NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Tisa – Tarehe 13 Septemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- MHE. ANDREW J. CHENGE - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO:- Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Nne na Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante sana Mwenyekiti, Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na maswali na kwa siku ya leo tutaanza na Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Bukwimba Mbunge wa Busanda sasa aulize swali lake. Na. 108 Upungufu wa Watumishi katika Sekta ya Afya - Geita MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA aliuliza:- Katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuna upungufu mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo hilo? MWENYEKITI: Majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 hadi 2018/2019, Serikali imeajiri watumishi 8,444 wa sekta ya afya nchini ambapo watumishi 45 walipangwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepata kibali cha kuajiri watumishi 550 wa sekta ya afya na taratibu zinakamilishwa ili waweze kupangwa kwenye 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) vituo vya kutolea huduma kote nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. MWENYEKITI: Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, swali la nyongeza. MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza kabisa, nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais alipokuja Geita aliweza kunipatia Hospitali ya Wilaya itakayojengwa Kata ya Buseresere. Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo, naomba niulize swali la nyongeza, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, naipongeza Serikali kwamba imekusudia kuajiri watumishi 550 lakini kwa kuwa Halmashauri ya Geita tuna upungufu mkubwa sana tungependa kujua ni lini sasa hao watumishi wataletwa ili waweze kuanza kufanya kazi katika Halmashauri ya Geita? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa katika Jimbo la Busanda kuna vituo vya kutolea huduma viwili ambavyo vimekamilika kabisa, vinatakiwa tu kufunguliwa, Buziba pamoja na Magenge. Napenda kupata kauli ya Serikali ni lini sasa watahakikisha vituo hivi vimefunguliwa kwa sababu vimekamilika kabisa? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu ya maswali hayo ya nyongeza. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Serikali, naomba nipokee pongezi ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitoa kwa Serikali. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza anauliza ni lini watumishi watapelekwa ili kuweza kuziba pengo la upungufu huo mkubwa. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mchakato uko kwenye hatua za mwisho kabisa kwa sababu katika suala la kuajiri lazima taratibu zote zifuatwe. Namwondoa mashaka muda si mrefu watumishi wataweza kupelekwa huko. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili anaongelea vituo vyake vya afya viwili ambavyo tayari vimeshakamilika, anachotaka kujua ni lini vituo hivyo vitafunguliwa. Kama azma ya Serikali ilivyo kwamba vituo vile vya afya vinajengwa ili vianze kutoa huduma, sina uhakika kama tayari kama vifaa vyote vilishapelekwa. Kama vifaa vilishapelekwa ni jambo jema kinachotakiwa ni kupeleka watumishi ili vituo hivyo vifunguliwe vianze kutoa huduma. Ndiyo makusudi ya Serikali na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. MWENYEKITI: Mheshimiwa Joseph Mkundi, nimekuona. MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na matatizo makubwa ya kijiografia yaliyoko katika Visiwa vya Ukerewe yanayoathiri utoaji wa huduma za afya lakini tuna madaktari 3 pekee kati ya 10 wanaotakiwa, tuna waganga wasaidizi 5 pekee kati ya 43 wanaotakiwa na tuna wauguzi 80 pekee kati ya 289 wanaotakiwa. Nini kauli ya Serikali wanayoweza kuwaambia wananchi wa Ukerewe juu ya kuboresha huduma za afya kwa kutoa wahudumu wa afya kiasi kinachotakiwa? 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu ya swali hilo la nyongeza. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Mkundi, Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu katika jibu langu la msingi ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo yana upungufu mkubwa wa watumishi, wakati tunaajiri hao 550 tutazingatia. Naamini na Ukerewe nao hatutawasahau, ipo nia kubwa kuhakikisha kwamba tunapunguza hilo pengo la upungufu wa watumishi. Naomba nimhakikishie Mbunge tutazingatia katika mgao. MWENYEKITI: Mheshimiwa Selasini, swali fupi la nyongeza. MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi hiki Serikali imefanya jitihada kubwa sana za kujenga hospitali, vituo vya afya, zahanati na kadhalika. Kwa hili kama Kambi Rasmi ya Upinzani tulivyosema jambo zuri lazima tulipongeze, kwa hiyo, napongeza sana jitihada hizi ambazo zimefanyika katika kipindi hiki. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo tumetatua tatizo moja tumekaribisha tatizo lingine. Watumishi katika sekta hii ya afya ni wachache sana. Katika jimbo langu kwa mfano kuna upungufu wa asilimia 52 ya madaktari na wahudumu wengine katika sekta mbalimbali za afya. Nataka Serikali itueleze mkakati ambao utakwenda sambamba na ongezeko hili la hospitali na vituo vya afya ili sasa wananchi wapate ile huduma ambayo Serikali imekusudia waipate na ambayo ni haki yao? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu ya swali hilo kwa ufupi. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Roman Selasini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee naomba kupokea pongezi kutoka kwa Kambi Rasmi, ni jambo ambalo limekuwa likifanyika mara chache sana. Sasa ikitokea ni wajibu na sisi tu-recognize hiki ambacho kimefanyika. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu katika swali langu la msingi ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba huduma za afya zinasogezwa jirani na wananchi. Ni ukweli usiopingika kwamba sasa hivi wananchi wengi wanavutiwa kwenda kupata huduma kwenye vituo vyetu vya Serikali tofauti na vile vya mashirika ya watu binafsi na dini. Naomba nimhikishie Mheshimiwa Mbunge hao watumishi 550 ambao tutakuwa tumewaajiri na kuwasambaza hivi karibuni ni mchakato wa kuendelea kuajiri na wengine kwa kadri bajeti itakavyokuwa inaruhusu ili tupunguze adha ya mwananchi kupata huduma kwa urahisi ikiwepo ni pamoja na Rombo ambayo wana Mbunge ambaye ni makini ameweza ku-recognize kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu. MWENYEKITI: Tunaendelea na swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum. Na. 109 Hitaji la Hospitali za Wilaya-Rukwa MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza:- Mkoa wa Rukwa una wilaya nne na hakuna Hospitali ya Wilaya:- 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali za Wilaya katika wilaya hizo? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu ya swali hilo. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali imeupatia Mkoa wa Rukwa kiasi cha shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Halmashauri za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo ambapo kila Halmashauri imepatiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.5. Vilevile katika mwaka wa fedha 2019/2020, Mkoa wa Rukwa umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali za Halmashauri za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo, ambapo kila Halmashauri itapewa kiasi cha shilingi milioni 500. Aidha, kiasi cha shilingi milioni 500 kimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. MWENYEKITI: Mheshimiwa Bupe, swali la nyongeza. MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza kabisa, nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kazi kubwa ambayo imeifanya katika Mkoa wa Rukwa kutujengea Hospitali za Wilaya. Wakati nauliza swali hili tulikuwa hatujajengewa hospitali hata moja lakini ndani ya kipindi kifupi hospitali na vituo vya afya zimejengwa. Kwa hiyo, naipongeza Wizara na Mhe. 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Dkt. John Pombe Magufuli, hakika kazi
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages183 Page
-
File Size-