Tarehe 23 Mei, 2016
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 23 Mei, 2016 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. CHARLES J. MLOKA – KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha mezani. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MWENYEKITI: Katibu! NDG. CHARLES J. MLOKA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaanza na maswali Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Richard Philip Mbogo Mbunge wa Nsimbo, sasa aulize swali lake. 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Na. 209 Uchaguzi wa Madiwani katika Kambi ya Katumba MHE. RICHARD P. MBOGO aliuliza: - Chaguzi za Madiwani zilifanyika katika kambi ya wakimbizi Katumba wa 2015:- Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili kukamilisha chaguzi za Serikali za Vijiji na Mtaa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Richard Philip Mbogo, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Katumba, Vijiji ambavyo havijafanya uchaguzi wa Vviongozi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2014 ni 14 na vitongoji 51. Uchaguzi ulishindwa kufanyika kwa sababu Kata hiyo ilikuwa ni kambi ya wakimbizi ambao walikuwa hawajapata uraia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria za nchi. Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Serikali kuwapa uraia wananchi wa maeneo hayo, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inaendelea na maandalizi ya kufanya uchaguzi mdogo katika vijiji na vitongoji hivyo na tayari katika bajeti ijayo ya mwaka 2016/2017 zimetengwa sh. 3,300,000 ili kuwezesha zoezi hilo. MWENYEKITI: Mheshimiwa Richard, swali la nyongeza. MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nifanye masahihisho kidogo ni Kata ya Katumba siyo Mtumba. Mheshimiwa Mwenyekiti, haya maeneo ambayo ilikuwa ni makazi ya wakimbizi yalikuwa yanapata ufadhili wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) katika huduma mbalimbali za jamii ikiwemo elimu, maji na barabara. Ningependa kujua Serikali ina mpango gani wa kuhusisha UNHCR kwa kuwa makambi yanaenda kuvunjwa, msaada gani ambao watautoa ili kuboresha miundombinu mbalimbali ambayo sasa hivi imekuwa ni hafifu? Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. 2 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema pale awali kwamba maeneo haya uchaguzi bado haujafanyika, japo uchaguzi haujafanyika jukumu kubwa la Serikali ni kuhakikisha katika maeneo hayo, wanaendelea kupata huduma za kijamii kwa ufanisi kama kawaida. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI jambo hilo tunaliangalia kwa karibu zaidi na kwa kuanza changamoto yetu kubwa ni kuisukuma bajeti hii ambayo sasa hivi imepitishwa kuhakikisha kwamba Halmashauri hii inafanya uchaguzi. Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo ni kuhakikisha kwamba, kwanza tunajua katika maeneo hayo huduma za kijamii nyingi zilikuwa zinatolewa na Shirika la Wakimbizi Duniani, sasa hivi ni jukumu la Serikali. Hili ni jukumu letu kubwa na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutapeana ushirikiano wa kutosha ili wananchi wa pale waweze kupata huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo miundombinu ya barabara, huduma ya elimu, huduma ya afya na ifike muda na wao wajione kwamba ni wananchi kama wananchi wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge pale, swali la nyongeza! MHE. MWANNE I. NCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naitwa Mwanne Ismail Nchemba. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, tatizo la Wakimbizi wa Katumba linafanana na tatizo la Wakimbizi wa Ulyankulu na kwa kuwa hawakufanya uchaguzi wa Madiwani. Je, Serikali inasema nini, ni lini utafanyika uchaguzi wa Madiwani katika Jimbo la Ulyankulu? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu hao ni wananchi wake, akiwa Mbunge wa Viti Maalum ana kila sababu ya kuona maeneo hayo yanafanyika uchaguzi. Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka swali hili nilijibu katika Mkutano wetu wa Bunge uliopita, nilisema pale kuna takribani Kata tatu uchaguzi haujafanyika kwa sababu za msingi, bado suala zima la utengamano linaendelea na pale sasa hivi bado Jeshi na Wizara ya Mambo ya Ndani wanaendelea kumiliki eneo lile. Utararibu utakapokamilika jukumu letu kubwa watu wa TAMISEMI baada ya ule mtangamano kuwa vizuri zaidi na eneo lile sasa rasmi likishakuwa chini ya TAMISEMI, mchakato wa uchaguzi sasa utaendelea ili watu wa pale wajikute 3 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) nao wana Serikali yao halali iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Namba 292. (Makofi) MWENYEKITI: Tunaendelea na swali la pili, Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Na. 210 Ukarabati wa Barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ni sehemu ya ghala la chakula la Taifa katika mikoa mitano (5) inayolima chakula kwa wingi nchini Tanzania; lakini kikwazo kikubwa ni usafirishaji wa mazao kufikia masoko ya nje ya Wilaya; Halmashauri imeomba ongezeko la bajeti ya barabara kufikia shilingi bilioni 7,969,000 ili kuweza kukarabati barabara zote muhimu na kuwezesha wakulima kusafirisha mazao yao kwa urahisi na hatimaye kuongeza kipato cha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe:- Je, Serikali ipo tayari kukubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe la kuongeza fedha katika bajeti ya 2016/2017? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe iliandaa makisio ya bajeti ya shilingi bilioni 7.9 kwa ajili ya matengenezo ya barabara katika bajeti ya mwaka 2016/2017. Hata hivyo, kutokana na ukomo wa bajeti, fedha zilizoidhinishwa ni shilingi milioni 920 ambazo zitatumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja. Katika mwaka wa fedha 2015/2016, Halmashauri hiyo ilitengewa shilingi milioni 870 na tayari Serikali imepeleka shilingi milioni 157.9. Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha za Mfuko wa Barabara katika bajeti ya mwaka 2016/2017 ni shilingi bilioni 247.5 ambazo endapo zingegawanywa sawa kwa kila Halmashauri zote 181 zilizopo, kila Halmashauri ingeweza kupata bajeti ya shilingi bilioni 1.3 tu. Hivyo, mara zote mahitaji yamekuwa ni makubwa kuliko uwezo wa rasilimali fedha kukidhi mahitaji hayo, ndiyo maana tunaweka vipaumbele ili kutekeleza mambo machache kwanza kulingana na uwezo 4 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) uliopo kibajeti. Serikali itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo utakavyowezekana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Sophia swali la nyongeza. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ahsante. Kwa kuwa Waziri amekiri kwamba bajeti iliyopita walitenga milioni 870, lakini ni milioni 157 tu ndiyo zimepelekwa. Je, haoni umuhimu wa kuhakikisha pesa iliyobaki inapelekwa. Swali la pili, kwa kuwa Halmashauri ya Rungwe imepata mafuriko na uharibifu wa barabara umekuwa mkubwa sana, naomba Wizara hii itutumie pesa za haraka kwa ajili ya emergency kwa ajili ya vijiji kama tisa zaidi ya kilometa 40; kama Kijiji cha Kyobo, Ikuti na sehemu za Lupepo. Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka pesa hizo haraka kwa ajili ya kusaidia barabara na madaraja yaliyoharibika? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika majibu yangu ya msingi nilisema bajeti ilikuwa ya shilingi milioni 870, zilizopelekwa mpaka sasa ni shilingi milioni 157, jibu hili nimekuwa nikilitoa kila mahali katika vipindi mbalimbali. Nilisema wazi, ukiachia changamoto ya ujenzi wa barabara, lakini kuna miradi mingi kipindi kilichopita ilikuwa haiendi vizuri. Nilitolea mifano miradi ya maji na miradi mingineyo kwamba upelekaji wa pesa ulikuwa ni tatizo kubwa sana, lakini kulikuwa na sababu zake za msingi. Katika mwaka uliopita pesa nyingi sana zilienda katika matukio makubwa ambayo yalikuwa yamejitokeza kama suala la uandikishaji na uchaguzi. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchakato wa hivi sasa, Serikali imejielekeza zaidi katika ukusanyaji wa mapato, ndiyo maana hivi sasa hata ukiangalia kwa mara ya kwanza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imevunja rekodi katika ukusanyaji wake wa mapato. Nilisema kwamba hata miradi iliyokuwepo mwanzo imesimama, lakini hivi karibuni miradi hiyo inapelekewa fedha. Mheshimiwa Mwenyekiti, nia yetu ni kwamba, katika kipindi hiki cha bajeti kilichobakia nina imani Serikali itajitahidi kupeleka fedha katika miradi yote iliyosimama nikijua wazi katika maeneo hayo mengine wakandarasi ambao ni wa ndani na wengine wa nje wanaendelea kudai. Kwa hiyo, suala hili tunaweka kipaumbele siyo kwa ajili ya maeneo hayo tu isipokuwa kwa Tanzania nzima kwa ujumla. 5 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mafuriko na kuharibu miundombinu ya barabara, hili nilisema ni kweli. mwaka huu ukiangalia maeneo mbalimbali tumekuwa na changamoto