VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI

Mhe. Dkt. Medard M. C. Kalemani (Mb.) Waziri wa Nishati

Mhe. Subira K. Mgalu (Mb.) Dkt. Hamisi H. Mwinyimvua Naibu Waziri wa Nishati Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

i

ii HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI MHE. DKT. MEDARD MATOGOLO CHANANJA KALEMANI (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2019/20

1 2 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia Taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2018/19 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa Mwaka 2019/20. 2. Mheshimiwa Spika, napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuendelea kuwajalia afya njema Viongozi wetu Wakuu wa Kitaifa, Waheshimiwa Mawaziri wenzangu, Waheshimiwa Wabunge na Viongozi wengine mbalimbali. Kipekee nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kuendelea kusimamia Sekta ya Nishati na leo kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2019/20. 3. Mheshimiwa Spika, naomba pia niungane na Mawaziri wenzangu, Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwa 1 ujumla kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa kwa maelekezo yake thabiti yanayonisaidia kuisimamia vema Sekta ya Nishati. Ni dhahiri kuwa Rais wetu amekuwa chachu katika kutekeleza mipango mikubwa na yenye tija katika Sekta ya Nishati hapa nchini. Mipango hiyo ni pamoja na kuanza kutekeleza Mradi Mkubwa wa kielelezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (MW 2,115). Napenda kuwaahidi Watanzania kuwa Wizara yangu kwa kushirikiana na Bunge lako Tukufu na wadau mbalimbali tutasimamia vema Mradi huu ili ukamilike kwa wakati. 4. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwashukuru Mhe. , Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo mbalimbali wanayonipatia katika kusimamia Sekta ya Nishati. Nikiri kuwa maelekezo na miongozo ya viongozi wetu hawa ni msingi wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Nishati. Aidha, napenda 2 kumpongeza pia Mhe. Dkt. , Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuendelea kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 5. Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii pia kuwapongeza Mawaziri walioteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nampongeza Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mhe. Angellah Jasmin Kairuki (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji); Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. Doto Mashaka Biteko (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Madini; Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo; na Mhe. Joseph George Kakunda (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. 6. Mheshimiwa Spika, niwapongeze pia Naibu Mawaziri Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa (Mb.), aliyeteuliwa 3 kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Mhe. Constantine John Kanyasu (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii; Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo; na Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI. Nawatakia wateule wote kila la kheri katika kutekeleza majukumu yao ya Kitaifa. 7. Mheshimiwa Spika, napenda nikupongeze wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wote wa Kamati Mbalimbali za Kudumu za Bunge pamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bunge lako Tukufu kwa utendaji kazi wenu mahiri. Kwa namna ya pekee natoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dunstan Luka Kitandula (Mb.), Makamu Mwenyekiti Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri (Mb.), na Wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa ushauri na maelekezo wanayotupatia. Nikiri kuwa Kamati hii imefanya kazi kubwa ya kuishauri Wizara katika masuala mbalimbali na kuchambua kwa kina mapendekezo 4 ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2019/20. Wizara itaendelea kushirikiana na Kamati hii katika kusimamia kwa ufanisi ustawi wa Sekta ya Nishati. 8. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, naomba sasa kuwasilisha Taarifa ya Mapato, Matumizi na Utekelezaji wa Shughuli za Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2018/19 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2019/20. B. TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA 2018/19 NA MWAKA 2019/20 Bajeti na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2018/19 9. Mheshimiwa Spika, Bajeti iliyopitishwa kwa ajili ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake kwa Mwaka 2018/19 ni jumla ya Shilingi Trilioni 1.692 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Bajeti ya Miradi ya Maendeleo ilikuwa Shilingi Trilioni 1.665 sawa na asilimia 98.4 ya bajeti yote ya Wizara na Bajeti ya Matumizi ya Kawaida ni Shilingi bilioni 27.15 sawa na asilimia 1.6 ya bajeti yote ya Wizara. 5 10. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi Trilioni 1.227. Fedha hizi zinajumuisha Shilingi bilioni 688.65 ambazo ni malipo ya awali (advance payment) kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Rufiji naShilingi bilioni 169.71 ambazo ni fedha za nje zilizopelekwa moja kwa moja (D-Funds) katika miradi ya REA, TANESCO na Sustainable Energy for All (SE4All). Kiasi hicho kilichopokelewa na Wizara ni sawa na asilimia 87 ya fedha zilizotarajiwa kupokelewa katika kipindi husika ambazo ni Shilingi trilioni 1.410. Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali 11. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati katika mwaka 2018/19 ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni 394.45. Kati ya makusanyo hayo, jumla ya Shilingi bilioni 394.44 zilitarajiwa kukusanywa kupitia shughuli za mafuta na gesi asilia na Shilingi milioni 10.0 kupitia shughuli za utawala. Hadi kufikia tarehe 15 Mei 2019, Wizara kupitia shughuli za TPDC za utafiti wa mafuta na mauzo ya gesi asilia imekusanya Shilingi bilioni 484.33. Makusanyo hayo ni sawa na asilimia 123 ya lengo la makusanyo ya 6 Shilingi bilioni 394.45 kwa mwaka 2018/19. Sababu ya kuvuka lengo ni kuongezeka kwa matumizi ya gesi asilia yanayotokana na kuunganishwa kwa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II na Kiwanda cha Saruji cha Dangote. Matumizi ya gesi asilia yameendelea kuongezeka na kufikia jumla ya futi za ujazo bilioni 59.2 mwaka 2018 kutoka futi za ujazo bilioni 32.2 mwaka 2015, sawa na ongezeko la asilimia 84. 12. Mheshimiwa Spika, makisio ya makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2019/20 ni Shilingi bilioni 602.05, sawa na ongezeko la asilimia 52.6 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 394.45 lililokuwa lengo la mwaka 2018/19. Ongezeko hilo la makisio ya makusanyo limetokana na kuongezeka kwa matumizi ya rasilimali ya gesi asilia. C. UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA 2018/19 13. Mheshimiwa Spika, Maeneo ya Kipaumbele ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2018/19 yalikuwa ni pamoja na: kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo Mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji MW 2,115; miradi

7 ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I - Extension MW 185 na Kinyerezi II MW 240; kuimarisha mifumo ya kusafirisha umeme nchini; kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini (REA III); kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); kuimarisha shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia; na kuendeleza miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo na umeme-jua). 14. Mheshimiwa Spika, Wizara pia ilizingatia maeneo mengine ambayo ni pamoja na: kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake katika kusimamia Sekta ya Nishati; kuboresha mazingira ya ofisi kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kutoa huduma bora zaidi; na kuendelea kuelimisha umma na kuboresha mawasiliano na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya nishati. 15. Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa kutokana na utekelezaji wa maeneo hayo ya kipaumbele, Wizara imepata mafanikio makubwa 22 ikiwa 8 ni pamoja na nchi kutokuwa na mgawo wa umeme katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/19. Aidha, pamoja na kutokuwa na mgawo wa umeme, Taifa letu limeanza kuwa na ziada ya umeme wa wastani wa MW 300 kwa siku kwa mwaka 2018/19 tofauti na hapo awali tulipokuwa na upungufu wa zaidi ya MW 100 kwa mwaka 2015. Mafanikio makubwa 21 ni kama ifuatavyo: (i) Kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji waMW 2,115 utakaokamilika mwaka 2022. Ujenzi wa bwawa hili kutaifanya Tanzania kuwa na umeme wa uhakika, unaotabirika na gharama nafuu. Aidha, Ujenzi wa bwawa la mradi huu utaifanya Tanzania kushika nafasi ya kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na bwawa kubwa, ya nne kwa Afrika na kuwa kati ya nchi 70 Duniani zenye mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme; (ii) Kukamilika kwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Makambako, Madaba hadi 9 Songea, pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Madaba na Songea na upanuzi wa kituo cha Makambako. Kukamilika kwa njia hii ya kusafirisha umeme kumefanya mikoa ya Njombe na Ruvuma kuunganishwa katika Gridi ya Taifa na hivyo kusitishwa kwa matumizi ya mitambo ya mafuta ambayo ilikuwa ikigharimu TANESCO na kuokoa wastani wa Shilingi bilioni 9.8 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununua mafuta katika Vituo vya Madaba, Ludewa, Songea, Mbinga na Namtumbo; (iii) Kuongezeka kwa kasi ya kusambaza umeme vijijini ambapo hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 Serikali imepeleka umeme katika vijiji 7,127 vya Tanzania Bara ikilinganishwa na vijiji 2,018 vilivyokuwa vimeunganishwa umeme Mwaka 2015. Hii ni sawa na ongezeko la vijiji 5,109 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ambalo ni ongezeko la asilimia 253 ya vijiji vilivyokuwa na umeme kufikia mwaka 2015. Aidha, ifikapo mwezi Juni, 2020 vijiji zaidi ya 10,278 kati ya 12,268 vya Tanzania 10 Bara vitaunganishwa umeme sawa na asilimia 84 ya vijiji vyote. Hivi sasa Wilaya na Halmashauri 15 za nchi yetu zimefikishiwa umeme katika vijiji vyake vyote na kazi inayoendelea ni kuunganisha umeme katika vitongoji vyake. Wilaya pamoja na Halmashauri hizo ni Mafia, Iringa Vijijini (Isimani), Pangani, Rufiji, Bahi, Siha, Moshi, Hai, Mwanga, Rombo, Madaba, Buhigwe, Makambako, Korogwe Mjini na Mafinga. Pamoja na kukamilisha wilaya na Halmashauri hizo, kwa sasa kazi za kuunganisha umeme zinaendelea katika wilaya nyingine nchini; (iv) Serikali kupitia TANESCO kuanza kuunganisha umeme kwa Shilingi 27,000 katika maeneo yote ya vijijini kulingana na Mpango wa Kupeleka Umeme Vijijini; (v) Kuunganisha Gridi ya Taifa katika maeneo mbalimbali yakiwemo Tunduru na Liwale na hivyo kuokoa jumla ya Shilingi bilioni 7.33 zilizokuwa zikitumika kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme katika maeneo hayo; 11 (vi) Kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na kuongeza jumla ya MW 248.22 katika Gridi ya Taifa. Kituo cha Kinyerezi II ni cha kwanza hapa nchini kutumia teknolojia ya kisasa ya combined cycle; (vii) Kuendelea kutumia vifaa vya ndani katika ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha umeme vikiwemo nguzo, mashineumba (transfoma), nyaya na mita za LUKU na hivyo kulipunguzia gharama kubwa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na kuokoa wastani wa Shilingi bilioni 162.57 kwa mwaka. Mpango huu umetengeneza ajira kwa watanzania wapatao 3,520 na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya umeme. Kutokana na mafanikio hayo, kwa sasa kuna zaidi ya viwanda vitatu (3) vya kuzalisha transfoma badala ya kimoja kilichokuwepo mwaka 2015, viwanda tisa (9) vya nguzo badala ya vitatu (3) vilivyokuwepo awali, viwanda vitano (5) vya nyaya badala ya kimoja cha East African Cables kilichokuwepo na kujengwa viwanda vitatu (3) vya Mita za LUKU tofauti na hapo awali ambapo hapakuwa na kiwanda hata kimoja; 12 (viii) Kuanza kutekeleza mradi wa kujenga njia ya kusafirisha umeme kV 132 ili kuunganisha mikoa ya Kigoma na Katavi katika Gridi ya Taifa kutoka Tabora – Urambo - Kaliua, Nguruka hadi Kidahwe (Kigoma) kilomita 391 na kutoka Tabora – Ipole, Inyonga hadi Nsimbo (Katavi) kilomita 381; (ix) Shirika la Umeme (TANESCO) kutohitaji ruzuku ya Serikali katika shughuli zake za uendeshaji kutokana na TANESCO kujiendesha lenyewe na kuokoa wastani wa Shilingi bilioni 143 zilizokuwa zikitumika kama ruzuku kutoka Serikalini kila mwaka; (x) Kuimarika kwa mapato ya TANESCO kwa kiwango cha ongezeko la asilimia 1.5 mwaka 2017/18 hadi asilimia 7.6 mwaka 2018/19. Hivyo ni matarajio kuwa TANESCO itaweza kuanza kutoa gawio Serikalini katika kipindi cha Mwaka 2019/20; (xi) Kuunganishiwa umeme kwa wateja wapya 969,431 katika kipindi cha kuanzia Julai, 2015 hadi tarehe 15 Mei, 2019 na kufikia jumla ya wateja

13 2,442,648 ikilinganishwa na wateja 1,473,217 waliokuwepo kuanzia nchi yetu ilipopata Uhuru hadi mwezi Juni, 2015 sawa na ongezeko la asilimia 66 kwa miaka mitatu; (xii) Kuongeza mtandao wa kusambaza gesi asilia viwandani na majumbani kwa takriban kilomita 9.64 kwa mwaka 2018/19 kutoka kilomita 6.31 kwa mwaka 2017/18. Mtandao huo utawezesha kuunganisha wateja wa gesi asilia majumbani zaidi ya 500 katika Jiji la Dar es Salaam. Kwa upande wa viwandani, viwanda vya: Dangote (awamu ya pili); Knauf; Cocacola; Lodhia; na kiwanda cha vifungashio kinachomilikiwa na Goodwill Ceramics Tanzania Limited vimeunganishwa. Aidha, matumizi ya gesi katika magari yameongezeka kutoka magari 80 mwaka 2017/18 na kufikia magari zaidi ya 200 mwaka 2018/19 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 150; (xiii) Kukamilika kwa ukarabati wa vituo vya kupoza umeme vya Kigamboni na Kurasini na hivyo kuimarisha hali ya

14 upatikanaji umeme katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo maeneo ya Kigamboni; (xiv) Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya kupeleka umeme katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba, Jijini Dodoma kwa kuunganisha umeme Wizara zote katika muda mfupi; (xv) Kuanzisha utaratibu mpya wa mawasiliano baina ya wateja na TANESCO kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo kuanzisha makundi ya whatsapp kwa kila wilaya yanayopatikana masaa 24 kila siku ili kuimarisha huduma kwa wateja na hivyo kuongeza ufanisi na mapato ya Shirika; (xvi) Kuongezeka kwa ufanisi wa makusanyo ya mapato ya Serikali ambapo hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 Wizara kupitia TPDC ilikuwa imekusanya Shilingi bilioni 484.33 sawa na asilimia 123 ya lengo la makusanyo ya Shilingi bilioni 394.45 kwa mwaka 2018/19; (xvii) Kuendelea kutekeleza kazi za awali za Mradi wa Bomba la Kusafirisha 15 Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani (Tanga) zikiwemo Geotechnical na majadiliano ya Host Government Agreement – HGA. Kazi hizo zitakamilika mwezi Juni, 2019 na kazi nyingine za maandalizi ya ujenzi zinaendelea;

(xviii) Kuongeza uzalishaji wa gesi asilia kufikia Futi za Ujazo milioni 190 kwa siku kwa mwaka 2018/19 kutoka Futi za Ujazo milioni 175 kwa siku mwaka 2017/18. Ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 8.6 limewezesha upatikanaji wa gesi zaidi kwa matumizi ya viwandani, majumbani na katika kuzalisha umeme; (xix) Kupungua kwa muda wa kushusha mafuta katika Bandari zetu za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara kutoka kati ya siku 30 na 60 hadi kati ya siku 3 na 8 kutokana na Serikali kuendelea kuimarisha Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja na hivyo kupunguza gharama zilizokuwa zinatokana na gharama za meli kuchelewa kushusha mafuta bandarini (Demurrage Charges);

16 (xx) Kupatikana kwa mafuta ya kutosha na ya uhakika katika kipindi chote cha mwaka 2018/19 ambapo hadi sasa kuna ziada ya lita milioni 125.22 za dizeli, lita milioni 94.67 za petroli, lita milioni 18.95 za mafuta ya taa na ndege yanayotosheleza kwa zaidi ya siku 32; (xxi) Kukamilika na kupitishwa kwa miundo ya Wizara, PURA na TPDC ambayo itawezesha Wizara na Taasisi zake kuendelea kutekeleza majukumu kwa ufanisi; na

(xxii) Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la awamu ya kwanza la Wizara na kuhamia Ofisi mpya katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba Jijini Dodoma. D. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA WIZARA KWA MWAKA 2018/19 NA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA 2019/20 16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizara ya Nishati itaendelea kutekeleza maeneo ya vipaumbele mbalimbali yakiwemo: kuongeza uzalishaji wa umeme nchini ili kufikia lengo la kuwa naMW 10,000 ifikapo mwaka 2025, kwa kutekeleza miradi 17 mikubwa ikiwemo: mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji (MW 2,115) na mradi wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I - Extension (MW 185), Mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo MW 80, Ruhudji MW 358 na Rumakali MW 222; Kuimarisha mifumo ya usafirishaji wa umeme nchini kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa North - West Grid Extension kV 400 yenye umbali wa kilomita 1,384 inayojumuisha Iringa – Mbeya – Sumbawanga – Mpanda – Kigoma hadi Nyakanazi; Singida – Arusha – Namanga kV 400, kilomita 414; Rufiji - Chalinze – Dodoma kV 400, kilomita 512; Rusumo – Nyakanazi kV 220, kilomita 98; Geita – Nyakanazi kV 220, kilomita 133; Tabora – Urambo – Kaliua – Nguruka hadi Kidahwe Mkoani Kigoma kV 132, kilomita 391; na Tabora – Ipole – Inyonga hadi Nsimbo (Katavi) kV 132, kilomita 381. 17. Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ya kisekta yatakayozingatiwa na Wizara ni: kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kupeleka Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), katika vijiji takriban 1,990 vilivyobaki 18 kati ya vijiji 12,268; kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP); kuimarisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia; kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi asilia; kuendeleza miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo na jua); kuvutia uwekezaji katika sekta ya nishati; na kuendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi za TANESCO, TGDC, REA, TPDC, PURA na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja ili kuongeza ufanisi na ushindani katika Sekta ya Nishati. 18. Mheshimiwa Spika, pamoja na maeneo hayo ya kisekta, Wizara itazingatia maeneo mengine ya kuboresha utendaji ambayo ni pamoja na: kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake katika kusimamia Sekta ya Nishati; kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kutoa huduma bora zaidi; na kuendelea kuelimisha umma na kuboresha mawasiliano kati ya Wizara na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya nishati.

19 SEKTA NDOGO YA UMEME HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI 19. Mheshimiwa Spika, hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika katika kipindi chote cha mwaka 2018/19. Aidha, mahitaji ya umeme nchini yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kukua na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi zinazohitaji nishati ya umeme wa kutosha, wa uhakika na wa gharama nafuu katika uzalishaji. Katika mwaka 2018/19 uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme (installed capacity) nchini umeongezeka na kufikiaMW 1,601.90 kutoka MW 1,517.47 zilizofikiwa mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la asilimia 5.6. Kati ya jumla ya MW 1,601.90 zilizopo nchini, MW 1,565.72 zimeunganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa na MW 36.18 zipo nje ya mfumo wa Gridi ya Taifa. 20. Mheshimiwa Spika, matumizi ya juu ya umeme yamefikia MW 1,116.58 ukilinganisha na MW 1,051.27 zilizofikiwa mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la asilimia 6.2. Aidha, umeme uliozalishwa nchini uliongezeka kutoka GWh 7,114 mwaka 2017 na kufikia GWh 7,374 mwaka

20 2018 sawa na ongezeko la asilimia 3.7. Hadi kufikia mwaka 2015, nchi yetu ilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 1,204 ikilinganishwa na uwezo wa sasa wa MW 1,601.90 sawa na ongezeko la asilimia 33. Katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda, Serikali kupitia Wizara ya Nishati imelenga kuzalisha umeme wa MW 10,000 ifikapo mwaka 2025.

MIRADI YA KUZALISHA UMEME Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Mto Rufiji (Rufiji Hydro Power Project) – MW 2,115 21. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji. Mkataba wa ujenzi wa mradi ulisainiwa tarehe 12 Desemba, 2018 kati ya TANESCO na Mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors na Elsewedy Electric za nchini Misri. Tukio hili lilishuhudiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Misri. Mkandarasi huyo alikabidhiwa eneo la mradi tarehe 14 Februari, 2019 na kuanza utekelezaji wa kazi za awali. Katika kipindi 21 cha mwaka 2018/19, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa miundombinu wezeshi ikijumuisha: njia ya kusafirisha umeme wa MW 8 yenye msongo wa kV 33 kutoka Msamvu, Morogoro hadi eneo la mradi yenye urefu wa kilomita 170; barabara za kiwango cha changarawe za Ubena – Zomozi na Kibiti – Mloka hadi eneo la mradi; mifumo ya maji; mawasiliano ya simu; na nyumba za kuishi Mkandarasi. Vilevile, kulingana na mahitaji ya umeme wakati wa ujenzi, TANESCO imeanza ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto kupitia Kisarawe hadi eneo la mradi urefu wa kilomita 245 itakayosafirisha umeme wa MW 22. 22. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2019/20 Serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi huu muhimu ambapo kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kuanza ujenzi wa bwawa (main dam and spillways); kuanza ujenzi wa njia za kupitisha maji (tunnels); na kukamilisha ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka Gongo la Mboto. Fedha za ndani Shilingi trilioni 1.443 zimetengwa katika mwaka 2019/20 22 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. Utekelezaji wa mradi umeanza mwezi Desemba, 2018 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022. Kwa ujumla Serikali imedhamiria kwa dhati kutekeleza Mradi huu bila kuyumbishwa, kucheleweshwa wala kukwamishwa na mtu yeyote kutoka ndani au nje ya nchi asiyeitakia mema nchi yetu. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80 23. Mheshimiwa Spika, mradi huu wa nchi tatu (3) za Tanzania, Burundi na Rwanda unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 80 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera kwa mgawanyo sawa kwa kila nchi. Kwa upande wa Tanzania, Mradi unagharimu Dola za Marekani milioni 113 sawa na takriban Shilingi bilioni 261.75 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilika kwa ujenzi wa barabara za kuingia eneo la Mradi; kukamilika kwa ujenzi wa kikinga maji (coffer dam) na kukamilika kwa uchimbaji wa eneo la kusimika mitambo (power house).

23 24. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni pamoja na kujenga miundombinu ya kukinga na kuingiza maji katika handaki (Dam and Intake); ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme (powerhouse); ufungaji wa mitambo katika kituo cha kuzalisha umeme; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme (Switchyard); na kukamilisha miradi ya kijamii kwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi (Local Area Development Plan – LADP na Livelihood Restoration Program - LRP). Fedha za nje Shilingi bilioni 3 zimetengwa na Serikali katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya mradi huu. Mradi huu umeanza mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2020. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Ruhudji – MW 358 25. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji mkoani Njombe. Ujenzi wa mradi huu utahusisha njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. 24 Katika mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: Serikali kuanza majadiliano ya ufadhili na Serikali ya China kwa ajili ya kutekeleza mradi; na kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi Yakinifu. Ujenzi wa mradi unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 407.40 sawa na takriban Shilingi bilioni 943.70 na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 53.2 sawa na takriban Shilingi bilioni 123.23. 26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kukamilisha taratibu za ufadhili wa mradi; kuhuisha Upembuzi Yakinifu (Updating of feasibility study); kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa kujenga mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 12.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 10.00 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.50 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Mei, 2020 na kukamilika mwezi Aprili, 2023.

25 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rumakali – MW 222 27. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme msongo wakV 220 yenye urefu wa kilomita 150 kutoka katika mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya. Gharama za mradi huu kwa pamoja zinakadiriwa kuwa jumla ya Dola za Marekani milioni 344.22 sawa na takriban Shilingi bilioni 899.27. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kumtafuta Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi Yakinifu wa mradi uliofanyika mwaka 1998; na kuanza usanifu wa miundombinu ya mradi. 28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kuhuisha Upembuzi Yakinifu (Updating of feasibility study); kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi; kufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii (ESIA); na kulipa fidia. Jumla ya Shilingi bilioni 3.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya 26 fedha hizo Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.50 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2021 na kukamilika mwezi Juni, 2023. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kakono – MW 87 29. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 87 kwa kutumia maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 220 kutoka Kakono hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita 38.8. Gharama za ujenzi wa mradi ni Dola za Marekani milioni 380 zitakazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD). Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilisha utafiti wa kijiolojia na haidrolojia; kukamilisha usanifu wa awali wa mradi; kufanya maandalizi ya zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi; kuhuisha tathmini ya athari za mazingira na kijamii (updating ESIA); na kukamilisha mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi (Resettlement Action Plan - RAP). 27 30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kutwaa ardhi na kulipa fidia katika eneo la mradi; na kutafuta Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 220. Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Desemba, 2019 na kukamilika mwezi Desemba, 2022. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 45 31. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 45 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi mkoani Kigoma na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 53 kutoka Malagarasi hadi Kidahwe mkoani Kigoma. Gharama za utekelezaji wa Mradi ni Dola za Marekani milioni 150.0 sawa na takriban Shilingi bilioni 346.30. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na kukamilisha: Upembuzi Yakinifu wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 28 132; usanifu (design) wa miundombinu ya mradi; upimaji na uthamini wa eneo la mradi na njia ya kusafirisha umeme; na mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha mradi. 32. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kutwaa ardhi na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; kumpata Mtaalam Mshauri na Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi na njia ya umeme msongo wa kV 132. Jumla ya Shilingi bilioni 3 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 600 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.40 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2020 na kukamilika mwezi Septemba, 2023. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kikonge – MW 300 33. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 300 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhuhu mkoani Njombe na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 53 kutoka Kikonge hadi kituo

29 cha kupoza umeme cha Madaba. Gharama za utekelezaji wa mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani Milioni 750 sawa na takriban Shilingi trilioni 1.737. Mradi huu pia unahusisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji. Kazi zilizotekelezwa kwa mwaka 2018/19 ni kumpata Mtaalamu Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study) na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira na Kijamii (Strategic Environmental & Social Assessment – SESA). Kazi hizi zinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). 34. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kukamilisha Upembuzi Yakinifu pamoja na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira na Kijamii (SESA); kukamilisha majadiliano ya ufadhili wa ujenzi wa mradi na kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Novemba, 2020 na kukamilika mwezi Oktoba, 2023.

30 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Murongo/Kikagati – MW 14 35. Mheshimiwa Spika, mradi huu wa nchi mbili za Tanzania na Uganda unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 14 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kV 33 yenye urefu wa kilomita 0.7 kutoka Kikagati (Uganda) hadi Murongo (Tanzania). Mradi utagharimu Dola za Marekani milioni 58 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 134.35 na unatekelezwa na mwekezaji binafsi, Kampuni ya Kikagati Power Company Ltd (KPCL). 36. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilisha ujenzi wa kambi ya kudumu ya wafanyakazi na miundombinu ya barabara za kuingia eneo la mradi; usanifu wa mitambo na vifaa ya umeme; na ujenzi wa miundombinu ya kukinga na kuingiza maji (Dam and Intake) na njia za kupitisha maji (waterways). Kazi zitakazotekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na: kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme; na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 33. Mradi huu ulianza mwezi Novemba, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2020. 31 Matengenezo ya Mtambo wa Kuzalisha Umeme wa Hale (Rehabilitation of Hale Hydro Power Plant) – MW 21 37. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji na ukarabati wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia maji wa Hale mkoani Tanga. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa SEK milioni 200 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 50.96 zitakazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Sweden kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (Sida). Kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni kukamilisha taratibu za kumpata Mkandarasi wa ukarabati wa mitambo. 38. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni pamoja na kuanza uchimbaji wa handaki la kuingia katika kituo cha kuzalisha umeme (access tunnel). Jumla ya Shilingi bilioni 7.80 zimetengwa kutekeleza kazi hizo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi milioni 300 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 7.50 ni fedha za nje. Kazi za ukarabati zinatarajiwa kuanza mwezi Agosti, 2019 na kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2021. 32 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi II – MW 240 39. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa mradi huu ulianza mwezi Machi, 2016 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 344, sawa na takriban Shilingi bilioni 794.12. Mradi huu ulihusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 240 kwa kutumia gesi asilia katika eneo la Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Kituo hiki chenye jumla ya mitambo nane (8), ambapo mitambo sita (6) ni ya kutumia gesi asilia (gas turbines) na mitambo miwili (2) ni ya kutumia mvuke (steam turbines) kilikamilika na kukabidhiwa rasmi kwa TANESCO mwezi Desemba, 2018. Kukamilika kwa kituo hiki kumeongeza jumla ya MW 248.22 katika Gridi ya Taifa.

Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi I Extension – MW 185 40. Mheshimiwa Spika, mradi huu ambao upo katika hatua za mwisho za utekelezaji unahusu upanuzi wa kituo cha Kinyerezi I – MW 150 kwa kuongeza mitambo itakayozalisha MW 185 na kufanya kituo hicho kuzalisha jumla ya MW 335. Mradi 33 huu unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na takriban Shilingi bilioni 435.48. Katika mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilika kwa utengenezwaji wa mitambo yote minne (4) na kuanza kufungwa katika eneo la mradi; kukamilika kwa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I kV 220 na kuendelea na upanuzi (upgrade) wa njia ya msongo wa kV 132 kutoka Kinyerezi I hadi kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto. Ujenzi wa mradi huu ulianza mwezi Juni, 2016 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2019. 41. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2019/20 kazi zitakazotekelezwa ni kukamilisha ufungaji wa mitambo na kuingiza jumla ya MW 185 katika Gridi ya Taifa. Fedha za ndani Shilingi bilioni 60.00 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo.

34 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Mtwara – MW 300 42. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha MW 300 kwa kutumia gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 360 sawa na takriban Shilingi bilioni 833.90. Mradi huu utatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA) kwa kushirikiana na Serikali. Kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilika kwa Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study) wa kituo cha kuzalisha umeme na miundombinu wezeshi ya maji, barabara na gesi asilia. 43. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 4.20 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 1.00 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 3.20 ni fedha za nje. Mradi 35 huu unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Machi, 2020 na kukamilika mwezi Septemba, 2022. Miradi ya Kufua Umeme Utokanao na Jua – MW 150, Upepo – MW 200 na Makaa ya Mawe – MW 600 44. Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba 2018, Serikali kupitia TANESCO ilitangaza miradi ya nishati jadidifu (Jua – MW 150 na Upepo – MW 200) na Makaa ya Mawe – MW 600 kwa wawekezaji binafsi. Lengo ni kupata miradi ya kuzalisha umeme wa jumla ya MW 950 kwa njia ya ushindani na kuingizwa katika Gridi ya Taifa. Hadi kufikia mwezi Februari, 2019 tathmini ya zabuni kwa kampuni zilizoshiriki ilikamilika. Taratibu zinazoendelea kwa sasa ni kampuni zilizopita hatua ya awali kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendeleza miradi husika baada ya kupatiwa Request for Proposals (RFPs). 45. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2019/20, TANESCO itakamilisha taratibu za kuwapata wawekezaji binafsi wenye bei nafuu na kuanza utekelezaji wa miradi hiyo. Utekelezaji wa miradi hii nafuu utapunguzia Shirika gharama za uendeshaji 36 na hivyo kuwepo matarajio ya kushuka kwa bei ya umeme. Utekelezaji huo unatarajiwa kuanza mwezi Novemba, 2019 na kukamilika mwezi Oktoba, 2022. MIRADI YA KUSAFIRISHA UMEME Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 wa Singida – Arusha – Namanga 46. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 414 kutoka Singida hadi Namanga kupitia Arusha. Mradi huu pia unahusisha ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme katika eneo la Kisongo mkoani Arusha, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme (bay addition) cha Singida na usambazaji wa umeme katika vijiji 22 vinavyopitiwa na mradi. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania. Gharama ya mradi ni Dola za Marekani milioni 258.82 sawa na takriban Shilingi bilioni 599.53. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kulipa fidia na kuanza shughuli za ujenzi wa mradi.

37 47. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kufanyika kwa mwaka 2019/20 ni: kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 4 fedha za nje zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Machi, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2020. 48. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Backbone awamu ya pili (Backbone Phase II) unaohusu kuongeza uwezo (upgrade) wa vituo vya kupoza umeme kutoka kV 220 mpaka kV 400 katika mikoa ya Iringa na Shinyanga kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na katika mikoa ya Singida na Dodoma kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA). Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 kutoka Makambako hadi Songea na Kusambaza Umeme Vijijini kwa Mikoa ya Njombe na Ruvuma 49. Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa

38 kV 220, yenye urefu wa kilomita 250 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Madaba na Songea na upanuzi wa kituo cha Makambako ulianza mwezi Mei, 2016 na kukamilika mwezi Septemba, 2018. Mradi huu ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 06 Aprili, 2019. Hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 jumla ya vijiji 112 kati ya 122 vilikuwa vimeunganishwa umeme. Jumla ya wateja wapatao 22,700 wanatarajiwa kuunganishwa umeme kupitia mradi huu katika wilaya za Makambako, Njombe na Ludewa katika Mkoa wa Njombe; na Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma. Gharama ya mradi huu ilikuwa ni Shilingi bilioni 216 chini ya ufadhili wa Serikali za Tanzania na Sweden. 50. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni: kuendelea kuunganisha wateja ikiwemo Vijiji vya Lutikila, Ifinga na Mbangamawe mkoani Ruvuma vilivyoongezeka pamoja na kukamilisha kazi ya kufunga Reactor na Distribution Panels katika vituo vya kupoza 39 umeme vya Makambako, Madaba na Songea. Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 2 ni fedha za ndani na Shilingi milioni 500 ni fedha za nje. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita 51. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi ni kujenga njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 55 kutoka Bulyanhulu hadi Geita. Mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kV 220, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu, usambazaji wa umeme katika vijiji 10 vilivyopo ndani ya eneo la mradi na kubadilisha mita za umeme za kawaida (conventional meters) 1,500 mkoani Geita. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 23 sawa na takriban Shilingi bilioni 53.28. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; kuanza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme; kupatikana kwa Mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini; na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi. 40 52. Mheshimiwa Spika, kazi zitakazofanyika mwaka 2019/20 ni kukamilisha: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme mkoani Geita; upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu; ujenzi wa njia za kusambaza umeme za msongo wa kV 33 na kV 0.4 katika vijiji 10; na kuunganisha wateja wapya 1,500. Jumla ya Shilingi bilioni 4.10 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 1.50 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.60 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu ulianza mwezi Januari, 2019 na unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2020. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Geita – Nyakanazi 53. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 133, kituo cha kupoza umeme Nyakanazi na kusambaza umeme katika vijiji 32 vinavyopitiwa na mradi. Gharama za utekelezaji wa mradi huu ni EURO milioni 45 sawa na takriban Shilingi bilioni 117.79. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni: kukamilisha upatikanaji wa Mkandarasi; 41 kukamilisha uhakiki wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuanza kulipa fidia. 54. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni kuanza: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Geita hadi Nyakanazi; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi; upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kitakachojengwa kupitia Mradi wa Bulyanhulu – Geita; na usambazaji wa umeme katika vijiji 32. Fedha za nje Shilingi bilioni 1 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya kazi hizo. Ujenzi wa mradi huu utaanza mwezi Agosti, 2019 na kukamilika mwezi Julai, 2021. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 Rusumo – Nyakanazi 55. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 98.2 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Rusumo hadi Nyakanazi. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 35 sawa na takriban Shilingi bilioni 81.07. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania. Katika

42 mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kumpata Mkandarasi ambaye ni ubia kati ya Kampuni ya Sterling & Wilson Pvt ya India na Electromontaji S.A ya Romania; kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi, ambapo takriban Shilingi bilioni 2.5 kutoka vyanzo vya ndani vya TANESCO zitatumika kulipa fidia hiyo; na Mkandarasi kuanza kazi za awali za ujenzi wa mradi. Kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni: kujenga njia ya kusafirisha umeme. Fedha za nje Shilingi bilioni 2.32 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya shughuli za mradi huu. Mradi huu unatarajiwa kuanza Julai, 2019 na kukamilika mwezi Juni, 2020. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400, Iringa - Mbeya – Tunduma - Sumbawanga – Mpanda - Kigoma – Nyakanazi (North West Grid) 56. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 kutoka Iringa - Mbeya – Tunduma - Sumbawanga – Mpanda - Kigoma – Nyakanazi yenye urefu wa kilomita 1,384. Mradi huu utatekelezwa kwa awamu tatu kama ifuatavyo:

43 Awamu ya Kwanza: Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Iringa – Mbeya – Tunduma hadi Sumbawanga 57. Mheshimiwa Spika, awamu hii inahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 kutoka Iringa kupitia Mbeya, Tunduma hadi Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 624. Mradi huu utahusisha ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Iringa, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga. Mradi utagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 465, sawa na takriban Shilingi trilioni 1.08 na utafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na Serikali ya Tanzania. Hadi sasa Benki ya Dunia imetoa Dola za Marekani milioni 365, sawa na takriban Shilingi bilioni 845.49. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja na kukamilisha taarifa ya awali ya Upembuzi Yakinifu kati ya Mbeya na Sumbawanga; kuanza uthamini wa mali kwa wananchi watakaopisha mradi pamoja na kuanza taratibu za kumpata Mkandarasi wa mradi.

44 58. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni: kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha eneo la mradi; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 6.35 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 5 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.35 ni fedha za nje. Shughuli za ujenzi zinatarajiwa kuanza mwezi Desemba, 2019 na kukamilika mwezi Novemba, 2022. Mradi huu ni kati ya miradi ya kikanda itakayounganisha njia za umeme kati ya nchi yetu na nchi jirani za SADC kupitia Zambia. Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya namna hii ili pamoja na faida nyingine, kuwezesha nchi yetu kuuza umeme katika nchi nyingine. Awamu ya Pili: Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Nyakanazi hadi Kigoma 59. Mheshimiwa Spika, awamu hii itahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 kutoka Nyakanazi hadi 45 Kigoma yenye urefu wa kilomita 280, ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kidahwe Mkoani Kigoma, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme (bay addition) cha Nyakanazi na usambazaji umeme katika vijiji 38. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 187 sawa na takriban Shilingi bilioni 433.17 zitakazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Korea (EDCF). Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni: kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; uthamini wa mali zitakazoathiriwa na ujenzi wa mradi; na kupata eneo la kujenga kituo cha kupoza umeme Kidahwe mkoani Kigoma. 60. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni: kuhakiki na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 4.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 3.50 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Desemba, 2019 na kukamilika mwezi Desemba, 2021. 46 Awamu ya Tatu: Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Sumbawanga – Mpanda – Kigoma 61. Mheshimiwa Spika, awamu hii inahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 kutoka Sumbawanga hadi Kigoma kupitia Mpanda yenye urefu wa kilomita 480. Mradi huu utagharimu Dola za Marekani milioni 165 sawa na takriban Shilingi bilioni 382.21. Benki ya Dunia imeonesha nia ya kufadhili ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na Shirika la Maendeleo la Korea (EDCF) limeonesha nia ya kufadhili kituo cha kupoza umeme cha Mpanda. Kazi iliyofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kuendelea na majadiliano na Washirika wa Maendeleo kuhusu upatikanaji wa fedha kufadhili mradi huu. 62. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kufanyika kwa mwaka 2019/20 ni: kufanya tathmini ya mali za wananchi zitakazoathiriwa na mradi; kuendelea na majadiliano na Washirika wa Maendeleo kuhusu ufadhili wa mradi; na kuandaa nyaraka za zabuni za kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia mradi. Jumla ya Shilingi milioni 500 fedha za ndani 47 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2021 na kukamilika mwezi Juni, 2024. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 Rufiji – Chalinze – Dodoma 63. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 512 kutoka kituo cha kuzalisha umeme Rufiji hadi Dodoma kupitia Chalinze Mkoa wa Pwani. Mradi huu pia unahusisha upanuzi wa vituo vya kupoza umeme (bay addition) katika Mji wa Chalinze na Jiji la Dodoma pamoja na kusambaza umeme katika vijiji 37 vitakavyopitiwa na mradi. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 276.36 sawa na takriban Shilingi bilioni 640.08. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi iliyofanyika ni kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi kutoka Rufiji hadi Chalinze. 64. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kwa mwaka 2019/20 ni: kukamilisha

48 Upembuzi Yakinifu; kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kulipa fidia; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia mradi; na kumpata Mkandarasi wa kujenga njia ya kusafirisha umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 11 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 8 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 3 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Machi, 2020 na kukamilika mwezi Desemba, 2021. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Kinyerezi hadi Chalinze 65. Mheshimiwa Spika, mradi huu utahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 115 kutoka Kinyerezi mkoani Dar es Salaam hadi Chalinze mkoani Pwani pamoja na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kinyerezi. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 120 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 282. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilisha taratibu za kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; 49 na kuanza taratibu za kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kufanya Upembuzi Yakinifu wa njia ya kusafirisha umeme. 66. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa mwaka 2019/20 ni: kukamilisha Upembuzi Yakinifu; kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na kituo cha kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 15 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 12 ni fedha za ndani ambazo zitatumika kulipa fidia na Shilingi bilioni 3 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2020 na kukamilika mwezi Desemba, 2021. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa North – East Grid (Chalinze – Segera kV 400, Segera – Tanga kV 220, Kibaha – Bagamoyo kV 220) 67. Mheshimiwa Spika, mradi huu utahusisha ujenzi wa: njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 104 kutoka Chalinze kwenda Segera; njia ya umeme msongo ya kV 220 yenye urefu wa kilomita 64 kutoka Segera

50 kwenda Tanga na kilomita 40 kutoka Kibaha kwenda Bagamoyo; na kujenga vituo vya kupoza umeme (bay addition) vya Chalinze, Segera, Bagamoyo na Tanga. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 468. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi; na kuainisha mipaka ya mkuza wa njia ya kusafirisha umeme na kutathmini mali za wananchi watakaopisha mradi katika eneo kati ya Segera na Tanga. 68. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa mwaka 2019/20 ni: kufanya Upembuzi Yakinifu; na kuwapata Wakanda- rasi wa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 3 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 2 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanzia mwezi Julai, 2020 na kukamilika Juni, 2022.

51 Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 Mwanza – Masaka 69. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi huu ni kuunganisha nchi ya Tanzania na Uganda kwa kujenga njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 kutoka Mwanza, Tanzania hadi Masaka, Uganda kupitia mikoa ya Geita na Kagera. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 75 sawa na takriban Shilingi bilioni 173.73. Kazi iliyofanyika katika mwaka 2018/19 ni majadiliano na Benki ya Dunia ili kupata fedha za kudurusu taarifa ya awali ya Upembuzi Yakinifu. Kazi zitakazofanyika kwa mwaka 2019/20 ni kudurusu Upembuzi Yakinifu wa mradi na kutafuta ufadhili wa ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 3 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.50 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Machi, 2021 na kukamilika mwezi Septemba, 2023. Utekelezaji wa mradi huo pamoja na manufaa mengine, utaiwezesha nchi yetu kuuza umeme kwa nchi jirani.

52 Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Mtwara hadi Somanga Fungu 70. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 253 kutoka Mtwara hadi Somanga Fungu na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika Mkoa wa Mtwara pamoja na kusambaza umeme katika vijiji 29 vinavyopitiwa na mradi. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 230 sawa na takriban Shilingi bilioni 532.77. Fedha hizi zitatolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na kukamilisha Upembuzi Yakinifu. 71. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kwa mwaka 2019/20 ni: kufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii; kufanya uthamini na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya usimamizi wa utekelezaji wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 10 zimetengwa 53 katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 3 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 7 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Machi, 2020 na kukamilika mwezi Aprili, 2022. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 kutoka Somanga Fungu hadi Kinyerezi 72. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi huu ni kujenga njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 kutoka Somanga Fungu mkoani Lindi hadi Kinyerezi Mkoani Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 198. Gharama za Mradi ni Dola za Marekani milioni 150 sawa na takriban Shilingi bilioni 347.46. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kukamilika kwa Upembuzi Yakinifu na kuendelea kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi. Hadi kufikia mwezi Mei, 2019 wananchi 3,085 kati ya 3,901 sawa na asilimia 79 walikuwa wameshalipwa fidia ya Shilingi bilioni 56 kati ya Shilingi bilioni 69.14. 73. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kwa mwaka 2019/20 ni: kukamilisha

54 malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha mradi; kumpata Mtaalam Mshauri; na kumpata Mkandarasi. Jumla ya Shilingi bilioni 8.65 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 5.80 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.85 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Desemba, 2020 na kukamilika mwezi Februari, 2022. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Kidahwe Mkoani Kigoma na kutoka Tabora hadi Nsimbo Mkoani Katavi 74. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 391 kutoka Tabora hadi Kidahwe mkoani Kigoma kupitia Urambo, Kaliua na Nguruka na vituo vyake vya kupoza umeme pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 381 kutoka Tabora hadi Nsimbo mkoani Katavi kupitia Ipole na Inyonga. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 92 sawa na takriban Shilingi bilioni 213.11. Mradi huu 55 unatekelezwa na TANESCO kwa kutumia wataalam wa Shirika na utafanikisha azma ya Serikali ya kuiunganisha mikoa ya Katavi na Kigoma katika Gridi ya Taifa. Kazi zilizofanyika mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilisha Upembuzi Yakinifu wa awali (Pre-feasibility Study); kuainisha mipaka ya mkuza wa njia ya usafirishaji umeme; na upatikanaji wa eneo la kujenga vituo cha kupoza umeme. 75. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kwa mwaka 2019/20 ni: kufanya tathmini ya athari za mazingira na jamii; kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi; kulipa fidia; na kuanza ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 1.50 fedha za ndani zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Aidha, TANESCO imetenga Shilingi bilioni 4.80 kutoka katika mapato yake kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao ulianza mwezi Januari, 2019 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2020.

56 Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 na Kituo cha Kupoza Umeme katika Mkoa wa Simiyu 76. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 160 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Ibadakuli Mkoani Shinyanga hadi kituo cha kupoza umeme cha Imalilo Mkoani Simiyu. Gharama ya mradi inakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 75. Kazi zilizopangwa kwa mwaka 2019/20 ni: kufanya Upembuzi Yakinifu; kufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii; kuainisha mipaka ya mkuza wa njia ya usafirishaji umeme; na kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaopisha mradi. Jumla ya Shilingi milioni 100 fedha za ndani zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Aidha, TANESCO imetenga Shilingi milioni 300 kutoka katika mapato yake kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2020 na kukamilika mwezi Desemba, 2021.

57 MIRADI YA KUBORESHA NJIA ZA USAMBAZAJI UMEME Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Usambazaji Umeme katika Jiji la Dodoma 77. Mheshimiwa Spika, mradi huu utahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 220 kutoka Zuzu kwenda Msalato na kutoka Zuzu kwenda Kikombo pamoja na ujenzi wa vituo viwili (2) vya kupoza umeme katika maeneo ya Msalato na Kikombo mkoani Dodoma. Gharama ya mradi ni Dola za Marekani milioni 167.7 sawa na takriban Shilingi bilioni 388.46. Kazi zilizofanyika mwaka 2018/19 ni pamoja na kukamilisha Upembuzi Yakinifu wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220; njia ya kusambaza umeme msongo wa kV 33; vituo vya kupoza umeme vya Haneti na Narco; na kuendelea na taratibu za kupata ufadhili wa mradi kutoka Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (JICA). 78. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kwa mwaka 2019/20 ni kukamilisha taratibu za ufadhili wa mradi na kuanza

58 utekelezaji. Katika mwaka 2019/20 jumla ya Shilingi bilioni 5.4 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 400 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 5 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Juni, 2020 na kukamilika mwaka 2022. 79. Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi hizo za ujenzi wa njia za usafirishaji umeme katika Jiji la Dodoma, Serikali pia imedhamiria kuufanya Mji Mpya wa Serikali kuwa Mji wa kisasa na wa Kimataifa. Katika hatua hiyo, Serikali kupitia TANESCO inadhamiria kusambaza umeme katika Mji huo kwa kutumia nyaya za chini ya ardhi (underground cables). Gharama za Mradi huo zinakadiriwa kuwa jumla ya Shilingi bilioni 16.9. Mradi wa Usambazaji Umeme kwa Maeneo ya Mijini (Urban Electrification Program) 80. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi huu ni kuwezesha TANESCO kuongeza kasi ya kuunganisha wateja maeneo ya mijini kwa kupanua miundombinu ya kusambaza umeme ili kuhamasisha ujenzi wa viwanda. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni 59 kuendelea na ujenzi wa njia za usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali ambapo jumla ya kilomita 592 za msongo wa kV 33, kilomita 1,550 za msongo wa kV 0.4 zimejengwa na kufunga mashineumba 683 na kuunganisha jumla ya wateja 112,308. Utekelezaji wa kazi hizo umegharimu jumla ya Shilingi bilioni 82.2 kupitia mapato ya ndani ya TANESCO. Serikali imeendelea kujadiliana na washirika wa maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya utekelezaji endelevu wa mradi. 81. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kutekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni: kuendelea kutanua wigo wa usambazaji wa umeme mijini na maeneo ya pembezoni mwa miji yanayohitaji umeme katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Jumla ya Shilingi bilioni 4.0 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 3.0 ni fedha za nje. Aidha, TANESCO kupitia mapato yake ya ndani, imetenga Shilingi bilioni 188.70 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu katika maeneo ya mijini mikoa yote. 60 MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA – III) 82. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (Rural Energy Agency - REA) unaendelea. Mradi huu unalenga kufikisha umeme katika vijiji ambavyo hadi kufikia mwezi Desemba, 2015 vilikuwa havijafikiwa na miundombinu ya umeme. Katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari, 2016 hadi kufikia mwezi Mei, 2019 jumla ya vijiji vipya vilivyoongezeka kwa kuunganishwa umeme kupitia mradi huu ni 5,109 zaidi ya vijiji 2,018 vilivyokuwa na umeme hadi mwezi Desemba, 2015 na hivyo kufikisha jumla ya vijiji 7,127 vilivyounganishiwa umeme. Mzunguko wa Kwanza wa mradi huu utakapokamilika mwezi Juni, 2020 jumla ya vijiji 10,278 vitakuwa vimeunganishiwa umeme kati ya vijiji 12,268 sawa na asilimia 84 ya vijiji vyote Tanzania Bara. Vijiji 1,990 vitakavyobaki sawa na asilimia 16 ya vijiji vyote vitaanza kupelekewa umeme kuanzia Julai 2020 na kukamilika ifikapo Juni, 2021 na kuifanya Tanzania kufikisha miundombinu ya umeme 61 vijijini katika vijiji vyote Tanzania Bara. Aidha, hadi sasa jumla ya Taasisi za Elimu 3,165; Maeneo ya Biashara 3,451; Pampu za Maji 210; Taasisi za Afya 1,211 na Nyumba za Ibada 984 zimefikishiwa umeme. 83. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Miradi iliyopo chini ya Mpango wa REA III ni kama ifuatavyo: (i) Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Grid Extension) – Mzunguko wa Kwanza 84. Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa katika vijiji 3,559 vya mikoa yote ya Tanzania Bara na kuhusisha ujenzi wa njia za kusambaza umeme na ufungaji wa mashineumba. Hadi kufikia tarehe 15 Mei 2019, kazi zilizofanyika ni pamoja na: kuendelea kujenga miundombinu ya kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya mradi na hivyo kuunganisha wateja wa awali zaidi ya 56,920. Kazi zilizopangwa kufanyika katika mwaka 2019/20 ni: kuendelea kujenga miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme; na kuunganisha wateja. Utekelezaji wa usambazaji wa umeme vijijini umeongezeka kwa kasi

62 ambapo hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2016 upatikanaji wa umeme vijijini ulifikia asilimia 49.5 ikilinganishwa na upatikanaji wa umeme vijijini wa asilimia 21 mwaka 2015. Hata hivyo, kwa sasa upatikanaji wa umeme umeongezeka zaidi ya kipindi hicho kufikia vijiji 7,127 mwezi Mei, 2019. Ongezeko hili linaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki katika kusambaza umeme vijijini. Inatarajiwa kuwa ifikapo mwezi Juni, 2020 vijiji 10,278 ambavyo ni sawa na asilimia 84 ya vijiji vyote nchini vitakuwa vimefikishiwa umeme. (ii) Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Grid Extension) – Mzunguko wa Pili 85. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili utahusisha kusambaza umeme katika vijiji vilivyobakia 1,190 sawa na asilimia 16 ya vijiji vyote 12,268 vya Tanzania Bara. Mradi huu utahusisha ujenzi wa kilomita 35,581 za njia za umeme msongo wa kV 33; ujenzi wa kilomita 21,777 za umeme msongo wa kV 0.4; kufunga mashineumba 7,386; na kuunganisha wateja wa awali zaidi 63 ya 582,937. Kazi zitakazofanyika katika mwaka 2019/20 ni kutangaza zabuni za kuwapata wakandarasi na kuanza kazi. (iii) Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban Rural Electrification Program) 86. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha kusambaza umeme katika jumla ya maeneo 250 yakiwemo ya kibiashara, mitaa na vitongoji/vijiji. Jumla ya wateja wa awali zaidi ya 37,843 wataunganishwa umeme katika wilaya za Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ikiwemo Kigamboni ili kujazilizia vitongoji vilivyoachwa na kuboresha huduma za umeme katika maeneo hayo. Katika mwaka 2018/19, kazi zilizofanyika ni pamoja na kuwapata wakandarasi kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme ambapo zitafanyika kwa muda wa miezi 9 kuanzia mwezi Mei 2019. Kazi zitakazofanyika kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na Wakandarasi kuanza kazi za ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme na kuunganisha wateja.

64 (iv) Mradi wa Usambazaji Umeme katika maeneo ambayo yamefikiwa na Miundombinu ya Umeme Mzunguko wa Pili (Densification Round Two) 87. Mheshimiwa Spika, baada ya Mradi wa Ujazilizi Mzunguko wa Kwanza katika mikoa nane (8) ambayo ni Arusha, Iringa, Mara, Mbeya, Njombe, Pwani, Tanga na Songwe kukamilika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi huo katika awamu ya pili. Mradi wa ujazilizi mzunguko wa pili unahusisha kuongeza wigo wa kuunganisha umeme katika vitongoji vilivyobaki (alimaarufu kurukwa) na kufanya wananchi wengi kufikiwa na umeme. Kazi zilizopangwa kufanyika kwa mwaka 2019/20 ni kukamilisha taratibu za zabuni na kuwapata wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo. 88. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019, Wakala wa Nishati Vijijini ulikuwa umepokea jumla ya Shilingi bilioni 393.31 kati ya Shilingi bilioni 412.08 zilizopangwa kutumika kwa mwaka 2018/19 sawa na asilimia 95.4 ya bajeti. Aidha, katika mwaka 2019/20 fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kusambaza umeme 65 vijijini ni Shilingi bilioni 423.10, kati ya hizo Shilingi bilioni 363.10 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 60 ni fedha za nje. SEKTA NDOGO YA NISHATI JADIDIFU 89. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia EWURA imekamilisha mapitio ya utaratibu wa uendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme (Review of Small Power Projects Framework) ili kuvutia wawekezaji na kutatua changamoto zilizojitokeza kwa wadau wakati wa utekelezaji. Katika kukamilisha mapitio hayo, EWURA imerekebisha Kanuni za Uendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme za Mwaka 2018 (The Electricity (Development of Small Power Projects) Rules, 2018) yaliyohusisha kikokotoo cha bei ya umeme kwa miradi hiyo inayouza umeme kwa TANESCO na ile ya gridi ndogo (mini/micro grids) zinazouza moja kwa moja kwa wateja. Kanuni hizo za Mwaka 2019 (The Electricity (Development of Small Power Projects) Rules, 2019) zimetangazwa kupitia Gazeti la Serikali GN No. 380 ya tarehe 10 Mei, 2019. Kanuni hizi zitasaidia kudhibiti bei za umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo ambapo kwa sasa wanajipangia bei wenyewe na bei hurekebishwa kunapokuwa na malalamiko kutoka kwa wateja asilimia 15 au zaidi. 66 90. Mheshimiwa Spika, ili kuleta usawa katika bei ya umeme kwa maeneo ambayo yanapata huduma za umeme kupitia mfumo wa Solar Mini Grid hususan maeneo ya Visiwani na ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa, maeneo hayo yataendelea kuunganishiwa umeme kwa gharama sawa na zinazotozwa na REA na TANESCO. Nishati inayotokana na Nguvu ya Jua, Upepo na Maporomoko Madogo ya Maji 91. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 Serikali iliendelea kuhamasisha matumizi ya nishati itokanayo na nguvu ya jua katika nyumba (Solar Home System) na taasisi za huduma za jamii. Kupitia mfumo huu, matumizi ya nishati ya jua yaliongezeka kwa jumla ya MW 10 na hivyo kufanya matumizi ya nishati hiyo hadi sasa kufikia MW 26. Vilevile, Serikali iliendelea na jitihada za kuhamasisha na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika nishati jua kwa kutumia mfumo wa gridi ndogo. Aidha, kwa mwaka 2019/20 mchango wa miradi midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko madogo ya maji na upepo unatarajiwa kuongezeka kwa jumla ya MW 7.7 kutokana na kukamilika kwa miradi ya 67 Lugarawa MW 1.7 Wilayani Ludewa; Maguta MW 1.2 Wilayani Kilolo; Luponde MW 1.0 Wilayani Njombe; Suma MW 1.4 Wilayani Rungwe; na Mradi wa Upepo wa Mwenga MW 2.4 Wilayani Mufindi. Matumizi Bora ya Nishati (Energy Efficiency) 92. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: Serikali kuridhia utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Matumizi Bora ya Nishati (Energy Efficiency Action Plan); na kukamilika kwa rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi Bora ya Nishati (Energy Efficiency Strategy). Aidha, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) zilibainishwa kama taasisi zitakazoshiriki katika utekelezaji wa Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati na kuanza kujengewa uwezo wa jinsi ya kutekeleza Mpango kazi huu. 93. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- pangwa kutekelezwa katika Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati kwa mwaka

68 2019/20 ni pamoja na: kuboresha Mpango Kazi huo kwa kuoanisha na Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi Bora ya Nishati; kuandaa muundo thabiti wa kitaasisi utakaokuwa na jukumu la kusimamia utekelezaji wa Mpango Kazi huu; na kutoa elimu ya matumizi bora ya nishati kwa wananchi na Taasisi za Serikali. Programu ya Nishati Endelevu kwa Wote (Sustainable Energy for All – SE4ALL) 94. Mheshimiwa Spika, katika programu ya upatikanaji wa nishati endelevu kwa wote inayolenga kuongeza mchango wa nishati jadidifu na kukuza matumizi bora ya nishati hapa nchini, kwa mwaka 2018/19 Serikali ilikamilisha maandalizi ya miongozo ya utekelezaji wa programu hii ikiwemo: mkakati wa upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kufikia malengo ya programu; Mkakati wa Mawasiliano; Mpango wa ushirikishwaji wa mamlaka zote na wananchi (Regionalization); na kuzijengea uwezo Wizara na Taasisi mbalimbali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya nishati. Aidha, kupitia programu hii, Mpango wa Kijinsia wa Utekelezaji wa Jitihada za Upatikanaji wa Nishati kwa Wote (Gender Action Plan for Implementation of Sustainable Energy for All Initiatives) 69 uliandaliwa na mfumo wa ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za nishati jadidifu hapa nchini ulianza kuandaliwa. 95. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2019/20 kazi zilizopangwa ni pamoja na: kuanza kwa utekelezaji wa Tanzania Energy Gender Action Plan; kukamilisha uandaaji wa mfumo wa ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za nishati jadidifu; na kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Serikali na Sekta Binafsi katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya nishati jadidifu nchini. Jumla ya Shilingi bilioni 3 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi milioni 500 fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.50 fedha za nje zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Uendelezaji wa Rasilimali ya Jotoardhi (Geothermal) 96. Mheshimiwa Spika, katika kutimiza azma ya nchi kuwa na usalama wa nishati (energy security) kwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali ambavyo ni nafuu, endelevu na rafiki kwa mazingira ikiwemo jotoardhi, Serikali kupitia Wizara ya Nishati imelenga kuzalisha umeme MW 200

70 utokanao na Jotoardhi ifikapo mwaka 2025. Pamoja na uzalishaji wa umeme, rasilimali ya jotoardhi ina manufaa mengine mengi kupitia mchango wake katika maendeleo ya sekta nyingine za uchumi kama vile kukausha mazao, ufugaji wa samaki, mabwawa ya maji moto kwa ajili ya kuogelea, uchakataji wa bidhaa za viwandani na hivyo kuboresha pato na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa. 97. Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza miradi mitano (5) ya kipaumbele katika maeneo ya Ngozi na Kiejo-Mbaka mkoani Mbeya, Songwe mkoani Songwe, Luhoi mkoani Pwani na Natron mkoani Arusha. Utekelezaji wa miradi hii upo katika hatua ya uhakiki wa rasilimali ya Jotoardhi kwa kuchoronga visima vya utafiti isipokuwa mradi wa Natron ambao upo katika hatua ya utafiti wa kina. Kwa kawaida, utekelezaji wa miradi ya jotoardhi hupitia hatua mbalimbali muhimu ikiwa ni pamoja na (i) utafiti (exploration), (ii) uhakiki (test drilling), (iii) uendelezaji (development), (iv) uvunaji (exploitation) na (v) utumiaji (utilization). 98. Mheshimiwa Spika, hatua hizo hutekelezwa kwa mpangilio maalumu bila kuruka hatua yoyote na unachukua muda 71 wa kati ya miaka 6 hadi 8 ili kukamilisha hatua hizi. Pamoja na kwamba hatua za awali za uendelezaji wa jotoardhi huchukua muda mrefu na ni wa gharama kubwa, umeme utokanao na jotoardhi ni wa uhakika na bei nafuu kwa kuwa uzalishaji wake hautegemei mafuta wala hali ya hewa. Miradi mitatu (3) ambayo itatekelezwa katika mwaka 2019/20 ni Ngozi, Songwe na Kiejo-Mbaka. (i) Mradi wa Ngozi (Mbeya) 99. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusu uzalishaji wa umeme unaotokana na Jotoardhi katika eneo la Ngozi, mkoani Mbeya kwa kuanza na uzalishaji wa MW 30. Kwa sasa mradi upo katika hatua ya uhakiki wa rasilimali ya Jotoardhi kwa kuchoronga visima vitatu (3) vya utafiti(exploratory wells). Shughuli za maandalizi ya uchorongaji wa visima hivyo vya utafiti zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni pamoja na: kuajiri Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuandaa mpango na kusimamia uchorongaji; taratibu za ununuzi wa mtambo wa uchorongaji wa visima vya utafiti; na maandalizi ya upimaji na uthamini wa ardhi hitajika kwa ajili ya uchorongaji. Katika mwaka 2019/20 Serikali itaendelea na taratibu za ununuzi wa mtambo 72 wa kuchoronga visima vya utafiti. Aidha, Serikali imetenga fedha Shilingi bilioni 8 kwa ajili ya kuchoronga visima vitatu (3) vya utafiti katika eneo la Ngozi. Kati ya fedha hizi Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 7.50 ni fedha za nje. Ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme unatarajiwa kuanza mwaka 2021 na kukamilika mwaka 2023. (ii) Mradi wa Songwe (Mkoani Songwe) na Mradi wa Kiejo-Mbaka (Mbeya) 100. Mheshimiwa Spika, Miradi hii inahusu uzalishaji wa umeme na matumizi mengineyo (direct uses) katika maeneo ya Songwe, mkoani Songwe na Kiejo- Mbaka, mkoani Mbeya ambapo imefikia hatua za uchorongaji wa visima vya utafiti. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizokamilika katika mradi wa Songwe ni Upembuzi Yakinifu wa Awali (Pre-feasibility Study) wa matumizi mengineyo ya Jotoardhi ambayo ni pamoja na kukaushia mazao ya kilimo na mifugo, mabwawa ya kuogelea na shughuli za utalii. 101. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- fanyika hadi sasa katika mradi wa

73 KiejoMbaka ni pamoja na kuwasilisha maombi ya ufadhili wa mradi kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jotoardhi Afrika (GRMF) kwa ajili ya uchorongaji wa visima vya utafiti. Kazi zilizopangwa kufanyika katika kipindi cha mwaka 2019/20 ni: kufanya maandalizi ya uchorongaji wa visima vya utafiti; na kuanza ujenzi wa miradi ya matumizi mengineyo ya jotoardhi katika maeneo hayo. Shilingi bilioni 1.31 fedha za ndani ya Kampuni (TGDC) zimetengwa katika mwaka 2019/20 kugharamia utekelezaji wa kazi hizo. Utekelezaji wa miradi ya matumizi mengineyo unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwaka 2021. 102. Mheshimiwa Spika, sambamba na utekelezaji wa miradi ya jotoardhi, Serikali inaendelea na juhudi za kuandaa mazingira wezeshi ya uendelezaji na utumiaji wa jotoardhi. Kwa sasa leseni za utafiti za jotoardhi zinasimamiwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Hata hivyo, Serikali inaendelea kutathmini changamoto za utekelezaji wa miradi ya jotoardhi kwa kutumia sheria husika na kuchukua hatua stahiki. Aidha, Serikali imeendelea kutoa fedha za uendelezaji wa miradi ya jotoardhi 74 kupitia bajeti ya kila mwaka na kujenga uwezo wa wataalam wa ndani. Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi mwezi Mei, 2019 zaidi ya wataalamu 15 walipata mafunzo mbalimbali ya muda mrefu katika nyanja za utafiti na uhakiki wa jotoardhi ikilinganishwa na wataalamu 7 waliokuwepo wakati TGDC inaanzishwa. SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI ASILIA Shughuli za Utafutaji, Uzalishaji na Usambazaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini 103. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Mei, 2019 jumla ya Futi za Ujazo Trilioni 57.54 za gesi asilia zimegunduliwa hapa nchini. Katika kipindi cha mwaka 2018/19, shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia zimeendelea kutekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni za Kimataifa za Mafuta (IOCs). Uchukuaji wa data za mitetemo (seismic data acquisition) za 2D zenye kilomita 442 za mstari katika Kitalu cha Ruvu umekamilika. Uchakataji na tafsiri

75 ya data hizo ili kubaini ukubwa wa mashapo na eneo zuri la kuchoronga visima vya utafutaji na uendelezaji bado unaendelea. Aidha, maandalizi ya awali ikiwemo ujenzi wa barabara na kupatikana kwa vibali kwa ajili ya kuchoronga visima vya Hammerkop-1 na Kito-1 katika Kitalu cha Rukwa Kusini na Kilosa-Kilombero sawia yamekamilika. 104. Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa gesi asilia nchini katika vitalu vya Mnazi Bay na Songo Songo umeongezeka hadi kufikia Futi za Ujazo Milioni 190 kwa siku kwa mwaka 2018/19, ikilinganishwa na wastani wa Futi za Ujazo Milioni 175 kwa siku kwa mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la asilimia 8.6. Ongezeko hili la uzalishaji wa gesi asilia limetokana na ongezeko la mahitaji katika matumizi viwandani, majumbani na kuzalisha umeme. Gesi asilia inachangia zaidi ya asilimia 60 ya umeme unaozalishwa nchini. Mahitaji ya gesi asilia katika kuzalisha umeme yameendelea kuongezeka ambapo yalifikia Futi za Ujazo bilioni 50.53 kwa mwaka 2018 kutoka Futi za Ujazo bilioni 42.79 mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 18.

76 UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA KATIKA VITALU VYA KIMKAKATI UNAOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC) 105. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kupitia TPDC unaendelea kwa kutoa kipaumbele katika Vitalu vya Eyasi – Wembere, 4/1B, Mnazi Bay Kaskazini na Songo Songo Magharibi. Aidha, Serikali inaendelea kukamilisha maandalizi ya Mkataba Kifani wa Ushirikiano katika Utekelezaji (Model Joint Operating Agreement) utakaosainiwa baina ya TPDC na Wabia katika kuendeleza vitalu vya kimkakati.

(i) Kitalu cha Eyasi – Wembere 106. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC imeendelea kutekeleza mradi wa utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Eyasi – Wembere kilichopo katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Kwa mwaka 2018/19, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kumpata Mshauri Mwekelezi wa kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira kwa ajili ya ukusanyaji wa data za mitetemo za 2D; kuandaa mkataba wa awali (MoU) kati ya Serikali za Tanzania 77 na Uganda kwa ajili ya utafiti wa awali; kukamilisha Hadidu za Rejea kwa lengo la kumpata Mbia wa Kimkakati; kukusanya taarifa za awali (reconnaissance survey); na kukamilisha maandalizi ya uchorongaji wa visima vifupi vya utafiti wa tabaka za miamba (Stratigraphic Boreholes) ambapo Mkandarasi wa kutekeleza kazi hiyo amepatikana.

107. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na: kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira kwa ajili ya ukusanyaji wa data za mitetemo za 2D; kuainisha na kufanya tathmini ya eneo litakaloathiriwa na mradi; kuchoronga visima vifupi vitatu (3) vya utafiti wa tabaka za miamba; kufanya utafiti wa kimaabara wa sampuli zitakazokusanywa kutoka katika visima vya stratigraphic; na kukusanya, kuchakata na kutafsiri data za mitetemo za 2D zenye urefu wa kilomita 150. Jumla ya Shilingi bilioni 1.00 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

(ii) Uchorongaji wa Kisima katika Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini 108. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC imeendelea na mpango wa kuchoronga 78 kisima cha utafutaji mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini kufuatia matokeo chanya ya tafsiri ya data za awali za mitetemo (3D) zenye kilomita za mraba 132. Tafsiri ya data hizo imeonesha uwezekano wa kuwepo kwa gesi asilia katika Kitalu hiki. Kwa mwaka 2018/19, Serikali imetekeleza kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kukamilisha uchakataji na tafsiri ya data za mitetemo kiasi cha kilomita za mraba 132; kuandaa Mpango wa Uchorongaji wa Kisima (Drilling Programme); na kukamilisha taratibu za kumpata Mbia wa Kimkakati. 109. Mheshimiwa Spika, kazi zitakazo- tekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na: kumpata Mtaalamu Mshauri wa uchorongaji (drilling management consultant); kupitia na kutafsiri taarifa za kijiolojia; na kuchoronga kisima cha utafutaji mwezi Mei, 2020. Fedha za ndani Shilingi milioni 800 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo.

79 (iii) Uchukuaji wa data za mitetemo katika Vitalu Na. 4/1B na Mnazi Bay Kaskazini 110. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ukusanyaji na uchakataji wa data za mitetemo katika Kitalu Na. 4/1B na Mnazi Bay Kaskazini ili kubaini uwepo wa mashapo yenye viashiria vya mafuta au gesi asilia. Kwa mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kuboresha Mpango wa Usimamizi wa Mazingira (Environmental Management Plan); na kukamilika kwa Hadidu za Rejea za kumpata mbia wa kimkakati. Kwa mwaka 2019/20 kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na: kumpata Mshauri Mwelekezi wa kukusanya, kuchakata na kutathmini taarifa za mitetemo ya 3D zenye ukubwa wa kilomita za mraba 693.1 kwa kitalu cha 4/1B na Mnazi Bay Kaskazini kwa maeneo ambayo hayajafanyiwa utafiti; na kumpata Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kutathmini athari za mazingira. Jumla ya Shilingi milioni 850 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. (iv) Kitalu cha Songo Songo Magharibi 111. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu utafutaji wa mafuta na gesi asilia

80 katika kitalu cha Songo Songo Magharibi chenye mashapo yenye viashiria vya uwepo wa gesi asilia. Kwa kipindi cha mwaka 2018/19, TPDC imekamilisha kazi za awali za kukusanya data za mitetemo za 3D (seismic scouting) za kilomita za mraba 183.4. Aidha, Hadidu za Rejea za kumpata mbia wa kimkakati zimekamilika. Vilevile, katika kipindi hicho, TPDC imeendelea na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira. Katika mwaka 2019/20, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na: kufanya tafiti za kijiolojia na kijiofizikia; kumpata mbia wa kimkakati wa kutekeleza mradi; na kufanya maandalizi ya awali ya uchorongaji wa kisima cha utafiti. Jumla ya Shilingi milioni 55 zimetengwa na TPDC kutekeleza shughuli hizo. MIRADI YA KUSAFIRISHA NA KUSAMBAZA GESI ASILIA NCHINI 112. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha gesi hiyo inatumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo ya viwandani, majumbani, katika magari na 81 kuzalisha umeme. Miradi hiyo ni kama ifuatayo: (i) Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia Viwandani 113. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, TPDC imekamilisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika Kiwanda cha Dangote (awamu ya pili), Lodhia, Cocacola, kiwanda cha vifungashio kinachomilikiwa na Goodwill Ceramic Tanzania Limited na kazi ya kuunganisha kiwanda cha Knauf imefikia asilimia 80. Aidha, TPDC imekamilisha majadiliano ya mauziano ya gesi asilia na Kiwanda cha Shreeji Silcates. Katika kuendelea kutafuta wateja zaidi wa viwandani, TPDC imeanza majadiliano ya mauziano ya gesi asilia na kiwanda cha MM-1 Intergrated Steel Mills Ltd kilichopo Mikocheni – Dar es Salaam, pamoja na LN Future Building Materials Co. Ltd na Kings Alluminium vilivyopo Mkuranga - Pwani. 114. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, kazi za mradi zitahusu ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha viwanda vya Shreeji Silicates Tanzania Limited,

82 LN Future na Kings Aluminium. Vilevile, TPDC inatarajia kujenga trunk-line kutoka Mwenge hadi Tegeta na kuunganisha wateja mbalimbali wakiwemo Estim Construction, Chem & Cortex, Polypet, Interchik, Giraffe Hotel, Jangwani Sea Breeze, Ramada Resort Hotel, Landmark Hotel, Seascape Hotel na White Sands Hotel. Katika kutekeleza mpango huo, Shirika litafanya majadiliano na kusaini mikataba ya mauziano ya gesi asilia na wateja hao pamoja na kumtafuta Mkandarasi (EPC contractor). Fedha za ndani za Shirika Shilingi bilioni 11.22 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huu. (ii) Miradi ya Kusambaza Gesi Asilia Majumbani na Ujenzi wa Vituo vya Kujazia Gesi Asilia katika Magari 115. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC inaendelea kusambaza gesi asilia kwa wateja wa majumbani walio karibu na miundombinu iliyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Mradi wa kuunganisha wateja wa majumbani ulianza kutekelezwa mwaka 2016 na ni endelevu kupitia GASCO, kampuni tanzu ya TPDC. Katika mwaka 2018/19, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kukamilisha ujenzi wa mtambo wa kupunguza msukumo 83 wa gesi (Pressure Reduction Station) eneo la Ubungo Kibo; kukamilisha kazi za awali za ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia kutoka Ubungo Maziwa kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Savei, Mlalakuwa, Changanyikeni, Makongo Juu kuelekea Tegeta. Miundombinu hiyo itawezesha kuunganisha wateja wa gesi asilia majumbani zaidi ya 500 katika Jiji la Dar es Salaam. Ili kuhamasisha Watanzania wengi kutumia gesi hii na hivyo kupunguza gharama za maisha na kukabiliana na uharibifu wa mazingira, gharama ya bei ya gesi majumbani ina punguzo la asilimia 40 ukilinganisha na bei ya gesi ya mitungi (LPG). 116. Mheshimiwa Spika, maandalizi ya kusambaza gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara yanaendelea ambapo kwa upande wa Mkoa wa Mtwara, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kukamilisha taratibu za manunuzi ya mabomba, mita za gesi na vifaa vya kupunguza mgandamizo wa gesi (pressure reduction stations); kukamilisha michoro ya usanifu wa ujenzi wa miundombinu; na kupatikana kwa vibali vya ujenzi wa mradi. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kutandaza mabomba makubwa (trunk-lines) katika njia mbili, ya kwanza ikielekea Shule ya Sekondari 84 Ufundi Mtwara kwa ajili ya kusambaza gesi katika taasisi mbalimbali na makazi ya watu zaidi ya nyumba 125 za awali pembezoni mwa bomba la gesi. 117. Mheshimiwa Spika, miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika njia ya pili itaelekea Gereza la Lilungu ikiwa na matoleo kwa wateja walio pembezoni mwa miundombinu hiyo. Maandalizi ya usambazaji wa gesi majumbani kwa Mkoa wa Lindi yameanza ambapo kazi ya kutoboa bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa eneo la Lindi itakamilika mwezi Januari, 2020. Ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi na kazi ya kuunganisha wateja itaanza mwezi Juni, 2020 na itakuwa endelevu. 118. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Serikali kupitia TPDC imepanga kuunganisha wateja wa awali zaidi ya nyumba 1,000 katika Jiji la Dar es Salaam na nyumba zaidi ya 300 mkoani Mtwara. Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na: kumpata Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira Jijini Dar es Salaam kupitia maeneo ya Bagamoyo Road, Kilwa Road na Mandela

85 Road (Changombe, Kurasini, Keko); kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira mkoani Mtwara kwa kata za Railway, Shangani, Chikongola, Tandika, Likombe, Magomeni, Chuno na Majengo; na kuwapata wakandarasi (EPC contractors) wa kuunganisha gesi asilia majumbani Jijini Dar es Salaam na mkoani Mtwara. 119. Mheshimiwa Spika, TPDC pia itajenga kituo mama cha kupunguza mgandamizo wa gesi asilia (Compressed Natural Gas – CNG Mother Station) chenye kituo cha kujazia gesi katika magari eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, vituo vidogo vya kupunguza mgandamizo wa gesi asilia (CNG Daughter Stations) vitajengwa maeneo ya Hospitali ya Muhimbili, Soko la Samaki Feri na Ubungo. Kituo cha Ubungo kitatumika kujaza gesi katika Mabasi ya Mwendokasi zaidi ya 300 pamoja na magari mengine zikiwemo daladala. Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.10 fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. 120. Mheshimiwa Spika, katika kuendelea na juhudi za kuwezesha mikoa mingine nchini kunufaika na rasilimali ya gesi asilia, Serikali itaendelea kufanya tafiti za 86 namna bora ya kuunganishia mikoa hiyo na miundombinu ya kusafirisha na kusambaza rasilimali hiyo. Kwa kuanzia, usambazaji wa gesi asilia unatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Pwani, Tanga, Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza na Arusha. Mpango huu unatarajiwa kutekelezwa kati ya sasa na mwaka 2025. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya gesi asilia majumbani, TPDC itaongeza kasi ya kusambaza gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini.

(iii) Mradi wa Usambazaji wa Gesi Asilia kwa kuhusisha Sekta Binafsi katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam 121. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC imeanza kutekeleza mradi wa kusambaza gesi asilia katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam. Mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia nchini (Natural Gas Utilization Master Plan - NGUMP). Mradi unahusu ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia kwa kushirikisha wawekezaji binafsi kwa baadhi ya maeneo katika mikoa husika.

87 122. Mheshimiwa Spika, Wawekezaji wa sekta binafsi watapatikana kwa njia ya zabuni za ushindani wa kimataifa ili kuweka usawa na kupata wawekezaji wenye uzoefu na uwezo wa kiteknolojia na fedha za kugharamia mradi kwa masharti nafuu kwa Serikali. Kupatikana kwa wawekezaji kutaharakisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia na hivyo kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa muda mfupi. Katika mwaka 2018/19, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kukamilisha Upembuzi Yakinifu wa Awali (Pre-Feasibility Study) wa mradi; na kuendelea na taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi anayetarajiwa kupatikana mwezi Juni, 2019. 123. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi na kuwapata wawekezaji binafsi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi. Baada ya kupatikana kwa wawekezaji, ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi Juni, 2020 na awamu ya kwanza ya ujenzi inategemewa kukamilika mwezi Desemba, 2021.

88 (iv) Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea Mkoani Lindi 124. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa kiwanda cha mbolea chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.3 za urea kwa mwaka. Kiwanda hiki kinatarajiwa kujengwa eneo la Kilwa Masoko – Lindi na Kampuni ya Tanzania Mbolea and Petrochemicals Company Limited (TAMPCO) ambayo ni ubia wa TPDC, Ferrostaal Industrial Project GmbH ya Ujerumani, Fauji Fertilizer Company Limited ya Pakistan na Haldor Topsoe ya Denmark. Ujenzi wa mradi huu utafanikisha upatikanaji wa uhakika wa mbolea aina ya urea na hivyo kuchochea ukuaji wa Sekta ya Kilimo nchini. Manufaa mengine ni pamoja na: mapato yatokanayo na gawio na kodi mbalimbali; kutoa ajira za moja kwa moja kwa Watanzania zaidi ya 400; kuongeza fursa za utoaji huduma na ugavi wa bidhaa kwa kampuni za Tanzania; kujenga uwezo wa Watanzania katika uendeshaji wa viwanda vya mbolea; na kuongeza matumizi ya gesi asilia kwa wastani wa futi za ujazo milioni 70 hadi 100 kwa siku. 125. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni: kuendelea 89 na majadiliano ya namna bora ya utekelezaji wa mradi kati ya wawekezaji na Serikali; kuandaliwa kwa moduli ya kiuchumi ya mradi; na kukamilika kwa tathmini ya madai mapya ya fidia kwa wananchi watakaopisha mradi. Kazi zitazotekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni kukamilisha majadiliano kati ya Serikali na wawekezaji ambako kutawezesha kuanza kwa ujenzi wa mradi. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwaka 2021 na kukamilika mwaka 2024. Gharama ya mradi ni Dola za Marekani bilioni 1.9 sawa na takriban Shilingi trilioni 4.401. (v) Mradi wa Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda 126. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Tanzania hadi Uganda kwa kutumia mkuza wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Uganda hadi Tanga. Mradi unalenga pia kusambaza gesi asilia maeneo yatakayopitiwa na bomba hilo. Katika mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kusainiwa kwa Makubaliano ya Awali (Memorandum of Understanding – MoU) kati ya Serikali ya Tanzania na Uganda mwezi Agosti, 2018; kuundwa kwa Kamati ya Pamoja ya 90 Wataalamu (Joint Technical Committee - JTC) kutoka nchi zote mbili; kuandaa Mpango Kazi wa Mradi (Project Workplan); na kuanza taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi atakayefanya Upembuzi Yakinifu wa mradi. Katika mwaka 2019/20, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na kumpata Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi. Serikali imetenga Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kutekeleza kazi za awali za mradi huu kwa mwaka 2019/20. (vi) Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tegeta hadi Bagamoyo 127. Mheshimiwa Spika, mradi huu unalenga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Tegeta hadi Bagamoyo ili kusambaza gesi asilia katika eneo la viwanda la Zinga, Bagamoyo pamoja na wateja wengine waliopo katika maeneo yanayopitiwa na mradi yakiwemo Bagamoyo Export Processing Zone – EPZ, majumbani na taasisi mbalimbali. Bomba la kusafirisha gesi asilia kwenda maeneo hayo linakadiriwa kuwa na urefu wa kilomita 30 na uwezo wa kusafirisha futi za ujazo milioni 250 kwa siku. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 22.74 91 sawa na takriban Shilingi bilioni 52.67. Kukamilika kwa mradi huu kutachochea ukuaji wa viwanda katika eneo la Bagamoyo kwa kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa nishati ya bei nafuu na kuongeza matumizi ya gesi asilia kwa wateja mbalimbali wanaopitiwa na miundombinu hiyo. 128. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- tekelezwa hadi sasa ni pamoja na kukamilisha utafiti wa masoko (market survey) kwa eneo litakalopitiwa na mradi, usanifu wa mradi (project design) na Upembuzi Yakinifu wa mradi (feasibility study). Katika mwaka 2019/20, shughuli zilizopangwa kutekelezwa zinajumuisha kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira na Kijamii zitakazotokana na utekelezaji wa mradi na kumpata Mkandarasi (EPC + Financing) wa kutekeleza mradi. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Juni, 2020 na kukamilika mwezi Juni, 2021. Serikali imetenga Shilingi milioni 300 fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza kazi za awali za mradi huu.

92 MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA (Liquefied Natural Gas - LNG) 129. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC imeendelea na maandalizi ya ujenzi wa mitambo ya kuchakata na kusindika gesi asilia iliyopo kina kirefu cha bahari katika Vitalu Na. 1, 2 na 4. Mitambo hiyo kwa ujumla itakuwa na uwezo wa kusindika tani milioni 10 za gesi asilia kwa mwaka (10 MTPA). Pamoja na gesi itakayosindikwa kusafirishwa nje, kipaumbele ni kupatikana kwa gesi ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi. Ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa maslahi mapana ya Taifa, Serikali iliekeleza Timu ya Majadiliano ya Serikali (Government Negotiation Team - GNT) kukutana na mwekezaji mmoja mmoja na si kwa pamoja kama ilivyokuwa awali. Katika kutekeleza hilo, GNT ilianza majadiliano na wawekezaji hao mwezi Aprili, 2019 na yanatarajiwa kukamilika ndani ya miezi saba (7). 130. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- tekelezwa kwa mwaka 2018/19 ni: kukamilisha Tathmini ya Athari za Mazingira na Kijamii (ESIA); kukamilisha Mpango wa uhamishaji wananchi watakaopisha Mradi (Resettlement Action Plan); kuanza kwa 93 majadiliano ya kimkataba (Host Government Agreement – HGA) baina ya Serikali na wawekezaji na kuandaliwa kwa moduli ya kiuchumi (economic model) ya Mradi. 131. Mheshimiwa Spika, mradi huu unatarajiwa kuleta manufaa makubwa nchini yakiwemo: kuongezeka kwa mapato ya Serikali yatakayotokana na mauzo ya gesi asilia; kuongezeka kwa fursa za ajira kwa Watanzania; kupatikana kwa gesi kwa ajili ya matumizi mbalimbali nchini; fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kutoa huduma na bidhaa katika mradi; na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Katika mwaka 2019/20, kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha majadiliano ya mradi na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi. Jumla ya fedha za ndani Shilingi bilioni 6.7 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi. Gharama za mradi ni Dola za Marekani bilioni 30 sawa na takriban Shilingi trilioni 69.49. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwaka 2022 na kukamilika mwaka 2028.

94 MIRADI YA KUHIFADHI NA KUSAFIRISHA MAFUTA (i) Mradi wa Hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta ya Akiba na Dharura Nchini 132. Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Petroli, 2015. Mradi huu pia unahusu ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi mafuta ya akiba ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta ya kutosha nchini wakati wote. Kwa kuanzia, TPDC imeainisha maeneo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga ambapo miundombinu hiyo itajengwa. Kwa upande wa Dar es Salaam, tathmini ya awali ya ardhi imekamilika na maandalizi ya kufanya tathmini kwa mikoa ya Tanga na Morogoro inaendelea. 133. Mheshimiwa Spika, kazi zilizo- tekelezwa kwa mwaka 2018/19 ni: kuandaliwa kwa Andiko la Biashara (Business Plan) pamoja na moduli ya kiuchumi; kuandaliwa kwa Hadidu za Rejea za kumpata mbia wa kimkakati; na kukamilika kwa kazi ya ukaguzi na usanifu wa Tenki Na. 8 litakalotumika kuhifadhia mafuta. Kazi zitakazotekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni kukarabati Tenki Na. 8 na kuendelea na taratibu za kutwaa ardhi 95 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga. Shilingi milioni 400 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo. Jumla ya Dola za Marekani milioni 250 sawa na takriban Shilingi bilioni 579.10 zinahitajika kwa kuanza uagizaji wa mafuta ya hifadhi. (ii) Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale (Uganda) hadi Bandari ya Tanga (Tanzania) 134. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi(crude oil) kutoka Kabaale nchini Uganda hadi mkoani Tanga nchini Tanzania. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 3.5 ambazo ni takriban Shilingi trilioni 8.1. Katika mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kuendelea na majadiliano ya mkataba kati ya kampuni ya mradi na Nchi Hodhi (Host Government Agereement – HGA); kuendelea na maandalizi ya majadiliano ya Mkataba wa Ubia (Shareholding Agreement – SHA) ambayo yanategemewa kukamilika mwezi Juni 2019; na kukamilika kwa tathmini ya fidia kwa maeneo ya kipaumbele (camps and coating yard) na eneo lote la mkuza. 96 135. Mheshimiwa Spika, mradi huu unatarajiwa kuleta manufaa makubwa nchini yakiwemo: kuongeza mapato ya Serikali kutokana na gawio la uwekezaji katika mradi kupitia TPDC na kodi mbalimbali; kuongeza ajira kwa Watanzania; fursa kwa Watanzania kutoa huduma na bidhaa katika mradi; kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika mikoa itakayopitiwa na Bomba; na ukuaji wa Bandari ya Tanga. Kwa mwaka 2019/20 kazi zilizopangwa kutekelezwa ni kukamilisha majadiliano ya Mkataba wa Ubia (SHA) kati ya nchi washirika na kampuni zilizowekeza katika mradi pamoja na kulipa fidia wakazi watakaohamishwa kupisha eneo la mkuza litakapopita bomba hili. Serikali imetenga Shilingi bilioni 7 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi. Ujenzi wa mradi unategemewa kuanza mwezi Septemba, 2019 na kukamilika mwaka 2021.

(iii) Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Safi (White Petroleum Products) kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola (Zambia) 136. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa bomba la kusafirisha 97 mafuta safi (white petroleum products) kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola (Zambia). Mradi utakuwa na matoleo (take– off points) katika maeneo ya Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe. Utekelezaji wa mradi huu utaongeza uhakika wa upatikanaji mafuta katika mikoa inayopitiwa na bomba hilo sambamba na kuongeza mapato na ajira. Aidha, utekelezaji wa mradi utaepusha uharibifu wa miundombinu ya barabara na kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam. Mradi huu vilevile utapunguza changamoto ya usambazaji mafuta kwa nchi zinazotumia bandari zetu kuingizia mafuta yao na pia utafungua fursa za kibiashara katika ukanda wa nyanda za juu kusini. Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia. 137. Mheshimiwa Spika, hadi sasa, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kuandaa Andiko la Mradi; na kuandaa Hadidu za Rejea za kumpata Mshauri Mwelekezi atakayefanya Upembuzi Yakinifu wa mradi na Tathmini ya Athari za Mazingira na Kijamii (ESIA). Kazi iliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni kufanya Upembuzi Yakinifu (feasibility study) utakaoainisha gharama za 98 mradi na namna bora ya kutekeleza mradi. Serikali imetenga Shilingi milioni 800 kwa ajili ya kazi hiyo. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 1.5 sawa na takriban Shilingi trilioni 3.474. UDHIBITI WA SHUGHULI ZA MKONDO WA JUU WA MAFUTA NA GESI ASILIA 138. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Serikali kupitia PURA imeendelea na udhibiti wa shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini katika vitalu 11 kupitia mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Mapato (Production Sharing Agreements – PSAs). Mikataba iliyopo ilisainiwa katika miaka ya 2001 hadi 2012 kabla ya Sheria ya Petroli ya Mwaka 2015. Aidha, Sheria za Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) pamoja na Natural Wealth and Resources (Re-negotiations of unconscionable terms) za mwaka 2017 zinahitaji mikataba mbalimbali kupitiwa upya ili iendane na mahitaji ya sasa yanayolenga rasilimali ya gesi kunufaisha ipasavyo Serikali na wananchi. Kutokana na matakwa hayo, kazi ya kudurusu mikataba hii inaendelea kutekelezwa chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 99 139. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu la kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli kwa mwaka 2018/19, Serikali kupitia PURA imeendelea: kusimamia uchukuaji wa data za mitetemo za 2D zenye kilomita 442 za mstari katika Kitalu cha Ruvu; na kusimamia maandalizi ya awali ya uchorongaji wa Visima vya Hammerkop-1 na Kito-1 katika vitalu vya Rukwa Kusini na Kilosa-Kilombero sawia. Vilevile, Mamlaka imeendelea kufanya kaguzi katika maeneo ya utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia. 140. Mheshimiwa Spika, PURA imeendelea na shughuli za uhakiki wa gharama za uwekezaji, ambapo hadi kufikia mwezi Aprili, 2019 gharama na mapato kwa mikataba yote 11 kwa miaka ya 2016 na 2017 vimehakikiwa. Lengo ni kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kupata stahiki yake kulingana na mikataba iliyopo. Vilevile, Mamlaka hiyo imehakiki na kupitisha Mpango Kazi na Bajeti ya mwaka 2019 kwa kampuni zote zinazotekeleza shughuli za utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia. 141. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, Serikali kupitia PURA itadhibiti shughuli za uchorongaji wa kisima cha Kito- 100 1 katika Kitalu cha Kilosa-Kilombero, Kisima cha Hammerkop-1 katika Kitalu cha Rukwa Kusini na visima viwili katika Kitalu cha Ruvu. PURA itasimamia uchukuaji data za mitetemo za 2D zenye jumla ya kilomita za mstari 150 katika Kitalu cha Eyasi-Wembere na data za 3D zenye jumla ya kilomita za mraba 693.1 katika kitalu cha 4/1B na Mnazi Bay Kaskazini. Serikali imetenga Shilingi billioni 1.69 kwa ajili ya kuwezesha Mamlaka hiyo kutekeleza shughuli zake kwa mwaka 2019/20. HALI YA UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI 142. Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa mafuta nchini imeendelea kuimarika. Serikali kupitia Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA) inaendelea kuagiza na kupokea mafuta ya kutosha wakati wote. Kampuni za mafuta zimeendelea kuagiza mafuta kupitia Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Bulk Procurement System - BPS) kupitia PBPA. Kati ya mwezi Januari hadi Desemba, 2018 jumla ya lita bilioni 5.70 za mafuta ziliagizwa kupitia Bandari za Dar es Salaam, Tanga na 101 Mtwara sawa na ongezeko la asilimia 6.3 ikilinganishwa na lita za mafuta bilioni 5.36 zilizoagizwa mwaka 2017. Kati ya kiasi hiki, lita bilioni 3.27 sawa na asilimia 57.4 ya mafuta yote yaliyoingizwa yalikuwa ni kwa ajili ya matumizi ya ndani, sawa na ongezeko la asilimia 2.5 ikilinganishwa na lita bilioni 3.19 zilizoingizwa mwaka 2017. 143. Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, lita bilioni 2.43, sawa na asilimia 42.6 ya mafuta yote yaliyoingizwa yalikuwa ni kwa ajili ya nchi jirani (on transit) sawa na ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na mafuta ya transit yaliyoingizwa mwaka 2017. Kiasi cha mafuta ya dizeli yaliongezeka kwa asilimia 1.3 tu wakati mafuta ya taa na mafuta mazito yalipungua kwa asilimia 11 na asilimia 54.4 sawia ikilinganishwa na mwaka 2017. Hii inatokana na kupungua kwa matumizi ya mafuta ya dizeli na mafuta mazito katika uzalishaji wa umeme. Pia, matumizi ya mafuta ya taa yanaendelea kupungua kutokana ongezeko la usambazaji wa umeme nchini hasa vijijini. 144. Mheshimiwa Spika, kuanzia mwezi Julai, 2018 Bandari ya Mtwara ilianza kupokea mafuta kwa ajili ya matumizi ya ndani 102 sambamba na Bandari za Dar es Salaam na Tanga. Kuanza kutumika tena kwa bandari hii kupokea mafuta kumeleta unafuu wa bei na upatikanaji wa mafuta kwa wananchi wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma. Unafuu huu wa bei umetokana na kupungua au kuondolewa kabisa kwa gharama za usafirishaji kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa hiyo. Mathalan, kwa Mkoa wa Mtwara takriban Shilingi 72 kwa lita zilizokuwa zinatumika kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara zimeondolewa. Pamoja na unafuu wa bei, kuanza kutumika kwa bandari hii kumepunguza muda uliokuwa ukitumika kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam hadi mikoa hiyo ya kusini na kupunguza uharibifu wa barabara. 145. Mheshimiwa Spika, Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja umewezesha upatikanaji wa mafuta ya kutosha yanayotabirika na gharama nafuu. Manufaa mengine ni pamoja na: upatikanaji wa mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi na yenye viwango vya ubora unaotakiwa; kupungua kwa gharama za uagizaji wa mafuta ikiwemo Demurrage Charges ambazo zimeshuka kutoka kati ya siku 30 na 60 hadi 103 kati ya siku 3 na 8; kupatikana kwa takwimu sahihi za mafuta nchini na hivyo kuimarisha ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali; kuvutia uwekezaji katika miundombinu ya kupokelea na kuhifadhi mafuta katika Bandari za Tanzania na sehemu mbalimbali za kimkakati (Strategic Areas) nchini; na kuendelea kuvutia nchi za jirani (Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia na Malawi) kupokea mafuta yao kupitia Bandari za Tanzania na hivyo kuongeza mapato ya nchi.

146. Mheshimiwa Spika, pamoja na manufaa hayo Serikali inaendelea kuvutia wawekezaji zaidi kutumia mfumo huu ambapo Serikali ya Tanzania imeanza majadiliano na Rwanda ili kuanza kutumia Bandari ya Kemondo iliyopo Bukoba kupokea mafuta kwa ajili ya matumizi ya nchi hiyo. Mafuta hayo yatasafirishwa kwa njia ya reli kutoka Dar es Salaam au Tanga. Aidha, Serikali ya Tanzania imedhamiria kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya Bandari ya Mbamba Bay pamoja na barabara ili kuleta wepesi kwa nchi ya Malawi kupitisha mafuta yake nchini kupitia Bandari ya Mtwara.

104 147. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na tafiti za namna bora ya kutekeleza uagizaji wa pamoja wa gesi ya mitungi kwa ajili ya kupikia majumbani (Liquefied Petroleum Gas LPG) nchini kwa Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja (BPS). Kiwango cha uagizaji wa gesi ya LPG kimeongezeka kufikia tani 142,940 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na tani 107,263 kwa mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 33. Ongezeko hili linatokana na: kuongezeka kwa uelewa wa watumiaji kuhusu faida za kutumia gesi; na kuongezeka kwa miundombinu ya kujazia, kuhifadhia, na kusambaza LPG. 148. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa katika maeneo mengi ya vijijini mafuta yanatunzwa na kuuzwa kwa namna hatarishi. Hali hiyo imetokana na kusuasua kwa uwekezaji wa ujenzi wa vituo vya mafuta katika maeneo hayo. Katika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo, mwezi Septemba, 2018 EWURA iliingia mkataba na Kitengo cha Ushirikiano na Viwanda (Bureau of Industrial Cooperation - BICO) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kubuni namna bora na salama ya kusambaza mafuta vijijini kwa kutumia vituo vinavyohamishika (mobile 105 fuel dispensing facilities). Tayari BICO wameshaanza kutengeneza mfumo huo kwa ajili ya majaribio ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2019. Ili kuwezesha Mfumo huo kufanya kazi, EWURA imeshaandaa Kanuni zitakazotumika kusimamia mfumo husika na zitapelekwa kwa wadau ili kupata maoni kabla ya kuanza kutumika. Lengo la Serikali ni kuhakikisha usalama na upatikanaji wa mafuta katika maeneo ya vijijini. MRADI WA KUJENGA UWEZO KATIKA SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI ASILIA 149. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Usimamizi wa Rasilimali za Mafuta na Gesi Asilia Nchini (Institutional Support Project for Domestic Resource Mobilization and Natural Resource Governance) una lengo la kujenga uwezo kwa watendaji wa tasnia ya uziduaji (extractive industry). Lengo kuu likiwa ni kuwezesha Serikali kusimamia mapato hususan katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia. Mradi huu unatekelezwa kwa makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa Maendeleo ya Afrika (African Development 106 Fund) ulio chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika. 150. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni: kukamilisha mikataba itakayowezesha ujenzi wa skana ya Bandari ya Dar es Salaam pamoja na ununuzi wa vifaa vya kuhifadhia data za Petroli za PURA. Aidha, kupitia mradi huu TPDC imefanikiwa kuchakata na kutafsiri data za mitetemo za 3D na kuandaa Mpango wa Uchorongaji kisima cha utafiti katika Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini. Vilevile, mradi umewezesha mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 8 kutoka TPDC na mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 50 wa Wizara, PURA, EWURA, TRA na Timu ya Majadiliano ya Mradi wa LNG katika masuala ya usimamizi na uendeshaji ya miradi ya mafuta na gesi asilia.

151. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2019/20, kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na: ununuzi wa mifumo ya ukusanyaji mapato, skana, mfumo wa kielektroniki wa uondoshaji shehena bandarini na katika mipaka, kukamilisha ununuzi na ufungaji wa vifaa vya kuhifadhia data za petroli.

107 Jumla ya Shilingi bilioni 6.34 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2019/20 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 2.60 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 3.74 ni fedha za nje. E. UIMARISHAJI WA MAWASILIANO KATI YA WIZARA NA JAMII 152. Mheshimiwa Spika, katika hatua ya kuimarisha mawasiliano kati ya Wizara na Jamii kuhusu masuala yanayotekelezwa na Serikali chini ya Sekta ya Nishati, Wizara imeendelea kuandaa na kutoa taarifa kwa wadau wa ndani na nje ya nchi. Taarifa hizo zinajumuisha: kuratibu mahojiano kati ya Waziri wa Nishati na Jarida la Forbes Afrika litakalochapisha mafanikio ya Sekta ya Nishati; kuratibu mikutano ya wadau wa umeme kuhusu Mradi wa Rufiji iliyofanyika katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya, Njombe na Pwani kwa lengo la kujenga uelewa kwa wananchi na kuwahamasisha juu ya utunzaji wa vyanzo vinavyotiririsha maji katika Mto Rufiji; kuratibu uandaaji na urushaji wa makala (documentary) iliyoeleza mafanikio ya Sekta ya Nishati ya miaka mitatu (2015-2018) ambayo ilirushwa na Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC 1) 108 tarehe 13 Septemba, 2018; na kusambaza habari za Wizara na Taasisi zake katika Magazeti na Mitandao ya Kijamii ikiwemo ya facebook, Twitter, Instagram na You Tube pamoja na kushughulikia kero za wananchi zinazotumwa katika mitandao hiyo. Aidha, Wizara imezindua jarida (Nishati News Bulletin) linalotoa taarifa mbalimbali kuhusu Sekta ya Nishati. 153. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/20, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuimarisha mawasiliano na Jamii ili kuendelea kukuza uelewa wa masuala yanayotekelezwa na Serikali chini ya Sekta ya Nishati. Pamoja na mambo mengine, Wizara itaendelea kutoa taarifa mbalimbali katika maeneo muhimu na miradi mikubwa inayotekelezwa na Wizara katika kipindi husika.

F. AJIRA NA MAENDELEO YA RASILIMALIWATU 154. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza majukumu ya Wizara kwa ufanisi baada ya kugawanywa kwa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Nishati iliandaa na kutekeleza Muundo wake ambao 109 uliidhinishwa mwezi Juni, 2018. Kutokana na kuidhinishwa kwa Muundo huo, Wizara imeandaa Mahitaji ya Kazi (Job Listing); Maelezo ya Kazi (Job Descripitions) na mapendekezo ya kujaza nafasi mbalimbali za Uongozi kulingana na Muundo huo. Nyaraka hizo ziliwasilishwa katika Mamlaka husika kwa hatua zaidi. Wizara pia ilisimamia maandalizi ya Miundo ya Taasisi zilizo chini yake (TPDC na PURA) baada ya Miundo yake kuidhinishwa. Taratibu za kujaza nafasi kulingana na Miundo hiyo zinaendelea kutekelezwa. Vilevile, Miundo ya TANESCO na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja (PBPA) bado inaendelea kukamilishwa ili kuziwezesha Taasisi hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. 155. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza tija na motisha kwa Watumishi, katika mwaka 2018/19 Wizara iliwapandisha vyeo Watumishi 41 na kubadilisha kada (re-categorization) Watumishi watatu (3). Katika mwaka 2019/20, Wizara inatarajia kubadilisha kada za Watumishi wanne (4), kujaza nafasi 13 za uongozi na kuwapandisha vyeo Watumishi 48. Aidha, Wizara na Taasisi zake zinatarajia kuajiri jumla ya Watumishi 110 217 ambapo kati ya idadi hiyo, Wizara itaajiri Watumishi 53; TPDC Watumishi 116; REA Watumishi 9 na PURA Watumishi 39. 156. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa masuala ya mafuta na gesi asilia nchini, Wizara imeendelea kushirikiana na Washirika wa Maendeleo ili kutoa ufadhili wa masomo kwa Watanzania katika Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na Wataalamu wake wa kutosha katika sekta hiyo. Katika mwaka 2018/19 Watanzania 18 walipata fursa ya ufadhili wa masomo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China katika tasnia ya mafuta na gesi asilia. Aidha, Watanzania wengine 22 wanatarajiwa kwenda masomoni kupitia ufadhili wa Serikali ya China kwa mwaka 2019/20. Wizara imewasilisha Ubalozi wa China mapendekezo ya waombaji wenye sifa kwa ajili ya kukamilisha hatua muhimu za uchambuzi. 157. Mheshimiwa Spika, vilevile, katika kuwajengea uwezo Watumishi wa Wizara na Taasisi nyingine za Serikali, katika mwaka 2018/19 Wizara imewezesha na kutoa ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu kwa Watumishi 10 na mafunzo ya muda mfupi 111 kwa Watumishi 47. Kwa mwaka 2019/20, Watumishi 10 wanatarajiwa kupata fursa ya mafunzo ya muda mrefu na Watumishi 75 mafunzo ya muda mfupi. 158. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa huduma ya lishe na mlo kamili pamoja na fedha kwa ajili ya usafiri wakati wa kuhudhuria matibabu kwa watumishi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI ili waendelee kulitumikia Taifa. Wizara pia iliendesha mafunzo ya namna ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY), Ushauri Nasaha na Lishe Bora. Sambamba na jitihada hizo, Wizara pia inaendelea kuwahamasisha Watumishi kufanya mazoezi ya mwili na kupima afya hususan katika Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, kisukari na saratani. 159. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/19, Wizara imekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Wizara katika Mji Mpya wa Serikali eneo la Mtumba Jijini Dodoma. Utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Desemba 2018 na kukamilika mwezi Aprili 2019. Aidha, jengo hilo la Wizara limeanza kutumiwa rasmi 112 tarehe 15 Aprili, 2019 na Viongozi Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Idara na baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Sehemu. Katika mwaka 2019/20 Wizara inatarajia kuanza ujenzi wa jengo la pili la ofisi litakalokidhi mahitaji ya watumishi wote ambapo Shilingi bilioni 2.4 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza ujenzi huo. G. USHIRIKIANO WA KIKANDA NA KIMATAIFA 160. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Nishati inapenda kuwashukuru Washirika wa Maendeleo na nchi wahisani ambao wameendelea kutoa michango yao katika kufanikisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wizara. Kwa niaba ya Serikali, napenda kutambua mchango wa: Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia (WB), Benki ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JBIC), United Bank for Africa (UBA); Economic Development Cooperation Fund (EDCF - Korea), Mfuko wa Uendelezaji Jotoardhi (Geothermal Risk Mitigation Facility - GRMF) pamoja na Taasisi na Mashirika ya: JICA (Japan), KfW (Germany), AFD (Ufaransa), Sida (Sweden), Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Umoja 113 wa Mataifa (UNDP), Shirika la Maendeleo la Canada (CIDA) na USAID (Marekani). 161. Mheshimiwa Spika, pia natoa shukrani kwa Serikali za Burundi, Canada, China, Finland, Iceland, Japan, Sweden, Ufaransa, Ujerumani, Norway, Korea ya Kusini, Misri, Rwanda, Uganda na Zambia kwa ushirikiano wao katika kuendeleza Sekta ya Nishati. Vilevile, nishukuru Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa ushirikiano katika masuala ya kikanda yanayohusu Sekta hii. Kwa kipindi cha mwaka 2019/20 Wizara itaendelea kushirikiana kwa karibu na Washirika hawa wa maendeleo na wadau wengine watakaojitokeza ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Nishati inaendelea kuwa chachu ya sekta nyingine katika kuleta maendeleo nchini.

H. SHUKRANI 162. Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Khamis Mgalu, (Mb.) kwa kunisaidia kwa kiasi kikubwa na kwa dhati kabisa katika kutekeleza majukumu 114 yangu. Aidha, napenda kumshukuru Katibu Mkuu Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua kwa uchapakazi mahiri na ushirikiano anaonipa katika kutekeleza shughuli za kila siku za Wizara. Vilevile, nawashukuru Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watumishi wote kwa ujumla kwa ushirikiano wao na juhudi zao wanazofanya kwa ajili ya kufanikisha kufikiwa kwa malengo ya Wizara. 163. Mheshimiwa Spika, kwa kipekee napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Chato kwa ushirikiano wanaonipa katika kutekekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ya jimbo. Nawaahidi kuwa sitawaangusha na nitaendelea kushirikiana nanyi katika kubuni mikakati mbalimbali ya kuendeleza shughuli za jimbo. Naishukuru sana familia yangu ikiongozwa na mke wangu Mama Kalemani pamoja na watoto wangu kwa kuendelea kuniombea na kuniunga mkono katika kutekeleza majukumu ya kitaifa.

115 I. HITIMISHO 164. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Mwaka 2019/20 inalenga kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa inazalisha umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na wenye gharama nafuu. Vilevile, bajeti imelenga kuimarisha shughuli za utafutaji na biashara ya mafuta na gesi asilia pamoja na kuwezesha wananchi kunufaika na rasilimali hizo. Lengo ni kuiwezesha Serikali kufikia azma ya kujenga uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. 165. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2019/20, Wizara ya Nishati inakadiria kutumia jumla ya Shilingi trilioni 2.142 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 1.692 iliyotengwa kwa Mwaka 2018/19, sawa na ongezeko la asilimia 26.6. Ongezeko hili limetokana na kuanza kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa Rufiji utakaozalisha MW 2,115.

166. Mheshimiwa Spika, fedha nyingi za ndani za miradi ya maendeleo zilizotengwa kwa mwaka 2019/20 zimeelekezwa katika miradi mitatu (3) ya kimkakati ambazo ni 116 Shilingi trilioni 1.86, sawa na asilimia 95.1 ya Bajeti yote ya Ndani. Miradi hiyo ni: Mradi wa Kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji, MW 2,115 (Shilingi trilioni 1.44); Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Shilingi bilioni 363.11); na Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Kinyerezi I Extension MW 185 (Shilingi bilioni 60). 167. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe bajeti ya jumla ya Shilingi 2,142,793,309,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake. Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo: (i) Shilingi 2,116,454,000,000 sawa na asilimia 98.8 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo za maendeleo, Shilingi 1,956,372,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 160,082,000,000 ni fedha za nje; na (ii) Shilingi 26,339,309,000 sawa na asilimia 1.2 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi 15,025,821,000 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 11,313,488,000 kwa ajili ya mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na

117 Taasisi zilizo chini yake. 168. Mheshimiwa Spika, naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Vilevile, Hotuba hii ina vielelezo mbalimbali ambavyo vimeambatishwa kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala muhimu yanayohusu Sekta ya Nishati. 169. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

118 VIELELEZO KUHUSU SEKTA YA NISHATI 1.0 UMEME NA NISHATI JADIDIFU Kielelezo Na. 1: Uwezo wa Mitambo ya Kufua Umeme Nchini hadi Mwezi Mei, 2019 1A: Mfumo wa Gridi ya Taifa

Jina la Kituo Uwezo (MW) Na. 1 Kidatu 204.00 2 Kihansi 180.00 3 Mtera 80.00 4 New Pangani Falls 68.00 5 Hale 21.00 6 Nyumba ya Mungu 8.00 7 Uwemba 0.84 8 Mwenga 4.00 9 Yovi 0.95 10 Matembwe 0.59 11 Darakuta 0.32 12 Andoya 1.00 13 Tulila 5.00

Jumla Ndogo - Maji 573.70 1 Songas 189.00 2 Ubungo Gas PP I 102.00 3 Tegeta Gas PP 45.00

119 4 Ubungo Gas PP II 129.00 5 Kinyerezi I 150.00 6 Kinyerezi II 248.22 7 Mtwara Gas PP 22.00 8 Somanga Gas PP 7.50 Jumla Ndogo - Gesi 892.72 1 Zuzu 7.40 2 Nyakato 63.00 3 Biharamuro 4.14 4 Ngara 2.50 5 Songea 7.67 6 Namtumbo 0.34 7 Ludewa 1.27 8 Mbinga 2.00 9 Madaba 0.48 Jumla Ndogo - Mafuta 88.80 1 TANWAT 1.50 2 TPC 9.00 Jumla Ndogo - Biomass 10.50 Jumla - Gridi 1,565.72 Chanzo: TANESCO

120 1B: Mfumo Nje ya Gridi ya Taifa Na. Jina la Kituo Uwezo (MW)

1 Bukoba 2.56 2 Kasulu 2.50 3 Kibondo 2.50 4 Kigoma 8.25 5 Liwale 0.85 6 Loliondo 5.00 7 Mafia 1.89 8 Mpanda 4.16 9 Sumbawanga 5.00 10 Tunduru 3.00 11 Inyonga 0.48 Jumla – Nje ya Gridi 36.18 Jumla Kuu 1,601.90 Chanzo: TANESCO

121 Kielelezo Na. 2: Njia za Kusafirisha Umeme na Vituo vya Kupoza Umeme

Urefu (km) Njia za Usafirishaji Umeme Na. hadi Mei, (Transmission Lines) 2019 1 Njia kuu za msongo wa 400kV 670 2 Njia kuu za msongo wa 220kV 2,940.7 3 Njia kuu za msongo wa 132kV 1,697.47 4 Njia kuu za msongo wa 66kV 543 Jumla 5,851.17

Vituo Vya Kupoza Umeme Na. Idadi (Substations) 1 Vituo vya msongo wa 220kV 20 2 Vituo vya msongo wa 132kV 27 3 Vituo vya msongo wa 66kV 7 Vituo vya msongo wa 4 67 33/11kV Jumla 121

Urefu wa Mkongo wa Na. Urefu Mawasiliano wa TANESCO Mkongo wa Mawasiliano (Op- 1 3,200 tic Fibre Cable) – km Chanzo: TANESCO

122 7 3 53 15 66 27 813 984 Nyumba za Ibada 7 1 6 22 11 412 752 1,211 Taasisi za Afya 3 4 3 0 64 10 126 210 Pump za Maji 8 0 27 15 10 ra 1,648 1,743 3,451 Biasha - 6 38 25 21 45 1,099 1,931 3,165 Taasisi za Elimu Mradi Miradi ya Awali Turnkey Phase II Turnkey Phase III BTIP_VEI Densification Round I Makambako-Songea Solar za Makonteina 1 2 3 4 5 6 7 Na Jumla Kielelezo Na. 3: Taasisi Zilizopatiwa Umeme Kupitia REA hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 Chanzo: REA 123 Kielelezo Na. 4: Maeneo yenye Viashiria vya Jotoardhi Nchini

Chanzo: TGDC

124 MAFUTA NA GESI ASILIA 2.0 Kielelezo Na. 5: Matumizi ya Gesi Asilia katika Kipindi cha Mwaka 2016 – 2018 (BCF) Chanzo: TPDC 125 Kielelezo Na. 6: Mwenendo wa Uagizaji Mafuta kwa Matumizi ya Ndani kwa Mwaka 2018 Chanzo: PBPA 126 Kielelezo Na. 7: Ujenzi wa Miundombinu ya Kusambaza Gesi Asilia Majumbani (Mikocheni – Dar es Salaam) Chanzo: TPDC 127 Kielelezo Na. 8: Mtambo wa Kupunguza Msukumo Gesi Asilia (Pressure Reduction and Metering Station – PRSM) uliosimikwa Ubungo Kibo katika Valvu Na. 15 Chanzo: TPDC 128 Kielelezo Na. 9: Mpango wa Kusambaza Gesi Asilia Mtwara (kwa kuanzia eneo la Bandari) 129 Chanzo: TPDC Kielelezo Na. 10: Mpango wa Kusambaza Gesi Asilia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Chanzo: TPDC

130 Kielelezo Na. 11: Gesi ya Kupikia (LPG) iliyoagizwa Nchini kwa Mwaka 2010 – 2018 Chanzo: EWURA 131 (Lita) 537,766 311,555 565,982 989,292 791,853 832,636 333,319 464,722 Wastani 2,467,365 1,265,405 wa Mauzo kwa Kituo kwa Mwaka 9 44 92 98 94 66 55 34 70 200 Mafuta Idadi ya Vituo vya 4,839,897 13,708,412 52,070,384 96,950,638 74,434,223 54,953,984 18,332,546 43,023,787 32,530,523 493,472,968 Mwaka (Lita) ya Mafuta kwa Wastani wa Matumizi Mikoa Kigoma Kilimanjaro Arusha Coast Dar es Salaam Dodoma Geita Iringa Kagera Katavi Kielelezo Na. 12: Wastani wa Mauzo ya Mafuta Kimkoa katika Vituo mbalimbali Nchini 132 (Lita) 438,150 314,706 255,242 838,406 140,557 931,819 808,344 778,259 665,670 Wastani 1,302,706 1,420,037 1,561,660 wa Mauzo kwa Kituo kwa Mwaka 32 48 55 62 73 36 88 26 32 17 39 53 Mafuta Idadi ya Vituo vya 3,654,477 14,020,811 15,105,887 14,038,293 80,767,764 61,203,623 51,121,346 29,818,207 13,741,841 30,352,084 35,280,506 137,426,041 Mwaka (Lita) ya Mafuta kwa Wastani wa Matumizi Mikoa Lindi Manyara Mara Mbeya Morogoro Mtwara Mwanza Njombe Rukwa Ruvuma Shinyanga Simiyu 133 (Lita) 328,110 604,185 822,296 Wastani 1,005,179 wa Mauzo kwa Kituo kwa Mwaka 20,775,220 28 30 59 20 1,460 Mafuta Idadi ya Vituo vya 9,187,073 18,125,550 59,305,549 16,445,910 Mwaka (Lita) ya Mafuta kwa 1,473,912,325 Wastani wa Matumizi Mikoa Jumla Tabora Tanga Singida Songwe Chanzo: EWURA 134 Kielelezo Na. 13: Mwenendo wa Bei za Mafuta Safi katika Soko la Dunia kwa Mwaka 2017 na 2018 Chanzo: EWURA 135 Kielelezo Na. 14: Idadi ya Vituo vya Mafuta Nchini hadi Mwezi Aprili, 2019

JUMLA YA JUMLA YA VITUO VYA VITUO VYA MKOA MAFUTA HADI MAFUTA HADI TAREHE 31 TAREHE 30 DESEMBA 2018 APRILI 2019 Arusha 98 98 Coast 94 104 Dar es Salaam 200 220 Dodoma 66 64 Geita 55 60 Iringa 34 35 Kagera 70 65 Katavi 9 11 Kigoma 44 39 Kilimanjaro 92 92 Lindi 32 25 Manyara 48 50 Mara 55 56 Mbeya 62 64 Morogoro 73 71 Mtwara 36 36 Mwanza 88 89 Njombe 32 32 Rukwa 17 18 Ruvuma 39 37 Shinyanga 53 59 136 JUMLA YA JUMLA YA VITUO VYA VITUO VYA MKOA MAFUTA HADI MAFUTA HADI TAREHE 31 TAREHE 30 DESEMBA 2018 APRILI 2019 Simiyu 26 28 Singida 20 22 Songwe 28 29 Tabora 30 31 Tanga 59 65 JUMLA YA IDADI YA 1460 1500 VITUO VYA MAFUTA Chanzo: EWURA

137 Waziri wa Nishati, Dkt (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori (wa kwanza kushoto), wakiwasha jiko linalotumia gesi asilia tayari kwa matumizi ya nyumbani katika eneo la Mikocheni Mtaa wa TPDC jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Palangu wilayani Songea, mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololiti Mgema. 138