Toleo la 84, September-Oktoba, 2010 Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha Toleo la 164, April, 2021 ISSN 0856-874X viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

‘Aprili mbaya’ kwa wanahabari

Uamuzi wa Samia Watoa taarifa Wanahabari utadumu? kuhamasishwa kutuzwa Z’bar Uk 5 Uk 8 Uk 17 Jarida la Baraza la Habari Tanzania TAHARIRIWaliomeremeta Magazeti haya yafunguliwe agazeti manne hayapo mitaani kufuatia uamuzi wa wenye mamlaka kuyafungia Mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Jesse Mmatatu kati yao na moja kulifutia Mikofu alivyokuwa baada ya kufanyiwa leseni. unynyasaji na askari Zanzibar. Wakati April 6, 2021 Rais Samia Suluhu alipoagiza kufunguliwa vyombo vya habari na kuboresha mwenendo wa demokrasia nchini, hatua hiyo MCT, MSHINDI WA ilipokewa kwa furaha kubwa. Na katika hotuba yake ya TUZO YA IPI 2003 kwanza Bungeni April 22, 2021, FREE MEDIA alisisitiza kuwepo uhuru wa habari na kulegeza vizuizi vya PIONEER kisiasa chini ya mfumo wa siasa za vyama vingi. Hata hivyo kwa magazeti yaliyofungiwa, furaha ya kunufaika agizo la Rais ilitoweka kutokana na wenye mamlaka kufafanua baadaye kwamba magazeti hayakuwemo katika agizo hilo la Rais. Watendaji wa serikali walidai kuwa agizo la kufungulia vyombo vya habari lilihusu runinga za mtandaoni na siyo magazeti ambayo walidai yalifungiwa kwa mujibu wa sheria. Msimamo huu unaibua swali kama hizo runinga za mtandaoni zilifungiwa kinyume cha sheria? Magazeti matatu yaliyofungiwa kwa sababu tofauti na vipindi tofauti yalifanikiwa kuishinda serikali mahakamani na mahakama zikaamuru yaruhusiwe kufanyakazi tena. Hata hivyo maofisa wa serikali walikataa kutekeleza maelekezo BODI YA UHARIRI: ya mahakama hatua ambayo Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCT imeibua maswali kuhusu Hamis Mzee Mhariri utawala wa sheria na kutokujali. Gazeti lililofutiwa leseni, MAWASILIANO liliomba upya leseni lakini Kwa Maoni na Malalamiko: maofisa wa serikali wanasema Katibu Mtendaji hawaafiki orodha ya wahariri na Baraza la Habari Tanzani (MCT) wakurugenzi wa gazeti hilo. S.L.P. 10160, Dar es Salaam Kutokana na kauli zake, ni Simu: +255 22 27775728, 22 2771947 wazi Rais anataka mwanzo mpya Simu ya Kiganjani: +255 784 314880 kuhusu uhuru wa habari, uhuru Fax: + +255 22 2700370 wa kujieleza na siasa za vyama Baruapepe: [email protected] vingi. Tovuti: www.mct.or.tz Kwa hiyo, ni muhimu wenye Facebook:- www.facebook.com/ mamlaka wakaruhusu magazeti mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter. haya yafunguliwe na com/mctanzania kufanyakazi tena.

2 Toleo la 84, September-Oktoba,Toleo la 164, Aprili, 20102021 WaliomeremetaHabari ‘Aprili mbaya’ kwa wanahabari

Na Mwandishi wa Barazani kufunguliwa vyombo vya habari 2021 mjini Mwanza ambapo na kutaka kuwepo hali bora na Mkuu wa Wilaya ya kutobinywa uhuru wa habari, Nyamagana Dk. Philis akati Rais Samia Suluhu mambo yamekuwa mabaya zaidi Nyimbi, alitishia kuchukua Hassan ametoa tamko la kukiwa na matukio ya hatua dhidi ya mwanahabari kufungua ukurasa mpya kunyanyasa wanahabari Mabere Makubi wa ITV Wkatika mahusiano ya kuongezeka. ambaye alimtuhumu vyombo vya habari na serikali, uhali- Furaha ilikuwa ya muda mfupi kuandika taarifa zinazotishia sia mambo ni tofauti kabisa. na mwezi huo kugeuka kuwa ajira yake. Aprili 6, 2021 Rais aliagiza Aprili mbaya kwa wanahabari. • Aprili 12, 2021 mwandishi Wizara ya Habari, Utamaduni, Ni kinyume kabisa na akili za wa kujitegemea Sanaa na Michezo kuvifungulia kawaida kwamba mwezi huo anayeandikia gazeti la The vyombo vya habari na kuwataka ambao Rais amelegeza hali Guardian kutoka Moshi, watendaji waepuke ngumu kwa wanahabari, vyombo James Lanka alikamatwa na kuvishughulikia kwa namna vya dola ndiyo vinaonyesha kuswekwa rumande na polisi ambayo inaweza kusababisha umwamba kwa wanahabari. kwa siku tatu bila serikali kulaumiwa kwa kubinya Matukio yaliyorekodiwa katika kufunguliwa shitaka lolote na uhuru wa habari. mwezi huo ni kama ifuatavyo:- polisi haikuchukua maelezo Baraza la Habari Tanzania na • Aprili 12, 2021 waandishi yake alipofuatilia kukamatwa wadau wengine wa vyombo vya wawili , Christopher James ovyo wafanyabiashara. habari walipokea vizuri hatua kutoka ITV na Radio One na • Tukio lingine lilitokea mkoa hiyo ya mkuu wa nchi kama ni Dickson Billikwija wa Island wa Katavi ambapo hatua chanya kwa kuzingatia hali TV waliwekwa ndani kwa mwanahabari anayeandikia ngumu kwa vyombo vya habari amri ya Mkurugenzi wa kituo cha runinga cha iliyokuwepo katika kipindi cha Manispaa ya Temeke, Channel 10, Pascal Katona miaka mitano iliyopita. Lusabilo Mwakabibi, ambaye alikuwa akiandika Inashangaza sana kwamba akiwatuhumu kwa kuvamia habari za uchaguzi wa Imamu katika mwezi huo huo wa Aprili mkutano wake. wa Msikiti wa Makanyagio ambapo Rais alitoa agizo hilo la • Tukio lingine ni la April 9, Endelea Ukurasa wa 4

Wanahabari wanafanyakazi muhimu ingawa baadhi ya watendaji wa dola hupenda kuwanyanyasa.

3 Jarida la Baraza la Habari Tanzania WaliomeremetaHabari

vifungulieni na kwamba vifuate sheria. Tusitoe mwanya kuhalalisha malalamiko kuwa tunabinya uhuru wa habari na ‘Aprili mbaya’ kujieleza” Rais Samia aliagiza. Baraza , taarifa hiyo iliendelea, linashangazwa na nini kinachoendelea kutokana na unyanyasaji wa wanahabari kuendelea hata baada ya agizo la Rais, kinyume cha matarajio ya kwa wanahabari watanzania wengi. Inatoka Ukurasa wa 3 aiharibu simu yake “Tunajiuliza ni wananchi ama aliyotumia kupigia picha. maofisa ndiyo hawakumwelewa alishambuliwa na baadhi ya MCT imelaani vikali tabia hii Rais?, Baraza limehoji katika wamuni ambao ya kuwanyanyasa wananahabari taarifa yake. hawakuridhika na matokeo wanapokuwa kazini. MCT inasimamia rejista ya ya uchaguzi huo na kuharibu Katika taarifa ya Baraza kurekodi matukio mbalimbali ya zana zake za kazi. iliyotiwa saini na Katibu Mtendaji ukiukwaji wa uhuru wa habari. • Aprili 21, 2021 mjini wake, Kajubi Mukajanga na Rejista hiyo ilianzishwa 2012. Zanzibar mwandishi wa kutolewa Aprili 22, 2021, Baraza Mwaka jana jumla ya matukio 43 Mwananchi , Jesse Mikofu limevikumbusha vvyombo vya ya ukiukaji wa uhuru wa habari alishambuliwa na askari wa dola kuwa uandishi wa habari yaliorodheshwa katika kanzi JKU. Alikutwa na kadhia siyo tu ni kazi ya kisheria bali ni data. hiyo alipokuwa anapiga picha muhimu katika jamii na lazima Kwa mujibu wa rejista hiyo, askari wakiwaondoa iheshimiwe. ingawa matukio ya ukiukaji wafanyabiashara ndogondogo Mukajanga alitolea mfano uhuru wa habari ni mengi, rejista katika eneo la Darajani agizo la Rais Samia S. Hassan ina matukio yale tu ambao waliamriwa kuhamia kwa Wizara ya Habari, yaliyoripotiwa kwa Baraza ama eneo la Kibandamaiti. Askari Utamaduni, Sanaa na Michezo la kupitia vyombo vya habari. hao licha ya kumtesa kufungulia vyombo vya habari na Ukiukaji huo ni pamoja na mwanahabari huyo na kuacha kuvitisha. vitisho, mashambulizi, kunyimwa kumgalagaza kwenye dimbwi “Ninaelewa kuwa kuna vyombo habari na kufungiwa vyombo vya la maji walimuamuru vya habari mmevifungia, habari.

Waandishi wa habari wakiwa kazini.

4 Toleo la 84, September-Oktoba,Toleo la 164, Aprili, 20102021 WaliomeremetaHabari

Rais ambaye ameleta matumaini mapya kwa tasnia ya habari. wakubwa , wanasiasa na majaji ni miongoni mwa masuala makubwa yaliyotangazwa mubashara kwenye runinga. Uamuzi wa Samia Utawala wa Magufuli awali ulizuia matangazao ya runinga ya taifa TBC na baadaye kukumba pia runinga binafsi. Matangazo mubashara sasa utadumu? yamebakia kwa vikao vya asubuhi vya Bunge kipindi cha maswali na majibu, Na Mwandishi wetu upinzani wakaanza kupewa nafasi lakini mijadala haionyeshwi tena katika kurasa za mbele za magazeti, mubashara. ais Samia Suluhu Hassan ali- jambo ambalo lisingefikiriwa katika Serikali ilidai kuwa matangazo ya poagiza kufunguliwa vyombo kipindi cha miaka sita cha utawala wa mubashara yalikuwa ghali na vya habari, alifungua ukurasa Magufuli. gharama ya mwezi ilikuwa sh. bilioni Rmpya kwa tasnia. Mahusiano mabaya ya Magufuli na 4.2. Uamuzi wa Rais alioutangaza vyombo vya habari yalianza mara Bunge lilianzisha utaratibu wake katika hotuba yake iliyokuwa na baada ya alipochukua madaraka ya wa matangazo. Runinga zikawa masuala mbalimbali Aprili 6, 2021 kuendesha nchi kutoka kwa Rais zinapewa taarifa zinazochujwa kwa ilikuwa ni hatua kubwa tofauti kabisa baada ya Uchaguzi ajili ya kutumia katika taarifa zao za na mtangulizi wake hayati John Mkuu wa Oktoba 2015. habari. Pombe Magufuli, aliyesifika kwa Hatua yake ya kwanza ilikuwa ni Uchunguzi kuhusu kusitishwa kwa msimamo wake mkali dhidi ya kuzuia matangazo mubashara ya matangazao hayo mubashara ya vyombo huru vya habari. runinga ya vikao vya Bunge ambayo Bunge uliofanywa na Baraza la Kwa vyombo vingi vya habari yalivutia watazamaji wengi. Habari Tanzania (MCT) ulionyesha ambavyo viliathirika kutokana na Kashfa ya Richmond ya kuzalisha kuwa vituo vya runinga kukosa mauzo, matangazo na umeme ambayo ilimlazimisha havikupendelea utaratibu wa kupewa waangaliaji, agizo la Rais Samia Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri taarifa na picha na kitengo cha habari lilikuwa ni hatua chanya ya mkuu mwaka 2008, na kashfa ya cha Bunge kwa maelezo kwamba kuvisaidia. akaunti ya Escrow ya mwaka 2014, hazikuwa za kiwango. Ghafla, vichwa vya habari vya ambayo ililazimisha baadhi ya Mhariri mmoja miongoni mwa kusisimua vilianza kuonekana mawaziri kuachia ngazi na kwenye magazeti na viongozi wa kuwahusisha wafanyabiashara Endelea Ukurasa wa 6

5 Jarida la Baraza la Habari Tanzania WaliomeremetaHabari Uamuzi wa Samia utadumu? Inatoka Ukurasa wa 5 kadhaa waliohojiwa katika uchunguzi huo alisema kuwa walilazimika kufanya juhudi za ziada kwa kufanya mahojiano na wabunge mwishoni mwa kila kikao nje ya Bunge ili kupata kazi yenye ubora. Hata hivyo licha ya madai ya gharama kubwa, matangazo ya mubashara yamekuwa ni kwa ajili ya Rais pekee kwani popote alipoenda hata vijijini alitangazwa mubashara. Baraza lilifanya uchunguzi mwingine wakati aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipovamia kituo cha runinga cha Clouds Media usiku wa Machi 17, 2017 akiwa na watu wenye silaha. Haijabainika ni watu kutoka taasisi gani ya ulinzi. Licha ya uchunguzi huo wa MCT uliofanyika Mei mwaka huo kueleza kuwa alikiuka uhuru wa uhariri na taarifa nyinginge iliyotolewa na timu Azory Gwanda mwanahabari Erick Kabendera mwanahabari wa iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa aliyetoweka katika kipindi cha utawala kujitegemea aliyeswekwa ndani kwa Habari, Nape Nnauye, hakuna hatua wa mtangulizi wa Rais Samia Suluhu miezi saba kwa tuhuma za uhujumu iliyochukuliwa dhidi ya Makonda na Hassan inadaiwa alitwaliwa na watu uchumi kutokana na kazi yake. badala yake Nnauye alitimuliwa kazi. wasiojulikana. Mwandishi Azory Gwanda, aliyekuwa akiripoti kwa gazeti la Mwananchi alitoweka Rufiji mwaka 2017 na hatma yake haijulikani hadi leo baada ya kuchukuliwa na watu wanaodaiwa hawajulikani. Vikundi vya kutetea haki na wanaharakati walichachamaa baada ya serikali kumkamata mwanahabari Erick Kabendera kwa tuhuma zenye shaka. Baadaye alifunguliwa mashtaka ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kujihusisha na makundi ya wahalifu kabla ya kuachiwa miezi saba baadaye baada kuingia makubaliano ya kukiri na waendesha mashtaka. Ufungaji na usimamishaji vyombo vya habari hasa magazeti ulikuwa katika hali ya juu katika utawala wa Magufuli ambapo baadhi yalisimamishwa kwa siku saba hadi Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Nape Nnauye aliyetimuliwa kazi ya miezi 24 wakati mengine yalifutiwa Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwaziri wa Habari baada ya kuunda leseni. kuonyesha umwamba alivamia studio kamati kuchunguza uvamizi wa Clouds Wakati wa hotuba ya Rais Samia za Clouds Media. Media. magazeti ya Mawio, Mwanahalisi, na Mseto yalikuwa bado yamefungiwa kieletroniki – runinga na redio na kuibuka malalamiko dhidi ya licha kufanikiwa kushinda kesi zao vyombo vya mtandaoni hali si shwari kubinywa kwa uhuru wa habari. dhidi serikali mahakamani ambazo pia kwani baadhi vilitozwa faini “Tusiruhusu hii kutokea ”, Rais ziliamuru yaruhusiwe kuendelea kubwa na vingine vilisimamishwa alisema kwa kauli ya muafaka. kuchapishwa. kwa madai ya kukiuka kanuni za Hata hivyo wachunguzi Gazeti la Tanzania Daima utangazaji. wanachukulia kauli ya rais kwa limefutiwa leseni na juhudi za Katika hotuba yake Rais Samia tahadhari wakijiuliza watendaji kuomba liruhusiwe kuchapishwa alikataza tabia ya kuvinyamazisha ambao wanapenda kubinya vyombo zimekwama. vyombo vya habari kwa kueleza kuwa vya habari watatekeleza agizo hilo? Kwa vyombo vya habari vya hatua kama hizo zinatoa mwanya wa Ni suala la muda tu.

6 Toleo la 84, September-Oktoba,Toleo la 164, Aprili, 20102021 WaliomeremetaHabari Vyama vya habari vyahimizwa kuchangamkia agizo la Rais Na Mwandishi wa Barazani

yama vya habari vimetakiwa kuchangam- kia agizo la Rais Samia VSuluhu Hassan la kuvi- fungulia vyombo vya habari. Baraza la Habari Tanza nia, Jukwaa la Wahariri na vyama vingine vya masuala ya habari ni muhimu vichangamkie fursa kutokana na uamuzi wa Rais, mwanahabari veterani, mshauri, na mkufunzi Ndimara Tegambwage amesema. Akizungumza katika mahojiano ya runinga moja ya mtandaoni, Tegambwage ametahadharisha kuwa fursa hii isipotee, akieleza kuwa vyombo vya habari vidai mambo zaidi ili kuweza kutelekeleza yaliyotolewa. Kuna sheria zinazobinya vyombo vya habari na haki zingine zimekaliwa , alisema. Pia alionya kuwa vyombo vya habari visitegemee fadhila au kukumbukwa. “Nalichukulia agizo hili kama jambo muhimu na la maana katika mazingira yaliyopo… na kwa vyombo vya habari kama alivyosema Rais kwa usahihi kuwa vilifungiwa kinyume cha taratibu”, alisema. Kauli ya Rais ina nguvu kubwa, Tegambwage alisema na kuongeza kuwa ina uzito wa ziada kwa kuruhusu vyombo vya habari Mwanahabari nguli, mkufunzi na mshauri wa masuala ya Habari, Ndimara kufanyakazi tena. Tegambwage. Aliwakumbusha wamiliki wa vyombo vya habari kuwa maoni yao watapoteza jukwaa la na taarifa”. walipopewa fursa ya kuanzisha kufanya hivyo. Kutokana na agizo la chombo cha habari na kinapoanza Kutokana na kauli ya Rais, kuvifungulia vyombo vya habari, kufanyakazi, chombo hicho siyo Tegambwage ambaye alisisitiza kuna uhuru na serikali itajua chako tena bali ni cha umma umuhimu wake, alisema kuwa mahitaji ya wananchi, alisema na unaokifuatilia”. kuna kitu cha ziada ndani yake.. kuongeza kuwa vyombo vya Kama mtu akifunga chombo kutakuwa na uhuru wa kujieleza, habari vitafanyakazi bila hofu, hicho, madhila kutokana na uhuru wa watu kuzungumza. vitatafuta na kupokea taarifa na hatua hiyo hayamsibu mmiliki Aliongeza kuwa bila vyombo kufikia watu wengi ambao sauti wake peke yake bali pia na vya habari watu watanong’ona na zao zitasikika. umma. unapofunga vyombo vya habari Vyombo vya habari Unapofunga vyombo vya unawaambia wanyamaze. vichangamke, vifanyekazi bila habari, wamiliki watafunga Alisema watu wasioongeza woga na kwa weledi kwa manufaa biashara na wafanyakazi wao hawatabiriki “kama unaongoza ya watu. Waboreshe utendaji wao watapoteza ajira na waliokuwa watu kama ng’ombe unakuwa na na kuwa na vyanzo vya wakitumia chombo hicho kutoa tatizo na hata serikali haitakuwa kuaminika.

7 Jarida la Baraza la Habari Tanzania WaliomeremetaHabari

Neville Meena mmoja wa watafiti wa Ripoti kuhusu upatikanaji wa taarifa na uhuru wa habari kwa maagizo ya Baraza la Habari Tanzania, akielezea ripoti hiyo kwa washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Baraza. Watoa taarifa wahitaji kuhamasishwa - Ripoti Na Mwandishi wa Barazani habari kujibu maombi ya taarifa hizi mbili. yanayotolewa na wanahabari. Pia lishauriane na wamiliki wa MCT imetakiwa kuandaa taratibu vyombo vya habari kuhusu haja ya uhamasisha watoa habari mbalimbali ikiwemo mafunzo na kutoa fursa za mafunzo kwa waandishi kuhusu sheria ya Haki ya Ku- uragbishi kufanyia mapitio vifungu wao na vitendea kazi stahiki kama vile pata Taarifa na wajibu wa vya sheria hiyo ya haki ya kupata rekoda, kamera na makrofoni kwa Kmaofisa habari wa serikali ni taarifa na sheria nyingine sababu katika baadhi ya matukio miongoni mwa mapendekezo ya ripoti zinazohusiana na uhuru wa habari. wanahabari hukataliwa kwa kuvikosa kuhusu haki ya kupata taarifa na hali Baraza limetakiwa kuhakikisha na badala yake wanakuwa na simu za ya uhuru wa habari nchini. wanahabari na vyombo vya habari mkononi ambazo baadhi ya watoa Watoa taarifa wametajwa kwenye hasa vyombo vya habari vya jamii habari huzikataa. ripoti kufuatia utafiti ulioandaliwa na kuelewa wajibu wao na aina gani ya Kuhusu Covid-19, Baraza Baraza la Habari Tanzania (MCT) ni msaada vinavyotaka kutoka katika limetakiwa kuandaa mafunzo kwa pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu Baraza vinapokabiliwa na wanahabari kutokana na mambo wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji changamoto hasa ukiukwaji wa uhuru yatokanayo na jangwa hilo na vipi wa Wilaya. wa habari. wanaweza kujiandaa vizuri kuripoti Imeelezwa kwenye ripoti hiyo Baraza pia lishauriane na serikali majanga mengine. wakihamasishwa viongozi hao katika masuala ya haki ya kupata Baraza pia limetakiwa kuandaa watakuwa na uelewa kwamba taarifa na uhuru wa habari na haja ya jukwaa kuhusu uhuru wa habari na wanawajibika kuwaruhusu maofisa kuwa na uhusiano mzuri kati ya pande haki ya kupata taarifa.

8 Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 164, Aprili, 2021 Picha Picha UJUMBE WA MCT WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI MOROGORO Toleo la 84, September-Oktoba,Toleo la 164, Aprili, 20102021 WaliomeremetaHabari

pili kwa wanahabari kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida, Mbeya, Iringa , Dodoma and Morogoro yalifanyika Morogoro. Wanahabari wa Mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa Uragbishi wa Data unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID). MCT inatekeleza mradi huo kwa upande wa vyombo vya habari kwa kushrikiana na Pact Tanzania na mikoa 12 Freedom House. Mafunzo hayo yanafuatia utafiti kuhusu uhuru wa habari na hali ya haki ya kupata taarifa nchini. Utafiti huo ulifanyika Machi 2021 katika mikoa sita – Arusha, Dar es wahudhuria Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza na Mtwara. Akifungua mafunzo ya kwanza Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa MCT , Kajubi Mukajanga amesisitiza umuhimu wa uragbishi mafunzo ya MCT wa data kwa lengo la kurahisishwa upatikanaji taarifa. Na Mwandishi wa Barazani yoendeshwa na Baraza la Habari Tan- Alisema watafiti walipelekwa mikoa zania (MCT) kuhusu uhuru wa habari sita kufuatilia utendaji wa wanahabari na haki ya kupata taarifa. na kupata taarifa kwa misingi ya atika muda wa wiki moja Mafunzo ya kwanza yalifanyika sheria ya Haki ya Kupata taarifa. mwezi April , 2021, wana- Jijini Dar es Salaam kwa waandishi Aliwahimiza washiriki wa mafunzo habari kutoka mikoa 12 kutoka Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Kwamehudhuria mafunzo yali- Tanga na Pwani wakati mafunzo ya Endelea Ukurasa wa 10

Ofisa Programmu wa Baraza la Habari Tanzania, Saumu Mwalimu, akiwasilisha mada katika mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Baraza.

9 Jarida la Baraza la Habari Tanzania WaliomeremetaHabari

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania,Kajubi Mukajanga, akifungua mafunzo ya wanahabari yaliyoandaliwa. Wanahabari wa Mikoa 12 wahudhuria mafunzo Inatoka Ukurasa wa 9 haukuripotiwa, na alisisitiza kuwa Mtwara, Geita na Ruvuma. ushahidi unahitajika katika Katika mafunzo hayo maofisa hayo kujadili changamoto uragbishi. wawili wa Baraza , Saumu Mwalimu wanazokabiliana na fursa kwa Alisema Baraza limefanya na Paul Mallimbo waliwasilisha mada maboresho. Mukajanga pia alihimiza uchunguzi kwa matukio kadhaa ya kuhusu Sheria ya haki ya Kupata wanahabari kuripoti matukio yote ya ukiukwaji wa uhuru wa habari. Habari (ATI) na Ukiukaji wa Uhuru ukiukaji wa uhuru wa habari kwa Baraza alisema limechunguza na wa Habari Neville Meena, Katibu wa Baraza ili kuliwezesha kuyafuatilia kutoa ripoti wakati mwanahabari Jukwaa la Wahariri (TEF) alielezea kwa ufumbuzi. Daudi Mwangosi alipouawa, wakati kwa upana ripoti utafiti inayoitwa Katibu Mtendaji alizungumza hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Haki ya Kujua na kusaidia na baada ya baadhi ya washiriki kutoa Salaam alipovamia studio ya Clouds mwandishi veterani na mtafiti, David maelezo yaliyoonyesha ukiukwaji wa Media, na wakati wanahabari Mbulumi. uhuru wa habari ambao waliponyanyaswa katika mikoa ya

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatilia kwa makini wakati mafunzo hayo.

10 Toleo la 84, September-Oktoba,Toleo la 164, Aprili, 20102021 WaliomeremetaHabari

Ofisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania, Paul Mallimbo akiwasilisha mada kuhusu ukiukwaji wa uhuru wa habari Mahusiano kati ya vyanzo na vyombo vya habari ya kinafiki? Na Mwandishi wa Barazani kueleza matatizo na mahitaji yao kukumbwa na kwa wenye mamlaka. ukiukaji wa uhuru Watafiti walitumia dodoso wa habari wakiwa naweza kufikiria kuwa kukusanyia data kutoka kwa kazini kati ya 2019 mahusiano kati ya vy- wanahabari 73 ( 43 wanaume na na 2021. anzo vya habari na 25 wanawake) wa magazeti, redio, Ukiukaji huo ulijumuisha Uwaandishi wa habari ni runinga na mtandaoni wenye vitisho, kutekwa kwa zana za kazi, ya kinafiki na kwamba watoa ta- uzoefu wa miaka miwili hadi kunyimwa habari na kwa kiwango arifa hasa maofisa wa serikali wa- miaka 25. Utafiti huo ulilenga kidogo kukamatwa na polisi. naona vyombo vya habari ni kuwahoji wanahabari 60. Habari za siasa na uchumi vibaya lakini ni muhimu kush- Utaratibu wa ukusanyaji data ambazo zinakosoa serikali, irikiana navyo? ulihusu majadiliano ya mtu kwa COVID-19, kutoa nafasi kwa Hali hii ndiyo imebainishwa na mtu, majadiliano ya kikundi vyama vya upinzani , masuala ya timu ya watafiti waliotumwa na lengwa na kufuatilia kwa maswali haki za binadamu na migongano Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuhusu Uhuru wa Habari, ni aina ya habari zenye kufuatilia hali ya uhuru wa habari Upatikanaji Taarifa , Uchaguzi na changamoto na hatari kuziripoti na upatikanaji habari nchini. COVID-19. kwa majibu ya waliohojiwa. Utafiti ulifanyika Machi 14 Waandishi waliohojiwa Kwa Mtwara waandishi hadi 18, 2021 katika mikoa sita walikuwa wa vyombo vya kitaifa, walisema walikabiliwa na – Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, mikoa na jamii. Jumla ya vyombo changamoto kuandika habari za Kilimanjaro, Mwanza na Mtwara. 56 viliwakilishwa. korosho na gesi. Hata hivyo kwa wananchi wa Kuhusu uhuru wa habari, zaidi Mwandishi mmoja aliyehojiwa kawaida vyombo vya habari ni ya nusu ya watu waliohojiwa alidai kuwa aliandika habari daraja na njia wanayotumia walidai kuwa wamewahi Endelea Ukurasa wa 12

11 Jarida la Baraza la Habari Tanzania Habari Mahusiano kati ya vyanzo na vyombo vya habari ya kinafiki? Inatoka Ukurasa wa 11 vyanzo vilipendelea zaidi vyombo Lakini ni baadhi tu walipewa vikubwa vya habari vya kitaifa vitambulisho , kusababisha madai kuhusu wakulima ambao badala ya vile kwenye maeneo kuwa zoezi hilo lililenga hawajalipwa baaada ya serikali katika wilaya na vya jamii. kuwanyima vitambulisho kuchukua korosho zao. Kuhusu sheria ya Haki ya waandishi wanaohoji fursa ya Alipompigia simu Mkuu wa Kupata Taarifa, miongoni mwa kuripoti uchaguzi. Mkoa wa Mtwara kupata maelezo wanaojua kanuni za sheria hiyo Baadhi ya waliohojiwa ya upande wa serikali, Mkuu wa asilimia 15 wamesema hawapendi walilaumu vyama vya siasa hasa Mkoa alitaka kujua kama kanuni inayowapa muda wa hadi chama tawala CCM na chama mwandishi huyo anaripoti kutoka 30 watoa taarifa kujibu maombi kikuu cha upinzani Chadema kwa mkoa gani. ya taarifa kwa maelezo kuwa kubagua wanahabari walioripoti Baada ya mwandishi taarifa itakayotolewa baada ya uchaguzi. kumwambia kuwa yuko mkoa wa kipindi kirefu kama hicho itakuwa Walisema CCM ilikuwa na Mtwara, Mkuu wa Mkoa si habari tena labda pengine kwa orodha ya waandishi ambao alimwambia kama anataka makala na vipindi maalum. ingefanyakazi nao na ilikataa mtu kuendelea kubaki kufanyakazi Kuhusu upatikanaji taarifa na mwingine yeyote asiyekuwemo mkoani humo, asitangaze habari uhuru wa habari wakati wa kwenye orodha yao. Chadema hiyo. uchaguzi mkuu, majibu waziwazi ilionyesha kutowaamini Habari za kusifu serikali ikiwa yalitofautiana kulingana na wapi wanahabari kutoka vyombo vya pamoja na za uzinduzi wa miradi, na lini habari inapotokea. habari vya serikali - Daily News taarifa za kiserikali na habari za Hata hivyo, imeripotiwa kuwa na Habari Leo, na runinga na kibinadamu zinapendelewa na upatikanaji wa habari katika redio za TBC. serikali. uchaguzi mkuu wa 2020 ulikuwa Hata pale vyombo hivi Majibu kuhusu mahusiano kati mzuri wakati wa uteuzi wa ndani vilipojitahidi kupeleka waandishi ya vyombo vya habari na vyanzo ya vyama na Tume ya Uchaguzi ya kufuatana na wagombea wa yalitofautiana kwa kila mkoa Taifa (NEC) imepongezwa kwa Chadema kwa gharama zao, wakati waliohojiwa Kilimanjaro kuweka utaratibu mzuri ikiwa chama hicho kilikataa. Katika wakisema kuwa mazuri, mazuri pamoja na vituo kwa wanahabari matukio mengine Chadema kiasi Dodoma (asilimia 75) na kwenda kupata taarifa kila haikuwaalika waandishi kutoka hafifu Arusha( asilimia 28.5). wakati kuhusu mchakato wa vyombo hivyo kwenye mikutano ya Mahusiano hayo, kwa mujibu uchaguzi. waandishi. wa waliohojiwa yalibadilika kwa Mambo yalibadilika katika Waliohojiwa walisema nyakati tofauti kutegemea kipindi cha kuelekea hatua za haikuwa rahisi kwa vyombo vyao maudhui na jinsi ya vyanzo mwisho za kampeni, kupiga kura, kufanya uchambuzi wa mchakato vinavyoripotiwa katika vyombo kuhesabu kura na utangazaji wa wa uchaguzi kwa sababu maofisa vya habari. matokeo ya uchaguzi. Kufungwa wa chama tawala walikataa Mahusiano yanaboreka wakati kwa intaneti kuliathiri zaidi mialiko kushiriki vipindi kuhusu vyanzo vikiripotiwa vizuri kwenye vyombo vya habari vya mtandaoni uchaguzi, zaidi kutokana na hofu. vyombo vya habari. Asilimia 75 ya ambavyo vilitegemea kupata Pia ilikuwa hatari kualika waliohjiwa Mwanza walisema taarifa kwa njia hiyo na kuzitoa. baadhi ya wagombea wakiwemo mahusiano ni ya kinafiki. Wasiwasi mwingine wa upinzani kwa mahojiano ya Katika matukio ambapo ulionyeshwa na watu waliohojiwa habari na uchambuzi kwa kuwa mahusiano kati ya vyanzo na ni kuwa mwongozo wa kuripoti walikuwa wanatumia lugha kali vyombo vya habari ni hafifu , uchaguzi wa NEC ulibana sana. wakati wa kampeni. asilimia 80 wamesema hali hiyo Vyombo vya habari Aidha, waliohojiwa wengine inatokana na hofu ya watoa habari viliruhusiwa tu kuripoti taarifa za walisema kulikuwa na hofu kwamba watapoteza kazi na hivyo maofisa a NEC. Taarifa zingine katika vyombo vyao kutoa muda kuamua kutotoa habari hasa pale zote hazikuruhusiwa. sawa kwa wagombea wa upinzani masuala yenyewe yakiwa nyeti na Pia walilalamika kuwa ni kuhofia kuonekana na wenye hasi. waandishi wachache tu ndiyo mamlaka kuwa wanasaidia ama Kiasi cha asilimia 15% ya waliruhusiwa kuripoti habari za wanakampeni kwa upinzani, na waliohojiwa wameeleza uchaguzi tofauti na chaguzi hiyo inaweza kuwagharimu. mahusiano hafifu kwa upande wa zilizopita. Waliohojiwa pia walitaja baadhi vyanzo vya habari ni kutojua NEC iliagiza vyombo vyote vya ya matukio ya ukiukaji wa uhuru sheria ya haki ya kupata taarifa habari kuwasilisha majina ya habari wakati wa uchaguzi. Kwa na kwa upande wa wanahabari ni waandishi watakaoripoti uchaguzi mfano, wahariri wawili wa Daily udhaifu wa weledi na maadili. wa 2020 ili wapatiwe News walisema walipata vitisho Kulikuwa pia na madai kuwa vitambulisho. Endelea Ukurasa wa 14

12 Toleo la 84, September-Oktoba,Toleo la 164, Aprili, 20102021 WaliomeremetaHabari

taaluma yaliyowekwa na tasnia yenyewe na kuendelea kuwa na mshikamano. Uhuru unakwenda pamoja na MCT yapongeza uwajibikaji hivyo wanahabari lazima wazingatia taaluma na maadili ya uandishi, alisema Mukajanga. Kufuatia agizo la Rais Samia , agizo la Rais Samia Baraza limewasihi viongozi waliopewa majukumu ya Na Mwandishi wa Barazani mengi. kusimamia vyombo vya habari Hotuba hiyo iliyotolewa wakati kulitekeleza bila visingizio kama wa kuapishwa kwa Makatibu ilivyotokea kwa vyombo vya habari adau wa Habari Wakuu , Manaibu Makatibu vilivyoishinda serikali wameeleza kuvutiwa na Wakuu na wakuu wa mashirika ya mahakamani na kuruhusiwa hatua ya Rais Samia umma imeinua matumaini, kufanyakazi lakini mpaka sasa WSuluhu kuagiza wenye alisema Mukajanga. bado vimefungiwa. mamlaka kuachana na tabia ya Alisema hotuba hiyo pia inaweka Wakati Baraza linachukulia kwa kufungia na kusimamiasha maandalizi ya marekebisho ya uzito agizo la serikali kwa vyombo vyombo vya habari, tabia ambayo sheria za vyombo vya habari na vya habari kuzingata sheria na aliyoieleza ni ya “umwamba”. kanuni zao na kuzirekebisha ili kanuni , limewataka watendaji wa “Tumefurahishwa na hatua taifa liwe taifa linalozungumza. Baraza kuwashirikisha wadau hiyo”, Kajubi Mukajanga ambaye Licha ya hotuba hiyo yenye katika mchakato wa kuandaa ni Katibu Mtendaji wa Baraza la matumaini, MCT imewakumbusha sheria na kanuni zake Habari Tanzania (MCT) alisema wanahabari kuwa ngao yao nzuri kuhakikisha zinakwenda sawa na katika taarifa kufuatia hotuba ya dhidi ya ukiukwaji wa uhuru wa Rais ambayo ilihusu masuala habari ni kuzingatia maadili ya Endelea Ukurasa wa 14

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga.

13 Jarida la Baraza la Habari Tanzania WaliomeremetaHabari Mahusiano kati ya vyanzo na vyombo vya habari ya kinafiki? Inatoka Ukurasa wa 12 alipokuwa akijiandaa kuripoti umma idadi ya walioathirika kuhusu mila za Wamasai ambapo katika mikoa yao ili wachukue kutoka kwa vyanzo vya habari wazee wa kabila hilo tahadhari au kuepusha taharuki wakati wa kampeni za uchaguzi walimwambia hawatoi habari hizo isiyo lazima. lakini hata hivyo hawakudhurika. kwa mwanamke. Vyombo vya habari Wakati wa kutangaza matokeo Mjini Mwanza, mhariri mmoja havikuruhusiwa kufanya ya uchaguzi ya wabunge wa alisema siku ya uchaguzi uchunguzi, kuhoji kutafuta habri majimbo ya Tandahimba, hakuwatuma waandishi zaidi. Vilitakiwa kuripoti Nanyumbu na Mtwara Mjini, wanawake kwa sababu za walichoambiwa na maofisa waandishi wachache kiuslama kutokana na hofu kuwa waliopewa jukumu hilo. waliruhusiwa kuripoti. zoezi hilo lingechukua muda Waliohojiwa walitaja baadhi ya Mjini Arusha kulikuwa na mwingi zaidi. athari ya utangazaji hafifu wa taarifa za polisi kutwaa kamera Kuhusu Covid-19, wahojiwa COVID-19 ni kuibuka taarifa za wanahabari watatu na kufuta wengi walisema upatikanaji wa zisizo kweli na za kutatanisha picha, wakati mwandishi mmoja taarifa kuhusu COVID-19 kwa umma na kukana uwepo wa alikamatwa kwa amri ya ulikuwa mzuri wakati mgonjwa ugonjwa na matokeo yake Kamanda wa polisi wa Mkoa. wa kwanza wa ugonjwa huo kuongezeka maambukizi. Radio ya Sunrise FM ya Arusha alipobainika nchini mapema Kuhusu matokeo ya habari za pia iliathirika wakati wa uchaguzi Machi, 2020. COVID-19 kutolewa na watu ilipoamriwa kusimamisha Serikali ilikuwa inatoa taarifa watatu tu (Waziri Mkuu, Waziri matangazo wakati wa kutangaza kila wakati hadi mwishoni mwa wa Afya na Msemaji wa Serikali), matokeo ya uchaguzi. Aprili 2020 iliposimama. wote waliohojiwa walisema hiyo Kulikuwa na tukio Mwanza Hata hivyo asilimia 88 ya ilikwaza upatikanaji taarifa kwa ambapo polisi walilazimisha waliohojiwa walisema kuwa kuwa kama watu hao wanahabari waliopiga picha ya vyombo vya habari havikuweza hawakuzungumza hakukuwa na mwanamke aliyetuhumiwa kutimiza wajibu wao kama taarifa yoyote iliyotolewa na kukutwa na karatasi feki za kura, ilivyotarajiwa kwa sababu umma uliathirika. kuzifuta picha zote. waandishi hawakuweza kupata Kuhusu athari za COVID-19 Asilimia 91.4% ya waliohojiwa taarifa za kuaminika kutoka kwa vyombo vya habari, asilimia wote wamesema kuwa kila vyanzo vya kuaminika na kufanya 80% ya waliohojiwa walikubaliana waliponyimwa habari hawakuona washindwe kuandika kwa upana kwamba tasnia ya habari hiyo imetoka na jinsi yao. kuhusu ugonjwa huo, ambao ni iliathirika kutokana na janga hilo Mtu mmoja Arusha alisema mpya kwao. ambapo mishahara ya wakati mmoja alikataliwa kupewa Waliohojiwa walifikiri kwamba wafanyakazi ilipunguzwa na taarifa kwa sababu ya jinsi yake ingekuwa vizuri kufahamisha wengine kuachishwa kazi. MCT yapongeza agizo la Rais Samia

Inatoka Ukurasa wa 13 Mashariki baada ya vifungu 16 vya kufanyakazi kwa karibu na serikali Sheria ya Huduma ya Habari katika shughuli za ujenzi wa taifa katiba ya nchi. kuonekana kukwaza kanuni za kwa kuzingatia utawala bora na Sheria na kanuni mbaya demokrasia za uhuru wa kujieleza utawala wa sheria. zitafifisha nia njema ya rais na na uhuru wa habari. Mpaka sasa, Washirika katika CoRI ni vyombo vya habari vilivyofungiwa uamuzi huo haujatekelezwa. Twaweza, Kituo cha Sheria na na vitafungiwa tena katika muda Baraza limeitaka serikali Haki za Binadamu (LHRC),Chama mfupi kutokana udhaifu wa kutekeleza uamuzi huo na cha Waandishi Habari Wanawake sheria. limeeleza utayari wake Tanzania (TAMWA), Chama cha Baraza limeikumbusha serikali kushirikiana na mamlaka kwa Wanasheria (TLS), Sikika, Policy kuhusu uamuzi wa mahakama ya kuwa “ sote tunajenga nyumba Forum, Jukwaa la Wahariri ya Afrika Mashariki wa Machi 28, moja”. Tanzania (TEF), MISA-Tan, TCIB, 2019 ambao uliamuru serikali Baraza na washirika wake Umoja wa Watetezi wa Haki za kurekebisha sheria kulingana na katika Umoja wa Haki ya Kupata Binadamu Tanzania (THRDC) Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Taarifa (CoRI) limeahidi Jamii Forum na MCT.

14 Toleo la 164, Aprili, 2021 Habari Mkanganyiko waibuka agizo la Rais la kufunguliwa magazeti Na Mwandishi wa Barazani

ara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza kufunguliwa Mkwa vyombo vya habari, kumeibuka mkanganyiko wa vyombo vipi vinavyostahili kufunguliwa. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dk. Hassan Abbasi aliripotiwa kueleza kuwa Rais alimaanisha kufungulia runinga za mtandaoni na siyo magazeti. Mkanganyiko ulizidishwa zaidi na kauli ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa alipoungana na mtazamo wa Dk. Abbasi. Suala hilo lilitulizwa kiana na Waziri wa Habari alipoawaalika wenye magazeti yaliyofungiwa kukutana naye kujadili suala hilo. Kwa kuamini kwamba kuna nia njema kutokana na agzio la Rais, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga amewashauri wamiliki wa magazeti yaliyofungiwa kuitikia mwito wa Waziri Bashungwa. Mukajanga, alieleza katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Ujerumani DW, Endelea Ukurasa wa 16

Waziri wa Habari Innocent Bashungwa

15 Jarida la Baraza la Habari Tanza- nia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dk. Hassan Abbasi

Mkanganyiko waibuka agizo la Rais

Inatoka Ukurasa wa 15 kuwa inashangaza kujaribu kutatua tatizo kwa kutumia sheria na kanuni zilizosababisha kuwepo tatizo hilo. “Tunachosema hapa ni kwamba huwezi kushughulikia tatizo la kubinywa kwa uhuru wa habari kwa kutumia sheria na vifungu zilizoandaliwa makusudi kukwaza haki ya kupata taarifa na uwezo wa wanahabari kufanyakazi kwa uhuru na kitaaluma. ” Baadhi ya vifungu, Mukajanga alisema mahakama imevieleza kuwa havifai na Mahakama ya Afrika Mashairiki imeitaka serikali kufanyia marekebisho vifungu 16 vya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016. Kwa hiyo ,amesema , kujadili suala hili kwa kutumia kanuni hizo hizo na sheria ni tatizo. Baadhi ya magazeti yaliyofungiwa ni Mawio, Mwanahalisi, na Mseto wakati Tanzania Daima imefutiwa leseni na Msajili wa Magazeti. Baadhi ya magazeti haya yalifanikiwa kuishinda serikali mahakamani na kuamriwa kuwa yafunguliwe lakini serikali imekaidi. Mmiliki wa Mwanahalisi na Mseto, Saed Kubenea tayari amekutana na Waziri wa Habari. Mmiliki wa Mawio, Simon Mkina alisema amepanga kwenda Dodoma kukutana na Waziri. Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa.

16 Toleo la 164, Aprili, 2021 Habari

Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakipitia kijitabu kilichorahisisha sheria ya Haki Kupata Taarifa. Waandishi Zanzibar kupewa tuzo Na Mwandishi wa Barazani • Uandishi wa habari za rushwa • Matokeo baada ya kutoka naUwajibikaji habari au kipindi • Uandishi wa habari za Serikali • Uwasilishaji wa mada husika anahabari Zanzibar ya Umoja wa kitaifa. • Mpangilio wa mada watapewa tuzo za • Uandishi wa habari za kulipa • Ufasaha na mtiririko wa lugha umahiri na weledi wa kodi • Kuzingatia maadili ya uandishi Wuandishi wa habari Kamati ya maandalizi wa habari katika kuadhimisha Siku ya imewaalika waandishi wa habari • Weledi na matumizi ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kukusanya kazi zao au kuandika takwimu. Duniani mwaka huu. katika maeneo hayo na • Kipindi chaRedio na runinga Kwa kuwa Mei 3, ambapo siku kuziwasilisha kwa wakati. kisizidi dakika 30 na pia sauti hiyo huadhumishwa imeangukia Habari zitakazochukuliwa ni za na picha ziwe katika ubora katika kipindi cha Mfungo wa uchunguzi, makala au vipindi vya unaostahiki. Mwezi Mtukufu wa Ramadhani redio na runinga. • Kipindi au makala Zanzibar itaadhimisha siku hiyo Vigezo muhimu vya kuzingatia iliyochapishwa au kurushwa Mei 23, 2021. katika kazi zinazoshindanishwa na chombo cha habari chochote Waandaaji wa tuzo hizo za ni: hapa Tanzania kuanzia wanahabari wamesema kuwa • Ubora wa kazi iliyowasilishwa Januari 2021 hadi Mei, 2021 zitahusisha kazi katika maeneo • Upekee wa mada Kazi ziwasilishwe katika ofisiya matano yafuatayo: • Umuhimu wa kuzingatia Jumuiya ya Waandishi wa Habari uwiano sawa wa jinsia. za Maendeleo Zanzibar • Uandishi wa habari za uchumi • Vyanzo vingi vya habari (WAHAMAZA) iliopo Weles wa buluu vilivyojitawanya. kuanzia Aprili 15 hadi Mei 1, • Uandishi wahabarizaJinsia • Ubunifu wa mada husika. 2021.

17