MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao Cha Saba – Tarehe 11 Aprili

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao Cha Saba – Tarehe 11 Aprili NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Saba – Tarehe 11 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae, Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazi ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Repoti ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual General Report of the Controller and Audit General of the Financial Statement of Local Governments For the Year Ended 30th June, 2017). Taarifa ya Majibu ya Serikali na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi ya Hali ya Uharibifu wa Ardhi na Misitu (Study on the Status of Environment With the Focus on Land Degradation, Forest Degradation and Deforestation) Repoti ya Ukaguzi wa Ufanisi na Usimamizi wa Taka za Kielektroniki (Performance Audit Report on Electronic Waste Management) NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Repoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Taarifa za Fedha za Taasisi za Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual General Report of The Controller and Auditor General on Financial Statement of Central Government for the Year ended 30th June, 2017). Ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Mashirka ya Umma kwa Mwaka wa Fedha2016/2017 (The Annual General Report on The Financial Statements of Public Authorities for the Financial year 2016/2017). Ripoti ya Jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi na Ukaguzi Maalum kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2018 (The General Report of The Controller and Auditor General on Performance and Specialized Audit for The Period Ended 31st March, 2018). Ripoti ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual General Report of The Controller and Auditor General on The Financial Statements of Development Projects for The Year ended 30th June, 2017). 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mapendekezo yaliyotolewa mwaka 2014 (Follow up Report on The Implementation of The Controller and Auditor General’s Recommendations for The Six Performance Audit Report issued and tabled to Parliament on April, 2014). Ripoti ya Ukaguzi ya Ufanisi ya Maandalizi ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Performance Audit Report on Preparedness for Implementation of Sustainable Development Goals). Majibu ya hoja na mpango wa kutekeleza mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioshia tarehe 30 Juni, 2017 volume I and II (A na B). NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Ripoti ya Ukaguzi wa ufanisi ya Utoaji wa huduma za Kusaidia Viwanda Vidogo na vya Kati Nchini (Performance Audit Report on the Provision of Support Service for Small and Medium Enterprises) NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi ya Usimamizi wa Utoaji wa Huduma za Maji taka Maeneo ya Mijini (Performance Audit Report on Provision of Sewage Services in Urban areas) NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Urejeshaji wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Performance Audit Report on Management of Repayment and Recovery of Higher Education Student Loans?. NAIBU WAZIRI WA KILIMO: 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Ripoti ya Ukaguzi na Usimamizi wa Viuatilifu vya Kilimo (Performance Audit Report on The Management of Pesticides in Agriculture) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE K.n.y. WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI): Taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Ugawaji wa Viwanja (Performance Audit Report on The Management of Plots Allocation) NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (Performance Audit Report on Marine Protected Areas Management) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2018/2019. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI UMMA NA UTAWALA BORA: Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2018/2019. MHE. JASSON S. RWEIKIZA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI YA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Utekelezaji Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. JASSON S. RWEIKIZA-MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI YA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019. MWENYEKITI: Ahsante Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 54 Idadi ya Watu Wenye Ulemavu Nchini. MHE. KHADIJA NASSIR ALI aliuliza:- Tanzania ina idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali. Je, Serikali inajua idadi kamili ya watu wenye ulemavu na aina ya ulemavu waliokuwa nao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. STELLA I. ALEX) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khadija Nassir Ali, Mbunge wa viti maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2012 inaeleza kuwa, ulemavu ni hali inayotokana na 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) dosari ya kimwili au ya kiakili ambayo inampunguzia mtu uwezo na fursa sawa katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika jamii. Upungufu huo unaweza kuchochewa na mazingira na mtazamo wa jamii kuhusu ulemavu. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna aina mbalimbali za ulemavu ambao umegawanyika katika makundi yafuatayo:- Ulemavu wa viungo, wasioona, viziwi, wasioona, ulemavu wa akili, wenye ualbino, ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi, ulemavu wa matatizo ya afya ya akili, yaani walioupata ukubwani bada ya kuugua kwa muda mrefu pamoja na ulemavu wa ngozi yaani walioathirika na mabaka mabaka ya ngozi mwilini. Sababu za kiujumla ni pamoja na ukosefu wa chakula bora au lishe duni, magonjwa kama malaria, uti wa mgono na surua, ajali mbalimbali, urithi na hali ya mama yaani umri na hali ya afya. Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema maelezo hayo, naomba kujibu sasa swali la Mheshimiwa Khadija Nassir Ali kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na wingi huo wa aina za ulemavu, Sense ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 imejumuisha vipengele mahususi kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusu watu wenye ulemavu hivyo Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani watu 44,928,923 ambao sasa kwa hapo mgawanyo wake uko kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wenye ualbino ni 16,477,000 ambayo ni sawa na asilimia 0.04, wasiiona ni 848,530 sawa na asilimia 1.19, ulemavu wa uziwi ni 425,322 sawa na asilimia 0.97, viungo ni 525,019 sawa na asilimia 1.9, ulemavu wa kumbukumbu ni 401,931 ambayo ni sawa na asilimia 0.9, ulemavu wa kushindwa kujihudumia ni 324,725 sawa na asilimia 0.74, na ulemavu mwingine yaani kwa ujumla wake ni 99,798 ambao ni sawa na asilimia 0.23. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Khadija Nassir una swali la nyongeza? MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa takwimu hizo zinatokana na sensa ya mwaka 2012 na Tanzania sasa inakadiriwa kuwa na watu wasiopungua milioni 50, hii inaonesha wazi kwamba Serikali haina takwimu sahihi kwa sasa. Swali langu la kwanza, Serikali haioni kwamba kukosekana kwa takwimu sahihi kunapelekea kushindwa kuwapatia mahitaji yao ipasavyo? Swali langu namba mbili, je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kufanya takwimu ili kuweza kupata idadi kamili ya watu wenye ulemavu? Ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwa ufupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. STELLA I. ALEX): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana mdogo wangu kwa ajinsi ambavyo anafuatilia masuala ya watu wenye ulemavu, lakini pia na yeye ni mdogo wetu yaani mdogo wa watu wote wenye ulemavu kwa sababu dada yake ni kiziwi. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa takwimu kwa watu wenye ulemavu, na sambamba na hilo kama tunavyofahamu, sensa inafanyika kila bada ya miaka 10 ambapo kutokana na kwamba ilifanyika mwaka 2012 kwa hiyo tunategemea sensa nyingine ifanyike mwaka 2022; lakini kwa sababu ya umuhimu wa jambo hili yaani takwimu kwa watu wenye ulemavu tayari Serikali imeshaanza kufanya mazungumzo na kuangalia ni jinsi sasa 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tunaweza kupata takwimu hizi kabla ya wakati huo.
Recommended publications
  • Tarehe 30 Machi, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kwanza – Tarehe 30 Machi, 2021 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA NA WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (Hapa Kwaya ya Bunge iliimba Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nitaleta kwenu Taarifa ya Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai. Waheshimiwa Wabunge, kama ambavyo wote tunafahamu aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi, 2021 katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Waheshimiwa Wabunge, kufuatia msiba huo wananchi wa Tanzania walipata fursa ya kutoa heshima za mwisho kama ifuatavyo; tarehe 20 hadi 21 Machi, 2021 Mkoani Dar es Salaam, tarehe 22 Machi, 2021 Mkoani Dodoma ambapo pia ilifanyika hafla ya kitaifa. Tarehe 23 Machi, 2021 ilikuwa Zanzibar na tarehe 24 Machi, 2021 ilikuwa mkoani Mwanza. Waheshimiwa Wabunge, nazisikia kelele sina hakika kama wote tuko pamoja kwenye jambo hili zito lililolipata Taifa letu. Tarehe 25 hadi 26 mkoani Geita na Chato. Waheshimiwa Wabunge, mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli yalifanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Machi, 2021 nyumbani kwake Chato, Mkoani Geita. Waheshimiwa Wabunge, kwa kuwa leo ni siku ya kwanza kwa Bunge hili kukutana tangu ulipotokea msiba huo naomba Waheshimiwa Wabunge tusimame kwa dakika moja ili kumkumbuka mpendwa wetu.
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 30 Machi, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali leo tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza, atauliza swali la kwanza. Na. 117 Mwakilishi wa Wazee katika Vyombo vya Maamuzi MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Kwa muda mrefu wazee wa nchi hii wamekuwa wakililia uwakilishi katika vyombo mbalimbali vya maamuzi kama vile Bunge, Halmashauri, Vijiji na kadhalika kama ilivyo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili sauti zao zisikike:- Je, ni lini Serikali itasikia kilio cha wazee hawa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Utaratibu wa kupata wawakilishi katika vyombo vya maamuzi kama vile Bunge, umeelezwa katika Ibara ya 66 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara hii imefafanua aina za Wabunge na namna ya kuwapata. Utaratibu wa kuwapata wawakilishi katika Halmashauri umeelezwa 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) katika Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 yaani The Local Authority Election Act, Cap. 292. Aidha, utaratibu wa kuwapata wawakilishi katika vijiji hutawaliwa na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 287 na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 288. Mheshimiwa Spika, wawakilishi wanaowakilisha makundi mbalimbali katika Bunge, Halmashauri na Vijiji, kwa mfano, wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na kadhalika, wamekuwa wakipatikana kupitia mapendekezo yanayowasilishwa na vyama vya siasa kwenye vyombo vinavyosimamia uchaguzi katika ngazi hizo.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 10 Februari, 2010 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE): Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Benki ya Posta Tanzania, kwa Mwaka 2008 [The Annual Report and Accounts of The Tanzania Postal Bank for the Year 2008]. The Mid-Term Review of the Monetary Policy Statement of The Bank of Tanzania for the Year 2009/2010. MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini juu ya Taarifa ya Serikali Kuhusu Ubinafsishwaji wa Mgodi wa Kiwira. Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Houston Texas - Marekani Mwaka 2006. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelzaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Uendeshaji Usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India. 1 Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Utendaji wa Kazi Usioridhisha wa Kampuni ya TICTS. MASWALI NA MAJIBU Na. 145 Usimamizi wa Ukaguzi wa Fedha za Halmashauri MHE. HERBERT J. MNTANGI aliuliza:- Kwa kuwa, kiasi cha fedha kinachopelekwa katika Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Jiji ni kikubwa na kinahitaji usimamizi wa ziada:- Kwa kuwa kitengo cha ukaguzi wa ndani kipo chini ya Mkurugenzi Mtendaji.
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania Mkutano Wa Tatu Yatokanayo Na Kikao Cha Arobaini Na Saba 21 Juni, 2016
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA TATU YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA 21 JUNI, 2016 MKUTANO WA TATU - YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA TAREHE 21 JUNI, 2016 I. DUA: Saa 3.00 Asubuhi Naibu Spika (Mhe. Dkt.Tulia Ackson) alisoma Dua na Kuongoza Bunge. Makatibu Mezani: 1. Ndg. Theonest Ruhilabake 2. Ndg. Zainab Issa Wabunge wa Kambi ya Upinzani walitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya dua kusomwa na Mhe. Naibu Spika. II. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali:- OFISI YA WAZIRI MKUU: Swali Na.399 – Mhe. Raphael Masunga Chegeni [kny. Mhe. Salome Makamba] Swali la nyongeza: (i) Mhe. Raphael Masunga Chegeni (ii) Mhe. Abdallah Hamisi Ulega (iii) Mhe. Joseph Kasheku Musukuma (iv) Mhe. Mariam Nassoro Kisangi OFISI YA RAIS (TAMISEMI): Swali Na.400 Mhe. Oran Manase Njeza Swali la nyongeza: (i) Mhe. Oran Manase Njeza (ii) Mhe. Desderius John Mipata (iii) Mhe. Goodluck Asaph Mlinga Swali Na.401 – Mhe. Boniventura Destery Kiswaga Swali la nyongeza: (i) Mhe. Boniventura Destery Kiswaga (ii) Mhe. Augustino Manyanda Maselle (iii) Mhe. Richard Mganga Ndassa (iv) Mhe. Dkt. Dalali Peter Kafumu Swali Na. 402 – Mhe. Fredy Atupele Mwakibete Swali la Nyongeza: (i) Mhe. Fredy Atupele Mwakibete (ii) Mhe. Njalu Daudi Silanga (iii) Mhe. Halima Abdallah Bulembo (iv) Mhe. Azza Hilal Hamad 2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Swali Na.403 – Mhe Joseph Kakunda. kny Mhe. Ally Saleh Ally Swali la nyongeza: (i) Mhe. Joseph George Kakunda (ii) Mhe. Mussa Azzan Zungu (iii) Mhe. Cosato David Chumi (iv) Mhe.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 22 Juni, 2021 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Hamsini na Sita na kabla hatujaendelea nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wasaidizi wangu wote wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa David Kihenzile, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Najma kwa kazi nzuri ambayo wameifanya wiki nzima kutuendeshea mjadala wetu wa bajeti. (Makofi) Sasa leo hapa ndio siku ya maamuzi ambayo kila Mbunge anapaswa kuwa humu ndani, kwa Mbunge ambaye Spika hana taarifa yake na hatapiga kura hapa leo hilo la kwake yeye. (Makofi) Katibu. NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali na tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 465 Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri Katika Mji wa Laela MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Sumbawanga katika Mji wa Laela baada ya agizo la Serikali la kuhamisha Makao Makuu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu la watu wa Kwela, Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 30 zilizohamia kwenye maeneo mapya ya utawala mwaka 2019.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Kumi Na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, sasa aulize swali lake. Na. 158 Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Zahanati – Busega MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Imalamate Wilayani Busega wamejenga zahanati na kumaliza maboma manne kwa maana ya zahanati moja kila kijiji:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi hao kuezeka maboma hayo ili waweze kupata huduma za afya kwenye zahanati hizo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • AUDITED FINANCIAL STATEMENTS for the YEAR ENDED 30Th JUNE 2017
    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRIME MINISTER’S OFFICE DRUG CONTROL AND ENFORCEMENT AUTHORITY (VOTE 091) AUDITED FINANCIAL STATEMENTS FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2017 AUDITED FINANCIAL STATEMENTS 1 FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2017 Drug Satchets VISION To have a society with zero tolerance on drug abuse and trafficking. MISSION To protect the well-being of Tanzanians against drug and related effects by defining, promoting and coordinating the Policy of the Government of the URT for the control of drug abuse and illicit trafficking. CORE VALUES In order to achieve the above Vision and Mission, the Authority has put forward core values, which are reliability, cooperation, accountability, innovativeness, professionalism, confidentiality, efficiency and effectiveness. Heroin Cocain Cannabis Miraa Precursor Chemicals AUDITED FINANCIAL STATEMENTS i FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2017 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRIME MINISTER’S OFFICE DRUG CONTROL AND ENFORCEMENT AUTHORITY (VOTE 091) TABLE OF CONTENTS List of Acronyms ......................................................................................................................iii General Information .................................................................................................................iv Statement from the Honorable Minister for State, Prime Minister’s Office; Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment, Youth and the Disabled ..........................1 Statement by the Accounting Officer .......................................................................................3
    [Show full text]
  • Tarehe 3 Februari, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Pili – Tarehe 3 Februari, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Tukae. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na maswali Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, sasa aulize swali lake. Na. 16 Ujenzi wa Barabara za Lami - Mji wa Mafinga MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza Ujenzi wa Barabara za lami na kufunga taa za barabarani katika Mji wa Mafinga chini ya Mpango wa Uendelezaji Miji nchini? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu, kwanza naomba nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenijalia mimi na Waheshimiwa Wabunge wote afya njema na kutuwezesha kuwa wawakilishi wa wananchi kupitia Bunge lako Tukufu. Mheshimiwa Naibu Spika, pili, naomba nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani kubwa aliyonipa kwa kuniteua kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, nawashukuru sana wananchi wa Jimbo la Wanging’ombe kwa kunichagua na kuchagua mafiga
    [Show full text]
  • MKUTANO WA 18 TAREHE 3 FEBRUARI, 2015 MREMA 1.Pmd
    3 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Saba - Tarehe 3 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- SPIKA: Hati za kuwasilisha mezani, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama au kwa niaba yake Mheshimiwa Capt. John Chiligati. MHE. CAPT. JOHN Z. CHILIGATI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Katika Kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. MHE. SELEMANI S. JAFO (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA): Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Katika kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. 1 3 FEBRUARI, 2015 MHE. DUNSTAN L. KITANDULA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara Katika Kipindi cha Januari, 2014 hadi Januari, 2015. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tumeletewa taarifa kwamba kwa sababu mgeni tulionao ndani ya nchi hii Rais wa Ujerumani vipindi vya TBC asubuhi hii vitakuwa kwenye TBC 2 na siyo TBC1, kwa sababu kule kuna mapokezi huko uwanja wa Taifa kule. Kwa hiyo, tutarudia tena baada ya mapokezi hayo kumalizika. Lakini pia jioni kwa sababu kutakuwa na dhifa ya kitaifa, pia matangazo hayatakuwa kwenye TBC1 na siyo vinginevyo.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 18 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita muuliza swali la kwanza nina matangazo kuhusu wageni, kwanza wale vijana wanafunzi kutoka shule ya sekondari, naona tangazo halisomeki vizuri, naomba tu wanafunzi na walimu msimame ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwatambua. Tunafurahi sana walimu na wanafunzi wa shule zetu za hapa nchini Tanzania mnapokuja hapa Bungeni kujionea wenyewe demokrasia ya nchi yetu inavyofanya kazi. Karibuni sana. Wapo Makatibu 26 wa UWT, ambao wamekuja kwenye Semina ya Utetezi na Ushawishi kwa Harakati za Wanawake inayofanyika Dodoma CCT wale pale mkono wangu wakulia karibuni sana kina mama tunawatakia mema katika semina yenu, ili ilete mafanikio na ipige hatua mbele katika kumkomboa mwanamke wa Tanzania, ahsanteni sana. Hawa ni wageni ambao tumetaarifiwa na Mheshimiwa Shamsa Selengia Mwangunga, Naibu Waziri wa Maji. Wageni wengine nitawatamka kadri nitakavyopata taarifa, kwa sababu wamechelewa kuleta taarifa. Na. 223 Barabara Toka KIA – Mererani MHE. DORA H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa, Mererani ni Controlled Area na ipo kwenye mpango wa Special Economic Zone na kwa kuwa Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani na inajulikana kote ulimwenguni kutokana na madini hayo, lakini barabara inayotoka KIA kwenda Mererani ni mbaya sana
    [Show full text]
  • THRDC's Report on the Situation of Human Rights Defenders in Tanzania
    THE 2018 REPORT ON THE SITUATION OF HUMAN RIGHTS DEFENDERS AND CIVIC SPACE IN TANZANIA RESEARCHERS ADVOCATES JONES SENDODO, DEOGRATIAS BWIRE, LEOPOLD MOSHA WRITERS ADVOCATES JONES SENDODO, DEOGRATIAS BWIRE, LEOPOLD MOSHA EDITORS PILI MTAMBALIKE ONESMO OLENGURUMWA The 2018 Report on the Situation of Human Rights Tanzania Human Rights Defenders Coalition Defenders and Civic Space in Tanzania ii [THRDC] Table of Contents ABREVIATIONS vi LIST OF STATUTES AND INTERNATIONAL INSTRUMENTS vii ACKNOWLEDGMENT ix PREFACE x VISION, MISSION, VALUES xi THE OVERAL GOAL OF THE THRDC xii EXECUTIVE SUMMARY xiii Chapter One 1 GENERAL INTRODUCTION 1 1.0 Introduction 1 1.1 Protection Mechanisms for Human Rights Defenders 3 1.1.1 Legal Protection Mechanism at International Level 4 1.1.2 Legal Protection Mechanism at Regional Level 7 1.1.3 Legal Protection Mechanism at the National Level 11 1.1.4 Challenges with Both International and Regional Protection Mechanisms for HRDS 13 1.2 Non Legal Protection mechanism 13 1.2.1 Non Legal Protection mechanism at International level 14 1.2.2 Non Legal Protection Mechanism at Regional level 15 1.2.3 Protection Mechanism at National Level 16 Chapter Two 20 VIOLATIONS COMMITTED AGAINST HUMAN RIGHTS DEFENDERS 20 2.0 Overview of the Chapter 20 2.1 Violations Committed against Human Rights Defenders in 2018 21 2.1.1 Arrests and Prosecution against HRDs in 2018 Other Strategic Litigation Cases for HRDs in Tanzania 21 2.2 Physical violence, Attacks, and Torture 30 2.2.1 Pastoralists Land Rights Defenders and the Situation in
    [Show full text]
  • Audited Financial Statements
    DRUG CONTROL AND ENFORCEMENT AUTHORITY AUDITED FINANCIAL STATEMENTS FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2018 The Guest of Honour Mama Samia Suluhu Hassan the Vice President of the Government of URT (centre) in a souvenir photo with Tanzania Artist participants of DCEA workshop held at JNICC Dar es salaam, on her right is Hon. Jenista Joakim Mhagama (MP) Minister of State (Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Youth, Employment and Disabled), and Rogers W. Siyanga DCEA Commissioner General, and on her left is Hon. Harrison Mwakiembe (MP) Minister of Information, Culture and Sports and Paul Makonda Dar es Salaam Regional Commissioner VISION To have a society with zero tolerance on drug abuse and trafficking. MISSION To coordinate and enforce measures towards control of drugs, drug use and trafficking through harmonizing stakeholders’ efforts, conducting investigation, arrest, search, seizure, educating the public on adverse effects of drug use and trafficking. CORE VALUES In order to achieve the above vision and mission the Authority has put forward the following core values which are reliability, cooperation , accountability, innovativeness, proffesionalism, confidentiality, efficiency and effectiveness Heroin Cocain Cannabis Miraa Precursor Chemicals AUDITED FINANCIAL STATEMENTS i FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2018 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRIME MINISTER’S OFFICE DRUG CONTROL AND ENFORCEMENT AUTHORITY (VOTE 091) CORE VALUES In order to achieve the above vision and mission the Authority has put forward the following core values: v Integrity: We will be guided by ethical principles, honesty and fairness in decisions and judgments v Cooperation: We will promote cooperation with domestic stakeholders and international community in drug control and enforcement measures.
    [Show full text]