1 Bunge La Tanzania
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Moja – Tarehe 14 Juni, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha kwa mwaka 2018/2019. Taarifa ya Mwaka ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 (The Annual Report of the Institute of Finance Management for the Financial Year 2015/2016). MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea, Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. RAMADHAN ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Maswali, swali letu la kwanza kwa siku ya leo linaulizwa na Mheshimiwa Omar Abdallah Kigoda, Mbunge wa Handeni na linaulizwa kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Kwa niaba yake, Mheshimiwa Shangazi. Na. 433 Tathmini Kuhusu 10% ya Wanawake na Vijana MHE. RASHID A. SHANGAZI (K.n.y. MHE. OMAR A. KIGODA) aliuliza:- Kumekuwa na utekelezaji hafifu wa kusaidia akinamama na vijana kutoka kwenye ile asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri:- Je, Serikali ina tathmini yoyote ya jinsi gani agizo hilo limetekelezwa kwa kila halmashauri? MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Kakunda. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omar Abdallah Kigoda, Mbunge wa Handeni, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hufanya ufuatiliaji na tathmini kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka kuhusu utekelezaji wa agizo la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 kwa ajili ya vikundi vya vijana na wanawake. Taarifa za 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ufuatiliaji na tathmini ndizo zimesaidia Serikali kubaini changamoto za usimamizi na uendeshaji unaotokana na upungufu wa kisheria, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanufaika wa mikopo kuwa wagumu kurejesha mikopo yao. Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Marekebisho ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 yatakayompa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa nguvu ya kutunga kanuni bora zaidi zitakazolazimisha halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mikopo ya akinamama na vijana, Serikali inaamini taratibu za utoaji wa mikopo hiyo, usimamizi na urejeshaji wake zitakuwa nzuri zaidi ukilinganisha na hali ilivyo sasa. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Shangazi. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Serikali, ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa, Serikali imenyang’anya vyanzo vya mapato vya halmashauri lakini pia imeshusha asilimia za mazao hasa ya kibiashara kutoka asilimia 5 mpaka 3, hivyo halmashauri nyingi kushindwa kutoa hii asilimia 10. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kusaidia kuongeza ruzuku katika eneo hili? Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa, zipo halmashauri ambazo zinategemea mazao ya kilimo pekee, kwa mfano Halmashauri ya Lushoto, Halmashauri ya Handeni na nyinginezo na zipo halmashauri ambazo zina rasilimali kama madini, hivyo mfuko huu unakuwa hauna ulingano kwa maana kwamba yapo maeneo ambayo wanapata mapato makubwa na mengine wanapata mapato kidogo sana. Hatuoni kwamba kwa kufanya hivi tunaleta misingi ya ubaguzi katika pato la Taifa? Ahsante. MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo, Mheshimiwa Kakunda. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Rashid Shangazi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza amesema kwamba, kuna baadhi ya vyanzo vya mapato halmashauri zimenyang’anywa. Nataka nimhakikishie kwamba, utaratibu wa Serikali ni mzuri. Katika baadhi ya vyanzo ambavyo vimechukuliwa, kwa mfano, vinavyokusanywa na TRA, bajeti ya halmashauri inakuwa iko palepale na baada ya ukusanyaji bajeti ambayo ilitengwa huwa inarudishwa kwa halmashauri. Kuhusu kwamba kwa nini tusiweke ruzuku maalum ili kufidia, nadhani ni wazo ambalo tunaweza tukalifanyia kazi kwa mwaka ujao wa fedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili kwamba baadhi ya halmashauri mapato ni kidogo ukilinganisha na halmashauri nyingine. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Shangazi na Waheshimiwa Wabunge kwamba katika ukokotoaji ambao tutaufanya hivi karibuni, kama sehemu ya kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kuziangalia hizi halmashauri zetu. Tutaangalia utaratibu ambao ni mzuri zaidi ili kusudi halmashauri ambazo zina uwezo mkubwa na halmashauri ambazo hazina uwezo kabisa tuangalie namna ya kutekeleza agizo hilo. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwakasaka, Mheshimiwa Zitto na Mheshimiwa Dkt. Chegeni. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu baadhi ya halmashauri kutoa mikopo hii ya vijana na akina mama kwa upendeleo. Serikali imewahi kulifanyia uchunguzi jambo hili na inasema nini kuhusu suala hili kama kweli lipo katika baadhi ya halmashauri? 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Jibu kwa swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Kakunda. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ngazi yetu sisi ya Wizara hivi karibuni hatujawahi kupokea malalamiko ambayo ni ya msingi kabisa kutoka katika halmashauri yoyote, kwamba kuna upendeleo katika utoaji wa mikopo. Kwa sababu utaratibu uliopo kila halmashauri inatakiwa iwe na Kamati ya Mikopo ambayo ndiyo hupitisha mikopo ile na miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya Mikopo ni Waheshimiwa Madiwani. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nijibu tu kwamba, kwa kweli utaratibu uliopo inawezekana kuna baadhi ya vikundi vikawa havijaguswa kwa mwaka ule husika kwa sababu fedha zenyewe zinakuwa hazitoshi, ni kidogo. Kwa mfano, unaweza ukawa na shilingi bilioni moja ukataka kutoa mikopo kwa vikundi 80 katika halmashauri, lakini halmashauri ina vikundi 600 kwa hiyo ni wazi kwamba kuna baadhi ya vikundi vitakosa. Kwa hiyo, jambo la msingi ambalo nataka nishauri halmashauri ni kwamba wasirudie kuvipa mikopo vikundi ambavyo vilipata mikopo mwaka jana na mwaka huu vikapata, bali vipate ambavyo mwaka jana havikupata. Huo ndiyo utaratibu mzuri zaidi na hiyo ni kupitia Kamati ya Mikopo ya Halmashauri. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Zitto. MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ilipitisha Sheria Ndogo ya Nyongeza ya Tozo mbalimbali katika Halmashauri na sheria ile ikasainiwa na Waziri mwenye dhamana wa TAMISEMI. Katika hali ya kushangaza, Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi alikuja Kigoma Machi, 2018 na 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kutangaza kwamba sheria ile isitekelezwe. Mpaka sasa watendaji wa halmashauri wanaogopa kukusanya ushuru kwa sababu ya agizo la Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi. Serikali inasema nini kuhusu jambo hili? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Kakunda, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ambazo tunazo katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI ni kwamba Baraza la Madiwani lilipitisha viwango vya tozo kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, hizo taarifa ndizo tulizonazo na hata Mkuu wa Wilaya ya Kigoma anazo taarifa hio na ametuarifu. Kwa hiyo, hizi taarifa ambazo Mheshimiwa Zitto amezileta ni mpya na yeye ni rafiki yangu, hajawahi hata kuja ofisini kuniambia. Kwa hiyo, tutafuatilia baada ya kuwa amezitoa hapa ili tuone zina ukweli kiasi gani. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Chegeni halafu Mheshimiwa Paresso. MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nami napenda tu kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa halmashauri nyingi kwa sasa hivi ziko taabani, kwa maana kwamba kimapato nyingi zinasuasua; na kwa kuwa Serikali imeendelea kuchukua baadhi ya vyanzo vingi vya halmashauri na hivyo kufanya halmashauri hizi kushindwa kufanya kazi na kutekeleza majukumu yake kama ilivyotakiwa. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri anaamini kwamba kwa mwenendo huu unazidi kuuwa ile dhana ya kugatua madaraka ya D-by-D? 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Kakunda. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Chegeni, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza jukumu la msingi kubwa la Serikali ni kusimamia maendeleo ya wananchi wake wote kwa usawa. Kuna baadhi ya halmashauri unaweza ukakuta katika maeneo yao kuna vyanzo ambavyo vinaweza vikawa vinawapatia mapato ambayo kimsingi