sixtus Raphael Mapunda Mbinga Mjini Mariam ndiyo kwa niaba haya endelea. Na. 38 Kuboresha Huduma za Afya – Hospitali ya Mbinga MHE. MARIAM N. KISANGI (K.n.y. MHE. SIXTUS R. MAPUNDA) aliuliza:- Tangu mwaka 2016, Serikali iliahidi kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga ikiwa ni pamoja na kujenga wodi ya watoto, chumba cha upasuaji na gari la wagonjwa:- Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hizo. SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sixtus Raphael Mapunda, Mbunge wa Mbinga Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga ambapo kupitia mapato yake ya ndani Halmashauri ya Mji Mbinga imefanya ukarabati wa jengo la „Grade A‟ kwa gharama ya Shilingi milioni 45 na kununua jokofu la kuhifadhia maiti lenye thamani ya Shilingi milioni 29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetoa kiasi cha Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kalembo ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga, ahsante. SPIKA: Mheshimiwa Mariam Kisangi nilikuona. 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri, kwa kuwa Wilaya ya Mbinga ni Walaya ambao iko pembezoni sana na wananchi wake wnachangamoto nyingi sana pamoja na majibu mazuri bado kuna tatizo kubwa la kuwa gari la wagonjwa katika hospitali hiyo. Je, Serikali ina mkakati saa wa kuhakikisha wanawapelekea gari la wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga? Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa matatizo ya hospitali haya yanaendana kabisa na hali ya hospitali Zakiemu Mbagala. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongezea hospitali ya Zakiem Mbagala ambayo imezidiwa wagonjwa ni wengi lakini majengo ni machache na wahudumu ni wachache, nakushukuru. SPIKA: Majibu ya maswali hayo kwa kifupi Mheshimwia Naibu Waziri TAMISEMI tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kusimamia Mkoa wa Dar es Salama, pia ni Tanzania kwa ujumla wake hususan jambo la afya ya akinamama na watoto na wazee. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba unapokua unajenga kuboresha huduma za afya ni muhimu kuwa na gari la wagonjwa ili inapokea dharura iwe ni rahisi kumuwaisha katika huduma nyingine ya ziara ya pale alipokuwa, lakini naomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba kadri kwa uwezo wa Serikali uwezo ukipatikana basi eneo hilo la Mheshimiwa Raphaeri Mapunda litapata gari la wagonjwa kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameulizia hapa. Mheshimiwa Spika, naomba niseme tu kwamba mpango wa Serikali ni kuboresha huduma zaafya na kupeleka hufuma karibu na wananchi, tumepokea hoja Mheshimiwa Mbunge bahati nzuri tunaenda kwenye mwaka wa bajeti 2020/2021 basi tuangalie uwezekano wa kupatikana ili tuweze kupeleka fedha katika eneo hili kuboresha huduma ya pale Mbagala pia Mkoa wa Dar es Salam kwa ujumla wake. Na natambua kwamba wnanchi wangu wa Jimbo la Ukonga pia wanaweza wakapata huduma pale Mbagala Zakiemu, ahsante sana. SPIKA: Ahsante nilikuwa mnadhimu wa upinzani Bungeni uliza swali lako. MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza, wnanchi wa Jimbo la Bunda Mjini na Wilaya ya Bunda kwa ujumla walikubaliana kwamba hospitali ya Manyamanyama iwe hospitali ya Wilaya. Lakini kuna baadhi ya mambo ambayo hospitali hiyo haina pamoja jokofu la kuhifazia maiti. Wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini wanapata tabu kupeleka maiti Nyamswa Jimbo la Bunda. Sasa ningependa kujua ni lini Serikali itapeleka jokofu katika hospitali ya Manyamanyama? SPIKA: Ahsante sana swlai kutoka Mkoa wa Mara hilo, kuna baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Mara siwaoni oni hapa na sina taarifa zao kwa mfano Mheshimiwa Heche simuoni kabisa hapa sijui yuko wapi, Mheshimiwa Naibu jibu swali hilo la Manyamanyama. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli maneno yako yako ya utangulizi yanafaa sana ndiyo 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) maana tufanye mabadiliko makubwa katika eneo hili ikiwa na Wabunge wanaopatikana wakatI wote Bungeni kusemea watu wao kama Mheshimiwa Ester Bulaya. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwanza Bunge imepata Kituo cha Afya ni suala la kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli tumepata hospitali pale inajenga katika eneo hili lengo ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hii. Mheshimiwa sema Mheshimiwa hoja yako imepokelewa tuangalie uwezo wa Serikali tupeleke jokofu katika eneo hili ili maiti ikipatikana pale basi iweze kuhifadhimiwa eneo la karibu na kupunguza gharama zausafirishaji wa ndugu wa marehemu, ahsante sana. SPIKA: Ahsante sana kwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages166 Page
-
File Size-