Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

BUNGE LA ______

MAJADILIANO YA BUNGE ______

MKUTANO WA TATU

Kikao cha Tisa – Tarehe 16 Aprili, 2011

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI

Muswada wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama wa Mwaka 2011 (The Judiciary Administration Bill, 2011)

(Majadiliano Yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, jana tulianza na Muswada huu na hivi leo tutaendelea na majadiliano hadi saa 4.30 asubuhi, halafu tutawaita wanaotoa ufafanuzi waweze kufanya kazi, baada ya hapo tutaingia kwenye Kamati ya Bunge Zima mpaka saa 6.00 mchana halafu itafuata hoja ya kuahirisha kikao. Kwa hiyo, leo ninaanza kumwita Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa , atakayefuata nitaangalia baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani; huwezi kuleta wadogowadogo tena watakuwa wanamsema sivyo. Mheshimiwa Freeman Mbowe. (Kicheko)

MHE. FREEMAN A. MBOWE (KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kwanza kabisa ya mimi binafsi kutoa mchango katika Muswada huu wa Dispensation of Justice, ambao ni muhimu sana katika nchi yetu. Kwanza, ninaomba niweke bayana kabisa kwamba, sisi kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kimsingi, tunaunga mkono hoja hii bila tatizo lolote. Yapo mambo kadhaa ya msingi ambayo tutajielekeza kwayo, kwa lengo zuri tu la kuboresha. Ninaomba Waheshimiwa Wabunge wote waelewe kwamba, wajibu wa Mahakama, unakamilisha mtiririko wote wa utoaji haki katika Taifa letu na investiment kama Taifa kwenye mfumo mzima wa utoaji haki ni priority ya Taifa.

Mheshimiwa Spika, lakini leo nitajielekeza zaidi kwenye takwimu ili pengine kuweza kulipa Bunge na kulipa Taifa uelewa wa hali halisi ilivyo ndani ya Mahakama zetu. Wenzangu watajikita kwenye masuala ya kisheria, mimi nitakwenda kwenye dhana yenyewe ya uendeshaji wa Mahakama zetu.

1 Mheshimiwa Spika, sidhani kama Watanzania wengi au pengine Serikali na hususan Waheshimiwa Wabunge, wangekuwa wanaelewa kabisa extent ya matatizo yaliyopo katika Idara ya Mahakama, kama wangeendelea na utamaduni huu wa business as usual. Hali ya Mahakama zetu ni mbaya na hali ikiwa mbaya ni kwamba, hali au utaratibu wa utoaji haki katika Taifa letu ni mbaya, una upungufu mwingi wa msingi. Matatizo yaliyopo yanaweza kabisa kutatulika pale ambapo patakuwepo na nia nzuri na thabiti kutoka kwa wenzetu wa upande wa Serikali. Nimesema nitajielekeza upande wa takwimu, kwa sababu sisi Wapinzani tunafanya utafiti sana na tunazungumza with confidence kwa sababu tunafanya research.

Mheshimiwa Spika, jana zimetolewa hoja kadhaa zikionesha kuna upungufu mkubwa wa watumishi katika Idara za Mahakama; hii ni sahihi kabisa. Kuna jambo moja linatisha zaidi kwamba, hata hao wachache walioko ndani ya ajira ya Mahakama wako under utilised by 71%; ni takwimu ambazo ukiambiwa katika utaratibu wa kawaida unaweza usiamini. Kwamba, Idara ya Mahakama ina upungufu mkubwa wa watumishi wa kitaalamu na watumishi wengine, lakini hata hao wachache waliopo wako under utilised.

Mheshimiwa Spika, siku za miaka ya karibuni, Mheshimiwa Rais, amefanya kazi nzuri ya kuteua Majaji wa Mahakama Kuu; ni uamuzi mzuri. Unapoteua Majaji halafu Serikali yako haiweki mikakati ya kuwatumia Majaji wale wakafanya kazi zao effectivel,y inakuwa umepoteza fedha za Serikali kwa sababu unawalipa Majaji na haki haitendeki kwa macho yako, tunajaza magereza kwenye kesi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa muda mfupi.

Mheshimiwa Spika, nimesema leo nitajielekeza kwenye masuala ya takwimu, kwa hiyo, sitakwenda kwenye vifungu vya kisheria; hilo tunawaachia wanasheria wetu watafanya kazi hiyo. Ninapozungumza hapa, ninaomba uniruhusu nisome kuhusu under utilisation ya capacity ya Mahakama yetu pamoja na upungufu wa staff ambao upo.

Mheshimiwa Spika, kwenye Mahakama ya Rufani, Mwaka huu wa Fedha, wakati wa kusikiliza mashauri, yaani vile vikao vyao au sessions za kusikiliza mashauri, walikuwa na uwezo wa kusikiliza mashauri katika sessions 30. Katika sessions hizi 30, wameweza kusikiliza 18 tu. Maana yake ni kwamba, wameweza kufanya kwa 60% ya capacity iliyopo sasa hivi na matokeo yake ni kwamba, kuna sessions 12 hazitasikilizwa pamoja na kwamba, Majaji wa Mahakama ya Rufaa wapo na muda upo; ina maana zitasikilizwa by less than 40%; kwa hiyo, kuna under utilisation ya capacity iliyopo sasa hivi by 40%, hii ni Mahakama ya Rufaa.

Mheshimiwa Spika, kwenye Mahakama Kuu, uwezo wa Majaji wetu waliopo siku ya leo ungeweza kusikiliza au kufanya vikao 432 katika Taifa zima, lakini vikao vilivyofanyika ni 214 tu, ambavyo ni sawasawa na 49.6%. Maana yake ni kwamba, kuna vikao 188 vya Mahakama Kuu ambavyo havitasikilizwa ambavyo ni sawasawa na 50.4% ya capacity imekuwa under utilised katika Mahakama Kuu.

2 Mheshimiwa Spika, ukija katika Mahakama za Mikoa, RMs Courts na za Wilaya, zilikuwa na uwezo wa kusikiliza mashauri 110,000 kwa capacity iliyopo leo lakini mpaka sasa hivi katika mwaka huu, kwa ceiling ya bajeti ambayo imewekwa, zitaweza kusikiliza mashauri 27,000 tu; maana yake ni nini? Hii ni 24.6% na matokeo yake ni kwamba, vikao ama sessions 83,000 hazitaweza kufanyika, ambayo ni sawasawa na 75.4% ya capacity imekuwa under utilised.

Mheshimiwa Spika, hili ni tatizo kubwa kweli. Sasa ukija katika Mahakama za Mwanzo, mashauri 132,000 yangeweza kusikilizwa kwa capacity ambayo ipo leo, lakini kwa sababu ya ukomo wa fedha, yataweza kusikilizwa mashauri 69,232, ambayo ni 28.5% ya capacity, 173,680 hayatasikilizwa. Kwa hiyo, in general ni kwamba, utakuta 68.3% ya Mahakama za Mwanzo, pamoja na upungufu mkubwa wa Mahakimu, masuala hayatasikilizwa kwa sababu hakuna fedha.

Mheshimiwa Spika, ukianza Mahakama ya Rufaa, ukashuka chini mpaka Mahakama ya Mwanzo, kuna under utilisation ya watu wetu katika Idara ya Mahakama by 71%. Sasa hizi ni takwimu ambazo tunategemea wenzetu wa Wizara hii watusaidie Wabunge ili tuweze kuelewa depth ya crisis iliyopo. Wabunge tukiweza kuelewa depth ya crisis iliyopo, nina hakika Wabunge wote bila kujali Chama cha Siasa, tutajua kwamba, tunawanyima Wananchi wetu haki. Tunapowanyima Wananchi wetu haki halafu sisi tunasema ni nchi ambayo inafuata Utawala wa Sheria na Utawala wa Haki, kwa vyovyote ni mambo ambayo yanatia mashaka sana.

Mheshimiwa Spika, infrastructure ya Mahakama na pengine kutokana na ukubwa wa Bajeti ya Serikali, watu wanaweza kufikiria Idara ya Mahakama inahitaji pesa nyingi sana. Component ya utoaji wa haki ina gharama, lakini tunapozungumzia Bajeti ya Idara ya Mahakama wala siyo bajeti kubwa.

Katika Mwaka huu wa Fedha, hii ambayo ndiyo inaitwa ceiling, inazungumza habari ya bilioni 29 tu ndiyo zimekuwa allocated kwa Mahakama. Katika nchi ambayo Mamlaka zake za Mapato zinakusanya zaidi ya bilioni 400 kwa mwezi mmoja; kweli kama Taifa tunatenga bilioni 29 kwa ajili ya utoaji haki katika Taifa? Kesi zinalala. Waheshimiwa Wabunge ni lazima tuelewe athari za maamuzi kama haya kwamba, hatuweki priority katika kutoa fedha kwa ajili ya Mahakama.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana tumekwenda kwenye uchaguzi, kuna watu kadhaa wanaona hawakutendewa haki. Kuna kesi kadhaa za uchaguzi karibu 50 ziko Mahakamani. Mahitaji ya kisheria ni kwamba, kesi hizi ni lazima ziwe zimesikilizwa kwenye Mahakama Kuu katika kipindi cha mwaka mmoja. Leo ni miezi sita kesi hizi bado zinasuasua sana. Mahakama ilipoleta maombi ya fedha Serikalini, ambayo ni kama bilioni mbili na kitu, wamepewa milioni 500; sasa milioni 500 halafu una deadline ya kumaliza kesi katika mwaka mmoja, hizi kesi haziwezi kwisha na matokeo yake ni kwamba, watu watanyimwa haki zao.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, sisi kama Upinzani, tumesema tunaunga mkono hoja hii na tunaona ni priority. Nimesema hatuja-invest hata katika

3 kujenga infrastructure za Mahakama. Tangu baada ya Uhuru, kwa miaka 50 iliyopita, kama tumejenga majengo ya Mahakama Kuu ni vituo ambavyo havizidi vinne. Ukienda kwenye Ofisi za Mahakama, unaona aibu Mahakimu wetu na Majaji wetu, wanafanya kazi katika mazingira gani.

Huko Mahakama za chini ndiyo kabisa usizungumze, watu wanaoza Magerezani kwa sababu kesi zao hazitajwi kwa ukosefu aidha wa Mahakimu ama wa Mahakimu na Majaji kutokuwa na Fungu la kuweza ku-conduct zile sessions za kawaida za utoaji haki. Tunaendelea kulisha mahabusu ambao pengine wangestahili kuwa acquited. Nina hakika wote mnajua uchungu wa kukaa katika mahabusu za tanzania.

Mheshimiwa Spika, pale ambapo nchi hii imeshuhudia kesi za vigogo, wenyewe mnaona mnavyozipeleka kasi kesi zetu. Kesi za vigogo nchi hii zinasikilizwa mpaka week-end, Mahakimu wanaitwa Mahakamani sijui ni vyeti vya dharura vinatoka, kesi zinasikilizwa usiku na mchana, wiki mbili maamuzi yamefanyika; nchi gani? Halafu watu ambao hawana utetezi tunawaacha kule wanaoza Magerezani.

Watu wakiandamana mnasema wanafanya makosa, lakini pressure inasaidia. Siku moja Majaji wakiandamana, watapewa Fungu la kufanyia kazi; maana nchi hii bila msukumo wa maandamano, watu hawasikii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ifike mahali tuone aibu. Tunapoweka shilingi bilioni 29 kwa Mahakama yote kuanzia Mahakama ya Mwanzo mpaka Mahakama Kuu; wenzetu hawa wameomba bilioni 152 tu, ukilinganisha na matumizi ya jumla ya Serikali katika Bajeti za Maendeleo ya Mikoa, yaani Mwaka huu wa Fedha tumeipa Idara ya Mahakama shilingi bilioni 500 tu za maendeleo; watajenga vipi infrastructure yao?

Ninatamani siku moja ingekuwa kwamba, labda Wabunge wote tuwe na mashtaka, tungejua maana ya kuwapa watu pesa. Tukakaa kule mahabusu, tukaishi kule, Mawaziri mkaishi kule mahabusu, Wabunge wa Chama kinachoongoza Serikali wakaishi mahabusu, halafu katika mazingira hayo pengine tungerudi Bungeni tungekuwa na mawazo mapya ya namna ya kuisadia Idara ya Mahakama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimesema hali halisi tunaiona, kesi za ndugu zetu, kesi za watoto wetu, tunazipeleka kwa kasi ya umeme, lakini wale wanaooza kule Magerezani watu wanaona ni jambo la kawaida! Mimi niliwekwa ndani huko Arusha baada ya maandamano ya kudai haki; tukalala mahabusu na nikaendelea kueleza Sera za Ukombozi wa Taifa kule mahabusu. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa, hiyo kesi iko Mahakamani, naomba usiizungumze. Mnayo kesi Mahakamani siyo?

MHE. FREEMAN A. MBOWE (KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): Mheshimiwa Spika, ninashukuru nilikuwa ninaeleza experience ya kule ndani.

4 SPIKA: Ahaa, basi endelea na hoja.

MHE. FREEMAN A. MBOWE (KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): Mheshimiwa Spika, kwa sababu labda wenzangu hawajapita huko ni vema wakajua; watu wanakaa mahabusu miezi mitatu, kesi haijasikilizwa.

SPIKA: Mwacheni achangie, mbona ninyi …

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Hai, mahabusu wa Wilaya yangu wanawekwa katika Gereza la Karanga. Kwa wiki wanaweza wakachukuliwa mara moja kupelekwa Mahakamani, kwa sababu hakuna usafiri wa kuwapeleka Hai Mjini kusikiliza kesi zao. Matokeo yake ni kwamba, akikosa karandinga la kumpeleka Mahakamani, atakaa mahabusu wiki nzima; halafu unasema tunatenda haki!

Mheshimiwa Spika, lazima tujue jamani hawa watu wengi ambao wako kule chini hata uwezo wa kuweka Mawakili hawana, kwa sababu Mahakama zetu za chini hazina uwezo wa kutumika kwa ajili ya Mawakili, kwa sababu zinaendeshwa na Mahakimu ambao hawana qualification, siyo graduate wa leo, hawawezi kuendesha kesi kwa Mawakili; kwa hiyo, wale watu hawana utetezi halafu tunawasweka ndani, hatuwawekei uwezo wa kusikiliza kesi zao. Tunakuomba Mheshimiwa Waziri, kwenye kikao kijacho cha bajeti, walete Majaji wetu waendeshe semina kwa Wabunge, tuweze kuelewa backup ya hii session. Hii ni crisis na kwa kweli tukiendelea kutoa fedha kidogo kidogo, nina hakika kabisa Serikali haishindwi kutoa shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kutenda haki katika nchi hii, kwa sababu kununua haki kuna gharama kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niunge mkono hoja huku nikiendelea kusisitiza kwamba, Idara ya Mahakama isaidiwe. Wenzetu katika mapendekezo yao waliomba wapewe 2% ya GDP, sina hakika ni kiasi gani exactly cha fungu la fedha katika hatua hii, lakini ukweli ni kwamba, tuna uwezo wa kutosha kabisa wa kuhudumia Bajeti ya Mahakama hii kama tutakubaliana.

Mheshimiwa Spika, tunaongeza Wilaya kila siku, kuongeza Wilaya tunatumia mabilioni na mabilioni kujenga majengo ya utawala wa kawaida wa sisi kukaa ofisini na viyoyozi wakati watu wanaoza Magerezani na Mahakamani. Priority zetu kama Taifa ziko wapi? Priority zetu ni nini? Kama katika Ilani ya Chama fulani hazionekani; priority ni kuboresha Mahakama na hata katika Hotuba za Viongozi hawaoni kwamba, priority ni kutenda haki katika Taifa; ni tatizo kubwa. Mimi ninaomba ndugu zangu, kama Serikali Kuu, haijaona ufinyu wa bajeti… (Makofi)

(Hapa Kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kwisha)

SPIKA: Ahsante.

MHE. FREEMAN A. MBOWE (KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): Mheshimiwa Spika, ya kwanza.

5

SPIKA: Kengele ya pili.

MHE. FREEMAN A. MBOWE (KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): Mheshimiwa Spika, ninakushukuru.

MHE. SYLVESTER M. MABUMBA: Mheshimiwa Spika, kwanza, ninaanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunipa nafasi hii, kusimama katika Bunge lako Tukufu, kuchangia hoja ambayo iko mbele yetu.

Pili, ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri, kwa kuleta Muswada huu katika Bunge hili Tukufu. Ninawapongeza pia Wajumbe wa Kamati, ambao walipitia wakati wa kukusanya maoni ya wadau na hata leo hii tunaweza kuzungumzia Muswada huu. Niipongeze Serikali kwa kuona umuhimu wa jambo hili kwa ajili ya ustawi na kuboresha uendeshaji wa Mahakama zetu hapa nchini. Tunafahamu mahakama ni mhimili muhimu sana katika utoaji wa haki.

Mheshimiwa Spika, ninapenda kuzingatia maeneo yafuatayo; kwanza, eneo hili ambalo Muswada unapendekeza kuwepo kwa Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Uendeshaji Utumishi wa Mahakama. Mtendaji Mkuu kama ilivyoelezwa katika Muswada, hasa ibara ya (7) ni kwamba, huyu ndiye atakuwa Mtendaji Mkuu atakayezingatia uendeshaji wa shughuli za Mahakama siku hadi siku chini ya ushirikiano wa maelekezo ya Jaji Mkuu wa Tanzania. Ninapenda kuwatoa wasiwasi Waheshimiwa Wabunge ambao walikuwa na hofu kwamba, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ni mtu ambaye hana taaluma ya kisheria, lakini ukiangalia sifa zake ambazo zimewekwa katika Muswada huu kwenye ibara ile (7) ni kwamba; ni mtu ambaye atakuwa ameshika nafasi ya juu katika Utumishi wa Umma, ambaye atakuwa na uzoefu katika masuala ya utawala na masuala ya fedha, pia atakuwa ni mtu mwenye haiba na uadilifu mkubwa. Kuwepo kwa Mtendaji Mkuu kutasaidia sana ule upungufu ambao ulikuwepo, kupunguzwa ama kuondolewa kabisa. Ninaipongeza pia Serikali kwa Muswada huu kuwepo na Tume ya Maadili ya Uongozi wa Mahakimu, yaani Judicial Officers Ethics Commission, hii itazingatia sana haki za Wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kama ilivypendekezwa, tunaamini ni wazi kwamba, kuna wakati watu wanakuwa wana hofu nyingi kwa sababu ya taratibu zilizoko kuingia Mahakamani, lakini kwa mapendekezo haya ukiangalia composition ya wale watu ambao watakuwepo pale; mfano, katika mkoa, kwenye mkoa imependekezwa Wajumbe wa Kamati hii ya Maadili atakuwepo Mkuu wa Mkoa, kwenye Wilaya atakuwepo Mkuu wa Wilaya na wengine. Sasa hawa ni watu ambao watasaidia kushughulikia hizi haki ambazo Wananchi watakuwa wanazihitaji. Pia wakati wa kukusanya maoni ya wadau, suala hili la kusema kwamba, kwenye eneo hili la pili la Mfuko ambao umependekezwa kuwepo ku-decide pawepo na percentage gani; hili huwezi kulifanya kwa sasa hivi kwa sababu kwanza, hatuna uhakika na mahitaji halisi ya mahakama zetu, lakini pia hatuna uhakika na GDP tunayokusanya, ukiangalia baada ya uchumi kuporomoka kutokana na mabadiliko ya hali ya uchumi duniani.

6 Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutakapokuwa na uhakika wa mahitaji halisi ya mahakama zetu na tutakapokuwa na uhakika wa makusanyo yetu kama nchi, suala la kiasi gani kitengwe kwa ajili ya shughuli hizi za Mahakama kwenye Mfuko huu ambao umependekezwa, itakuwa ni rahisi. Tunaamini kwamba, kama huna utafiti huwezi kuzungumza. Sasa tutakapokuwa na uhakika baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu uwezo wa nchi yetu na hali halisi za mahitaji ya Mahakama zetu, itakuwa ni rahisi sana kuamua sasa ni kiwango gani.

Kwa hiyo, ninawaomba Waheshimiwa Wabunge Bunge wote wa Bunge hili Tukufu, wauridhie Muswada huu kwa vile umekuja kwa lengo la kuboresha utendaji wa Mahakama zetu. Kuwepo kwa hawa watu ambao wamependekezwa, Mtendaji Mkuu, Mfuko wenyewe lengo lake ni kuhakikisha kwamba, Mahakama zetu zinafanya kazi za utoaji wa haki kama Wananchi wanavyotarajia na kama Katiba inavyoelezea kwamba, haki zetu zote zitatolewa kupitia mhimili mwingine katika Uongozi wa Nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ninapenda pia kuzungumzia kuwepo kwa Tume ya Utumishi, ambayo imependekezwa ndani ya Muswada huu. Tume ambayo itakuwa inafanya kazi kuangalia utendaji wote wa Mahakama zetu. Ninaomba Wajumbe wairidhie Tume hii, ambayo kazi yake itakuwa ni kuratibu kazi zote za Watumishi wa Mahakama. Kwa kuwa tunaelewa ndani ya Mahakama kuna Watendaji wa aina mbili; kuna wale wanaoshughulika moja kwa moja na masuala ya kisheria; na wale ambao hawashughuliki moja kwa moja na masuala ya kisheria kwa vile ili wote waone wanatendewa haki, Tume hii itazingatia mahitaji ya kila upande; upande wa Wanasheria, Majaji na Waheshimiwa Mahakimu, lakini pia upande wa Watumishi ambao siyo direct, wame-involve na mambo ya kisheria (Non Judicial Officers); hawa wanahitaji kuzingatia mambo yao, kuna masuala ya promotion, kuna masuala ya mafunzo ya kuwajengea uwezo kusimamia kazi hizi.

Kwa vile Tume hii kama ilivyoelezewa ndani ya Muswada huu, itakapokuwa imepewa ridhaa kupitia Bunge lako Tukufu, itakuwa na nguvu ya kuweza kuhakikisha kwamba, kazi ambazo imepangiwa itazifanya; Tume hii itakuwa na nguvu kwa sababu itakuwa imepewa meno Kikatiba. Watumishi ambao tunawazungumzia hapa, wanahitaji sana kuwepo kwa Tume hii. Tume hii itazingatia mahitaji yao bila ya upendeleo kwa Wanasheria na wasiokuwa Wanasheria. Kwa hiyo, ninaomba Bunge lako Tukufu, liweze kuridhia uwepo wa Tume hii.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyozungumzia Tume ya Maadili ya Watumishi, pale ambapo haki itakapoonekana haikutendeka; ni kazi ya Tume ya Utumishi kukaa na kufanya uchunguzi kwa nini suala lile limetokezea na hivyo kutoa maamuzi ya haki kwa pande zote mbili. Kwa yule ambaye atahisi hakutendekewa haki, basi Tume itaweza kuzingatia na kumsaidia. Pia kwa yule ambaye atakuwa amepindisha haki, Tume itakuwa na nguvu ya kumwita, kumwonya, kumchukulia hatua kali ya onyo, kumsimamisha au adhabu nyingine. Kuwepo kwa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Mahakama, kutasaidia sana kujenga imani ya Wananchi wetu kwa mhimili huu muhimu. Wananchi kama watakuwa na imani finyu kwenye mhimili huu muhimu, nchi yetu itayumba, lakini kwa

7 Muswada huu nina imani tutaboresha sana uaminifu wa Wananchi wetu na kuleta matumaini makubwa kwa Wananchi wetu katika mhimili huu muhimu.

Ninawaomba sana Waheshimiwa Wabunge wasiwe na wasiwasi na suala hili, Serikali ina mapenzi mema kuhakikisha kwamba, Wananchi wanatendewa haki kadiri Katiba inavyoelekeza.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Waheshimiwa Wabunge wenzangu, hasa ambao wameonesha wasiwasi kwamba, Muswada huu haukuzingatia mahitaji halisi ya Mahakama zetu; siyo kweli kwa sababu mpaka tumeweza kuleta Muswada huu hapa ni kwamba, watu wengi walihusishwa kuweka maoni yao ili kuweza kupata picha halisi ya Mahakama zilivyo.

Pia wakati wa kukusanya Maoni ya Wadau, Wadau wenyewe waliridhika sana na kuwepo kwa Muswada huu na wakati wa majadiliano nao, waliunga mkono na kupongeza Serikali. Wadau walisisitiza kwamba, yafaa Bunge liridhie ili kuhakikisha kwamba, haki ya kutoa haki katika nchi yetu kupitia Mhimili wa Mahakama inatolewa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ninaomba kuunga mkono hoja na ninawaomba pia Wajumbe wenzangu wauridhie kwa asilimia zote. Ahsante sana. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Ndiyo.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, toka jana kumekuwa na mjadala kuhusiana na kiwango cha Mfuko wa Mahakama na mzungumzaji aliyepita amezungumzia kwamba, hatuwezi kuweka kiwango hivi sasa kwa sababu hatuna takwimu. Ninataka nilikumbushe Bunge lako Tukufu kwamba, kila mwaka mwezi wa sita, Waziri wa Fedha na Uchumi, anatoa Taarifa ya Hali ya Uchumi na anaelezea kiwango cha Pato la Taifa tulilonalo kwa maana ya GDP.

Pili, Waheshimiwa Wabunge wakumbuke kwamba, hivi sasa Vyama vyote vya Siasa vinapata ruzuku kutoka Serikalini na kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, ruzuku ile imewekwa kwa kiwango cha asilimia mbili ya Recurrent Budget. Kwa maana hiyo ni kwamba, hata leo tukiamua kwamba, asilimia fulani ya Pato la Taifa, itakuwa ni kwa ajili ya Mhimili wa Mahakama na kwa ajili ya Mhimili wa Bunge pia kama jinsi ambavyo tumekuwa tukihitaji miaka yote iliyopita, bado hatutakuwa tumefanya makosa kwa sababu tayari tunazo sheria ambazo zimetenga kiwango maalumu cha asilimia kutokana na vitu mbalimbali.

8 Kwa hiyo, kwanza, GDP inafahamika; GDP ya Tanzania sasa hivi ni trillion 28. Kwa hiyo, tunaweza tuka-calculate na kujua asilimia mbili inayopendekezwa ama asilimia moja au asilimia 0.5; kiasi gani?

Tatu, hatutakuwa tunafanya kitu kipya kwa sababu Vyama vya Siasa tayari vinapata asilimia kutokana na Recurrent Budget. Nilikuwa ninaomba taarifa hiyo, Waheshimiwa Wabunge waliochangia jana, aliyemaliza kuchangia na watakaokuja kuchangia, wafahamu kwamba, takwimu zipo. (Makofi)

SPIKA: Mimi nilifikiri kwamba, taarifa yako ingekuwa mwafaka tukikaa kama Kamati ya Bunge Zima, maana ndiyo ita-make sense. Sasa hivi kila mtu anachangia anavyoona, Serikali itakuja itujibu.

Tunaendelea na Mheshimiwa Moza Saidy; hayupo? Kwa hiyo, sasa namwita Mheshimiwa Stephen Hilary Ngonyani.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kabla sijaanza kuchangia, ninataka niunge mkono hoja. Mimi kwenye upande wa Sheria nitaondoka kidogo ila nitakwenda kwa hawa watumishi wanaofanya kazi; ninaamini kwamba, wenzangu waliochangia, wamechangia vizuri sana na yote yaliyoongelewa hapa ninafikiri ndiyo tunatakiwa tuyatekeleze.

Mheshimiwa Spika, ila katika Mahakama, ukiizungumzia Mahakama, lazima uizungumzie na wale Makarani wa Mahakama, Matarishi wa Mahakama, Wazee wa Mahakama, Mahakama za Mwanzo za Wilaya pamoja na kule juu. Kinachoumiza zaidi, mimi nitarudi katika Mahakama, hizi hela ambazo walikuwa wanatengewa ni ndogo sana, hazilingani na matumizi. Sasa hivi katika magereza mengi Wananchi wengi wamerundikana, hasa katika Wilaya yangu ya Korogwe. Mahakama zile za Mwanzo ambazo zilikuwepo sasa hivi hakuna hata moja.

Kwa mfano, Mahakama ya Mwanzo ilitakiwa ijengwe kule Mkomazi, lakini mpaka sasa hivi haijajengwa na zile Mahakama za Mwanzo za siku za nyuma zote zimekufa. Sasa hao watu ambao tunawaita Mahakimu, Hakimu mmoja anapewa kazi ya kufanya Mahakama zaidi ya tatu; mazingira wanayofanyia kazi si kwamba atapewa usafiri; Hakimu huyu huyu anakuwa anakwenda mwenyewe kwa kutegemea usafiri wa mabasi na ndani ya basi lile kunakuwa na wale watu ambao anakwenda kuwahukumu; usalama wao unakuwa upo wapi?

Kuna matukio mengi yanatokea kule kwetu, ambapo Hakimu anaonekana mzuri pale anapokuwa anahukumu, lakini akishatoka pale anakuwa hapewi msaada wowote ambao unamfanya awe salama. Wengine wanafanikiwa kupewa, mwingine akilalamika inakuwa ni haraka sana kuhudumiwa. Hawa Mahakimu ninaomba wahudumiwe, kama ni usafiri wapewe usafiri wa kwao ambao utawasaidia kufika kila sehemu wakiwa wako tayari wamepatiwa ulinzi. Ulinzi siyo lazima apatiwe polisi, hata walinzi wa mgambo pia wanaweza wakasaidia Mahakimu. Unashangaa Hakimu anakwenda kuhumu kesi ya

9 ng’ombe, mtu anayetakiwa kufungwa miaka 30, halafu anapanda gari moja na mtuhumiwa. Huu usalama wake uko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja hii ni nzuri sana, lakini tusiangalie kwenye maslahi tu kwamba, waongezewe kipato gani, hata usafiri kama kuna mahali wanatakiwa wapewe, wapewe. Hata mimi kule kwangu kulikuwa na Mahakama ya Vugili, Mnyuzi, Magoma, kulikuwa kuna Mahakama kwenye Kata zote, lakini Mahakama zote zile zimekufa kwa sababu hakuna Mahakimu; Hakimu huyo huyo anakaa pale Korogwe Mjini, anatakiwa atoke Korogwe aende Korogwe Vijijini, huyo huyo anatakiwa aende kwenye kesi ya shamba akasimamie hukumu ya shamba; sasa kwa kweli mimi binafsi maoni yangu ninasema hawa watu hata kama kuna Miradi mingine, ipunguzwe hawa wapewe kiwango kikubwa sana cha pesa kiwasaidie. (Makofi)

Kwa hiyo, kila mmoja ameongea hapa lakini muelewe kwamba, Hakimu peke yake hawezi kufanya kazi bila kuwa na Watumishi. Hawa Watumishi ni wale Makarani wa Mahakama; unamkuta Karani wa Mahakama anaombaomba usafiri hafanyi kazi mahakamani; sasa usawa uko wapi hapa na hawa pia ni binadamu?

Huwezi kuwa na Hakimu bila kuwa na Watumishi wake na hawa Watumishi lazima wawepo ili wamsaidie kuandaa kesi na kuipeleka mahali panapohusika, lakini kila mtu akifika tunaona Mahakama zinakuwa ni kitu kingine kabisa wakati ni Mhimili Mkuu; inatisha sana.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli mimi binafsi ninaunga mkono mara mia moja hii hoja. Katika bajeti yao, ninaomba pia Watumishi wa chini wale mpaka Wazee wa Baraza; wenzangu jana wameongea sana na inatisha sana, Mzee wa Baraza anatoka pale ametoa hukumu nzuri, lakini ikifika pale chini anarubuniwa na kitu kidogo tu anageuka. Anageuka si kwa sababu hana sheria kichwani mwake, sheria anaijua lakini atafanyaje wakati kila siku anakanyaga kwa mguu. Leo hii magereza kumejaa watu utafikiri sasa Wananchi wote wa Tanzania wako ndani ya magereza; sababu ni nini? Kwa sababu Mahakimu ni wachache, ninaomba tuongezewe Mahakimu kwa kila Wilaya, kila Mkoa na kwa kila Mahakama Kuu.

Pesa zipo, tupunguze matumizi mengine tuweke kwa hawa watu wanaoisaidia Serikali. Huwezi kuwa na Serikali kama huna Mhimili ambao utatoa hukumu vizuri. Tuangalie kule nchi za jirani; wenzetu wamezipa kipaumbele sana Mahakama na wanafanya mambo ambayo yanatakiwa hata Mwananchi mwingine anayaona yanafanyika; lakini hapa kwetu kwenye nchi kubwa kama Tanzaniam yenye rasilimali nyingi, ambazo zinaweza kuwasaidia Wananchi na hawa Mahakimu wakawa na huruma kwa nini tusiwaone? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ninaongea nikiwa ninatamani kulia kwa hawa Mahakimu, inatia uchungu mno. Watu wengine wakipeleka maoni yao Serikalini, kwa dakika kumi tu wanasaidiwa lakini Mahakimu hawa ambao wana shida tunawazungusha; kwa nini? Ninaomba tuwaangalie hawa ambao ni Mhimli.

10 Jana wenzangu walizungumza kwamba, utamkuta Hakimu ana tai, lakini tai ile haina kitu, njaa zimemjaa tu, ukimpa shilingi 10,000 kama ahsante siyo lazima iwe rushwa, unampa ahsante tu kwamba amefanya kazi yake nzuri, mtu mwingine anakuja anamwambia umepewa rushwa, basi wanaanza kuandamwa. Sasa hiki kitu ninaomba tukiangalie kwani kama kuna kiwango ambacho kinatakiwa Mahakimu wapewe, basi wapewe kikubwa zaidi ili wafanye kazi zao kwani wanajituma zaidi.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Mahakama kilichopo Lushoto Tanga, kina Walimu wachache, lakini wakihudumiwa vizuri kama alivyozungumza Mheshimiwa Mbunge jana, Mahakimu wengi watakuwa wanatoka zaidi. Vilevile hao Mahakimu wanaotoka wasipelekwe mijini tu, bali wapelekwe hata vijijini kwenye shida, huku mjini ni kurundikana tu, lakini kule vijijini ndiko kwenye matatizo. Kila Hakimu anayemaliza chuo anapelekwa mjini, sasa hizi Mahakama za Vijijini ni nani atazihudumia? Mahakama za Vijijini ndiyo chanzo, vita kubwa haiko mjini iko vijijini. Shida kubwa inawapata watu wa vijijini; kwa mfano, kijijini mkulima amekwenda kulima shamba, lakini anapelekwa Mahakamani anahukumiwa na wakati mwingine anaambiwa Hakimu hayupo, basi anahukumiwa na Karani wa Mahakama, anaambiwa wewe nenda Mahabusu wiki mbili, wakati huo huo shamba lake linadorora, yaani halilimwi, jamani inatisha! Waziri wa Sheria, tumuunge mkono mia kwa mia na Mahakama pia tuiunge mkono kwa asilimia mia kwa mia.

Mheshimiwa Spika, mimi nikiongea sana nitakuwa kama ninapiga debe, wenzangu jana wameongea sana na wameongelea mambo mazito sana ila ninasema hizo hela mwanzo wa bajeti wapewe, siyo kila siku wawe wanasikiliza kwa wenzao. Mnajua kuwa wao pia wana roho, Wafanyakazi wote wanaandamana lakini hawa wamenyamaza tu, Walimu wameandamana lakini Mahakimu wamenyamaza tu na wao wakiandamana hizi kesi za Wabunge zitasikilizwa na nani? Tafadhali wapewe haki yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ninaunga mkono hoja mia kwa mia ili Mahakimu wapewe haki yao tena ikiwezekana hata leo hii. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mimi nilifikiri ukiendelea kusema zaidi utalia kwa nguvu, ahsante sana. Sasa ninamwita Mheshimiwa Dkt. Titus Mlengeya Kamani.

MHE. DKT. TITUS M. KAMANI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi hii na mimi nichangie katika Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, kabla sijachangia, nilifikiri ni vema nikatoa shukrani zangu za dhati kwa Waheshimiwa Wabunge, kwa uchaguzi uliofanyika jana wa Mwakilishi wa SADC. (Makofi)

SPIKA: Ndiyo maana nimekwita, niliona utumie nafasi hiyo kutoa shukrani pia. (Makofi/Kicheko)

11 MHE. DKT. TITUS M. KAMANI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana. Ninawashukuru wote walioniunga mkono. Ninawashukuru vilevile wale wote ambao hawakuniunga mkono, kwa sababu ndiyo demokrasia. Ila ninapenda tu kuwahakikishia wote kwa pamoja na kama nilivyojieleza jana kwamba, nitawawakilisha kwa uhakika, nitachukua mawazo ya Waheshimiwa Wabunge wote ili kuhakikisha kwamba, Bunge letu linawakilishwa ilivyo na kuhakikisha kwamba, Taifa letu linapata stahili sahihi katika Bunge hilo la SADC. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Muswada huu umekuja wakati muafaka na Muswada huu ni muhimu sana kwa sababu unalenga kuweka mazingira mazuri ya Mahakama kufanya kazi kwa uhakika na ufanisi. Kwa hiyo, ninaona ni lazima nitumie nafasi hii kuipongeza Serikali ya , kwa kuchukua hatua ya kuleta mwafaka huu ili Bunge lako Tukufu liweze kuupitisha Muswada huu. Serikali tiifu ni ile ambayo inasikia kilio cha Wananchi na Watendaji wake na kuchukua hatua stahiki, kwa hiyo, ninawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Muswada huu umekuja kwa wakati mwafaka, kwa sababu mazingira ya Mahakama zetu na Watendaji wetu ni duni; ni muhimu sana Muswada huu ukapitishwa ili mambo yarekebishwe kwa haraka iwezekanavyo.

Watendaji wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu; ukiangalia Mahakama za Mwanzo kwanza hakuna Majengo ya Mahakama yenyewe wala Mahakimu hawana nyumba za kuishi. Nikiangalia kwa mfano kule kwetu, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, amepangiwa kwenda kufanya kazi kijijini, lakini yeye ni msomi ametoka Chuo cha Mahakama Lushoto, anapelekwa kuishi katika eneo ambalo linahitaji sana ushujaa wa kuishi. Kwa hiyo, ni muhimu sana mazingira hayo yakaboreshwa.

Mheshimiwa Spika, vilevile hata kwenye Mahakama Kuu ambapo ndipo tunategemea maamuzi makubwa kabisa yafanyike, unakuta chumba cha Hakimu ni kidogo na chembamba, lakini ana Mawakili wamejaa pale wamekuja kusikiliza au kuwatetea wateja wao, yaani kwa kweli hakina tofauti kubwa sana na chumba ambacho wanawekwa washukiwa na unakuta hata wateja wenyewe hawana hata sehemu ya kusimamia au kukaa ndani ya Mahakama, hata kama wamekuja kwa kesi zao. Kwa kweli mazingira hayo ni magumu, lakini ni muhimu sana tukabadilisha hata kama hii fedha inaanza kupatikana, basi itengwe na tufanye juhudi za makusudi, awamu kwa awamu ili tuweze kuboresha mazingira haya.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu sana kuwepo na Mfuko kwa sababu tunategemea kwamba, tunapokuwa tumewasomesha Wataalamu wengi, basi tuwape na ajira bora, yaani ajira nadhifu na nadhifu, siyo elimu tu ni pamoja na ubora wa mazingira ya kufanyia kazi. Kwa hiyo, ni muhimu sana wakawekewa mazingira mazuri ili hata maamuzi yanayotolewa yawe ya uhakika. Hatuna shaka na Wataalamu wetu, elimu wanayoipata ni nzuri kabisa, Vyuo vyetu vya Sheria vinafanya kazi vizuri na utaratibu uliowekwa wa School of Law unafanya kazi vizuri.

12 Kwa hiyo, nina hakika katika competence ya kazi, hatuna shida na Wataalamu, ila ni muhimu sana wakatengenezewa mazingira mazuri ili waweze kufanya kazi vizuri.

Taratibu za kutopandishwa vyeo ni moja kati ya vitu ambavyo vinaweza kuwakatisha tamaa Watendaji. Hakimu anakaa kwenye nafasi moja kwa muda mrefu, hata kama nafasi hiyo ni bora lakini hakaguliwi, yaani hakuna mtu anayemwangalia, hatimaye mtu anakata tamaa anaanza kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa. Kwa hiyo, ni muhimu sana Muswada huu umekuja kwa wakati mwafaka.

Mheshimiwa Spika, vilevile ninapenda nitahadharishe kuhusu Uhuru wa Mahakama. Hiki kitu kimeombwa muda mrefu; ni kitu kipya na kitaanza kufanya kazi kama kitu kipya katika Mahakama zetu. Mara nyingi kitu kipya kinapoanza, kinakuwa na changamoto zake. Uhuru wakati mwingine unaweza ukatumika visivyo na tunaposema Mahakama ni moja ya Mihimili ya Serikali, inapaswa itegemeane katika utoaji wa haki na iende sambamba na utungaji wa Sheria na utekelezaji wa Sheria kwa maana ya Serikali.

Kwa hiyo, tunategemea sana Mahakama yetu inapopata uhuru iutumie vizuri, kusiwe na sababu ya Mamlaka, moja ya Mhimili, kutunisha msuli kwa Mamlaka nyingine kwa kusema sisi ni Mahakama tusiingiliwe hata kama wanafanya visivyo. Kwa hiyo; ni vizuri sana tukauchukua uhuru huu kwa uangalifu na nidhamu na tukautumia vizuri kwa nia njema ya kujenga Taifa letu lenye Uhuru na Umoja.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri nikazungumzia matatizo yaliyopo kwenye Mahakama hususan hii ya kutotunza siri za wateja; hili limekuwa ni tatizo. Kwa mfano, mtu ana kesi yake, majadiliano bado yanaendelea, lakini unakuta habari zinatoka ndani ya Mahakama zinamfikia yule mshindani, sasa utaratibu wa namna hiyo siyo mzuri. Kwa hiyo, ni vizuri sana Mamlaka ambayo itaundwa ya Kusimamia Nidhamu na Maadili ya Watendaji, ifanye kazi yake sawasawa ili kurejesha heshima na nidhamu katika Mahakama zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikijiuliza; Taasisi nyingi zinakuwa na Clients Charter, yaani Mkataba wa Wateja kwamba, unapopeleka hoja fulani unategemea uwe umeshapata majibu yake baada ya muda fulani. Ninafahamu kwamba, Mahakama inaongozwa na misingi mbalimbali, ikiwemo masuala ya upelelezi kutoka kwa chombo kingine cha Serikali, yaani Polisi; lakini kesi inapokaa muda mrefu sana, kwanza, inakuwa ni mateso na kero kwa Serikali yenyewe kwa sababu ya gharama, lakini pia kero kwa Mwananchi ambaye hapatiwi haki yake anayostahili. Sasa mimi sielewi, kwa kweli hili nilifikiri kwamba, wanapojipanga kama Mamlaka ambayo ina uhuru wake, wafikirie namna ya kupunguza muda wa kesi kwisha katika Mahakama zetu.

Kwa kweli hata msongamano wa washukiwa walioko Mahabusu wanarundikana kwa sababu kesi nyingine zinakuwa hazina msingi wa kukaa muda mrefu sana. Ninashauri kwamba, wanapojipanga kama Mamlaka ambayo inajitegemea, watumie

13 nafasi hii kuangalia namna gani wataharakisha kesi kwisha haraka kwenye Mahakama zetu.

Mheshimiwa Spika, vinginevyo, ninauona Muswada huu ni mzuri na ninashukuru sana kwamba, umeletwa wakati huu na ninaomba sasa uandaliwe kuingizwa kwenye Bajeti ya Serikali ili uweze kutekelezwa mara mwaka mpya wa fedha utakapoanza.

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa ninamwita Mheshimiwa Joseph Roman Selasini.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika, nami ninaomba nichukue nafasi hii, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia katika Muswada huu muhimu sana kwa mustakabali wa haki katika Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, niliposoma Muswada huu, kuna maeneo matatu ambayo yalinivutia sana kuchangia. Eneo la kwanza ni lile linalohusu Mtawala Mkuu wa Mahakama, eneo la pili ni lile linalohusu Mfuko wa Mahakama na eneo la tatu ni lile linalohusu Maadili ya Watumishi wa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, nimewasikiliza wachangiaji wenzangu kwa umakini sana, kwanza, ninaomba niseme kwamba, Muswada huu umekuja wakati mwafaka na unastahili kuungwa mkono. Kwa kweli ni Muswada ambao utaweka utaratibu mzuri katika Utawala wa Mahakama zetu na katika utoaji haki kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, wenzangu wametoa maoni yao kuhusu sifa ambazo anapaswa kuwa nazo Mtawala Mkuu wa Mahakama na baadhi ya mapendekezo ni kwamba, sifa mojawapo ya hitaji la ujuzi wa Sheria iongezewe katika sifa zilizopo.

Mheshimiwa Spika, kwa maoni yangu ni kwamba, sifa zilizopo zinatosha pamoja na kwamba, hilo la sifa ya kisheria litasaidia. Mimi ninataka niwatoe hofu wenzangu kwamba, Mtawala Mkuu katika Mahakama, yaani Kiongozi Mkuu wa Mahakama, bado ataendelea kuwa Katibu Mkuu na hili tunaliona hata upande wa Serikali kwamba, Katibu Mkuu Kiongozi hawezi kuwa na Mamlaka makubwa kuliko ya Rais au Katibu wa Bunge, wala hawezi kuwa na Mamlaka makubwa kuliko Spika. Kwa hiyo, ninawaondoa hofu wenzangu kwamba, kwa vyovyote vile, Mtawala Mkuu wa Mahakama, kwa sifa zilizowekwa ni kwamba, atakuwa na uwezo mzuri na wa kutosha katika kufanya kazi zake akishirikiana na Jaji Mkuu.

Mheshimiwa Spika, pia kuhusu ni Mfuko wa Mahakama na hapa ndipo wengi tumejikita katika kutoa maoni yetu; hili ni jambo ambalo limechelewa na kama nilivyosema kuja kwake wakati huu ni jambo zuri kwa sababu ni ukweli usiofichika kwamba; kutokana na Mahakama kuitegemea Hazina kupata fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, imekuwa haitekelezi kikamilifu mipango iliyojipangia. Kwa sababu hiyo, mambo mengi kama walivyosema wenzangu, hayaendi sawasawa na

14 isitoshe ni kwamba, Mahakama imeshindwa kujipanua kila sehemu ili kuwafikia wanaohitaji huduma zake.

Kwa sababu hiyo, mimi ninaungana na wenzangu wote ambao wamechangia eneo hili, wakitutaka sisi Wabunge katika ujumla wetu, tuunge mkono uanzishwaji wa Mfuko huu wa Mahakama ili Mahakama zipate nafasi ya kujipangia mambo yake kwa jinsi inavyofaa.

Wenzangu wameeleza mambo mengi jinsi Majaji na Mahakimu wanavyopata matatizo na mimi siko mbali nao. Ukienda kwenye Mahakama zetu utaona kinachotokea, ukizungumza na Majaji na ukienda katika Mahabusu zetu utaona jinsi watu walivyorundikana kwa sababu kesi zao zinakosa nafasi ya kusikilizwa. Huo ni ushahidi tosha kwamba, sasa tunapaswa tuzipe Mahakama uwezo wa kujipangia mambo yake halafu baadaye tuzihoji maana wao wanasema wanashindwa kufanya kazi kwa sababu ya ufinyu wa bajeti na sisi tunaona kweli kuna matatizo. Sasa la muhimu, tuwape uwezo ili tuone ni nini kitafanyika.

Mimi nina imani kwamba, kwa bidii kwa hali tunayoiona kwa Mahakimu na Majaji wetu, kwa vyovyote vile kama wataweza kusikilizwa na Mfuko huu ukaanzishwa, basi lazima hali ya Mahakama zetu itabadilika. Tunaweza tukashuhudia Mahakama mpya zikijengwa, zile zilizopo zikaboreshwa, maslahi ya Hakimu na Majaji yakaboreshwa na kwa sababu hiyo, utendaji wa kazi ukawa mzuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wengi wamezungumza kuhusu mambo haya na mimi sitaki kurudiarudia, ninapenda nimalizie kwa kusema kwamba, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nami pia ninaunga mkono hoja hii na ninampongeza Waziri kwa kuileta hoja hii kwa wakati mwafaka, hajachelewa kwani huu ndiyo wakati wake na ni wajibu wetu tuipitishe ili kazi iweze kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mheshimiwa Moza Abedi Saidy, ninafikiri ndiye atakuwa mchangiaji wetu wa mwisho.

MHE. MOZA A. SAIDY: Mheshimiwa Spika, ninashukuru. Nami ninaungana na wenzangu waliochangia hoja hii.

Mheshimiwa Spika, ni vema Serikali ikaliona tatizo la fedha linaloikabili Mahakama zetu hapa nchini ili kuziwezesha kufanya kazi kwa ufanisi. Kufanya hivi kutasaidia kuondoa rushwa ndani ya Mahakama iliyojijenga kama Taasisi ili haki itendeke.

Katika kuboresha Mahakama zetu na kuzijengea heshima kubwa kwa Watanzania ni vema Majaji, Mawakili pamoja na Watumishi wa Mahakama wajengewe nyumba kwani kukaa pamoja na raia …

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, hutakiwi kusoma!

15 MHE. MOZA A. SAIDY: Kukaa pamoja na raia inasababisha rushwa nyingi na mazoea ambayo haki nyingi za Wananchi zinakuwa hazitendeki, kwa sababu ya uhusiano wa karibu kati ya Watendaji na Wananchi.

Pamoja na raia, hii itasababisha mara nyingi rushwa na mazoea ambayo kwamba haki nyingi za wananchi zinakuwa hazitendeki kwa sababu ya mahusiano yaliyokuwa karibu. (Makofi)

Mahakama itakuwa na hadhi kubwa kwa kutenda haki kwa wananchi iwapo itapewa ruzuku kubwa kwa kutenda haki kwa wananchi ambayo inaweza kuboreshwa ikawasaidia hata Wazee wa Baraza wanaochangia kutoa hukumu, wakawawezesha bila kungojea hela ambazo zingeweza kutoka kwa watuhumiwa ili kujikimu hapo kidogo. Pia ningependa kuishauri Serikali kuwepo na mfuko wa kuiwezesha Mahakama ili iweze kuendesha kesi zao vizuri na kuweza kutenda haki kwa wananchi wote.

Mheshimiwa Spika, naunga hoja hii mkono percent mia kwa mia kwa sababu mengi yamesemwa na wenzangu, sina budi hoja hii ipite. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kuniweka salama hadi leo hii hata nimeweza kuchangia Muswada huu kupitia maandishi.

Mheshimiwa Spika, katika Muswada huu ningependa kuchangia katika suala la Ethics Committee ambayo kama ni Mkoani, Mwenyekiti wake ni RC, kama ni Wilayani Mwenyekiti ni DC. Jaji au Hakimu hana nafasi ya kushika cheo cha Mwenyekiti katika Kamati hizo, jambo ambalo siyo fani kwa Mhimili na Mahakama.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. SELEMANI SAIDI JAFO: Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru Serikali kwa kuleta Muswada huu hapa Bungeni. Kuwepo kwa Mkuu wa Utawala kutasaidia sana kuleta tija katika Idara ya Mahakama. Ninashauri kwamba Mkuu huyu wa Utawala lazima Kanuni ziwekwe wazi juu ya taratibu za ajira. Napendekeza kwamba ajira iwe kwa Mkataba ili kuongeza ufanisi na uadilifu katika utendaji kazi.

Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana Muswada kuja na kipaumble muhimu cha kuanzisha Mfuko Maalum wa Mahakama. Mimi ninaamini Mfuko huu utasaidia sana katika kuimarisha miundombinu ya Mahakama. Ninashauri upatikanaji wa fedha za kutosha katika Mfuko huu ili uweze kutekeleza mahitaji ya Mahakamani.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

16 MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Naomba Muswada uzingatie yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, sasa hivi tunao uhaba wa Mahakimu wakati wahitimu wa digrii ya Sheria ni wengi na hawana kazi, wanazurura mitaani. Naomba wahitimu wa digrii za Sheria wapelekwe Mahakama za Mwanzo na Wilaya pia.

Mheshimiwa Spika, maslahi ya Mahakimu wa mwanzo, Wilaya, Mkoa na Watendaji wote wa Mahakama kuanzia Mahakama za mwanzo hadi Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ni duni, mishahara ni midogo, haiendani na wakati, hawana nyumba wala usafiri. Naiomba Serikali iwapewe mikopo, matibabu na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, vifaa vya kurekodi mwenendo wa kesi Mahakamani (Hansard) ni muhimu ziwekwe kwenye Mahakama zote kuanzia Mahakama za mwanzo hadi Mahakama ya Rufaa.

Mheshimiwa Spika, upandaji vyeo uzingitie Seniority, usiwe wa upendeleo. Wapo wanaopata vyeo vya kuwa Majaji na kuwaacha watumishi wenye uzoefu wa siku nyingi na wenye uwezo na maadili mema. Hii hali imevunja moyo Watumishi waadilifu.

Mheshimiwa Spika, bajeti ya asilimia mbili ya bajeti ya Taifa siyo mbaya kwa kuanzia, lakini Serikali iwe tayari kuiongeza mara kwa mara ili iendane na hali halisi ya kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha na naunga mkono hoja.

MHE. SALEH A. PAMBA: Mheshimiwa Spika, kwanza, naunga mkono hoja. Napenda kuipongeza Serikali kwa kuleta hoja hii Bungeni. Muswada huu umekuja kwa wakati, kwani msingi mkubwa wa Muswada huu ni kuonyesha kwa vitendo ile dhana ya separation of powers kati ya mihimili mitatu, yaani Bunge, Serikali na Mahakama.

Mheshimiwa Spika, kwa kuanzisha Mfuko wa Mahakama, mhimili huu utapata uhakika wa Bajeti yake ambayo itakuwa ni fungu maalum. Wataweza kupanga maslahi yao, Bajeti yao ya maendeleo na kuimarisha miundombinu ya Mahakama.

Mheshimiwa Spika, tatizo moja kubwa ambalo Mahakama inabidi itekeleze ni kuongeza idadi ya Mahakimu kwa kuajiri Mahakimu wapya wa kutosha na Watumishi wengine.

Mahakama inabidi itumie vifaa vya kisasa katika kusikiliza kesi. TEKNOHAMA ni muhimu. Hii itapunguza gharama za shajala (stationeries) na savings, hizo zitumike katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.

Napongeza pia kwa kuanzishwa Judicial Ethics Committee. Hili ni jambo zuri ambalo linaweka checks kwa Mahakimu ili Mahakimu wetu wasi-abuse madaraka yao. Ethics Committee isiwabane Mahakimu tu, lakini pia iwabane Watendaji wengine wa

17 Mahakama (Non – Judicial Staff) kwani wao nao pia ni sehemu ya infrastucture ya Mahakama. Wahusika wa hili ni Makarani wa Mahakama, Wazee wa Baraza na kadhalika, tukiwaachia washughulikiwe na mamlaka nyingine, hii inaondoa uwajibikaji.

Mheshimiwa Spika, nawatakia kila la heri, naunga mkono hoja.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, naomba Waziri afanye marekebisho yafuatayo kwenye Muswada husika.

Mosi, kifungu cha tatu, aongeze tafsiri ya maneno Court Administrator kama lilivyotumika kwenye kifungu 11(1); Judiciary Services, kama lilivyotumika kwenye kifungu 4(1); na Judiciary officer; kama lilivyotumika kwenye kifungu 4(2).

Pili, kwenye kifungu 7(3) kuongezwe kifungu kidogo (d) ili kiweke sifa ya kuomba anayepaswa kuteuliwa kuwa Chief Court Adminstrator awe na sifa sawa na mtu anayeweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kama vigezo vilivyotajwa kwenye uteuzi wa baadhi ya Wajumbe na Tume ya Uchaguzi au Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora.

Tatu, kwenye kifungu cha 16 kiongezwe kifungu cha tano, yaani 16(5) ili kitaje Wajumbe wa Sekretarieti ambayo imetajwa kwenye kifungu 16(2).

Nne, kifungu cha 50 (1) kiboreshwe ili Wajumbe watoke kwenye Kada ya Mahakama badala ya kutoka Serikali Kuu, yaani Wakuu wa Mikoa na Maafisa Tawala. Marekebisho hayo yatazingatia muktadha na kifungu 46(2) ambapo Wajumbe wametoka au wameteuliwa na Kada ya Mahakama. Mwenyekiti wa Kamati iliyotajwa kwenye 50(1) awe ni Resident Magistrate In Charge of the Region.

Tano, Napenekeza kifungu cha 50(14) kifutwe kwa kuwa mamlaka na majukumu yaliyotolewa yanakinzana na Public Services Act. Kupitishwa kwa Muswada huu bila mabadiliko haya kufanyika kutaathiri uhuru, ufanisi, utawala na uwajibikaji wa Mahakama na hivyo kukosesha faida kamili ambayo ingepatikana kwa kifungu cha Sheria mpya.

MHE. CHRISTINA L. MUGHWAI: Mheshimiwa Spika, napenda nikushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kutoa mchango wangu katika Muswada huu wa Sheria ya Utawala wa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nina wasiwasi kuhusu Muswada huu kuwasilishwa kwa hati/njia ya dharura katika Bunge lako Tukufu. Aina hii ya uwasilishaji inapunguza muda wa kutosha kwa Wabunge na wadau mbalimbali kuupitia kwa makini ili wauboreshe kwa manufaa ya nchi. Mimi sioni udharura wowote wa kuuwasilisha Muswada, kwani nchi haiko katika hatari ya vita au janga lolote.

Mheshimiwa Spika, Muswada huu unazungumzia kuanzishwa kwa Tume ya Utumishi ya Mahakama, lakini itakayoongozwa na mtu asiye na taaluma yoyote ya

18 Kimahakama. Idara ya Mahakama inaongozwa na taaluma mahsusi zenye mila na desturi maalum, itakuwaje? Basi Tume ya Utumishi wa Mahakama iongozwe na mtu asiye na taratibu, mila na desturi za Mahakama? Aidha, mtawala huyu wa Mahakama kwa mujibu wa Muswada huu anakuwa chini ya mamlaka tatu tofauti ambazo ni Rais, aliyemteua, Tume ya Mahakama iliyopendekeza jina lake kwa Rais na pia atawajibika kwa Jaji Mkuu. Hali hii inamfanya mtawala huyu wa Mahakama kushindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa kuhofia kumridhisha ama kutomfurahisha Mkuu wa Mamlaka mojawapo inapotokea mgongano wa maslahi. Hivyo basi, napendekeza mtawala wa Mahakama awajibike kwa mamlaka moja tu ambayo ni Tume iliyopendekeza jina lake.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuzungumzia hali duni inayozikabili Mahakama zetu zote. Mishahara isiyoendana na gharama halisi za maisha, mazingira mabovu ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa muhimu vya kufanyia kazi. Hali hii inasababisha mlundikano wa kesi, mlundikano wa mahabusu katika Magereza yetu na mbaya zaidi ni vitendo vya rushwa vinavyotokea katika Idara ya Mahakama. Katika mazingira kama haya wananchi wengi wanakosa haki zao.

Mheshimiwa Spika, ikiwa Mahakama ni mojawapo ya mihimili mitatu inayojitegemea/yenye uhuru kamili katika nchi yetu, ni kwa vipi basi mhimili huu umekuwa haupewi umuhimu wa kutosha hasa katika bajeti ya kuendesha Mahakama kama ilivyo kwa Serikali na Bunge?

Mheshimiwa Spika, Serikali inapuuza umuhimu wa kazi muhimu ya Idara ya Mahakama na hivyo basi, kuwapuuza wananchi wanaotafuta haki zao. Naishauri Serikali ianze kuipa Idara ya Mahakama fedha za kutosha ili kuendesha shughuli zake na kama fedha hazitoshi, basi mgawanyo ufanyike kwa uwiano sawa na mihimili mingine ambayo ni Bunge na Serikali.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itambue umuhimu wa kuipa mihimili mingine uhuru kamili. Rais ambaye ni Mkuu wa Serikali anaingilia uhuru wa Mahakama kwa kumteua Mtawala Mkuu wa Mahakama, Jaji Mkuu pamoja na viongozi wengine wa Mahakama kama ilivyo katika Muswada huu na Katiba yetu. Hapa ni kuifanya Idara ya Mahakama kuwa chini ya Serikali badala ya kuwa mhimili ulio na uhuru kamili.

Mheshimiwa Spika, ikiwa Muswada huu una nia njema na Idara ya Mahakama na wananchi kwa ujumla, ninaiomba Serikali izingatie maoni haya na ya wadau wenyewe ambao wanahusiana moja kwa moja na Mahakama ama Mahakama yenyewe.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kupata fursa ya kuchangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, ningependa kujikita katika suala la fedha. Mahakama kutopewa fedha kulingana na mahitaji yake halisi ni kupunguza uwezo wa chombo hiki muhimu cha kutafsiri sheria na utoaji wa haki. Upungufu mkubwa wa fedha katika

19 chombo hiki muhimu kunapelekea kudorora kwa nguvu kazi na uchumi wa Tanzania kwa sehemu fulani.

Ninasema hayo kwa kuwa kuna mlundikano mkubwa sana wa kesi ambazo upungufu wa fedha umepunguza vikao hasa vya Mahakama Kuu na mahabusu wanaosubiri sheria ifuate mkondo na haki itendeke kwa ama kifungo, faini au kuachiwa huru wanaokuwapo katika jela kwa kusubiri haki itendeke ilhali mtu (kijana) ambaye yupo Rumande kwa muda mrefu anakuwa amezuiliwa kufanya shughuli za maendeleo yake binafsi au ya Taifa kwa ujumla. Hapo ndipo maana ya tafsiri yangu kuwa, kutokuwa na fedha za kukidhi mahitaji ya Mahakama kunapunguza ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kuwa nguvu kazi, vijana wengi wanacheleweshewa kupata haki kwa either kupata adhabu na kuitumikia mapema au kuachiwa huru ili wakalijenge Taifa.

Mheshimiwa Spika, pia ugumu wa kazi za Mahakama utajitokeza kama malipo na hali ya maisha ya Watumishi na Watendaji wa Mahakama yatakuwa duni jambo ambalo litasababisha baadhi ya watu kujitoa katika fani ya Sheria na kufanya kazi nyingine ikiwemo Mahakimu na Majaji kufanya shughuli nyingine zenye kipato na hapo patapelekea mhimili huu kuanguka au kulegea na hapo ni hatari kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, suala la utoaji haki sio dogo, linahitaji sana kuridhika kwa mtoa haki na kuwa na mazingira mazuri ya kufanya kazi na kuwavutia watu wengi hasa waliopo vyuoni kusomea sheria na kuwa na Mahakimu wengi na Majaji ili Mahakama zote kuanzia Mahakama za Mwanzo hadi Mahakama za Juu kuwa na Watumishi wa kutosha na hapo mhimili huu utakuwa imara.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa, amani inadumu kama haki itatendeka. Bila haki, amani haipo kwa kuwa nchi yetu inajulikana kama kisiwa cha amani (island of peace), basi ni vizuri kuhakikisha kuwa chombo cha kutoa haki kinakuwa imara na kinakuwa huru.

Mheshimiwa Spika, mimi naunga mkono hoja ya kuwa na Mfuko wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, ila napenda kutoa tu angalizo kwamba ni lazima kuwe na nidhamu kuu katika fedha na utendaji, maana power without control is nothing.

Mheshimiwa Spika, napenda kusisitiza tena ni muda muafaka wa Muswada na napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa waliochangia kwa kuongea.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hasa kwa yale ambayo Kambi rasmi ya Upinzani imeyaongea na hasa katika kuipa Mahakama uwezo na kuepuka fedheha. Naunga mkono hoja.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nichukue fursa hii kumpongeza Waziri wa Sheria na Katiba - Mheshimiwa Celina O. Kombani pamoja na timu yake yote ya Wizara ya Sheria. Pia nawapongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge kwa ushauri walioutoa kuhusu uwasilishwaji wa Muswada huu unaohusu uendeshaji wa Mahakama wa mwaka 2011.

20

Mheshimiwa Spika, nina imani kupitishwa kwa Muswada huu sasa kutazipa hadhi Mahakama zetu na kuwa chombo kilicho bora na kitakachoweza kutenda haki kwa wananchi wake.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kuwa hali za Mahakama nchini ni matatizo matupu, ambayo yanapelekea Mahakimu na Watendaji wake kupokea rushwa na kutotenda haki kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, mahabusu zetu hazifai kwa mlundikano wa kesi zisizokwisha, sababu kubwa ni uhaba wa Mahakimu na ucheleweshaji wa upelelezi wa kesi. Kupitishwa kwa Muswada huu kutasaidia hata ubora wa vitendea kazi na samani za Mahakama. Siyo jambo la ajabu kupotea kwa mafaili katika Mahakama zetu nyingi. Imani yangu Mahakama zetu sasa zitakuwa na mfumo mzuri zaidi wa uhifadhi wa majarida ya kesi za wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, kupitishwa kwa Muswada huo kutasaidia hata maslahi kuanzia Majaji, Mahakimu na Watendaji wote wa chombo hiki cha Sheria. Ni aibu chombo cha Mahakama kuwa na madeni yasiyolipika. Tuna imani baada ya kupitishwa Muswada huu mambo kama hayo hayatajitokeza. Kupitishwa kwa Muswada huu kutasaidia hata wananchi kupatiwa elimu ya kujua Sheria ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Bunge lako Tukufu limetunga sheria nyingi sana, lakini wananchi hawapati fursa ya kuelimishwa na kujua haki zao. Wananchi wengi hawatendewi haki kwa kutojua sheria na wengine wanavunja sheria kwa kutojua kama ni makosa. Hivyo, ninaomba uwepo utaratibu mzuri wa kutoa elimu kwa wananchi kuanzia vijijini mpaka Mijini. Pia kuwepo na utaratibu wa kufuatilia kama hizi sheria zinatekelezeka.

Mheshimiwa Spika, tunaomba uwepo uboreshaji wa jinsi ya ufuatiliaji wa jinsi ya kuripoti kesi zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia. Wanawake wengi wanashindwa kuripoti na kuwa wawazi kwa matendo maovu wanayotendewa kutokana na utaratibu mbovu uliopo sasa wa kuripoti matukio. Hii inasababisha kutotekelezeka kwa Sheria inayomlinda mwanamke.

Mheshimiwa Spika, baada ya mchango wangu huo, naomba nami naunga mkono hoja hiyo.

MHE. REGIA E. MTEMA: Mheshimiwa Spika, kuna haja ya kuongeza Kanda za Mahakama Kuu ili kuwapunguzia gharama watumiaji na vile vile kupunguza msongamano kwenye ofisi husika.

Mheshimiwa Spika, bajeti ya Mahakama iongezwe na Mtawala Mkuu wa Mahakama apunguziwe majukumu.

21 MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, inabidi ikumbukwe na kuzingatia kuwa umuhimu wa siku ya mtu anayetimiza vigezo vya kuteuliwa kuwa Chief Court Administrator kwa mujibu wa kifungu 7(3) pamoja na vigezo vingine awe pia na taaluma ya sheria kwa kiwango cha kutimiza sifa ya kuteuliwa kuwa Wakili, Hakimu au hata Jaji.

Mheshimiwa Spika, Waziri ametoa hoja kuwa Muswada umeletwa kwa hati ya dharura ili liingizwe kwenye bajeti. Hii ni hoja isiyo na uzito kwa kuwa tungeweza kuuleta Muswada huu kusomwa kwa mara ya kwanza, mara ya pili ungesomwa wakati wa Bunge la Bajeti.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa historia ya nchi yetu inaonyesha kuwa ipo Miswada ambayo imewahi kusomwa wakati wa bajeti, bado Sheria ingeweza kupitishwa wakati wa Bunge la Bajeti na kuweza kutengewa fedha, au hata fedha ingeweza kutengwa kama fungu la ujumla na Sheria ingetungwa mwezi Novemba au hata Bajeti yake kuwekwa kama Supplementary Budget. Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 50(1), Wajumbe wote ambao ni Wanasiasa kama Wakuu wa Mikoa na Maafisa Tawala waondolewe ili Mahakama zisiingiliwe na Wanasiasa.

Mheshimiwa Spika, muundo wa Kamati kama ilivyo sasa ni kinyume na misingi ya mgawanyo wa madaraka uliopo kwenye Katiba, kwa kuwaweka Wakuu wa Mikoa na Maafisa Tawala ambao ni Watumishi wa Serikali na Wapambe wa Rais ni kuingilia uhuru wa mhimili wa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na ninaomba mawazo yangu yafanyiwe kazi.

MHE. AMINA ANDREW CLEMENT: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia Muswada wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama. Awali ya yote, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika itakapokuwa kuna Idara ya Utawala itakayoshughulikia shughuli za utawala, utumishi itawezesha Mahakimu kushughulikia shughuli za Mahakama tu. Naunga mkono hoja.

MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja, ila napendekeza marekebisho yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa saba, kifungu cha 7(3) kinaonyesha sifa za mtu atakayeteuliwa kuwa Mtawala Mkuu. Pendekezo langu ni kwamba, mtu huyu pia awe ni Mwanasheria anayefahamu mfumo wa kimahakama wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ukurasa 24 mpaka 27 unahusu Kamati za Maadili za Watumishi wa Kimahakama, ngazi ya Mkoa na Wilaya. Kifungu cha 50 hadi 51 Kamati

22 hizi zisisimamiwe na Wakuu wa Mikoa/Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Mkoa/Wilaya. Mimi napendekeza kwamba Kamati iundwe na watumishi wa Kimahakama kwenye ngazi husika.

Mheshimiwa Spika, pia napendekeza Mtawala Mkuu wa Mahakama awajibike kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama kinidhamu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 7(3) kinazungumzia Mtawala Mkuu wa Mahakama kwamba hatakuwa Mwanasheria. Eneo la Mahakama na Sheria ni eneo muhimu sana, kwa kuwa na Mtawala asiyejua Sheria ni hatari kwa Taifa.

Mfano, sentencing procedures ziko very complex kama detribution ni adhabu kwa ajili ya kulipa faini au fidia lakini deterrence ni adhabu ya kumsahihisha mtuhumiwa ili awe mtu mwema. Adhabu kama rehabilitation inatolewa kwa mtuhumiwa ili apate matibabu wakati incapacitation inatolewa ili kumwondolea mtuhumiwa uwezo wa kufanya kosa tena. Endapo Mtawala Mkuu wa Mahakama hataijua Sheria, yaani hatakuwa Mwanasheria, nina wasiwasi mkubwa sana kama utendaji wenye tija katika Taifa letu utakuwepo. Hivyo ingekuwa vyema Mtawala huyu awe Mwanasheria.

Mheshimiwa Spika, suala la rushwa limetawala katika Mahakama zetu, hii ni kwa sababu Watumishi hawa hawapati mishahara inayokidhi mahitaji yao. Ni bora tuangalie nyongeza ya mishahara kwa Watumishi hawa ili wasishawishike kuchukua rushwa.

Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kuwasilisha.

MHE. MWANAMRISHO T. ABAMA: Mheshimiwa Spika, mchango wangu ni mdogo tu. Kwanza, budget za Mahakama ni ndogo sana na pia hazifiki kwa muda muafaka. Aidha, hawana usafiri na usalama wao huwa mdogo sana na ndio maana rushwa katika Mahakama zetu haziondoki.

Mheshimiwa Spika, ushauri, kwanza budget zifike muda muafaka na ziongezwe. Pili, Mahakimu waongezwe katika Mahakama zetu ili kuondokana na kulimbikiza Mahabusu wengi na Mahakimu wapatiwe usafiri ili kulinda usalama wao.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC: Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kuleta Muswada huu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama. Ni kweli kabisa Mahakama zetu nchini zina upungufu sana.

Mheshimiwa Spika, kwanza, Wanasheria hawatoshi hivyo kuna haja ya kuhakikisha Mahakimu wanaajiriwa katika Mahakama za Mikoa na Wilaya ili kuondoa msongamano wa kesi zinazochukua muda mrefu bila kusikilizwa.

23

Mheshimiwa Spika, pili, Serikali ihakikishe Mahakama zote zinaondokana na tatizo la ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi kama vile karatasi za kuandikia, fedha za kuendeshea mambo ya dharura ya kiofisi, majengo ya nyumba za Mahakama yanayoridhisha tofauti na sasa majengo mengi ya Mahakama za Mwanzo ni magofu yaani nyumba zilizochoka.

Mheshimiwa Spika, mwisho, Mahakimu wapewe mafunzo kuhusu kuepukana na rushwa, kwani inapindisha haki na hivyo kuwafanya Mahakimu wasitoe haki inayostahili kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii kama nimekosea naomba radhi kwani ni mara yangu ya kwanza, ahsante.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri wa Katiba na Sheria kwa kuleta Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, kwanza, Mahakama iliyonyong’onyea kwa kukosa funds au autonomy yake ya kipato, haiwezi kutenda haki inayostahili kwa muda mrefu. Tulizoea kuwaita “Lords” lakini hawafanani na hali halisi. Lord asiye na uwezo au mwenye mawazo ya jinsi gani ataendesha shughuli zake wakati huo huo akipokea malalamiko mengi ya upungufu wa utekelezaji wake anazidi kuchanganyikiwa, ni sawa na kuwa na meno ya plastic.

Nashauri Mahakama ipewe pesa za kutosha ili huduma hizi zifike mpaka vijijini. Wananchi wanapata shida sana kupata haki zao. Ni usumbufu mtupu, mtu mpaka aende Wilayani au katika Tarafa nyingine ndio apate huduma ya Mahakama. Mfano, wakazi wa Kata ya Kihagara mpaka aende Mahakama ya Mwanzo ya Nyoni, hivi kweli sio mateso? Naomba katika mipango yetu, Kata ya Kihagara, Wilaya ya Ziwa Nyasa ipewe kipaumbele, Wananchi tutakuwa tayari kuchangia ili mradi tusaidiwe utaratibu wa kufuata.

Mheshimiwa Spika, mwisho, Mahakama imesahaulika kwa muda mrefu, pia hawana majengo ya kutosha. maeneo yamejaa, Mahakama Kuu itafute eneo Dodoma na ipate pesa za kutosha ili Ofisi Kuu iwe Dodoma kama ndugu zao Bunge na watu wapate huduma hii kirahisi.

Mheshimiwa Spika, mishahara ya Watumishi pia iboreshwe ama sivyo rushwa dhidi yao haitaisha, kwani sio rushwa, bali ni hali halisi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kutoa mchango wangu kuunga mkono Muswada wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama wa mwaka 2011 (The Judiciary Administration Bill, 2011).

24 Mheshimiwa Spika, katika kuunga mkono Muswada huu, napenda kupendekeza mambo yafuatayo:-

Kwanza, mazingira ya kazi ya Majaji wetu yaboreshwe, hii ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi vilivyo bora kama vile kompyuta na kadhalika.

Pili, ni muhimu maslahi ya Majaji yaboreshwe kama vile kupatiwa mishahara inayokidhi ili waweze kuepukana na vishawishi vya kupokea rushwa.

Mheshimiwa Spika, tatu, kwa kuwa wengi wao Majaji wetu wana umri mkubwa basi wapatiwe kozi fupifupi ili waweze kuendana na wakati kwa kufahamu mambo mapya katika taaluma yao.

Mheshimiwa Spika, nne, ni vema pia idadi ya Majaji Vijana ikaongezeka, hii itaongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Mahakama zetu na hivyo kesi nyingi kuweza kusikilizwa kwa muda mfupi na hivyo kupunguza idadi ya Mahabusu wetu ambao kesi zao huchukua muda mrefu kutokana na upungufu wa Majaji katika Mahakama zetu.

Mheshimiwa Spika, kwa haya machache, naomba kuwakilisha, ahsante.

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Spika, naomba nichangie katika maeneno machache kwenye Muswada huu wa Sheria ya Utawala wa Mahakama, 2011.

Mheshimiwa Spika, kama inavyopendekezwa kwenye Kifungu cha 7 cha Muswada kuhusu nani ataongoza Tumishi ya Mahakama na kwamba Muswada unapendekeza Tumishi hii iongozwe na Mtawala Mkuu wa Mahakama ambaye atateuliwa na Rais kutoka kwenye mapendekezo ya watu watatu toka Tume ya Utumishi wa Mahakama, ushauri wangu ni kwamba badala ya mtu huyu kuwa ameshikilia nafasi ya juu kule Utumishi wa Umma, mtu huyu awe ana ujuzi wa Sheria kwa hali ya juu ili aweze kumudu hekaheka za Mahakama ambazo zinaongozwa zaidi na sheria na taratibu za Kimahakama. Mtu ambaye hana ujuzi huu itamuia vigumu kufanya kazi yake ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni tatizo la pesa zinazozikabili Mahakama zetu katika utendaji kazi wake. Uhaba huu wa fedha umekuwa ukikwamisha kesi kumalizika kwa wakati na vilevile wananchi walio wengi na ambao ni maskini hupata shida ya kuzunguka Mahakamani ili kufuatilia haki zao, matokeo yake ni wengine kukata tamaa na kuacha kufuatilia kesi zao na hivyo kupoteza haki zao. Suala hili linajitokeza katika mgawanyo wa Mahakama za Kikanda ambazo hazikidhi mahitaji ya wananchi. Mfano mtu analazimika kutoka Singida ambako hakuna Mahakama Kuu na kufuata haki yake Dodoma palipo na Mahakama Kuu. Gharama hizi ni tatizo si kwa Mahakama peke yake bali pia kwa wananchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, uhaba huu wa fedha unatokana na bajeti ndogo inayotengwa kwenye Mahakama zetu. Kutokana na hilo si ajabu kuona kwamba rushwa inatawala

25 kwa upande wa Mahakama na hata Majaji wasio waaminifu. Matokeo yake ni kuwa na jamii ambayo inategemea kupata haki yake ya msingi kwa kununua hata mahali ambapo haki hiyo ni ya lazima kwake kama raia wa Tanzania. Ushauri wangu ni kwamba Mahakama zitengewe fedha za kutosha katika bajeti ijayo ili ziweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, si hilo tu, Mahakama zetu zina upungufu mkubwa wa Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu ambao unapelekea mlundikano wa kesi Mahakamani. Hii nayo inapelekea vitendo vya rushwa ili mtu aweze kupata haki yake upesi kama Wanasheria wanavyosema kwamba “Haki iliyocheleweshwa ni sawasawa na haki iliyonyimwa”. Kwa hiyo, uamuzi unaochelewa kutolewa kwenye kesi ni sawa na mtu kupoteza haki yake. Ushauri wangu ni kwamba vipaumbele vya ajira viwe kwa wanavyuo wanaomaliza masomo yao, waajiriwe kwenye Mahakama zetu bila kujali uzoefu walionao ili waweze kufanya kazi kama wasaidizi wakati huohuo wakipata uzoefu kutoka kwa Mahakimu wazoefu.

Mheshimiwa Spika, Muswada huu pia haukuzingatia mgawanyo wa madaraka uliowekwa na Katiba ya nchi, Ibara 4(1) na (2) baina ya vyombo vyenye mamlaka ya utendaji, utoaji haki na kutunga sheria pamoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma. Muswada huu unampa Rais ingawa bila kuonekana, madaraka makubwa kutoka utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Kimahakama. Hii inajitokeza pale ambapo Rais anamteua Mtawala Mkuu wa Mahakama badala ya Bunge wala chombo kingine cha uwakilishi wa wananchi na usimamizi ambacho kina mamlaka ya kuthibitisha uteuzi wa Rais, Kifungu 7(1). Rais pia ndiye anayetoa masharti ya ajira ya Mtawala Mkuu, Kifungu 9 na mamlaka ya nidhamu juu yake.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kwamba Rais afanye kazi yake kulingana na Katiba ya nchi na mgawanyo wa madaraka uwe wazi ili kila mtu afanye kazi yake kwa ufanisi. Matokeo ya Rais kupewa kazi ya kumteua Mtawala Mkuu wa Mahakama yatasababisha kusuasua kwa maamuzi pale ambapo Mtawala Mkuu anapokabiliwa na uamuzi wa kutii mamlaka ipi, si ajabu akatiii na kuwajibika kwa mamlaka inayoweza kumuondolea ajira yake, ile iliyomteua yaani Rais.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMIS: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe binafsi na Bunge lako Tukufu. Pia napenda kumpongeza Waziri wa Sheria, Mheshimiwa pamoja na timu yake ya wataalam kwa kuleta Muswada huu mbele ya Bunge hili.

Mheshimiwa Spika, napenda nianze kwa kuunga mkono hoja. Muswada huu ni muhimu sana kwani bila ya haki hakuna demokrasia na demokrasia ya kweli haiwezi kupatikana bila ya uhuru halisi wa Mahakama. Uhuru wa kweli wa Mahakama hauwezi kupatikana bila ya Idara ya Mahakama kupatiwa fedha zitakazokidhi mahitaji halisi ya Idara ya Mahakama. Kwa vile Mahakama ni mhimili mmoja kati ya mihimili mitatu ya

26 dola, hapana budi mhimili huu wa Mahakama uboreshwe kwa kupatiwa bajeti ya fedha inayostahili ili iweze kujiendesha na kufanya kazi kwa ufanisi, usawa na kwa haki kabisa.

Mheshimiwa Spika, katika ulimwengu huu wa Sayansi na Teknolojia, soko huru na utandawazi ni wazi pia uhalifu unakuwa ni wa kisayansi na wenye wigo mpana. Kwa mantiki hiyo basi, ushawishi wa rushwa ili kupindisha haki nao pia unakuwa wa kisayansi na mkubwa zaidi. Kwa hoja hiyo, ni dhahiri kabisa bajeti inayotosheleza ndiyo suluhisho la haki kutendeka. Pamoja na uadilifu wa Majaji na Mahakimu wetu walionao kutokana na uzalendo wa nchi yao, lakini njaa na mahitaji muhimu ya ufanisi wa kutenda kazi katika Idara ya Mahakama ni jambo zuri mno.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kuishauri Serikali juu ya matumzi ya fedha za Mahakama hasa zikiwa zinasimamiwa na Administrator kama Mtendaji Mkuu. Hapo siku za nyumba, pesa hizi zimekuwa zikirudi Serikalini ilihali Mahakama zetu zina uhaba wa vifaa na uchakavu wa majengo. Pamoja na kuunga mkono Muswada huu, tungependa msimamizi huyu awe na proper ultilization ya fedha zinazotolewa kwa ajili hiyo na kusiwe na pesa inayorudishwa kwa kukosa kutumiwa kwani kutakuwa hakuna tofauti kati ya wasimamizi wa Mahakama wa zamani na wa sasa.

Pamoja na hayo tunaunga mkono kuanzishwa kwa Mfuko huu ila gharama za kesi zimekuwa kubwa sana hasa gharama za kesi za uchaguzi hali inayofanya Watanzania wengi wapoteze haki ijulikanayo kama “Access to Justice”.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, naomba, kwa muhtasari nichangie kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kuhusu bajeti ndogo kuliko mahitaji. Serikali ijitahidi kutenga bajeti ya Idara ya Mahakama, lakini sambamba na maeneo mengine ya kipaumbele.

Mheshimiwa Spika, pili, kutotolewa kwa fedha zote zinazotengwa katika bajeti. Hali hii inazikumba Idara nyingi na maeneo mbalimbali. Ikumbukwe kuwa bajeti ni mpango wa makusanyo na matumizi. Hivyo, matumizi hayawezi kuzidi mapato, hata hivyo tuzingatie vipaumbele.

Mheshimiwa Spika, tatu, malipo ya stahili kama mishahara, posho, marupurupu na kadhalika kuwa madogo. Hoja hii ijadiliwe kwa kuzingatia ukweli kwamba Wanasheria kwa maana ya Mahakimu, Majaji na kadhalika wanazo stahili mbalimbali kama ilivyo kwa Wataalamu wa taaluma zingine. Kwa mfano, fedha nyingi za Serikali hutengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, wataalam au wahusika wakuu ni Wahandisi. Tukiwa na Engineers waliohamasika kwa kulipwa stahili

27 zao vizuri, wakawa makini katika kazi zao na idadi yao ikawa ya kutosha, Serikali itaweza kuokoa fedha nyingi sana ambazo zinaweza pia kusaidia katika maeneo mengine ya vipaumbele ikiwemo Idara ya Mahakama na mengineyo. Tuzingatie kuboresha maslahi ya wataalam wetu kwa kuzingatia umuhimu.

Nne, upangaji wa bajeti kwa kutumia GDP. Siungi mkono utaratibu huu kwa ujumla wake. GDP ni source moja tu ingawa ndiyo kubwa. Hata hivyo tusifanye makosa ya kudhani kwamba GDP hiyo hasa unapotaja asilimia huisha, maana ukisema asilimia mia moja (100%) ya GDP maana yake ugawaji wake lazima uwe makini kuliko kutumika tu asilimia fulani itumike hivi au vile. Tutajikuta vipaumbele vingine havina kipande cha GDP cha kuvisaidia. Hivyo naunga mkono hoja ya kujipanga kwa takwimu ya mahitaji na vipaumbele kabla ya kuigawanya GDP.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kipindi kirefu tumekuwa tukitunga Sheria mbalimbali lakini jamii imekumbwa na upungufu mkubwa wa kutozielewa Sheria husika, ninapendekeza Wizara ya Sheria na Katiba iweke mikakati ya kutoa vijarida vyenye lugha rahisi ya wanajamii ili waweze kuzielewa sheria hizi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Sheria ya Utumishi wa Mahakama, Sura ya 237 inafutwa kutokana na ujio wa Sheria hii mpya, napendekeza kwamba Watumishi wa Idara ya Mahakama wanaohusika na usimamizi na utekelezaji wa Sheria hii, wanapaswa kujielekeza katika kuzielewa Sheria hii na vipengele vyake ili waweze kutenda haki kwa mujibu wa Sheria hii husika kama inavyoelekeza.

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Wanyamapori inawagusa wananchi wengi maskini wanaoishi vijijini ambao uelewa wao juu ya Sheria mbalimbali ni mdogo sana. Naomba Idara ya Mahakama na Wizara ya Maliasili na Utalii iweke utaratibu ili wananchi wanaoishi maeneo ya hifadhi wapate elimu pana juu ya Sheria hii ili kuwaepusha wananchi hao kuingia katika makosa kutokana na uelewa wao mdogo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, ni Muswada mzuri, umekuja wakati muafaka ili kuwezesha Mahakama zetu zifanye kazi kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, endapo hii Tume ya Utumishi wa Mahakama itaundwa, ihakikishe inawapandisha vyeo Mahakimu na kuangalia upya mishahara ya watumishi wa Mahakama hususan Mahakimu ili kuwajengea morali ya kufanya kazi na kuepusha rushwa.

Mheshimiwa Spika, Mtendaji Mkuu wa Mahakama (Chief Court Administrator) muda wake wa kazi uelezwe na siyo Rais kuamua ili kuwezesha uwajibikaji kama ilivyo kwa Kamisheni (3 years). Kwa kuwa Kamisheni ndiyo inayopendekeza majina matatu ya Chief Court Administrator, basi awajibike kwa Kamisheni na isiwe kwa Rais kwani yeye

28 ndiye Katibu wa Kamisheni pale ambapo hatekelezi majukumu yake, basi Kamisheni imuwajibishe.

Mheshimiwa Spika, madaraka ya Rais ni makubwa sana, mfano, anateua Kamisheni, Mkurugenzi Mkuu wa Mahakama, Msajili, hii bado inaleta maswali kwa walio wengi katika uhuru wa Mahakama kufanya maamuzi.

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Mahakama kupewa nafasi ya kupokea fedha toka nje au Serikali yoyote nje ya nchi au ya kigeni, iangaliwe kwa makini, isije ikatumika kuongeza deni la Taifa (Mkopo wa Serikali). Uwazi na uwajibikaji uwepo kwenye hizi fedha. Vilevile ngazi za Wilaya, Mikoa ihusishwe katika bajeti na matumizi ya fedha za Mfuko wa Mahakama. Pia Chief Court Administrator wakati wa kuandaa bajeti awahusishe watu wa ngazi za chini.

MHE. ZAHRA ALI HAMAD: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia Muswada huu ulio mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, Mahakama ni mhimili muhimu katika nchi yetu. Kuletwa kwa Sheria hii, naipongeza Serikali kwa dhati. Umuhimu wa Mahakama kuwa na Tume ya Uendeshaji, ni jambo la muhimu sana. Itaweza kuweka heshima kwa Majaji wetu na pia kuboresha Mahakama zetu na kupelekea msukumo wa kesi zetu na kuondokana na msongamano katika mahabusu zetu.

Mheshimiwa Spika, tunakusudia kuanzisha Mfuko, Mfuko unaonekana kuwa na nia nzuri, hivyo ni vizuri Mfuko huo kutizama vipaumbele na kusimamia vizuri kwa ajili ya kufanikisha utendaji mzuri wa Mahakama na kufanya kazi katika sehemu zote. Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono Muswada wa Sheria kama ulivyowasilishwa na Waziri pamoja na maoni ya Kamati yaliyowasilishwa na Mheshimiwa Simbachawene.

Mheshimiwa Spika, Muswada huu ni muhimu sana hasa muda huu tulinao. Kwanza, Muswada umechelewa, naipongeza Serikali kwa kuuleta kwa Hati ya Dharura ambapo ni utaratibu wetu kufuatana na Kanuni za Bunge letu. Ni lazima twende na wakati, hatuwezi kusubiri eti tuwaogope Wapinzani wanaosema kwa nini tumeleta Muswada kwa Hati ya Dharura. Naiomba Serikali isiogope kuleta Muswada wowote kwa Hati ya Dharura kwa kuwaogopa Wapinzani, hii ni kwa manufaa ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali, tunapoboresha Muswada wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama, iboreshe maslahi ya watumishi wa Mahakama, vitendea kazi, majengo, usafiri kwa Mahakama hasa kwa Mahakama za Mwanzo na Mahakama za Wilaya. Mfano, Mahakama ya Kwimba, Wilaya ya Ngudu, ofisi hiyo inalo gari la Mahakama, lakini gari hilo halina Dereva wa kuliendesha, huwabidi waombe Dereva kwa Mkurugenzi. Mbaya zaidi, gari hilo hukosa mafuta ya kuliendesha na inabidi waombe mafuta kwa Mbunge au Halmashauri. Si jambo baya kuomba, lakini isiwe kila

29 mara kuomba kutokana na ofisi hiyo kutopewa OC kwa matumizi ya uendeshaji wa ofisi hiyo. Naomba Serikali, mbali na kuboresha Sheria, basi tuboreshe mazingira ya ofisi hizo zinazotoa haki.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono.

MHE. FATUMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Spika, kwanza, naunga mkono asilimia mia kwa mia.

Mheshimiwa Spika, Serikali ichukue hatua za makusudi za kuendeleza ujenzi wa majengo ya Mahakama na kuongeza Mahakimu wa Wilaya, Mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Rufaa. Watendaji hao ni wachache sana, hivyo kusababisha kurundikana kwa kesi mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, tunaomba Serikali iongeze bajeti ili kukidhi haja.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, kama mmoja wa mihimili mitatu nchini mwetu, ni muhimu sana kuwa na Mfuko wa Mahakama unaosimamiwa ipasavyo. Hili ni jambo la muhimu sana ili kuwezesha kupanga na kutekeleza shughuli zao bila kucheleweshwa na mhimili mwingine. Mfuko wa mhimili huu ukianza kufanya kazi utaongeza ufanisi wa kazi za Mahakama ili haki za wananchi zitolewe kwa wakati. Suala hili limechelewa sana kutekelezwa, kwa hiyo, Mfuko uwepo na upewe kipaumbele.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsante.

MHE. SALOME D. MWAMBU: Mheshimiwa Spika, Serikali iangalie upya bajeti ya Mahakama kuanzia Mahakama Kuu hadi Mahakama za Mwanzo. Serikali isimamie mazingira yote ya kazi za Uhakimu yawe mazuri ili kulinda na kurudisha hadhi za Mahakakimu wetu pamoja na watumishi wa Mahakama. Vitendea kazi viboreshwe pamoja na majengo na usafiri.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja asilimia mia moja, ahsante.

MHE. MOZA A. SAIDY: Mheshimiwa Spika, nami naungana na wenzangu waliochangia Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama. Ni vema Serikali ikaliona hilo, kuziwezesha Mahakama zetu hapa nchini, hii itaondosha rushwa iliyojengeka katika taasisi hiyo ili haki itendeke.

Mheshimiwa Spika, kuboresha Mahakama zetu itatujengea heshima kwa Watanzania. Mahakimu, Majaji, Mawakili, wajengewe nyumba pamoja na watumishi wa Mahakama, kwani kukaa sehemu moja na raia ni moja ya vyanzo vya rushwa. Iwapo tukiiwezesha Mahakama, tutaipa hadhi kubwa kutenda haki na kuepusha lawama ya Mahakama na raia. Kuwe na Mfuko Maalum wa Mahakama ili waendeshe kesi zao vizuri.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsante.

30

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika, pongezi kwa Waziri na Watendaji wote wa Wizara kwa kuandaa na kuuleta Muswada huu Bungeni.

Mheshimiwa Spika, Mahakamani ni sehemu muhimu sana katika kutoa haki kwa wananchi. Wapo Watanzania wanaokaa rumande kwa muda mrefu kwa sababu tu hakuna fungu la kutosha kwa Mahakama kuendesha kesi za wahalifu kwa haraka. Kuna mifano hai wananchi wanakaa zaidi ya mwaka rumande, kesi zao hazisikilizwi, ni makosa makubwa sana na inawezekana kabisa kwamba wamehisiwa tu na wala hawajatiwa hatiani hadi hapo kesi zao zitakaposikilizwa. Kwa Muswada huu sasa Mahakama zetu zitatengewa fungu la kutosha kujiendesha na hivyo kuondoa kero kubwa zinazolalamikiwa.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni Mahakimu waliohitimu masomo yao kutoka vyuoni zaidi ya miaka miwili sasa wameomba kazi lakini hawaajaajiriwa na wakati huohuo hakuna Mahakama za kutosha. Wahitimu wengine wamebadili fani na kufanya mambo mengine baada ya kusota kwa muda mrefu bila kuajiriwa. Wengine wamefanyiwa interview na wamefaulu tangu mwaka jana Aprili, 2010 hadi leo wameambiwa wasubiri. Kwa kweli hili ni tatizo na linakatisha tamaa wasomi wetu. Kwa kuwepo Mfuko Maalum, naomba Serikali na Bunge tuhakikishe tunawezesha Mfuko huu ili Mahakama zetu zitoe huduma kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, lipo tatizo kubwa sana la kesi nyingi za ardhi kutosikilizwa kwa miaka mingi kwa sababu Mahakimu wa Ardhi hawapo na Kanda za Mahakama ya Ardhi ni chache sana. Mkoa wa Tabora, Mahakama Kuu ya Mkoa zipo kesi zimekaa pale miaka zaidi ya minne hata siku moja hazijawahi kusikilizwa, wananchi wengine wenye kesi hizo wamekufa bila kupatiwa haki zao. Namwomba Mheshimiwa Waziri asaidie kupatikana kwa Mahakimu wa Ardhi wa Kanda ili kusaidia wananchi wanaoteseka miaka mingi.

Mheshimiwa Spika, Mahakimu wetu kule vijijini wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. Pamoja na kukosa vitendea kazi vya ofisini pia wanaishi mitaani kwenye nyumba za uswahilini na hivyo kutofanya kazi zao kwa ufanisi mzuri. Hatuwezi kuondoa rushwa Mahakamani kama Mahakama zetu hazitaboreshwa na watumishi wake hususani Mahakimu kuwekewa mazingira mazuri na kulipwa vizuri pia.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Celina Kombani, Waziri wa Sheria na Katibu pamoja na watendaji wote walioshiriki kuandaa Muswada huu ambao utasaidia sana kuboresha shughuli za uendeshaji wa Mahakama. Hii inaonesha wazi kuwa Serikali iko makini kutambua upungufu unaokwamisha shughuli za Mahakama. Vilevile naipongeza sana Kamati kwa kazi nzuri iliyofanya kujadili Muswada huu ambao umelenga kupunguza usumbufu wa watuhumiwa kutembea Mahakamani kila siku.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kuwa matatizo yote yanayojitokeza katika uendeshaji wa Mahakamani ni kutokana na bajeti kuwa ndogo na kusababisha

31 Mahakimu kukosa magari, nyumba za kuishi, vifaa vya ofisini na kadhalika. Hivyo, katika kuboresha Muswada, tuanze na suala zima la bajeti ili kuboresha makazi ya Mahakimu, kupata magari, mishahara mizuri, posho mbalimbali, vifaa vya ofisini na kadhalika. Nina hakika hata rushwa zitapungua ama kumalizika kabisa.

Mheshimiwa Spika, Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo, Wilaya, Mkoa, ni wachache na Majaji pia. Hivyo kama kweli Serikali inataka kujenga misingi bora kwa kuendesha Mahakama zetu ni kupata Mahakimu wa kutosha. Hii itasaidia kuondoa tatizo la kulimbikiza kesi ama kuchelewesha kesi.

Mheshimiwa Spika, upungufu wa Mahakama za Mwanzo za Wilaya, ni vema Muswada huu uone umuhimu wa kuwasogezea wananchi huduma huko waliko kwa kujenga Mahakama za Mwanzo kila Kata ili kuwapunguzia wananchi gharama za kusafiri mbali kufuata Mahakama. Aidha, Wilaya ambazo hazina Mahakama za Wilaya zijengwe ili wasiendelee kukodi au kuchukua majengo ya Mahakama za Mwanzo.

Mheshimiwa Spika, rushwa kwa Mahakimu na Watumishi wa Mahakama. Pamoja na Watumishi na Mahakimu kupata mishahara midogo bado sio kigezo cha kuomba rushwa bali wamejenga mazoea ya kupokea rushwa. Hivyo, nashauri Muswada huu uweke utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi kukataa kutoa rushwa. Vilevile kuwa na Kitengo cha Mawakili wa Serikali wa kusaidia wananchi wasiojua sheria na ambao hawana uwezo kifedha waweze kupata haki zao.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Muswada huu utakuwa na Mfuko Maalumu, ni vema sasa Wazee wa Mahakama kuongezewa kiwango cha posho ili wasishaurike kuomba rushwa pia kuwapa moyo wa kazi na kutenda haki. Vilevile ili Mfuko huu uweze kutumika vizuri, ni vema mchanganuo wa matumizi uainishwe ili kuondoaka na matumizi mabaya.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nimalizie mchango wangu kwa kumpongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa busara zake nyingi akishirikiana na watendaji wa ofisi yake kwa kazi kubwa inayofanyika kuleta Bungeni Miswada mbalimbali kufanyiwa marekebisho ili Sheria zote ambazo zimeshapitwa na wakati zifanyiwe marekebisho na Bunge. Ninamwombea maisha marefu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake yote ili waendelee kuboresha Sheria mbalimbali za nchi hii kwa maslahi ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, sasa nitamke rasmi kuunga mkono Muswada huu mia kwa mia nikiwa na imani utaondoa mianya yote ya kuwanyima haki Watanzania wakiwemo wanawake.

MHE. PHILIPA G. MTURANO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nampongeza Mheshimiwa kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa kwa kuwa ni mwanamke.

Mheshimiwa Spika, uazishwaji wa mamlaka hii ya utawala wa Mahakama ni hatua mojawapo ya kimaendeleo ya kuboresha mhimili huu wa Mahakama. Kutokana na

32 malengo ya Sheria hii kama yatatekelezwa bila kuingiliwa na mhimili mwingine hususani Executive, basi pengine kilio cha Mahakama zetu kitapungua kama siyo kuisha kabisa.

Mheshimiwa Spika, Watanzania wengi wamekuwa wakipoteza haki zao kwa kisingizio kuwa Mahakama hazina fedha za kuendeshea kesi na hivyo kusababisha mrundikano mkubwa wa Mahabusu lakini pia na uwepo wa wafungwa wengi Magerezani waliokataa rufaa ambapo nyingi hazijasikilizwa. Hata majengo, vifaa vya Mahakama viko hoi. Kwa hiyo basi, tunaomba Sheria hii inayopitishwa leo itelekezwe vyema kwa kuufanya Mfuko wa Mahakama ufanye kazi iliyokusudiwa na siyo vinginevyo.

Mheshimiwa Spika, huyu mtawala wa Mahakama pamoja na kwamba anatakiwa awe mtaalamu wa hesabu lakini pia ni muhimu awe na taalum ya sheria, hii itamsaidia sana katika utendaji wake wa kazi. Naomba huyu mtawala wa Mahakama awe na uhuru katika wadhifa wake huo na uwajibike kwa mamlaka moja tu ambayo ni Rais.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. UMMY A. MWALIMU: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naunga mkono hoja. Pili, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria kwa kuleta Muswada huu ambao naamini kwa kiasi kikubwa utaweka mazingira mazuri na muafaka ya kisheria katika utekelezaji wa shughuli za Mahakama hapa nchini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu katika hoja hii umejikita zaidi katika maeneo mawili ambayo ni uwepo wa Maafisa wa Utawala wa Mahakama yaani Court Administrators na uwiano wa Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kusisitiza kuwa kada hii ya Maafisa Utawala wa Mahakama (Court Administrator) ni kada muhimu sana na ni integral party katika suala zima la uwepo wa Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wake wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote. Kada hii ndiyo inahusika moja kwa moja na masuala ya uandaaji wa bajeti, taarifa mbalimbali za Mahakama, manunuzi na masuala mengine ya kiutawala ambayo si rahisi kwa Jaji au Hakimu kuyaelewa au kuyafanyia kazi kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, wakati Wizara imefanya juhudi kubwa ya kuongeza idadi ya Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu, bado hatujaweza kuweka msukumo wa kutosha katika kuhakikisha kuwepo kwa Maafisa Tawala wa Mahakama wa kutosha katika ngazi mbalimbali za Mahakama. Hali hii imechangia kuwepo kwa huduma zisizoridhisha katika baadhi ya Mahakama zetu. Utakubaliana na mimi kuwa suala zima la utoaji haki kwa wananchi (access to justice) linahusisha Mahakama yaani Mahakimu na Majaji kwa upande mmoja na Utawala (Administrators) kwa upande mwingine ambao wote wana lengo la kutimiza kazi za Mahakama kama zilivyoelezewa katika Katiba.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu sana Wizara ikatengewa bajeti ya kutosha si tu kwa ajili ya kuajiri na kuwa-maintain Mahakimu na Majaji lakini pia iweze kuajiri

33 Maafisa Tawala wa Mahakama (Court Administrators) wa kutosha katika ngazo zote za Mahakama kuanzia Mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama Kuu. Naamini kuwa watu hawa wataweza kusimamia vizuri matumizi ya rasilimali za Mahakama hasa fedha na rasilimali watu, manunuzi na kuhakikisha uwepo wa mipango ya kuchochea na kuongeza uwezo (Capacity Building Programs) kwa Majaji, Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, changamoto mojawapo inayokwamisha utekelezaji mzuri wa Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (Legal Sector Reform Programme) hapa nchini ni suala la uwezo katika kupanga na kutekeleza mipango ya manunuzi (procurement), ukweli shughuli hii inabidi ifanywe na watendaji wenye sifa na uwezo katika masuala ya fedha na manunuzi na si wataalamu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, hivyo ni maoni yangu kuwa suala zima la utoaji haki na utendaji wa Mahakama hapa nchini linahusiana moja kwa moja na uwepo wa Maafisa Tawala wa Mahakama kama ilivyoiainishwa katika Kifungu cha 11 cha Muswada huu. Maafisa hawa wataweza kuisaidia Mahakama kupanga mikakati na mipango mizuri ya kuboresha mazingira ya utoaji haki, watasaidia kuandaa taarifa mbalimbali za utekelezaji na watakaosimamia vizuri rasilimali zinazotolewa na Serikali na wadau wa maendeleo katika kuboresha utendaji wa Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu suala la usawa wa jinsia kuzingatiwa katika uundwaji wa Tume ya Huduma ya Mahakama (Judicial Service Commission). Napenda kwa dhati kabisa kutambua na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuteua Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa wakiwemo Majaji wanawake. Mfano mwaka 2008, aliteua Majaji wanawake saba kati ya kumi na moja na mwaka 2009, aliteua Majaji sita wanawake kati ya Majaji kumi. Wakati ninaamini kuwa Mheshimiwa Rais ataendelea kuteua wanawake wengi zaidi wanaotimiza vigezo, nashauri itamkwe wazi katika Muswada huu kuwa kutakuwa na uwiano mzuri wa wajumbe wanawake.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naona kabla sijamwita mtoa hoja, napenda nitoe matangazo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii - Mheshimiwa Magreth Sitta, anaomba niwatangazeie Wajumbe wa Kamati yake kwamba leo Jumamosi kitafanyika kikao mara baada ya uchaguzi wa CPA ukumbi wa . Kwa hiyo, tukimaliza ule uchaguzi wa CPA pale Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii watakutana.

Nina tangazo lingine la Mheshimiwa Idd Azzan Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, yeye anaomba niwatangazie Waheshimiwa Wabunge kuwa leo tarehe 16 aPRILI, 2011 kutakuwa na mechi ya mpira wa miguu na mechi ya mpira ya pete (Netball) kati ya timu ya Waheshimiwa Wabunge na LAPF itakayofanyika katika uwanja wa Jamhuri

34 Dodoma. Mechi wa mpira wa pete (Netball) itaanza saa 9.30 alasiri ikifuatiwa na mpira wa miguu kuanzia saa 10.00 jioni. Aidha, Kamati ya ufundi ikiongozwa na Mheshimiwa Prof. Maji Marefu imeshafanya kazi yake usiku kucha, hivyo muwe na uhakika wa ushindi tu leo. (Makofi)

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wote mnaombwa kuhudhiria mechi hii muhimu ya kwanza kwa Bunge hili la Jamhauri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo, wote mnatakiwa mfike. Mnasema Spika wa sasa wa Bunge atakuwa Mgeni Rasmi na Spika wa zamani pia atakuwepo, kwa hiyo, msikose kuhudhuria huko. Msituaibishe maana ni kikao cha kwanza hiki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI - Mheshimiwa Lediana Mng’ong’o anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kuwa wanatakiwa kufika ofisi ndogo ya Bunge Dar es Salaam tarehe 18 Aprili, 2011 saa tatu asubuhi. Nadhani mtaanza kikao chenu huko Dar es Salaam, tarehe 18 saa 3.00 asubuhi pale ofisi ndogo ya Bunge.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira - Mheshimiwa , anaoamba niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba leo tarehe 16 Aprili, 2011, kutakuwa na kikao cha Kamati kitakachofanyika katika jengo la Utawala ukumbi Na.231 mara baada ya uchaguzi wa CPA.

Kama nilivyoeleza kwamba tukimaliza hapa Waheshimiwa Wabunge wote itabidi twende ukumbi wa Msekwa, kwa sababu Wajumbe wanachama wa CPA Tanzania Branch ni sisi Wabunge wote. Kwa hiyo, pale tutakwenda kuchagua viongozi wetu kama walivyojaza fomu, tutaambiwa kule, lakini Wabunge wote ni wanachama. Kwa hiyo, twende pale tukafanye kazi fupi tu ya kuwachagua viongozi wetu, halafu waendelee na shughuli nyingine.

Waheshimiwa Wabunge, tuna wageni wetu pale kwenye Speaker’s Gallery. Yuko Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria - Bwana Oliva Mhaiki, Jaji wa Mahakama Kuu Dodoma - Mheshimiwa Sivangilwa Mwangesi na Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma - Mheshimiwa Renatus Utatisibwa. Kama wanavyosema, ndiyo wadau wa Muswada huu wanafuatilia kazi yao. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya hapo, kama nilivyosema, wengi tumekuwa tunakubaliana kuhusu Muswada huu, sasa tukiendelea tunarudia tu yale yale. Kwa hiyo, afadhali twende kwenye hatua inayofuata.

Mheshimiwa mtoa hoja - Mwanasheria Mkuu wa Serikali, sogea pale Mheshimiwa.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, kwanza ninafarijika sana kwa ruhusa yako inayoniruhusu kuchangia na kufafanua baadhi ya mambo ambayo Waheshimiwa Wabunge wamechangia. Lakini pia ninamshukuru sana

35 Mheshimiwa Celina O. Kombani - Waziri wa Katiba na Sheria kwa hotuba yake alipokuwa anawasilisha Muswada huu.

Ninawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge akiwemo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, walioonesha hisia zao za kweli kuhusu hali ya Mahakama zetu. Mahakama ya Tanzania inayo matatizo na mapungufu kadhaa.

Mheshimiwa Spika, shabaha ya Muswada huu kama ilivyowasilishwa na Mheshimiwa Waziri ni kuweka Mfuko wa Mahakama kwa ajili ya kukabiliana na matatizo yote ambayo Waheshimiwa Wabunge wameyasema na kuyazungumzia kwa hisia kali. Muswada huu unaanzisha Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atashughulikia masuala ya utawala na fedha na kwa hiyo, kumwezesha kubuni na kusimamia miradi (projects) na kusimamia projects circle kwa ajili ya kupata ufanisi kwa sababu ya utaalam alionao. Kwa ajili hiyo, itawapa nafasi Maafisa wa Mahakama ambao kazi yao ni kushughulikia masuala Mahakamani wafanye kazi hiyo badala ya kujishughulisha na masuala ya utawala.

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna suala la nidhamu kama mtakavyoona kwenye vifungu mahsusi ambalo litatusaidia kurekebisha pale ambako kutatokea hitilafu.

Mheshimiwa Spika, kuna suala hili limejirudia humu kuhusiana na hati ya dharura kuhusiana na Muswada huu. Ninakubaliana na wale waliochangia kwamba siyo desturi nzuri kuleta Miswada kwa hati ya dharura, lakini kwa mujibu wa kanuni zetu ziko tahadhari za kutosha kuzuia Miswada ambayo haina uharaka wowote. Kwa ajili hiyo, Kanuni ya 80(5) na (6) hati ya dharura huwasilishwa kwenye Kamati ya Uongozi ambacho ni chombo muhimu cha Bunge hili na Mwenyekiti wake ni Spika. Mpaka pale ambapo Kamati hiyo itakapomshauri Mheshimiwa Spika kwamba Muswada huu ni wa dharura ndiyo Muswada huletwa hapa Bungeni. Kwa hiyo kuna safe guards za kutosha na nadhani siyo jambo ambalo linatokea mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala moja la asilimia mbili ya pato la Taifa. Ni kweli kwamba ingekuwa vyema kuwa hivyo, lakini katika utaratibu wetu wa mambo ya sera na mambo ya kupanga bajeti itakuwa vigumu kufanya hivyo katika Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, Bunge lako limesema vizuri, lakini kwa maoni yangu ambayo yanaungwa mkono na Ibara ya 99 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, tunahitaji tafakuri ya kina ambayo itahusisha pia Mfuko wa Bunge. Hatuna takwimu ambazo zilituwezesha kufanya uamuzi huu wa kuweka asilimia mbili ya pato la Taifa kwenye bajeti ya Mahakama. Aidha, hoja hii haitokani na Muswada tuliowasilisha au pendekezo la Mheshimiwa Rais, au kauli ya Waziri aliyewasilisha Muswada huu. Kwa hiyo, kwa maoni yangu, masharti ya Ibara ya 99 ya Katiba yanatufanya sisi tusiweke kiwango hicho.

Mheshimiwa Spika, maana ya masharti haya ya Ibara ya 99 ya Katiba ni kwamba ingawa tunayo mamlaka ya kuidhinisha mfuko, tulivyo sasa na bila kuwa na takwimu hizo wala pendekezo la Mheshimiwa Rais, itakuwa ni vigumu sana sisi kujigeuza kuwa

36 Kamati ya kugawa pato la Taifa kwa asilimia yoyote. Lakini rai yangu ni kwamba mfuko huu na ule wa Bunge kwa wakati muafaka tunaweza tukiwa na takwimu zinazohusika kufanya hayo mabadiliko.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu mambo mengi yako kwenye vifungu vya Sheria, naomba niache muda huu kwa ajili ya Mheshimiwa Waziri ili akamilishe hotuba yake kwa kirefu. Nakushukuru sana.

SPIKA: Mheshimiwa mtoa hoja.

WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA: Mheshimiwa Spika, kwa ridhaa yako, naomba nikushukuru wewe binafsi kwa kusimamia mjadala wa Muswada huu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama wa Mwaka 2011 kwa umakini na umahiri mkubwa. Pia nitumie fursa hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa umakini wenu mliouonesha wakati wote wa mjadala huu. Hii inadhihirisha kwamba Bunge lako Tukufu linaheshimu na kuutakia mema mhimili mwingine wa dola ambao ni Mahakama.

Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa, ninawashukuru Waheshimiwa wote waliochangia Muswada huu ama kwa maandishi, ama kwa kuzungumza hapa Bungeni. Niseme tu kuwa michango yao tumeipokea na ina thamani kubwa kwa mustakabali wa utoaji wa haki katika nchi yetu. Sanjari na hilo, maoni yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo yamezingatiwa na tumetayarisha jedwali la Marekebisho ambalo limesambazwa hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea, napenda kuwatambua Waheshimiwa Wabunge waliochangia kwa njia moja au nyingine katika Muswada huu. Nikianza na wale waliochangia kwa kuzungumza ni hawa wafuatao:-

Mheshimiwa , Mheshimiwa , Mheshimiwa , Mheshimiwa Rashid Abdallah, Mheshimiwa Kombo Hamis Kombo, Mheshimiwa Juma Njwayo, Mheshimiwa Chiku Abwao, Mheshimiwa Jerome Bwanausi, Mheshimiwa Henry Shekifu, Mheshimiwa , Mheshimiwa Kange Lugola, Mheshimiwa John Magalle Shibuda, Mheshimiwa Mohammed Missanga, Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mheshimiwa Sylvester Mabumba, Mheshimiwa Stephen Ngonyani, Mheshimiwa Dr. , Mheshimiwa Joseph Selasini na Mheshimiwa Moza Abeid Saidy. Hao ndiyo waliochangia kwa kuongea.

Mheshimiwa Spika, waliochangia kwa Maandishi ni pamoja na Mheshimiwa Pauline Gekul, Mheshimiwa Amina Andrew Clement, Mheshimiwa , Mheshimiwa Magreth Sitta, Mheshimiwa Regia Mtema, Mheshimiwa Salome Mwambu, Mheshimiwa Philipa Mturano, Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Mheshimiwa Vicent Nyerere, Mheshimiwa Christina Mughwai, Mheshimiwa Fatma Mikidadi, Mheshimiwa Zahra Mohamed, Mheshimiwa Esther Matiko, Mheshimiwa Moza Abeid Saidy, Mheshimiwa Prof. Kalikoyela Kahigi, Mheshimiwa Ummy Ali Mwalimu, Mheshimiwa Ritta Kabati, Mheshimiwa Diana Chilolo, Mheshimiwa , Mheshimiwa Sabreena Hamza Sungura, Mheshimiwa Christowaja Mtinda, Mheshimiwa Haroub

37 Muhammed Shamis, Mheshimiwa Rebecca Mngodo, Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya, Mheshimiwa David Mallole, Mheshimiwa Albert Obama Ntabaliba, Mheshimiwa Makani, Mheshimiwa , Mheshimiwa Blandes, Mheshimiwa Saleh A. Pamba, Mheshimiwa Joyce Mukya na Mheshimiwa Suleiman Jafo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwatambua Waheshimiwa Wabunge waliochangia Muswada huu, sasa naomba nijibu hoja za Waheshimiwa Wabunge zilizojitokeza wakati wa michango yao kwa ujumla tu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wabunge wengi sana wamechangia kuhusu matatizo ya Mahakama kama vile matatizo ya upungufu wa bajeti, matatizo ya vitendea kazi, matatizo ya ucheleweshaji wa kazi na matatizo ya majengo. Wabunge wengi sana wamechangia karibuni kila mmoja alionesha concern yake kuhusu mapungufu yaliyopo Mahakamani na matatizo ya Mahakama. Niseme tu kwamba mimi nimefarijika kwa sababu, jamani kuiongoza Wizara ambayo Bajeti yake ni finyu napo ni mzigo. Kwa hiyo, nasema nawashukuru, ndiyo maana tumeleta Muswada huu.

Mheshimiwa mmoja alitoa historia kwamba Muswada huu ni wa zamani sana, yaani nia ya kuanzishwa huo Mfuko ilikuwa ni nia ya muda mrefu, amesema mwaka 1995. Ni kweli Muswada huu umechukua muda mrefu na tumeuleta kwa makusudi ili tuweze kutatua matatizo haya. Kwa hiyo, niseme kwamba nawashukuru sana kama mmeliona hilo, nami nasema mmenifariji na Serikali imekuwa sikivu ndiyo maana imeleta Muswada huu kwa Hati ya Dharura.

Mhessimiwa Spika, Mheshimiwa Freeman Mbowe ametoa takwimu nzuri za kuhusu uendeshaji kesi na upungufu wake. Mimi nakubali kwamba takwimu zake amezitoa, lakini takwimu hizo mwaka haujakwisha bado, tuna miezi mitatu, nina uhakika katika miezi mitatu hii flow ya fedha iko vizuri na kesi nyingi zitasikilizwa. Kwa hiyo, nasema kwamba takwimu hizo ni sawa mpaka Machi, 2011. Lakini baada ya miezi mitatu najua kabisa kwamba takwimu hizo zitaongezeka na kesi nyingi zitasikilizwa.

Mheshimiwa Spika, pia kumejitokeza suala la kuanzishwa kwa Judiciary Services. Katika Muswada wa Sheria ya uendeshaji wa Mahakama ya mwaka 2011, inapendekezwa kuanzisha utumishi wa Mahakama kwa masharti ya Ibara ya (4). Utumishi huu utawahusu Watumishi wote, yaani Majaji, Mahakimu, Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo, Makarani, Madereva, Wahudumu, kwa ujumla watumishi wote wa Mahakama (Judicial Officers and Non Judicial Officers). Sasa ili kusimamia vema Utumishi wa Mahakama kwa masharti ya Ibara ya 112, Katiba imeunda Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Katika ibara 113 ya Katiba, imeainisha kazi za Tume hiyo. Muswada katika ibara yake ya 13 inatambua kuwepo kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama na inaainisha jinsi Tume hiyo itakavyofanya kazi. Katika ibara ya 14 ya Muswada huu inapendekeza kuipatia Tume kazi za ziada licha ya kazi zilizoainishwa kwenye Katiba. Kazi na mamlaka ya ziada inayopewa Tume kuhusu Watumishi wasiofanya kazi za kuamua kesi,

38 yaani non judiciary function haziathiri wala kukinzana na kazi za Tume zilizoainishwa katika ibara ya 113 ya Katiba.

Kwa mantiki hiyo, hakuna ukiukwaji wa masharti ya Katiba kulikopendekezwa katika Muswada wa Sheria hii ya Uendeshaji wa Mahakama wa mwaka 2011. Kwa sababu katika ibara ya 113(5) inaeleza katika Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba: “Bunge linaweza kutunga sheria itakayoweka masharti ya utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo.” Kwa hiyo, hilo la Judiciary Services hatukuona kwamba limekinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo limechangiwa na Waheshimiwa Wabunge ni mambo ya msingi kwa ajili ya uhuru wa uendeshaji wa Mahakama yanayopaswa kuzingatiwa ipasatavyo ili kuimarisha zaidi misingi ya utawala wa sheria. Hilo limetolewa na Kamati na sisi tumesema kwamba tunapokea ushauri huu na tunaahidi kwamba tutaufanyia kazi.

Pia Kamati ilitoa rai kwamba utungaji wa kanuni chini ya sheria inayotarajiwa kutungwa izingatie namna bora ya usimamizi wa Mfuko wa Mahakama bila kuathiri utekelezaji wa dhana ya uhuru wa Mahakama. Hilo pia limechangiwa na Waheshimiwa Wabunge wengi. Mimi niahidi kwamba ushauri huu ni mzuri, utazingatiwa na Wizara yangu pindi kanuni hizo zitakapokuwa zimeandaliwa.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo limejitokeza ni kwamba kwa kuwa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu zimeanzishwa kwa mujibu wa Katiba, hivyo Tumishi wa Mahakama haiwezi kuanzishwa kwa msaada. Nimelitolea maelezo kwa kifupi kama ilivyokuwa hapo awali.

Suala linguine suala la Muswada kutoonyesha uhusiano kati ya Tume ya Utumishi wa Mahakama na Tumishi, yaani Utumishi wa Mahakama. Hilo ni kama nilivyolitolea maelezo katika maelezo yangu ya awali.

Suala lingine ambalo limechangiwa na Wabunge wengi ni Mtendaji wa Mahakama pamoja na taaluma nyingine awe na taaluma ya sheria kwa mujibu wa sheria itakayotungwa. Mtendaji Mkuu atakuwa mtumishi wa Mahakama na hataruhusiwa kupata maelekezo yoyote nje ya Utumishi wa Mahakama. Tumeanzisha nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama. Mtendaji Mkuu wa Mahakama tumesema kwamba basic qualification yake, awe mtaalamu wa Utawala pamoja na Utaalamu wa Fedha. Kama tulivyosema kwenye ibara ya 52 na 53, majukumu yake ni kama Afisa Masuuli. Kwa hiyo, Afisa Masuuli lazima ayajue mambo ya fedha na utawala. Kwa hiyo, sisi tunaona ni sawa kabisa, qualification hizi zinatosha kabisa kwa Afisa Masuuli au Msimamizi Mkuu wa Mfuko wa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kutokana na ukosefu wa fedha. Mahakama imeshindwa kuanzisha Kanda katika kila Mkoa na pia vipaumbele vya Mahakama vimekuwa havizingatiwi. Ni kweli kama nilivyosema mwanzo kwamba kulikuwa na ufinyu wa bajeti, ndiyo maana tumeleta hiyo hati ya dharura ili Waheshimiwa Wabunge

39 mridhie Mfuko wa Mahakama. Wakiwa na Mfuko wa Mahakama wataweza kupanga mambo yao, watapanga vipaumbele vyao kulingana na matatizo yao. Kwa hiyo, ni kweli nia ni njema tunataka tuwe na Mahakama Kuu kwa kila Kanda na kila Mkoa, lakini sasa hivi hatujafanya hivyo. Mkiridhia mfuko huu tuna uhakika kwamba mambo hayo yatafanyika vizuri.

Mheshimiwa Spika, rai nyingine ambayo imetolewa ni kwamba fedha ipelekwe moja kwa moja kwenye Mfuko wa Mahakama bila kupitia Mfuko wa Hazina. Ushauri huu tumeupokea, ni ushauri mzuri na umezingatiwa katika Muswada wetu katika kifungu cha 53. Pamoja na ukweli huo Serikali pia ina utaratibu wake wa kupokea fedha za misaada ambapo pamoja na ukweli kwamba Taasisi inayopewa fedha za msaada ndiyo itatumia fedha hizo, lakini Mfuko wa Hazina lazima ufahamu nchi iliyotoa fedha hizo, kiwango cha fedha na malengo ya msaada huo kwa Taasisi husika.

Mheshimiwa Spika, rai nyingine ambayo ilitolewa na Waheshimiwa Wabunge ni kwamba Mahakama isiwekewe ukomo wa bajeti. Ni bora Muswada huu uweke kanuni za wazi kwamba bajeti ya Mahakama iandaliwe kutokana na mahitaji halisi ya Mahakama. Suala hili tumelipokea na katika kupanga bajeti ya nchi, kuna vigezo ambavyo hutumika ikiwemo uwezo wa kifedha kwa Serikali, hivyo bajeti ya Mahakama kama zilivyo bajeti za vyombo vingine vya umma ikiwemo Bunge hupangwa kulingana na mahitaji ya vyombo hivyo na kwa kuzingatia uwezo wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo limechangiwa na Waheshimiwa Wabunge lilihusu Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wasio Wenyeviti wa Kamati za Maadili, za Mahakama za Mikoa na Wilaya kwa kuwa wanahatarisha uhuru wa Mahakama. Katika Muswada huu majukumu ya Kamati hizi sio ya kutoa uamuzi au adhabu dhidi ya Hakimu, isipokuwa Kamati hizi hufanya uchunguzi baada ya kupokea malalamiko ya wananchi na kutoa ripoti kwa Jaji Mfawidhi wa Kanda husika ambaye naye hupeleka taarifa hizo kwenye Tume. Viongozi hawa wamewekwa kwa nia njema ya kuhakikisha kuwa haki inaonekana kuwa imetendeka kwa sababu watuhumiwa ni Mahakimu na siyo vyema Mahakimu hao hao kuchunguza kesi zao zinazowahusu. Kwa hiyo, ndiyo sababu kubwa ya kuweka mhimili mwingine katika hizo Kamati za Maadili za Mikoa na za Wilaya.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ni kwamba, siyo sahihi kwa Rais kutomteua Mtendaji Mkuu wa Mahakama na vile vile kuwa ni Mamlaka ya Nidhamu ya Mtendaji huyo. Kwa taratibu za kisheria, mwenye mamlaka wa kuteua ndiye mwenye mamlaka ya nidhamu dhidi ya mteule wake. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri ya Sheria Sura ya nne kuhusu kwa nini Mtendaji huyu ateuliwe na Rais. Ni wazi kuwa kwa mujibu wa Katiba yetu, Viongozi Wakuu wa Mahakama wote huteuliwa na Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, rai nyingine iliyotolewa ni kuweka kanuni zitakazomwezesha Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kukagua mahesabu ya fedha kwenye Mfuko wa Mahakama ili kuondoa uwoga wa Mkaguzi wa Hesabu kukagua hesabu hizo. Mpaka sasa kwa mujibu wa sheria zetu, mahesabu ya Mahakama yanakaguliwa na Mkaguzi

40 Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, hivyo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na wataalamu wake hawana uwoga wowote kutekeleza majukumu hayo na Mahakama inawapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kwamba wanakagua hesabu hizo kama ilivyo kwa Taasisi nyingine.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kuwepo kwa hoja ya kuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Waheshimiwa Wabunge walitoa rai kwamba ni vyema kuwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Mahakama. Lakini suala hili limewekewa utaratibu ambao unampa mamlaka Jaji Mkuu kumteua Ofisa Mwandamizi kufanya shughuli za Mtendaji Mkuu wa Mahakama ikiwa atakuwa hayupo katika kituo cha kazi. Kwa hiyo, tumesema kwamba tunaona hakuna sababu za msingi za kuwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Mahakama. Hapo tutakapoona kwamba kuna ulazima huo tunaweza tukaleta marekebisho katika Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama awekewe muda wa ukomo wa Utumishi. Katika rai hii tunasema kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali hawawekewi ukomo wa Utumishi wao.

Suala lingine ambalo Wabunge walilitoa ni Mawakili wawekewe Kamati za Kusimamia nidhamu zao. Jibu lake ni kwamba kwa mujibu wa Sheria za Mawakili Sura ya 341 nidhamu za Mawakili huangaliwa na Kamati za Mawakili. Hata hivyo, kuna Muswada ambao nitauwasilisha Bungeni kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mawakili, kwa hiyo, michango yenu mtaitoa kwa wakati huo. Kama kuna umuhimu huo tutaufanyia marekebisho.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo limechangiwa na Waheshimiwa Wabunge ni kwamba wananchi hawana elimu kuhusu Kamati za Maadili na aina gani ya malalamiko yanayoweza kuwasilishwa kwenye Kamati hizo. Ni ukweli kwamba wananchi wetu hawana elimu kuhusu Kamati za Maadili na aina ya malalamiko yanayoshughulikiwa na Kamati hizo. Lakini kwa kulitambua hilo, Tume kwa mwaka uliopita, yaani 2010 ilifanya ziara katika Mikoa kadhaa kwa minajili ya kujitambulisha na kuzitambulisha Kamati za Maadili za Mikoa na Wilaya mwezi Mei na pia mwezi Mei mwaka huu Tume itatembelea katika Mikoa mbalimbali ikiwapo Pwani pamoja na Tanga. Kwa hiyo, suala hili ni kweli tunalifahamu na linafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo Waheshimiwa Wabunge wamechangia ni ngazi za Wilaya na Mikoa zihusishwe katika kupanga bajeti. Suala hili ni jema, lakini limezingatiwa katika Muswada wetu katika kifungu cha 58. Ndiyo maana pale unaona kwamba kuna Baraza la Wafanyakazi litahusishwa katika kushauri na kupitisha bajeti na tunavyojua Mabaraza ya Wafanyakazi huwa ni Wawakilishi wa Watumishi wengi. Kwa hiyo, wanashirikishwa katika upangaji wa bajeti.

Mheshimiwa Spika, suala lingine ambalo limechangiwa na Waheshimiwa Wabunge ni wahitimu wa sheria waliosailiwa na Mahakama tangu mwezi Aprili, 2010 mpaka sasa bado hawajaajiriwa. Suala hili tunalifanyia kazi na tutalifuatilia kwa karibu

41 ili tuone tatizo liko wapi. Suala lingine ambalo limechangiwa ni Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi kuwa na mlundikano wa kesi. Ni kweli tatizo hili Serikali tumeliona na baada ya kuliona sheria imebadilishwa na sasa kila Mahakama Kuu ina uwezo wa kusikiliza mashauri ya ardhi. Kwa hiyo, ule mlundikano wa mashauri wa ardhi utapungua katika Divisheni ya Mahakama Kuu ya Ardhi.

Mheshimiwa Spika, mengi yaliyotolewa ni ushauri, niseme nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa kuona tatizo la Mahakama na sisi kama Serikali tunatambua matatizo ya Mahakama, ndiyo maana kama nilivyosema mwanzo, tumeleta Muswada huu ili Waheshimiwa Wabunge muupitishe na mkiupitisha tutarudi kujipanga ili tuone vipaumbele vyetu katika Mahakama zetu na tupange utaratibu wa kuyatekeleza hayo, kuyatatua ili Mahakama zetu ziweze kutenda haki.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru wewe, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Muswada wa Sheria ya Serikali Ulisomwa Mara ya Pili)

KAMATI YA BUNGE ZIMA

Muswada wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama wa Mwaka 2011 (The Judiciary Administration Bill, 2011)

Ibara ya 1

Ibara ya 2

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila ya mabadiliko yoyote)

Ibara ya 3

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu, nadhani umepokea marekebisho ya Serikali. Kama ni hivyo, nakuruhusu uendelee.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kupendekeza mabadiliko ya ibara ya (3) ya tafsiri kwa kuweka tafsiri mpya ifuatayo in the appropriate alphabetical order.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri ninayoipendekeza, inasomeka kama ifuatavyo: “Judiciary Service, means the Judiciary Service of the United Republic and includes Judiciary and non Judiciary Officers of the Court of Appeal, The High Court and the

42 Courts Subordinates thereto and the Judiciary Service Commission established by the Constitution”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la mapendekezo haya ni kuweka tafsiri ya neno “Judiciary Service” ambalo halipo katika Muswada. Kama nilivyosema jana, kukosekana kwa hili neno “Judiciary Service” kwa tafsiri yake kunafanya ionekane kama tunatengeneza taasisi mpya wakati ukweli ni kwamba hatutengenezi taasisi mpya. Kwa hiyo, kwa kuweka hii tafsiri mpya ya “Judiciary Service” inaondoa huo utata ambao upo katika Muswada na inaongeza clarity zaidi katika hili neno Tumishi ya Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri ya haya ambayo Mheshimiwa Mbunge anayaleta utayakuta kwenye tafsiri ya neno “Service” kwenye ukurasa wa sita wa Muswada. Service ilivyotafsiriwa kwenye Muswada ina maana ni service ambayo Mheshimiwa Mbunge anaitaja ina-include Judiciary na Non Judiciary Officer of the Court of Appeal, The High Court and Courts Subordinates thereto and that of the Commission. Kwa hiyo, tafsiri iliyoko kwenye Muswada inatosheleza na hii ambayo ana propose inajirudia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nashauri kwamba neno hilo “Service” lilivyotafsiriwa libaki kama lilivyo na “Judiciary Service” linalopendekezwa na Mheshimiwa Mbunge lisikubalike. (Makofi)

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikiliza kwa makini sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali na naomba Kamati yako Tukufu ikatae hoja ya Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Muswada neno “service” ni kweli limetafsiriwa, lakini linasomekaje? “Service means, the judicially service established under this Act.” Halafu neno “Judicially” limetafsiriwa kumaanisha the Court of Appeal, the High Court and the Courts Subordinate thereto. Sasa kuwepo kwa tafsiri mbili judicially na service kunaashiria kama kuna vitu viwili na kuna taasisi mbili mpya wakati kama nilivyosema, hatutengenezi taasisi mpya hapa.

Hii service ambayo ina include Judicial Service Commission na Mahakama zetu zote ni kitu kimoja. Sasa uzuri wa tafsiri yangu mpya ninayoipendekeza ni kwamba ina- cover vyote vile ambavyo katika Muswada vinaonekana kama vitu tofauti. Sasa lazima niseme kwamba tafsiri iliyoko katika Muswada kwa kweli ina matatizo mengi na tuki- adopt hii tafsiri mpya itaondoa huu utata ambao nimeusema. Tafsiri kwa mfano ya service, haijumuishi Judicial Service Commission. Judicial Service Commission ina Makamishna, ina wafanyakazi, lakini hawako included katika hii tafsiri ya service. Kwa hiyo, naomba mapendekezo yangu ya kutoa tafsiri mpya ya Judicially Service yakubaliwe na Kamati yako Tukufu.

43 MWANASHERIA MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, niwie radhi kwa kutumia maneno haya, lakini huu ni upotoshaji uliokithiri kwa sababu sheria hii kwa mujibu wa kifungu cha 29 kinazungumzia Judicially Service Commission. Kwa hiyo, siyo kweli anavyosema Mheshimiwa Tundu Lissu na nakuomba usiwe unapotosha mambo ambayo yako wazi. Bado msimamo wangu ni ule ule wa mwanzo na kwa sababu hajasema kitu kipya.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kama kuna amendments zimeletwa na Mbunge, amendments za Mbunge tunazisikiliza kwanza, tukishasikiliza tunasikiliza upande wa Serikali, tena tunamrudishia mwenye hoja, maana yule Mbunge anakuwa ndiye aliyetoa hoja. Baada ya hapo, sisi tunaamua, maana sasa tuko kwenye hoja ya Mheshimiwa Tundu Lissu. Sasa nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Haja iliamuliwa na Kukataliwa)

MWENYEKITI: Kwa hiyo, hoja imeondoka, tunaendelea na tafsiri na Serikali.

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 4 Ibara ya 5

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 6

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 7

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza mabadiliko katika Ibara ya (7) ya Muswada mapendekezo manne. Pendekezo la kwanza ni kuingiza Ibara ndogo mpya ya (3) ambayo itasomekana kama ifuatavyo: “The Chief Court Administrator shall not take office until his appointment has been confirmed by resolution of the National Assembly.” Pendekezo la pili ni kuzi-number hizo Ibara ndogo zinazofuata ya (4), (5) na ya (6) kama Ibara ndogo ya (4), (5), (6) na (7). Pendekezo la tatu ni linasomeka kama ifuatavyo: “By inserting the word law between the words in and public appearing in a new sub clause (4).”

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ibara ya 7(3), inayoweka qualifications za Chief Courts Administrator, hakuna qualification ya Chief Court Administrator kuwa na

44 ufahamu wa masuala ya sheria. Kama nilivyosema katika hoja yangu niliyoitoa jana na vilevile imechangiwa na Waheshimiwa Wabunge wengi sana, Mahakama ina mahitaji maalum ambayo yako tofauti na Idara nyingine za Serikali hata na Bunge hili. Kwa hiyo, Mtawala Mkuu wa Mahakama lazima awe mtu anayefahamu mahitaji maalum ya Mahakama na mtu anayefahamu mahitaji muhimu ya Mahakama ni nani kama mtu asiyefahamu sheria? Kwa hiyo, pendekezo ni kuweka Sheria kama moja ya hizo qualification, kwa hiyo, new sub clause (4).

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo la nne linahusu kufanya mabadiliko katika Ibara mpya ndogo ya (7) ambayo ni Ibada ya zamani ya (6): “The Chief Court Administrator shall hold office on such terms and conditions as the President shall determine.” Inapendekezwa kuondoa maneno the President katika hiyo Ibara na kuwe neno “the Commission” ili isomeke: “the Chief Court Administrator shall hold office on such terms and conditions as the Commission shall determine.”

Pendekezo hili linalenga kuongeza uhuru wa Mahakama na uhuru wa Mahakama unakuwa mkubwa pale ambapo watumishi wa Idara ya Mahakama wanaweza wakafanya shughuli zao kufuatana na terms and conditions, masharti yanayowekwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Tume ya Utumishi wa Mahakama ina utaalam mkubwa zaidi juu ya terms and conditions za watumishi wake kuliko mtu mwingine yeyote nje ya judicially. Kwa hiyo, inapendekezwa kwamba badala ya Rais kuamua masharti ya kazi ya Chief Court Administrator, kazi hiyo ifanywe na Tume.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie pendekezo la kwamba Chief Court Administrator awe confirmed na Bunge hili Tukufu. Nchi hii inafuata mfumo wa Separation of powers na checks and balances na moja ya namna ya ku-introduce checks and balances katika Mfumo wetu, ni kuhakikisha kwamba hizi appointments muhimu na kubwa katika utawala wa dola zinakuwa confirmed na vyombo vingine. Kwa hiyo, pendekezo la ku-confirm appointment ya Chief Court Administrator na Bunge hili itaongeza hiyo separation of powers itaongeza checks and balances katika mfumo wetu wa utawala itaboresha zaidi mfumo wetu wa utawala. Ahsante sana, naomba mabadiliko ninayopendekeza yakubaliwe. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine inasikitisha sana wanasheria wetu wanapotupotosha. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado inafanya kazi na kama bado inafanya kazi Watendaji Wakuu wote wanateuliwa na Rais. Kwa hiyo, hiyo lazima tuiheshimu. Chief Justice anakuwa confirmed na Bunge mpaka sasa hivi?

WABUNGE FULANI: Hapana.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Anateuliwa na Rais periodically. What is so special kwa huyu Court Administrator aje hapa Bungeni? Mimi naomba kwanza tuheshimu Katiba yetu iliyopo. Suala lingine la kisera ni suala la qualification za Chief Court Administrator. Mimi kwa bahati nzuri by profession ni Administrator. Qualification za Chief Court Administrator ni lazima awe na qualification za utawala

45 pamoja na mambo ya fedha na siyo vinginevyo. Huwezi ukamweka Mwanasheria mwenye Digrii umwambie sasa awe Chief Court Administrator. Jamani tunapotosha katika Scheme of Service za nchi hii! Hili halipo! Naomba kwa kuwa Kanuni hizi na Sheria hizi bado zipo, tuziheshimu na tuendelee nazo. Kwa hiyo, hayo mapendekezo mawili naomba yasikubaliwe.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, wakati tunakuwa kwenye Kamati ya Bunge Zima, naomba msije kuzungumza na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu hapa tunafanya maamuzi. Sasa nyie mnapomzunguka Waziri Mkuu na kumweleza mambo yenu, hasikilizi tunayofanya hapa. Waheshimiwa Wabunge, wakati tunakaa kama Kamati, naomba msisogee kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, maana tunafanya maamuzi. (Makofi)

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba sina lengo la kupotosha, wala siyo bahati mbaya, ni kutokana na ujuzi tu. (Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lissu, usisikilize maneno ya watu, endelea.

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo la kutaka Chief Court Administrator awe confirmed na Bunge hili Tukufu inatokana na uzito wa kazi ambayo inapendekezwa kumpa huyu Chief Court Administrator. Hiyo moja.

Pili, ni kweli kabisa kwamba nyadhifa muhimu kama wadhifa wa Jaji Mkuu bado anateuliwa na Rais na mchezo unaishia hapo. Lakini moja ya mambo makubwa ambayo tumekuwa tunayapigia kelele katika Mfumo wetu wa Kikatiba ni pamoja na Urais wa kifalme (Imperial Presidency) haya Mamlaka ya kufanya Rais anateua kila kitu bila checks and balances.

Sasa tunaelekea kwenye Mjadala wa Katiba mpya, ni muhimu tuanze kuangalia hizi appointments kubwa kubwa, ni muhimu kuangalia hizi nafasi muhimu ziwe confirmed na Bunge. (Makofi)

MWANASHERIA MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Mheshimiwa Mbunge anasema hili ni jambo ni la Katiba na litahusu mchakato wa Katiba unaokuja, hana haja ya kulileta kwenye Kamati yako.

MWENYEKITI: Hata mimi nasema hivi, kwa sasa tunatumia Katiba iliyopo. Sasa katika mchakato, hayo ndiyo maneno. Lakini tusiyaingize sasa. Hata wewe mwenyewe unajua kwamba siyo sahihi. Kwa sasa hivi na Sheria hii tufate utaratibu uliopo hapa.

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza sijaingiza Katiba humu ndani, ninachozungumza ni kwamba huu Muswada unapendekeza Chief Court Administrator atateuliwaje, nami napendekeza utaratibu wa namna ya kumteua kwamba badala ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais peke yake, awe confirmed na hili Bunge. Sijasema tubadili Katiba hapa. (Makofi)

46

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nafikiri Mheshimiwa Waziri hajaielewa hata hoja yangu juu ya requirement ya mtu anayefahamu sheria. Haina maana kwamba huo ujuzi mwingine wa administration, wa finance sio muhimu, hiyo sio hoja yangu. Ninachosema ni kwamba pamoja na hizo requirements za kuwa mjuzi wa administration kuwa mjuzi wa finance, vilevile huyu mtu kwa kuzingatia umuhimu wa mahitaji ya Mahakama ajue Sheria.

Kuna watu wanasheria wana MBA, kuna wanasheria wamesoma engineering, mimi ninawafahamu, kuna wanasheria wamesoma Public Administration. Sasa pamoja na hizo qualifications za Public Administration na Finance tutafute watu ambao their proper qualified to head this position ya Chief Court Administrator. Usituletee mtu ambaye haelewi mahitaji ya Mahakama. Jaji akisema majoho yangu yametoboka, hailewi umuhimu wa Jaji kuvaa joho. Kwa hiyo, tunahitaji mtu anayefahamu mahitaji ya Mahakama na mtu anayefahamu mahitaji ya Mahakama awe anafahamu Sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumalizia kwenye hiyo hoja yangu kwamba kwenye hiyo ya tatu ambayo ni renumbering, kwa hiyo, naomba haya marekebisho ninayoyapendekeza yakubaliwe. (Makofi)

MWANASHERIA MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Chief Court Administrator hatahusika na majoho ya Majaji. Hili pendekezo la Chief Court Administrator kuwa confirmed na Bunge siyo utaratibu na tunaomba lisikubalike. Pili, hili suala la Chief Court Administrator kuwa na elimu ya sheria ni suala zuri, lakini hatuwezi kuweka kwenye sheria kwa sababu hii itakuwa ni added advantage tu ambako katika matangazo ya kazi, na wewe nakuomba uombe tutaku-access. Lakini nasema tusifanye hili jambo kwa mzaha.

Moja ya matatizo yanayofanyika ni kwa sababu watawala wa Mahakama ni wanasheria ambao hawakwenda kujifunza masuala ya utawala na matatizo mengi yanatokana na kusimamia zile projects za Mahakama. Kwa sababu kama mnavyofahamu wale ambao mmebobea kwenye masuala ya projects cycle kusimamia mradi, lazima uwe umeu-plan, umeufanyia tathmini na unau-monitor mara kwa mara. Sasa hawa muda wao mwingi wanatumia uendeshaji wa kesi. Nafikiri kuna loop hole. Mimi nafikiri hili jambo la kusema awe mwanasheria lisikubalike. Isipokuwa kama atakuwa na degree ya sheria na MBA, siyo kila mtu mwenye MBA is a material to be a Court Administrator.

La tatu, katika Ibara zilizotangulia tumeona role ya President sasa huwezi kumwondoa hapa kwa njia hiyo. Kwa hiyo, nashauri pia pendekezo hilo lisikubalike.

MWENYEKITI: Sasa tunafanya uamuzi.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Haja iliamuliwa na Kukataliwa)

47 MWENYEKITI: Kwa hiyo, mapendekezo hayo pia yamekataliwa.

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 8

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ibara ya 9 ya Muswada, mamlaka ya kinidhamu ya Mtawala Mkuu wa Mahakama ni Rais. Maana yake ni kwamba Rais anaingilia masuala ya Mahakama (Judiciary). Maana yake ni kwamba hiyo inakwenda kinyume na separation of powers, inakwenda kinyume na independence of the Judiaciary. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa inapendekezwa kwamba Ibara ya 9 ifanyiwe marekebisho kwa kuondoa neno President lililopo katika Ibara hiyo na kuweka neno the Commission. Lengo la mapendekezo haya ni kuhakikisha kwamba masuala ya kinidhamu ya watumishi wa Tume ya Mahakama yanashughulikiwa ndani ya Tume ya Mahakama. Ubora wa pendekezo hili ni kwamba, hakutakuwa na interference katika masula ya uendeshaji wa Mahakama, hakutakuwa na ukiukwaji wa Nguzo Kuu ya Kikatiba ya Separation of Powers na vile vile tutalinda uhuru wa Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafasi ya Chief Court Administrator inapendekezwa kwingine kwamba ndiye anayeshikilia pesa zote. Tukiruhusu aondolewe at the whim of the President, itakuwa ku-interfere with the independence of the Court na hii itavuruga kabisa mfumo wetu wa Kikatiba unaoheshimu independce of the Court na vile vile Separation of Powers.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuboresha utendaji wa kazi za Mtawala Mkuu wa Mahakama, masuala yote ya kinidhamu ya Mtendaji huyu yashughulikiwe na Tume ya Utumishi wa Mahakama kama inavyopendekezwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pendekezo langu likubaliwe. (Makofi)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la Separation of Powers nalo pia nadhani ni upotoshwaji. Kwa sababu, Rais, kwanza, ni Rais. Pili, ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu, tatu ni Mkuu wa Nchi. Ni lazima ujue mambo haya matatu kwa sababu ndiyo msingi wa mambo unayoyasema. Sasa ni kwa nini mamlaka ya kuteua kwa mujibu wa Chapter 1 ya Sheria zetu, mtu anayeteua, ndiye pia anakuwa mamlaka ya nidhamu. A simple law na ndiye anayetengua. Hiyo ni sheria rahisi sana, kwa hiyo nafikiri kwamba ungerudi ukasome Cap 1, ukasome Katiba. Kufanya siasa hapa ni kitu kingine, lakini kusema mambo ambayo ni ya kisheria ni kitu kingine pia.

48 Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kimsingi bila kupoteza muda wako, maoni yetu ni kwamba mamlaka ya Chief Court Administrator iwe kwa Rais na ufahamu, kama umesoma sheria vizuri, kuna mtu anaitwa Chief Registrar. Huyu na Court Administrator wako at per, wote wanaripoti kwa Chief Justice. Sasa mamlaka ya huyu iwe kwenye Commission, mamlaka ya yule mwingine iko sehemu gani? Kwa hiyo, hata ile administration inabidi nayo pia uifahamu. Nafikiri nikubali kwamba, you know, naogopa sana nisije nikawa unguided missile, ukiwa unguided missile, ni kwamba hutasikia ushauri mwingine wa upande mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili liko wazi kabisa. Lakini, kama kuna mchakato wa Katiba, Watanzania wanasema hii hapana, hatujafika huko, tungojee kwenye daraja hilo, tutavuka salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nirudie tena kwamba sipotoshi. Vile vile niseme kwamba nafahamu sheria na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye amekubali hivyo mara kadhaa humu ndani. Kwa hiyo, asifikiri kwamba hivyo anavyovisema sivijui. Ni kweli kwamba Rais wetu ni Amiri Jeshi Mkuu na mimi sijaleta hoja ya kumvua Uamiri Jeshi Mkuu humu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli vile vile kwamba Rais wetu ni Mkuu wa Nchi na mimi sijaleta hoja ya kum-impeach humu. Ninachokisema ni rahisi sana, mamlaka ya kudhibiti nidhamu ya Maafisa wa Kimahakama, ya watumishi wa Mahakama, isiende nje ya Tume ya Mahakama. Ikienda nje ya Tume ya Mahakama, kutakuwa na interference by the Executive na nchi hii, tuna historia ndefu sana ya kivuli kirefu cha interference ya Executive kwenye Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, ninachotaka hapa ni kuhakikisha kwamba Mahakama zetu zinakuwa huru, kuhakikisha kwamba kuna proper separation of powers. We are not challenging the Amiri Jeshi Mkuu, we are not trying to impeach Him, it’s sympathy. Tunachohitaji, Mahakama zetu ziwe huru na pendekezo hili la kudhibiti nidhamu ya Mtawala Mkuu wa Mahakama within the parameters za Utumishi wa Mahakama, inafaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata utaratibu wa nidhamu ya watumishi wengine wa juu wa Mahakama, Majaji, Majaji wa Mahakama ya Rufaa na nini, kuna utaratibu ambao una-ensure independence of the Court. Kwa hiyo, hiki ninachokipendekeza kitakuwa sambamba na utaratibu wa kudhibiti nidhamu ya Maafisa wakubwa wa Kimahakama. Sifanyi kitu kipya hapa. Kuniita unguided missile, kwa kweli ni tusi ambalo sikulitegemea kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

MWENYEKITI: Nilivyosikia mimi, anajiita yeye atakuwa unguided missile. Yeye, siyo wewe.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Angesema who is the unguided missile.

49

MWENYEKITI: Himself! (Kicheko)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Sawa sawa, kama yeye anaogopa kuwa an unguided missile, kwa kweli hilo ni tatizo lake na pengine achukue tahadhari tu za kutokuwa unguided missile.

(Hapa Kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Afadhali kengele imegonga.

(Pendekezo lilitolewa liamuliwe) (Pendekezo liliamuliwa na Kukataliwa)

(Ibara Iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 10

MHE. TUNDU. A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 10 inapendekezwa kufanya mabadiliko katika Ibara Ndogo ya (2) kwa kuondoa neno President katika Ibara Ndogo ya (2) na kuweka neno Commission.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 10(2) inazungumzia pale ambapo Jaji Mkuu anapoteua Kaimu Mtawala Mkuu wa Mahakama. Kama ilivyo, inapendekeza kwamba Jaji Mkuu anapoteua Kaimu Mtawala Mkuu wa Mahakama wakati Mtawala mwenyewe hayupo kwa muda, basi amtaarifu Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, Rais wetu ni Amiri Jeshi Mkuu kama tulivyoambiwa, anaongoza Baraza la Mawaziri, ni Mkuu wa Nchi, ana kazi nyingi. Hata ya kuambiwa kwamba tumeweka Kaimu Mtawala Mkuu wa Mahakama na yeye apelekewe taarifa! Ili kumpunguzia Rais mamlaka makubwa aliyonayo, ili a-concentrate kwenye mambo makubwa ya Uamiri Jeshi Mkuu na Kuongoza Baraza la Mawaziri na vitu kama hivyo, inapendekezwa kwamba pale ambapo Jaji Mkuu anateua Kaimu Mtawala Mkuu wa Mahakama wakati Mtawala mwenyewe yuko nje temporalily, basi taarifa ya uteuzi huo ipelekwe kwenye Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la pendekezo hili liko wazi, siyo tu kwamba litampunguzia Rais kazi, lakini vile vile litaongeza ufanisi wa Utawala wa Mahakama. Vile vile, muhimu kabisa, lita-ensure independence of the Judiciary na separation of powers. Mambo ya Kimahakama yaende Kimahakama, mambo ya nje ya Kimahakama yaende nje ya Kimahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

50 MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, inakuwa monotonous, lakini hatuna njia nyingine. Kwa mujibu wa Ibara ya 112 ya Katiba, Mwenyekiti wa Judicial Service Commission ni Judge Mkuu, kwa hiyo, unaposema hapa kwamba Jaji Mkuu aiarifu Commission ni kama vile unasema tutology na kwa sababu hili lilishaamuliwa huko nyuma, sisi mapendekezo yetu ni kwamba ibaki kama ilivyo.

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimshukuru sana Mheshimiwa rafiki msomi mwenzangu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maelezo mazuri sana tangu tuanze katika kikao cha Kamati yako. Katika hili ambalo Mheshimiwa rafiki msomi mwenzangu, Mheshimiwa Tundu Lissu amelisema, nataka tu Kamati yako ijielekeze kwenye Kifungu hicho hicho cha 10(b). Kifungu hiki kinasema: “Iwapo mtu anayeshikilia ofisi hiyo atakuwa hayupo kwenye nafasi yake kwa kipindi cha zaidi ya siku 30, Tume lazima iteue mtu mwingine kushikilia nafasi hiyo”. Tume ndiyo inayoteua, sasa Tume yenyewe haiwezi ikateua, halafu yenyewe ijipatie taarifa. It’s a contradiction term na ndiyo maana yule aliyemteua anapelekewa taarifa. Unauona mtiririko wa uwajibikaji kwa uwazi kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengine ni vizuri unapoongea katika Nyumba hii kubwa ya Watanzania, waongoze vizuri, tusiache haya ya ku-play to the gallery. Kwa heshima zote kabisa, naomba kwenye eneo hili kama alivyosema Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu, Kifungu hicho kibaki kama kilivyo kwamba watatoa taarifa kwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni utaratibu mzuri na ni mila na desturi nzuri kwa wale wenye utalaam wa sheria kukubali pale ambapo kuna hoja nzuri imetolewa. Nakubaliana na hoja ya Mheshimiwa kwamba hili pendekezo kwa jinsi alivyoliweka halikuwa limeletwa sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, I concede, tuendelee. (Makofi)

MWENYEKITI: Kwa hiyo, sasa, alichokifanya Mheshimiwa Tundu Lissu, ni kuondoa mwenyewe pendekezo lake la mabadiliko. Kwa hiyo, linabaki pendekezo lililokuwepo la Serikali.

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 11 Ibara ya 12 Ibara ya 13 Ibara ya 14 Ibara ya 15 Ibara ya 16

51

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 17 Ibara ya 18 Ibara ya 19 Ibara ya 20 Ibara ya 21 Ibara ya 22 Ibara ya 23

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 24

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake) Ibara ya 25 Ibara ya 26

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 27 Ibara ya 28 Ibara ya 29 Ibara ya 30 Ibara ya 31

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 32 Ibara ya 33

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 34

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

52 Ibara ya 35 Ibara ya 36

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 37 Ibara ya 38 Ibara ya 39

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 40

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote) Ibara ya 41

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 42 Ibara ya 43 Ibara ya 44 Ibara ya 45

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 46

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 47 Ibara ya 48 Ibara ya 49

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 50

53 MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ibara ya 50(1) ya Muswada inapendekeza kuundwa kwa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Kimahakama wa Mikoa.

Ibara ndogo ya (1) inaweka composition ya hizo Kamati. Inasema kwamba Wajumbe wa Kamati watakuwa:-

(a) Mkuu wa Mkoa.

(b) Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa.

(c) Katibu Tawala wa Mkoa.

(d) Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Mkuu wa Mkoa.

(e) Maafisa wawili wa Kimahakama watakaoteuliwa na Jaji Mfawidhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza kuondoa kipengele cha (a) kilichoko katika Ibara ndogo ya (1) kinachomfanya Mkuu wa Mkoa Mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Kimahakama na Mwenyekiti wa Kamati na vile vile kumwondoa Katibu Mtendaji wa Mkoa na vile vile kuwaondoa wajumbe wawili watakaoteuliwa na Mkuu wa Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, badala yake inapendekezwa kwamba, Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Kimahakama ya Mkoa iwe na Wajumbe wafuatao:-

(a) Msajili wa Mahakama Kuu atakayekuwa Mwenyekiti.

(b) Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa.

(c) Nafasi ya Katibu Tawala ichukuliwe na nafasi ya Mwakilishi wa Chama cha Mawakili wa Tanzania Bara.

(d) Nafasi ya Wajumbe wawili wanaoteuliwa na Mkuu wa Mkoa ichukuliwe na Mwanasheria wa Serikali, Wakili wa Serikali Mfawidhi au Mwakilishi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwaweka Wakuu wa Mikoa na watawala wengine katika Kamati za Maadili ya Maafisa wa Kimahakama ni kuingilia uhuru wa Mahakama, ni ku-interfere with independence of Judiciary na vile vile ni kuvuruga separation of powers. Pili, Mkuu wa Mkoa ni Kada wa Chama cha Mapinduzi, Mkuu wa Mkoa ni Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa. Si tu Mwakilishi wa Rais vile vile ni Mwakilishi wa CCM. Haiwezekani Kada wa CCM huyu akawa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mahakimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ili kulinda uhuru wa Mahakama zetu na ili kuhakikisha kwamba kuna proper separation of functions kati ya mihimili mikuu ya dola

54 huyu Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wajumbe anaowateua waondoke kwenye Kamati ya Maadili ya Mkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile pendekezo langu ni kwamba hizo nafasi zichukuliwe na watu ambao aidha, wako ndani ya Utumishi wa Mahakama kama vile Msajili wa Mahakama Kuu na vile vile watu hata kama hawako kwenye Utumishi wa Mahakama lakini wanaufahamu wa mila na desturi na masuala ya kinidhamu na maadili ya Kimahakama kama Mawakili. Vile vile kuwe na mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu pamoja na kwamba yeye si mtumishi wa Mahakama vile vile ana ufahamu wa mila, desturi na maadili ya Kimahakama. Kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa shughuli za Kamati ya Maadili ya Mkoa na vile vile hakuta-interfere na uhuru wa Mahakama, hakuta-interfere mgawanyo wa mamlaka katika hizi mamlaka tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Muswada kama ulivyo unahatarisha uhuru wa Mahakama zetu za chini. Kila siku itakuwa ni kelele kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na makada wenzake wa CCM. Ahsante.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri wakati najibu Mheshimiwa Tundu Lissu hakunisikiliza naomba nijibu tena kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukumu ya Kamati hizi siyo kutoa uamuzi au adhabu dhidi ya Hakimu, isipokuwa Kamati hizi hufanya uchunguzi baada ya kupokea malalamiko ya wananchi na kutoa ripoti kwa Jaji Mfawidhi wa Kanda husika, ambaye naye hupeleka taarifa hiyo kwenye Tume, Viongozi hawa wamewekwa kwa nia njema na kuhakikisha kuwa haki inaonekana kuwa inatendeka kwa sababu wanaotuhumiwa ni Mahakimu na si vema Mahakimu hao kuchunguza kesi zinazowahusu. Kwa hiyo, naomba ibaki kama ilivyo.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna good practice, Bunge lina Kamati yake ya maadili, Mbunge akikosea anahukumiwa na Wabunge wenyewe kwa mujibu wa yale makosa ambayo anayo. Sioni hili kwa nini halifanyiki kwa upande wa Mahakama, hilo la kwanza. Lakini jambo la pili, kama kuna malalamiko ya wananchi na Jaji Mfawidhi amepelekewa malalamiko ya wananchi, Jaji Mfawidhi anaweza akaunda Kamati ya maadili kushughulikia matatizo yale kwa kuteua watu ambao wanaifahamu Idara ya Mahakama. Kuchanganya wanasiasa kushughulikia maadili ya Mahakimu ni wrong.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili naomba Bunge likubaliane na mabadiliko ambayo Mheshimiwa Lissu ameyaleta ili kuhakikisha kwamba Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya hawaingilii utendaji. Waziri atakuwa anafahamu hata kama Mkuu wa Mkoa au wale Wajumbe wa Kamati ya Maadili hawahusiki na maamuzi, kitendo cha kumwita Hakimu mbele ya Mkuu wa Mkoa, kinaondoa uhuru wa Hakimu kufanya kazi yake inavyotakiwa.

55 Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Bunge lako Tukufu likubaliane na mapendekezo ya Mheshimiwa Mbunge ambaye ameleta schedule of amendment, ili tuimarishe utawala unavyotakiwa kwa kuhakikisha kwamba Kamati ya Maadili haiingizi wanasiasa.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Nadhani Waziri hajaelewa hoja yangu. Ninachopendekeza siyo Mahakimu wanaotuhumiwa kujifanyia uchunguzi, ninachopendekeza ni kwamba, Hakimu anayetuhumiwa afanyiwe uchunguzi na Kamati ya Maadili ambayo Mwenyekiti wake ni Msajili wa Mahakama Kuu siyo Hakimu mwenyewe.

Pili, ninachopendekeza ni kwamba, Wajumbe wa Kamati hiyo wasiwe wanasiasa na wasiwe makada wa CCM kwa kumwondoa Mkuu wa Mkoa, kwa kuondoa wateule wake, kwa kumwondoa Katibu Tawala wa Mkoa na hata Mjumbe wa CHADEMA for that matter. Tatu, ninachokipendekeza ni kwamba Mwakilishi wa Chama cha Mawakili wa Tanzania Bara, Mawakili vile vile ni Maafisa wa Mahakama, lakini Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara na Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wawe wajumbe wa Kamati hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa ni watu wanaofahamu mila na desturi na miiko ya Kimahakama, siyo wanasiasa. Nashukuru sana Mheshimiwa Kabwe Zitto ameeleza vizuri kwamba nidhamu ya Wabunge inashughulikiwa Bungeni, nidhamu ya Mawakili inashughulikiwa na Kamati ya Mawakili ambayo Mwenyekiti wake ni Jaji Kiongozi, kwa sababu Mahakama inafahamu mila na miiko na desturi za Mawakili, tunapoweka wanasiasa katika kushughulikia nidhamu za Mahakama wataleta siasa zao mle ndani. Itavuruga uhuru wa Mahakama, itavuruga mgawanyo wa Mahakama, tutakuwa kichekesho. (Makofi)

MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Tundu Lissu ameifikiria hii hoja kwa mtizamo wa aina moja tu. Lakini hapa kuna sababu inayopelekea kuwepo kwa hizi Committees. Zamani zilikuwepo pia na ziliitwa Bodi na zimesaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi wa jambo hili, ni kwamba wananchi na watu wa kawaida kabisa pale wanapodhani kwamba wanakosa mahala pa kwenda kusemea jambo lao linalohusiana na utoaji haki, na pengine niunganishe hii na ile aliyosema Mheshimiwa Zitto, kwamba Bunge siyo sawa sawa na Mahakama, Bunge linafanya shughuli zake ndani lenyewe, lakini Mahakama ni chombo cha kutoa huduma ambacho kuna mtu mwingine anaweza akawa aggrieved akahisi kwamba utaratibu wa jambo lake mbali na utaratibu wa kawaida wa Kimahakama ambao ndiyo Judicial Process ya kwenda ku-appeal na kuomba vitu vya namna hiyo, lakini hapa katikati wakati haki yake inatafutwa anaona hatendewi sawasawa, anasema hiki katika utoaji wa ushahidi kwa mfano na Hakimu inatokea anaandika kinyume (improper recording) au anakwenda mwananchi wa kawaida Mahakamani wanahangaika anaambiwa faili halionekani sasa akalalamike wapi? Katika misingi ya kisheria Mheshimiwa Lissu ni Mwanasheria you can not be a judge on your own case.

56

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakimu hawa ni binadamu, siyo wote. Wapo baadhi ambao pengine hawafanyi vizuri, tunadhani ni bora kukawa na kioo cha yeye kujitazama watu wengine ndiyo waangalie na process wanayoifanya, hii Kamati ni process ya kawaida tu ya kuuliza na kuangalia ukweli ukoje na baadaye wanarudishiwa wao wenyewe waamue juu ya mwenzao, ubaya wake upo wapi? Hii Kamati ipo tu kwa ajili ya kuuliza inafanya inquiries na baadaye inarudishwa kwa wao wenyewe waamue kwa misingi na taratibu za Kimahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna ubaya, nadhani kusema hapa kwamba Wakuu wa Mikoa ni wa CCM lakini kesho wanaweza wakawa wa Chadema. Hii ni situation ambayo ipo, kwa hiyo hii ni very temporary solution. Unadhani ni kwa mtazamo tu wa sasa lakini sheria hii ipo kwa ajili ya mazingira yoyote yale, ningeshauri na ningeomba wenzangu wanaoona hoja hii kwamba msingi wake hakika ni kujitazama kwamba mtu mwingine ndiye akutazame na yeye haamui dhidi ya Mahakama wala Hakimu. Ile Kamati kazi yake ni kuuliza na wajumbe wake ndiyo hapo yupo Hakimu Mkazi, wapo wenyewe kwa wenyewe ni Wajumbe mle, kwa hiyo wanaangalia matatizo yaliyofanywa na mwenzao kwamba jamani Hakimu huyu au Afisa fulani wa Mahakama hajafanya vizuri. Kwa hiyo, mimi nadhani ni process ya kawaida. Nakushukuru sana.

KUHUSU TAARIFA

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa taarifa kwamba hata hapa Bungeni kuna mwananchi anaweza kuwa aggrieved na kauli ya Mbunge, atakuandikia utapeleka Kamati ya Maadili ya Bunge, kwa hiyo, Wabunge ndiyo tutakaolishughulikia hilo. Ni hali hiyo hiyo kwenye Mahakama, kwa hiyo, tusitake kujenga hoja labda tu kwa sababu imetoka upande wa pili.

MWENYEKITI: Unajadili au unatoa taarifa?

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa natoa taarifa, taarifa nyingine ni kwamba tumepitisha utaratibu wa Mahakama kuanza kurekodi kwa kutumia vyombo vya kisasa kama ilivyo Hansard za Bunge. Kwa hiyo, wasiwasi wake wa kwamba kuna rekodi zinaweza zikawa zimefanyiwa makosa auondoe. Naomba Bunge likubaliane na mapendekezo ya Mheshimiwa Lissu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa usichanganye mambo, mnachokisema wote ni sawa. Huyu anasema watakusanya mawazo watapelekewa wanaohusika, hivyo hivyo hata hapa Bungeni Kanuni ile ya 71, kama wewe umemsema mwananchi vibaya ataniandikia mimi na mimi nitapeleka kwenye Kamati yangu inayohusika. Mwananchi yule hataruhusiwa kuja hapa itakuwa ni sisi wenyewe. Kwa hiyo wanaofikiria kwamba pendekezo la Marekebisho…..

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapana hoja ni ya kwangu, mimi ndiye nafunga halafu ndiyo utaratibu.

57 MHE. KABWE Z. ZITTO: Na Serikali haijajibu

MWENYEKITI: Taratibu, kwa nini mnahamaki wakati mimi ninakaa hapa mezani? Nipo hapa kwa sababu ya kuongoza kikao, sasa mnahamaki bila sababu. Mimi nafuata utaratibu, kama una nafasi yako nitakwambia una nafasi yako. Nafasi yako ya dakika tatu kwa mfano yule nimempa dakika tatu na mwingine atakayejadili nje ya wewe kipindi cha kwanza unapewa dakika tano, cha pili unapewa dakika tatu na wengine wote ambao siyo wenye Muswada wao watajadili kwa dakika tatu tu, sasa nitakupa tu kwa sababu Simbachawene ameingia.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali bado haijajibu.

MWENYEKITI: Wameshajibu. Siyo lazima wajibu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu hoja ya Mheshimiwa Simbachawene, amesema kweli mimi ni Mwanasheria na ni kweli kabisa nafahamu sheria. Ni nidhamu za Madaktari zinashughulikiwa na Medical Council of Tanzania, nidhamu za Wafamasia tumepitisha sheria hapa juzi zinashughulikiwa na Baraza la Famasia, nidhamu za Mainjinia zinadhibitiwa na Engineers Registration Board, Nidhamu za Mawakili zinadhibitiwa na Advocates Committee, nidhamu ya Mahakimu idhibitiwe na the profession pia siyo na wanasiasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi hoja ni kwa sababu ya kutaka kuingiza ukada tu. Tatizo nilisema juzi na naomba nirudie tena, msiniangalie mimi wafikirieni Watanzania. Mimi naweza nikawa nawaudhi kweli, lakini fikiria unatunga sheria hii kwa ajili ya Watanzania siyo kwa ajili ya Tundu Lissu. (Makofi)

MWENYEKITI: Je, Serikali unataka kusema chochote?

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume zote alizozitaja zinatoa maamuzi, hii Kamati haitoi maamuzi, maamuzi yanakuja kutolewa na Tume.

MWENYEKITI: Haya tunafika mwisho, maana sasa mmeshaanza kujadili.

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti naomba kura zihesabiwe kwa wanaosema ndiyo na siyo.

MWENYEKITI: Toa hoja.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja kwamba, sauti za waliosema ndiyo na siyo zimeelekea kukubaliana, naomba Mbunge mmoja mmoja kura zihesabiwe ziwe on records.

58 MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Mwenyekiti naafiki.

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

MWENYEKITI: Sawa, kengele ipigwe na watu waingie ndani. Serjeant At Arms funga milango.

MWENYEKITI: Mimi hapa sipigi kura. Anayefikiri kwamba hoja aliyoleta Mheshimiwa Tundu Lissu ikubaliwe atasema ndio. Yule anayefikiri kwamba hoja iliyoletwa na Mheshimiwa Tundu Lissu isikubaliwe atasema siyo. Kwa hiyo, siyo kwa wanaokataa hoja ya Mheshimiwa Tundu na ndio kwa wale wanaotaka hoja ya Mheshimiwa Tundu ipite. Sasa maana niliwahoji vile kwa mdomo lakini nikasema nafikiri waliosema siyo ndio wameshinda wakaseka hawakubaliana, kwa hiyo, tunakwenda kwa jina. Kwa hiyo, wanaokubali kwamba hoja ya Mheshimiwa Tundu Lissu ikubaliwe katika paragraph ya 50 ndio watakaosema ndio. Wanaopinga watasema siyo. Sasa tunaanza.

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda...... Ndiyo

MWENYEKITI: Naomba urudie Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunaanza upya.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni zetu kura zinarekodiwa mara moja.

MWENYEKITI: Ahaa, hapana kabisa.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, amekubaliana na hoja ya Mheshimiwa Lissu. Kwa hiyo, naomba na Wabunge wote wa CCM wakubaliane nayo. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema siyo.

MBUNGE FULANI: Acha kampeni.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nikikwita kama sijakuelewa nitakuuliza tena ulisemaje? Ndio utaratibu. Tatizo lenu ninyi mnapenda kila saa kuzomea. Hata wewe nikikwita kama sikukusikia nitakuita tena. Tunaanza.

MBUNGE FULANI: Unachakachua kura.

MWENYEKITI: Tunaanza tena.

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda...... Ndiyo

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda amekubaliana.

59

MBUNGE FULANI: Kwa nini umsemee?

MHE. KABWE Z. ZITTO: Na amerejea mara ya pili tayari. (Makofi) MBUNGE FULANI: Ndiyo, tunaendelea.

MWENYEKITI: Unajua tatizo nyie Waheshimiwa Wabunge...

(Hapa Mheshimiwa Waziri Mkuu alisimama)

MWENYEKITI: Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu ukae.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti...

MWENYEKITI: Naomba ukae kidogo.

WAZIRI MKUU: Nikae?

MWENYEKITI: Ndiyo, naomba ukae.

Tatizo la Waheshimiwa Wabunge wanapenda zile fujo tu zisizokuwa na msingi ni kawaida tumekaa katika Bunge hili kama kiti hakikuelewa yule anayesema amesema nini unaweza kumuita tena. Acheni mambo yasiyokuwa na maana. Mengine hayana hata msingi. Ninaanza tena.

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda...... Siyo Mheshimiwa Job Yustino Ndugai...... Hayupo Mheshimiwa Samuel John Sitta...... Siyo Mheshimiwa ...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Mary Michael Nagu ...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ...... Hayupo Mheshimiwa Prof. Mark James Mwandosya...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi...... Hayupo Mheshimiwa Stephen Masatu Wasira ...... Siyo Mheshimiwa Prof. Jumanne Abdallah Maghembe...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa...... Siyo Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia...... Siyo Mheshimiwa Sophia Mattayo Simba...... Siyo Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe...... Siyo Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe ...... Siyo Mheshimiwa Mustafa Haidi Mkulo...... Hayupo Mheshimiwa William Mganga Ngeleja...... Hayupo Mheshimiwa George Huruma Mkuchika...... Siyo Mheshimiwa Celina Ompeshi Kombani...... Siyo Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Emmanuel John Nchimbi...... Siyo

60 Mheshimiwa Dkt. Cyril August Chami...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. ...... Hayupo

MWENYEKITI: Sihitaji kelele zisizo na sababu zikome.

Mheshimiwa Gaudentia Mugosi Kabaka...... Hayupo Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige...... Hayupo Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Terezya Pius Luoga Huvisa...... Hayupo Mheshimiwa Prof. Makame Mnyaa Mbarawa...... Siyo Mheshimiwa Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka...... Siyo Mheshimiwa Omari Rashid Nundu...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Hadji Hussein Mponda...... Siyo Mheshimiwa Jaji Frederick Mwita Werema...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Milton Makongoro Mahanga...... Hayupo Mheshimiwa Eng. Christopher Kajoro Chiza...... Hayupo Mheshimiwa Balozi Khamis Juma Suedi Kagasheki...... Siyo Mheshimiwa Lucy Sawere Nkya...... Hayupo Mheshimiwa Adam Kighoma Malima ...... Hayupo Mheshimiwa Aggrey Deaisile Joshua Mwanri...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Harrison George Mwakyembe...... Hayupo Mheshimiwa Lazaro Samuel Nyalandu...... Siyo Mheshimiwa Benedict Ngalama Ole-Nangoro...... Hayupo Mheshimiwa Majaliwa ...... Siyo Mheshimiwa Gregory George Teu...... Siyo Mheshimiwa Pereira Ame Silima...... Hayupo Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim...... Siyo Mheshimiwa Charles Muhangwa Kitwanga...... Siyo Mheshimiwa Goodluck Joseph Ole-Medeye...... Hayupo Mheshimiwa Athumani Rashid Mfutakamba...... Siyo Mheshimiwa Philipo Augustino Mulugo...... Hayupo Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Fenella Ephraim Mukangara...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadalla... .Hayupo Mheshimiwa Eng. Gerson Hosea Lwenge...... Hayupo Mheshimiwa Mwanamrisho Taratibu Abama...... Ndiyo Mheshimiwa Maida Hamad Abdallah...... Hayupo Mheshimiwa Anna Margareth Abdallah...... Siyo Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah...... Ndiyo Mheshimiwa Munde Tambwe Abdallah...... Hayupo Mheshimiwa Bahati Ali Abeid...... Hayupo Mheshimiwa Abdul-Aziz Mohamed Abood...... Hayupo Mheshimiwa Chiku Aflah Abwao...... Ndiyo Mheshimiwa Khalfan Hilaly Aeshi...... Hayupo Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed...... Ndiyo Mheshimiwa Lameck Okambo Airo...... Hayupo

61 Mheshimiwa Mustaph Boay Akunaay...... Hayupo Mheshimiwa Abdalla Haji Ali...... Hayupo Mheshimiwa Juma Othman Ali...... Siyo Mheshimiwa Salim Mbarouk Ali...... Ndiyo Mheshimiwa Sara Msafiri Ally...... Hayupo Mheshimiwa Hussein Nassor Amar...... Siyo Mheshimiwa Kheri Khatib Ameir ...... Hayupo Mheshimiwa Abdallah Sharia Ameir...... Siyo Mheshimiwa Abdulsalaam Selemani Amer...... Siyo Mheshimiwa Amina Abdallah Amour...... Hayupo Mheshimiwa Said Amour Arfi...... Hayupo Mheshimiwa Jaku Hashim Ayoub...... Hayupo Mheshimiwa Rostam Abdulrasul Aziz...... Hayupo Mheshimiwa Iddi Mohamed Azzan...... Siyo Mheshimiwa Azzan...... Siyo Mheshimiwa Omary Ahmad Badwel...... Hayupo Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar...... Siyo Mheshimiwa Salum Khalfan Barwany...... Ndiyo Mheshimiwa Elizabeth Nkunda Batenga...... Siyo Mheshimiwa Gosbert Begumisa Blandes...... Siyo Mheshimiwa Lolesia Jeremiah Maselle Bukwimba...... Siyo Mheshimiwa Ester Amos Bulaya ...... Hayupo Mheshimiwa Selemani Said Bungara ...... Ndiyo Mheshimiwa Felister Aloyce Bura...... Siyo Mheshimiwa Agripina Zaituni Buyogera...... Ndiyo Mheshimiwa Saidi Ramadhani Bwanamdogo...... Hayupo Mheshimiwa Jerome Dismas Bwanausi...... Siyo Mheshimiwa Josephine Tabitha Chagulla...... Siyo Mheshimiwa Kisyeri Werema Chambiri...... Hayupo Mheshimiwa Pindi Hazara Chana...... Siyo Mheshimiwa Mary Pius Chatanda...... Siyo Mheshimiwa Andrew John Chenge...... Siyo Mheshimiwa John Momose Cheyo...... Hayupo Mheshimiwa Hezekiah Ndahani Chibulunje...... Siyo Mheshimiwa John Zefania Chiligati ...... Hayupo Mheshimiwa Diana Mkumbo Chilolo...... Siyo Mheshimiwa Muhammad Amour Chomboh...... Siyo Mheshimiwa Amina Andrew Clement...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Maua Abeid Daftari ...... Siyo Mheshimiwa Mohamed Gulam Dewji...... Hayupo Mheshimiwa Deo Haule Filikunjombe...... Hayupo Mheshimiwa Paulina Philipo Gekul...... Ndiyo Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke...... Siyo Mheshimiwa ...... Siyo Mheshimiwa Khatib Said Haji ...... Hayupo Mheshimiwa Zahra Ali Hamad...... Hayupo

62 Mheshimiwa ...... Ndiyo Mheshimiwa Azza Hillal Hamad...... Hayupo Mheshimiwa Asaa Othman Hamad...... Ndiyo Mheshimiwa Neema Mgaya Hamid...... Hayupo Mheshimiwa Shawana Bukheti Hassan...... Siyo Mheshimiwa Maria Ibeshi Hewa...... Siyo Mheshimiwa Mansoor Shanif Hiran...... Hayupo Mheshimiwa Agness Elias Hokororo...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Christina Gabriel Ishengoma...... Hayupo Mheshimiwa ...... Siyo Mheshimiwa Waride Bakari Jabu...... Siyo Mheshimiwa Jaddy Simai Jaddy...... Siyo Mheshimiwa Selemani Saidi Jafo...... Siyo Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha...... Siyo Mheshimiwa ...... Hayupo Mheshimiwa Riziki Omar Juma...... Ndiyo Mheshimiwa Abuu Hamoud Jumaa...... Siyo Mheshimiwa Ritta Enespher Kabati ...... Siyo Mheshimiwa David Zacharia Kafulila...... Hayupo Mheshimiwa Prof. Kulikoyela Kanalwanda Kahigi...... Ndiyo Mheshimiwa Haji Khatib Kai...... Ndiyo Mheshimiwa Naomi Amy Mwakyoma Kaihula...... Ndiyo Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki ...... Siyo Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso...... Siyo Mheshimiwa Innocent Edward Kalogeris...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Titus Mlengeya Kamani...... Siyo Mheshimiwa Vick Paschal Kamata...... Hayupo Mheshimiwa Josephat ...... Siyo Mheshimiwa Prof. Juma Athuman Kapuya...... Hayupo Mheshimiwa Mariam Reuben Kasembe...... Hayupo Mheshimiwa Rosweeter Faustin Kasikila...... Siyo Mheshimiwa Sylvester Mhoja Kasulumbayi ...... Ndiyo Mheshimiwa Eustace Osler Katagira...... Hayupo Mheshimiwa Vita Rashid Mfaume Kawawa...... Siyo Mheshimiwa Zainab ...... Siyo Mheshimiwa Gaudence Cassian Kayombo...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Kebwe ...... Siyo Mheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa...... Hayupo Mheshimiwa Ali Kheir Khamis...... Ndiyo Mheshimiwa Sadifa Juma Khamis...... Siyo Mheshimiwa Salim Hemed Khamis...... Ndiyo Mheshimiwa Yussuf Haji Khamis...... Ndiyo Mheshimiwa ...... Hayupo Mheshimiwa Aliko Nikusuma Kibona...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omar Kigoda...... Siyo Mheshimiwa Mendrad Lutengano Kigola...... Siyo

63 Mheshimiwa Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla...... Siyo Mheshimiwa Pudenciana Wilfred Kikwembe...... Hayupo Mheshimiwa Modestus Dickson Kilufi...... Siyo Mheshimiwa Mkiwa Adam Kimwanga...... Hayupo Mheshimiwa Rosemary Kasimbi Kirigini...... Hayupo Mheshimiwa Mariam Nasoro Kisangi...... Siyo

SPIKA: Naomba watu wote to pay attention, kila mtu atapiga kura anavyoona yeye. Kama sisi hatujasikia tutauliza tena.

Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula ...... Siyo Mheshimiwa Susan Limbweni Aloyce Kiwanga ...... Ndiyo Mheshimiwa Grace Sindato Kiwelu...... Ndiyo Mheshimiwa Highness Samson Kiwia...... Ndiyo Mheshimiwa Silvestry Francis Koka ...... Hayupo Mheshimiwa Capt. John Damiano Komba...... Hayupo Mheshimiwa Mussa Haji Kombo...... Siyo Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo...... Ndiyo Mheshimiwa Maulidah Anna Valerian Komu...... Ndiyo Mheshimiwa Al-Shaymaa John Kwegyir ...... Siyo Mheshimiwa Michael Lekule Laizer...... Siyo Mheshimiwa Godbless Jonathan Lema...... Hayupo Mheshimiwa James Daudi Lembeli...... Hayupo Mheshimiwa Devotha Mkuwa Likokola...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Festus Bulugu Limbu...... Hayupo Mheshimiwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu...... Ndiyo Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa...... Hayupo Mheshimiwa Alphaxard Kangi Ndege Lugola...... Hayupo Mheshimiwa Riziki Said Lulida...... Hayupo Mheshimiwa Livingstone Joseph Lusinde...... Siyo Mheshimiwa John Paul Lwanji...... Hayupo Mheshimiwa Susan Anselm Jerome Lyimo...... Hayupo Mheshimiwa Sylvester Massele Mabumba ...... Siyo Mheshimiwa Moses Joseph Machali...... Ndiyo Mheshimiwa Betty Eliezer Machangu...... Siyo Mheshimiwa Zarina Shamte Madabida...... Hayupo Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba Madelu... ..Hayupo Mheshimiwa John Shibuda Magalle...... Ndiyo Mheshimiwa Catherine Valentine Magige...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Binilith Satano Mahenge...... Siyo Mheshimiwa Amos Gabriel Makalla...... Siyo Mheshimiwa January ...... Hayupo Mheshimiwa Faki Haji Makame...... Ndiyo Mheshimiwa Ramo Matala Makani ...... Siyo Mheshimiwa Amina Nassoro Makilagi...... Hayupo Mheshimiwa Anne Kilango Malecela...... Siyo

64 Mheshimiwa AnnaMaryStella John Mallac...... Ndiyo Mheshimiwa Ignas Aloyce Malocha...... Siyo Mheshimiwa David Mciwa Mallole...... Siyo Mheshimiwa Murtaza Ally Mangungu...... Siyo Mheshimiwa Eng. ...... Siyo Mheshimiwa Abdul Jabiri Marombwa ...... Siyo Mheshimiwa Eng. Hamad Yussuf Masauni...... Siyo

SPIKA: Naomba wote tu-concetrate maana tukiirudia hii kazi, kila mtu asikilize jina lake.

Mheshimiwa Augustino Manyanda Masele...... Siyo Mheshimiwa Stephen Julius Masele...... Hayupo Mheshimiwa Ester Nicholas Matiko...... Ndiyo Mheshimiwa Donald Kelvin Max...... Hayupo Mheshimiwa Lucy Thomas Mayenga...... Siyo Mheshimiwa Kiumbwa Makame Mbaraka...... Siyo Mheshimiwa Anthony Gervase Mbassa...... Ndiyo Mheshimiwa Joseph Osmund Mbilinyi...... Ndiyo Mheshimiwa Freeman Alkaeli Mbowe...... Ndiyo Mheshimiwa Kuruthum Jumanne Mchuchuli...... Ndiyo Mheshimiwa Halima James Mdee...... Hayupo Mheshimiwa Zakia Hamdani Meghji ...... Hayupo Mheshimiwa Mariam Salum Mfaki...... Siyo Mheshimiwa ...... Hayupo Mheshimiwa William Augustao Mgimwa...... Siyo Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama...... Siyo Mheshimiwa Zabein Muhaji Mhita...... Siyo Mheshimiwa Esther Lukago Minza Midimu...... Siyo Mheshimiwa Fatuma Abdallah Mikidadi ...... Siyo Mheshimiwa Desderius John Mipata...... Hayupo Mheshimiwa Mohamed Hamisi Missanga...... Siyo Mheshimiwa Faith Mohamed Mitambo...... Hayupo Mheshimiwa Margareth Agnes Mkanga...... Siyo Mheshimiwa Dunstan Daniel Mkapa...... Hayupo Mheshimiwa Nimrod Elirehema Mkono...... Hayupo Mheshimiwa Felix Francis Mkosamali...... Hayupo Mheshimiwa Rita Louise Mlaki...... Hayupo Mheshimiwa Martha Moses Mlata...... Siyo Mheshimiwa Rebecca Michael Mngodo...... Ndiyo Mheshimiwa Lediana Mafulu Mng’ong’o ...... Siyo Mheshimiwa Herbert James Mntangi...... Siyo Mheshimiwa Mohamed Habib Juma Mnyaa...... – Mheshimiwa John John Mnyika...... Ndiyo Mheshimiwa Ally Keissy Mohamed...... Hayupo Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed...... Hayupo

65 Mheshimiwa Rajab Mbarouk Mohammed...... Siyo Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina...... Hayupo Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema...... Ndiyo Mheshimiwa Maryam Salum Msabaha...... Ndiyo Mheshimiwa Assumpter Nshunju Mshama ...... Siyo Mheshimiwa Mch. Peter Simon Msigwa...... Ndiyo Mheshimiwa Prof. Peter Mahamudu Msolla...... Siyo Mheshimiwa Saidi Mohamed Mtanda...... Siyo Mheshimiwa Abdul Rajab Mteketa ...... Hayupo Mheshimiwa Regia E. Mtema...... Ndiyo Mheshimiwa Abas Zuberi Mtemvu...... Siyo Mheshimiwa Christowaja Gerson Mtinda...... Ndiyo Mheshimiwa Philipa Geofrey Mturano...... Ndiyo Mheshimiwa Mtutura Abdallah Mtutura ...... Siyo Mheshimiwa Chritina Lissu Mughwai ...... Ndiyo Mheshimiwa Thuwayba Idrisa Muhamed ...... Ndiyo Mheshimiwa Joyce John Mukya ...... Hayupo Mheshimiwa Hasnain Mohamed Murji...... Hayupo Mheshimiwa Benardetha Kasabago Mushashu...... Siyo Mheshimiwa Mussa Hassan Mussa ...... Hayupo Mheshimiwa Eugen Elishininga Mwaiposa...... Siyo Mheshimiwa Prof. David Homeli Mwakyusa...... Hayupo Mheshimiwa Victor Kilasile Mwambalaswa...... Siyo Mheshimiwa Salome Daudi Mwambu ...... Siyo Mheshimiwa Mchungaji Luckson Ndaga Mwanjale...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa...... Siyo Mheshimiwa Clara Diana Mwatuka...... Hayupo Mheshimiwa Amina Mohamed Mwidau...... Ndiyo Mheshimiwa Charles John Poul Mwijage...... Siyo Mheshimiwa Hussein Mussa Mzee...... Siyo Mheshimiwa Yusuph Abdallah Nassir...... Siyo Mheshimiwa Mchungaji Israel Yohana Natse...... Ndiyo Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa...... Hayupo Mheshimiwa Philemon Kiwelu Ndesamburo...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile ...... Siyo Mheshimiwa Stephen Hilary Ngonyani ...... Siyo Mheshimiwa Cynthia Hilda Ngoye...... Siyo Mheshimiwa Ahmed Juma Ngwali...... Hayupo Mheshimiwa Brig. Jen. Hassan Athuman Ngwilizi...... Siyo Mheshimiwa Juma Abdallah Njwayo...... Siyo Mheshimiwa Juma Selemani Nkamia...... Hayupo Mheshimiwa Said Juma Nkumba...... Hayupo Mheshimiwa Albert Obama Ntabaliba...... Siyo Mheshimiwa Deogratias Aloyce Ntukamazina...... Hayupo Mheshimiwa Abia Muhama Nyabakari...... Siyo Mheshimiwa Nyambari C. Mariba Nyangwine...... Hayupo

66 Mheshimiwa Tauhida Cassian Galos Nyimbo...... Hayupo Mheshimiwa Leticia Mageni Nyerere...... Hayupo Mheshimiwa Vincent Joseph Nyerere...... Ndiyo Mheshimiwa Tauhida Cassian Galos Nyimbo...... Siyo Mheshimiwa Christopher Olonyokie Ole-Sendeka... Hayupo Mheshimiwa Rashid Ali Omar ...... Ndiyo Mheshimiwa Asha Mohamed Omari...... Siyo Mheshimiwa Suleiman Nassib Omar...... Hayupo Mheshimiwa Meshack Jeremiah Opulukwa...... Ndiyo Mheshimiwa Lucy Philemon Owenya...... Ndiyo Mheshimiwa Saleh Ahmed Pamba...... Ndiyo Mheshimiwa Ismail Aden Rage...... Hayupo Mheshimiwa Dkt. Seif Seleman Rashidi...... Siyo Mheshimiwa Rachel Mashishanga Robert...... Ndiyo Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya...... Ndiyo Mheshimiwa Mch. Dkt. Getrude P. Rwakatare...... Hayupo Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza...... Ndiyo Mheshimiwa Jasson Samson Rweikiza...... Hayupo Mheshimiwa Mwanakhamis Kassim Said...... Hayupo Mheshimiwa Said Suleiman Said...... Ndiyo Mheshimiwa Moza Abedi Saidy...... Ndiyo Mheshimiwa Magdalena Hamis Sakaya...... Ndiyo Mheshimiwa Kidawa Hamid Saleh...... Siyo Mheshimiwa Ramadhani Haji Saleh...... Hayupo Mheshimiwa Masoud Abdalla Salim...... Hayupo Mheshimiwa Ahmed Ali Salum...... Hayupo Mheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga...... Siyo Mheshimiwa Muhammad Ibrahim Sanya...... Hayupo Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd...... Siyo Mheshimiwa ...... Ndiyo Mheshimiwa Joseph Roman Selasini...... Ndiyo Mheshimiwa Haji Juma Sereweji ...... Hayupo Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba...... Hayupo Mheshimiwa Ahmed Mabkhut Shabiby...... Hayupo Mheshimiwa Abdulkarim Esmail Hassan Shah...... Siyo Mheshimiwa Haroub Muhammed Shamis...... Ndiyo Mheshimiwa Henry Daffa Shekifu...... Siyo Mheshimiwa Beatrice Matumbo Shellukindo...... Siyo Mheshimiwa Fakharia Khamis Shomar ...... Siyo Mheshimiwa Mussa Khamis Silima...... Siyo Mheshimiwa David Ernest Silinde...... Ndiyo Mheshimiwa George Boniface Simbachawene...... Siyo Mheshimiwa ...... Siyo Mheshimiwa Namelok Edward Moringe Sokoine...... Hayupo Mheshimiwa Jitu Vrajlal Soni ...... Hayupo Mheshimiwa Rose Kamili Sukum...... Ndiyo

67 Mheshimiwa Suleiman M.Nchambi Suleiman...... Hayupo Mheshimiwa Shaffin Ahmedali Sumar ...... Siyo Mheshimiwa Jeremiah Solomon Sumari...... Hayupo Mheshimiwa Sabreena Hamza Sungura...... Ndiyo Mheshimiwa Kaika Saning’o Telele...... Siyo Mheshimiwa Dkt. Charles John Tizeba...... Siyo Mheshimiwa Salim Hassan Abdullah Turky...... Hayupo Mheshimiwa Martha Jachi Umbulla...... Siyo Mheshimiwa Zaynabu Matitu Vullu...... Hayupo Mheshimiwa Anastazia James Wambura...... Hayupo Mheshimiwa Ezekiah Dibogo Wenje...... Ndiyo Mheshimiwa Godfrey Weston Zambi...... Siyo Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi...... Hayupo Mheshimiwa Kabwe Zubeir Zitto...... Ndiyo Mheshimiwa Said Mussa Zubeir...... Siyo

MWENYEKITI: Tumemaliza orodha sasa tunahesabu kura.

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, jina halijaitwa bado.

Mheshimiwa Maida Hamad Abdallah...... Siyo Mheshimiwa Deo Haule Filikunjombe...... Siyo Mheshimiwa Ramadhani Haji Saleh...... Siyo Mheshimiwa Desderius John Mipata...... Siyo Mheshimiwa Khalfan Hilaly Aeshi...... Siyo Mheshimiwa Eng. Salvatory Naluyaga Machemli...... Ndiyo

MWONGOZO

MWENYEKITI: Taratibu, kwanza mbona mnapenda mwongozo wa Spika, mimi sikusikia jina la aliyetaja sasa hivi. Tatizo mnasema halafu mnaendelea kuongea. Naomba unitajie jina lako vizuri. Mheshimiwa Kheri Ali Khamis...... Siyo

MWENYEKITI: Tumalize upande huu.

Mheshimiwa Mkiwa Adam Kimwanga...... Ndiyo

MWONGOZO

MHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako kwenye hili kwamba mimi naamini kwamba tunapiga kura kwa jambo ambalo tunalijua, tunatoa utashi wetu. Sasa sidhani kama tunawatendea haki Watanzania kama Mbunge anakuja sasa hivi na anapiga kura kwenye jambo ambalo halijui. I don’t think if we are doing justice to this country na hao waliokuja sasa hivi sidhani hata ukiwahoji sasa hivi

68 atakuwa anajua anasema hapana kwa jambo ambalo analijua. Nafikiri ni ushabiki. Naomba mwongozo kwenye hili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Felix Mkosamali hiyo argument hatujampendelea mtu yeyote, hii kura tumepiga wakati wengine wako kwenye committee wamekwenda kuitwa ndio maana kitabu hiki kinaonyesha aliyepiga tumemwona ambaye hakupiga naye tunamwona, ndio maana tunasema subiri kidogo tupate jina la huyu anayesema mimi sikuwepo wakati jina lake limeitwa.

MHESHIMIWA KABWE Z. ZITTO: Kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Sitaki kuhusu utaratibu.

MWONGOZO WA SPIKA

MBUNGE FULANI: Kabla kura hazijahesabiwa katika roster ya majina iliyotajwa ametajwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa mujibu wa Katiba ya Nchi yetu ni ex – official member wa Bunge na alipotajwa aliitikia. Sasa sijui naomba mwongozo wako kwenye jambo hili.

MWENYEKITI: Ambaye hapigi kura ni mimi tu basi.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. EZEKIA D. WENJE: Kuhusu Utaratibu Mheshimiwa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Siruhusu Kuhusu Utaratibu, nataka wenye majina ambao hawakupiga kura.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Naitwa Luhaga Johnson Mpina. Siyo!

MWENYEKITI: Kuna mwingine ambaye ameingia sasa hivi hakuwepo?

KUHUSU UTARATIBU

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Ambao ni upi huo, Kanuni gani ya utaratibu wako?

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 4(2) ya Katiba inasema, kazi ya Bunge ...

MWENYEKITI: Tunaanza na Kanuni kwanza.

MBUNGE FULANI: Ahaaa! Naanza na Kanuni. Kanuni ya 61(1) inasema, kutozungumza jambo lenye maslahi ya kifedha na inasomwa pamoja na Ibara ya 4(2) ya

69 Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambayo inasema kazi ya Bunge ni kutunga sheria za nchi na siyo sheria za vyama vya siasa. Sasa hawa makada wa CCM ambao wanataka kuingizwa hapa huwa wanaisaidia CCM kupata pesa za ruzuku...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge naomba ukae chini.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, bado sijamaliza.

MWENYEKITI: Nikisimama mimi lazima ukae chini. Mheshimiwa Mbunge, zoezi tunalolifanya sasa ni kuhesabu kura, sasa unaingiza mambo mengine unataka nifanye nini? Jamani mnaangaliwa na Watanzania wote, vituko vyenu hapa kila Mtanzania anawaoneni. (Makofi)

Msifanye vituko, tunahesabu kura. Mwenye maslahi ya hela ni nani hapa? Waheshimiwa, waliowapigia kura wanawaona mnavyofanya vituko, haya!

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie.

MWENYEKITI: Hakuna kumaliza, nimekuambia kazi tunayoifanya sasa ni kuhesabu kura.

MBUNGE FULANI: Tunaminywaaa!

(Hapa zoezi la kupiga kura lilimalizika na kura zilihesabiwa)

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaendelea na maelezo. Idadi ya Wabunge wanaopaswa kuwemo ndani ya Bunge hili kama wote tungejaa humu ndani, tunatakiwa kuwa 350, ambao hawapo humu ndani leo ni 128. Kwa hiyo, waliosema “Ndiyo” ni 69, waliosema “Siyo” ni 152. Kwa hiyo, waliosema “Siyo” wameshinda. (Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

(Hoja ya Mheshimiwa Tundu A.M. Lissu ilikataliwa na Bunge)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Kifungu cha 51

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 51 kinahusu Kamati za Maadili ya Maafisa wa Kimahakama za Wilaya na Kifungu Kidogo cha Kwanza kinazungumzia composition ya Kamati hiyo na katika kipengele (a) imemweka Mkuu wa Wilaya ambaye atakuwa Mwenyekiti, kipengele (c) kimemweka

70 Katibu Tawala wa Wilaya ambaye atakuwa Katibu, kipengele (d) kimeweka Wajumbe wawili walioteuliwa na Mkuu wa Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inapendekezwa kwamba kipengele (a) kifutwe chote, Mkuu wa Wilaya aondolewe badala yake awekwe Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania atakayekuwa Mwenyekiti. Inapendekezwa vilevile Katibu Tawala aondolewe nafasi yake ichukuliwe na mwakilishi wa Law Socciety. Inapendekezwa kipengele (d) kiondolewe na badala yake awekwe Wakili wa Serikali Mfawidhi au mwakilishi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkuu wa Wilaya ni Mwakilishi wa Rais katika Wilaya, ni sehemu ya Serikali, ni sehemu ya Executive. Vilevile kwa mila na desturi za Chama cha Mapinduzi, Mkuu wa Wilaya ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM kwenye Wilaya. Ni makada wa CCM. Wawakilishi wake atakaowateua atateua makada wa CCM. Kwa hiyo, kumweka Mkuu wa Wilaya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mahakimu katika Wilaya ni kuingiza siasa katika masuala ya nidhamu za Maafisa wa Kimahakama. Ni kukiuka miiko wa mgawanyo wa madaraka, ni kukiuka miiko ya uhuru wa Mahakama ambayo yote yanalindwa na kuheshimiwa na Katiba yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wanasiasa, Wakuu wa Wilaya, makada wa CCM au makada wa CHADEMA siku tutakapoiondoa CCM madarakani, wanatakiwa wafanye kazi za kiutawala, wasiingilie kazi za kinidhamu za Maafisa wa Mahakama. Masuala ya kinidhamu ya Kimahakama yafanyiwe kazi kwa taratibu za Kimahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki si kitu kigeni. Katika taaluma nyingi zinazotambuliwa na Sheria zetu, masuala ya kinidhamu ya taaluma hizo yanashughulikiwa ndani ya taaluma. Ndiyo maana masuala ya kinidhamu ya Mawakili yanashughulikiwa na Kamati ya Mawakili. Masuala ya kinidhamu ya ma-Engineer yanashughulikiwa na Bodi za ma-Engineer. Masuala ya kinidhamu ya Madaktari yanashughulikiwa na Medical Council of Tanzania na ya Wafamasia hivyo hivyo na taaluma zote. Masuala ya kinidhamu ya Wabunge, yanashughulikiwa ndani humu, hatujawahi kumleta Mkuu wa Mkoa. Kwa hiyo, naomba integrity, independency and impartiality ya Mahakama ilindwe kwa kuwazuia wanasiasa kuingia katika masuala ya kinidhamu ya taaluma ambazo hawazijui na haziwahusu. (Makofi)

TAARIFA

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Taarifa Mheshimiwa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Mtajadili tu kama mnataka kujadili, haya Taarifa lakini alikuwa hajamaliza…

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Naenda kwa Vifungu Mheshimiwa Mwenyekiti. Taarifa yangu naitoa kwa mujibu wa Kanuni ya 68(8), ambayo inasema kwamba wakati Mbunge anachangia naweza na mimi nikatoa Taarifa yangu.

71

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejaribu kufuatilia mwenendo mzima wa shughuli yetu hii ya Muswada na pia kwa hoja ambazo tunaletewa na upande wa pili na Mheshimiwa Tundu Lissu. Nimejaribu pia kuangalia katika mazingira yetu ya maeneo tunayotoka na uwakilishi wetu mpana kwa wananchi na wajibu wa Serikali iliyopo madarakani katika kulinda amani na haki za wananchi wake katika sehemu zote zinazotolewa haki pamoja na kazi za kawaida…

MWENYEKITI: Naomba Taarifa sasa.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Taarifa yangu, naona pamoja na kwamba Mtoa Hoja anajaribu kusisitiza masuala ya siasa yasitumike vibaya katika mazingira yetu ya kazi mbalimbali za wananchi lakini naona hapa ameamua kwa makusudi kuuza siasa zake za CHADEMA na kupoteza muda wa Wabunge…

WABUNGE FULANI: Umepotea! Umechemsha!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu endelea...

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, inaelekea Mheshimiwa Stella Manyanya hajui kitu kinachoendelea humu ndani, nitamsamehe.

MBUNGE FULANI: Hajui kabisa, mkiritimba!

MWENYEKITI: Nakataa Taarifa tu kwamba sikubali, sasa wewe vipi tena?

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, umesema kwamba wala hajatoa Taarifa yoyote na mimi wala sihitaji kusema kitu, naomba niendelee. Nilikuwa nasema kwamba hawa watawala, Wakuu wa Wilaya, Makada wa CCM wasiingizwe katika Kamati ya Maadili ya Kimahama. Hiyo wala siyo hoja ya CHADEMA, ni utendaji mzuri wa shughuli za Kimahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zamani tulikuwa na Bodi za Nidhamu za Mahakama ambazo zilikuwa na Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, tukaziondoa kwa sababu Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaingiza siasa kwenye mambo ya kitaaluma, wanavuruga. Sasa Muswada huu unapendekeza kuwarudisha, naomba isikubaliwe, badala yake mapendekezo ambayo nimeyaleta, tuweke Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mahakimu Wilayani awe Msajili wa Mahakama Kuu na vilevile Chama cha Mawakili ambao wanajua mila na desturi na miiko ya Kimahakama waingizwe na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayo inafahamu mila, desturi, sheria na maadili ya Kimahakama vilevile iingizwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Upande wa Serikali, hii inafanana na ile nyingine.

72 MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimwa Mwenyekiti, hili jambo linalojadiliwa sasa hivi linafanana na lile ambalo tumelipigia kura lakini pia naomba kutoa taarifa kwamba Sheria ilivyo sasa ndivyo hivi ilivyo kwenye Muswada sio kwamba tunaleta kitu kipya. Mheshimiwa Tundu anafahamu kwamba Sheria inakua, Sheria inazeeka, Sheria inajirudia, kwa hiyo, ukifika wakati muafaka tutafanya utaratibu kama huu anaopendekeza, tusiwe kama tunaishi kwenye dunia nyingine. Kwa hiyo, mimi naomba tu Kamati yako ikatae lakini kwa heshima mapendekezo ambayo Mheshimiwa Tundu anayatoa kwa sababu yanafanana na yale ya kwanza.

Mhshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu, punguza maneno kwa sababu muda umepita, Mheshimiwa Tundu Lissu.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Mwanasheria Mkuu wa Serikali anasema muda muafaka utakapofika, huu ni muda muafaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunatunga Sheria ya Utawala wa Mahakama inayoleta mapendekezo ya namna ya kushughulikia nidhamu za Maafisa wa Kimahakama, huwezi ukasema huu si muda muafaka. Ni muda gani huo kama sio huu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya msingi ni kwamba tunahitaji kulinda integrity, independency na impartiality ya Mahakama zetu. Tunahitaji to keep politicians pembeni ili Mahakama zifanye kazi za kutenda haki kufuatana na Sheria bila woga wala upendeleo, bila woga wa Wakuu wa Mikoa na Waku wa Wilaya, ndiyo hoja iliyoko hapa, ndiyo pendekezo langu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema Waheshimiwa Wabunge wa upande wa pili mnapopiga kura hii fikirieni kwamba mnatunga Sheria hii kwa ajili ya Watanzania sio kwa ajili ya CHADEMA, ni kwa ajili ya wananchi wanaotuangalia nje. Tupige kura ili tuamue kwa ajili ya integrity ya mfumo wetu wa utawala. Kwa hiyo, ndugu zangu, naomba mapendekezo ambayo nimeyaleta yakubaliwe, nashukuru sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Sasa tuamue hoja hii.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

(Hoja ya Mheshimiwa Tundu A.M. Lissu ilikataliwa na Bunge)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

73 MWONGOZO WA SPIKA

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!

MWENYEKITI: Hakuna Mwongozo.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mwongozo wako endapo Bunge linapitisha Sheria inayokiuka Katiba…

MWENYEKITI: Kwa hiyo, tunaendelea, huo Mwongozo utaniambia mwishoni nikimaliza kazi hii, haya tunaendelea.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti…

MWENYEKITI: Tunapitia Vifungu, hakuna biashara nyingine hapa.

Kifungu cha 52

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Najua wanaotaka tupitishe mambo kiharaka haraka wanakwazika lakini nielezee mapendekezo ambayo napendekeza katika Kifungu cha 52 cha Muswada huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 52 kinaunda mfuko wa Mahakama na Kifungu Kidogo cha Pili kinasema kwamba fedha za mfuko wa Mahakama zitapelekwa kwenye Mfuko huo na Treasury. Pendekezo langu ni kuingiza maneno “not exceeding three percentum of the total Government Budget of the fiscal year concerned,” between the words money required appearing in subclause 2.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo la pili linasomeka, “by deleting the word “Chief Court Administrator” and substuting for them the word “Commission.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo la tatu linasomeka, by deleting the phrase “subject to the requirements of Part V of the Government Loans Guarantees and Grants Act and The Public Finance Act” and substuting for them the following phrase, “paid directly into the Juduciary Fund.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na la kwanza. Kama pendekezo langu litakubaliwa, hicho Kifungu Kidogo cha Pili kitasomeka, “Subject to the provisions of the Constitution, the sums of money not exceeding three percentum of the total Government Budget of the fiscal year concerned required for purposes of the judiciary shall be paid by the Treasury into the Judiciary Fund.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu jana na leo, takwimu zilizoletwa mbele ya Bunge lako Tukufu, zinaonesha kwamba siku zote tatizo kubwa la Mahakama limekuwa ni fedha pungufu inazotengewa na Serikali. Mahakama haijawahi kupewa fedha kulingana na mahitaji yake. Sasa lengo la pendekezo hili ni kuweka kiwango kwenye Sheria

74 ambacho kitahakikisha kwamba kwa muda wote Mahakama zina fedha. Waheshimiwa Wabunge, wamesema tuweke 3% wengine 2%, kwa hiyo sio kitu ambacho hakina msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na inaweka ceiling ya ruzuku inayotolewa kwa ajili ya Vyama vya Siasa ya 2% ya recurrent budget ya Serikali na kwa sasa Vyama vya Siasa vinavyopata ruzuku hiyo ni vitano tu. Mahakama zetu zinashindwa kufanya kazi, Majaji wanashindwa kwenda kwenye sessions kwa sababu hawana fedha, tukiwatengea fedha katika Sheria, tukaweka kiwango, Majaji wetu watakuwa na fedha muda wote, haitawalazimu waende kuombaomba Hazina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana tumetoa takwimu hapa Majaji wetu hawalipwi mafao yao, Mahakimu hawalipwi mafao yao, Majaji wana madeni, Mahakama imekuwa ni mdeni mkubwa, deni la karibu bilioni ngapi sijui, tunawadhalilisha Majaji, tunadhalilisha Mahakama. Huu ni muda muafaka wa kuhakikisha kwamba Sheria hii inayounda Mfuko wa Mahakama iweke kiwango katika bajeti ya Taifa ya kila mwaka ambayo itakwenda kwenye mfuko wa Mahakama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo la pili linazungumzia Kifungu cha 52(3), ambayo imempa Mtawala Mkuu…

MWENYEKITI: Muda tayari, upande wa Serikali?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kwanza ni lazima niwe mkweli kwamba kuna hitilafu kwenye pendekezo la Mheshimiwa Mbunge, kwamba amount not exceeding 3% haikuhakikishii hicho unachokitaka, pengine ingekuwa ni vizuri kama ungetafuta wataalamu wanaojua kuandika Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, kama nilivyosema, Kamati hii haina data za kusema kwamba pato la Taifa na mahitaji ya Mahakama kwa sasa yatakidhiwa na hiyo asilimia ambayo Mheshimiwa Mbunge anapendekeza au asilimia yoyote ile. Nafikiri kinachoweza kusemwa na nafahamu kwamba pia kuna Mfuko wa Bunge ambao hauna asilimia kama hii ambayo inapendekezwa sasa, kwa sababu tumesikia, Serikali ilifanyie kazi jambo hili kwa ajili ya mifuko yote miwili, Mfuko wa Bunge pamoja na Mfuko wa Mahakama, ili kusudi tutakapofanya maamuzi yawe ni maamuzi ambayo yanaegemea kwenye tarakimu na ni maamuzi ya kisayansi. Nashauri marekebisho hayo yasikubalike. (Makofi)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, si kweli kwamba hakuna data zinazoonesha mahitaji ya Mahakama. Kama Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali angeangalia taarifa mbalimbali ambazo zimezalishwa na Mpango wa Kurekebisha Sekta ya Sheria, angeona kuna study zimefanyika zinazoonesha mahitaji ya

75 Mahakama vis-a-vis fedha ambazo zimekuwa zinatolewa na ndiko tulikotoa takwimu ambazo upande wa Serikali wenyewe wamezikubali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii habari ya kusema kwamba hakuna taarifa, ni maneno ya watu ambao hawasomi. Legal Sector Reform Program imefanya kazi kubwa ya kuonesha upungufu uliopo katika funding ya Mahakama. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, itakuwa ni vizuri nikushauri ukaangalie taarifa hizo, zipo hata kwenye mtandao, kama hujui namna ya ku-google unaweza ukafundishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, fund ya Political Parties chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ilifanywa bila studies. Bunge lilipoletewa hoja kwamba Vyama vya Siasa vinahitaji ruzuku, hakuna aliyeuliza kwamba study ziko wapi. Leo Mahakama ambayo ni mhimili wa dola, inahitaji ipate fedha za kutosha, imekuwa haipewi fungu la fedha ambazo zinalingana na mahitaji yake, wanasema hakuna study; wakati hawajasoma taarifa wanazozalisha kwenye shughuli zao wenyewe. Kwa hiyo, mnachotaka kusema Vyama vya Siasa ni bora kuliko Idara ya Mahakama? Ni arguments gani hizi! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni hii 3%, bajeti ya mwaka jana…

(Hapa Kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Haya tunaendelea na kuamua hoja hii.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

(Hoja ya Mheshimiwa Tundu A.M. Lissu ilikataliwa na Bunge)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naomba tufanye uamuzi wa kuendelea mpaka tutakapomaliza shughuli hii, Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, naomba utoe Hoja ya kuendelea kufanya kazi mpaka tumalize shughuli zilizoandaliwa, ni Kanuni ya 28.

KUTENGUA KANUNI ZA BUNGE

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, naomba Bunge lako Tukufu likubali kutengua Kifungu

76 cha 28 cha Kanuni za Bunge ili shughuli zilizopo mbele yetu pamoja na Hotuba ya Kufunga Bunge hili, ziweze kukamilika.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Bunge liliafiki Hoja ya Kutengua Kanuni za Bunge ili kuongeza muda mpaka shughuli zilizopangwa zikamilike)

KAMATI YA BUNGE ZIMA

Kifungu cha 53

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)

Kifungu cha 54 Kifungu cha 55 Kifungu cha 56

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Kifungu cha 57

MWENYEKTI: Mheshimiwa Tundu Lissu!

MBUNGE FULANI: Duh! Huyu bwana hachoki?

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mtu amesema, wewe huchoki…

MWENYEKITI: Naomba uendelee, acha kusikiliza maneno, mimi niko hapa.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, this is a legislative business at its best.

MWENYEKITI: Naomba usiwasikilize, wewe fanya kazi yako.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kifungu cha 57(3), kina maneno yanayosema, “The Chief Court Administrator shall prepare the

77 estimate for the Judiciary within the funding requirements for the relevant fiscal year.” Inapendekezwa hayo maneno, “Within funding requrements for the relevant fiscal year,” yaondolewe na badala yake maneno yafuatayo yawekwe “in accordance with the needs of the administration of the judiciary service for the relevant fiscal year.” Iwapo mapendekezo haya yatakubaliwa, Kifungu cha 57(3) kitasomeka, “The Chief Court Administrator shall prepare the estimate for the Judiciary in accordance with the needs of the administration of the judiciary service for the relevant fiscal year.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo hili lina lengo la kuhakikisha kwamba bajeti ya Mahakama inatokana na mahitaji ya Mahakama. Lengo hili linapendekeza kuondoa kizingiti kikubwa katika funding ya Mahakama ambacho kimekuwepo miaka yote, ukomo wa bajeti. Kama tulivyoonesha kwenye takwimu zetu, funding ya Mahakama, siku zote wanaambiwa ukomo wa bajeti. Wakishapewa ukomo wa bajeti, wakapeleka mahitaji yao na huo ukomo wa bajeti nao hauzingatiwi, Serikali inaweka ukomo wa bajeti ambao vilevile haiuheshimu.

KUHUSU UTARATIBU

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Afrika Mashariki!

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Nampongeza Mheshimiwa Tundu Lissu, ana mawazo mazuri sana na pengine katika mchakato unaokuja wa kujadili Katiba, huyu atakuwa ni mtu muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tulivyo sasa hatuwezi, haturuhusiwi kabisa na Ibara ya 99 ya Katiba ya nchi, kukubali mapendekezo yoyote ya mabadiliko au ya kutunga sheria ambayo yanakiuka Ibara hii ambayo inasema hivi, “The National Assembly shall not deal with any of the matters to which, this Article relates.” na mojawapo ni imposition of any charge…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, naomba tukupe ile ya Kiswahili.

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ibara ya 99 inasema, “Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika na Ibara hii...” Mojawapo ni “kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au Mfuko wa Serikali mwingine wowote au kubadilisha kiwango hicho kwa namna nyingine yoyote, isipokuwa kupunguza”. Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo analolitoa Mheshimiwa, lina mwelekeo wa kuweza kubadili kabisa ukomo wa bajeti kwa sababu tunachoruhusiwa kujadili humu ni kwamba bajeti ikishapangwa, hatuwezi kupitisha Azimio lolote au kutunga sheria ambayo itapitiliza ukomo uliowekwa katika bajeti. Kwa hiyo, tutajitahidi kuisaidia Mahakama lakini hatuwezi kuvunja Katiba iliyopo, hata kama ni mbovu, ahsante. (Makofi)

78 MWENYEKITI: Mimi sasa namwomba Mheshimiwa Tundu Lissu amalize kusema yale aliyokuwa anayasema. Si ulikuwa unazungumza bado?

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Ndio!

MWENYEKITI: Ndio nakwambia uendelee.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nilikuwa nasema kwamba tatizo kubwa ambalo tumelithibitisha kwa takwimu za Serikali ni kwamba ukomo wa bajeti ambao Mahakama siku zote inawekewa, hauheshimiwi na Serikali. Inaambiwa ukomo wenu ni huu, halafu inapewa fedha pungufu ya ukomo huo. Ukomo hauzingatii mahitaji halisi ya Mahakama na vilevile hauheshimiwi. Sasa ili kuhakikisha kwamba Mahakama zinapata fedha kufuatana na mahitaji yao, kufuatana na mahitaji mahsusi ya Mahakama, inapendekezwa kwamba bajeti itakayotungwa na Mahakama izingatie mahitaji halisi ya Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikiliza hoja ya Mheshimiwa na niseme for the record…

MWENYEKITI: Ni Waziri wa Afrika Mashariki.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ni Waziri wa Afrika Mashariki. Nimesikiliza hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Afrika Mashariki na niweke for purposes of record, ninamheshimu sana na anaheshimiwa sana na Waheshimiwa Wabunge na nchi hii lakini pamoja na heshima zote ambazo ninazo kwa Mheshimiwa Samuel Sitta, naomba nitofautiane na yeye juu ya uelewa wake wa Ibara ya 99. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti...

MWENYEKITI: Nakupa dakika moja tu, maana yeye alikuwa na dakika moja tu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, alinizuia kumaliza hoja yangu.

MWENYEKITI: Sasa nimekuongezea dakika moja.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ibara ya 99(2)(a)(ii) inazungumzia utaratibu pale ambapo Bunge linabadili bajeti, hili siyo Bunge la Bajeti, hapa tunaweka utaratibu wa namna ya Mahakama kutengeneza mambo yake ya fedha, hatujadili bajeti, ndiyo maana hakuna hata mmoja hapa aliyekuja akasema Mahakama ipewe bilioni 100 au mia mitano au ipewe shilingi sifuri. Hoja anayoisema

79 Mheshimiwa Waziri wa Afrika Mashariki ingekuwa na nguvu kama tungekuwa tunazungumzia viwango vya fedha lakini hatuzungumzii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mapendekezo yangu ambayo lengo lake ni kuziwezesha Mahakama kutengeneza bajeti zao kulingana na mahitaji yao halisi likubaliwe na Bunge lako Tukufu, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Waziri, kwa niaba ya Serikali unajibu hata wewe.

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Najua Mheshimiwa Tundu Lissu anajitahidi sana kujenga hoja, lakini asikilize hoja za Wanasheria wazoefu kama mimi, mimi si mtu wa kukurupuka na kusimama hapa kusema kitu cha ovyo hata siku moja, nina rekodi nzuri kabisa. Ibara hii ipo katika eneo linaitwa utaratibu wa kutunga sheria, hapa tunatunga sheria siyo tunaidhinisha bajeti, ipo hapa, soma Ibara ya 97, 98 yapo mambo ya kubadili Katiba. Sasa hapa kuna mambo tunakatazwa wakati wowote hatuwezi kuyakiuka siyo wakati wa bajeti tu. Tunaambiwa sisi hapa Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo haya, haikusema wakati wa bajeti, hayo ni maneno ambayo unayaweka wewe labda ulete mabadiliko ya Katiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama unaambiwa hutashughulikia jambo lolote linaloagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina na mfuko mwingine wowote, kubadilisha viwango kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza, tunaruhusiwa tu kupunguza. Mimi naheshimu sana Mahakama na nakubali Waziri wa Katiba na Sheria katika bajeti tutawaongezea Mahakama na ndiyo maana ya kuwa na Mfuko wa Mahakama. Mimi nina hakika kama ulivyokuwa ule wa Bunge, tutawaongezea. Lakini jamani Katiba iko wazi hapa hata kama hatuipendi kwa sasa na ndiyo maana Rais ameleta Muswada ambao tumeuleta hapa na utaendelea kujadiliwa mwezi wa sita ili tubadili baadhi ya mambo lakini kama Wanasheria lazima tukubali Katiba inasema nini. Naomba Mwenyekiti tuendelee tusipoteze muda na jambo ambalo litatuingiza kwenye matata. (Makofi)

MWENYEKITI: Zaidi ya hapo mwenyewe huyu anayesema, ameifanyia sana kazi Article ya Katiba anayoizungumzia, aliifanyia sana kazi kwenye Mfuko huu wa Bunge ndiyo maana anasema kwa uhakika, Mheshimiwa Tundu Lissu. (Makofi)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, namheshimu sana Mheshimiwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, lakini kwenye jambo hili, is dead wrong.

MWENYEKITI: Huna haja ya kuhamaki Mheshimiwa Lissu, tumia busara tu kuelezea.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema namheshimu sana Mheshimiwa Waziri wa Afrika Mashariki lakini hapa amekosea moja kwa moja. Pendekezo langu linahusu namna Mtawala Mkuu wa Mahakama atakavyotengeneza

80 bajeti, halizungumzii kwamba hela italipwa kutoka kwenye Mfuko wa Hazina, Mfuko Mkuu wa nini, haizungumzii figures. Kwa hiyo, Ibara ya 99 inayohusu utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha haihuisiki. Ni Mwanasheria wa siku nyingi, mzoefu sana, amekuwa Waziri wa Sheria ni kweli kabisa lakini hapa amekosea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, tuweke utaratibu wa Mtawala Mkuu wa Mahakama kuandaa bajeti ya Mahakama kulingana na mahitaji ya Mahakama. Mnataka aandae bajeti kulingana na kitu gani kama sio mahitaji ya Idara ya Mahakama, kama si kwa kulingana na mahitaji ya taasisi hiyo anayoisimamia, ndiyo pendekezo langu hapa. Kwa hiyo, naomba pendekezo langu likubaliwe na kwa sababu bado nina muda ninajua litapigiwa kura kama ambavyo tumeona hapa ijulikane nani wanaotetea Mahakama zetu, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Hilo halipo. KUHUSU UTARATIBU

MWENYEKITI: Kuhusu utaratibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mtoa Hoja anaweza kuwa ana nia nzuri na ndiyo utaratibu kila Afisa Masuuli katika bajeti yake anatakiwa kupeleka bajeti halisi ya mahitaji yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, si jambo la Msajili wa Mahakama au Court Administrator peke yake, kila Katibu Mkuu anapeleka mahitaji halisi ya Wizara yake na hilo analolisema Mheshimiwa Mbunge ni sahihi, hiyo ni kazi ya Court Administrator kupeleka mahitaji yake. Hata Bunge, Katibu wa Bunge anapeleka mahitaji yake, kwa hiyo, ni kazi za kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunachokisema hapa haiwezekani kila Afisa Masuuli, maana huyu Court Administrator sasa atakuwa ndiyo Afisa, haiwezekani kila Afisa Masuuli apate kulingana na mahitaji yake. Kwa hiyo, ukiweka kwenye Sheria hii maana yake unalazimisha kila kitakachofanywa au mahitaji yote kwa kadri ya mahitaji ya Mahakama lazima yawe funded, hapana, nchi hii tunakwenda kulingana na uwezo tulionao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni mjumbe wa Tume ya Bunge kama alivyo Kiongozi wa Upinzani Bungeni, tunajua hata sisi hapa Bungeni hatuendi kulingana na mahitaji yetu, Wizara zote haziendi kulingana na mahitaji yao. Hoja hapa iwe nia njema ya Serikali ya kuleta Muswada huu udhihirishwe kutokana na namba ya pesa zitakazoongezeka kulingana na uwiano katika bajeti hii. Mheshimiwa mtoa hoja angesema haina maana kutunga mfuko huu na kiwango cha pesa kikabaki kilekile, basi this time kwa mfuko huu, Mahakama zipewe fedha za kutosha na ndiyo hoja amekuwa anasisitiza Mheshimiwa Mbunge na ndiyo hoja ya Waheshimiwa Wabunge wote,

81 walikuwa wanasisitiza kutokana na shida na Serikali inajua umuhimu wa Mahakama na inayo nia hiyo hiyo lakini haiwezekani tukaweka kwenye Sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda nikupe tu taarifa, tunaweza tukatoa mfano kwa sheria tuliyokwishakuitunga ya Vyama vya Siasa, sio kwamba tulichokifanya, inawezekana tulifanya kwa wakati ule pengine tunaweza kuwa tulikosea vilevile, hata vyenyewe tunawapa sio kwa asilimia mbili ambayo wamesema, hatujawahi kupata hata asilimia moja Vyama vya Siasa, kwa sababu hakuna uwezo. Sasa kwa nini tusichukue ile experience ya mwanzo badala ya kuweka tu namba ya kujifurahisha wakati hatuwezi kutekeleza, twende kwa hali halisi. (Makofi)

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, mimi namuunga mkono kwamba Chief Administrator aandike mahitaji halisi ya bajeti yake lakini uwezo ndiyo uta-determine na bila shaka Serikali itaangalia uwezo wake katika bajeti ijayo ili kuwezesha Mahakama zetu zifanye kazi kama nia ya Wabunge wote sio nia ya mtoa hoja kama alivyosema kwamba aweke rekodi wao kwamba ndiyo waonekane wanatetea Mahakama, ni nia ya Bunge lakini nia ya Serikali ndiyo maana imeleta Muswada huu. (Makofi)

MWENYEKITI: Tunaendelea, hakuna kipya, tunabishana tu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ndiyo mwenye hoja, siyo Serikali.

MWENYEKITI: Ilikuwa taarifa hiyo, basi nampa nafasi huyu lakini tunaendelea tunabishana kitu ambacho kipo.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kukataliwa)

(Hoja ya Mheshimiwa Tundu A.M. Lissu ilikataliwa na Bunge)

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Kifungu cha 58

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja marekebisho yake)

Kifungu cha 59 Kifungu cha 60 Kifungu cha 61

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

82

Kifungu cha 62 Kifungu cha 63

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)

Kifungu cha 64

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Kifungu cha 65

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja mabadiliko yake)

Kifungu cha 66

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Kifungu cha 67

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)

Kifungu cha 68 Kifungu cha 69

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Jedwali la 1

(Jedwali lililotajwa hapo juu lilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)

Jedwali la 2 Jedwali la 3

(Majedwali yaliyotajwa hapo juu yalipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Jedwali la 4

83

(Jedwali lililotajwa hapo juu lilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kitita hiki cha marekebisho, ukurasa wa nane, kuna ile fifth schedule...

MWENYEKITI: Ukurasa gani?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Ukurasa wa nane wa Serikali, fifth schedule isomeke forth schedule.

MWENYEKITI: Schedule zile tumeshapitia.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Bunge lilirudia)

Muswada wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama wa Mwaka 2011 (The Judiciary Administration Bill, 2011)

(Kusomwa Mara ya Tatu)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa kwamba Kamati ya Bunge Zima imeupitia Muswada wa Uendeshaji wa Mahakama wa Mwaka 201I yaani The Judiciary Administration of 2011, Kifungu kwa Kifungu na kuupitisha pamoja na marekebisho yake. Hivyo naomba kutoa hoja kwamba Muswada huu sasa ukubaliwe na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Muswada wa Sheria ya Serikali Ulisomwa Mara ya Tatu na Kupitishwa na Bunge)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa mara nyingine tena, niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa kazi nzuri mliyofanya kupitia Muswada huu na pia niishukuru Kamati ya Sheria ndogo kwa kutumia muda mwingi sana kupitia Muswada huu na wadau mbalimbali walioshikiri katika Muswada. Niwashukuru kwa namna ya pekee Waheshimiwa Wabunge kwa kazi ya kupitia Muswada kwa kuandika sio kupitisha Vifungu. Kwa hiyo, tunakushukuru sana Mheshimiwa Tundu Lissu, ndiyo kazi yako na

84 inakupendeza na ndiyo maana ya kutunga sheria, mbishanie Vifungu, mkikubaliana, mnakubaliana, kwa hiyo, tunashukuru kwa hilo. (Makofi)

Lakini lingine ambalo napenda niishukuru ni kwamba kitendo cha kukubali kwamba tupige kura kimeonyesha kwamba tunafika mahali watu mnaondoka wakati kazi haijaisha, kati ya Wabunge 350, 128 walikuwa hawapo, kwa hiyo, kama ingekuwa ni suala zito kama la kupitisha Katiba hapa ingekuwa shughuli. Kwa hiyo, napendekeza kwamba Wabunge tunapofika Bungeni usianze kufanya assumption kwamba labda hakuna kazi, kila mtu ana kazi ya kutunga sheria hapa.

Lakini pia napenda kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge kama ninavyoomba siku zote hapa, ni kauli yako na kuna taratibu zetu tumeziweka, hamaki hamaki hapa mnakuwa kama mpo sokoni haipendezi, tuna utaratibu wetu. Hili nalisema kwa Wabunge wote sio Wabunge wa upande mmoja ni Wabunge wote tunatawaliwa na hii Kanuni na zaidi ya hapo tuelewe kwamba tunapofanya kazi yetu hapa wananchi wanatuangalia, kwa hiyo, wanakuona kila Mbunge unafanya kitu gani hapa. (Makofi)

Sasa mimi nasema huu Mkutano wa Tatu, nikipima mafanikio kati ya Mkutano wa Pili na wa Tatu, kuna maendeleo mazuri, tuendelee kufanya hivyo, tuna Wabunge vijana wengi sana, heshima yenu itapatikana kama mtafuata taratibu. Lakini kama mkifanya bila kufuata taratibu, heshima yenu itashuka. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, naomba sana tutakapokuwa tunapumzika sasa mpaka Bunge la Bajeti tuweze kushika Kanuni, inatoa heshima maana vitu vingine tunavyofanya kelele, fujo, hazitoi matunda yanayostahili, stahili yetu hapa ni kutunga sheria na kuwaacha Watanzania watufuatilie tunafanyaje, lakini tunapofika mahali tunafanya vitu vyetu vya ovyo, haiwasaidii wananchi wala sisi wala kutunga sheria. Kwa hiyo, nawashukuru sana kwa kazi mliyofanya na kama nilivyosema Bunge bado jipya, tunaendelea kujifunza na mimi nitakuwa mvumilivu kwa sababu najua nina kazi ya kuwafundisha.

Suala la Mheshimiwa Lema ambaye wakati ule nilimwambia atoe maelezo, kama nilivyoeleza wakati ule Mheshimiwa Lema alitoa maelezo na mimi nimeyapeleka kwenye Kamati yangu na wamenipa matokeo. Lakini kutokana na kazi zilivyokuwa nyingi hapa sikupenda tena kutumia muda wa kusoma uamuzi wangu ingechukua muda mrefu. Kwa hiyo, kikao kinachokuja itakuwa kitu cha kwanza.

Vilevile Waheshimiwa Wabunge wengine walikuwa wanapenda kuingia kwenye maelezo binafsi lakini mpaka tulipofikia hapa wakawa hawawezi kupata nafasi hiyo kutokana muda tulionao. Lakini maelezo mengine binafsi hayaharibiki hata wakisubiri tutakapokuja, ni maelezo ambayo ni ya mfumo kidogo tunaweza kuendelea nayo wakati ujao. Ndiyo sababu hatukuwa na hoja binafsi lakini tulikuwa na maombi ya hoja binafsi, ni Adjourning Motion, kwa hiyo, kama nilivyosema tunaweza tukayarejea kipindi kinachofuata.

Baada ya kusema hayo, nawashukuru tena kama nilivyosema kwa kazi nzuri mliyofanya, Katibu!

85 KATIBU MEZANI: Naomba kutoa taarifa kwamba shughuli zilizopangwa katika Mkutano huu wa Tatu wa Bunge sasa zimekamilika.

SPIKA: Ahsante. Kabla sijamwita Mheshimiwa Waziri Mkuu, leo jioni saa 1.30 kutakuwa na tafrija ya Wabunge, inaitwa Usiku wa TDL, ni Tanzania Distillers Limited katika viwanja vya Bunge. Kadi za mwaliko zitatolewa kwa Wabunge wote, hata kama hujapata kadi unakaribishwa. Kutakuwa na burudani za bendi za Sikinde, Taarab na miziki ya kileo, nafikiri Mr. II leo ndiyo kwake huko. (Kicheko)

Pia Wanachama wa CCM mnajulishwa kwamba mara baada ya kikao cha uchaguzi wa CPA kutakuwa na kikao katika ukumbi wa Pius Msekwa, naomba tufike pale tufanye kazi moja fupi sana.

Mheshimiwa Waziri Mkuu!

HOJA YA KUAHIRISHA BUNGE

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, leo tunahitimisha shughuli zilizopangwa kwenye Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kufikia sehemu hii ya leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tangu tulipohitimisha Mkutano wa Pili wa Bunge hili, nchi yetu imekumbwa na wimbi la majanga mbalimbali yakiwemo ya mafuriko na ajali za barabarani. Majanga hayo hususani ajali za barabarani zimesababisha vifo vingi vya Watanzania wasio na hatia. Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi, amina!

Mheshimiwa Spika, mbali na vifo hivyo majanga hayo pia yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali na hasara kwa watu binafsi na Taifa kwa ujumla. Nitumie fursa hii kutoa pole kwa Watanzania wote walioguswa na majanga haya na waliopata majeraha katika ajali hizo. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki na Mungu awape ndugu jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao moyo wa subira na nguvu ya kuhimili wakati huu mgumu. Kwa wale walioumia na bado wanajiuguza namuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe kupona haraka na kurejea katika shughuli zao.

Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kutoa wito kwa wenye vyombo vya moto kuwaajiri madereva wenye uzoefu na ambao muda wote wanatambua kuwa wamebeba roho za watu. Kwa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Sheria ninatoa wito wa kutumia Sheria, Kanuni na taratibu kutoa adhabu kali kwa madereva wote wazembe. Ninaamini kila mtu kuanzia mwenye gari, kondakta, dereva, abiria na Jeshi la Polisi tutazuia ajali zisizo za lazima na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kuwapongeza Waheshimiwa Jenista Mhagama, Mheshimiwa George Simbachawene na Mheshimiwa Sylvester Mabumba

86 kwa kuchaguliwa kuwa Wenyeviti wa Bunge. Vilevile nawapongeza Waheshimiwa Benardetha Mushashu, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, Mheshimiwa , Mheshimiwa na Mheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa kwa kuchaguliwa kuwa Wajumbe wa Bunge la Afrika yaani PAP na ninawapongeza pia Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya na Mheshimiwa Dkt. Titus Kamani kwa kuchaguliwa kuwa Wajumbe wa SADC. Mwisho lakini siyo kwa umuhimu nampongeza Mheshimiwa Anastazia Wambura kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa APRM na Mheshimiwa Martha Umbulla, tunawapongeza sana. (Makofi)

Kwa maoni yangu ninaamini kuchaguliwa ni jambo moja na kutekeleza majukumu yaliyo mbele yenu kwa ufanisi ni jambo lingine. Changamoto iliyo mbele yenu ni katika kutekeleza wajibu wenu kwenye vyombo mlivyochaguliwa na manufaa ya Tanzania. Nawatakia wote mafanikio mema katika kuiwakilisha nchi yetu kwenye vyombo hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika mkutano huu maswali 113 ya msingi na 240 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa. Vilevile jumla ya maswali nane ya msingi na maswali matatu ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa Maswali ya Papo kwa Papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Majibu ya maswali hayo yameiwezesha Serikali kutoa ufafanuzi wa maeneo muhimu ambayo Waheshimiwa Wabunge walipenda kujua maendeleo na utekelezaji wake. Ninaamini kwa kupitia majibu hayo wananchi wameweza kujua mipango, mikakati na maamuzi ambayo Serikali imechukua katika kutekeleza majukumu yake hasa yale yanayochochea ukuaji wa uchumi na kuondoa umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu Bunge lako Tukufu limepitisha Miswada ifuatayo; Muswada wa Sheria ya Famasi wa mwaka 2010 yaani The Pharmacy Bill, 2010, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Maeneo ya Maendeleo ya Kiuchumi ya mwaka 2011 (The Economic Zones Laws Miscellaneous Amendments Bill, 2011), Muswada wa Sheria ya Utawala wa Mahakama wa mwaka 2011 yaani The Judiciary Administration Bill, 2011 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2011 yaani The Written Laws Miscellaneous Amendments Bill 2011. Vilevile katika Mkutano huu Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 yaani The Constitutional Review Bill, 2011 umesomwa kwa mara ya kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu Bunge lako Tukufu lilipokea, lilijadili na kisha kukubali mapendekezo na maoni yaliyomo kwenye taarifa za Kamati za Bunge kama zifuatazo; Taarifa ya Hesabu za Serikali, Taarifa ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Taarifa ya Hesabu za Mashirika ya Umma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mkutano huu pia uliridhia maazimio manne yafuatayo; Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa UNESCO wa Kulinda kwa Urithi wa Kiutamaduni Usioshikika wa 2003 yaani Convention for the Safeguarding of the Intangible Cultural Heritage 2003. Pili ni Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa UNESCO unaohusu Kulindwa na Kukuzwa kwa Uamuzi wa Kujieleza Kiutamaduni wa

87 2005 yaani The Convention and Protection and Promotion of the Diversity of Cultural Expressions 2005. Tatu ni Azimio la Kuridhia Itifaki ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yaani The Protocol and Science Technology and Innovation. Azimio la nne ni la Bunge Kurekebisha Mfuko wa Kutoa Mkopo yaani Advances Fund kwa Wabunge, Kuunda Mfuko wa Mikopo kwa Watumishi wa Serikali Kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla hali ya upatikanaji wa chakula nchini umeendelea kuwa wa kuridhisha, hadi tarehe 10 Aprili, 2011 Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ilikuwa na tani 212,003 za mahindi kufuatia ununuzi wa tani 181,0019 za mahindi sawa na 90.5% ya lengo tani 200,000 katika msimu wa mwaka 2010/2011 na akiba kutoka mwaka 2009/2010. Akiba hii ni kubwa kuliko iliyowahi kuwepo wakati wowote ule, hiki ni kiashiria cha utayari wa Serikali kukabiliana na matatizo ya upungufu wa chakula punde yatakapojitokeza nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naendelea kuzisihi Halmashauri nchini kupeleka maombi haraka katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maafa kuhusu maeneo yanayokabiliwa na tatizo la njaa ili yashughulikiwe mapema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na upungufu wa chakula, Serikali imefanya tathmini mbili, ya kwanza ambayo ni ya awali ilifanyika mwezi Septemba, 2010. Katika tathmini hiyo watu 123,430 walikuwa na upungufu wa chakula wa tani 13,760, chakula hiki kilishapelekwa kwa walengwa na tathimi ya pili ilifanyika mwezi Februari, 2011, tathmini hii ilionyesha kuwepo na watu 794,337 ambao walikuwa wanahitaji chakula cha msaada cha tani 15,460. Taratibu za kusambaza chakula hiki kwa wahusika zimeanza. Maeneo yenye upungufu huo ni katika Halmashauri 34 za Longido, Monduli, Ngorongoro, Bahi, Dodoma Mjini, Chamwino, Mpwapwa, Kongwa, Same, Mwanga, Mvomero, Babati, Kiteto na Simanjiro.

Mheshimiwa Spika, zipo pia Morogoro, Kwimba, Iringa, Lindi, Liwale, Ruangwa, Masasi, Nanyumbu, Manyoni, Kishapu, Shinyanga, Shinyanga Mjini, Meatu na Nzega. Wilaya nyingine ni Rombo, Manyoni, Lindi, Ruangwa, Liwale na Nzega.

Mheshimiwa Spika, kati ya Julai, 2010 na Machi, 2011 Serikali kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa yaani NFRA imekamilisha zoezi la kuhamisha tani 52,350 za mahindi kutoka maeneo yenye ziada ya Sumbawanga, Makambako na Songea na kupeleka kwenye maghala yaliyopo karibu na maeneo yenye upungufu wa chakula ya Dar es Salaam, Dodoma na Arusha kwa utayari wa kukabiliana na upungufu wa chakula. Aidha, kuanzia sasa hadi Juni, 2011 kiasi cha tani 13,500 za mahindi kitahamishwa kutoka Songea kwenda Dar es Salaam. Tani 10,000 zitahamishwa kutoka Mpanda kwenda Dodoma na tani 5,000 zitahamishwa kutoka Mpanda kwenda Shinyanga. Serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa hali ya chakula nchini kuhakikisha maeneo yote yenye tahadhari ya njaa yanapatiwa chakula kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Tanzania ina mazingira mazuri ya uzalishaji wa mazao ya nyuki yenye ubora wa hali ya juu kutokana na aina mbalimbali za mimea ambayo

88 hutumiwa na nyuki. Zaidi ya 50% ya mimea iliyopo hapa nchini ikiwemo misitu ya hifadhi huzalisha chakula cha nyuki kwa wingi, ufugaji wa nyuki unaweza kufanywa katika misitu yenye ukubwa wa hekta milioni 38.8 na kwenye maeneo ya mashamba ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mimea mingi iliyopandwa iliyoweza kuendeleza ufugaji nyuki, zaidi ya 90% ya mimea iliyopandwa inafaa kwa ufugaji wa nyuki. Mimea hii ni pamoja na alizeti, ufuta, mimea jamii ya kunde, matunda, katani, kahawa, migomba, mbogamboga, mahindi na kadhalika. Hivyo, inawezekana kuendesha ufugaji nyuki katika maeneo ya ardhi ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, Tanzania pia kuna fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya ufugaji nyuki hasa katika nyanja za viwanda vya kutengeneza vifaa vya ufugaji nyuki, viwanda vya bidhaa zitokanazo na nta, viwanda vya bidhaa zitokanazo na asali, viwanda na bidhaa zitokanazo na uchavushaji wa mazao ya kilimo, utalii wa ekojia na uwekezaji wa teknolojia katika mazao ya nyuki badala ya asali na nta. Haya ni baadhi ya maeneo ambayo ni fursa nzuri kwa uzalishaji wa bidhaa za zo la nyuki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ufugaji nyuki umetumika sana katika nchi za Afrika ambazo zimefanikiwa sana, nchi hizo ni Angola, Burundi, Cameroon na Afrika ya Kati. Nchi nyingine ni Chad, Ethiopia, Guinea, Guinea Bissau, Kenya na Madagascar. Kwa kuangalia uzalishaji wa asali duniani, nchi zinazoongoza kwa ufugaji wa nyuki ni China, Uturiki, Argentina, Marekani na Ukraine. Nchi nyingine ni Urusi, India, Mexico, Ethiopia na Spain. Tukiangalia faida wanayoipata nchi hizo nashawishika kusema kwamba Tanzania tunayo fursa kubwa sana kama tutaendeleza ufugaji wa nyuki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, inakadiriwa kuwa uzalishaji wa mazao ya nyuki nchini Tanzania unaweza kufikia takribani tani 138,000 za asali na tani 900,200 za nta kwa mwaka. Hii ni kutokana na idadi kubwa ya makundi ya nyuki yanayokadiriwa kuwa milioni 9.2 mikoa yote ya Tanzania inazo fursa za ufugaji nyuki. (Makofi)

Hata hivyo, maeneo ambayo sasa yanajishughulisha zaidi na uzalishaji wa mazao ya nyuki ni Wilaya 27 tu ambazo ni Lindi, Mpanda, Manyoni, Songea, Sikonge, Urambo na Chunya. Wilaya nyingine ni Iringa, Tabora, Bukombe, Kahama, Kibondo, Biharamulo na Nzega. Zipo pia Wilaya za maeneo ya Kasulu, Newala, Tunduru, Kondoa, Handeni, Kigoma na Singida. Wilaya nyingine ni Rufiji, Hai, Kiteto, Arumeru, Nkansi na Babati. Hii ni idadi ndogo ikilinganishwa na fursa na uwezo uliopo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sasa wastani wa tani 900,000 za asali zenye thamani ya shilingi bilioni 18 huzalishwa nchini kwa mwaka, kwa upande wa nta wastani wa tani 600,000 za nta zenye thamani ya shilingi bilioni tatu huzalishwa nchini kwa mwaka. Hii ni 6.5% tu ya uwezo wa uzalishaji wa jumla wa mazao ya nyuki kwa maana ya asali na nta. Matumizi madogo ya fursa hii yametokana na vipaumbele vidogo ambavyo sekta ya nyuki imekuwa ikipewa kwa kipindi kirefu. (Makofi)

89 Kwanza, Tanzania kuna viwanda vya kuchakata na kufungasha asali (processing and packaging) takriban saba. Viwanda hivyo ni Honey Care Africa (T) Ltd., Fidahusein Co. Ltd. na Tan Dairies vyote vya Dar es salaam. Vingine ni Lalan Agency na Jampem Enterprises vya Tabora, Yamahedo Food Health Company cha Arusha na Dabaga Food Processing cha Iringa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu masoko ya asali ya ndani na nje ya nchi, kwa upande wa masoko, wanunuzi wakuu wa asali ya Tanzania ni Kenya, Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Ubelgiji, Hispania na Italia. Aidha, wanunuzi wakuu wa nta ya Tanzania ni Japan, Uholanzi, Marekani, Ujerumani na Ufaransa. Katika soko la nje asali huuzwa wastani wa dola za Kimarekani 3.7 (shilingi 5,550) kwa lita moja. Kwa upande wa nta, bei ya wastani huuzwa dola za Kimarekani 4.5 (shilingi 6,750) kwa kilo. Hapa nchini asali huuzwa kwa bei ya wastani ya shilingi 8,000 kwa lita moja. Hivyo inaonyesha kuwa asali ina bei nzuri kwenye soko la ndani kuliko soko la nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, faida ya mazao ya nyuki ukilinganisha na ya kilito, ulinganifu wa mazao ya kilimo na ufugaji nyuki unaonesha faida kubwa kwa upande wa utumiaji nyuki. Kwa mfano, mkulima mwenye mtaji wa shilingi 150,000/= na akalima ekari moja ya mahindi na kupata magunia 10 kwa msimu kwa eka, kama akiuza mahindi hayo kwa shilingi 35,000/= kwa gunia atapata shilingi 350,000/= kwa msimu kwa mwaka. Mkulima wa mpunga kama atatumia mtaji huo na kulima ekari moja na kupata magunia 12, kama akiuza mpunga huo kwa bei ya shilingi 25,000/= kwa gunia atapata shilingi 300,000/= kwa msimu kwa mwaka. Mfugaji wa nyuki akitumia mtaji kama huo wa shilingi 150,000/= kwa kuwekeza mizinga 10 na kuvuna lita 15 kwa mzinga kwa msimu. Kama akiuza asali hiyo kwa hapa nchini kwa bei ya shilingi 8,000/= kwa lita atapata shilingi 1,200,000/= kwa msimu. (Makofi)

Kwa maeneo mengi ufugaji wa nyuki una misimu miwili ya mavuno. Hivyo, nfugaji huyu hata kama akiuza kwa shilingi 5,000 tu kwa lita hapa nchini atapata shilingi 750,000/= kwa msimu au shilingi 1,500,000/= kwa mwaka kwa misimu miwili. Kwa bei hizi ni dhahiri kwamba ufugaji wa nyuki una manufaa makubwa kwa mfugaji. Aidha, ufugaji wa nyuki huongeza ajira, kipato kwa mwananchi mmoja mmoja na huongeza Pato la Taifa kwa ujumla. Inakadiriwa kuwa kama kutakuwa na wafugaji milioni 1.5 ambao wanaweza kujiajiri kwenye ufugaji nyuki, hata kama ni kuwekeza mizinga kumi tu kila mmoja, mapato yake ni sawa na shilingi bilioni 1.8 kwa mwaka. Huu ni mchango wa kutambulika katika kuchangia Pato la Taifa na kupunguza umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu Kituo cha Utafiti wa Nyuki na Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), nimezungumza kwa kirefu kuhusu zao la asali na nta inayotokana na ufugaji nyuki. Hii ni kwa sababu, kwa maoni yangu, naona kuna fursa katika ufugaji nyuki ambazo hatujazitumia ipasavyo. Tarehe 31 Machi, 2011, nilitembelea Kituo cha Utafiti wa Nyuki kilichoko Njiro, Arusha. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 1973 kwa msaada wa Canadian International Development Agency (CIDA) kwa lengo la kuendeleza utafiti wa nyuki wa Tropikali ya Afrika. Mwaka 1980, Kituo hiki kiliunganishwa na Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori kilichoanzishwa kwa Sheria Na. 4 ya Wanyamapori ya mwaka 1980 ambacho kinajulikana kwa jina la Kituo

90 cha Utafiti cha Wanyamapori Tanzania – TAWIRI. Muungano huu ulipotosha dhana ya utafiti wa nyuki kwa sababu TAWIRI wanajihusisha zaidi na utafiti wa wanyamapori. Hivi tangu lini nyuki akawa mnyamapori? Kuweka masuala ya nyuki pamoja na wanyamapori, imefanya sekta ya nyuki kusahaulika. Natoa wito kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya tathmini itakayowezesha asasi hizi mbili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na Kituo cha TAWIRI, tunacho Kituo cha Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora. Chuo hiki kimeanza kutoa mafunzo rasmi mwaka wa fedha 2010/2011, baada ya kuhamisha mafunzo hayo kutoka Chuo cha Misitu Olmotonyi. Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora ndicho Chuo pekee nchini kinachotoa mafunzo ya taaluma ya ufugaji nyuki katika ngazi ya ufundi. Kazi kuu ya Chuo hiki ni kutoa mafunzo ya ufugaji nyuki, lakini pia hufanya kazi za utafiti na utalaamu ushauri (consultancy) katika fani ya ufugaji nyuki. Chuo hiki kimeanza kwa kudahili wanafunzi 34 kwa kozi ya Astashahada ya Ufugaji Nyuki na mwaka wa fedha 2011/2012 kitaanza kudahili wanafunzi wa Kozi ya Stashada ya Ufugaji Nyuki. Hii ni baada ya kuboresha miundombinu na kuongeza idadi ya wakufunzi. (Makofi)

Mimi naamini, Chuo hiki kikipewa kipaumbele tunaweza kuzalisha wataalam wa nyuki wa kutosha kutusaidia kukuza zao la nyuki. Sioni mantiki ya kuwaacha nyuki wanazunguka na kuzagaa kwenye miti kwa vile hawapati mizinga ya kutengeneza asali. Tunao nyuki wa kutosha kutuwezesha kuzalisha asali ambayo inaweza kutuinua kiuchumi. Nawaomba Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Halmashauri zetu zisaidie kuwaelekeza wananchi kujikita katika biashara hii ya ufugaji wa nyuki. Ni biashara rahisi na nyepesi kupata kipato kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tathimini iliyofanywa na watalaamu wa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini mwanzoni mwa mwaka huu, ilionesha kwamba patakuwepo na upungufu wa wastani wa Megawati 264 za nishati ya umeme katika Mfumo wa Gridi ya Taifa mwaka 2011. Tathmini hiyo ilitokana na hali ya ukame iliyokuwa inaendelea, kutokana na kupungua kwa mvua za vuli mwishoni mwa mwaka 2010. Kufuatia taarifa za hivi karibuni za Wakala wa Utabiri wa Hali ya Hewa, bado hali ya mvua za masika hairidhishi ingawaje kumekuwa na mvua za hapa na pale katika maeneo mengi nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maji yanayoingia kwenye vituo vya kuzalisha umeme bado ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji. Hata hivyo, maji kidogo yaliyoongezeka yamesaidia kupunguza mgao wa umeme. Bwawa ambalo linategemewa zaidi ni la Mtera ambalo bado kina cha maji kiko chini. Hadi kufikia tarehe 13 Aprili 2011, kina cha maji katika Bwawa la Mtera kilikuwa kimeongezeka kidogo kufikia mita 691.16 yaani sentimita 116 juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo cha mita 690. Hili ni ongezeko la sentimita 25 juu ya kiwango cha mita 690.91 au sentimeta 91 zilizokuwepo tarehe 24 Machi, 2011. Kwa sasa ni mashine moja tu hutembezwa wakati wa kiwango cha juu cha mahitaji ya umeme yaani kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tano asubuhi na saa moja hadi saa nne usiku. Aidha, mgao wa umeme kwa sasa unatokana na upungufu wa wastani wa Megawati 60 katika Gridi ya Taifa ikilinganishwa na mgao wa umeme

91 katika mwezi Februari, 2011 uliokuwa unatokana na upugufu wa Megawati 264. (Makofi) Mheshimiwa Spika, nchi yetu inatarajia kuwa na upungufu wa umeme wa wastani wa Megawati 60 katika mwaka wa 2011. Sababu kubwa za upungufu huo ni kutokana na mahitaji ya umeme kuongezeka kwa kasi kuliko uwekezaji katika miradi mipya ya kuzalisha umeme ambapo mwaka 2008, mahitaji ya juu (peak demand) yalikuwa Megawati 729 na mwaka 2010 mahitaji ya juu yamefika MW 833 hivyo, kuwa na upungufu wa zaidi ya Megawati 100 katika na Gridi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hali ya hewa iliyosababisha kupungua maji katika Bwawa la Mtera na kupunguza uwezo wa kuzalisha umeme unaokidhi mahitaji. Upungufu huo wa nishati ya umeme unategemewa kuondolewa kutokana na hatua mbalimbali zilizoanza kuchukuliwa na Serikali. Mwezi Februari 2011, Waziri wa Nishati na Madini alitoa taarifa ya hali ya umeme nchini. Katika taarifa hiyo, alieleza mikakati ya Serikali ya kukabiliana na upungufu wa umeme ikiwemo ya kupata umeme wa dharura, mipango ya muda mfupi na kati (2011 – 2015) na muda mrefu (2015 – 2018). Mipango hii ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Mheshimiwa Spika, hatua za muda mfupi za kukabiliana na upungufu wa umeme nchini zimeendelea kuchukuliwa tangu mwezi Novemba, 2010 hadi sasa. Serikali imelazimika kugharamia ununuzi wa mafuta mazito ya mitambo ya IPTL ili kuimarisha kiwango cha uzalishaji wa umeme kwenye Gridi ya Taifa. Aidha, TANESCO inaendelea na mchakato wa kukodi mitambo ya dharura yenye uwezo wa kuzalisha MW 260. Zabuni za kuzalisha umeme wa dharura zilitangazwa tarehe 18 Machi, 2011 na ilipangwa zifunguliwe tarehe 15 Aprili, 2011. Hivyo, mkataba unatarajiwa kusainiwa tarehe 30 Aprili, 2011 na mradi unatarajiwa kukamilika Julai, 2011. Ni matumaini yetu kuwa kuanzia mwaka 2012 tutakuwa tumeanza kuondokana na tatizo la upungufu wa umeme. (Makofi)

Mheshimwa Spika, katika mwaka 2010/2011, Serikali iliahidi kuongeza idadi ya walimu nchini ili kukidhi mahitaji yanayotokana na ongezeko kubwa la shule pamoja na wanafunzi katika ngazi zote za elimu nchini. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imetoa kipaumbele cha kuajiri walimu 21,891 katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu kuanzia mwezi Julai, 2010 hadi Machi, 2011. Kati ya walimu hao, wenye shahada ni 4,920, stashahada 4,306 na daraja la III A ni 12,665. Aidha, katika idadi hiyo, walimu waliopangwa kufundisha katika shule za msingi ni 12,665; shule za sekondari 9,039 na walimu 187 wamepangwa katika vyuo vya ualimu.

Mheshimiwa Spika, walimu wanaotarajiwa kuhitimu katika mwaka 2010/2011 ni 30,000. Kati yao, walimu wenye shahada watakaohitimu ni 11,649, wenye stashahada ni 7,382 na walimu wa ngazi ya Cheti – Daraja la IIIA ni 10,969. Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika kuajiri walimu wote watakaohitimu ili kuziba pengo la upungufu wa walimu 74,286 wanaohitajika katika shule za msingi na sekondari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha kwamba stahili za walimu zinatolewa kwa wakati. Vilevile, Serikali imeendelea kuboresha

92 maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi. Serikali pia inahakikisha kwamba inaondoa tatizo la kuchelewesha mishahara na stahili za walimu wapya.

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa pia kuwa suala hili lilisisitizwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipofanya ziara katika Wizara mbalimbali mwezi Machi, 2011. Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Rais alielekeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Fedha na Uchumi kuandaa takwimu za walimu wanaotarajiwa kuhitimu katika mwaka husika wa fedha ili stahili na mishahara yao itengwe katika Bajeti.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni kumejitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya walimu hususan walimu wa sekondari kuhusu stahili zao. Napenda kuchukua fursa hii kutoa ufafanuzi wa suala hili. Kimsingi, stahili za walimu kama walivyo watumishi wa umma wanapoajiriwa na kuripoti katika vituo vya kazi kwa mara ya kwanza (first appointment) zimeainishwa vizuri katika Sheria za Utumishi wa Umma na kanuni mbalimbali zinazotolewa mara kwa mara. Hivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 (Chapisho la Tatu) hususan vifungu L6, J2, J3, J5, J6 na J8 pamoja na Waraka wa Utumishi namba tano wa mwaka 2008 stahili hizo ni kama ifuatavyo:-

Kwanza, posho ya kujikimu (subsistence allowance) kwa mwajiri kwa muda wa siku 14 kulingana na viwango vya posho vinavyotolewa na Serikali, pili, gharama za nauli za mtumishi na familia yake (kama ipo) kutoka anakoishi (place of domocile) na kwenda Kituo cha kazi, tatu, gharama za kusafirisha mizigo isiyozidi kilo elfu moja (tani moja) ambayo mtumishi ameambatana nayo anapokwenda kuripoti kwa mara ya kwanza. Aidha, ikiwa mtumishi anayeajiriwa kwa mara ya kwanza ana mizigo inayozidi kilo 1,000 au tani moja akisharipoti katika kituo chake cha kazi, anapaswa kabla ya kusafirisha mizigo hiyo iliyozidi, awasiliane kwanza na mwajiri wake, ili mwajiri aweze kuidhinisha aina ya usafiri wa mizigo hiyo ambao ni wa gharama nafuu na unaokubalika kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, vipengele hivi nilivyovitaja, ndivyo vinavyotamkwa katika Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma. Napenda kusisitiza kwamba waajiri wote kuanzia sasa, vipengele hivi viainishwe kwenye barua ya mtumishi ambaye anaajiriwa kwa mara ya kwanza ili kila mtumishi aelewe stahili yake mapema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua hatua za dhati za kuhakikisha kuwa walimu wapya wanalipwa stahili zao kwa wakati mara wanapofika kuripoti katika vituo walivyopangiwa. Ili kutekeleza dhamira hiyo, Hazina imehakikisha kuwa fedha za malipo kwa walimu wapya wa shule za sekondari na vyuo vya ualimu zinapelekwa moja kwa moja katika Halmashauri zote na vyuo vya ualimu husika kulingana na idadi ya walimu waliopangwa katika maeneo hayo. Hadi tarehe 31 Machi, 2011 kiasi cha fedha kilichopelekwa katika Halmashauri na vyuo vya ualimu nchini kwa ajili ya malipo ya walimu wapya 9,039 wa sekondari na vyuo vya ualimu ni shilingi bilioni 15.3. (Makofi)

93 Mheshimiwa Spika, napenda kusisitiza kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwasumbue walimu katika kuwalipa malipo ya stahili zao mara wanapofika kuripoti katika vituo walivyopangiwa kuanza kazi. Pamoja na maelekezo haya, napenda kutoa tahadhari kwamba imebainika kuwa baadhi ya walimu wapya wanapofika kwenye vituo vyao walivyopangwa wanachukua fedha za stahili zao na kutoroka kwa kisingizio cha kwenda kuchukua mizigo. Serikali itawafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria walimu hao popote walipo. (Makofi)

Vilevile, imebainika kuwa watendaji wa Halmashauri wasio waaminifu wanashirikiana na baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari kufanya udanganyifu wa idadi ya walimu walioripoti na kuchukua mishahara na stahili za walimu wanaoshindwa kuripoti katika vituo vyao walivyopangiwa. Serikali inafuatilia kwa karibu suala hili na hatua stahiki zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na udanganyifu huo.

Mheshimiwa Spika, Tanzania inakabiliwa na maradhi makubwa kama vile Malaria, Kifua Kikuu, Shinikizo la Damu, Kisukari, Saratani na UKIMWI. Taarifa zinaonyesha kwamba magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu na UKIMWI yamepata msukumo mkubwa Kitaifa na Kimataifa katika kupambana nayo. Hata hivyo, magonjwa ya Shinikizo la Damu, Kisukari na Saratani yamekuwa yakiongelewa lakini bado hayajapata msukumo wa kutosha Kitaifa. Vilevile, watu wengi wamekuwa wakipima Malaria, Kifua Kikuu na Kisukari lakini wamekuwa wazito kupima magonjwa mengine niliyoyataja hapo juu na hasa na UKIMWI. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Saratani ni ugonjwa wa seli za mwili kwenye viungo mbalimbali vya binadamu. Ugonjwa huu hutokea pale ambapo chembechembe ndani ya seli za mwili zinaleta msukumo na kusababisha seli kugawanyika bila mpangilio na hatimaye kutengeneza uvimbe ambao huongezeka. Uvimbe huu hubakia hapo hapo kwenye kiungo husika au kusambaa sehemu zingine na kuathiri viungo vingine vya mwili. Sababu za seli kugawanyika bila mpangilio bado hazijulikani kwa ukamilifu. Hata hivyo, baadhi ya sababu zinazotajwa kuchangia mgawanyiko wa seli bila mpangilio au ugonjwa wa Saratani ni pamoja na uvutaji wa sigara na kunywa pombe kupita kiasi; kupatwa na miale ya jua na kemikali mbalimbali; ulaji wa aina za vyakula kama nyama nyekundu kwa wingi; unene kupita kiasi na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali ambavyo vinathiri baadhi ya viungo kama ini, kibofu cha mkojo na tezi zake. Vipodozi hivi pia vinasemekana kuathiri ngozi, damu, macho na figo. Utafiti unaonesha kuwa zipo aina zaidi ya 100 za Saratani ambazo zinaathiri binadamu wa rika na jinsia zote.

Mheshimiwa Spika, aina za Saratani zinazoongoza hapa nchini ni pamoja na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake; saratani ya koo, saratani ya matiti kwa wanawake, saratani ya ngozi, saratani ya macho, saratani ya damu, saratani ya kibofu cha mkojo na saratani ya tezi ya kibofu cha mkojo kwa wanaume. Kwa Tanzania, uwezo wa kutambua magonjwa ya saratani, umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, takwimu za wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kwamba mwaka 2004 kulikuwa na wagonjwa 2,866 na mwaka 2010 wagonjwa waliongezeka na kufikia 3,898.

94

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuongezeka kwa uwezo wa kutambua magonjwa ya saratani bado takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 hadi 85 ya wagonjwa wanaofika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road huwa katika hatua ya juu ya ugonjwa na hivyo mgonjwa huwa ameathirika kwa kiasi kikubwa. Hatua hii inasababisha tiba ya ugonjwa huo kuwa ngumu na ya gharama. Takwimu zinaonyesha kwamba ni kati ya asilimia 15 hadi 20 tu ya wagonjwa wanaokuwa katika hali hiyo, hupata nafuu baada ya matibabu. Kwa maana nyingine asilimia 80 hadi 85 ya wagonjwa hao huugua kwa muda mrefu na mwisho wake wanapoteza maisha.

Mheshimiwa Spika, madhara ya saratani ni wananchi kuwa na afya dhaifu na kupoteza nguvu kazi ya Taifa, kwani wagonjwa hukaa muda mrefu hospitalini kwa kutibiwa na wengine hufariki wakiwa na umri mdogo. Aidha, gharama za kutibu wagonjwa wa saratani ni kubwa sana. Kwa mfano, mchakato wa kutibu mgonjwa mmoja ambao unachukua kati ya miezi sita na mwaka mmoja unaweza kuhitaji dawa zenye gharama hadi shilingi milioni tano. Gharama hizi zinajumuisha hatua za kupigwa mionzi pamoja na dozi ya dawa ambayo imethibitika kuwa ni ya gharama kubwa kwa mwananchi wa kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau imetayarisha mpango mkakati wa kupambana na saratani hapa nchini. Mpango huu mahsusi unaelekeza jitihada mbalimbali za kupambana na saratani, ikiwemo kutoa elimu ya kufanya uchunguzi wa saratani mapema. Hospitali za Bugando, Mbeya, KCMC na Hospitali za Rufaa za Mikoa zinatoa huduma ya kupima saratani aina mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa na vyama mbalimbali inakabiliana na tatizo la saratani nchini. Wataalam wanasema kama saratani hasa za tezi ya kibofu cha mikojo na ile ya matiti zikigundulika mapema uko uthibitisho kwamba ugonjwa huu unazuilika. Hivyo, ni muhimu wananchi kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa saratani hasa za tezi ya kibofu cha mkojo na matiti. Kuhusu saratani ya tezi ya kibofu cha mkojo kwa wanaume (Prostate Cancer), utaratibu unaandaliwa ili Hospitali za Rufaa za Mikoa na za Kanda ziweze kupima na pia kufanya uchunguzi wa maabara kwa tatizo hilo. Wananchi wanashauriwa kuzingatia elimu inayotolewa na wataalam mbalimbali kuhusu kujiepusha na desturi zinazochangia kusababisha ugonjwa huu. Wito wangu kwa Watanzania wote ni kuwaombeni kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya viungo, kupima afya mara kwa mara na kuwahi kutibiwa wanapogundulika kuwa na tatizo la saratani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeamua kuelezea kwa kifupi kuhusu tatizo tulilo nalo la magonjwa haya kwa makusudi kwa sababu, hivi karibuni tumesikia kutokea wimbi la watu ambao wanasema wameoteshwa na Mwenyezi Mungu kuweza kutibu maradhi sugu mbalimbali. Tumesikia habari za Babu wa Loliondo, tumesikia habari za walioibuka Rombo, Mbeya, Tabora, Rukwa, Morogoro, na Dar es Salaam. Napenda kusisitiza kwamba Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Namba 23 ya mwaka 2002 inaweka utaratibu unaopaswa kuzingatiwa na mtu yeyote anayejishughulisha na shughuli za dawa na tiba mbadala. Hii ni pamoja na kujitambulisha kisheria kwa kujaza fomu

95 maalum ya kujisajili na kuthibitisha usalama wa dawa hiyo katika Maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa na kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba jambo hili limekuja chini ya mwamvuli wa imani ya kuoteshwa, jukumu la Serikali ni kujiridhisha na mambo ya msingi kwa kuhakikisha kwamba dawa hizo zinapelekwa katika Maabara ya Kisayansi na kuthibitika kwamba ni salama kwa matumizi ya binadamu. Wito wangu kwa Watanzania na kwa wananchi ni kwamba pamoja na kwamba suala hili ni la imani, bado nawasihi sana tena sana wote wanaotumia dawa hizo, wasiache kujiridhisha kwa kufanya utaratibu wa kupima afya zao hospitali ili kuona kama tatizo la kiafya walilokuwa nalo limekwisha. (Makofi)

Aidha, natoa wito kwa kila mtoa Huduma wa Tiba Asili au Tiba Mbadala kuzingatia Sheria za nchi kwa kuhakikisha kuwa wanasajiliwa wao wenyewe, vituo vyao na dawa wanazozitumia kutoa tiba. Nawaelekeza waratibu wa tiba asili na tiba mbadala katika kila mtoa huduma ya tiba asili au mbadala katika eneo lake anasajili kituo na dawa zake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha hivi karibuni, uharamia umekuwa ni tishio ambalo limeshamiri katika pwani ya nchi za bara la Afrika zilizopo kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi. Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na vitendo hivyo vya uharamia wa utekaji meli.

Mheshimiwa Spika, hadi sasa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeweza kukamata watuhumiwa 11 wa uharamia na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Hata hivyo, matukio ya uharamia bado yanajitokeza katika eneo la nchi yetu kwa kasi kubwa. Kwa mfano, katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Machi, 2010 hadi Aprili 2011, kumekuwa na matukio kumi na moja ya kiharamia ndani au jirani na eneo la nchi yetu. Vitendo vya kiharamia vimeleta athari kubwa za kiulinzi, kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu. Kutokana na vitendo vya kiharamia, imebidi kuongeza ulinzi katika eneo hili hivyo kutumia kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingeweza kutumika kwenye sekta za uzalishaji. Vitendo hivyo vinachangia sana kuongezeka kwa gharama za kufanya biashara kutokana na gharama za meli kupanda zikiwemo za bima. Hali hiyo imelazimu Serikali kuchukua hatua mbili muhimu, hatua ya kwanza ikiwa ni kusindikiza meli zinazoomba msaada wa ulinzi pindi zinapokuwa katika eneo letu la Bahari na pili Serikali kutoa ulinzi katika vyombo vinavyotafiti gesi na mafuta katika bahari yetu.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali isiyotabirika ya uharamia, Serikali imechukua hatua kwa kufanya marekebisho ya sheria za nchi yetu dhidi ya uharamia. Kutokana na mabadiliko hayo, Serikali inaweza kuwakamata maharamia hata wakiwa nje ya mipaka yetu, kuwaleta nchini na kuwafungulia mashtaka kwenye Mahakama zetu. Tanzania pia imesaini Kanuni za Ushirikiano wa Kupambana na Uharamia (Djibouti Code of Conduct) na kutekeleza Maazimio yake. Pamoja na hatua zingine, Serikali imeanzisha kituo cha kupashana habari zinazohusu uharamia na uokoaji (Maritime Rescue Coordination Centre - MRCC) kwa madhumuni ya kupambana na

96 uharamia kwenye Pwani yetu. Aidha, Serikali inashirikiana na nchi zilizopo kwenye Ukanda wa Bahari kufanya semina, kozi na mikutano mbalimbali ikiwa ni juhudi za kuongeza nguvu ya pamoja ya Kikanda katika kupambana na uharamia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali imekumbwa na changamoto kubwa ya kiusalama kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya kiharamia katika eneo letu. Wakati eneo letu la bahari ni kubwa, meli zetu hazina uwezo wa kulifikia eneo lote la Bahari la nautical miles 200 kwa kukosa meli zenye uwezo huo. Serikali inaangalia uwezekano wa kununua meli yenye uwezo wa kufika kwenye eneo hilo ili kukabiliana na uharamia kwa kuzingatia hali ya uchumi na Sheria ya Manunuzi. Tathmini kuhusiana na suala hili bado inafanywa na Jeshi letu. Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na vyombo vya Kimataifa ili kulinda usalama wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, tarehe 31 Desemba, 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alitoa hotuba ambayo ilionesha nia ya Serikali ya kuanzisha mchakato wa maandalizi ya kutungwa kwa Katiba itakayokidhi mahitaji ya Watanzania wa leo. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali ilizingatia mambo kadhaa muhimu yakiwemo yafuatayo:-

Kwanza utaratibu wa kuunda Tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni kutoka kwa Watanzania kuhusu masuala mbalimbali ya Kikatiba.

Pili, nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uundwaji wa Tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni kuhusu Katiba.

Tatu, nafasi ya Bunge na Baraza la Wawakilishi katika kujadili na kupitisha Katiba Mpya ya nchi, nne, mamlaka ya wananchi katika kutoa maoni yao juu ya Katiba na kuipitisha kwa njia ya kura ya maoni, tano, nafasi ya Vyama vya Siasa na viongozi wake katika mchakato wa kukusanya maoni, kujadili na kupitishwa kwa Katiba Mpya na sita, ratiba ya ukamilishaji wa zoezi la kukusanya maoni, kuandika Katiba, kujadili na kuipitisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili kuyatekeleza mambo haya, Mheshimiwa Rais aliahidi kuwa Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa Sheria kwa ajili ya Kuunda Tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni na mambo mengine yanayohusika. Muswada huo wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011 (The Constitutional Review Bill, 2011) uliwasilishwa katika Bunge lako Tukufu chini ya hati ya dharura kwa lengo la kujadiliwa hatua zote na hatimaye kuweza kupitishwa na Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2007, Muswada huo ulipelekwa kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ili iweze kuuchambua na kukusanya maoni kutoka kwa wadau na wananchi kupitia mikutano maalum (public hearing). Zoezi hili lilifanyika katika vituo vitatu vya Zanzibar, Dar es Salaam na Dodoma. Kamati hiyo baada ya kupokea maoni mbalimbali

97 ya wadau na kuyachambua, iliwasilisha maoni yake kwa Mheshimiwa Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Aprili, 2011, uliliarifu Bunge lako Tukufu juu ya kuridhika na ushauri uliopewa na Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na ukaamua kutoa muda zaidi kwa Kamati hiyo kuendelea na kazi ya kuchambua maoni yaliyotolewa na wadau na wananchi mbalimbali. Aidha, ulielekeza Kamati hiyo kuendelea kukusanya maoni zaidi kwa nia ya kuuboresha zaidi Muswada huu ili uweze kukidhi matakwa ya Watanzania. Vilevile, ulitoa wito kwa Watanzania wote sasa kutumia fursa hii ya ongezeko la muda kujadili mapendekezo yaliyomo katika Muswada badala ya kulumbana, kuzomeana na maandamano kwani maoni, ushauri na mapendekezo ndiyo yatakayowezesha kutungwa kwa Sheria nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa upande wake imeweza pia kushiriki kikamilifu katika upokeaji wa maoni ya wananchi katika vituo vyote vitatu kupitia Mawaziri na watendaji wake. Ni dhahiri kuwa wananchi wengi wameonyesha shauku kubwa ya kutoa maoni yao katika mikutano hiyo ya kupokea maoni (public hearing). Hivyo, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa Serikali inakubaliana na uamuzi wako wa kuongeza muda zaidi kwa lengo la kuendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau na wananchi ili kuboresha Muswada kwa kadri itakavyowezekana. (Makofi)

Naomba pia nitumie nafasi hii kukupongeza wewe binafsi pamoja na Kamati yako kwa kuona umuhimu huu kwa manufaa ya Taifa letu. Wakati muafaka utakapowadia, Serikali itatoa ushirikiano thabiti kwa Kamati ili kuwasilisha Muswada Bungeni utakaozingatia mambo ya msingi yatakayotolewa na wananchi kuanzia sasa. Vilevile, kutoa ushirikiano wa dhati kwa viongozi na Serikali ili Taifa na wananchi wake waweze kujiletea maendeleo katika hali ya amani, upendo, mshikamano na utulivu. Maandamano yasiyo na tija, fujo, vurugu na migomo vyote hivi havina tija wala manufaa kwa Watanzania. Aidha, si busara kubeza mafanikio ya Watanzania yaliyokwishapatikana hadi sasa. Kama Taifa tumefika hapa tulipo chini ya uongozi madhubuti wa viongozi waliopo sasa na waasisi ambao katika uongozi wanaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar, kubeza viongozi hawa au Katiba ni kudhalilisha Taifa letu. (Makofi)

Sasa tunayo fursa nyingine ya kutazama upya Katiba yetu. Basi sote tushirikiane kwa dhamira moja ya kutoa maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali ili kwa pamoja tuweze kupata Katiba itakayowanufaisha Watanzania wote. Katiba itakayotokana na michango yetu mbalimbali na kumilikiwa na wananchi wenyewe, haina budi kutokana na Watanzania wote wenye nia ya kulitakia Taifa hili na wananchi amani, upendo na utulivu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baadhi ya Watanzania wanabeza Katiba zetu kwa msingi tu kuwa zimerekebishwa mara nyingi na hivyo kuzifananisha na viraka. Kama ilivyo kwa Sheria, Katiba nazo hufanyiwa marekebisho kila inapobidi ili kuzingatia hali mpya inayojitokeza katika Taifa ambayo inaonekana kuwa na uzito wa kulazimika kurekebisha

98 Katiba ili kutambua hali hiyo Kikatiba, ndiyo maana Katiba yetu imerekebishwa mara 14 tangu mwaka 1977. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimefahamishwa kuwa kwa msingi huo huo Katiba ya Afrika ya Kusini iliyotungwa mwaka 1997 na iliyopitia hatua mbalimbali za Kidemokrasia na kusifika ulimwenguni kote kwamba ni Katiba ya watu, katika uhai wake wa miaka 14 sasa tayari imekwishafanyiwa marekebisho mara 16. Katiba ya Marekani nayo nimejulishwa kuwa tayari imerekebishwa mara 27 na ile ya India mara 94 na bado wananchi wa nchi hizo wana fahari na Katiba hizo! Kimsingi, wataalam wa historia wanaeleza kuwa katika kuona marekebisho ya Katiba mbalimbali za mataifa mtu anaweza kuona historia kamili ya Taifa husika na kujua mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika kipindi husika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimelazimika kuyasema haya ili kuondoa ile dhana ya kuwa Katiba tuliyonayo sasa hivi haifai hasa kwa sababu imefanyiwa marekebisho mara 14. Ikumbukwe kuwa, mwaka 1992 Taifa letu lilionyesha ukomavu wake kwa kutambua mfumo wa vyama vingi nchini na ndiyo maana leo tupo hapa chini ya mwamvuli wa vyama vingi vya siasa. Huu ni ushahidi tosha wa ukomavu wa Taifa katika utawala wa sheria na demokrasia na si ishara ya upungufu unaosababisha kupewa jina la kuweka kiraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivyo, natoa wito kwa wananchi wote kuwa hawana budi kuendelea kuiheshimu na kuifuata Katiba iliyopo mpaka pale Katiba Mpya inayoanza mchakato wake sasa itakapokamilika. Vile vile ningependa kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuwa Tanzania siyo kama inatunga Katiba Mpya kwa kuwa hatuna Katiba, wala kana kwamba tumetoka katika ukoloni, la hasha! Wala kana kwamba tumetoka katika ukoloni la hasha! Tunatunga Katiba Mpya kwa ajili ya kukidhi mazingira mapya ya leo na matakwa ya wananchi wa leo baada ya miaka 50 ya Uhuru kama alivyosema Mheshimiwa Rais katika hotuba yake ya hivi karibuni. Ni kutokana na maelezo haya, napenda kutoa wito kwa Watanzania wenzangu kuwa tushirikiane katika hatua zote zinazofuata katika mchakato wa kuelekea kutungwa kwa Katiba Mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu Muswada huu wa Kuunda Tume ya kukusanya maoni ya wananchi, Serikali itahakikisha Muswada unachapishwa kwa lugha ya Kiswahili na kuusambaza kwa wananchi kwa lengo la kuwawezesha kujadili kwa wepesi na kueleweka zaidi. Muswada huu pia utachapishwa katika magazeti mbalimbali ya kawaida ya kila siku nchini kwa lengo hilo hilo kama ulivyokuwa umeshauri. Matarajio yangu ni kwamba Muswada huu utapata nafasi ya kuwasilishwa katika Bunge la Bajeti la mwezi Juni kulingana na ratiba itakayopangwa na Bunge ukiwa umeimarika zaidi kwa manufaa ya Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Serikali ya Chama cha Mapinduzi ndiyo iliyopewa mamlaka na wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kuliongoza Taifa letu. Hivyo, natoa wito kwa Watanzania wote kwamba sasa tuelekeze nguvu zetu zote kufanya mambo muhimu yanayolenga kutuletea maendeleo ya Taifa letu. (Makofi)

99

Mheshimiwa Spika, napenda kuhitimisha hotuba yangu kwa kusisitiza mambo machache yafuatayo, kwanza nchi yetu ina fursa nyingi kwa wananchi wake katika kujiletea maendeleo. Uwekezaji katika ufugaji wa nyuki ni fursa mojawapo ambayo tukiitumia vizuri wananchi wengi wanaweza kujikomboa kiuchumi. Nawasihi wananchi tutumie fursa hii ya ufugaji nyuki ambayo ni nyepesi na rahisi katika kutuongezea kipato, poli, kuhusu utabiri wa hali ya hewa unaonesha kwamba bado hali ya mvua za masika hairidhishi ingawa kumekuwa na mvua za hapa na pale katika maeneo mengi nchini. Tutumie taarifa hii kujihadhari na matumizi yetu ya chakula tulichonacho na tatu, kumekuwa na matatizo ya mara kwa mara ya walimu na hasa waajiriwa wapya kuhusu stahili zao. Zipo Kanuni na Taratibu ambazo zimeelezwa wazi katika Waraka wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2009 (Chapisho la Tatu). Nawataka watendaji wa Halmashauri wafuate utaratibu kama ilivyobainishwa katika Kanuni za Ajira ya Walimu. Aidha, waepuke kuwasumbua walimu katika kuwalipa malipo ya stahili zao bila sababu za msingi.

Mheshimiwa Spika, nne, tunalo tatizo la maradhi sugu makubwa yanayowakabili wananchi wetu. Aidha, suala la matibabu ya maradhi haya yamekuwa yakihusishwa na imani ya dawa na tiba mbadala, napenda kuwaomba wananchi wote kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara. Aidha, pale ambapo kuna umuhimu wa kutumia dawa na tiba mbadala, ni vizuri kujiridhisha na usalama wa dawa zinazotumika na kurejea kupima maradhi husika katika maabara zinazojulikana kisheria ili kujiridhisha kama maradhi yamekwisha na tano, tumekubaliana kimsingi kuhusu mchakato wa kufikia upatikanaji wa Katiba inayozingatia mahitaji ya Watanzania wa leo kwa kuanzia na hatua ya awali ya Kuunda Tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi. Nawasihi Watanzania wote tushirikiane katika kufanikisha mchakato huu kwa amani. Tunayo nafasi ya kutoa maoni na tunayo nafasi ya kushiriki kikamilifu katika kupata Katiba tunayoridhika nayo. Nawaomba wote tuvumiliane na pale tunapotetereka tusahihishane kwa ustarabu. Nchi hii ni yetu sote. Tufanye yote kwa amani, utulivu, upendo na mshikamano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia, napenda kuwashukuru wote waliosaidia kufanikisha Mkutano huu. Niwashukuru kipekee wewe Mheshimiwa Spika pamoja na Naibu Spika na Wenyeviti kwa kutuongoza vizuri. (Makofi)

Pia niwashukuru Wenyeviti wa Kamati za Bunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwa michango yenu wakati wa kujadili Miswada, Maazimio na Taarifa mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano huu. Namshukuru Katibu wa Bunge na wasaidizi wake pamoja na watalaam wa Serikali kwa misaada yao ya kitaalam na huduma mbalimbali iliyofanikisha Mkutano wetu. Wote kwa ujumla nawashukuruni sana! Nawashukuru waandishi wa habari, madereva na wasaidizi wengine. Mungu awabariki na awajalie afya njema ya kuendelea kulitumikia Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwatakia Waheshimiwa Wabunge wote na Watanzania wenzangu heri kwa maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano. Vile vile, nawatakia Watanzania wenzangu na hasa wakristo heri ya sikukuu ya Pasaka. (Makofi)

100

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini siyo kwa umuhimu, nawatakia wote safari njema ya kurejea majumbani kwenu na kwenye maeneo yenu ya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liahirishwe hadi tarehe 7 Juni, 2011, saa tatu asubuhi, litakapokutana tena hapa Mjini Dodoma kwa ajili ya Mkutano wa Nne mahsusi kwa ajili ya Bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, naafiki. (Makofi)

WIMBO WA TAIFA

(Hapa Waheshimiwa Wabunge waliimba wimbo wa Taifa)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kama tulivyosema kwanza tunampongeza sana Waziri Mkuu kwa hotuba yake makini, itawasaidia Watanzania na sisi Wabunge kuendeleza mambo mbalimbali katika nchi yetu. Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge napenda kuahirisha shughuli za Mkutano wa Tatu wa Bunge hili mpaka siku ya Jumanne, tarehe 7 Juni, 2011 saa tatu asubuhi hapa Dodoma. (Makofi)

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Saa 8.15 mchana Bunge liliahirishwa mpaka siku ya Jumanne, Tarehe 7 Juni, 2011 saa tatu asubuhi)

101