Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA THELATHINI NA SITA 29 MEI, 2017 MKUTANO WA SABA KIKAO CHA THELATHINI NA SITA TAREHE 29 MEI, 2017 I. DUA: Dua ilisomwa Saa 3.00 Asubuhi na Mhe. Spika, Job Ndugai alikiongoza Kikao hadi saa 4.20 asubuhi ambapo alimpisha Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Zungu ambae aliendelea kukiongoza Kikao. Makatibu mezani: 1. Ndugu Laurence Makigi 2. Ndugu Zainab Issa II. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI (i) Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kwa niaba ya Waziri aliwasilisha Mezani Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. (ii) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba aliwasilisha Mezani Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. (iii) Mhe. Juliana Shonza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama aliwasilisha Mezani Taarifa ya Kamati kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. 1 (iv) Mhe. Riziki Mngwali kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani aliwasilisha Mezani Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. III. MASWALI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA Swali Na. 288: Mhe. Ritta Enespher Kabati Nyongeza: Mhe. Ritta Enespher Kabati Mhe. Nape M. Nauye WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI Swali Na. 289: Mhe. Desderius John Mipata Nyongeza: Mhe. Desderius John Mipata WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO Swali Na. 290: Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia Nyongeza: Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI Swali Na. 291: Mhe. Mbarouk Salum Ali (Kny: Mhe. Yusufu Salum) Nyongeza: Mhe. Yusuf Salum Mhe. Goodluck A. Mlinga 2 Swali Na. 292: Mhe. Abdallah Dadi Chikota Nyongeza: Mhe. Abdallah Dadi Chikota Mhe. Omar T. Mgumba WIZARA YA NISHATI NA MADINI Swali Na. 293: Mhe. Constantine John Kanyasu Nyongeza: Mhe. Constantine John Kanyasu Swali Na. 294: Mhe. Josephat Sinkamba Kandege Nyongeza: Mhe. Josephat Sinkamba Kandege Swali Na. 295: Mhe. Augustino Manyanda Masele Nyongeza: Mhe. Augustino Manyanda Masele WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI Swali Na. 296: Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda Nyongeza: Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO Swali Na. 297: Mhe. Mwita M. Waitara (Kny: Mhe. Anatropia Lwehikila Theonest) Nyongeza: Mhe. Mwita M. Waitara 3 IV. MATANGAZO Wageni mbalimbali walioko kwenye gallaries za Ukumbi wa Bunge walitambulishwa ikiwemo na Wachezaji wa Simba Sports Club. V. HOJA ZA SERIKALI Hoja ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwamba, Bunge sasa likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. Waziri aliwasilisha Hotuba yake. Taarifa na maoni ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliwasilishwa na Mhe. Kanal (Mst), Masoud Ali Khamis Makamu Mwenyekiti kuhusu Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa 2017/2018. Hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani iliwasilishwa na Mhe. Mchungaji Peter Msigwa kuhusu Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. Wabunge wafuatao nao walichangia Hoja ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki:- (1) Mhe. Prof. Anna Tibaijuka - CCM (2) Mhe. Haji Khatibu Kai - CUF (3) Mhe. Godbless J. Lema - CHADEMA (4) Mhe. Mary M. Mwanjelwa - CCM (5) Mhe. Kanali (Mst) Masoud Ali Khamis - CCM (6) Mhe. Rose C. Tweve - CCM (7) Mhe. Esther A. Mahawe - CCM (8) Mhe. Sophia H. Mwakagenda - CHADEMA (9) Mhe. Cosato D. Chumi - CCM (10) Mhe. Tundu A. Lissu - CHADEMA (11) Mhe. Juliana D. Shonza - CCM 4 (12) Mhe. Daniel N. Nsanzugwanko - CCM (13) Mhe. Peter J. Serukamba - CCM VI. KUSITISHA BUNGE Shughuli za Bunge zilisitishwa Saa 7.00 mchana hadi saa 10.00 Alasiri. VII. BUNGE KURUDIA Saa 10.00 jioni Bunge lilirudia Mjadala wa Hoja ya Waziri wa Mambo ya Nje uliendelea kama ifuatavyo:- (14) Mhe. George Mcheche Masaju - AG (15) Mhe. Susan Alphonce Kolimba - Naibu Waziri VIII. KUHITIMISHA HOJA Mtoa Hoja Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alipewa fursa ya kujibu Hoja mbalimbali zilizotolewa na Wabunge na kutoa Hoja ambayo iliungwa mkono kisha Bunge likaingia kwenye Hatua ya Kamati ya Matumizi. IX. KAMATI YA MATUMIZI Fungu 34: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Waheshimiwa wafuatao walisimama kuomba ufafanuzi na kutoa shilingi kama ifuatavyo (Mshahara ya Waziri). (i) Mhe. Mch. Peter S. Msigwa na alitoa shilingi na kuungwa mkono na Waheshimiwa Wabunge wafutao:- (1) Mhe. Ali Saleh (Mb) (2) Mhe. Balozi Mohamed Adad Rajab (Mb) (3) Mhe. Cosato J. Chumi (Mb) (4) Mhe. Ali S. Khamis (Mb) (5) Mhe. William Ole Nasha (Mb) (6) Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala (Mb) 5 (7) Mhe. Masoud A. Salim (Mb) (8) Mhe. Sued A. Kubenea (Mb) (9) Mhe. Riziki Shahali Ngwali (Mb) (10) Mhe. Charles J. Mwijage (Mb) (11) Mhe. George B. Simbachawene (Mb) (12) Mhe. Godbless J. Lema (Mb) Walioomba ufafanuzi wengine ni kama ifuatavyo:- (ii) Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) (iii) Mhe. Cosato J. Chumi (Mb) alitoa shilingi na kuungwa mkono na Wabunge wafuatao:- (1) Mhe. Tundu A. Lissu (Mb) (2) Mhe. Faustine E. Ndugulile (Mb) (3) Mhe. Balozi Adadi Rajab (Mb) (4) Mhe. Charles J. Mwijage (Mb) (5) Mhe. Juliana Daniel Shonza (Mb) (iv) Mhe. Martha Mlata (Mb) Shughuli za Kamati ya Matumizi ziliingia kwenye Guillotine kwa kusoma fungu kwa fungu. KAMATI YA MATUMIZI Shughuli za Kamati ya Matumizi zilimalizika na mtoa Hoja kutoa Taarifa. X. KUAHIRISHA SHUGHULI ZA BUNGE Shughuli za Bunge ziliahirishwa Saa 12.00 jioni hadi kesho tarehe 30/5/2017 saa 3.00 asubuhi. 6 .