Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA TANO Kikao cha Tano – Tarehe 14 Novemba, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 54 Tatizo la Maji katika Mji wa Namanyere MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE (K.n.y. MHE. ALLY MOHAMED KEISSY) aliuliza:- Mji wa Namanyere ambao ni Makao Makuu ya Wilaya ya Nkasi una wakazi zaidi ya 15,000, Hospitali ya Wilaya, Chuo cha Manesi, Shule za Msingi Sita, Sekondari Tatu na Kituo cha Afya, lakini una uhaba mkubwa wa maji hasa ifikapo mwezi Julai hadi Novemba. Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo hilo ili kuwaondolewa kero hiyo wananchi wa Mji wa Namanyere? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA LA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mohamed Keissy, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mji wa Namanyere wenye wakazi zaidi ya 19,000 unapata maji chini ya asilimia 20 kutokana na ukosefu wa vyanzo vya maji vya uhakika. Mheshimiwa Spika, Serikali kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, alililotoa mwezi Oktoba, 2010 imefanya upembuzi yakinifu (Feasibility study) ili kubaini vyanzo vipya vya maji kwa ajili ya Mji wa Namanyere. Baada ya upembuzi yakinifu gharama zimekadiriwa kufikia bilioni 1.9. Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi katika bajeti ya mwaka 2011/2012 iliomba maombi maalum ili kupata fedha hizo kwa lengo la kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa huduma za maji. Fedha hizi hazikupatikana. Aidha, Halmashauri kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira imeidhinishiwa shilingi 600,000,000 kwa ajili ya miradi ya maji ya vijiji kumi (10). Mheshimiwa Spika, mipango ya Halmashauri ya kukabiliana na matatizo ya maji yaliyopo ni pamoja na kuandaa rasimu ya sheria ndogo ya uvunaji wa maji ya mvua ambayo mpaka sasa iko katika mchakato wa kukamilika, kuwekwa kwa sharti la kuhakikisha kila mchoro wa nyumba unakuwa na mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua ili upitishwe na mamlaka zinazohusika na kufanya tathimini ya kutumia nishati ya umeme wa jua kwa ajili ya kuendesha pampu za maji. Wananchi wa Mji wa Namanyere kwa sasa wanapata maji kutoka katika visima vinne vilivyochimbwa pamoja na bwawa la Msiri ambavyo ni vyanzo vinavyotumia pampu zinazohitaji nishati ya umeme. Halmashauri imenunua generator ili kuvuta maji kutoka katika visima hivyo kwenda wa wananchi. 1 MHE. ALLY MOHAMED KEISSY: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri nina maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mji wa Namanyere ni Mji unaokua siku hadi siku na wananchi wanapata tabu hata ya kujenga nyumba, maji ya kunywa na kila kitu hivyo visima vinne havitoshi kabisa na huwa vinaharibika mara kwa mara pampu zake. Watu wa Namanyere wanapata shida siku hadi siku yaani hata maji ya kunawa hakuna na hizo alizosema shilingi milioni 600,000,000 walizotenga zimeshindwa kukidhi. Wamechimba visima kule maji hakuna na hizo fedha hazijatumika hata senti tano. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka kusaidia wakazi wa Namanyere? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mohamed Keissy, kama ifuatavyo:- Kwanza nakubali kweli Mji wa Namanyere kutokana na ongezeko la watu mahitaji ya maji hayatoshi. Kitu kinachofanyika sasa hivi tumekasimu madaraka kwa Mamlaka ya Sumbawanga kufanya stadi tuweze kuona mahitaji, kuainisha vyanzo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Mji wa Namanyere na miji mingine kama Laila kwa miaka 20 ijayo kazi hiyo imeshaanza kuainishwa term of reference na tutaiingiza katika program ya maji awamu ya pili. MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo la Namanyere karibu linalingana na Mji Mdogo wa Mbalizi ambao una watu karibu 60,000 naomba kuuliza ni lini Mji huo utapewa maji ya uhakika kwa sababu mpaka sasa hivi kuna matatizo makubwa sana? Ahsante. (Makofi) NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwanjale kama ifuatavyo:- Kama nilivyojibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Keissy Miji Mikuu ya Wilaya na Miji Midogo yote tunaifanyia stadi ili tuweze kuainisha mahitaji ya maji kwa miaka 20 ijayo ndio kazi ambayo tunaifanya sasa. (Makofi) Na. 55 Ujenzi wa Miundombinu ya Maji MHE. TUNDU A. M. LISSU aliuliza:- Katika mwaka wa fedha wa 2010/2011 jumla ya shilingi 534,865,999/= zilitengwa kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji Halmashauri ya Wilaya ya Singida likiwemo Jimbo la Singida Mashariki, lakini fedha hizo zimetengwa wakati Wilaya mpya ya Ikungi yenye majimbo mawili ya Singida Mashariki na Singida Magharibi na Halmashauri havijaanzishwa rasmi:- (a) Je, kati ya fedha hizo ni kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya Wilaya mpya ya Ikungi hasa Jimbo la Singida Mashariki kwa kusudi hilo? (b)Je, ni Vijiji na Kata zipi za Jimbo la Singida Mashariki zitanufaika na ujenzi wa miundombinu ya maji iliyotengewa fedha hizo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA LA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika mwaka 2010/2011 ilitengewa shilingi 664,470,000 kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini kwa ajili ya 2 miradi ya maji katika vijiji 10. Kati ya fedha hizo kiasi kilichopokelewa ni shilinig 532,451,429 na zilizotumika ni shilingi 379,264,336. Fedha hizi zilitengwa kwa ajili ya miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na hakukuwa na bajeti kwa ajili ya Wilaya mpya ya Ikungi na Jimbo jipya la Singida Mashariki ambayo ilikuwa haijaanzishwa wakati huo. Wilaya mpya ikiwemo ya Ikungi zitaanza baada ya kukamilika kwa hatua za mwisho za utoaji maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kufuatia notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya iliyotolewa tarehe 9/9/2011. Aidha, Bajeti ya Halmashauri inayoandaliwa huzingatia vipaumbele vya miradi iliyopangwa kutekelezwa bila kujali iko katika Jimbo lipi la uchaguzi. (b) Mheshimiwa Spika, vijiji na Kata za Jimbo la Singida Mashariki zilizopata mgao wa bajeti hiyo kwa ajili ya miradi ya maji kwa mwaka 2010/2011 ni Kijiji cha Siuyu kilichopo katika Kata ya Siuyu na Kijiji cha Nkuhi kilichoko katika Kata ya Issuna. Kiasi cha fedha kilichotumika kwa ajili ya miradi katika Vijiji hivyo ni shilingi 84,503,200. Kati ya fedha hizo shilingi 33,484,000 zilitumika kwa ajili ya uchimbaji wa kisima kimoja (1) katika Kijiji cha Siuyu, utafiti wa maji ardhini, upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi na shilingi 51,019,200 zilitumika kwa ajili ya uchimbaji wa visima vitatu katika Kijiji cha Nkuhi, utafiti wa maji ardhini, upembezi yakinifu na usanifu wa mradi. MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika, naomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri, swali la nyongeza naomba Mheshimiwa Naibu Waziri aliambie Bunge lako Tukufu kama ana taarifa kwamba shilingi milioni 51,000,000 zinazodaiwa kutumika Kijiji cha Nkuhi hazijatumika, hakuna maji na matokeo yake imebidi Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo la Singida Mashariki utoe shilingi milioni 4 ili kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Nkuhi maji. Kama atakubali kwamba fedha hazijatumika naomba alieleze Bunge Tukufu ni hatua gani zitakazochukuliwa na Serikali ili kushughulikia hawa ambao wanapelekewa fedha kwa ajili ya maji ya wananchi halafu anazielekeza kwingine? (Makofi) SPIKA: Pamoja na kurudisha hela zako za jimbo. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA LA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tundu A. M. Lissu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, sina tatizo na anachosema Mheshimiwa Lissu, yeye kama amekwenda ametumia hela za constituency development catalyst fund kwa ajili ya shughuli za maji pale mimi sioni tatizo kabisa hela hizi zilikusudiwa kuchochea maendeleo ya wananchi pale walipo. Kwa hiyo, kama ametumia Mbunge ameonyesha tu busara yake kwamba mimi nafikiria ni priority area kuna tatizo akapeleka pale there is no problem. Anachokizungumza hapa anatuambia kwamba milioni 51,000,000 ana hakika kwamba hazikuelekezwa kule zilizokwenda. Na mimi nilipokuja hapa wala sijaja hapa kwamba nakuja hivi hapa nasikia usingizi kwa sababu ya kujiandaa kwa ajili ya kujibu swali hili. De-central contradiction iliyoko katika vijiji hivi anavyozungumza Mheshimiwa Tundu Lissu ni kwamba visima vimekwenda vimechimbwa lakini watu hawajaanza kupata maji. Kwa maana ya kwamba hawajapeleka katika simtanki na kuanza kusambaza na kupeleka. Wanacho kigezo walichokitumia hapa. Kuna kitu kinachoitwa counter part fund wakasema wale wananchi ambao wamejitoa wakatoa michango na wale ambao wamefanya kazi kwa mikono yao wanawapa kipaumbele namba moja. Asilimia inayotumika pale ni asilimia 5. asilimia 2.5 wananchi na 2.5 kutoka kwenye Halmashauri. Wakaenda wakachukua vijiji vyote pale Singida wakaviorodhesha. Hiki kijiji kinachosemwa ninacho hapa ninacho na Mheshimiwa Lissu akitaka tutakaa tutazungumza vizuri. 3 Wakasema hivi tunatoa kipaumbele kwa vile vijiji ambavyo vilionyesha nia ya kuchangia mpango huu. Vijiji hivi anavyovitaja hapa havikukidhi hiyo haja vikasukumwa mbele kwa ajili ya program inayokuja. Sasa mimi nataka niseme maneno yafuatayo: Ametaka kujua kwamba ni hatua gani zinazochukua? Mimi hapa nikimaliza natoka nje nazungumza na Mkurugenzi namwambia hivi taarifa mliyonipa Mbunge amekataa anasema kwamba milioni 51,000,000 hazikutumika hatuwezi tukakaa hapa ndani tukaambiwa milioni 51,000,000 hazikutumika,