13 Aprili, 2012 1 Bunge La Tanzania

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

13 Aprili, 2012 1 Bunge La Tanzania Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) 13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Nne – Tarehe 13 Aprili, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na ratiba ya Mkutano wetu wa Saba wa Bunge ambao leo ni kikao cha Nne, Katibu. MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge leo hatuna Hati za Kuwasilishwa Mezani kwa hiyo tunaenda moja kwa moja kwenye maswali yaliyopo kwenye Ratiba ya Shughuli za leo na swali la kwanza linaenda ofisi ya Waziri Mkuu na litaulizwa na Mhehsimiwa Rukia Kassim Ahmed Mbunge wa Viti Maalum. Na. 39 Shule ya Kolo kuwa na Wanafunzi watatu Kidato cha Nne MHE. RUKIA K. AHMED aliuliza:- Kukosekana kwa walimu wa kutosha, vifaa vya maabara na mazingira magumu katika shule ya Sekondari ya Kolo- Wilaya ya Kondoa kumesababisha wanafunzi wengi kuacha 1 13 APRILI, 2012 shule na kubakiwa na wanafunzi watatu (3) tu katika Kidato cha Nne:- (a) Je, Serikali inawasaidiaje wanafunzi hao waliokumbwa na kadhia hiyo? (b) Je, Serikali haioni kwamba wanafunzi hao wana haki ya kupata elimu kama wanafunzi wengine? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a)Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zilizopo kuhusu walimu na wanafunzi katika shule ya Sekondari Kolo kwa kipindi cha miaka minne ni kama ifuatavyo:- Mwaka 2008 shule ilikuwa na walimu 5 na wanafunzi 36, mwaka 2009 shule ilikuwa na walimu 3 na wanafunzi 28, mwaka 2010 shule ilikuwa na walimu 5 na wanafunzi 26, mwaka 2011 shule ilikuwa na walimu 7 na wanafunzi 25. Kwa sasa shule hii ina jumla ya walimu 10 kwa takwimu hizi hakuna mwaka ambao shule hiyo ilikuwa na wanafunzi watatu. (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua haki ya watoto kupata elimu na hivyo imekuwa inahakikisha kuwa wanafunzi wa shule zote nchini ikiwemo Kolo wanapata elimu kwa kuzingatia sheria na miongozo inayotawala utoaji wa elimu nchini. Serikali pia imekuwa ikihakikisha wanafunzi wote nchini wakiwemo wa Kolo wanapata huduma ua elimu ipasavyo kwa kupanga walimu pamoja na uboreshaji miundombinu ya shule. Aidha, Serikali inatambua kuwepo 2 13 APRILI, 2012 shule ya Sekondari ya Changaa iliyokuwa na wanafunzi watatu wa kidato cha nne mwaka 2011. Mheshimiwa Spika, shule ya Changaa iliyoanza mwaka 2006 ilikuwa na wanafunzi 22 waliosajiliwa kidato cha kwanza mwaka 2008, kati ya hao, wanafunzi 3 waliacha shule kwa utoro mwaka 2010 na wanafunzi 16 walihamia katika shule ya sekondari ya Ula mwaka 2009 na mwaka 2010 na hivyo kubakia na wanafunzi 3. Serikali kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi hawa watatu kupata elimu ipasavyo iliwasaidia kwa kuwahamishia katika shule ya sekondari ya Ula ambako walifanyia mtihani wa kidato cha Nne mwaka 2011. Mwaka huu shule hii imepangiwa walimu wanne, wawili wamesharipoti na hivi sasa ina jumla ya walimu watano. Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wito kwa Mheshimiwa Mbunge kuendelea kuwahamasisha wananchi wa Halmashauri kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu za kutosha pamoja na majengo mengine ili kuwavutia walimu kwa kuwa na mazingira bora ya kuishi na kufundishia. MHE. RUKIA K. AHMED: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. (a)Je, Serikali haioni kama kukosekana kwa elimu katika baadhi ya Wilaya ni kudumaza Wilaya hiyo kimaendeleo? (b) Je, Serikali haioni kama iko haja ya kuongezewa mishahara walimu pamoja na mafao mengine ili nao waweze kuhamasika na wasomeshe watoto vizuri? NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU-ELIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kukosekana kwa elimu baadhi ya Wilaya hili kwa sasa limeshafanyiwa kazi kwa sababu kila Wilaya ina shule za Msingi zilizo katika kila Kijiji na hata kitongoji kilicho kikubwa katika Wilaya zetu. 3 13 APRILI, 2012 Lakini pia tuna shule za Sekondari sasa katika kila Kata na sasa tuna jumla ya sekondari 3242 kwa Kata zote nchini ambazo zina uwezo wa kupokea vijana kutoka shule za msingi zilizopo ndani ya Kata yenyewe. Hii ina maana kwamba Serikali imepania kutoa elimu katika kila Wilaya katika shule zake za msingi na Sekondari. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili la uongezaji wa mishahara ni kweli kwamba hata mimi nilipokuwa nafanya ziara kwenye Wilaya mbalimbali nchini na kukutana na Walimu, nilipokuwa natoa nafasi ya wao kuchangia katika uboreshaji wa elimu hiyo ilikuwa ni moja ya hoja zao ambazo wanazieleza na Serikali tumelichukua, na kwa bahati nzuri sana Walimu wameshafikisha ombi hili kwa Rais kupitia Chama cha Walimu Tanzania na Rais aliwaahidi kwamba analichukua analifanyia kazi na anaweza kufanyia kazi hilo kadri fedha za Serikali zinavyoweza kupatikana ili pia kuboresha sekta hii na kuwafanya walimu waweze kufanya kazi yao vizuri. Ahsante sana MHE. AMOS G. MAKALA: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante kwa kuniona. Naomba kumwuliza Waziri kwamba matatizo yaliyopo katika Sekondari ya Kolo yapo katika sehemu kubwa sana ya Tanzania na hasa Jimbo la Mvomero ukizingatia kwamba hatuna walimu wa kutosha kuna walimu watatu tu katika sekondari moja hasa Unguru Mascat walimu wanne na maeneo mengi katika Tarafa ya Mgeta; Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu kuongeza walimu wa kutosha kupitia Bunge hili? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) : Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya jitihada za kutosha za kuongeza idadi ya walimu nchini ili kusaidia kupunguza ugumu wa kazi ya 4 13 APRILI, 2012 walimu waliopo sasa kwa kuwaongezea idadi ya walimu ili wafundishe kwa urahisi na kufanyakazi zao kwa urahisi zaidi. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2011 Serikali iliajiri walimu 9226 wakiwepo wa Shule za Msingi na Sekondari na wote tuliwasambaza nchi nzima, mwaka huu tumeongeza idadi hiyo mara tatu zaidi kwamba tumeajiri walimu 24,621 walimu wa shule za msingi kati ya hao ni 11,379 na pia walimu 13242 ni wa sekondari. Na walimu wote wameshasambazwa nchi nzima na kufikia mwezi Machi tarehe 30 mwaka huu, walimu 21,681 wamesharipoti kwenye vituo mbalimbali. Walimu wa shule za msingi kati ya hao 10,491 wamesharipoti na walimu 11,190 wamesharipoti kwenye shule mbalimbali za sekondari nchini. Mpango huu wa ajira utaendelea kuongezeka kadiri ambavyo wamedahiliwa kupata mafunzo ya ualimu kwenye Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ualimu nchini ili kuongeza idadi ya Walimu na kuweza kupunguza mzingo kama nilivyosema wa Walimu waliopo sasa. Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi ni jitihada ya Serikali ya kuweza kuboresha sekta ya elimu na walimu hawa ni pamoja na wale ambao tumewapeleka Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. MWENYEKITI: Itakuwa ni vizuri kama orodha hiyo Naibu Waziri ikasambazwa kwa Wabunge wote ili waweze kuona mgawanyo wao na kwa kila Wilaya na namna matatizo yalivyobaki katika Wilaya angalau kila Mbuneg aweze kujua mwenendo wa tatizo hilo kwenye Wilaya yake. (Makofi) NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU-ELIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, orodha hiyo itapatikana kufikia saa saba mchana. MWENYEKITI: Nakushukuru sana tunaendelea na swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa Said Mohammed Mtanda, Mbunge wa Mchinga. 5 13 APRILI, 2012 Na. 40 Ahadi ya Ujenzi wa Daraja Kati ya Mchinga I na Mchinga II MHE. SAID M. MTANDA aliuliza:- Mheshimiwa Rais wa nchi aliahidi ujenzi wa daraja la kuunganisha Mchinga I na Mchinga II:- (a) Je, ujenzi huo utaanza lini? (b) Je, ni fedha kiasi gani zitatumika kwa kazi yote hadi kukamilika kwa daraja? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda, Mbunge wa Mchinga, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mhehsimiwa Rais aliahidi kujenga daraja kuunganisha Mchinga I na Mchinga II kutokana na adha wanayoipata wananchi wa maeneo hayo. Eneo hilo ni Mkondo wa bahari ambao hujaa maji katika miezi ya Agosti hadi Novemba kuanzia saa 10 jioni hadi saa 2 usiku ( highest tide mark ) ambazo kule wanaziita Bamvua. Kwa kuzingatia ahadi hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi imekamilisha usanifu wa daraja hilo ili kazi ya ujenzi iweze kuanza. Kazi ya ujenzi imepangwa kuanza katika mwaka wa fedha 2012/2013. 6 13 APRILI, 2012 (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, usanifu uliofanyika umebainisha kwamba zinahitaji shilingi 380,294,000/- ili kukamilisha ujenzi wa daraja hilo hadi kutumika. Fedha hizi zimeombwa na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi katika bajeti ya 2012/2013 kupitia maombi maalum. MHE. SAID M. MTANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza niishukuru Serikali kwa kuanza kutekeleza baadhi ya ahadi ambazo zilitolewa katika kipindi cha uchaguzi uliopita katika Jimbo langu. Lakini nina swali dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa tayari Serikali imepokea maombi lakini Serikali haijasema wazi kwamba maombi hayo yamekubaliwa ili kuwaondoa hofu wananchi wa Jimbo la Mchinga hususani watumiaji wa barabara ile inayotoka Mchinga I, II hadi kule Kijiweni kwamba maombi haya yamekubaliwa na sasa wananchi wakae tayari kusubiri utekelezaji wake katika kipindi hiki cha mwaka 2012/2013. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa niaba ya Serikali mimi naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Mtanda kwa kutoa shukrani kwa sababu ameonesha na neno la Mungu linasema shukuruni kwa kila jambo. Amekuwa mkweli hapa maana yake nilifikiri kwamba hatasema ukweli, Rais alipokwenda pale katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi alitoa ahadi mbili, ahadi ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kituo cha afya cha Kitomanga, zimejengwa wodi mbili pale na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, amekwenda pale akaenda kuzindua na kufungua kituo kile kwa maana ya hizo wodi mbili. Kwa hiyo, anavyoshukuru hapa namwelewa. 7 13 APRILI, 2012 Pia nimshukuru pia Mheshimiwa Mtanda kwamba ni Mbuneg makini ambaye anafuatilia sana masuala haya yanayohusu Jimbo lake la Uchaguzi, kila siku asubuhi ukiamka unamkuta pale kwangu mpaka inafika mahali namwambia Mtanda sasa inatosha.
Recommended publications
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who Will Benefit from the Gas Economy, If It Happens?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013 Who will benefit from the gas economy, if it happens? Supported by: 2 TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? ACKNOWLEDGEMENTS Policy Forum would like to thank the Foundation for Civil Society for the generous grant that financed Tanzania Governance Review 2013. The review was drafted by Tanzania Development Research Group and edited by Policy Forum. The cartoons were drawn by Adam Lutta (Adamu). Tanzania Governance Reviews for 2006-7, 2008-9, 2010-11, 2012 and 2013 can be downloaded from the Policy Forum website. The views expressed and conclusions drawn on the basis of data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. TGRs review published and unpublished materials from official sources, civil society and academia, and from the media. Policy Forum has made every effort to verify the accuracy of the information contained in TGR2013, particularly with media sources. However, Policy Forum cannot guarantee the accuracy of all reported claims, statements, and statistics. Whereas any part of this review can be reproduced provided it is duly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. ISBN:978-9987-708-19-2 For more information and to order copies of the report please contact: Policy Forum P.O. Box 38486 Dar es Salaam Tel +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] Suggested citation: Policy Forum 2015.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 22 Juni, 2021 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Hamsini na Sita na kabla hatujaendelea nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wasaidizi wangu wote wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa David Kihenzile, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Najma kwa kazi nzuri ambayo wameifanya wiki nzima kutuendeshea mjadala wetu wa bajeti. (Makofi) Sasa leo hapa ndio siku ya maamuzi ambayo kila Mbunge anapaswa kuwa humu ndani, kwa Mbunge ambaye Spika hana taarifa yake na hatapiga kura hapa leo hilo la kwake yeye. (Makofi) Katibu. NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali na tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 465 Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri Katika Mji wa Laela MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Sumbawanga katika Mji wa Laela baada ya agizo la Serikali la kuhamisha Makao Makuu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu la watu wa Kwela, Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 30 zilizohamia kwenye maeneo mapya ya utawala mwaka 2019.
    [Show full text]
  • Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Nne – Tarehe 9 Mei, 2014 (Mkutano Uianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA) PAMOJA NA (UTAWALA BORA): Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) pamoja na (Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU): Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. JAKU HASHIM AYOUB (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Taarifa ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora) pamoja na (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na maoni 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA), (UTAWALA BORA) PAMOJA NA (MAHUSIANO NA UTARATIBU):- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora) pamoja na (Mahusiano na Uratibu) kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hizo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza Maswali na Ofisi ya Waziri Mkuu.
    [Show full text]
  • 1447734501-Op Kikao
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA ORODHA YA SHUGHULI ZA LEO MKUTANO WA KWANZA KIKAO CHA KWANZA 17 NOVEMBA, 2015 ORODHA YA SHUGHULI ZA LEO _________________ MKUTANO WA KWANZA KIKAO CHA KWANZA – TAREHE 17 NOVEMBA, 2015 Kikao Kuanza Saa Tatu Kamili Asubuhi I. TANGAZO LA RAIS LA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE: II. UCHAGUZI WA SPIKA: III. KIAPO CHA UAMINIFU NA KIAPO CHA SPIKA: IV. WIMBO WA TAIFA NA DUA KUSOMWA: V. KIAPO CHA UAMINIFU KWA WABUNGE WOTE: DODOMA DKT. T. D. KASHILILAH 17 NOVEMBA, 2015 KATIBU WA BUNGE 2 1. Mhe. George Mcheche Masaju 2. Mhe. Andrew John Chenge 3. Mhe. Mary Michael Nagu, Dkt. 4. Mhe. William Vangimembe Lukuvi 5. Mhe. Richard Mganga Ndassa 6. Mhe. Tulia Ackson, Dkt. 7. Mhe. Abbas Ali Hassan Mwinyi, Capt. 8. Mhe. Abdallah Ally Mtolea 9. Mhe. Abdallah Dadi Chikota 10. Mhe. Abdallah Haji Ali 11. Mhe. Abdallah Hamis Ulega 12. Mhe. Abdul-Aziz Mohamed Abood 13. Mhe. Agnes Mathew Marwa 14. Mhe. Adadi Mohamed Rajab, Balozi. 15. Mhe. Ahmed Ally Salum 16. Mhe. Ahmed Juma Ngwali 17. Mhe. Ahmed Mabkhut Shabiby 18. Mhe. Aida Joseph Khenan 19. Mhe. Aisharose Ndogholi Matembe 20. Mhe. Ajali Rashid Akbar 21. Mhe. Upendo Furaha Peneza 3 22. Mhe. Joseph Leonard Haule 23. Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi 24. Mhe. Albert Obama Ntabaliba 25. Mhe. Alex Raphael Gashaza 26. Mhe. Ali Hassan Omar, King 27. Mhe. Ali Salim Khamis 28. Mhe. Allan Joseph Kiula 29. Mhe. Ally Mohamed Keissy 30. Mhe. Ally Saleh Ally 31. Mhe. Ally Seif Ungando 32. Mhe. Almas Athuman Maige 33. Mhe.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Arobaini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 15 Juni, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, tunaendelea na Mkutano wetu wa 19, Kikao cha 46, bado kimoja tu cha kesho. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na: NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 (Monetary Policy Statement for the Financial Year 2020/2021). MHE. ALBERT N. OBAMA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI:Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. RHODA E. KUNCHELA - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). MHE. DKT. TULIA ACKSON - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KANUNI ZA BUNGE: Azimio la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Bunge SPIKA: Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika, Katibu MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 426 Migogoro ya Mipaka MHE.
    [Show full text]
  • Kitabu Cha Kumbukumbu Za Wabunge
    BUNGE LA TANZANIA ____________ KITABU CHA KUMBUKUMBU ZA WABUNGE BUNGE LA KUMI NA MBILI Toleo la Pili - Machi, 2021 1 SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Bunge limekuwepo toka tupate Uhuru mwaka 1961 na kabla ya Uhuru kuanzia mwaka 1926. Wabunge nao wameendelea kuwepo kwa vipindi tofauti na kwa idadi inayobadilika kila wakati wakitekeleza wajibu wao muhimu wa kutunga sheria na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Bunge lilipoanza mwaka 1926, Wabunge walikuwa ishirini na moja (21) na mwaka 1961 ulipopatikana Uhuru Wabunge waliongezeka kufikia themanini (80) na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 idadi ya Wabunge iliongezeka na kufikia Wabunge 357. Hata hivyo, baada ya Tume ya Uchaguzi kuona umuhimu wa kuongeza idadi ya majimbo kutokana na sababu mbalimbali sasa hivi idadi ya Wabunge ni 393. Kitabu hiki cha Kumbukumbu za Wabunge kimegawanyika katika Sehemu kuu Kumi na Nne. Katika sehemu hizo, kitabu kimeorodhesha Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na anuani zao, namba zao simu za mkononi na majimbo au aina ya uwakilishi wao Bungeni chini ya picha zao ili kurahisisha mawasiliano. Katika mchanganuo wa kila sehemu, Sehemu ya Kwanza ni Utangulizi. Aidha, Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge ambao ndio wasimamizi wa shughuli za Bunge wameorodheshwa katika Sehemu ya Pili ya kitabu hiki ikifuatiwa na Uongozi wa Ofisi ya Bunge katika Sehemu ya Tatu. 2 Sehemu ya Nne imeorodhesha Wabunge wote wa Majimbo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mikoa ikifuatiwa na Sehemu ya Tano ambayo imeorodhesha Wabunge wote wa Viti Maalum kulingana na uwakilishi wa vyama vyao Bungeni ikianzia na Chama cha Mapinduzi (CCM) na ikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Sehemu ya Sita imeorodhesha Wabunge kupitia nafasi ya Kuteuliwa na Rais na Sehemu ya Saba itaorodhesha Wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi.
    [Show full text]
  • Kitabu Cha Kumbukumbu Za Wabunge
    BUNGE LA TANZANIA ____________ KITABU CHA KUMBUKUMBU ZA WABUNGE BUNGE LA KUMI NA MBILI Toleo la Tatu - Aprili, 2021 1 SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Bunge limekuwepo toka tupate Uhuru mwaka 1961 na kabla ya Uhuru kuanzia mwaka 1926. Wabunge nao wameendelea kuwepo kwa vipindi tofauti na kwa idadi inayobadilika kila wakati wakitekeleza wajibu wao muhimu wa kutunga sheria na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Bunge lilipoanza mwaka 1926, Wabunge walikuwa ishirini na moja (21) na mwaka 1961 ulipopatikana Uhuru Wabunge waliongezeka kufikia themanini (80) na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 idadi ya Wabunge iliongezeka na kufikia Wabunge 357. Hata hivyo, baada ya Tume ya Uchaguzi kuona umuhimu wa kuongeza idadi ya majimbo kutokana na sababu mbalimbali sasa hivi idadi ya Wabunge ni 393. Kitabu hiki cha Kumbukumbu za Wabunge kimegawanyika katika Sehemu kuu Kumi na Nne. Katika sehemu hizo, kitabu kimeorodhesha Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na anuani zao, namba zao simu za mkononi na majimbo au aina ya uwakilishi wao Bungeni chini ya picha zao ili kurahisisha mawasiliano. Katika mchanganuo wa kila sehemu, Sehemu ya Kwanza ni Utangulizi. Aidha, Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge ambao ndio wasimamizi wa shughuli za Bunge wameorodheshwa katika Sehemu ya Pili ya kitabu hiki ikifuatiwa na Uongozi wa Ofisi ya Bunge katika Sehemu ya Tatu. 2 Sehemu ya Nne imeorodhesha Wabunge wote wa Majimbo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mikoa ikifuatiwa na Sehemu ya Tano ambayo imeorodhesha Wabunge wote wa Viti Maalum kulingana na uwakilishi wa vyama vyao Bungeni ikianzia na Chama cha Mapinduzi (CCM) na ikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Sehemu ya Sita imeorodhesha Wabunge kupitia nafasi ya Kuteuliwa na Rais na Sehemu ya Saba itaorodhesha Wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi.
    [Show full text]
  • 271980 Mia Orange
    Sustaining Authoritarianism Clientelism and Repression in Kazakhstan, Kenya, Kyrgyzstan and Tanzania Orange, Mia 2019 Document Version: Publisher's PDF, also known as Version of record Link to publication Citation for published version (APA): Orange, M. (2019). Sustaining Authoritarianism: Clientelism and Repression in Kazakhstan, Kenya, Kyrgyzstan and Tanzania. Lund University. Total number of authors: 1 General rights Unless other specific re-use rights are stated the following general rights apply: Copyright and moral rights for the publications made accessible in the public portal are retained by the authors and/or other copyright owners and it is a condition of accessing publications that users recognise and abide by the legal requirements associated with these rights. • Users may download and print one copy of any publication from the public portal for the purpose of private study or research. • You may not further distribute the material or use it for any profit-making activity or commercial gain • You may freely distribute the URL identifying the publication in the public portal Read more about Creative commons licenses: https://creativecommons.org/licenses/ Take down policy If you believe that this document breaches copyright please contact us providing details, and we will remove access to the work immediately and investigate your claim. LUND UNIVERSITY PO Box 117 221 00 Lund +46 46-222 00 00 MIA ORANGE MIA Sustaining Authoritarianism – Clientelism and in Repression Kazakhstan, Kenya, Kyrgyzstan and Tanzania Kazakhstan, Kenya, Kyrgyzstan and Tanzania share a past and present as authoritarian states. Dominant parties are in power in Tanzania and Kazakhstan, while elections are competitive but not democratic in Kenya and Kyrgyzstan.
    [Show full text]
  • 19 Desemba, 2013
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kumi na Tatu - Tarehe 19 Desemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:- Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2012 (The Annual Report and Audited Accounts of the National Housing Corporation (NHC) for The Year ended 30th June, 2012). 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA KAZI NA AJIRA:- Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa Mwaka 2011/2012 (The Annual Report of Social Security Regulatory Authority (SSRA) for the Year 2011/2012). MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo ni siku ya Alhamisi, tunakuwa na Maswali kwa Waziri Mkuu. Kawaida yetu kama Kiongozi wa Upinzani yupo basi ndiye anayeanza. Naona sijamwona. Kwa hiyo, nitaanza na Mheshimiwa Murtaza Mangungu. Mheshimiwa Murtaza Mangungu. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kipindi cha miaka ya 1970 kuja 1980 Serikali ilifanya jitihada kubwa sana kupanua elimu ya juu nchini. Lakini kutokana na matatizo ambayo hayajaelezeka kipindi kirefu hatujawekeza vya kutosha hivyo kuna upungufu mkubwa sana wa Wahadhiri katika Vyuo Vikuu hasa ukizingatia Sheria yetu ya ajira inatoa ukomo wa kustaafu siyo zaidi ya miaka 65 na maprofesa wote ambao ni full Professor wamezidi umri wa miaka 65.
    [Show full text]
  • Uchaguzi Mkuu Wa 2015 Pakua
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JATUMEMHURI YA YA TAIFA MUUNG AYANO WAUCHAGUZI TANZANIA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TAARIFA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU TAARIFA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI, 2015 UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI, 2015 Posta House Simu: +255 22 2114963-6 7 Mtaa wa Ghana, Nukushi: +255 22 211674 Tovuti: www.nec.go.tz S. L. P. 10923, Barua pepe: [email protected] 11300 Dar Es Salaam Posta House Simu: +255 22 2114963-6 7 Mtaa wa Ghana, Nukushi: +255 22 211674 S.L.P. 10923, Tovuti: www.nec.go.tz 11300 Dar Es Salaam, Barua pepe: [email protected] Tanzania a a Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta House 7 Mtaa wa Ghana, S. L. P. 10923, 11300 Dar Es Salaam © Tume ya Taifa ya Uchaguzi, 2016 ISBN 978 – 9976 – 9957 – 0 – 1 Imepigwa chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Dar Es Salaam - Tanzania Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili au kutoa kitabu hiki kwa njia yoyote ile bila idhini ya maandishi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi c YALIYOMO YALIYOMO ORODHA YA MAJEDWALI ................................................................ORODHA.......... YA VII MAJEDWALI .......................................................................... VII ORODHA YA VIAMBATISHO ................................................................ORODHA..... YAVIII VIAMBATISH O ..................................................................... VIII ORODHA YA MICHORO ................................................................ORODHA............... YA IX MICHORO ..............................................................................
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TANO Kikao Cha Kwanza – Tarehe 1 Novemba, 2016
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA TANO Kikao cha Kwanza – Tarehe 1 Novemba, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wimbo wa Taifa Uliimbwa) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Katibu. DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa Nne wa Bunge, Bunge lilipitisha Miswada ya Sheria ifuatayo:- (i) Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa wa mwaka 2016(The Access to Information Bill 2016); (ii) Muswada wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini wa mwaka 2016 (The Valuation and Valuers Registration Bill, 2016); (iii) Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2016 (The Government Chemist Laboratory Authority Bill, 2016); (iv) Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016, (The Chemist Professionals Bill, 2016); (v) Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania wa mwaka 2016 (The Agricultural Research Institute Bill, 2016); na 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) (vi) Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Uvuvi wa Tanzania wa mwaka 2016 (The Fisheries Research Institute Bill, 2016). Kwa taarifa hii, napenda kuliarifu Bunge hili Tukufu kwamba, tayari Miswada hiyo imekwishapata kibali cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Sheria za nchi ambazo sasa zinaitwa:- (i) Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa Na. 6 ya mwaka 2016 (The Access to Information Act. No.6, 2016); (ii) Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini, Na. 7 ya mwaka 2016 (The Valuation and Valuers Registration Act, No.7, 2016); (iii) Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Na.
    [Show full text]