Tarehe 13 Septemba, 2019

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Tarehe 13 Septemba, 2019 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Tisa – Tarehe 13 Septemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- MHE. ANDREW J. CHENGE - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO:- Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Nne na Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante sana Mwenyekiti, Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na maswali na kwa siku ya leo tutaanza na Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Bukwimba Mbunge wa Busanda sasa aulize swali lake. Na. 108 Upungufu wa Watumishi katika Sekta ya Afya - Geita MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA aliuliza:- Katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuna upungufu mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo hilo? MWENYEKITI: Majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 hadi 2018/2019, Serikali imeajiri watumishi 8,444 wa sekta ya afya nchini ambapo watumishi 45 walipangwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepata kibali cha kuajiri watumishi 550 wa sekta ya afya na taratibu zinakamilishwa ili waweze kupangwa kwenye 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) vituo vya kutolea huduma kote nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. MWENYEKITI: Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, swali la nyongeza. MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza kabisa, nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais alipokuja Geita aliweza kunipatia Hospitali ya Wilaya itakayojengwa Kata ya Buseresere. Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo, naomba niulize swali la nyongeza, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, naipongeza Serikali kwamba imekusudia kuajiri watumishi 550 lakini kwa kuwa Halmashauri ya Geita tuna upungufu mkubwa sana tungependa kujua ni lini sasa hao watumishi wataletwa ili waweze kuanza kufanya kazi katika Halmashauri ya Geita? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa katika Jimbo la Busanda kuna vituo vya kutolea huduma viwili ambavyo vimekamilika kabisa, vinatakiwa tu kufunguliwa, Buziba pamoja na Magenge. Napenda kupata kauli ya Serikali ni lini sasa watahakikisha vituo hivi vimefunguliwa kwa sababu vimekamilika kabisa? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu ya maswali hayo ya nyongeza. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Serikali, naomba nipokee pongezi ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitoa kwa Serikali. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza anauliza ni lini watumishi watapelekwa ili kuweza kuziba pengo la upungufu huo mkubwa. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mchakato uko kwenye hatua za mwisho kabisa kwa sababu katika suala la kuajiri lazima taratibu zote zifuatwe. Namwondoa mashaka muda si mrefu watumishi wataweza kupelekwa huko. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili anaongelea vituo vyake vya afya viwili ambavyo tayari vimeshakamilika, anachotaka kujua ni lini vituo hivyo vitafunguliwa. Kama azma ya Serikali ilivyo kwamba vituo vile vya afya vinajengwa ili vianze kutoa huduma, sina uhakika kama tayari kama vifaa vyote vilishapelekwa. Kama vifaa vilishapelekwa ni jambo jema kinachotakiwa ni kupeleka watumishi ili vituo hivyo vifunguliwe vianze kutoa huduma. Ndiyo makusudi ya Serikali na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. MWENYEKITI: Mheshimiwa Joseph Mkundi, nimekuona. MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na matatizo makubwa ya kijiografia yaliyoko katika Visiwa vya Ukerewe yanayoathiri utoaji wa huduma za afya lakini tuna madaktari 3 pekee kati ya 10 wanaotakiwa, tuna waganga wasaidizi 5 pekee kati ya 43 wanaotakiwa na tuna wauguzi 80 pekee kati ya 289 wanaotakiwa. Nini kauli ya Serikali wanayoweza kuwaambia wananchi wa Ukerewe juu ya kuboresha huduma za afya kwa kutoa wahudumu wa afya kiasi kinachotakiwa? 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu ya swali hilo la nyongeza. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Mkundi, Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu katika jibu langu la msingi ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo yana upungufu mkubwa wa watumishi, wakati tunaajiri hao 550 tutazingatia. Naamini na Ukerewe nao hatutawasahau, ipo nia kubwa kuhakikisha kwamba tunapunguza hilo pengo la upungufu wa watumishi. Naomba nimhakikishie Mbunge tutazingatia katika mgao. MWENYEKITI: Mheshimiwa Selasini, swali fupi la nyongeza. MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi hiki Serikali imefanya jitihada kubwa sana za kujenga hospitali, vituo vya afya, zahanati na kadhalika. Kwa hili kama Kambi Rasmi ya Upinzani tulivyosema jambo zuri lazima tulipongeze, kwa hiyo, napongeza sana jitihada hizi ambazo zimefanyika katika kipindi hiki. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo tumetatua tatizo moja tumekaribisha tatizo lingine. Watumishi katika sekta hii ya afya ni wachache sana. Katika jimbo langu kwa mfano kuna upungufu wa asilimia 52 ya madaktari na wahudumu wengine katika sekta mbalimbali za afya. Nataka Serikali itueleze mkakati ambao utakwenda sambamba na ongezeko hili la hospitali na vituo vya afya ili sasa wananchi wapate ile huduma ambayo Serikali imekusudia waipate na ambayo ni haki yao? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu ya swali hilo kwa ufupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Roman Selasini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee naomba kupokea pongezi kutoka kwa Kambi Rasmi, ni jambo ambalo limekuwa likifanyika mara chache sana. Sasa ikitokea ni wajibu na sisi tu-recognize hiki ambacho kimefanyika. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu katika swali langu la msingi ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba huduma za afya zinasogezwa jirani na wananchi. Ni ukweli usiopingika kwamba sasa hivi wananchi wengi wanavutiwa kwenda kupata huduma kwenye vituo vyetu vya Serikali tofauti na vile vya mashirika ya watu binafsi na dini. Naomba nimhikishie Mheshimiwa Mbunge hao watumishi 550 ambao tutakuwa tumewaajiri na kuwasambaza hivi karibuni ni mchakato wa kuendelea kuajiri na wengine kwa kadri bajeti itakavyokuwa inaruhusu ili tupunguze adha ya mwananchi kupata huduma kwa urahisi ikiwepo ni pamoja na Rombo ambayo wana Mbunge ambaye ni makini ameweza ku-recognize kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu. MWENYEKITI: Tunaendelea na swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 109 Hitaji la Hospitali za Wilaya-Rukwa MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza:- Mkoa wa Rukwa una wilaya nne na hakuna Hospitali ya Wilaya:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali za Wilaya katika wilaya hizo? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu ya swali hilo. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali imeupatia Mkoa wa Rukwa kiasi cha shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Halmashauri za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo ambapo kila Halmashauri imepatiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.5. Vilevile katika mwaka wa fedha 2019/2020, Mkoa wa Rukwa umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali za Halmashauri za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo, ambapo kila Halmashauri itapewa kiasi cha shilingi milioni 500. Aidha, kiasi cha shilingi milioni 500 kimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. MWENYEKITI: Mheshimiwa Bupe, swali la nyongeza. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza kabisa, nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kazi kubwa ambayo imeifanya katika Mkoa wa Rukwa kutujengea Hospitali za Wilaya. Wakati nauliza swali hili tulikuwa hatujajengewa hospitali hata moja lakini ndani ya kipindi kifupi hospitali na vituo vya afya zimejengwa. Kwa hiyo, naipongeza Wizara na Mhe. 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Dkt. John Pombe Magufuli, hakika kazi
Recommended publications
  • Global Report
    In Focus Tanzania ruling party are no longer as united and pre- years. These include bribes paid to well- dictable as they have been throughout the connected intermediaries by the UK’s BAE country’s history as an independent nation. Systems, irregular payments of millions Political commentators of dollars from special here say that there are accounts at the central now at least two fac- bank (Bank of Tanza- tions within the party nia – BoT), inlated battling it out for in- construction contracts luence. In essence the for the BoT’s ‘twin two sides are those said towers’ headquarters, to be championing the as well as improperly ight against corruption awarded contracts for Women want more and those determined to the provision of emer- maintain the status quo gency electric power. In representation of kulindana (a Swahili one of the latter cases, Tanzania’s upcoming general elections term that can be loosely former Prime Minister, should bring great progress in women’s translated as ‘scratch Edward Lowassa, and empowerment and their participation in my back and I’ll scratch two cabinet colleagues, decision-making. That is if the ruling Chama yours’). Ibrahim Msabaha and Although it lost its Nazir Karamagi, took Cha Mapinduzi (CCM) keeps the promise status as the country’s political responsibility made in its 2005 election manifesto, that sole political party in for the so-called ‘Rich- it would achieve 50 percent women’s 1992, the Chama Cha President Jakaya Kikwete seeks election for mond affair’ by resign- participation in Parliament and local councils Mapinduzi (CCM – a second five-year term in October ing in 2008.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Sita – Tarehe 27 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo ni Kikao cha 36. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CATHERINE V. MAGIGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI) Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu utekelezaji na Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. TUNZA I. MALAPO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA MADINI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza Malapo, tunakushukuru. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Azza Hilal, Mbunge wa Viti Maalum - Shinyanga.
    [Show full text]
  • Check Against Delivery HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA
    Check Against Delivery HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA, (MB), WAKATI WA KUTOA HOJA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA SITA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DODOMA, TAREHE 9 FEBRUARI, 2007 Mheshimiwa Spika, Mkutano wa sita wa Bunge lako Tukufu umehitimisha shughuli zote zilizokuwa zimepangwa. Mkutano huu ni wa kwanza baada ya Serikali ya Awamu ya Nne kutimiza mwaka mmoja madarakani. Taarifa za mafanikio na changamoto zilizojitokeza zimewasilishwa kupitia mikutano mbalimbali ya Chama Tawala, Serikali na vyombo mbalimbali vya habari. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa, nachukua nafasi hii tena kwa niaba ya Serikali na wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa rambirambi kwako wewe Mheshimiwa Spika, kwa Waheshimiwa Wabunge wote, kwa familia, jamaa na marafiki kwa msiba uliotokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tunduru, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Bunge na Uratibu) Marehemu Juma Jamaldin Akukweti. Wote tulimfahamu Marehemu Akukweti kwa umakini na umahiri wake hapa Bungeni. Marehemu Akukweti alifariki kutokana na ajali ya ndege iliyokuwa inamrejesha Dar es Salaam baada ya kumaliza kazi ya kukagua soko la Mwanjelwa lililoteketea kwa moto mkoani Mbeya. Katika ajali hiyo Watumishi wa Serikali walipoteza maisha. Watumishi hao ni Bibi Theresia Nyantori, Mwandishi wa Habari wa Idara ya Habari; Bwana Nathaniel Katinila, Mratibu wa Mradi wa Masoko; na Bwana George Bendera, Afisa Habari Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu. Majeruhi katika ajali hiyo ambao bado wanapata matibabu lakini wametoka hosptali ni Bw. Nisetas Kanje, Katibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Bunge na Uratibu); na rubani wa ndege hiyo Bw. Martin Sumari. Tunamwomba Mwenyezi Mungu awasaidie majeruhi wote waweze kupona haraka na kurudia katika afya zao.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019 Feathers Ruffled in CCM Plastic Bag Ban TSh 33 trillion annual budget Ben Taylor: FEATHERS RUFFLED IN CCM Two former Secretary Generals of the ruling party, CCM, Abdulrahman Kinana and Yusuf Makamba, stirred up a very public argument at the highest levels of the party in July. They wrote a letter to the Elders’ Council, an advisory body within the party, warning of the dangers that “unfounded allegations” in a tabloid newspaper pose to the party’s “unity, solidarity and tranquillity.” Selection of newspaper covers from July featuring the devloping story cover photo: President Magufuli visits the fish market in Dar-es-Salaam following the plastic bag ban (see page 5) - photo State House Politics 3 This refers to the frequent allegations by publisher, Mr Cyprian Musiba, in his newspapers and on social media, that several senior figures within the party were involved in a plot to undermine the leadership of President John Magufuli. The supposed plotters named by Mr Musiba include Kinana and Makamba, as well as former Foreign Affairs Minister, Bernard Membe, various opposition leaders, government officials and civil society activists. Mr Musiba has styled himself as a “media activist” seeking to “defend the President against a plot to sabotage him.” His publications have consistently backed President Magufuli and ferociously attacked many within the party and outside, on the basis of little or no evidence. Mr Makamba and Mr Kinana, who served as CCM’s secretary generals between 2009 to 2011 and 2012-2018 respectively, called on the party’s elders to intervene.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 4 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Leo ni kikao cha tatu cha Mkutano wetu wa Kumi na Tano. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, AJIRA, KAZI VIJANA NA WAZEE NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. HASNA S.K. MWILIMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tume ya Uratibu na Udhibiti wa UKIMWI) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA SITA ______________ Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 27 Julai, 2009) (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita anayeuliza swali la kwanza, karibuni tena baada ya mapumziko ya weekend, nadhani mna nguvu ya kutosha kwa ajili ya shughuli za wiki hii ya mwisho ya Bunge hili la 16. Swali la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Waziri Mkuu na linauliza na Mheshimiwa Shoka, kwa niaba yake Mheshimiwa Khalifa. Na.281 Kiwanja kwa Ajili ya Kujenga Ofisi ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI MHE KHALIFA SULEIMAN KHALIFA (K.n.y. MHE. SHOKA KHAMIS JUMA) aliuliza:- Kwa kuwa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa Ofisi; na kwa kuwa Tume hiyo imepata fedha kutoka DANIDA kwa ajili ya kujenga jengo la Ofisi lakini inakabiliwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa kiwanja:- Je, Serikali itasaidia vipi Tume hiyo kupata kiwanja cha kujenga Ofisi? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Shoka Khamis Juma, Mbunge wa Micheweni kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, tatizo la kiwanja cha kujenga Ofisi za TACAIDS limepatiwa ufumbuzi na ofisi yangu imewaonesha Maafisa wa DANIDA kiwanja hicho Ijumaa tarehe 17 Julai, 2009. Kiwanja hicho kipo Mtaa wa Luthuli Na. 73, Dar es Salaam ama kwa lugha nyingine Makutano ya Mtaa wa Samora na Luthuli. MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri, naomba kumuuliza swali moja la nyongeza.
    [Show full text]
  • Coversheet for Thesis in Sussex Research Online
    A University of Sussex DPhil thesis Available online via Sussex Research Online: http://sro.sussex.ac.uk/ This thesis is protected by copyright which belongs to the author. This thesis cannot be reproduced or quoted extensively from without first obtaining permission in writing from the Author The content must not be changed in any way or sold commercially in any format or medium without the formal permission of the Author When referring to this work, full bibliographic details including the author, title, awarding institution and date of the thesis must be given Please visit Sussex Research Online for more information and further details Accountability and Clientelism in Dominant Party Politics: The Case of a Constituency Development Fund in Tanzania Machiko Tsubura Submitted for the Degree of Doctor of Philosophy in Development Studies University of Sussex January 2014 - ii - I hereby declare that this thesis has not been and will not be submitted in whole or in part to another University for the award of any other degree. Signature: ……………………………………… - iii - UNIVERSITY OF SUSSEX MACHIKO TSUBURA DOCTOR OF PHILOSOPHY IN DEVELOPMENT STUDIES ACCOUNTABILITY AND CLIENTELISM IN DOMINANT PARTY POLITICS: THE CASE OF A CONSTITUENCY DEVELOPMENT FUND IN TANZANIA SUMMARY This thesis examines the shifting nature of accountability and clientelism in dominant party politics in Tanzania through the analysis of the introduction of a Constituency Development Fund (CDF) in 2009. A CDF is a distinctive mechanism that channels a specific portion of the government budget to the constituencies of Members of Parliament (MPs) to finance local small-scale development projects which are primarily selected by MPs.
    [Show full text]
  • (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Sita – Tarehe 18 Mei, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kutokana na maagizo yaliyotolewa humu wiki iliyopita kuhusu Hati za kuwasilisha Mezani. Kama kuna kundi lolote, Kamati, Serikali au Upinzani hawajaleta Hati hazisomwi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais! Mheshimiwa Naibu Waziri! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO): Randama za Makadirio ya Matumizi kwa Ofisi ya Makamu wa Rais na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) pamoja na (Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU): Hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. JASSON S. RWEIKIZA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA: 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu) kwa mwaka wa fedha 2014/2015 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. ESTHER N. MATIKO - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA MAHUSIANO NA URATIBU: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza maswali Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Engineer Athumani Mfutakamba.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Ishirini - Tarehe 30 Juni, 2010 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anna S.Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na: NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA : Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha, 2010/2011. MHE. MOHAMED H. MISSANGA, MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya ya Miundombinu Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 pamoja na maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. MHE. GRACE S. KIWELU, MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:- Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. NAIBU WAZIRI WA VIWANDA,BIASHARA NA MASOKO: Randama za Makadiro ya Matumizi ya Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011. 1 MASWALI NA MAJIBU Na. 141 Barabara ya Nyakagomba- Katoro MHE.ESTHER K. NYAWAZWA (K.n.y. MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA) aliuliza:- Barabara ya Nyakagomba – Katoro kupitia Inyala inahudumia Kata zilizo katika Tarafa ya Butundwe kusafirisha mazao na bidhaa za biashara, lakini barabara hii haipitiki katika majira yote na kuwafanya wananchi wa maeneo husika kushindwa kufanya shughuli za maendeleo, na kwa sababu Halmashauri husika imeshindwa kulitatua tatizo hilo kutokana na Bajeti finyu.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA 18 TAREHE 5 FEBRUARI, 2015 MREMA 1.Pmd
    5 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Tisa – Tarehe 5 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, leo sijamwona. Kwa hiyo tunaendelea na Maswali kwa Waziri Mkuu na atakayeanza ni Mheshimiwa Murtaza A. Mangungu. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa vipindi tofauti vya Bunge Mheshimiwa Peter Msigwa, Mheshimiwa Mussa Zungu na hata Mheshimiwa Murtaza A. Mangungu wamekuwa wakiuliza swali kuhusiana na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara Wadogo Wadogo pamoja na Mamalishe. Kwa kipindi hicho chote umekuwa ukitoa maagizo na maelekezo, inavyoonekana mamlaka zinazosimamia hili jambo haziko tayari kutii amri yako. 1 5 FEBRUARI, 2015 Je, unawaambia nini Watanzania na Bunge hili kwa ujumla? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Murtaza Mangungu swali lake kama ifuatavyo:- Suala hili la vijana wetu ambao tunawajua kama Wamachinga, kwanza nataka nikiri kwamba ni suala kubwa na ni tatizo kubwa na si la Jiji la Dar es Salaam tu, bali lipo karibu katika miji mingi. Kwa hiyo, ni jambo ambalo lazima twende nalo kwa kiwango ambacho tutakuwa na uhakika kwamba tunalipatia ufumbuzi wa kudumu. Kwa hiyo, ni kweli kwamba mara kadhaa kuna maelekezo yametolewa yakatekelezwa sehemu na sehemu nyingine hayakutekelezwa kikamilifu kulingana na mazingira ya jambo lenyewe lilivyo. Lakini dhamira ya kutaka kumaliza tatizo hili la Wamachinga bado ipo palepale na kwa bahati nzuri umeuliza wakati mzuri kwa sababu jana tu nimepata taarifa ambayo nimeandikiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ambayo wanaleta mapendekezo kwangu juu ya utaratibu ambao wanafikiri unaweza ukatatua tatizo hili ambalo lipo sehemu nyingi.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA TANO Kikao cha Nane – Tarehe 17 Novemba, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2010. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza maswali kwa Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa mujibu wa Kanuni yetu ya 38(2), leo Waziri Mkuu hayupo, kwa hiyo, tunaendelea na maswali ya kawaida. Na. 99 Kukosekana kwa Huduma ya Maji Safi na Salama Tarime MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE aliuliza:- Tangu enzi za Uhuru hadi sasa Wilaya ya Tarime haijawahi kupata maji safi na salama kwa matumizi ya Wananchi:- (a) Je, Serikali haioni kuwa haiwatendei haki Wananchi wa Tarime kwa kutowapatia huduma ya maji safi na salama? (b) Je, Serikali ina mkakati gani katika kutatua tatizo hilo haraka iwezekanavyo? (c) Je, Serikali inasema nini juu ya ahadi zilizowahi kutolewa za kutatua tatizo la maji Wilaya ya Tarime? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, NInaomba kujibu swali la Mheshimiwa Nyambari Chacha Mariba Nyangwine, Mbunge wa Tarime, lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Wilaya ya Tarime ni asilimia 30 kwa maeneo ya Vijijini na asilimia 52 katika maeneo ya Mijini hadi kufikia mwaka 2010.
    [Show full text]