NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Saba – Tarehe 11 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae, Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazi ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Repoti ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual General Report of the Controller and Audit General of the Financial Statement of Local Governments For the Year Ended 30th June, 2017). Taarifa ya Majibu ya Serikali na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi ya Hali ya Uharibifu wa Ardhi na Misitu (Study on the Status of Environment With the Focus on Land Degradation, Forest Degradation and Deforestation) Repoti ya Ukaguzi wa Ufanisi na Usimamizi wa Taka za Kielektroniki (Performance Audit Report on Electronic Waste Management) NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Repoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Taarifa za Fedha za Taasisi za Serikali Kuu kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual General Report of The Controller and Auditor General on Financial Statement of Central Government for the Year ended 30th June, 2017). Ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Mashirka ya Umma kwa Mwaka wa Fedha2016/2017 (The Annual General Report on The Financial Statements of Public Authorities for the Financial year 2016/2017). Ripoti ya Jumla ya Ukaguzi wa Ufanisi na Ukaguzi Maalum kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2018 (The General Report of The Controller and Auditor General on Performance and Specialized Audit for The Period Ended 31st March, 2018). Ripoti ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017 (The Annual General Report of The Controller and Auditor General on The Financial Statements of Development Projects for The Year ended 30th June, 2017). 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi ya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Mapendekezo yaliyotolewa mwaka 2014 (Follow up Report on The Implementation of The Controller and Auditor General’s Recommendations for The Six Performance Audit Report issued and tabled to Parliament on April, 2014). Ripoti ya Ukaguzi ya Ufanisi ya Maandalizi ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Performance Audit Report on Preparedness for Implementation of Sustainable Development Goals). Majibu ya hoja na mpango wa kutekeleza mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioshia tarehe 30 Juni, 2017 volume I and II (A na B). NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Ripoti ya Ukaguzi wa ufanisi ya Utoaji wa huduma za Kusaidia Viwanda Vidogo na vya Kati Nchini (Performance Audit Report on the Provision of Support Service for Small and Medium Enterprises) NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi ya Usimamizi wa Utoaji wa Huduma za Maji taka Maeneo ya Mijini (Performance Audit Report on Provision of Sewage Services in Urban areas) NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Urejeshaji wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Performance Audit Report on Management of Repayment and Recovery of Higher Education Student Loans?. NAIBU WAZIRI WA KILIMO: 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Ripoti ya Ukaguzi na Usimamizi wa Viuatilifu vya Kilimo (Performance Audit Report on The Management of Pesticides in Agriculture) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE K.n.y. WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI): Taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Ugawaji wa Viwanja (Performance Audit Report on The Management of Plots Allocation) NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Taarifa ya Ukaguzi wa Ufanisi wa Usimamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (Performance Audit Report on Marine Protected Areas Management) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2018/2019. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI UMMA NA UTAWALA BORA: Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2018/2019. MHE. JASSON S. RWEIKIZA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI YA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Utekelezaji Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. JASSON S. RWEIKIZA-MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI YA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2017/2018 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019. MWENYEKITI: Ahsante Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa. Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 54 Idadi ya Watu Wenye Ulemavu Nchini. MHE. KHADIJA NASSIR ALI aliuliza:- Tanzania ina idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali. Je, Serikali inajua idadi kamili ya watu wenye ulemavu na aina ya ulemavu waliokuwa nao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. STELLA I. ALEX) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khadija Nassir Ali, Mbunge wa viti maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2012 inaeleza kuwa, ulemavu ni hali inayotokana na 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) dosari ya kimwili au ya kiakili ambayo inampunguzia mtu uwezo na fursa sawa katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika jamii. Upungufu huo unaweza kuchochewa na mazingira na mtazamo wa jamii kuhusu ulemavu. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna aina mbalimbali za ulemavu ambao umegawanyika katika makundi yafuatayo:- Ulemavu wa viungo, wasioona, viziwi, wasioona, ulemavu wa akili, wenye ualbino, ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi, ulemavu wa matatizo ya afya ya akili, yaani walioupata ukubwani bada ya kuugua kwa muda mrefu pamoja na ulemavu wa ngozi yaani walioathirika na mabaka mabaka ya ngozi mwilini. Sababu za kiujumla ni pamoja na ukosefu wa chakula bora au lishe duni, magonjwa kama malaria, uti wa mgono na surua, ajali mbalimbali, urithi na hali ya mama yaani umri na hali ya afya. Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema maelezo hayo, naomba kujibu sasa swali la Mheshimiwa Khadija Nassir Ali kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na wingi huo wa aina za ulemavu, Sense ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 imejumuisha vipengele mahususi kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusu watu wenye ulemavu hivyo Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani watu 44,928,923 ambao sasa kwa hapo mgawanyo wake uko kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wenye ualbino ni 16,477,000 ambayo ni sawa na asilimia 0.04, wasiiona ni 848,530 sawa na asilimia 1.19, ulemavu wa uziwi ni 425,322 sawa na asilimia 0.97, viungo ni 525,019 sawa na asilimia 1.9, ulemavu wa kumbukumbu ni 401,931 ambayo ni sawa na asilimia 0.9, ulemavu wa kushindwa kujihudumia ni 324,725 sawa na asilimia 0.74, na ulemavu mwingine yaani kwa ujumla wake ni 99,798 ambao ni sawa na asilimia 0.23. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Khadija Nassir una swali la nyongeza? MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa takwimu hizo zinatokana na sensa ya mwaka 2012 na Tanzania sasa inakadiriwa kuwa na watu wasiopungua milioni 50, hii inaonesha wazi kwamba Serikali haina takwimu sahihi kwa sasa. Swali langu la kwanza, Serikali haioni kwamba kukosekana kwa takwimu sahihi kunapelekea kushindwa kuwapatia mahitaji yao ipasavyo? Swali langu namba mbili, je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kufanya takwimu ili kuweza kupata idadi kamili ya watu wenye ulemavu? Ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwa ufupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. STELLA I. ALEX): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana mdogo wangu kwa ajinsi ambavyo anafuatilia masuala ya watu wenye ulemavu, lakini pia na yeye ni mdogo wetu yaani mdogo wa watu wote wenye ulemavu kwa sababu dada yake ni kiziwi. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa takwimu kwa watu wenye ulemavu, na sambamba na hilo kama tunavyofahamu, sensa inafanyika kila bada ya miaka 10 ambapo kutokana na kwamba ilifanyika mwaka 2012 kwa hiyo tunategemea sensa nyingine ifanyike mwaka 2022; lakini kwa sababu ya umuhimu wa jambo hili yaani takwimu kwa watu wenye ulemavu tayari Serikali imeshaanza kufanya mazungumzo na kuangalia ni jinsi sasa 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tunaweza kupata takwimu hizi kabla ya wakati huo.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages375 Page
-
File Size-