Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) 13 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Nne – Tarehe 13 Aprili, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na ratiba ya Mkutano wetu wa Saba wa Bunge ambao leo ni kikao cha Nne, Katibu. MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge leo hatuna Hati za Kuwasilishwa Mezani kwa hiyo tunaenda moja kwa moja kwenye maswali yaliyopo kwenye Ratiba ya Shughuli za leo na swali la kwanza linaenda ofisi ya Waziri Mkuu na litaulizwa na Mhehsimiwa Rukia Kassim Ahmed Mbunge wa Viti Maalum. Na. 39 Shule ya Kolo kuwa na Wanafunzi watatu Kidato cha Nne MHE. RUKIA K. AHMED aliuliza:- Kukosekana kwa walimu wa kutosha, vifaa vya maabara na mazingira magumu katika shule ya Sekondari ya Kolo- Wilaya ya Kondoa kumesababisha wanafunzi wengi kuacha 1 13 APRILI, 2012 shule na kubakiwa na wanafunzi watatu (3) tu katika Kidato cha Nne:- (a) Je, Serikali inawasaidiaje wanafunzi hao waliokumbwa na kadhia hiyo? (b) Je, Serikali haioni kwamba wanafunzi hao wana haki ya kupata elimu kama wanafunzi wengine? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a)Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zilizopo kuhusu walimu na wanafunzi katika shule ya Sekondari Kolo kwa kipindi cha miaka minne ni kama ifuatavyo:- Mwaka 2008 shule ilikuwa na walimu 5 na wanafunzi 36, mwaka 2009 shule ilikuwa na walimu 3 na wanafunzi 28, mwaka 2010 shule ilikuwa na walimu 5 na wanafunzi 26, mwaka 2011 shule ilikuwa na walimu 7 na wanafunzi 25. Kwa sasa shule hii ina jumla ya walimu 10 kwa takwimu hizi hakuna mwaka ambao shule hiyo ilikuwa na wanafunzi watatu. (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua haki ya watoto kupata elimu na hivyo imekuwa inahakikisha kuwa wanafunzi wa shule zote nchini ikiwemo Kolo wanapata elimu kwa kuzingatia sheria na miongozo inayotawala utoaji wa elimu nchini. Serikali pia imekuwa ikihakikisha wanafunzi wote nchini wakiwemo wa Kolo wanapata huduma ua elimu ipasavyo kwa kupanga walimu pamoja na uboreshaji miundombinu ya shule. Aidha, Serikali inatambua kuwepo 2 13 APRILI, 2012 shule ya Sekondari ya Changaa iliyokuwa na wanafunzi watatu wa kidato cha nne mwaka 2011. Mheshimiwa Spika, shule ya Changaa iliyoanza mwaka 2006 ilikuwa na wanafunzi 22 waliosajiliwa kidato cha kwanza mwaka 2008, kati ya hao, wanafunzi 3 waliacha shule kwa utoro mwaka 2010 na wanafunzi 16 walihamia katika shule ya sekondari ya Ula mwaka 2009 na mwaka 2010 na hivyo kubakia na wanafunzi 3. Serikali kwa kutambua umuhimu wa wanafunzi hawa watatu kupata elimu ipasavyo iliwasaidia kwa kuwahamishia katika shule ya sekondari ya Ula ambako walifanyia mtihani wa kidato cha Nne mwaka 2011. Mwaka huu shule hii imepangiwa walimu wanne, wawili wamesharipoti na hivi sasa ina jumla ya walimu watano. Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wito kwa Mheshimiwa Mbunge kuendelea kuwahamasisha wananchi wa Halmashauri kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu za kutosha pamoja na majengo mengine ili kuwavutia walimu kwa kuwa na mazingira bora ya kuishi na kufundishia. MHE. RUKIA K. AHMED: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. (a)Je, Serikali haioni kama kukosekana kwa elimu katika baadhi ya Wilaya ni kudumaza Wilaya hiyo kimaendeleo? (b) Je, Serikali haioni kama iko haja ya kuongezewa mishahara walimu pamoja na mafao mengine ili nao waweze kuhamasika na wasomeshe watoto vizuri? NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU-ELIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kukosekana kwa elimu baadhi ya Wilaya hili kwa sasa limeshafanyiwa kazi kwa sababu kila Wilaya ina shule za Msingi zilizo katika kila Kijiji na hata kitongoji kilicho kikubwa katika Wilaya zetu. 3 13 APRILI, 2012 Lakini pia tuna shule za Sekondari sasa katika kila Kata na sasa tuna jumla ya sekondari 3242 kwa Kata zote nchini ambazo zina uwezo wa kupokea vijana kutoka shule za msingi zilizopo ndani ya Kata yenyewe. Hii ina maana kwamba Serikali imepania kutoa elimu katika kila Wilaya katika shule zake za msingi na Sekondari. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili la uongezaji wa mishahara ni kweli kwamba hata mimi nilipokuwa nafanya ziara kwenye Wilaya mbalimbali nchini na kukutana na Walimu, nilipokuwa natoa nafasi ya wao kuchangia katika uboreshaji wa elimu hiyo ilikuwa ni moja ya hoja zao ambazo wanazieleza na Serikali tumelichukua, na kwa bahati nzuri sana Walimu wameshafikisha ombi hili kwa Rais kupitia Chama cha Walimu Tanzania na Rais aliwaahidi kwamba analichukua analifanyia kazi na anaweza kufanyia kazi hilo kadri fedha za Serikali zinavyoweza kupatikana ili pia kuboresha sekta hii na kuwafanya walimu waweze kufanya kazi yao vizuri. Ahsante sana MHE. AMOS G. MAKALA: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante kwa kuniona. Naomba kumwuliza Waziri kwamba matatizo yaliyopo katika Sekondari ya Kolo yapo katika sehemu kubwa sana ya Tanzania na hasa Jimbo la Mvomero ukizingatia kwamba hatuna walimu wa kutosha kuna walimu watatu tu katika sekondari moja hasa Unguru Mascat walimu wanne na maeneo mengi katika Tarafa ya Mgeta; Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu kuongeza walimu wa kutosha kupitia Bunge hili? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) : Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya jitihada za kutosha za kuongeza idadi ya walimu nchini ili kusaidia kupunguza ugumu wa kazi ya 4 13 APRILI, 2012 walimu waliopo sasa kwa kuwaongezea idadi ya walimu ili wafundishe kwa urahisi na kufanyakazi zao kwa urahisi zaidi. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2011 Serikali iliajiri walimu 9226 wakiwepo wa Shule za Msingi na Sekondari na wote tuliwasambaza nchi nzima, mwaka huu tumeongeza idadi hiyo mara tatu zaidi kwamba tumeajiri walimu 24,621 walimu wa shule za msingi kati ya hao ni 11,379 na pia walimu 13242 ni wa sekondari. Na walimu wote wameshasambazwa nchi nzima na kufikia mwezi Machi tarehe 30 mwaka huu, walimu 21,681 wamesharipoti kwenye vituo mbalimbali. Walimu wa shule za msingi kati ya hao 10,491 wamesharipoti na walimu 11,190 wamesharipoti kwenye shule mbalimbali za sekondari nchini. Mpango huu wa ajira utaendelea kuongezeka kadiri ambavyo wamedahiliwa kupata mafunzo ya ualimu kwenye Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ualimu nchini ili kuongeza idadi ya Walimu na kuweza kupunguza mzingo kama nilivyosema wa Walimu waliopo sasa. Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi ni jitihada ya Serikali ya kuweza kuboresha sekta ya elimu na walimu hawa ni pamoja na wale ambao tumewapeleka Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. MWENYEKITI: Itakuwa ni vizuri kama orodha hiyo Naibu Waziri ikasambazwa kwa Wabunge wote ili waweze kuona mgawanyo wao na kwa kila Wilaya na namna matatizo yalivyobaki katika Wilaya angalau kila Mbuneg aweze kujua mwenendo wa tatizo hilo kwenye Wilaya yake. (Makofi) NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU-ELIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, orodha hiyo itapatikana kufikia saa saba mchana. MWENYEKITI: Nakushukuru sana tunaendelea na swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa Said Mohammed Mtanda, Mbunge wa Mchinga. 5 13 APRILI, 2012 Na. 40 Ahadi ya Ujenzi wa Daraja Kati ya Mchinga I na Mchinga II MHE. SAID M. MTANDA aliuliza:- Mheshimiwa Rais wa nchi aliahidi ujenzi wa daraja la kuunganisha Mchinga I na Mchinga II:- (a) Je, ujenzi huo utaanza lini? (b) Je, ni fedha kiasi gani zitatumika kwa kazi yote hadi kukamilika kwa daraja? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda, Mbunge wa Mchinga, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mhehsimiwa Rais aliahidi kujenga daraja kuunganisha Mchinga I na Mchinga II kutokana na adha wanayoipata wananchi wa maeneo hayo. Eneo hilo ni Mkondo wa bahari ambao hujaa maji katika miezi ya Agosti hadi Novemba kuanzia saa 10 jioni hadi saa 2 usiku ( highest tide mark ) ambazo kule wanaziita Bamvua. Kwa kuzingatia ahadi hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi imekamilisha usanifu wa daraja hilo ili kazi ya ujenzi iweze kuanza. Kazi ya ujenzi imepangwa kuanza katika mwaka wa fedha 2012/2013. 6 13 APRILI, 2012 (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, usanifu uliofanyika umebainisha kwamba zinahitaji shilingi 380,294,000/- ili kukamilisha ujenzi wa daraja hilo hadi kutumika. Fedha hizi zimeombwa na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi katika bajeti ya 2012/2013 kupitia maombi maalum. MHE. SAID M. MTANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza niishukuru Serikali kwa kuanza kutekeleza baadhi ya ahadi ambazo zilitolewa katika kipindi cha uchaguzi uliopita katika Jimbo langu. Lakini nina swali dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa tayari Serikali imepokea maombi lakini Serikali haijasema wazi kwamba maombi hayo yamekubaliwa ili kuwaondoa hofu wananchi wa Jimbo la Mchinga hususani watumiaji wa barabara ile inayotoka Mchinga I, II hadi kule Kijiweni kwamba maombi haya yamekubaliwa na sasa wananchi wakae tayari kusubiri utekelezaji wake katika kipindi hiki cha mwaka 2012/2013. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa niaba ya Serikali mimi naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Mtanda kwa kutoa shukrani kwa sababu ameonesha na neno la Mungu linasema shukuruni kwa kila jambo. Amekuwa mkweli hapa maana yake nilifikiri kwamba hatasema ukweli, Rais alipokwenda pale katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi alitoa ahadi mbili, ahadi ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kituo cha afya cha Kitomanga, zimejengwa wodi mbili pale na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, amekwenda pale akaenda kuzindua na kufungua kituo kile kwa maana ya hizo wodi mbili. Kwa hiyo, anavyoshukuru hapa namwelewa. 7 13 APRILI, 2012 Pia nimshukuru pia Mheshimiwa Mtanda kwamba ni Mbuneg makini ambaye anafuatilia sana masuala haya yanayohusu Jimbo lake la Uchaguzi, kila siku asubuhi ukiamka unamkuta pale kwangu mpaka inafika mahali namwambia Mtanda sasa inatosha.
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages342 Page
-
File Size-