Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Nane – Tarehe 4 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alikalia Kiti HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA PAMOJA NA UTAWALA BORA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma pamoja na (Utawala Bora) kwa mwaka wa Fedha 2011/2012. Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. PINDI H. CHANA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, pamoja na Utawala Bora, kwa Mwaka 2010/2011 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. DR. ABDALLAH O. KIGODA - MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, kwa Mwaka 2010/2011 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2011/2012. 1 MHE. SUZAN A. J. LYIMO - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, PAMOJA NA UTAWALA BORA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) pamoja na (Utawala Bora) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. MCH. ISRAEL YOHANA NATSE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA RAIS, UHUSIANO NA URATIBU: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza maswali na Ofisi ya Waziri Mkuu na kufuatana na utaratibu wa Serikali The most Senior Minister ndiye anachukua nafasi ya kusimamia Shughuli za Serikali hapa Bungeni naye ni Mheshimiwa Samuel Sitta, ndiye atafanya kazi hiyo kwa muda wa wiki moja. (Makofi) MASWALI NA MAJIBU Na. 165 Kero ya Maji Katika Mji Mdogo wa Ngudu MHE. RICHARD M. NDASSA (K.n.y. MHE. MANSOOR SHANIF HIRANI) aliuliza:- Mji mdogo wa Ngudu ambao ndio Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, una wakazi wengi na taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii na kiuchumi lakini una matatizo makubwa ya maji ambayo hutokana na uchakavu wa pampu mbili za kuvuna maji na pump moja ya kusukuma na kusambaza maji kutoka kwenye vyanzo vya maji vilivyo eneo la Kilyaboya. Gharama za pump hizo kwa pamoja hazizidi shilingi milioni hamsini za Kitanzania. Je, Serikali inajipanga vipi kuhakikisha tatizo hili la maji linamalizika kwa wakati ili kuondoa kero hiyo iliyopo kwa muda mrefu sasa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- 2 Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mansoor Shanif Hirani Mbunge wa Kwimba kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mji Mdogo wa Ngudu una wakazi 18,715 wanaohudumiwa na mradi wa maji chini ya mamala ya Maji Mji Mdogo wa Ngudu. Chanzo cha maji katika Mji Mdogo wa Ngudu na visima vya kati sita (6) vilivyochimbwa ambapo na kati ya hivyo visima 4 vina mitambo ya kuvutia maji kupeleka katika sampu ni tanki la kukusanyia maji kutoka katika visima. Vipo visima viwili (2) mitambo yake imeharibika na havifanyi kazi kwa sasa. Aidha, jumla ya visima vitatu (3) vinahitaji kusafishwa ili kuhuisha uwezo wake wa uzalishaji maji. Kutoka kwenye sampo ya kukusanyia maji kuna mitambo miwili (2) ambayo husukuma maji katika matanki ya usambazaji yaliyopo katika maeneo mawili ya Mjini. Mtambo mmoja umeharibika na unahitaji kununuliwa mtambo mpya. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na matatizo ya maji Mji Mdogo wa Ngudu, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, kupitia Bajeti yake ya mwaka 2011/2012 imetenga kiasi cha shilingi milioni 100. Fedha hizo ni kwa ajili ya kununua mtambo mmoja wa kusukuma maji kutoka katika sampu hadi matanki ya usambazaji maji pale mjini. Vile vile pampu tatu za kuvuta maji katika visima ili kuongeza kiwango cha maji kitakachokusanywa. Mamlaka ya Maji Mji Mdogo wa Ngudu, nayo katika Bajeti yake ya mwaka 2011/2012 imetenga kiasi cha shilingi milioni 6 kwa ajili ya kusafisha visima vitatu ili kuongeza kiwango cha maji katika visima hivyo. Mheshimiwa Spika, kupitia mradi wa maji na usafi wa mazingira unaotekelezwa chini ya programu ya maji na usafi wa mazingira kitaifa (WSSDP), Mhandisi Mshauri Don Consult Ltd. Anaendelea kufanya upembezi yakinifu. Baada ya usanifu na kuandaa tender document ndipo shughuli za kutafuta mkandarasi zitafanyika. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, inashauriwa kuendelea kuzingatia katika vipaumbele vyake na kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya maji ili kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo. MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, kwa sababu maji ni uhai na maji hayawezi kusubiri. Je, Serikali sasa kutokana na ufinyu wa fedha ambazo Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, inazo Serikali inaweza mpango mkakati wa kuyatoa maji katika Kijiji Maro ambapo ni kilomita 70 kutoka Maro kwenda Ngudu maji ya Ziwa Victoria ili maji hayo sasa yaweze kusaidia Mji wa Ngudu? NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali imeshachukua hatua ndio maana imemwajiri na Mshauri ili aweze kufanya usanifu wa kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria. Lakini kwa muda wa matokeo ya haraka tumefanya utafiti pia wa kuweza 3 kuongeza visima na kusafisha vile vilivyopo ili wakati tunasubiri huu mradi angalau wananchi wa Magu waweze kupata maji. MHE. MWIGULU L. MCHEMBA MADELU: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo la pampu kuharibika hata Iramba lipo na gharama ya kusafisha pampu na kuhuisha visima vya Songambele, Kibaya, Misuna, Makunda na Kisharita ni dogo kuliko la kuchimba visima vipya. Je, Serikali inatoa kauli gani ili kuvihuisha visima hivyo ambavyo sasa wananchi wanapata tabu sana katika vijiji hivyo na vingine? (Makofi) SPIKA: Mambo ya kusafisha visima yanatosha TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimejibu katika jibu kwenye jibu la msingi ya kwamba huduma za maji kwa jamii yetu linaona kwanza na jamii husika na kule tuna mamlaka zetu za Serikali za Mitaa ambako kuna Baraza la Madiwani, Baraza la Madiwani linao uwezo sasa kubaini kuwa tatizo lililopo katika eneo hilo na kutenga Bajeti kupitia fedha ambazo zipo. Pia niweze kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge, kwa kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo tumeikamilisha juzi na sasa suala la kupeleka fedha kwenye Halmashauri zetu sasa linaanza mara moja na kwa hiyo, sasa kama kunahitaji kuchimba visima vivyo hivyo, kuhuisha visima vilivyopo, kununua pampu ni maamuzi ya Halmashauri yenyewe ili kuweza kutoa huduma ya maji kwa jamii husika. (Makofi) Na. 166 Uanzishwaji wa Kidato cha Tano na Sita katika Kila Tarafa Nchini MHE. KAIKA SANING’O TELELE aliuliza:- Serikali ya Awamu ya Nne katika sekta ya Elimu inahamasisha Uanzishwaji wa Kidato cha Tano na cha Sita katika kila Tarafa hapa nchini:- Je, Serikali itasaidia vipi Tarafa ya Ngorongoro ambayo ni hifadhi mseto kupata kibali cha tathmini ya mazingira Environmental Impact Assessment (EIA) toka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) haraka ili ujenzi na uanzishwaji wa vidato hivyo uweze kuanza kama ilivyo kwenye maeneo mengine nje ya Hifadhi? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kaika Saning’o Telele, kama ifuatavyo:- 4 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tarafa ya Ngorongoro, ina hifadhi mseto na kwa kuwa kibali kinachoombwa kinatolewa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) nashauri Halmashauri husika iwasiliane na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Mazingira ili waiandikie NEMC barua ya kuomba eneo husika kufanyiwa Environmental Impact Assessment (EIA) ili kuona uwezekano wa kujenga shule hiyo katika eneo hilo. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa EIA ni itifaki ya Kimataifa na kwa kuwa ripoti itakayotolewa itahusisha mambo ya usalama wa wanafunzi katika hifadhi mseto Halmshauri ikubaliane na ushauri utakaotolewa na NEMC na kuona uwezekano wa kujenga shule hiyo katika eneo jingine endapo eneo hilo walilochagua litaonekana halifai. Mheshimiwa Spika, baada ya kibali hicho kupatikana, Wizara yangu itatoa kibali cha kuanza ujenzi wa shule kwa kuzingatia taratibu na vigezo vilivyopo vya kuanzisha shule yenye kidato cha Tano na Sita. Aidha, Wizara yangu itakuwa tayari kusajili shule hiyo haraka baada ya kukamilisha ujenzi kwani azma ya Serikali ni kuwa na shule yenye kidato cha 5 na 6 kwa kila tarafa hapa nchini ili kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. MHE. KAIKA SANING’O TELELE: Mheshimiwa Spika, naona upatikanaji wa kibali kutoka Baraza la Taifa la Mazingira ina mlolongo mrefu. (a) Je, Serikail haiwezi kupandisha hadhi Sekondari ambayo iko katika Tarafa ya Ngorongoro ya O’level ili iwe na kidato cha Tano na Sita? (b) Kama hilo litafanyika na kwa sababu tulikuwa tumeshaanza maandalizi. Je, Serikali iko tayari kutoa kibali hata mwishoni mwa mwaka huu tuanze Februari mwaka kesho? NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, kama nilivyosema ni Hifadhi Mseto na kama Mheshimiwa Mbunge, mwenyewe alivyogundua kwamba utaratibu wa hawa wa kuwaandikia NEMC barua ni taratibu ndefu. Lakini kwa kuwa vile vile agizo la Mheshimiwa Rais tunataka angalau kila tarafa iwe na sekondari ya A- level, mimi nawashauri Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro waweze kufikiri namna ya kutafuta vigezo vya kupandisha hadhi katika shule moja zilizopo kwenye Halmashauri sisi Wizara ya Elimu hatuna matatizo kabisa, tutatuma wakaguzi watakuja kukagua Kanda ya Kaskazini, kule Arusha watakapokuwa tayari tutatoa kibali cha kuanzisha shule moja iwe A- level katika Halmashauri hiyo.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages146 Page
-
File Size-