Majadiliano Ya Bunge ______

Majadiliano Ya Bunge ______

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 5 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Randama za Makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Mwaka ya Utendaji kazi na Hesabu za Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 (The Annual Report of Activities and Accounts of Tanzania Education Authorities for the Financial Year 2009/2010). MASWALI NA MAJIBU Na. 175 Ubovu wa Barabara ya Mombasa – Kivule MHE. EUGEN E. MWAIPOSA aliuliza:- Barabara ya Mombasa – Mazizini – Kivule ni mbovu kwa kipindi kirefu sasa na imekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo licha ya kwamba Mheshimiwa Rais aliahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi mwaka 2010 kwamba barabara hiyo itajengwa:- (a) Je, ujenzi huo wa barabara utaanza na kukamilika lini? 1 (b) Je, Serikali itawalipa fidia wananchi waiojenga pembezoni mwa barabara ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo? NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU,TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, ELIMU alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Eugen Elishiringa Mwaiposa Mbunge wa Ukonga lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, barabara ya Mombasa – Mazizini – Kivule yenye urefu wa kilomita 6 ni mojawapo ya barabara muhimu inayohudumia idadi kubwa ya wakazi wa Kata ya Ukonga na Kivule. Mwishoni mwa mwezi wa Mei mwaka 2011, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilifanya matengenezo ya dharura kwa kuweka vifusi vya changarawe kwenye barabara hiyo kuanzia eneo la Mombasa hadi Moshi – bar urefu wa kilomita nne kwa gharama ya shilingi milioni 19.5 ili iweze kuhudumia vizuri wananchi wa eneo hilo. Aidha, katika mwaka wa fedha 2011/2012 Serikali kupitia wakala wa barabara(TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam imetenga jumla ya shilingi milioni 105 kwa ajili ya matengenezo ya maeneo korofi ya barabara hiyo. (b) Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais, Serikali kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeshafanya tathimini ya fidia kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara hiyo ambapo nyumba sabini na nne zilifanyiwa uthamini na gharama ya fidia hiyo kufikia shilingi bilioni 2,209,551,375. Aidha utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kwiango cha lami utafanyika mara fedha hizo zitakapopatikana. MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa barabara hiyo anayozungumzia Waziri na kiasi hicho cha shilingi milioni 105 zilikuwa zimetengwa kwa kipindi cha bajeti ya 2010/2011 na hazikuweza kutumika na zimepelekea sasa kupelekwa kwenye bajeti ya mwaka 2011/2012 uliotajwa hapa katika majibu yake. Je, Waziri anaweza au Serikali inaweza ikawaeleza wananchi wa Jimbo la Ukonga kwamba ni ka nini fedha hizo hazikuweza kutumika kwa kipindi hicho na jambo ambalo limepelekea sasa fedha hizo zipelekewe katika bajeti ya 2011/2012? NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana na Naibu Waziri, naomba niongezee tu kwa kusema Wizara ya Ujenzi nayo inachangia kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri katika kusimamia ukarabati wa barabara hii. Ningependa tu nimWeleze Mheshimiwa Mbunge kwamba pamoja na shilingi milioni 105 ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri amesema tumetenga kwa ajili ya 2 ukarabati katika mwaka wa fedha 2011/2012, Wizara ya Ujenzi kuanzia mwaka 2004 mpaka mwaka jana anaouzungumzia Mheshimiwa Mbunge, tumetumia zaidi ya shilingi nusu bilioni kwa ajili ya ukarabati ya barabara hii, kuchonga tuta, kuweka changarawe, kuweka makaravati (box caravats) na hata kuinua matuta. Na. 176 Upungufu wa Shule za A - Level Mbulu MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY aliuliza:- Sera ya Serikali ni kujenga shule za sekondari katika kila Kata au hata kila kijiji, sehemu kubwa ya shule hizo zimejengwa kwa nguvu za wananchi. Kuwepo kwa shule hizo katika kila kata kumeleta hitaji la kujenga shule za A – level zisizopungua sita katika kila Wilaya. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga shule za A – Level katika Wilaya na hasa Wilaya ya Mbulu ambayo pamoja na kuwa na shule za sekondari 33 ina shule moja tu ya A- Level? WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mustapha Boay Akunaay Mbunge wa Mbulu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, shule za sekondari za kidato cha tano na sita ni za kitaifa na hivyo ni lazima ziwe za bweni kwa kuwa zinadahili wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi isipokuwa shule chache za kutwa zilizopo katika maeneo ya miji. Mheshimiwa Spika, ili kutimiza adhima ya kuwa na shule za kidato cha tano na sita kwa kila tarafa Serikali kupitia mpango wa maendeleo ya Elimu ya Sekondari Awamu ya II(MES) imelenga kujenga shule mpya na kupandisha hadhi shule zilizopo ili kupanua elimu katika ngazi hiyo. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Wilaya ya Mbulu ina shule za sekondari 32 za kidato cha kwanza hadi cha nne na shule moja tu ya kidato cha tano na sita na kwa kuwa azma ya Serikali ni kuwa na shule za aina hii kwa kila tarafa nashauri uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, ubiani shule zinazoweza kupandishwa hadhi kuwa za kidato cha tano na sita kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na Wizara yangu. Wizara yangu itakuwa tayari kutoa kibali cha kuanzisha mikondo ya kidato cha tano na sita kwa shule zitakazopendekezwa iwapo zitakuwa zimekidhi vigezo vilivyowekwa. MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswalimawili ya nyongeza. 3 (a) Kwa kuwa Wilaya ya Mbulu ina tarafa sita na kwa kuwa tayari katika hizo tarafa sita shule tano tayari zina bwalo na mabweni. Je,Serikali iko tayari katika mwaka huu wa fedha kutuma wataalamu wa kutazama kama vigezo hivyo tayari na kupanga bajeti ya chakula na kuleta walimu ili shule hizo zianze, angalau hata shule tatu? (b) Kwa kuwa hata hii shule moja iliyoko sasa hivi haina walimu hasa wa sayansi, Je katika mwezi huu wa Julai 2011, katika wanafunzi wanaotoka chuoni, Mheshimiwa Waziri, Serikali itapanga walimu wa kwenda kwenye shule hii ya Haidom? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mustapha Akunaay,Mbunge wa Mbulu kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, suala la kupandisha hadhi ndani ya Halmashauri ya Mbulu, shule moja au mbili kuwa za A level ni suala la Halmashauri yenyewe, namshauri Mheshimiwa Mbunge wafanye mawasiliano na Ofisi ya Ugazuzi Kanda, pale kanda ya kaskazini ili waweze kutuma maafisa wakaguzi pale wakagague shule hizo, kama zitakidhi vigezo, Wizara yangu haina matatizo juu ya kutoa kibali kwa kuanzisha A leve, lakini vigezo vyenyewe ni pamoja na mabweni, kwa sababu kama nilivyosema kwamba shule hizi ni za Kitaifa lazima watoto watoke Mikoa yote ya Tanzania wafike pale, maana yake watakaa pale, watakula pale, watalala pale. Mheshimiwa Spika, kuhusu suala lingine la walimu wa A level katika shule ambayo iko moja pale Mbulu, namuakikishia tu Mbunge kwamba tayari mwezi huu wa Julai 2011, Wizara yangu inafanya utaratibu wa kuwapanga walimu kwenda kuripoti kwenye shule ambazo ziko mbali na maeneo hayo na walimu wataripoti na tayari programu za Wizara kwamba tuna vyuo vingi sana sasa hivi ambavyo vinatoa kada hii ya uwalimu, MUSE, DUSE, TEKU kama ni vyuo binafsi na vyuo vyote nchini vinatoa mafunzi haya ya uwalimu, kwa hiyo tutasambaza walimu kwenye shule za Mbule. MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize swali moja la nyongeza. Kwa sababu kwa harakaharaka uzoefu uliopo umeonyesha kwamba ongezeko hili la shule hasa za kidato cha tano na sita kwenye shule kwa ngazi ya tarafa, zina tatizo la kukosa wanafunzi kama ilivyojitokeza Wilaya ya Tandahimba ambayo tayari ilikuwa na shule, lakini ikakosa wanafunzi wa kuingia pale kuanza masomo ya kidato cha tano. Je, Serikali imejiandaa aje kuongeza ufaulu wa wanafunzi ili shule hizo zisikose wanafunzi na kuacha majengo tu yakiwa yao pale wakati nguvu ya wananchi imetumika? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mhehsimiwa Juma Njwayo, Mbunge wa Tandahimba kama ifuatavyo:- 4 Mheshimiwa Spika, suala la kukosa wanafunzi katika baadhi ya shule za A level na hasa limejitokeza sana katika mwaka huu (2011), hilo ni suala la ufaulu wa wanafunzi kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano. Sasa suala hili ni suala la kitaaluma ambavyo kama nilivyosema kwamba tamko litakuja hapa Bungeni juu ya ufaulu wa wanafunzi uliokuwa umetokea mwaka huu, lakini mambo mengi yaliyojitokeza huko ni pamoja na upungufu wa vitabu pamoja na walimu ambapo nimesema kwamba Serikali tayari ina juhudi za kusambaza walimu kwenye shule zetu za kata ili kuweza sasa kubaini tatizo ni nini. Lakini suala la ufaulu ni suala la baraza la mitihani, tuone na mwaka huu mambo yatakueje, lakini nawashauri Wabunge wote tuhamasishe vijana wetu wasome, wasichezecheze na wala wasiwe na mambo mengine ya mitahani. Wasiangalie mambo ya miziki na mambo mengine, wasome ili ufaulu uongezeke and then tutapata wanafunzi wengi sana wanaojiunga na A level. MHE. SAID J. NKUMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. nina swali dogo moja la nyongeza. Kwa kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imejitahidi sana ikishirikiana na wananchi kujenga kwa kiasi kikubwa sana kwa maeneo mengi sana hasa ya Katani shule hizi za sekondari za kata na kwa kuwa Serikali inaahidi hapa kwamba inapeleka kwa wingi sana sasa walimu katika shule hivi. Kikwazo kikubwa kimekuwa mazingira mazuri ya walimu hawa kuishi na hasa nyumba.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    191 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us