Majadiliano Ya Bunge ______

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Majadiliano Ya Bunge ______ Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 5 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Randama za Makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Mwaka ya Utendaji kazi na Hesabu za Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 (The Annual Report of Activities and Accounts of Tanzania Education Authorities for the Financial Year 2009/2010). MASWALI NA MAJIBU Na. 175 Ubovu wa Barabara ya Mombasa – Kivule MHE. EUGEN E. MWAIPOSA aliuliza:- Barabara ya Mombasa – Mazizini – Kivule ni mbovu kwa kipindi kirefu sasa na imekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo licha ya kwamba Mheshimiwa Rais aliahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi mwaka 2010 kwamba barabara hiyo itajengwa:- (a) Je, ujenzi huo wa barabara utaanza na kukamilika lini? 1 (b) Je, Serikali itawalipa fidia wananchi waiojenga pembezoni mwa barabara ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo? NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU,TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, ELIMU alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Eugen Elishiringa Mwaiposa Mbunge wa Ukonga lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, barabara ya Mombasa – Mazizini – Kivule yenye urefu wa kilomita 6 ni mojawapo ya barabara muhimu inayohudumia idadi kubwa ya wakazi wa Kata ya Ukonga na Kivule. Mwishoni mwa mwezi wa Mei mwaka 2011, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilifanya matengenezo ya dharura kwa kuweka vifusi vya changarawe kwenye barabara hiyo kuanzia eneo la Mombasa hadi Moshi – bar urefu wa kilomita nne kwa gharama ya shilingi milioni 19.5 ili iweze kuhudumia vizuri wananchi wa eneo hilo. Aidha, katika mwaka wa fedha 2011/2012 Serikali kupitia wakala wa barabara(TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam imetenga jumla ya shilingi milioni 105 kwa ajili ya matengenezo ya maeneo korofi ya barabara hiyo. (b) Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais, Serikali kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeshafanya tathimini ya fidia kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara hiyo ambapo nyumba sabini na nne zilifanyiwa uthamini na gharama ya fidia hiyo kufikia shilingi bilioni 2,209,551,375. Aidha utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kwiango cha lami utafanyika mara fedha hizo zitakapopatikana. MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa barabara hiyo anayozungumzia Waziri na kiasi hicho cha shilingi milioni 105 zilikuwa zimetengwa kwa kipindi cha bajeti ya 2010/2011 na hazikuweza kutumika na zimepelekea sasa kupelekwa kwenye bajeti ya mwaka 2011/2012 uliotajwa hapa katika majibu yake. Je, Waziri anaweza au Serikali inaweza ikawaeleza wananchi wa Jimbo la Ukonga kwamba ni ka nini fedha hizo hazikuweza kutumika kwa kipindi hicho na jambo ambalo limepelekea sasa fedha hizo zipelekewe katika bajeti ya 2011/2012? NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana na Naibu Waziri, naomba niongezee tu kwa kusema Wizara ya Ujenzi nayo inachangia kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri katika kusimamia ukarabati wa barabara hii. Ningependa tu nimWeleze Mheshimiwa Mbunge kwamba pamoja na shilingi milioni 105 ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri amesema tumetenga kwa ajili ya 2 ukarabati katika mwaka wa fedha 2011/2012, Wizara ya Ujenzi kuanzia mwaka 2004 mpaka mwaka jana anaouzungumzia Mheshimiwa Mbunge, tumetumia zaidi ya shilingi nusu bilioni kwa ajili ya ukarabati ya barabara hii, kuchonga tuta, kuweka changarawe, kuweka makaravati (box caravats) na hata kuinua matuta. Na. 176 Upungufu wa Shule za A - Level Mbulu MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY aliuliza:- Sera ya Serikali ni kujenga shule za sekondari katika kila Kata au hata kila kijiji, sehemu kubwa ya shule hizo zimejengwa kwa nguvu za wananchi. Kuwepo kwa shule hizo katika kila kata kumeleta hitaji la kujenga shule za A – level zisizopungua sita katika kila Wilaya. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule za A – Level katika Wilaya na hasa Wilaya ya Mbulu ambayo pamoja na kuwa na shule za sekondari 33 ina shule moja tu ya A- Level? WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mustapha Boay Akunaay Mbunge wa Mbulu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, shule za sekondari za kidato cha tano na sita ni za kitaifa na hivyo ni lazima ziwe za bweni kwa kuwa zinadahili wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi isipokuwa shule chache za kutwa zilizopo katika maeneo ya miji. Mheshimiwa Spika, ili kutimiza adhima ya kuwa na shule za kidato cha tano na sita kwa kila tarafa Serikali kupitia mpango wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari Awamu ya II(MES) imelenga kujenga shule mpya na kupandisha hadhi shule zilizopo ili kupanua elimu katika ngazi hiyo. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Wilaya ya Mbulu ina shule za sekondari 32 za kidato cha kwanza hadi cha nne na shule moja tu ya kidato cha tano na sita na kwa kuwa azma ya Serikali ni kuwa na shule za aina hii kwa kila tarafa nashauri uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, ubiani shule zinazoweza kupandishwa hadhi kuwa za kidato cha tano na sita kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na Wizara yangu. Wizara yangu itakuwa tayari kutoa kibali cha kuanzisha mikondo ya kidato cha tano na sita kwa shule zitakazopendekezwa iwapo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswalimawili ya nyongeza. 3 (a) Kwa kuwa Wilaya ya Mbulu ina tarafa sita na kwa kuwa tayari katika hizo tarafa sita shule tano tayari zina bwalo na mabweni. Je,Serikali iko tayari katika mwaka huu wa fedha kutuma wataalamu wa kutazama kama vigezo hivyo tayari na kupanga bajeti ya chakula na kuleta walimu ili shule hizo zianze, angalau hata shule tatu? (b) Kwa kuwa hata hii shule moja iliyoko sasa hivi haina walimu hasa wa sayansi, Je katika mwezi huu wa Julai 2011, katika wanafunzi wanaotoka chuoni, Mheshimiwa Waziri, Serikali itapanga walimu wa kwenda kwenye shule hii ya Haidom? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mustapha Akunaay,Mbunge wa Mbulu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, suala la kupandisha hadhi ndani ya Halmashauri ya Mbulu, shule moja au mbili kuwa za A level ni suala la Halmashauri yenyewe, namshauri Mheshimiwa Mbunge wafanye mawasiliano na Ofisi ya Ugazuzi Kanda, pale kanda ya kaskazini ili waweze kutuma maafisa wakaguzi pale wakagague shule hizo, kama zitakidhi vigezo, Wizara yangu haina matatizo juu ya kutoa kibali kwa kuanzisha A leve, lakini vigezo vyenyewe ni pamoja na mabweni, kwa sababu kama nilivyosema kwamba shule hizi ni za Kitaifa lazima watoto watoke Mikoa yote ya Tanzania wafike pale, maana yake watakaa pale, watakula pale, watalala pale. Mheshimiwa Spika, kuhusu suala lingine la walimu wa A level katika shule ambayo iko moja pale Mbulu, namuakikishia tu Mbunge kwamba tayari mwezi huu wa Julai 2011, Wizara yangu inafanya utaratibu wa kuwapanga walimu kwenda kuripoti kwenye shule ambazo ziko mbali na maeneo hayo na walimu wataripoti na tayari programu za Wizara kwamba tuna vyuo vingi sana sasa hivi ambavyo vinatoa kada hii ya uwalimu, MUSE, DUSE, TEKU kama ni vyuo binafsi na vyuo vyote nchini vinatoa mafunzi haya ya uwalimu, kwa hiyo tutasambaza walimu kwenye shule za Mbule. MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize swali moja la nyongeza. Kwa sababu kwa harakaharaka uzoefu uliopo umeonyesha kwamba ongezeko hili la shule hasa za kidato cha tano na sita kwenye shule kwa ngazi ya tarafa, zina tatizo la kukosa wanafunzi kama ilivyojitokeza Wilaya ya Tandahimba ambayo tayari ilikuwa na shule, lakini ikakosa wanafunzi wa kuingia pale kuanza masomo ya kidato cha tano. Je, Serikali imejiandaa aje kuongeza ufaulu wa wanafunzi ili shule hizo zisikose wanafunzi na kuacha majengo tu yakiwa yao pale wakati nguvu ya wananchi imetumika? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mhehsimiwa Juma Njwayo, Mbunge wa Tandahimba kama ifuatavyo:- 4 Mheshimiwa Spika, suala la kukosa wanafunzi katika baadhi ya shule za A level na hasa limejitokeza sana katika mwaka huu (2011), hilo ni suala la ufaulu wa wanafunzi kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano. Sasa suala hili ni suala la kitaaluma ambavyo kama nilivyosema kwamba tamko litakuja hapa Bungeni juu ya ufaulu wa wanafunzi uliokuwa umetokea mwaka huu, lakini mambo mengi yaliyojitokeza huko ni pamoja na upungufu wa vitabu pamoja na walimu ambapo nimesema kwamba Serikali tayari ina juhudi za kusambaza walimu kwenye shule zetu za kata ili kuweza sasa kubaini tatizo ni nini. Lakini suala la ufaulu ni suala la baraza la mitihani, tuone na mwaka huu mambo yatakueje, lakini nawashauri Wabunge wote tuhamasishe vijana wetu wasome, wasichezecheze na wala wasiwe na mambo mengine ya mitahani. Wasiangalie mambo ya miziki na mambo mengine, wasome ili ufaulu uongezeke and then tutapata wanafunzi wengi sana wanaojiunga na A level. MHE. SAID J. NKUMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. nina swali dogo moja la nyongeza. Kwa kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imejitahidi sana ikishirikiana na wananchi kujenga kwa kiasi kikubwa sana kwa maeneo mengi sana hasa ya Katani shule hizi za sekondari za kata na kwa kuwa Serikali inaahidi hapa kwamba inapeleka kwa wingi sana sasa walimu katika shule hivi. Kikwazo kikubwa kimekuwa mazingira mazuri ya walimu hawa kuishi na hasa nyumba.
Recommended publications
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who Will Benefit from the Gas Economy, If It Happens?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013 Who will benefit from the gas economy, if it happens? Supported by: 2 TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? ACKNOWLEDGEMENTS Policy Forum would like to thank the Foundation for Civil Society for the generous grant that financed Tanzania Governance Review 2013. The review was drafted by Tanzania Development Research Group and edited by Policy Forum. The cartoons were drawn by Adam Lutta (Adamu). Tanzania Governance Reviews for 2006-7, 2008-9, 2010-11, 2012 and 2013 can be downloaded from the Policy Forum website. The views expressed and conclusions drawn on the basis of data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. TGRs review published and unpublished materials from official sources, civil society and academia, and from the media. Policy Forum has made every effort to verify the accuracy of the information contained in TGR2013, particularly with media sources. However, Policy Forum cannot guarantee the accuracy of all reported claims, statements, and statistics. Whereas any part of this review can be reproduced provided it is duly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. ISBN:978-9987-708-19-2 For more information and to order copies of the report please contact: Policy Forum P.O. Box 38486 Dar es Salaam Tel +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] Suggested citation: Policy Forum 2015.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 1 Julai, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 132 Kuimarisha Ulinzi na Usalama Jiji Dar es Salaam MHE. CHARLES N. KEENJA : Kwa kuwa, Serikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua madhubuti za kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye Jiji la Dar es Salaam kwa kuligawa Jiji kwenye Mikoa na Wilaya za Ki-ulinzi ; na kwa kuwa, hatua hiyo haikwenda sanjari na ile ya kuigawa Mikoa ya Kiutawala:- (a) Je, ni lini Serikali itachukua hatua za kuligawa eneo la Jiji la Dar es Salaam kwenye Mkoa/Wilaya zinazokwenda sanjari na zile za Ulinzi na Usalama ? (b) Je, Serikali haioni kwamba Viongozi kwenye eneo lenye hadhi zinazotofautiana kunaleta matatizo ya ushirikiano na mawasiliano hatimaye kukwamisha utendaji kazi ? (c) Kwa kuwa, zaidi ya 10% ya wananchi wa Tanzania wanaishi Dar es Salaam. Je, Serikali haioni kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuweka utaratibu mzuri zaidi wa Uongozi kwenye Jiji hilo ? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 1 Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Charles Keenja, Mbunge wa Ubungo, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa katika hatua za kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye Jiji la Dar es Salaam Serikali iliamua kuligawa eneo katika ngazi ya Mikoa ambapo Wilaya zote tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala ni Mikoa ya Kiulinzi na ngazi ya Mkoa kupewa hadhi ya Kanda Maalum ya Ulinzi na Usalama.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kwanza – Tarehe 27 Januari, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA Hapa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua TAARIFA YA SPIKA Waheshimiwa Wabunge katika mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge tulipitisha Miswada saba ya Sheria ya Serikali ifuatayo: The Contractors Registration Amendment Bill , 2008, The Unity Titles Bill 2008, The Mortgage Finance Special Provisions Bill 2008, The Height Skins Bill, 2008, The Animal Welfare Bill 2008, The workers Compensation Bill 2008 na The Mental Health Bill 2008. Baada ya kupitishwa na Bunge Miswada hiyo iliwasilishwa kwa Mheshimiwa Rais ili kama inavyohitaji Katiba yetu ipate kibali chake. Kwa taarifa hii nawaarifu Waheshimiwa Wabunge kwamba tayari Mheshimiwa Rais amekwishatoa kibali chake na sasa Miswada hiyo ni sheria za nchi na sasa inaitwa The Contractors Registration Amendment Act, 2008 Na. 15 ya mwaka 2008, The Unit Titles Act, 2008 Na. 16 ya 2008, The Mortgage Finance Special Provisions Act, 2008 Na. 17 ya mwaka 2008 The Height Skins and Leather Trade Act, 2008. Kwa hiyo, ni sheria Na. 18 ya Mwaka 2008. The Animal Welfare Act 2008 Sheria Na. 19 ya mwaka 2008 na The Mental Health Act 2008 Sheria Na. 21 ya mwaka 2008 huu ndiyo mwisho wa taarifa. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA):- Taarifa ya Matoleo yote ya Gazeti la Serikali pamoja na nyongeza zake zilizochapishwa tangu Kikao cha mwisho cha Mkutano wa Bunge uliopita.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 10 Februari, 2010 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE): Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Benki ya Posta Tanzania, kwa Mwaka 2008 [The Annual Report and Accounts of The Tanzania Postal Bank for the Year 2008]. The Mid-Term Review of the Monetary Policy Statement of The Bank of Tanzania for the Year 2009/2010. MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini juu ya Taarifa ya Serikali Kuhusu Ubinafsishwaji wa Mgodi wa Kiwira. Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Houston Texas - Marekani Mwaka 2006. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelzaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Uendeshaji Usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India. 1 Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Utendaji wa Kazi Usioridhisha wa Kampuni ya TICTS. MASWALI NA MAJIBU Na. 145 Usimamizi wa Ukaguzi wa Fedha za Halmashauri MHE. HERBERT J. MNTANGI aliuliza:- Kwa kuwa, kiasi cha fedha kinachopelekwa katika Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Jiji ni kikubwa na kinahitaji usimamizi wa ziada:- Kwa kuwa kitengo cha ukaguzi wa ndani kipo chini ya Mkurugenzi Mtendaji.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Sita – Tarehe 27 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo ni Kikao cha 36. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CATHERINE V. MAGIGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI) Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu utekelezaji na Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. TUNZA I. MALAPO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA MADINI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza Malapo, tunakushukuru. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Azza Hilal, Mbunge wa Viti Maalum - Shinyanga.
    [Show full text]
  • No. 63 MAY - AUGUST 1999
    No. 63 MAY - AUGUST 1999 UNDERMINING MULTI-PARTYISM WOMEN HAPPy WITH NEW LAND LEGISLATION CHARGES REVEALED IN ZANZIBAR TREASON TRIAL FOREIGN DEBTS - PROPSECTS FOR RELIEF DEATH OF SIR RICHARD TURNBULL EIGHT REVIEWS .. - .. MIXED REACTIONS TO NEW LAND LEGISLATION The endorsement of two important land bills by the National Assembly on 11 February has generated mixed reactions among commentators on land reform in Tanzania. Much to the delight of women Members of Parliament, the Land Bill and the Village Land Bill recognise equal access to land ownership and use by all citizens - men and women - and give them equal representation on land committees. The new legislation also prevents the ownership of land by foreigners, and recognises customary land tenure as equal to granted tenure. Other issues covered by the bills include leases, mortgages, co-occupancy and partition, and the solving of land disputes. 900 PAGES OF TEXT Several commentators took issue with the short time available for consultation and debate in Parliament of the nearly 900 pages of text contained in the bills. Now that they are endorsed, special pamphlets and periodicals are to be prepared and distributed in villages to ensure that people are conversant with the bills' contents. Land offices in the regions will be provided with essential equipment and facilities to prove quality of administration, and functionaries will attend training courses to sharpen their skills on handling land issues more effectively. Customary ownership of land among peasants and small livestock keepers is now legally safeguarded and recognised as of equal status with the granted right of occupancy. Livestock keepers will now be able to own pasture land either individually or in groups.
    [Show full text]
  • BDP Mps Refuse Pay
    The PatriotWARNING: on Sunday | www.thepatriot.co.bw Stay Home, | May Wash 03, 2020 hands with Soap & Water, Avoid crowds, Don’t Touch, Hug or KissNews 1 www.thepatriot.co.bw MAY 03, 2020 | ISSUE 372 P12.00 BDP MPs refuse pay cut COVID-19 • Tsogwane to approach MPs for salary cut • Backbenchers to reject Cabinet proposal confidentiality • ‘Cabinet donated their salaries voluntarily’ - BDP Whip Kablay BAKANG TIRO Chairman Slumber Tsogwane, who is “I haven’t received any official When reached for comment, BDP Letlhakeng-Lephephe MP said. critical [email protected] also the Vice President. It has always information with regards to us to Chief Whip Liakat Kablay who also Asked if they are to be forced to been believed that the backbenchers donate voluntarily take salary cut to forms part of the backbench, said contribute how he will respond, he ruling Botswana will easily accept a pay cut as donate to COVID-19 but if someone he is not aware of any information Kablay held that MPs have authority • Data censorship prevents stigmatisation Democratic Party (BDP) donation to the COVID-19 relief brings that up it will cause an uproar regarding MPs expected to take pay to decide what they do with their -Govt T backbench is refusing to take fund in solidarity with cabinet. within the party. As an MP I am also cuts. money. a pay cut as contribution to COVID- Sources indicated that most of affected economically,” said one BDP He said cabinet agreed on its He advised his colleagues that • Tough balancing exercise; patients’ 19 Relief Fund just weeks after the BDP backbench have found MP who preferred anonymity.
    [Show full text]
  • Tanzania Human Rights Report 2008
    Legal and Human Rights Centre Tanzania Human Rights Report 2008: Progress through Human Rights Funded By; Embassy of Finland Embassy of Norway Embassy of Sweden Ford Foundation Oxfam-Novib Trocaire Foundation for Civil Society i Tanzania Human Rights Report 2008 Editorial Board Francis Kiwanga (Adv.) Helen Kijo-Bisimba Prof. Chris Maina Peter Richard Shilamba Harold Sungusia Rodrick Maro Felista Mauya Researchers Godfrey Mpandikizi Stephen Axwesso Laetitia Petro Writers Clarence Kipobota Sarah Louw Publisher Legal and Human Rights Centre LHRC, April 2009 ISBN: 978-9987-432-74-5 ii Acknowledgements We would like to recognize the immense contribution of several individuals, institutions, governmental departments, and non-governmental organisations. The information they provided to us was invaluable to the preparation of this report. We are also grateful for the great work done by LHRC employees Laetitia Petro, Richard Shilamba, Godfrey Mpandikizi, Stephen Axwesso, Mashauri Jeremiah, Ally Mwashongo, Abuu Adballah and Charles Luther who facilitated the distribution, collection and analysis of information gathered from different areas of Tanzania. Our 131 field human rights monitors and paralegals also played an important role in preparing this report by providing us with current information about the human rights’ situation at the grass roots’ level. We greatly appreciate the assistance we received from the members of the editorial board, who are: Helen Kijo-Bisimba, Francis Kiwanga, Rodrick Maro, Felista Mauya, Professor Chris Maina Peter, and Harold Sungusia for their invaluable input on the content and form of this report. Their contributions helped us to create a better report. We would like to recognize the financial support we received from various partners to prepare and publish this report.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Hamsini na Mbili - Tarehe 22 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa masikitiko makubwa natoa taarifa kwamba Mheshimiwa Mussa Hamisi Silima, Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, jana Jumapili, tarehe 21 Agosti, 2011 majira ya jioni kama saa mbili kasorobo hivi walipokuwa wakirejea kutoka Dar es Salaam, yeye na familia yake walipata ajali mbaya sana katika eneo la Nzuguni, Mjini Dodoma. Katika ajali hiyo, mke wa Mbunge huyo aitwaye Mwanaheri Twalib amefariki dunia na mwili wa Marehemu upo hospitali ya Mkoa hapa Dodoma ukiandaliwa kupelekwa Zanzibar leo hii Jumatatu, tarehe 22 August, 2011 kwa mazishi yatanayotarajiwa kufanyanyika alasili ya leo. Kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge tusimame dakika chache tumkumbuke. (Heshima ya Marehemu, dakika moja) (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa dakika moja) Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, amina. Ahsanteni sana, tukae. Kwa hiyo sasa hivi tunavyoongea Mheshimiwa Mbunge ambae nae pia ameumia vibaya na dereva wake wanaondoka na ndege sasa hivi kusudi waweze kupata yanayohusika kule Dar es Salaam na pia kule watakuwa na watu wa kuwaangalia zaidi. Lakini walikwenda Zanzibar kumzika kaka yake na Marehemu huyu mama. Kwa hiyo, wamemzika marehemu basi wakawa wanawahi Bunge la leo ndiyo jana usiku wamepata ajali. Kwa hiyo, watakaokwenda kusindikiza msiba, ndege itaondoka kama saa tano watakwenda wafuatao, watakwenda Wabunge nane pamoja na mfawidhi zanzibar yeye anaongozana na mgonjwa sasa hivi lakini ataungana na wale kwenye mazishi.
    [Show full text]
  • Coversheet for Thesis in Sussex Research Online
    A University of Sussex DPhil thesis Available online via Sussex Research Online: http://sro.sussex.ac.uk/ This thesis is protected by copyright which belongs to the author. This thesis cannot be reproduced or quoted extensively from without first obtaining permission in writing from the Author The content must not be changed in any way or sold commercially in any format or medium without the formal permission of the Author When referring to this work, full bibliographic details including the author, title, awarding institution and date of the thesis must be given Please visit Sussex Research Online for more information and further details Accountability and Clientelism in Dominant Party Politics: The Case of a Constituency Development Fund in Tanzania Machiko Tsubura Submitted for the Degree of Doctor of Philosophy in Development Studies University of Sussex January 2014 - ii - I hereby declare that this thesis has not been and will not be submitted in whole or in part to another University for the award of any other degree. Signature: ……………………………………… - iii - UNIVERSITY OF SUSSEX MACHIKO TSUBURA DOCTOR OF PHILOSOPHY IN DEVELOPMENT STUDIES ACCOUNTABILITY AND CLIENTELISM IN DOMINANT PARTY POLITICS: THE CASE OF A CONSTITUENCY DEVELOPMENT FUND IN TANZANIA SUMMARY This thesis examines the shifting nature of accountability and clientelism in dominant party politics in Tanzania through the analysis of the introduction of a Constituency Development Fund (CDF) in 2009. A CDF is a distinctive mechanism that channels a specific portion of the government budget to the constituencies of Members of Parliament (MPs) to finance local small-scale development projects which are primarily selected by MPs.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 18 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita muuliza swali la kwanza nina matangazo kuhusu wageni, kwanza wale vijana wanafunzi kutoka shule ya sekondari, naona tangazo halisomeki vizuri, naomba tu wanafunzi na walimu msimame ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwatambua. Tunafurahi sana walimu na wanafunzi wa shule zetu za hapa nchini Tanzania mnapokuja hapa Bungeni kujionea wenyewe demokrasia ya nchi yetu inavyofanya kazi. Karibuni sana. Wapo Makatibu 26 wa UWT, ambao wamekuja kwenye Semina ya Utetezi na Ushawishi kwa Harakati za Wanawake inayofanyika Dodoma CCT wale pale mkono wangu wakulia karibuni sana kina mama tunawatakia mema katika semina yenu, ili ilete mafanikio na ipige hatua mbele katika kumkomboa mwanamke wa Tanzania, ahsanteni sana. Hawa ni wageni ambao tumetaarifiwa na Mheshimiwa Shamsa Selengia Mwangunga, Naibu Waziri wa Maji. Wageni wengine nitawatamka kadri nitakavyopata taarifa, kwa sababu wamechelewa kuleta taarifa. Na. 223 Barabara Toka KIA – Mererani MHE. DORA H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa, Mererani ni Controlled Area na ipo kwenye mpango wa Special Economic Zone na kwa kuwa Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani na inajulikana kote ulimwenguni kutokana na madini hayo, lakini barabara inayotoka KIA kwenda Mererani ni mbaya sana
    [Show full text]