1 6 Juni, 2013 Bunge La Tanzania
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
6 JUNI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Arobaini na Nne - Tarehe 6 Juni, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM): Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka 2013/2014. MHE. SAID MUSSA ZUBEIR (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 6 JUNI, 2013 MHE. DAVID E. SILINDE (MSEMAJI MKUU WA UPINZANI KWA WIZARA YA FEDHA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na swali la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na atakayeuliza swali letu la kwanza ni Mheshimiwa Omar Rashid Nundu. Na. 351 Wananchi Kuuawa kwa Tuhuma za Wizi Mdogo Mdogo MHE. OMAR R. NUNDU aliuliza:- Kumezuka hulka mbaya kwa baadhi ya watu kuchukua sheria mkononi mwao kwa kuwaua wenzao kutokana na tuhuma za wizi mdogo mdogo kama wa simu za mkononi na kadhalika:- (a) Je, ni Wananchi wangapi wameuawa katika mazingira haya? (b) Je, Serikali inachukua hatua gani kukomesha vitendo hivyo? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Rashid Nundu, Mbunge wa Tanga Mjini, kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2012 hadi Aprili, 2013 jumla ya watu 1,666 waliuawa kwa kupigwa na Wananchi waliojichukulia Sheria mkononi. 2 6 JUNI, 2013 (b) Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imekuwa ikichukua hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa wote wanaohusika na matukio ya aina hiyo na kuwafikisha Mahakamani. Aidha, Jeshi la Polisi chini ya dhana ya utii wa sheria bila shuruti, hutoa mafunzo kupitia vyombo vya habari ili kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa kufuata Sheria, pia kuwashirikisha Viongozi wa Dini kuwataka waumini wao kuacha ukatili. Serikali inalaani vikali tabia ya Wananchi kujichukulia sheria mkononi na inawataka Wananchi kufuata sheria za nchi. MHE. OMAR R. NUNDU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya ufasaha lakini ya kusitusha kutokana na idadi kubwa ya watu ambao wameuwa kwa kipindi kifupi na ukichukulia kuwa uhai wa binadamu ni tuzo nadhimu ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia:- (i) Je, ni kesi ngapi za mauaji ya aina hii zimekwishatolewa hukumu na hukumu hizo ni za aina gani? (ii) Kwa kuwa Vituo vya Polisi vikiwa karibu na sehemu ambazo zimejificha husaidia kujua uhalifu unaotokea; na kwa kuwa kuna vitu vingi ambavyo vimejengwa kwa muda mrefu ambavyo mpaka leo havina Polisi kama kile ambacho kipo kwa Munduwangu, Kijiji cha Mwambani kule Tanga kilichojengwa takribani miaka mitano iliyopita na kinaota nyasi tu lakini hakuna polisi. Sasa ni hatua gani Serikali inachukua kuhakikisha kuwa Polisi wako karibu na sehemu ambayo matukio kama haya yanaweza kutokea ili kuyazuia? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwanza, kuhusu kesi ngapi. Kesi nyingi ambazo zimetokea katika suala hili bado ziko kwenye upelelezi, kwa sababu hii ni mob justice na siyo rahisi kupata msaada wa Wananchi katika kuwaonesha wahusika. 3 6 JUNI, 2013 Pamoja na hivyo, bado upelelezi unaendelea kwenye kesi nyingi za namna hii na nyingine zimefikia hatua karibu kuzipeleka mahakamani. Mheshimiwa Spika, la pili kuhusu vituo vya polisi; naomba niseme kwamba, Vituo vya Polisi kuwa kwenye maeneo mengi ni faida, lakini siyo Vituo vya Polisi ambavyo vitatufanya tusiuane kiholela. Hili ni suala la elimu, kuthamini maisha na kutaka kila mtu, kila raia, akubali kutii sheria bila shuruti, lakini pia kwa yule ambaye anamwona mwenzake bado analegalega, amsaidie kumuweka sawa. Mheshimiwa Spika, suala muhimu pamoja na Wananchi wenyewe kukataa kuuana, kuna doria ambazo tunazifanya katika maeneo mengi; hizi ndizo ambazo zinaweza zikasaidia kuliko kusema kila litakapotokea tukio pawe na kituo. Pamoja na hayo, vituo ambavyo vimeshajengwa na bado havijawekewa askari, hili tunalifanyia kazi lakini mara nyingi kuna standards au mambo ambayo yanakuwa hayajatimia, ndiyo maana inakuwa tabu kupeleka askari. Namwomba Mheshimiwa Mbunge, kama ana specific issue au kituo, tutalizungumza na tutalifanyia kazi kama tutakavyokubaliana. SPIKA: Ahsante. Sikuona wengine walioomba, tunaenda swali linalofuata; Mheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa! Na. 352 Raia wa Kigeni Kuhesabiwa na Kujipatia Vitambulisho vya Taifa MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA aliuliza:- Zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa linaendelea katika nchi yetu ambayo inazungukwa na nchi nyingine zenye migogoro:- 4 6 JUNI, 2013 (a) Je, raia wa nchi nyingine hawawezi kujipatia vitambulisho hivyo? (b) Je, zoezi la kuhesabu watu (sensa) halikuwagusa raia wa nchi nyingine? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa, Mbunge wa Gando, lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa nchi yetu imezungukwa na nchi zenye migogoro; hivyo, kutoa viashirio vya kuweza kuandikisha watu wasiostahili. Kwa kulitambua hilo, NIDA inaendesha zoezi hili kwa umakini na kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kama vile TAMISEMI, RITA na Uhamiaji ili kuthibitisha makazi ya mwombaji, kutambua umri wa mwombaji na kupata uthibitisho wa uraia wa mwombaji kabla ya kutoa kitambulisho. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa hatuandikishi watu wasiohusika, Serikali imepeleka Madaftari ya Wakazi yanayoratibiwa na Serikali za Mitaa, ambayo lengo lake kubwa ni kuandikisha wakazi wote wa kila kaya zilizo katika kijiji au shehia na kuzihifadhi taarifa hizo. Taarifa zilizoko kwenye Madaftari ya Wakazi ndizo zitakazotumika kumwandikisha mwombaji wa kitambulisho cha Taifa kama kigezo kikuu. Mheshimiwa Spika, baada ya kujaza fomu ya maombi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji au Shehia, ikijumuisha Wajumbe wa Vitongoji, itachambua maombi hayo na kubainisha watu ambao siyo Raia wa Tanzania. Hatua hii itazuia raia wa nchi nyingine kuweza kujipatia Vitambulisho vya Mtanzania. Mheshimiwa Spika, zoezi la kuhesabu watu lina lengo la kujua idadi ya watu waliopo nchini. Katika kutekeleza zoezi hilo, kila mtu anayehesabiwa hutakiwa kutoa taarifa 5 6 JUNI, 2013 ya uraia wake. Lengo la kufanya hivyo ni kuiwezesha Serikali kutambua nani ni raia na nani siyo raia. SPIKA: Mheshimiwa Khalifa swali la nyongeza, naomba kidogo msimame ninyi mlioomba. MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili madogo ya kumwuliza kama ifuatavyo:- (i) Sote tunaelewa kuwa zoezi la sensa lililopita, lilikumbwa na matatizo kiasi kwamba wako baadhi ya Watanzania wenzetu hawakutaka kujiandikisha au hawakuandikishwa na wao pia wanayo haki ya kupata vitambulisho. Katika mazingira hayo ambayo mtu hakuandikishwa kwenye sensa, lakini anataka kitambulisho cha Utanzania na anayo haki ya kupata; inakuwaje katika suala hilo? (ii) Kielelezo cha msingi cha mtu kuandikishwa kuwa raia au kupata haki za uraia ni cheti chenyewe cha kuzaliwa na tunaielewa nchi yetu kwa sasa kuwa mara nyingi fedha zinakufanya upate kitu hata kama siyo haki yako. Inapotokea watu wamepewa vyeti vya kuzaliwa kwa kununua halafu wakapewa Vitambulisho vya Taifa ambavyo vitawafanya wawe Watanzania wa kudumu. Katika mazingira hayo Serikali inatoa tamko gani na hivi vitu siyo vigeni kwa sababu kuna watu hivi sasa tunaelewa wapo Tanzania Bara lakini wanakuja Zanzibar wanapiga kura, wako watu wa nchi nyingine wanapiga kura hapa na tunajua hilo. Je, unatoa kauli gani? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khalifa kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, kulitokea matatizo katika uandikishaji wa watu kwenye sensa iliyopita, lakini naomba niseme kwamba, utaratibu wa kuandikisha 6 6 JUNI, 2013 na kutoa vitambulisho hauendani moja kwa moja na sensa iliyopita. Vina uhusiano, lakini usajili wa watu unafanywa kivyake na hilo ndiyo muhimu kwamba, madaftari tumeyatoa na watu wanafuatwa kwenye kaya zao kuandikishwa. Hapo ndipo ambapo mtu ambaye hakuandikisha anaweza akapata tatizo, lakini siyo lazima mtu aliyeandikishwa sensa ndiyo apate kitambulisho; hilo haliko sawa kwa sababu siku ya sensa wengine hawakulala nchini. Kwa hiyo, wote hao watapata vitambulisho ikiwa mchakato huu wa vitambulisho utafuatwa na kukamilika ilivyo. Mheshimiwa Spika, kuhusu vyeti vya kuzaliwa na uraia na Vitambulisho vya Kitaifa. Kama nilivyosema awali ni kwamba, nguvu kubwa ya kuamua na kuhakiki nani ni Mtanzania wa kuzaliwa ni kijijini alikotoka. Sasa nguvu tunaziweka huko ili ile Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji ndiyo ambayo inajua nani kamzaa nani na nani mjukuu wa nani. Kwa hiyo, kwa kutumia daftari ambalo tumelipeleka, tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi na kutaka kuilinda hii nchi, hakuna raia wa nje mwenye cheti atakayepata Kitambulisho cha Taifa. MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kwa kuwa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vipya limekuwa likiendelea lakini