VIONGOZI WAKUU WA WIZARA YA NISHATI Mhe. Dkt. Medard M. C. Kalemani (Mb.) Waziri wa Nishati Mhe. Subira K. Mgalu (Mb.) Dkt. Hamisi H. Mwinyimvua Naibu Waziri wa Nishati Katibu Mkuu Wizara ya Nishati i ii HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI MHE. DKT. MEDARD MATOGOLO CHANANJA KALEMANI (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2019/20 1 2 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia Taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2018/19 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa Mwaka 2019/20. 2. Mheshimiwa Spika, napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuendelea kuwajalia afya njema Viongozi wetu Wakuu wa Kitaifa, Waheshimiwa Mawaziri wenzangu, Waheshimiwa Wabunge na Viongozi wengine mbalimbali. Kipekee nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kuendelea kusimamia Sekta ya Nishati na leo kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2019/20. 3. Mheshimiwa Spika, naomba pia niungane na Mawaziri wenzangu, Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwa 1 ujumla kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maelekezo yake thabiti yanayonisaidia kuisimamia vema Sekta ya Nishati. Ni dhahiri kuwa Rais wetu amekuwa chachu katika kutekeleza mipango mikubwa na yenye tija katika Sekta ya Nishati hapa nchini. Mipango hiyo ni pamoja na kuanza kutekeleza Mradi Mkubwa wa kielelezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (MW 2,115). Napenda kuwaahidi Watanzania kuwa Wizara yangu kwa kushirikiana na Bunge lako Tukufu na wadau mbalimbali tutasimamia vema Mradi huu ili ukamilike kwa wakati. 4. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwashukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo mbalimbali wanayonipatia katika kusimamia Sekta ya Nishati. Nikiri kuwa maelekezo na miongozo ya viongozi wetu hawa ni msingi wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Nishati. Aidha, napenda 2 kumpongeza pia Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuendelea kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 5. Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii pia kuwapongeza Mawaziri walioteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nampongeza Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mhe. Angellah Jasmin Kairuki (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji); Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. Doto Mashaka Biteko (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Madini; Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo; na Mhe. Joseph George Kakunda (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara. 6. Mheshimiwa Spika, niwapongeze pia Naibu Mawaziri Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa (Mb.), aliyeteuliwa 3 kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Mhe. Constantine John Kanyasu (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii; Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo; na Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (Mb.), aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI. Nawatakia wateule wote kila la kheri katika kutekeleza majukumu yao ya Kitaifa. 7. Mheshimiwa Spika, napenda nikupongeze wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wote wa Kamati Mbalimbali za Kudumu za Bunge pamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bunge lako Tukufu kwa utendaji kazi wenu mahiri. Kwa namna ya pekee natoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dunstan Luka Kitandula (Mb.), Makamu Mwenyekiti Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri (Mb.), na Wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa ushauri na maelekezo wanayotupatia. Nikiri kuwa Kamati hii imefanya kazi kubwa ya kuishauri Wizara katika masuala mbalimbali na kuchambua kwa kina mapendekezo 4 ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2019/20. Wizara itaendelea kushirikiana na Kamati hii katika kusimamia kwa ufanisi ustawi wa Sekta ya Nishati. 8. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, naomba sasa kuwasilisha Taarifa ya Mapato, Matumizi na Utekelezaji wa Shughuli za Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2018/19 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2019/20. B. TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA 2018/19 NA MWAKA 2019/20 Bajeti na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2018/19 9. Mheshimiwa Spika, Bajeti iliyopitishwa kwa ajili ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake kwa Mwaka 2018/19 ni jumla ya Shilingi Trilioni 1.692 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Bajeti ya Miradi ya Maendeleo ilikuwa Shilingi Trilioni 1.665 sawa na asilimia 98.4 ya bajeti yote ya Wizara na Bajeti ya Matumizi ya Kawaida ni Shilingi bilioni 27.15 sawa na asilimia 1.6 ya bajeti yote ya Wizara. 5 10. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi Trilioni 1.227. Fedha hizi zinajumuisha Shilingi bilioni 688.65 ambazo ni malipo ya awali (advance payment) kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa Rufiji naShilingi bilioni 169.71 ambazo ni fedha za nje zilizopelekwa moja kwa moja (D-Funds) katika miradi ya REA, TANESCO na Sustainable Energy for All (SE4All). Kiasi hicho kilichopokelewa na Wizara ni sawa na asilimia 87 ya fedha zilizotarajiwa kupokelewa katika kipindi husika ambazo ni Shilingi trilioni 1.410. Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali 11. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati katika mwaka 2018/19 ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni 394.45. Kati ya makusanyo hayo, jumla ya Shilingi bilioni 394.44 zilitarajiwa kukusanywa kupitia shughuli za mafuta na gesi asilia na Shilingi milioni 10.0 kupitia shughuli za utawala. Hadi kufikia tarehe 15 Mei 2019, Wizara kupitia shughuli za TPDC za utafiti wa mafuta na mauzo ya gesi asilia imekusanya Shilingi bilioni 484.33. Makusanyo hayo ni sawa na asilimia 123 ya lengo la makusanyo ya 6 Shilingi bilioni 394.45 kwa mwaka 2018/19. Sababu ya kuvuka lengo ni kuongezeka kwa matumizi ya gesi asilia yanayotokana na kuunganishwa kwa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II na Kiwanda cha Saruji cha Dangote. Matumizi ya gesi asilia yameendelea kuongezeka na kufikia jumla ya futi za ujazo bilioni 59.2 mwaka 2018 kutoka futi za ujazo bilioni 32.2 mwaka 2015, sawa na ongezeko la asilimia 84. 12. Mheshimiwa Spika, makisio ya makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2019/20 ni Shilingi bilioni 602.05, sawa na ongezeko la asilimia 52.6 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 394.45 lililokuwa lengo la mwaka 2018/19. Ongezeko hilo la makisio ya makusanyo limetokana na kuongezeka kwa matumizi ya rasilimali ya gesi asilia. C. UTEKELEZAJI WA BAJETI KWA MWAKA 2018/19 13. Mheshimiwa Spika, Maeneo ya Kipaumbele ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka 2018/19 yalikuwa ni pamoja na: kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo Mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji MW 2,115; miradi 7 ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I - Extension MW 185 na Kinyerezi II MW 240; kuimarisha mifumo ya kusafirisha umeme nchini; kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini (REA III); kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); kuimarisha shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia; na kuendeleza miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo na umeme-jua). 14. Mheshimiwa Spika, Wizara pia ilizingatia maeneo mengine ambayo ni pamoja na: kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake katika kusimamia Sekta ya Nishati; kuboresha mazingira ya ofisi kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kutoa huduma bora zaidi; na kuendelea kuelimisha umma na kuboresha mawasiliano na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya nishati. 15. Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa kutokana na utekelezaji wa maeneo hayo ya kipaumbele, Wizara imepata mafanikio makubwa 22 ikiwa 8 ni pamoja na nchi kutokuwa na mgawo wa umeme katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/19. Aidha, pamoja na kutokuwa na mgawo wa umeme, Taifa letu limeanza kuwa na ziada ya umeme wa wastani wa MW 300 kwa siku kwa mwaka 2018/19 tofauti na hapo awali tulipokuwa na upungufu wa zaidi ya MW 100 kwa mwaka 2015. Mafanikio makubwa 21 ni kama ifuatavyo: (i) Kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji waMW 2,115 utakaokamilika mwaka 2022. Ujenzi wa bwawa hili kutaifanya Tanzania kuwa na umeme wa uhakika, unaotabirika na gharama nafuu. Aidha, Ujenzi wa bwawa la mradi huu utaifanya Tanzania kushika nafasi ya kwanza Afrika Mashariki kwa kuwa na bwawa kubwa, ya nne kwa Afrika na kuwa kati ya nchi 70 Duniani zenye mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme; (ii) Kukamilika kwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Makambako, Madaba hadi 9 Songea, pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Madaba na Songea na upanuzi wa kituo cha Makambako. Kukamilika kwa njia hii ya kusafirisha umeme kumefanya mikoa ya Njombe na Ruvuma kuunganishwa katika Gridi ya Taifa na hivyo kusitishwa kwa matumizi ya mitambo ya mafuta ambayo ilikuwa ikigharimu TANESCO na kuokoa wastani wa Shilingi bilioni 9.8 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununua mafuta katika Vituo vya Madaba, Ludewa, Songea, Mbinga na Namtumbo; (iii) Kuongezeka kwa kasi ya kusambaza umeme vijijini ambapo hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 Serikali imepeleka umeme katika vijiji 7,127 vya Tanzania Bara ikilinganishwa na vijiji 2,018 vilivyokuwa vimeunganishwa umeme Mwaka 2015.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages142 Page
-
File Size-