Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Hamsini na Mbili - Tarehe 22 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa masikitiko makubwa natoa taarifa kwamba Mheshimiwa Mussa Hamisi Silima, Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, jana Jumapili, tarehe 21 Agosti, 2011 majira ya jioni kama saa mbili kasorobo hivi walipokuwa wakirejea kutoka Dar es Salaam, yeye na familia yake walipata ajali mbaya sana katika eneo la Nzuguni, Mjini Dodoma. Katika ajali hiyo, mke wa Mbunge huyo aitwaye Mwanaheri Twalib amefariki dunia na mwili wa Marehemu upo hospitali ya Mkoa hapa Dodoma ukiandaliwa kupelekwa Zanzibar leo hii Jumatatu, tarehe 22 August, 2011 kwa mazishi yatanayotarajiwa kufanyanyika alasili ya leo. Kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge tusimame dakika chache tumkumbuke. (Heshima ya Marehemu, dakika moja) (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa dakika moja) Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, amina. Ahsanteni sana, tukae. Kwa hiyo sasa hivi tunavyoongea Mheshimiwa Mbunge ambae nae pia ameumia vibaya na dereva wake wanaondoka na ndege sasa hivi kusudi waweze kupata yanayohusika kule Dar es Salaam na pia kule watakuwa na watu wa kuwaangalia zaidi. Lakini walikwenda Zanzibar kumzika kaka yake na Marehemu huyu mama. Kwa hiyo, wamemzika marehemu basi wakawa wanawahi Bunge la leo ndiyo jana usiku wamepata ajali. Kwa hiyo, watakaokwenda kusindikiza msiba, ndege itaondoka kama saa tano watakwenda wafuatao, watakwenda Wabunge nane pamoja na mfawidhi zanzibar yeye anaongozana na mgonjwa sasa hivi lakini ataungana na wale kwenye mazishi. Kwa hiyo, atakwenda yupo Mbunge Mstaafu Juma Suleiman N’hunga, kwa sababu ni ndugu yake lakini pia anafahamu mazingira ya kule, lakini pia atakwenda Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha, Mheshimiwa Waridi Bakari Jabu, Mheshimiwa Mnadhi Juma Maalim, Mheshimiwa Juma Habib Mnyaa, Mheshimiwa Heri Khamis Ali, atakwenda na Mheshimiwa Zaynab Vulu na atakwenda na Mheshimiwa Rosweeter Kasikila. Hawa inabidi wajiandae ndege itakayochukua mwili wa Marehemu itaondoka kama saa tano. Kwa hiyo, wataondoka na ndege mpaka Zanzibar, maandalizi yote yanayotakiwa ya kiisalam yatafanyika hapa halafu yatamalizikia huko Zanzibar. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wale niliowataja basi wajiandae vizuri. Katibu. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatayo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Halmashauri ya Biashara ya Nje kwa Mwaka wa Fedha 2007/2008 [The Annual Report and Audited Accounts of the Board of External Trade (BET) for the Financial Year 2007/2008]. 1 Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Wakala wa Usajilio wa Biashara na Leseni kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009 [The Annual Report and Audited Accounts of Business Registration and Licensing Agency (BRELA) for the Financial Year 2008/2009]. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya maji kwa Mwaka wa Fedha, 2011/2012. MHE. NEEMA M. HAMID (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2010/2011 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA MAJI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Maji Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MWASWALI NA MAJIBU Na. 460 Ujenzi wa Barabara ya Bukoba Mjini hadi Rubafu MHE. PETER J. SERUKAMBA (K.n.y. MHE. JASSON S. RWEIKIZA) aliuliza:- Ujenzi wa barabara ya Bukoba Mjini hadi Rubafu (Bukoba Kabanga Bay km 42) kwa kiwango cha lami haujaanza licha ya mipango iliyopo na licha ya vituo vya ujenzi na makambi ya mkandarasi kukamilishwa. Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza na kukamilishwa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jasson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Bukoba Mjini, hadi Rubafu yenye urefu wa kilomita 42 ulianza mwezi Oktoba 2007 baada ya kupatikana kwa Mhandisi Mshauri (M/S ITECO Consults (T) Ltd). Ujenzi wa barabara hii utagharimu shilingi bilioni 45.6 na utafanyika kwa awamu tano hadi kukamilika kwake. Mkataba wa ujenzi ulisainiwa tarehe 19 Juni, 2008 kati ya Mkandarasi wa Kampuni ya Jessie and Company Ltd. Fedha zilizokwisha tolewa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi ni shilingi bilioni 1.4. Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya mwaka 2010/2011 mradi huu ulitengewa shilingi bilioni 1. Aidha katika Bajeti ya mwaka 2011/2012 zimetengwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu. Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii kutategemea upatikanaji wa fedha zinazotengwa katika Bajeti ya kila mwaka. MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majawabu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, Waziri anasema barabara hii kukamilika inahitaji bilioni 45 na tayari wameshasaini mkataba, huoni kwamba sasa kwa kutotenga fedha maana yake mwisho wa siku tutalipa pesa nyingi sana kama interest na idle time na mkandarasi kufanya kazi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Peter Serukamba kama ifuatavyo:- 2 Mheshimiwa Spika, anachosema Mheshimiwa Peter Serukamaba ni sahihi, najua yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ile Miundombinu analielewa hilli, hela hizi ambazo ziliombwa na mradi huu tunaouzungumzia hapa uko chini ya RAS Mkoa wa Kagera ni mradi wa huko nyuma nimeeleza hapa na shilingi bilioni 45.6 ndizo zinazohitajika ambacho tumezungumza nao, tumekubaliana, ukiacha mpango huu chini ya RAS, haitawezekana, mishahara pamoja na maendeleo na kila kitu wanapata bilioni 3.8 na hapa tunapozungumza bilino 1 waliyoomba hawakupata. Mheshimiwa Spika, wamepata milioni 250, tunachofanya sasa hivi na walichoshauri ni kwamba tunawasiliana na wale wadau wengine wote, Waziri wa Ujenzi ananisikia hapa, wa Uchukuzi ananisikia hapa na wale Mawaziri wengine wanahusika wa East African Community, wote hawa wametamkwa katika hili. Mpango tulionao ni kuzungumza na wadau hao ili kila mmoja achukue kipande chake tuweze kusaidia katika jambo hili ambalo ni muhimu sana kwa uchumi wan chi yetu. (Makofi) Na. 461 Ajira ya Watu Wenye Ulemavu MHE. REGIA E. MTEMA aliuliza:- Kwa muda mrefu sana jamii ya watu wenye ulemavu imekuwa nyuma katika kupata ajira na kuna walemavu wengi sana wenye fani mbalimbali lakini hawako kwenye soko la ajira yeyote. Je, Serikali ina mkakati gani mahsusi ya kukabiliana na changamoto hiyo? NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kazi na Ajira,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema, Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo: Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2008 na Shirika la Takwimu la Taifa NBS ni asilimia 3.1 ya watu wenye ulemavu nchini walio kwenye ajira za kipato na silimia 14.5 wapo kwenye ajira za kujiajiri wenyewe. Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa katika ajira ya kulipwa na kujiajiri kulingana na ujuzi na uwezo walio nao. Mikakati ya Serikali katika kukabiliana na changamoto za ajira kwa watu wenye ulemavu ni pamoja na ifuatayo:- (a) Bunge lako Tukufu imetunga Sheria ya watu wenye ulemavu namba 9 ya mwaka 2010. Ndani ya Sheria hii kifungu namba 31(2) kinamtaka kila mwajiri mwenye wafanyakazi kuanzia 20 na zaidi kuajiri watu wenye ulemavu wasiopungua asilimia tatu. (b) Serikali imeendelea kutoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia vyuo vya ufundi stadi mbalimbali. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita takribani watu wenye ulemavu 2,500(wanawake 980 na wanaume 1520) wamepata mafunzo ya kuwawezesha kuajiriwa na kuajiri. (c) Programu ya mafunzo ya kuwezesha wananchi kujiajiri kwa Wilaya za vijijini (Demand Driven Skills Development Programme) iliyotekelezwa katika Halmashauri za Wilaya nchini mwaka 2001/1002- 2009/2010 ilizingatia kuwapa pia fursa watu wenye ulemavu. (d) Kuwapa fursa wajasiriamali wadogo wenye ulemavu kushiriki kwenye maonyesho ya nguvu kazi/jua kali za nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki. 3 (e) Kushirikisha watu wenye ulemavu kupitia shirikisho la vyama vyao kwenye Kamati za Kukuza ajira za Mikoa na Wilaya wakiwa ni wajumbe watakao wakilisha kundi hili katika kamati husika. (f) Kuendelea kuhamasisha watu wenye ulemavu kujiunga kwenye vikundi vya kiuchumi na SACCOS ili kuweza kufaidika na huduma mbalimbali za kibiashara ikiwa ni pamoja na mafunzo na mikopo ya kuwawezesha kuanzisha na kuboresha miradi yao ya kiuchumi ya kujiajiri na kuajiri wengine. MHE. REGIA E. MTEMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo marefu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini kuna kipengele hayuko sahihi. Amesema kwamba sheria Na. 9 ya mwaka 2010 ya watu wenye ulemavu imeanza kutekelezwa si kweli, sheria hii bado haijaanza kutekelezwa kwa kuwa Kanuni ndogo za utekelezaji wa sheria hii bado haijatungwa mpaka sasa, ningependa alithibitishie Bunge hili je ni kweli sheria hii imeanza kutekelezwa? Bahati nzuri Mwanasheria yuko hapa. Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wao wana mwongozo wa huduma za watumishi wa Umma kwa watu wenye ulemavu ambayo inaelekeza