1 Bunge La Tanzania

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

1 Bunge La Tanzania Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Nane – Tarehe 4 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alikalia Kiti HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA PAMOJA NA UTAWALA BORA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma pamoja na (Utawala Bora) kwa mwaka wa Fedha 2011/2012. Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. PINDI H. CHANA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, pamoja na Utawala Bora, kwa Mwaka 2010/2011 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. DR. ABDALLAH O. KIGODA - MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, kwa Mwaka 2010/2011 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2011/2012. 1 MHE. SUZAN A. J. LYIMO - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, PAMOJA NA UTAWALA BORA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) pamoja na (Utawala Bora) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. MCH. ISRAEL YOHANA NATSE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA RAIS, UHUSIANO NA URATIBU: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza maswali na Ofisi ya Waziri Mkuu na kufuatana na utaratibu wa Serikali The most Senior Minister ndiye anachukua nafasi ya kusimamia Shughuli za Serikali hapa Bungeni naye ni Mheshimiwa Samuel Sitta, ndiye atafanya kazi hiyo kwa muda wa wiki moja. (Makofi) MASWALI NA MAJIBU Na. 165 Kero ya Maji Katika Mji Mdogo wa Ngudu MHE. RICHARD M. NDASSA (K.n.y. MHE. MANSOOR SHANIF HIRANI) aliuliza:- Mji mdogo wa Ngudu ambao ndio Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, una wakazi wengi na taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii na kiuchumi lakini una matatizo makubwa ya maji ambayo hutokana na uchakavu wa pampu mbili za kuvuna maji na pump moja ya kusukuma na kusambaza maji kutoka kwenye vyanzo vya maji vilivyo eneo la Kilyaboya. Gharama za pump hizo kwa pamoja hazizidi shilingi milioni hamsini za Kitanzania. Je, Serikali inajipanga vipi kuhakikisha tatizo hili la maji linamalizika kwa wakati ili kuondoa kero hiyo iliyopo kwa muda mrefu sasa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- 2 Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mansoor Shanif Hirani Mbunge wa Kwimba kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mji Mdogo wa Ngudu una wakazi 18,715 wanaohudumiwa na mradi wa maji chini ya mamala ya Maji Mji Mdogo wa Ngudu. Chanzo cha maji katika Mji Mdogo wa Ngudu na visima vya kati sita (6) vilivyochimbwa ambapo na kati ya hivyo visima 4 vina mitambo ya kuvutia maji kupeleka katika sampu ni tanki la kukusanyia maji kutoka katika visima. Vipo visima viwili (2) mitambo yake imeharibika na havifanyi kazi kwa sasa. Aidha, jumla ya visima vitatu (3) vinahitaji kusafishwa ili kuhuisha uwezo wake wa uzalishaji maji. Kutoka kwenye sampo ya kukusanyia maji kuna mitambo miwili (2) ambayo husukuma maji katika matanki ya usambazaji yaliyopo katika maeneo mawili ya Mjini. Mtambo mmoja umeharibika na unahitaji kununuliwa mtambo mpya. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na matatizo ya maji Mji Mdogo wa Ngudu, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, kupitia Bajeti yake ya mwaka 2011/2012 imetenga kiasi cha shilingi milioni 100. Fedha hizo ni kwa ajili ya kununua mtambo mmoja wa kusukuma maji kutoka katika sampu hadi matanki ya usambazaji maji pale mjini. Vile vile pampu tatu za kuvuta maji katika visima ili kuongeza kiwango cha maji kitakachokusanywa. Mamlaka ya Maji Mji Mdogo wa Ngudu, nayo katika Bajeti yake ya mwaka 2011/2012 imetenga kiasi cha shilingi milioni 6 kwa ajili ya kusafisha visima vitatu ili kuongeza kiwango cha maji katika visima hivyo. Mheshimiwa Spika, kupitia mradi wa maji na usafi wa mazingira unaotekelezwa chini ya programu ya maji na usafi wa mazingira kitaifa (WSSDP), Mhandisi Mshauri Don Consult Ltd. Anaendelea kufanya upembezi yakinifu. Baada ya usanifu na kuandaa tender document ndipo shughuli za kutafuta mkandarasi zitafanyika. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, inashauriwa kuendelea kuzingatia katika vipaumbele vyake na kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya maji ili kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, kwa sababu maji ni uhai na maji hayawezi kusubiri. Je, Serikali sasa kutokana na ufinyu wa fedha ambazo Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, inazo Serikali inaweza mpango mkakati wa kuyatoa maji katika Kijiji Maro ambapo ni kilomita 70 kutoka Maro kwenda Ngudu maji ya Ziwa Victoria ili maji hayo sasa yaweze kusaidia Mji wa Ngudu? NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali imeshachukua hatua ndio maana imemwajiri na Mshauri ili aweze kufanya usanifu wa kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria. Lakini kwa muda wa matokeo ya haraka tumefanya utafiti pia wa kuweza 3 kuongeza visima na kusafisha vile vilivyopo ili wakati tunasubiri huu mradi angalau wananchi wa Magu waweze kupata maji. MHE. MWIGULU L. MCHEMBA MADELU: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo la pampu kuharibika hata Iramba lipo na gharama ya kusafisha pampu na kuhuisha visima vya Songambele, Kibaya, Misuna, Makunda na Kisharita ni dogo kuliko la kuchimba visima vipya. Je, Serikali inatoa kauli gani ili kuvihuisha visima hivyo ambavyo sasa wananchi wanapata tabu sana katika vijiji hivyo na vingine? (Makofi) SPIKA: Mambo ya kusafisha visima yanatosha TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimejibu katika jibu kwenye jibu la msingi ya kwamba huduma za maji kwa jamii yetu linaona kwanza na jamii husika na kule tuna mamlaka zetu za Serikali za Mitaa ambako kuna Baraza la Madiwani, Baraza la Madiwani linao uwezo sasa kubaini kuwa tatizo lililopo katika eneo hilo na kutenga Bajeti kupitia fedha ambazo zipo. Pia niweze kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge, kwa kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo tumeikamilisha juzi na sasa suala la kupeleka fedha kwenye Halmashauri zetu sasa linaanza mara moja na kwa hiyo, sasa kama kunahitaji kuchimba visima vivyo hivyo, kuhuisha visima vilivyopo, kununua pampu ni maamuzi ya Halmashauri yenyewe ili kuweza kutoa huduma ya maji kwa jamii husika. (Makofi) Na. 166 Uanzishwaji wa Kidato cha Tano na Sita katika Kila Tarafa Nchini MHE. KAIKA SANING’O TELELE aliuliza:- Serikali ya Awamu ya Nne katika sekta ya Elimu inahamasisha Uanzishwaji wa Kidato cha Tano na cha Sita katika kila Tarafa hapa nchini:- Je, Serikali itasaidia vipi Tarafa ya Ngorongoro ambayo ni hifadhi mseto kupata kibali cha tathmini ya mazingira Environmental Impact Assessment (EIA) toka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) haraka ili ujenzi na uanzishwaji wa vidato hivyo uweze kuanza kama ilivyo kwenye maeneo mengine nje ya Hifadhi? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kaika Saning’o Telele, kama ifuatavyo:- 4 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tarafa ya Ngorongoro, ina hifadhi mseto na kwa kuwa kibali kinachoombwa kinatolewa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) nashauri Halmashauri husika iwasiliane na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Mazingira ili waiandikie NEMC barua ya kuomba eneo husika kufanyiwa Environmental Impact Assessment (EIA) ili kuona uwezekano wa kujenga shule hiyo katika eneo hilo. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa EIA ni itifaki ya Kimataifa na kwa kuwa ripoti itakayotolewa itahusisha mambo ya usalama wa wanafunzi katika hifadhi mseto Halmshauri ikubaliane na ushauri utakaotolewa na NEMC na kuona uwezekano wa kujenga shule hiyo katika eneo jingine endapo eneo hilo walilochagua litaonekana halifai. Mheshimiwa Spika, baada ya kibali hicho kupatikana, Wizara yangu itatoa kibali cha kuanza ujenzi wa shule kwa kuzingatia taratibu na vigezo vilivyopo vya kuanzisha shule yenye kidato cha Tano na Sita. Aidha, Wizara yangu itakuwa tayari kusajili shule hiyo haraka baada ya kukamilisha ujenzi kwani azma ya Serikali ni kuwa na shule yenye kidato cha 5 na 6 kwa kila tarafa hapa nchini ili kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. MHE. KAIKA SANING’O TELELE: Mheshimiwa Spika, naona upatikanaji wa kibali kutoka Baraza la Taifa la Mazingira ina mlolongo mrefu. (a) Je, Serikail haiwezi kupandisha hadhi Sekondari ambayo iko katika Tarafa ya Ngorongoro ya O’level ili iwe na kidato cha Tano na Sita? (b) Kama hilo litafanyika na kwa sababu tulikuwa tumeshaanza maandalizi. Je, Serikali iko tayari kutoa kibali hata mwishoni mwa mwaka huu tuanze Februari mwaka kesho? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, kama nilivyosema ni Hifadhi Mseto na kama Mheshimiwa Mbunge, mwenyewe alivyogundua kwamba utaratibu wa hawa wa kuwaandikia NEMC barua ni taratibu ndefu. Lakini kwa kuwa vile vile agizo la Mheshimiwa Rais tunataka angalau kila tarafa iwe na sekondari ya A- level, mimi nawashauri Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro waweze kufikiri namna ya kutafuta vigezo vya kupandisha hadhi katika shule moja zilizopo kwenye Halmashauri sisi Wizara ya Elimu hatuna matatizo kabisa, tutatuma wakaguzi watakuja kukagua Kanda ya Kaskazini, kule Arusha watakapokuwa tayari tutatoa kibali cha kuanzisha shule moja iwe A- level katika Halmashauri hiyo.
Recommended publications
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 27 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kwa Mwaka 2012/2013 (The Annual Report and Accounts of Arusha International Conference Centre for the Year 2012/2013). Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. BETTY E. MACHANGU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. ABDULKARIM E.H. SHAH (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ BUNGE LA KUMI NA MOJA ___________ MKUTANO WA KWANZA Kikao cha Kwanza - Tarehe 17 Novemba, 2015 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Naomba tukae. TANGAZO LA RAIS LA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa masharti ya Katiba, Mkutano huu wa Kwanza unaanza kwa Rais kuuitisha. Naomba kuchukua nafasi hii kusoma Tangazo la Rais kama ambavyo tumelipokea. Tangazo la Serikali Na. 513 la tarehe 6 Novemba, 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sura ya Pili, hati iliyotolewa kwa mujibu wa Ibara ya 90(1). Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya. KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; NA KWA KUWA, masharti ya Ibara ndogo ya kwanza ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, yanamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu; NA KWA KUWA, matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 yalitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2015; HIVYO BASI, mimi John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyonayo chini ya Ibara ya 90(1) ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, naitisha Mkutano wa Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ufanyike katika ukumbi wa Bunge uliopo Mjini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi.
    [Show full text]
  • Conference Report
    2 ND GOPAC GLOBAL CONFERENCE Arusha, Tanzania September 19-23, 2006 FINAL REPORT GLOBAL ORGANISATION OF PARLIAMENTARIANS AGAINST CORRUPTION: 2ND GLOBAL CONFERENCE Acknowledgements The Global Organisation of Parliamentarians Against Corruption wishes to thank the following organisations for their contributions to the 2nd Global Conference: Parliament of Tanzania African Parliamentarians Network Against Corruption (APNAC) Barrick Gold Canadian International Development Agency (CIDA) US Agency for International Development (USAID) World Bank Institute (WBI) Events Hosts Dr. Zainab A. Gama, MP, Chair, APNAC – Tanzania Arusha Regional Commissioner Col (Rtd). Samuel Ndomba H.E. Dr. Ali Mohamed Shein the Vice President of the United Republic of Tanzania Hosted by Hon. Samuel Sitta, MP – Speaker of the National Assembly Guest Speakers Deputy Barrister Emmanuel Akomaye, Economic and Financial Crimes Commission of Nigeria Doris Basler, Transparency International Hon. Ruth Kavuma, MP, Vice Chair, APNAC Uganda Mr. Paul Wolfowitz, President, World Bank (Taped message) Conference and Workshop Speakers Conference Chair: John Williams MP (Canada) Edward Doe Adjaho, MP (Ghana) Naser Al Sane, MP (Kuwait) Edgardo Angara, Senator (Philippines) Stella Cittadini, Senator (Argentina) Roy Cullen, MP (Canada) César Jauregui, Senator (Mexico) Edith Mastenbroek, MEP (Netherlands) J.T.K. Green-Harris, MP (Gambia) Mary King, Senator (Trinidad and Tobago) Omingo Magara, MP (Kenya) Augustine Ruzindana, Former MP (Uganda) Willibroad Slaa, MP (Tanzania) Navin Beekarry (IMF) Giovanni Gallo (UNODC) Scott Hubli (UNDP) Latifah Merican Cheong (World Bank) Carmen Lane (DAI) Luis Gerardo Villanueva, Former MP (Costa Murray Michel (Egmont Group and Rica) FATF) Patrick Moulette (IMF) Keith Schulz (USAID) Ingeborg Schwarz (IPU) Emiko Todoroki (WB) Frederick Stapenhurst (WBI) Stuart Yikona (WB) GOPAC wishes to thank the following individuals for their significant contribution to the conference and its administration: Canadian High Commission - Tanzania Parliament of Tanzania H.E.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 10 Februari, 2010 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE): Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Benki ya Posta Tanzania, kwa Mwaka 2008 [The Annual Report and Accounts of The Tanzania Postal Bank for the Year 2008]. The Mid-Term Review of the Monetary Policy Statement of The Bank of Tanzania for the Year 2009/2010. MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini juu ya Taarifa ya Serikali Kuhusu Ubinafsishwaji wa Mgodi wa Kiwira. Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Houston Texas - Marekani Mwaka 2006. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelzaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Uendeshaji Usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India. 1 Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Utendaji wa Kazi Usioridhisha wa Kampuni ya TICTS. MASWALI NA MAJIBU Na. 145 Usimamizi wa Ukaguzi wa Fedha za Halmashauri MHE. HERBERT J. MNTANGI aliuliza:- Kwa kuwa, kiasi cha fedha kinachopelekwa katika Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Jiji ni kikubwa na kinahitaji usimamizi wa ziada:- Kwa kuwa kitengo cha ukaguzi wa ndani kipo chini ya Mkurugenzi Mtendaji.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 22 Juni, 2021 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Hamsini na Sita na kabla hatujaendelea nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wasaidizi wangu wote wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa David Kihenzile, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Najma kwa kazi nzuri ambayo wameifanya wiki nzima kutuendeshea mjadala wetu wa bajeti. (Makofi) Sasa leo hapa ndio siku ya maamuzi ambayo kila Mbunge anapaswa kuwa humu ndani, kwa Mbunge ambaye Spika hana taarifa yake na hatapiga kura hapa leo hilo la kwake yeye. (Makofi) Katibu. NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali na tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 465 Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri Katika Mji wa Laela MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Sumbawanga katika Mji wa Laela baada ya agizo la Serikali la kuhamisha Makao Makuu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu la watu wa Kwela, Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 30 zilizohamia kwenye maeneo mapya ya utawala mwaka 2019.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Februari, 2013
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Tano – Tarehe 4 Februari, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 53 Hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale Kupatiwa Watumishi MHE. JOSEPHINE T. CHAGULLA aliuliza:- Hospitali ya Karumwa ambayo ni ya Wilaya mpya ya Nyang’hwale haina watumishi wa kutosha kwani ina daktari mmoja, Manesi watatu na mtaalam mmoja wa Maabara:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka watumishi wa kutosha katika hospitali hiyo? 1 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Tabitha Chagulla, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Kituo cha Afya, Karumwa kilichoko katika Wilaya mpya ya Nyang’hwale kina Daktari mmoja, Manesi watatu na Mtaalam mmoja wa maabara. Kutokana na tatizo la upungufu wa watumishi wa sekta ya afya kuwepo katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati zote nchini kikiwemo kituo cha afya Karumwa, Serikali imechukua jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa udhahili wa wanafunzi wanaojiunga na fani za Udaktari na Uuguzi unaongezeka katika vyuo vikuu na vyuo vya ngazi ya Diploma na cheti. Aidha, Serikali imerejesha kada za chini za afya zilizokuwa zimefutwa. Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jitihada hizo, hivi sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inawapanga wahitimu wa fani za afya moja kwa moja katika vituo vya kazi baada ya kibali kutolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
    [Show full text]
  • Tanzania Human Rights Report 2008
    Legal and Human Rights Centre Tanzania Human Rights Report 2008: Progress through Human Rights Funded By; Embassy of Finland Embassy of Norway Embassy of Sweden Ford Foundation Oxfam-Novib Trocaire Foundation for Civil Society i Tanzania Human Rights Report 2008 Editorial Board Francis Kiwanga (Adv.) Helen Kijo-Bisimba Prof. Chris Maina Peter Richard Shilamba Harold Sungusia Rodrick Maro Felista Mauya Researchers Godfrey Mpandikizi Stephen Axwesso Laetitia Petro Writers Clarence Kipobota Sarah Louw Publisher Legal and Human Rights Centre LHRC, April 2009 ISBN: 978-9987-432-74-5 ii Acknowledgements We would like to recognize the immense contribution of several individuals, institutions, governmental departments, and non-governmental organisations. The information they provided to us was invaluable to the preparation of this report. We are also grateful for the great work done by LHRC employees Laetitia Petro, Richard Shilamba, Godfrey Mpandikizi, Stephen Axwesso, Mashauri Jeremiah, Ally Mwashongo, Abuu Adballah and Charles Luther who facilitated the distribution, collection and analysis of information gathered from different areas of Tanzania. Our 131 field human rights monitors and paralegals also played an important role in preparing this report by providing us with current information about the human rights’ situation at the grass roots’ level. We greatly appreciate the assistance we received from the members of the editorial board, who are: Helen Kijo-Bisimba, Francis Kiwanga, Rodrick Maro, Felista Mauya, Professor Chris Maina Peter, and Harold Sungusia for their invaluable input on the content and form of this report. Their contributions helped us to create a better report. We would like to recognize the financial support we received from various partners to prepare and publish this report.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • Coversheet for Thesis in Sussex Research Online
    A University of Sussex DPhil thesis Available online via Sussex Research Online: http://sro.sussex.ac.uk/ This thesis is protected by copyright which belongs to the author. This thesis cannot be reproduced or quoted extensively from without first obtaining permission in writing from the Author The content must not be changed in any way or sold commercially in any format or medium without the formal permission of the Author When referring to this work, full bibliographic details including the author, title, awarding institution and date of the thesis must be given Please visit Sussex Research Online for more information and further details Accountability and Clientelism in Dominant Party Politics: The Case of a Constituency Development Fund in Tanzania Machiko Tsubura Submitted for the Degree of Doctor of Philosophy in Development Studies University of Sussex January 2014 - ii - I hereby declare that this thesis has not been and will not be submitted in whole or in part to another University for the award of any other degree. Signature: ……………………………………… - iii - UNIVERSITY OF SUSSEX MACHIKO TSUBURA DOCTOR OF PHILOSOPHY IN DEVELOPMENT STUDIES ACCOUNTABILITY AND CLIENTELISM IN DOMINANT PARTY POLITICS: THE CASE OF A CONSTITUENCY DEVELOPMENT FUND IN TANZANIA SUMMARY This thesis examines the shifting nature of accountability and clientelism in dominant party politics in Tanzania through the analysis of the introduction of a Constituency Development Fund (CDF) in 2009. A CDF is a distinctive mechanism that channels a specific portion of the government budget to the constituencies of Members of Parliament (MPs) to finance local small-scale development projects which are primarily selected by MPs.
    [Show full text]
  • Tanzania Human Rights Report 2016
    Tanzania Human Rights Report 2016 LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTRE & ZANZIBAR LEGAL SERVICES CENTRE NOT FOR SALE Tanzania Human Rights Report - 2016 Mainland and Zanzibar - i - Tanzania Human Rights Report 2016 Part One: Tanzania Mainland - Legal and Human Rights Centre (LHRC) Part Two: Zanzibar - Zanzibar Legal Services Centre (ZLSC) - ii - Tanzania Human Rights Report 2016 Publishers Legal and Human Rights Centre Justice Lugakingira House, Kijitonyama P. O. Box 75254, Dar es Salaam, Tanzania Tel: +255222773038/48, Fax: +255222773037 Email: [email protected] Website: www.humanrights.or.tz & Zanzibar Legal Services Centre P. O. Box 3360, Zanzibar, Tanzania Tel: +2552422384 Fax: +255242234495 Email: [email protected] Website: www.zlsc.or.tz Partners The Embassy of Sweden The Embassy of Norway Oxfam Rosa Luxemburg UN Women Open Society Initiatives for Eastern Africa Design & Layout Albert Rodrick Maro Munyetti ISBN: 978-9987-740-30-7 © LHRC & ZLSC 2017 - iii - Tanzania Human Rights Report 2016 Editorial Board - Part One Dr. Helen Kijo-Bisimba Adv. Imelda Urio Ms. Felista Mauya Adv. Anna Henga Researchers/Writers Paul Mikongoti Fundikila Wazambi - iv - Tanzania Human Rights Report 2016 About LHRC The Legal and Human Rights Centre (LHRC) is a private, autonomous, voluntary non- Governmental, non-partisan and non-profit sharing organization envisioning a just and equitable society. It has a mission of empowering the people of Tanzania, so as to promote, reinforce and safeguard human rights and good governance in the country. The broad objective is to create legal and human rights awareness among the public and in particular the underprivileged section of the society through legal and civic education, advocacy linked with legal aid provision, research and human rights monitoring.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA SABA Kikao Cha Thelathini Na Tisa – Tarehe 1 Juni
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 Juni, 2017 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, Katibu. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018. MHE. CATHERINE V. MAGIGE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI): Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. ESTHER N. MATIKO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Nishati na Madini juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Maswali kwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu tutaanza na Mheshimiwa Devotha Mathew Minja. MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa ni sera ya Serikali kuboresha kilimo hapa nchini, ikizingatiwa kwamba kilimo kinatoa ajira kwa Watanzania kwa zaidi ya asilimia 80 na kilimo kimekuwa kikihudumia Watanzania kwa maana ya kujitosheleza kwa chakula, lakini kwa kuwa pia ni sera Serikali iliamua kuja na mikakati ya kuboresha sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kutoa majukumu kwa mawakala wa pembejeo hapa nchini ili waweze kutoa huduma hizo za pembejeo kwa wakulima wetu hapa nchini.
    [Show full text]
  • Consequences for Women's Leadership
    The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures by Christie Marie Arendt B.A. in Interdisciplinary Studies in Social Science, May 2004, Michigan State University M.A. in International Affairs, May 2006, The George Washington University A Dissertation submitted to The Faculty of The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University in partial fulfillment of the requirements for the degree of Doctor of Philosophy January 31, 2017 Dissertation directed by Kimberly J. Morgan Professor of Political Science and International Affairs The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University certifies that Christie Marie Arendt has passed the Final Examination for the degree of Doctor of Philosophy as of December 16, 2016. This is the final and approved form of the dissertation. The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures Christie Marie Arendt Dissertation Research Committee: Kimberly J. Morgan, Professor of Political Science and International Affairs, Dissertation Director Jennifer Brinkerhoff, Professor of International Affairs, International Business, and Public Policy & Public Administration Eric Kramon, Assistant Professor of Political Science and International Affairs, Committee Member ii © Copyright 2017 by Christie Marie Arendt All rights reserved iii Dedication To my parents, Anne and Steve Arendt, none of this was possible without your enduring love and support. iv Acknowledgments This dissertation benefitted from the encouragement and guidance of a number of people. As an alumna of The George Washington University’s Elliott School of International Affairs, I knew that GW would provide a perfect environment to pursue my doctoral studies.
    [Show full text]