Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

BUNGE LA ______

MAJADILIANO YA BUNGE ______

MKUTANO WA KUMI NA NNE

Kikao cha Tisa – Tarehe 6 Februari, 2009

(Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

MASWALI NA MAJIBU

Na. 107

Mikakati ya Kupambana na Uharibifu wa Mazingira

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA aliuliza:-

Kwa kuwa, mwaka 2006 Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais ilitangaza mambo muhimu ya kuzingatia katika mikakati ya kupambana na uharibifu wa mazingira hapa nchini:-

(a) Je, ni miti kiasi gani imepandwa kwa kila mkoa na kwa maeneo yapi?

(b)Je, matumizi ya mkaa yamepunguzwa kwa kiasi gani hapa nchini kuanzia mwaka 2006 – 2008?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS – MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ikipokea taarifa za upandaji miti kutoka mikoa yote Tanzania Bara, kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa. Taarifa zilizowasilishwa toka kila mkoa, zinatoa mchanganuo wa miti iliyopandwa katika kila wilaya. Katika kipindi cha mwaka 2006/2007, jumla ya miti 95,411,580 ilipandwa na kutunzwa ambayo ni sawa na 73.6% ya lengo la miti

1 129,597,818. Idadi hii ni ya miti ilipandwa katika mikoa yote 21 na katika Wilaya zake zote.

Mchanganuo huu ni mrefu, hivyo nitampatia Mheshimiwa Mbunge, kama kiambatanisho. Labda tu kwa faida ya wananchi, Mkoa unaoongoza kwa upandaji miti ni Iringa ikiwa na jumla ya miti 17,486,732; ikifuatiwa na Mkoa wa Tanga ikiwa na jumla ya miti 6,873,579 na Mara ikiwa na jumla ya miti 5,443,842. Aidha, mikoa mitatu ya mwisho kwa upandaji miti ni Mtwara ikiwa na jumla ya miti 1,713,806; ikifuatiwa na Dar-es-Salaam ikiwa na jumla ya miti 1,668,801 na mwisho Singida ikiwa na jumla ya miti 830,458.

Mheshimiwa Naibu Spika, Takwimu za upandaji miti katika kipindi cha 2007/2008 bado zinafanyiwa mchanganuo na hivyo zitawasilishwa.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha 2006 hadi 2008 hakuna utafiti uliofanywa kubaini kupungua kwa matumizi ya mkaa. Hata hivyo, kufuatana na ripoti ya matumizi ya familia (House Hold Budget Survey) ya mwaka 2006/2007 imeonyesha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2001 – 2007, familia nyingi zimeendelea kutegemea mkaa kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia.

Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, SUA mwaka 2000 ulionyesha kuwa 69% ya familia za Dar-es-Salaam zilitumia mkaa tu kwa kupikia wakati 88% ya familia zilitumia mkaa pamoja na vyanzo vingine vya nishati ikiwemo kuni, mafuta ya taa, gesi na umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wastani takwimu zilizokusanywa na vituo vya Idara ya Misitu na Nyuki vilivyoko barabara kuu za kuingia Dar-es-Salaam (Morogoro, Kilwa na Bagamoyo), zinaonyesha kuwa kila siku magunia kati ya 15,000 na 20,000 yanaingizwa Jijini Dar-es-Salaam.

Pia uzoefu unaonyesha kuwa magunia mengi ya mkaa huingia Dar-es-Salaam bila ya kupitia au kukaguliwa na vituo vya ukaguzi wa mazao ya misitu.

Mfano kupitia baiskeli, magari madogo binafsi au ya umma (Magari ya Serikali), malori ya kubebea mizigo ambayo hayako wazi na hata malori ya kubebea mafuta huweka magunia ya mkaa pembeni mwa tanki la mafuta. Hali hii inaashiria kuwa matumizi ya mkaa Dar-es-Salaam ni makubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya juhudi mbalimbali za kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ikiwemo kuondoa kodi kwenye vifaa vya umeme jua, gesi ya kupikia na mafuta ya taa. Jitihada zingine ni kuhamasisha matumizi ya majiko banifu na moto poa. Hatua hizi zinategemewa kupunguza matumizi ya mkaa na hivyo kupunguza kasi ya ukataji miti.

2 Nachukua fursa hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge na Viongozi wa Halmashauri zetu kuwahimiza wananchi ili watumie nishati mbadala na majiko banifu ili waweze kutunza na kuhifadhi mazingira.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa imeonekana kabisa kwenye majibu ya msingi kwamba matumizi ya mkaa yameendelea kuongeeka na Mheshimiwa Waziri amekiri hapa kwamba hakuna utafiti uliofanyika kwa muda wa miaka miwili iliyopita hata baada ya kuweka mikakati ya kuzuia. Je, Serikali haioni kwamba kutokufanya utafiti hakutoi picha kamili kwamba ni nini kinachofanyika na matokeo yake ni kuendelea kuharibu mazingira?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa, makali ya umeme na gharama kuendelea kupanda ni chanzo kikubwa cha kuendelea kutumia mkaa hapa nchini na Mheshimiwa Waziri katika jibu lake la msingi limeeleza. Sasa Serikali haioni sababu za kubeba gharama za capacity charges za umeme ili gharama ipungue na hivyo kupunguza makali kwa wananchi na pia kuhifadhi mazingira? (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS – MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwishasema kwamba tafiti za moja kwa moja za matumizi ya mkaa bado hazijafanyika. Lakini Wizara yetu kwa kushirikiana na Wizara ya Madini na Nishati, tuko katika hatua za kuweza kuangalia pamoja na mambo mengine matumizi haya ya nishati mbadala na hii ni katika hatua mojawapo ya kuweza kukamilisha kanuni ya kusimamia masuala mazima ya nishati jadidifu na matumizi mengineyo.

Kwa hiyo, ni kweli kabisa kwamba tunaendelea na utafiti na utafiti huu utajumuisha sasa matumizi ya mkaa na kuona kwamba ni kwa jinsi gani nishati ile ambayo tunaipendekeza, nishati jadidifu, itaweza kuja na kupunguza matumizi haya ya mkaa.

Mheshimiwa naibu Spika, ama kuhusu swali lake la pili, kama Bunge lako linavyojua kwamba Bunge lako liko katika hatua ya kuweza kuhakikisha kwamba tunatumia nishati ya gesi asilia badala ya maeneo ambayo walikuwa wanatumia kuni ama kupunguza pia matumizi ya mafuta.

Lakini vilevile niseme tu kwamba katika sera yetu ya umeme vijijini lengo ni kuhakikisha kwamba umeme unafika vijijini na uweze kuwa na gharama nafuu. Lakini kwa maeneo ambayo tutaweza kupeleka gesi asilia tutapenda tupeleke gesi hiyo na itumike kwa umeme na iwe na faida na ikawa na unafuu kwa wakazi mbalimbali kama inavyofanyika katika mikoa ya kusini na mikoa mingine pia itaendelea kufanyika.

NAIBU SPIKA: Ingawa swali hili limechukua muda mrefu, lakini nitamuita Mwana Mazingira, Profesa Mwalyosi.

MHE. PROF. RAPHAEL B. MWALYOSI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa katika Bajeti iliyopita tuliruhusu ruzuku katika kitu kinaitwa moto poa ambayo

3 ilizua mjadala mrefu sana humu Bungeni kuhusu kuhalalisha kutumia ruzuku kwenye gesi hiyo. Sijui Waziri anaweza akatueleza ni mafanikio gani yanaelekea kutokea au kujionyesha kupunguza athari ya mazingira kwa kutumia moto poa?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS – MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli nitakuwa nasema uwongo nikisema kwamba tayari tathmini imeshafanyika kuweza kuona mafanikio ya utumiaji wa moto poa hasa ukizingatia kwamba suala hili limefanyika katika kipindi hiki tu cha mwaka huu. Mimi ningependa kumweleza Mheshimiwa Mbunge, tuuache mwaka huu, kipindi hiki cha Bajeti hii kiishe tuweze kufanya tathmini lakini vilevile tukiangalia aina mbalimbali za nishati ambazo zitawafikia wengi na itawafaidisha watu wengi wa vijijini.

NAIBU SPIKA: Hiyo tathmini itafanywa siku za usoni. Naenda Wizara ya Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Clemence Lyamba, kwa niaba ya Mheshimiwa Ligalama.

Na. 108

Hifadhi ya Wanyama ya Mikumi

MHE. CASTOR R. LIGALLAMA K.n.y. MHE. CLEMENCE B. LYAMBA aliuliza:-

Kwa kuwa, Serikali imeendelea kukosa mchango mkubwa wa mapato ya utalii katika Hifadhi ya wanyama ya Mikumi kwa miaka mingi kutokana na mgogoro wa muda mrefu kati ya Serikali na mmiliki wa Hoteli ya Mikumi Wildlife Lodge:-

(a) Je, mgogoro huo ulimalizika lini na kwa masharti gani kwa kila upande?

(b) Je, wawekezaji gani ambao tayari wameonyesha nia ya kuwekeza katika ukarabati wa jengo la hoteli hiyo lililoungua moto tarehe 5/9/2006 au wanaotaka kuwekeza sehemu nyingine katika hifadhi hiyo?

(c) Je, Serikali ina mikakati gani mahsusi ya kuhakikisha kuwa inaweka mazingira ya kuwavutia wawekezaji katika hifadhi hiyo ili kuifanya iwe sehemu ya mizunguko, (circuit) kwa watalii watakaokuwa wakielekea kwenye kifadhi zinazovutia watalii Kanda za Selous na Ruaha?

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Clemence Beatus Lyamba, Mbunge wa Mikumi, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Mgogoro wa Loji ya Mikumi umekwisha baada ya Mahakama kuamua kuwa aliyekuwa mkodishaji, Hotel Travertine Ltd, wa loji hiyo alipwe madai yake aliyokuwa anaidai Serikali. Mkodishaji ameshalipwa madai yake.

4

(b)Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mgogoro wa Loji ya Mikumi umekwisha hivi karibuni, Wizara yangu kwa kushirikiana na Consolidated Holdings tunafanya utaratibu wa kumpata mwekezaji mwingine. Hata hivyo katika jitihada za kuongeza huduma ya malazi kwa watalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Wizara yangu ilitangaza maeneo mapya ya kuwekeza katika maeneo ya Mahondo na Lumanga kupitia magazeti na tovuti ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA). Jumla ya makampuni 12 zimewasilisha maombi ya kuwekeza na hivi sasa TANAPA wanaendelea na mchakato wa tathmini ya maombi hayo na baadaye yawasilishwe kwenye Kikao cha Bodi ya TANAPA kabla ya mwezi Aprili, 2009.

(c)Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inayo mikakati mahsusi ya kuhakikisha mazingira ya Hifadhi ya Mikumi yanavutia wawekezaji pamoja na kuiunganisha Hifadhi hii na Mzunguko wa Utalii Kusini, Southern Tourist Circuti. Mojawapo ya mikakati hiyo ni Mpango wa Usimamizi Hifadhi ya Mikumi 2008–2013 ambao umebainisha utengenezaji wa barabara itakayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Pori la Akiba la Selous.

Aidha, utekelezaji wa Mkakati huu utasaidia kufungua barabara ndani ya hifadhi na kuboresha kiwanja cha ndege kilichoko ndani ya hifadhi. Pia Sekta binafsi inahamasishwa kuwekeza katika huduma za usafiri wa anga.

MHE. CASTOR R. LIGALLAMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa loji ile ya Mikumi ilikuwa imeigharimu Serikali hela nyingi kwa maana ya miundombinu na ukaribu wa watalii kwenda kuangalia wanyama. Je, baada ya kesi hii kwisha, hatuwezi kufanya mkakati wa haraka ili iweze kupatiwa mwekezaji mwingine?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa sehemu alizotaja Mheshimiwa Waziri za Lumanga na Mahondo ni sehemu mbali kidogo na Loji ile; haitakuwa vizuri kuzingatia kwanza Mikumi Wildlife Lodge iendelezwe kabla ya sehemu hizo alizozitaja?

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ni miezi kama mitatu iliyopita ndipo ambapo huyu mwekezaji amelipwa madai yake. Na kwa hivi sasa tunashirikiana na Consolidated Holdings ili kuanza kuandaa upya kwa ajili ya kutangaza tena ili wawekezaji wapya waweze kuomba Mikumi. Na jinsi ambavyo haraka itakavyowezekana tutakuwa tayari kuhakikisha kwamba sehemu hiyo inapata mwwekezaji na ujenzi uanze mara moja. Kwa hali hiyo basi, kwa sasahivi hatuna la zaidi isipokuwa wawekezaji watakapojitokeza ndipo ambapo tutahakikisha panapatikana. Lakini na hizi sehemu nyingine mbili ni kiasi tu cha baada ya muda zikitengenezwa vizuri nina uhakika kwamba watalii watapapenda pia na watapazoea kama walivyokuwa wamezoea Mikumi.

MHE. AZIZA S. ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na majibu ya msingi ambayo Mheshimiwa Waziri amejibu; amesema kwamba mwekezaji huyu amelipwa pesa. Je, pesa hizi ni kiasi gani alicholipwa mwekezaji huyu na wale ambao

5 walisababisha mpaka pesa za Serikali kutumika muwekezaji wamechukuliwa hatua gani?

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya shilingi bilioni nne ndizo ambazo mwekezaji amelipwa. Na ukweli ni kwamba sababu ambayo aliitoa haina uhusiano na kusema kwamba kuna wafanyakazi wowote ambao walizembea. Ni kwamba mwekezaji huyu yeye alipewa masharti ya kukarabati na kuhakikisha kwamba hoteli hii inafanya kazi. Lakini alipofanya ukarabati na tulipokwenda kukagua na kushirikisha wataalamu mbalimbali wakiwemo Idara ya Majengo ya Wizara ya Ujenzi na wataalamu wengine, tukakuta kwamba ukarabati alioufanya haukufikia kiwango ambacho hoteli ile ilikuwa inatakiwa kuwa; basi tulimkatalia na kumwambia kwamba haiwezekani aweze kurudia tena na arekebishe mpaka ifikie standard inayotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo mwekezaji huyu yeye hakufanya hivyo. Baada ya muda akatupeleka Mahakamani akidai fidia kwa kipindi kile chote ambacho tumemfanya asiweze kuingiza mapato yoyote. Na tukaenda Mahakamani, tukajaribu kuongea hiyo kesi na tukaomba kwamba tukubaliane tusuluhishane lakini madai aliyokuwa anayadai sisi Serikali hatukuyataka. Tulipotoka nje ya Mahakama kusuluhishana tulishindwa na yeye alitukatalia, tukarudi Mahakamani na Serikali tukashindwa.

Baada ya hapo tukakata rufaa lakini tukashindwa. Kwa hiyo, baada ya muda tukaona kwamba tukiendelea na mchezo wa kukata naye rufaa ina maana Serikali tutazidi kuumia kiasi ambacho, manaake alianza kudai na riba zote manaake deni limekuwa kubwa na hizo ni riba. Tukaona kwamba imefikia hatua ambayo ni lazima tumlipe ili tuondokane na hili jambo ambalo riba ingeongezeka mwishowe Serikali ingeweza kulipa mpaka kwenye bilioni 10 na zaidi. Kwa hiyo, kwa hali hiyo ni kwamba mwekezaji mwenyewe kwa njia zake za maarifa na ujanja ndio ilifikia hatua kwamba akageuza kesi akawa anatudai sisi.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hoteli yenyewe mwishoni ikaungua. Tunaendelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mheshimiwa Vuai Abdallah Khamis, atauliza swali.

Na. 109

Zanzibar Kufaidika na Jumuiya za Kimataifa

MHE. VUAI ABDALLAH KHAMIS aliuliza:-

Kwa kuwa, kuna Jumuiya za Ushirikiano wa Kikanda kwa Mataifa mbalimbali kama vile COMESA, SADC, na kadhalika:-

Je, Tanzania Zanzibar inafaidika vipi na jumuiya hizo?

6 WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Vuai Abdallah Khamis, naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania sio Mwanachama wa COMESA.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo haya, sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vuai Abdallah Khamis, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, na Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC. Kwa kuwa, Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar inanufaika kama vile Tanzania yote kwa ujumla inavyonufaika katika kujiunga na Jumuiya hizo. Baadhi ya faida ambazo tunazipata ni kwa kuwa katika Jumuiya hizo ni:-

1.Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kujiunga katika Jumuiya hizo Tanzania imepanua soko la bidhaa zinazozalishwa Tanzania na kuuzwa nchi za nje. Aidha bidhaa za Tanzania zinazouzwa Jumuiya ya Afrika Mashariki hazitozwi ushuru wa forodha, hii inaipa fursa Tanzania kushindana vizuri zaidi na bidhaa kutoka nchi ambazo si wanachama wa EAC. Aidha, 85% ya bidhaa toka Tanzania hazitozwi ushuru wa forodha zinapouzwa katika nchi wanachama wa SADC. Ni vizuri Watanzania wafanyabiashara hasa kutoka pande zote mbili za Muungano kuhangaika na watumie fursa hii ya kuuza bidhaa katika masoko ya SADC na Afrika Mashariki. 2. Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ya pamoja ya kama vile ya kilimo na mifugo, inaiwezesha Tanzania kupambana na magonjwa ya midomo na miguu, FMD, homa za mapafu ya ng’ombe, CBPP, kwa pamoja.

Kwa sababu nchi moja inapopatwa na matatizo haya inaambukiza nchi nyingine. Kwa hiyo kwa kujiunga na Jumuiya hizi Tanzania pamoja na nchi hizi zinapambana na magonjwa ya aina hii kwa pamoja.

3. Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumekuwa tukipokea watalii wengi ambao wengi wao wamekuwa wakitoka katika nchi wanachama wa SADC. Katika kipindi cha mwaka 2006 peke yake tumepokea watalii zaidi ya laki sita na arobaini na nne elfu kutoka kwenye Kanda hizi.

4.Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna Programu za Afya ambazo zinatekelezwa na nchi wanachama wa SADC. Kwa mfano, Progaramu za kupambana na magonjwa ya binadamu ya kuambukiza kama vile UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

Vile vile Tanzania iko kwenye majadiliano ya kuunganisha gridi ya umeme toka nchi za SADC na gridi ya Taifa letu ili mikoa ya kusini ifaidike na gridi hiyo. Gridi hizi

7 zitakapounganishwa, zitaiwezesha Tanzania kunufaika na upatikanaji wa uhakika wa nishati hii muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni katika sekta ya Siasa, Ulinzi na Usalama, ambapo Tanzania Bara na Zanzibar hunufaika kwa amani na utulivu, hali ambayo inatoa fursa ya kutekeleza programu nyingi za maendeleo.

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri amesema kwamba Tanzania sio mwanachama wa COMESA.

Lakini anaweza kuliambia Bunge hili pamoja na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni nini kilichopelekea Tanzania kuwa si mwanachama wa COMESA. Inakosa nini kutokuwa mwachama wa COMESA? WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, uamuzi wa Tanzania kujiondoa kwenye soko la COMESA ulitokana na wadau mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo wafanyabiashara wenyewe kuona kwamba Tanzania haikuwa na ulazima wa kuendelea kuwemo katika Jumuiya ya COMESA.

Mheshimiwa Spika, sababu kubwa iliyotolewa ni kwamba bado Tanzania tulikuwa na soko kubwa la watu wa SADC pamoja na Afrika Mashariki ambayo wingi wake unazidi watu karibu milioni 800. Hilo ni la kwanza kwamba tulikuwa na soko la kutosha na kujiunga na COMESA au kuendelea kuwepo katika COMESA ilionekana kama redundance.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu ya pili ni kwamba tulikuwa na madeni ya nchi katika uanachama wetu wa hizi Jumuiya zote. Mpaka wakati tunaacha COMESA Tanzania ilikuwa inadaiwa dola karibu 1,800,000 katika michango yake ya jumuiya zile. Kwa hiyo, Tanzania ilipima faida ya kuendelea kutoa michango yake ya dola zaidi ya milioni moja katika jumuiya ya COMESA wakati tuna soko la kutosha katika upande wa SADC na Afrika Mashariki.

Kwa mantiki hizo na baada ya kupata ushauri wa wafanyabiashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Jamhuri ya Muungano iliona haikuwa na umuhimu kwa wakati huo kujiunga na COMESA. Lakini kama hali itaruhusu mbele ya safari, milango iko wazi.

Na. 110

Kuzuia Biashara ya Chuma Chakavu

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH aliuliza:-

Kwa kuwa, biashara ya chuma chakavu inaendelea kwa kasi kubwa hapa nchini, na kwa kuwa hadi leo Serikali haijatangaza wala kupiga marufuku biashara hiyo:-

8 (a) Je, wauzaji hao wanapata wapi vyuma hivyo?

(b) Je, Serikali haioni kuwa fedha zinazotumika kwa ujenzi wa miundombinu ya reli, kingo za barabara, madaraja na mengineyo zinapotea bure?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maida Hamad Abdallah, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, vyuma chakavu vinavyouzwa nchini hupatikana kutoka katika vyanzo mbalimbali kutegemeana na aina ya chuma. Vyanzo hivyo ni pamoja na vifuatavyo:-

(i) Chuma cha pua hupatikana kutokana na mitambo iliyotumika viwandani ambayo baada ya uwezo wake wa kufanya kazi kwisha hutolewa na kuuzwa kama chuma chakavu, mataruma ya reli yaliyotumika, vyuma vya meli vilivyochakaa, na kadhalika.

(ii) Chuma aina ya shaba hupatikana kutokana na mabaki ya viwanda vinavyotengeneza nyaya za umeme za shaba ambapo katika uzalishaji hupatikana vipande vipande ambavyo haviwezi kutumika.

Vilevile, kutokana na vifaa vyenye shaba vilivyotumika ambavyo matumizi yake yamesitishwa.

(iii) Chuma chakavu aina ya bati, kinatokana na vifungashio vya vinywaji, makopo, vinavyotumia bati kama vile soda, juisi na bia baada ya vinywaji hivyo kutumika ambapo makopo hutupwa na hivyo kuokotwa na kuuzwa kama chuma chakavu, Tin Scrap.

(iv) Chuma chakavu aina Zinc Dross ni mabaki yanayotokana na shughuli za galvanization katika kampuni kama vile za ALAF na MM Steel.

(v) Wafanyabiashara ambao sio waaminifu wamekuwa wakikata nyaya za umeme na simu, kung’oa mataruma ya reli, nguzo za madaraja na mengineyo na kuzijumuisha katika makusanyo ya chuma chakavu bila kujali hasara kubwa wanayoliingizia Taifa.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kuona hasara kubwa inayotokana na uharibifu wa miundombinu muhimu kama vile, reli, kingo za barabara, madaraja na mengineyo, imeandaa waraka wenye mapendekezo ya kuomba kutunga sheria itakayosimamia biashara ya chuma chakavu nchini ili kudhibiti biashara holela ya chuma chakavu.

9 Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la matumizi mabaya ya chuma chakavu ni suala linalogusa hisia za wananchi na Wabunge wengi, kama ambavyo limewahi kuulizwa hapa Bungeni na Mheshimiwa Hassan Chande Kigwalilo, Mbunge wa Liwale, tarehe 7 Agosti, 2008 na Mheshimiwa Profesa Raphael B. Mwalyosi, Mbunge wa Ludewa, tarehe 3 Novemba, 2008.

Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Maida Hamad Abdallah kama nilivyowahakikishia Waheshimiwa Kigwalilo na Mwalyosi kuwa Serikali inatambua uzito wa tatizo na Wizara yangu inakamilisha taratibu za kuuleta muswada wa sheria juu ya jambo hili hapa Bungeni mapema iwezekanavyo.

MHE. IDDI M. AZZAN: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali inajiandaa kuleta Muswada wa sheria kudhibiti biashara hii, na kwasababu biashara hii imekuwa na athari kubwa sana katika nchi yetu. Je, Serikali haioni umuhimu wa kupiga marufuku biashara hii hadi hapo sheria itakapokuwa tayari? (Makofi)

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naomba Bunge lako tukufu lijue kwamba biashara ya chuma chakavu ambazo zinahusu mataruma ya reli na hizo ambazo zinaleta athari, hairuhusiwi.

Ila biashara ya chuma chakavu zingine ambazo hazihusiani mataruma ya reli haijakatazwa na kwa hivyo kwa kutumia fursa hiyo kwa kutumia mwanya huo biashara hiyo imeshamiri.

Kwa hiyo, kukataza kusafirisha vyuma hivyo pengine si siluhisho lakini jambo ambalo linaonekana ni kwamba mahitaji ya chuma chakavu na chuma ghafi yameongezekana sana nchini, kwa sababu viwanda vya kutengeneza chuma vimeongeza ndani ya nchi. Kwa hivyo sio tu kwa ajili ya kusafirisha nje, hata hapa ndani kuna mahitaji makubwa sana kwa hivyo Serikali kama suluhisho la kudumu inaleta sheria ya kukataza vyuma vyote kusafirishwa na inaweka masharti ambayo pengine itaondoa matatizo ambayo yamekuwa yakitokea. Lakini vilevile hivi karibuni tutaanza kutengeneza chuma ghafi na kwa hivyo kuondoa matatizo hayo.

NAIBU SPIKA: Ahsante kwa sababu sheria itakuja tunaendelea.

Na. 111

Uwekezaji katika eneo la Mabibo

MHE. MZEE NGWALI ZUBEIR aliuliza:-

Kwa kuwa, eneo la uwekezaji la Mabibo liko hatua za mwisho kukamilika na kwamba wawekezaji wengi na kutaka kuwekeza katika eneo hilo:-

(a) Je, Serikali itakuwa tayari kukubali maombi ya wawekezaji hao?

10 (b) Je, huu si wakati mzuri kwa Serikali kutafuta eneo lingine kama hilo?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Mzee Ngwali Zubeir, Mbunge wa Mkwajuni, napenda kutoa maelezo ya jumla kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa eneo la uwekezaji la Mabibo ulianza mwaka 2005. Eneo hilo linaendelea kujengewa miundombinu yote muhimu kama maji, umeme, gesi mawasiliano, barabara za ndani na kituo cha Zimamoto pamoja na huduma muhimu za kijamii kama kituo cha Huduma kwa Wawekezaji (One Stop Servcie Centre), Zahanati na Kantini. Kwa sasa uendelezaji wa eneo umefika asilimia 90. Serikali inaendelea kunadi eneo hilo kwa wawekezaji wa ndani na nje na tayari maombi kumi (10) kutoka kwa wawekezaji yamepokelewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, sasa napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mzee Ngwali Zubeir, Mbunge wa Kwanjuni, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iko tayari kuwakubali wawekezaji wa nje na ndani watakaokidhi vigezo vivyowekwa. Vigezo hivyo ni pamoja na:-

(i) Kifungua kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa kwa ajili ya kuuza nje na ndani ya nchi. Mwekezaji atakayeuza nje ya nchi kwa asilimia (80%) ya kile atakachozalisha (EPZ) atapewa kipaumbele.

(ii) Uwekezaji uwe wa Viwanda vya kati (light industries).

(iii) Mtaji wa kuwekeza kwa mwekezaji wa ndani ni USD. 1,000,000,000.00 wakati mwekezaji toka nje ni USD. 5,000,000,000.00.

(iv) Makadirio ya mauzo kwa mwaka (annual turnover) yasipungue USD. 100,000,000.00 kwa wawekezaji wa ndani na USD. 5,000,000,000.00 kwa wawekezaji wa nje.

(v) Uwekezaji uwe wenye kutoa ajira nyingi walau wafanyakazi 100 kwa kila mwekezaji.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ingependa yawepo maeneo mengi ya aina hiyo kila mkoa kwa ajili ya maendeleo ya mikoa husika hata hivyo zipo changamoto nyingi zinazofanya lengo hilo lisifikiwe mapema. Changamoto hizo ni pamoja na:-

11 (i) Kutokuwepo kwa miundombinu ya uhakika kila mkoa kama vile barabara, reli, viwanja vya ndge, bandari, maji, umeme wa uhakika, na kadhalika. (ii) Ufinyu wa Bajeti ya kutengeneza miundombuni hiyo kwa upande wa Serikali.

(iii) Ukosefu wa malighafi kwenye maeneo husika miundombinu ya masoko na uhifadhi wa mazao.

(iv) Uhaba wa teknolojia za kisasa na uhaba wa wataalam katika baadhi ya maeneo katika sekta ya viwanda, biashara na masoko.

(v) Ni ukosefu wa mitaji ya kufanyia kazi kutokana na masharti magumu yanayotolewa na mabenki na ukubwa wa riba zinazotozwa na mabenki hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, zoezi la ujenzi wa miundombinu kwa ajili y a viwanda linaendelea hatua kwa hatua kadri Serikali itakavyokuwa ikipata fedha. Kwa sasa Serikali inaendelea na maandilizi ya awali ya kuendeleza eneo la Mbegani, Wilayani Bagamoyo na Bandari ya Mtwara kwa kushirikisha sekta binafsi.

MHE. MZEE NGWALI ZUBEIR: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili madogo nyongeza. Amesema kuwa ana maombi kumi hivi sasa wameshayapata.

Je, maombi hayo ya wawekezaji wangapi wa nje na wangapi wa ndani?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kuwa katika eneo lile lililopo Wizara ina mpango wa kuwafidia wale jirani waliopo pale kwa kuhakikisha kuwa usalama na mazingira wa lile eneo hayaharibiki.

Je, Wizara tayari imeshawalipa wale majirani waliopo pale?

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu haya maombi kumi hapa nilipo sina mchanganuo ya kwamba wangapi ni wa ndani, na ni wangapi wa nje. Ninaomba Mheshimiwa Zubeir nimpatie baada ya Bunge hili baada ya kuwauliza ndugu zetu wa export promotion zone.

Swali la pili la kuwafidia kwanza naomba niweke rekodi sahihi kwamba sijasema kwamba Serikali inafidia mtu yeyote kwa sababu eneo lile kwanza lilikuwa la Serikali na tangu tumeanza kujenga pale ujenzi unafanywa kwa namna ambapo hakutakuwa na uharibifu wa mazingira ambao utalazimu mtu ambaye yuko pale jirani afidiwe. Kwa hiyo, mpango huo wa kufidiwa haupo na hakuna wananchi ambao wamedai fidia mpaka sasa hivi.

MHE. RITA L. MLAKI: Mheshimiwa Naibu Spika, samahani, nashukuru kwa kunipa nafasi naomba kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo. Kwa kuwa tangu sheria imeundwa ya IPZD na marekebisho au kuambatanishwa na sheria ya special economic zone wawekezaji wamesua sua sana kuja kuweza katika maeneo haya, na tumeona kuna

12 umuhimu mkubwa wa kuweza kuwa na maeneo haya kwa sababu ya kukuza uchumi wa nchi.

Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kulichulia hili jambo kutafuta fedha kama walivyofanya wenzetu wa Mauritius na Lesotto kutoka World Bank na taasis mbalimbali za kifedha kwa kuwasaidia Watanzania wawekeze? Katika maeneo haya na pia kuwatafutia masoko kutoka nje, kwa sababu bila Serikali kuweka mkono wake kwa nguvu japo hatufanyi tena biashara tumeona bado suala IPZD na special economic zone litasua sua na ambapo imeshafika miaka sita kuanzia tumeanza kuongea mambo hayo.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli analosema kwamba ziko changamoto mbalimbali za kuendeleza mamlaka hii ya mauzo ya nje na ukizingatia kwamba kuna wawekezaji wengine ambao wangependa vilevile kuwekeza kwa ajili ya soko la ndani. Serikali inajidhatiti sasa kuweka mamlaka moja ambayo inaitwa ni economic development zone ili kwamba mwekezaji yeyote akija pale asilazimike kuzalisha kwa ajili ya kuuza tu nje au kwa ajili ya kuuza labda kwa ajili ya soko la ndani. Tunataka kuweka mamlaka ambayo itamruhusu mtu yoyote ambaye anawekeza kwa kiwango kikubwa mwenye kutoa ajira kwa wingi hata kama anauza kwa masoko ndani au masoko ya nje aweze kupata vile vivutio ambavyo vinatolewa katika mamlaka hii. Hili lingine alilosema kuhusu kutafuta fedha, kutafuta masoko napenda nimhakikishie kwamba inajitahidi kufanya hivyo hilo analosema na bado tutaendelea na jitihada hizo. Tunachoomba tu ni ushirikiano kwake yeye mwenyewe Waheshimiwa Wabunge na wadau wengine ambao wanajua namna bora ya kuendeleza suala hili ili kumwendeleza Mtanzania. (Makofi)

Na. 112

Maafisa Ushirika Kusomeshwa

MHE. MARTHA J. UMBULLA – (K.n.y. MHE. DR. CHRISANT MAJIYATANGA MZINDAKAYA) aliuliza:-

Ili kutekeleza kwa ufanisi Sera nzuri ya uanzishaji wa SACCOS katika kuondoa umaskini.

Je, Serikali ina mipango gani ya kuwasomesha maafisa Ushirika wa kutosha watakaomudu kusajili kwa wakati uanzishaji na uendelezaji wa SACCOS nchini?

WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dr. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, Mbunge wa Kwela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, usajili wa vyama vya Ushirika vikiwemo Vyama vya Ushirika wa akiba na mikopo (SACCOS) hufanya chini ya sheria ya vyama vya Ushirika Na. 20 ya mwaka 2003.

13

Kazi hiyo hufanywa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika na anasaidiwa na warajis wasaidizi. Katika ngazi ya mkoa Mshuri wa Ushirika katika Sekretarieti ndiye huteuliwa kuwa Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika kwa mkoa husika. Kwa kuwa kila mkoa una Mrajis Msaidizi mwenye dhamana ya kuandikisha Vyama vya Ushirika zikiwemo SACCOS. Mfumo huu unakidhi mahitaji ya huduma ya kuandikisha vyama mkoani.

Maombi ya kuandikisha Chama cha Ushirika huanzia kwa Afisa Ushirika wilayani ambako chama kinaanzishwa na ndiye anayehakikisha kuwa utaratibu wote umetimizwa kwa mujibu wa sheria. Maafisa ushirika hawa ndio wanaopaswa kuwaelekeza wanaoomba juu ya utayarishaji wa masharti ya chama na kisha kutuma au kupeleka maombi hayo kwa Mrajis Msaidizi Mkoani.

Kama hakuna kasoro katika maombi yaliyowasilishwa kwa Mrajis Msaidizi chama hicho huandikishwa na endapo itahitajika kufanya marekebisho yoyote Afisa Ushirika wa wilaya huelekezwa kufanya marekebisho hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kusaidia kuwajengea uwezo Maafisa Ushirika wa wilaya na mikoa, Wizara yangu imekuwa ikitoa udhamini wa mafunzo kwa kozi mbalimbali za muda mfupi na muda mrefu. Katika mwaka 2006/2007 Wizara ilitoa udhamini wa mafunzo kwa maafisa ushirika 52 kwa kozi ya Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili. Mwaka 2007/2008 Maafisa Ushirika 10 walipata udhamini ambapo mwaka 2008/2009 maafisa Ushirika 14 wamepewa udhamini wa mafunzo kwa kozi mbalimbali.

Hata hivyo jitihada za Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kuwawezesha kupata mafunzo zinakwamishwa na baadhi ya waajiri wao yaani Serikali za mitaa husika ambapo hawapangia maafisa Ushirika majukumu mengine kwenye idara nyingine kama vile uhasibu, ukaguzi, usimamizi wa miradi na ukaguzi wa Hesabu za vijiji. Naomba kutoa wito kwa mamlaka zinazohusika kuwasaidia maafisa Ushirika kutekeleza majukumu yao ya msingi waliyoajiriwa kuyafanya.

Aidha, Wizara yangu inatoa ushauri kwa Halmashauri za Jiji/Miji na Wilaya kutenga fedha kwenye Bajeti zao kwa ajili ya kuwasomesha Maafisa Ushirika na watendaji wengine ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu yao.

MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa SACCOS haziwezi kuendelea bila mitaji ya kutosha na kwa kuwa mfuko wa Rais wa uwezeshaji ulikuwa na malengo makubwa ya kusaidia hizo SACCOS ambapo zilienda sambamba na uhamasishaji wa kuanzisha SACCOS nyingi nchini. Je, kuna matatizo gani yaliyoikumba huo mfuko kwa sababu kwa maeneo mengi ya mkoa hasa mkoa wa Manyara licha ya kwamba hazijafika hata hausikiki?

WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, msingi wa kwanza kabisa wa mtaji wa SACCOS unatokana na wanachama wake,

14 ili SACCOS iwe SACCOS ya wanachama lazima msingi wa kwanza wa mtaji utokane na wao baada ya kupata msingi wa awali ndiyo sasa vyombo vingine vinapoanza kuingia. Taarifa tulizonazo ni kwamba viko vyombo ambavyo vinasaidia SACCOS mahali pengi nchini, moja ni SCAT ambayo ni Muungano wa Vyama vya Kuweka na Kukopa nchini. Vilevile yako mabenki kama CRDB ambayo imekuwa inatoa mikopo kupitia SACCOS na hivyo kuimarisha uwezekano wa kufikisha mikopo kwa wanachama waliojiunga katika SACCOS.

Kuhusu mfuko wa Rais anaoulizia Mheshimiwa Umbulla, maelezo yake yalikwisha tolewa na Wizara inayohusika ambayo fedha zake zilipitia aidha kupitia kwenye mabenki au kupitia katika SCAT au kupitia katika taasisi nyingine zinazotoa mikopo.

Kwa hiyo, kama suala linalohusu mkoa wa Manyara, kwamba mkoa wa Manyara haujapata, suala ambalo Wizara langu inaweza ikashirikiana na Wizara inayohusika na mfuko ule ili tuweze kujua nini hasa kilichotokea. Lakini kwa sasa hatuna takwimu zinazoonyesha kilichotokea huko Manyara.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hata viongozi wengi wanaoendesha SACCOS zilizopo nchini zikiwemo SACCOS za mkoa wa Singida na za Njombe, hawana elimu kabisa ya jinsi gani ya kuendesha SACCOS hizo, hasa namna ya kuweka kumbukumbu za fedha.

Je, Serikali haioni kwamba kuna kila sababu ya kutenga fedha kwa kila Halmashauri kwa malengo tu ya kutoa elimu kwa viongozi wa SACCOS hizi mbalimbali ili wapate uelewa wa kuendesha SACCOS zao? (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana naye kabisa kwamba elimu ni msingi mkubwa wa kuendesha SACCOS kwa sababu kama wanaoendesha SACCOS hawana elimu, uwezekano wa kuweza kufilisika utakuwa mkubwa sana. Kwa hiyo, taratibu ambazo ziko kwa sasa ni mafunzo kwa viongozi hawa kuendeshwa na Maafisa Ushirika katika wilaya husika.

Tunacho chuo sasa hivi kule Kizumbi ambacho kinachukua maafisa hao au watu wanaoendesha hizo SACCOS na kuwapa mafunzo ya muda mfupi ya namna ya kuendesha hizo SACCOS. Kwa hiyo wito wangu naoweza kutoa ni kwa Halmashauri zote nchini ambazo zinaendesha na zina miradi ya SACCOS na watu wao wanashiriki katika hii kazi ili ziweke katika bajeti zao fungu litakalowezesha mafunzo waendeshaji wa SACCOS na viongozi wao.

15

Na. 113

Muda unaoruhusiwa kwa viongozi kuweka watu Kizuizini.

MHE. ALI KHAMIS SELF aliuliza:-

Kwa kuwa, wapo viongozi wenye mamlaka ya kisheria ya kumweka mtu kizuizini kwa saa maalum wakiwemo wakuu wa mkoa na wilaya:-

Je, muda gani waliopewa viongozi hao kuweka watu kizuizini kabla mhusika hajapendelekwa mahakamani?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ali Khamis Seif, Mbunge wa Mkoani kama ifuatavyo:-

Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanayo mamlaka ya kisheria ya kuamuru kukamatwa na kuwekwa kizuizini mtu yeyote ambaye anasababisha au anataka kusababisha uvunjifu wa utulivu na amani, endapo uvunjifu huo wa utulivu na amani hauwezi kuzuiwa kwa njia nyingine yeyote ile isipokuwa kwa kukamatwa na kuwekwa kuzuizini kwa mtu huyo.

Mamlaka haya ya wakuu wa Mikoa na Wilaya yameanishwa chini ya Sheria ya Tawala za Mikoa “The Regional Administration Act Cap. 97” kwa mujibu wa sheria hii mtu atakaye kamatwa na kuzuiliwa kwa utaratibu huu ni lazima afikishwa mbele ya Hakimu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai yanayomkabili ndani ya saa arobaini na nane (48) toka akamatwe. Endapo muda huu utapita bila kufikishwa kwa Hakimu basi mtu huyo ataachiwa huru na hatakamatwa tena kwa kosa hilo.

Vilevile Mkuu wa Mkoa au Wilaya analazimika kutoa maelezo kwa maandishi kuhusu sababu za kukamatwa na mtu huyo. Nakala ya maelezo hayo yatapelekwa kwa Hakimu pamoja na mtu huyo. Sheria ya Tawala za mikoa inazuia matumizi mabaya ya mamlaka ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Endapo Mkuu yeyote wa Mkoa au Wilaya atatumia mamlaka hayo vinginevyo atakuwa amefanya kosa la kutumia mamlaka vibaya na atashughulikiwa kwa mujibu wa Fungu la 96 la sheria ya Kanuni ya Adhabu, sura ya 16. (Makofi)

MHE. ALI KHAMIS SEIF: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante pamoja na jibu la Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu nina swali moja dogo la nyongeza. Je, kama itathibitika kuwa OCD amesimamia kuwekwa ndani mtuhumiwa kinyume na sheria atachukuliwa hatua gani?

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, OCD hatawaliwi na sheria hii uliyoitaja. OCD anatawaliwa na sheria ya polisi pamoja na

16 Criminal Procedure Act. Sheria hizo ndizo zimepanga muda kwamba kama atafanya kosa kama hilo ambalo amelizungumzia Mheshimiwa Mbunge, basi hatua zinaweza kuchuliwa dhidi yake. Hatua ambazo zinachukuliwa dhidi yake ni pamoja na hatua za kinidhamu pamoja na kama ni kuna ushahidi wa kukosa labda kosa linaitwa a law of confinement.

Na. 114

Kupanua na Kuboresha Hospitali ya Jeshi – Tabora

MHE. SIRAJU J. KABOYONGA aliuliza:-

Kwa kuwa, Hospitali ya jeshi katika kambi ya Jeshi Tabora ni ya siku nyingi na inahudumia askari wote wa Brigedi ya magharibi (Tabora Musoma, Mwanza, Kigoma); na kwa kuwa, ni dhahiri kwamba uwezo wa Hospitali hiyo kumudu mahitaji ya matibabu ya askari wetu pamoja na familia zao ni mdogo sana:-

Je, Serikali ina mpango gani kwa kupanua na kuboresha huduma za Hopsitali hiyo?

NAIBU WAZIRI WA ULINZI JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Siraju Juma Kaboyonga, Mbunge wa Tabora Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, wagonjwa wanaopata rufaa kutoka hospitali na zahanati zilizo katika vikosi mbalimbali vya Brigedi ya Magharibi wanahudumiwa na hospitali za jeshi za Mwanza na Tabora. Kwa kutambua umuhimu wa kuboresha huduma za afya, Wizara ilipeleka ombi kwa Serikali ya Ujerumani kuboresha hospitali za Jeshi. Serikali ya Shirikisho la Ujerumani kupitia kikundi chake cha ushauri wa kijeshi kilichopo nchini kiitwacho GAFTAG kimeshafanya tathimini ya awali ya eneo linalokusudiwa kujengwa hospitali ya kisasa ya JWTZ mjini Tabora. Aidha, michoro ya hospitali hiyo imeshakamilika. Kinachosubiriwa kwa sasa ni fedha za ujenzi wa hospitali hiyo kutoka Ujerumani na ujenzi unatarajiwa kuanza mwakani.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ujenzi huu utakapokamilika Serikali ya Ujerumani itaweka vifaa vya kisasa na JWTZ litapeleka wataalam wa kutosha kuendesha hospitali hiyo kama ilivyofanyika kwa hospitali nyingine zilizojengwa kwa msaada wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani zinazomilikiwa na JWTZ ambazo ni Hospitali ya Jeshi Mbeya, Hospitali ya Jeshi Mwanza na Hospitali ya Jeshi Bububu, Zanzibar.

MHE. SIRAJU J. KABOYONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kwa niaba ya wapiganaji wetu wa Brigedia ya Magharibi pamoja na wananchi wa Tabora kuishukuru sana Serikali kwa uamuzi huu.

17 Pili naomba kuuliza swali la nyongeza kama ifutavyo, Serikali imeiomba Serikali ya Ujerumani itusaidie kujenga maana yake civil works na kuleta vifaa, sasa hivi kwa nini Serikali isitumie fursa hii ikatumia fedha za ndani kujenga civil works halafu ikaiachia Serikali ya ujerumani kutuletea vifaa kutoka nje kwa sababu hilo ndilo tatizo hatuna tatizo na civil.

Kwa hiyo, naomba Serikali inieleze kwanini isitumie nguvu zetu za ndani hususani kwa mikopo ya mashirika yetu ya pensheni kujenga na kuachia jukumu la vifaa na mashine Serikali ya Ujerumani?

NAIBU WAZIRI WA ULINZI JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa niaba ya Wizara napokea shukrani ulizozitoa kwa Wizara kwa hatua ambazo tumefikia.

La pili Serikali haina mpango wowote wa kuomba Serikali ya Kijerumani isitusaidie tena jambo ambalo imeshatusaidia. Kwa hiyo, kwa kweli kwa kuwa tumeshasaidiwa fedha ambayo tutapata tutazitumia kuimarisha zaidi hospitali hiyo lakini kwa sasa kazi ya ujenzi na vifaa tunaomba Ujerumani waharakishe tu kutuletea na sisi tuendelee na jukumu tulilokubaliana la kuandaa wataalam. Na. 115

Kambi la Wazee Bukumbi

MHE. JACOB D. SHIBILITI aliuliza:-

Kwa kuwa, Kambi ya Wazee Bukumbi inakabiliwa na matatizo ya ongezeko la watu; na kwa kuwa, watu hao ni wazee sana, walemavu wa viungo na wasioona:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupanuakambi hiyo?

(b) Je, Serikali itawapatia lini gari la kuwasaidia pindi mgonjwa anapopatiwa rufaa?

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jacob Dalali Shibiliti, Mbunge wa Misungwi, lenye sehemu a na b kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inasimamia jumla ya makazi 17 yakiwemo Bukumbi yanayotoa huduma kwa wazee wasiojiweza hapa nchini, aidha, yapo makazi mengine 24 yanayosimamiwa na wakala za hiari. Lengo kuu la makazi yote haya ni kutoa huduma za msingi kwa wale wazee wasiojiweza ikiwa pamoja na kuwapatia wazee ulinzi chakula, malazi na matibabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 inaelekeza kuwa jukumu la kutoa mafunzo ya wazee ni la jamii na kwamba familia ndiyo mhimili mkuu wa kuwatunza wazee au watu wenye ulemavu na wasiojiweza katika

18 familia husika. Sera hiyo inasisitiza kuwa kuwatunza wazee wasiojiweza katika makao makuu yaani Institution Care itakuwa ni hatua ya mwisho baada ya wahusika kukosa kabisa mtu wa kuwatunza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha mzee hatengwi na jamii na ili kupunguza hali ya upweke na masononeko yanayotokana na kukaa katika makazi, Serikali inaendelea kuzihamasisha familia na jamii ili ziweze kuwatunza wazee wasiojiweza na watu wengine wanaohitaji msaada wa matunzo ndani ya familia au jamii wanazotoka.

Aidha, hamasa inatolewa zaidi kwa vijana ili waweze kujiandaa vema kukabili maisha ya uzeeni na hivyo kupunguza utegemezi usio wa lazima katika familia na jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hiyo kwa sasa Serikali bado haijaona sababu ya kupanua makazi ya wazee wasiojiweza yakiwemo ya Bukumbi, mipango yetu ni kuendelea kuyatunza ili yawe katika hali bora zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, makazi ya Bukumbi yana wakazi zaidi ya 364 wakiwemo wanawake 192, wanaume 172 lakini asilimia kubwa ni vijana ambao wana uwezo wa kujitegemea.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaandaa utaratibu wa kuwatenganisha vijana hao kushirikiana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia mafunzo ya ujasiliamali na mita.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa makazi ya wazee wasiojiweza ya Bukumbi pamoja na sehemu zingine hayana magari, hali hii inatokana na ufinyu wa Bajeti ya Wizara na Bajeti itakaporuhusu Wizara itaangalia uwezekano wa kupeleka magari kwenye makazi hayo.

MHE. LUCAS L. SELELII: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana ingawa sana katika Bajeti yake Mheshimiwa Waziri ya 2008/2009 aliahidi kwamba ataipatia kambi hii ya wasiojiweza ya wazee wasiona gari. Sasa hapa anasema mpaka Bajeti itakapokuwa imetegemaa sasa hiyo ahadi alikuwa na maana gani na hatua iliyofikia ni hatua gani?

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Bajeti yetu makazi ya Bukumbi kama nilivyosema kupata gari ina maana kununua na kununua ina maana ni fedha na nilisema kwamba wakati ule nilipokuwa nazungumza tulisema kwamba tutaangalia uwezekano wa kuipatia kambi ya wazee wa Bukumbi gari kwa maana hiyo naendelea kusema kwamba kwa sababu ya ufinyu wa Bajeti ndiyo tunaangalia uwezekano. (Makofi)

Kwa hiyo, bado nasema kwamba tunajua kwamba wanahitaji gari kama makambi mengine, kwa hiyo tunaangalia utaratibu wa Bajeti ikiruhusu na tukipata gari basi hatuna sababu kwanini Bukumbi tusiipatie gari.

19

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa matatizo yaliyoko katika kituo cha Bukumbi yanafanana sana na kituo cha wazee kilichoko katika Manispaa ya Moshi Kati ya mji mpya na kwa kuwa nilishauliza swali kama hili na Mheshimiwa Naibu Waziri akatoa ahadi ya kufanya matengenezo katika nyumba za wazee wale. Na kwa kuwa kipindi cha masika kinakaribia na nyumba zile zinavuja.

Je, Waziri anawaambia nini wazee wale angalau waendelee kuishi kwa matumaini?

NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Mheshimiwa Naibu Spika, makambi mengi kama tulivyokuwa tunazungumza ya wazee nchini ni mabovu yako katika hali mbaya. Kuna maeneo ambayo yako katika mpango wa ukarabati kwa mwaka huu wa fedha 2008/2009 kwa sababu hatuwezi kukarabati makambi yote ni Korandoto, Shinyanga, Singida na makambi ya vyuo vingine vya ustawi. Kwa Sababu hatuna fedha za kutosha ni kwamba tunakarabati kwa awamu.

Kwa hiyo, ni kweli kwamba hali ya mvua inakuja na ni kweli nilishatembelea makambi yale nimeyaona ni mabovu na yanahitaji ukarabati. Lakini bado nasema kwamba tutaangalia sasa katika Bajeti nyingine kwa sababu pesa bado tulizozipata haziwezi kutosheleza.

Kwa hiyo, bado tutaangalia sehemu zile ambazo ni mbaya zaidi na yale Makambi ambayo yana hali mbaya sana ndiyo ambayo tunaanza kuyakarabati, halafu baadaye hela zitakapopatikana ndiyo tutaendelea kukarabati yale Makambi mengine yatakayobakia. (Makofi)

Na. 116

Wanafunzi Wanaosoma Nje ya Nchi

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA (K.n.y. MHE. HAMAD RASHID MOHAMED) aliuliza:-

(a) Je, ni wanafunzi wangapi wanapewa mikopo nje ya nchi na wako katika nchi gani?

(b) Je, ni fedha kiasi gani zilikwishatumwa kwa wanafunzi hao na zimepelekwa kwa njia gani?

(c) Je, ni utaratibu gani unaotumika kwa wanafunzi walioko nje ya nchi kulipiwa na Serikali kwa njia ya mkopo; na je, watoto wa Maafisa wa Kibalozi wanalipiwa na Serikali au wanakopeshwa?

20 NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. GAUDENTIA M. KABAKA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya wanafunzi 1,791 wanaosoma nje ya nchi, wamenufaika na mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kati ya mwaka 2005/2006 na mwaka 2007/2008. Wanafunzi hao wapo katika nchi za China (255), India (158), Urusi (267), Poland (64), Ukraine (86), Algeria (238), Marekani (4), Uingereza (12), Uganda (594) Kenya (17), Rwanda (1), Cuba (25), Finland (1), Malyasia (1), Uturuki (1), Czech (5), Afrika Kusini (54) Canada (4) na Sweeden (1).

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, tangu mwaka 2005/2006 mpaka mwaka 2007/2008, jumla ya Sh. 12,446,049.842 zilikopeshwa kwa wanafunzi walioko nje kama ifuatavyo:-

Mwaka Kiasi (Tshs)

2005/2006 2,562,611.789 2006/2007 4,853,840.247 2007/2008 5,029,597.806 Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za mikopo za wanafunzi hao, zilikuwa zinatumwa kupitia Benki kwenda katika Balozi za Tanzania katika nchi hizo, ambapo zikishapokea, wanafunzi walikuwa wanalipwa moja kwa moja fedha taslimu au kuziweka katika akaunti zao benki. Kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika baadhi ya Balozi zetu, Serikali iliamua kuanzia mwaka 2008/2009, kupeleka fedha moja kwa moja kwenye akaunti za wanafunzi wanaosoma nchi za nje.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu unaotumika kuwalipia wanafunzi walioko nje ya nchi ni kwa njia ya mikopo. Kwa wale wanafunzi waliopata ufadhili wa Serikali toka nchi rafiki, ufadhili hutolewa kwa utaratibu wa kuchangia gharama za masomo, malazi na usafiri. Nchi wahisani kwa mfano, hulipia gharama za mafunzo na baadhi ya gharama za malazi, wakati usafiri wa kwenda na kurudi nyumbani, pamoja na gharama za mafunzo kwa vitendo wakiwa masomoni, zinakuwa juu ya wanafunzi husika. Kwa vile Serikali kwa wakati huo inatekeleza awamu ya tatu ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu, kwa wale wanafunzi wanaopata ufadhli wa nchi rafiki na ambao hawana uwezo, hulazimika kukopa baadhi ya gharama za mafunzo wakiwa chuoni toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzia mwaka 2005/2006, kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu vya nje na vya ndani ya nchi, gharama za elimu ya juu zinatolewa na Serikali kwa njia ya mikopo kwa wanafunzi wote waliotimiza vigezo. Aidha, mikopo hiyo haiwabagui watoto wa Maofisa wa Kibalozi wa Kitanzania, ilimradi

21 wawe wamekidhi masharti ya mikopo yanayotongazwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kila mwaka.

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuru kwa kunipa fursa hii. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kumuuliza kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa inatokea Serikali kuchelewesha mikopo hii kuwapelekea wanafunzi waliopo nje na kuwasababishia adha kubwa kama ilivyotokea kwa wanafunzi wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba kule Urusi mpaka baadhi yao ilibidi warudishwe nyumbani mwaka jana. Je, Naibu Waziri, anaweza kulieleza Bunge hili ni sababu zipi zilisababisha vijana hao kurudishwa nyumbani na nini hatma yao hasa tukitilia maanani kuwa tunahitaji sana wataalamu wa Sayansi na mambo mengine kwa wakati tulionao?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. GAUDENTIA M. KABAKA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa, kama ifuatavyo:-

Kabla ya yote, napenda nitoe taarifa kwamba, wanafunzi waliorudi siyo kwa sababu ya kucheleweshewa mikopo. Ucheleweshaji wa mikopo, mara nyingi una sababu mbalimbali, mojawapo ni wanafunzi wenyewe kuchelewa kujaza zile form na kuzipeleka katika Ofisi za Mabalozi na pia zile form lazima ziwe zimepitia kule vijijini kwao. Kwa hiyo, process hii yote wanafunzi wanakwenda kabla hawajazikamilisha na hivyo form zinapoturudia sisi unakuta pia muda umeshapita.

Sababu ya pili, kama tulivyosema, mwaka huu wa fedha (2008/2009), sasa hivi hatupeleki tena fedha zile katika Akaunti za Ofisi za Ubalozi, tunawapelekea wanafunzi wenyewe. Wanafunzi hawa waliambiwa taratibu za ku-deal na zile akaunti zao, watuletee swift code ili pesa ziweze kuingizwa kwenye akaunti. Baadhi ya wanafunzi hawakufanya hivyo, kwa hiyo, hawa pia pesa zilichelewa. Kwa hiyo, waliorudishwa siyo kwa sababu ya kucheleweshewa pesa.

Na. 117

Upungufu wa Walimu Mikoa ya Kusini

MHE. SULEIMAN O. KUMCHAYA aliuliza:-

Kwa kuwa Mikoa ya Kusini bado inakabiliwa na upungufu mkubwa wa Walimu:-

(a) Je, Serikali ina utaratibu gani wa kupata walimu wa kutosha kwa mikoa hiyo?

(b) Je, Serikali itatoa lini kipaumbele cha posho ya mazingira magumu kwa Walimu?

22

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Suleiman Omar Kumchaya, Mbunge wa Lulindi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uwepo wa uhaba mkubwa wa walimu nchi nzima, ikiwemo Mikoa ya Kusini. Mikakati ya Wizara ya kuwapata Walimu wa kutosha kwa lengo la kuondoa upungufu huo ni pamoja na:-

(i) Kuendelea kuajiri wahitimu wote wanaomaliza Vyuo vya Ualimu na Wataalam wengine, wanaopenda kujiunga na kazi ya Ualimu;

(ii) Kupanua Vyuo vya Ualimu ili kuongeza nafasi za wanachuo kulingana na mahitaji ya Walimu;

(iii) Kuendelea kushawishi sekta binafsi kuanzisha na kuendeleza Vyuo vya Ualimu ili kukabiliana na upungufu wa Walimu;

(iv) Kutoa vibali vya ajira kwa Walimu wa kujitolea kutoka Mashirika mbalimbali kama vile VSO, Peace Corps, KOICA na JICA; na

(v) Kuajiri kwa mkataba walimu wastaafu kufundisha katika shule zilizopo kwenye maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kutoa motisha na vivutio kwa walimu wanaofundisha katika maeneo yenye mazingira magumu. Wizara yangu imeweka kipaumbele katika ujenzi wa njumba za walimu na kuboresha mazingira ya shule zilizopo ili kupunguza ugumu wa mazingira ya kazi kwa walimu.

Pamoja na jitihada hizi, Serikali inatoa wito kwa Halmashauri zote kuandaa mazingira mazuri na vivutio kwa walimu wapya, mara wanapopangwa kufundisha kwenye Halmashauri zao, kwa lengo la kuwavutia kufanya kazi huko. Mfano mzuri ni Mkoa wa Rukwa, ambao umekuwa ukitoa fedha taslim na samani kwa walimu waliopangiwa kazi na kuripoti katika shule mbalimbali katika Mkoa huo. Aidha, Wilaya ya Tandahimba, imetoa jukumu kwa kila Kata, kuwawezesha walimu wanaoripoti na kufanya kazi katika Kata zao.

MHE. SULEIMAN O. KUMCHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa moja kati ya sababu zinazochangia uhaba wa walimu katika Mikoa ya Kusini ni kutoa ruhusa mfululizo kwa walimu wanaokwenda kusoma zaidi. Je, Serikali

23 haioni kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu hizi ili walimu wengine wabaki waendelee kufundisha kuliko kutoa ruhusa hizi kwa walimu wote katika shule moja?

Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kuna mipango ambayo ipo, kwa mfano, kupanua vyuo vya ualimu, kuruhusu Sekta Binafsi ili walimu wengine waweze kupatikana. Je, mpango huu umeshaanza kufanya kazi hivi sasa ama ni mpango wa baadaye?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI (MHE. MWANTUMU B. MAHIZA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Suleiman Kumchaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ruhusa kutolewa kwa walimu, zinafuata utaratibu kwamba, mwalimu aliyetoka katika Vyuo vya Ualimu anapopangiwa kazi, anapaswa kutumikia kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuendelea na mafunzo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, zipo taratibu nyingi ambazo mwalimu anaweza akajiruhusu bila kusubiri idhini kutoka Wizara ya Elimu.

Moja, ni kuchukua likizo bila malipo na kwa kuwa katika vyuo vikuu wanapata mkopo, anapopata sifa za kupata mkopo anaacha kazi. Tatizo lake ni kwamba, tunamkosa sasa hivi lakini tutakuja kumwajiri tena akiwa na shahada. Kwa hiyo, kuna ugumu hapa kutokana na kujiendeleza na hasa ikizingatiwa kwamba, umri wanakwambia wakati ni huu nikisubiri naweza nisipate hiyo fursa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala tunalifanyia kazi na hivi sasa tunao utaratibu wa kuorodhesha ambao watapata vibali vya kwenda kusoma, lakini inapobidi mwalimu akachukua likizo bila malipo, huna la kumfanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kuongeza idadi ya walimu na mipango tuliyoieleza kwa muda mrefu, kila mara tumekuwa tukielezea hapa Bungeni kwamba, tunayo mipango ya muda wa kati na muda mrefu. Mipango hii ya muda wa kati, imeshaanza kutoa matunda. Mipango ya muda mrefu ni ya Walimu wa Shahada ambao kuanzia mwaka jana, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitengo cha Ualimu, kimeanza kutoa matunda yake na walimu hawa tayari wameshapangiwa kazi. Mwaka huu baadhi ya vyuo kama vine, kikiwemo Chuo Kikuu cha Ualimu Mkwawa, watatoa wanafunzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba tujiridhishe kwamba, tunalifahamu hili tatizo, tuna dhamira ya dhati kabisa ya kuhakikisha uhaba huu mkali unaondoka.

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nashukuru sana kwa majibu mazuri yaliyotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri. Ninamshukuru sana ndugu yangu Suleiman Kumchaya kwa swali hili zuri.

24 Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imechukua hatua za aina mbalimbali katika kuhakikisha kwamba, inakabiliana na tatizo hili la ukosefu wa walimu ambalo lipo nchi nzima.

Ningependa niongezee tu kwamba, pamoja na kuongeza nafasi za ualimu kwa kufungua Vyuo Vikuu vya Ualimu; Chang’ombe na Mkwawa, Serikali pia imefungua Chuo cha Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma, ambacho tunategemea kitakuwa na wanafunzi 15,000. Chuo hiki kimeanza kufanya kazi na hivi sasa tunao wanafunzi pale wanaokaribia 4,000. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaendelea kufungua vyuo pamoja na Sekta Binafsi katika maeneo mbalimbali nchini kwetu. Nikitoa mfano, mwaka jana nimeweka jiwe la msingi kwa ajili ya kufungua Chuo cha Ualimu katika Shirika la Umma kule Tunduru, kama hatua ya kuongeza walimu katika Mikoa ya Kusini.

Na. 118

Uhaba wa Askari Polisi Nchini

MHE. KAIKA S. TELELE aliuliza:-

Kwa kuwa katika Bajeti ya Mwaka 2008/2009 ilidhihirishwa kuwa hapa nchini kuna uhaba mkubwa sana wa Askari Polisi ikilinganishwa na ukubwa wa nchi kijiografia na mtawanyiko wa wananchi nchini:-

(a) Je, kiuwiano askari mmoja anapaswa kulinda Watanzania wangapi kama ilivyo kwa mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi 40 - 45?

(b) Je, ni kwa nini askari wachache waliopo waruhusiwe kuajiriwa na mashirika ya umma kabla ya mikataba yao na Serikali kumalizika?

(c) Je, isingekuwa busara kwa askari hao kuajiriwa kwingine baada ya kustaafu kwa kuwa bado wana nguvu na ukakamavu?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kaika Telele, Mbunge wa Ngorongoro, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na idadi ya askari tulionao, kiuwiano askari mmoja analinda wananchi 1,300, wakati uwiano unaokubalika Kimataifa ni askari mmoja wananchi 400 - 500.

25 (b) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sheria inayoanzisha Jeshi la Polisi (The Police Force and Auxiliary Services Act, Cap. 322 R.E 2002), hairuhusiwi kwa askari yeyote kuajiriwa kokote, kabla hajamaliza mkataba wake wa ajira katika Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, kwa kuwa katika Jeshi la Polisi tunao Wataalamu wa fani mbalimbali, ambao utaalamu wao unahitajika pia katika kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali, Jeshi la Polisi limekuwa likiwaruhusu kujiunga na Taasisi za Serikali, ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tumekuwa tunawaruhusu askari ambao wanachukua elimu za juu kama vile Madaktari, Wahasibu na Wahandisi, ambao mojawapo ya matakwa ya kuhitimu taaluma zao ni kufanya mazoezi ya vitendo (internship), katika Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma. Uwepo wa askari hawa ni kwa kipindi cha mafunzo yao tu na si kwamba wameajiriwa huko.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana sana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, baada ya kustaafu kazi katika Jeshi la Polisi au kuacha kwa mujibu wa Sheria, askari hakatazwi kuajiriwa mahali popote, iwapo atatimiza masharti ya mwajiri mpya.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na maelezo mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa Wilaya ya Ngorongoro ni kubwa sana kijiografia zaidi ya kilomita za mraba 14,000; na kwa kuwa Wilaya hiyo inapakana na Jamhuri ya Kenya kwa ukanda mrefu sana ambapo kuna njia nyingi sana za panya zinazotumiwa na majambazi wa Kisomali kuingia nchini na kupora mali ya wananchi na kuteka au kuua watalii; je, Serikali ina mkakati gani wa makusudi wa kuongeza askari katika Wilaya hiyo na kuwaongezea nyenzo za kazi kama vile magari na silaha ya AK 47 ili waweze kukabiliana na uharifu huo?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kaika Telele kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hali anayoisema tunaitambua na tunaizingatia. Vilevile afahamu kwamba, kutokana na uhaba wa vitendea kazi ni suala ambalo tumekuwa tunalizungumzia sana, lakini hiyo haina maana kwamba, kuna ulegevu kwa upande wetu katika kutazama na kuhakikisha kwamba, amani inakuwepo katika taifa letu.

Haya niliyoyasema ya vitendea kazi na haya aliyoyasema ya kuhakikisha kwamba, tunachukua hatua zinazostahili kwa majambazi ambao wanatoka nchi jirani na sisi tumeyazingatia na tutafanya kila jitihada kuhakikisha mambo yanakwenda sawa sawa.

26 Na. 119

Kurekebisha Mfumo wa Utawala Katika Vituo vya Mipakani

MHE. BASIL P. MRAMBA aliuliza:-

Kwa kuwa kuna ongezeko la wahamiaji haramu kupitia mipaka yetu; na kwa kuwa yapo matatizo mengine ya uvunjifu wa Sheria kwa mfano katika biashara na kadhalika; je, ni lini Serikali itarekebisha mfumo wa utawala kwenye vituo vya mipakani nchini kwa lengo la kuongeza uwajibikaji kwa mfano kuwa na Mkuu mmoja wa kituo kama ilivyo kwa TRA?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Basil Mramba, Mbunge wa Rombo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakubaliana na maoni ya Mheshimiwa Mramba na Wabunge wengine wengi, kuhusu baadhi ya matatizo katika mipaka ya Taifa letu. Kutokana na hayo, Serikali imefanya marekebisho katika mfumo wa Uongozi wa Idara ya Uhamiaji.

Katika muundo huo mpya, kumeongezwa Kitengo cha Border Management and Operation, ambacho pamoja na mambo mengine, kinasimamia operesheni, misako na doria katika mipaka ya ndani ya nchi, kwa lengo la kudhibiti uhamiaji haramu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vituo vyote vya uhamiaji vya mipakani huongozwa na Wakuu wa Vituo, ambapo kwa mujibu wa muundo wa Idara, wanawajibika kwa Wakuu wa Uhamiaji wa Wilaya katika baadhi ya Mikoa. Pale inapokuwa hakuna Afisa wa Uhamiaji wa Wilaya, Mkuu huyo wa kituo, anawajibika kwa Mkuu wa Uhamiaji wa Mkoa husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

MHE. BASIL P. MRAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, sisi tunaokaa mikapani tunaelewa kwamba, vituo vya mpakani vina uhamiaji, usalama wa taifa, watu wa forodha, watu wa TBC na watu wengine wengi wako pale kutegemea eneo.

Je, Naibu Waziri anataka kunieleza kwamba huyo wa Uhamiaji atatawala na wa Forodha na wa Idara nyingine pale itakapotokea tatizo; kwa mfano, kama ungetokea uvamizi kutoka upande wa pili au vurugu kati ya wananchi wa upande mmoja na upande wa pili, huyu Bwana Uhamiaji ndiye atakayetoa amri ya kukabiliana na tatizo hilo ama atakuwa ni nani?

27 Kwa maana hiyo, nadhani ningetaka maelezo zaidi kwa sababu sidhani kama jibu hilo linatosheleza tatizo lenyewe.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Basil Mramba, kama ifuatavyo:-

Swali lake la msingi, alikuwa anataka kujua ongezeko la wahamiaji haramu na unapozungumzia wahamiaji haramu kwangu mimi ni suala ambalo wanashughulikia watu wa Uhamiaji.

Kwa suala la pili, amepanua wigo wa swali lake ambalo amezungumzia mambo ya Forodha na kadhalika na hiyo ni kweli kwa sababu katika mpaka wapo watu wengi; wapo wa TRA kama alivyosema, wapo watu wa Polisi, wapo watu wa TBS na kadhalika. Kwa hiyo, hilo ni suala pana na tutajaribu kumtafutia jibu, kwa sababu si jibu la Wizara ya Mambo ya Ndani peke yake, lakini ni suala ambalo linagusa Wizara nyingine mbalimbali na hili linataka mawasiliano na Wizara mbalimbali.

Kwa hali ilivyo hivi sasa ingawa anasema kweli anatoka mpakani, jitihada zinafanyika kuhakikisha kwamba, haya yote yanakwenda sawasawa na kila sehemu inatekeleza wajibu wake, kuhakikisha kwamba, hali katika mipaka yetu inakuwa ni ya usalama.

Kama kuna upungufu, basi hayo tutazungumza na Waheshimiwa hao na tutaona ni njia gani tuchukue ili kuweza kupata suluhu katika matatizo kama haya.

Na. 120

Ahadi ya Kufungua Tawi la NMB Bukombe

MHE. BUJIKU P. SAKILA (K.n.y. MHE. EMMANUEL J. LUHAHULA) aliuliza:-

Kwa kuwa Serikali kupitia ziara ya Mheshimiwa Rais iliahidi kuwa ifikapo Oktoba, 2007 Tawi la NMB litakuwa limefunguliwa Bukombe:-

(a) Je, ni nini kimesababisha ahadi hiyo isitekelezwe?

(b) Je, ni lini sasa tawi hilo litafunguliwa Bukombe ili kutekeleza ahadi ya Mheshimwia Rais kwa wapiga kura wetu?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Uchumi, naomba kijibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Luhahula, Mbunge wa Bukombe, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

28 Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, NMB haina Tawi Bukombe na huduma za kibenki zinahitajika katika meneo mengi hapa nchini. NMB tayari imefanya tathmini ya kufungua tawi katika eneo la Bukombe ili kuona uwezekanao wa kufungua tawi la Benki hiyo hapo. Hivyo, kwenye mpango mkakati wa NMB, imepangwa pamoja na kufungua matawi kadhaa mengine, kufungua tawi hili linaloombwa la Bukombe.

Tayari NMB imetathmini jengo lililopatikana kwa ajili ya kuanzisha tawi hilo, lakini kwa bahati mbaya lilionekana kutokukidhi viwango vinavyohitajika. Kutokana na hali hiyo, Benki ya NMB imelazimika kuanza taratibu upya za kununua au kujenga jengo litakalokidhi viwango vya Benki, Tawi la Bukombe.

MHE. BUJIBU P. SAKILA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ninamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa jibu lake zuri sana, lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika hivi sasa mtandao wa NMB, umekuwa ni mkubwa sana na Wilaya nyingi sana zina matawi yake, lakini wateja wake wengi wanatoka vijijini na kwenye Kata. Kwa nini sasa NMB isianze kufungua matawi yake katika Tarafa ili kuwapunguzia kazi watumishi wanaokwenda Wilayani kwa wingi?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Bujibu Sakila, kama ifuatavyo:-

Kwa kumhakikishia kwamba dhamira ya NMB ni kufika mpaka kwenye Tarafa, lakini kwanza kwa sababu kuna ngazi ya Wilaya, inaonekana ni vizuri kumaliza ngazi ya Wilaya, ingawa pamoja na hilo, kabla tawi lolote halijafunguliwa, kuna vigezo ambavyo vinatathminiwa na vikishafikiwa basi matawi yanafunguliwa hata kama ni kwenye ngazi ya Tarafa.

Na. 121

Taarifa za Mashirika ya Serikali

MHE. MWADINI A. JECHA aliuliza:-

Kwa kuwa Mashirika yote ya Serikali yana mfumo wa Uongozi na Bodi kwa lengo la kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kuwasilisha taarifa ya hesabu za mapato na matumizi kila mwaka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali, lakini kuna mashirika ambayo hayajatoa hesabu zake kwa Mkaguzi Mkuu kuanzia mwaka 2005 – 2007:-

(a) Je, ni Mashirika mangapi ya Serikali ambayo hayajatoa hesabu zake kwa Mkaguzi Mkuu kuanzia mwaka 2005 - 2007?

29 (b) Je, hatua gani zimechukuliwa dhidi ya Uongozi na Bodi za Mashirika hayo?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Uchumi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwadini Jecha, Mbunge wa Wete, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma ya Mwaka 2001 na kama ilivyorekebishwa Mwaka 2004, Taasisi na Wakala zote za Serikali na Mashirika, ambazo nusu ya mapato yake yanatolewa na Serikali, pamoja na mashirika ambayo Serikali inamiliki zaidi ya 50% ya hisa, yanawajibika kuandaa taarifa za hesabu za kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesbu za Serikali (CAG), kwa ajili ya ukaguzi.

Hesabu hizo zinatakiwa ziwasilishwe kwa Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), katika kipindi cha miezi sita baada ya kufunga mwaka wa Shirika au Taasisi husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mashirika na Taasisi ambazo Serikali inamiliki zaidi ya 50% ya hisa na ambazo zilikuwa hazijawasilisha taarifa ya hesabu za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 hadi 2007 ni 56.

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Fedha na Uchumi, imekuwa ikitoa maelekezo kwa Mashirika ya Umma na Taasisi za Umma, kuhakikisha hesabu zake zinakamilika na kuwasilishwa kwa wakati kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Inapothibitika kwamba, hili halikufanyika, hatua zinazochukuliwa ni pamoja na kuishauri Wizara husika, kurekebisha Bodi ya Wakurugenzi na pia kuuwajibisha uongozi, kwa mujibu wa taratibu za Shirika la Ajira za Viongozi husika.

MHE. MWADINI ABBAS JECHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tumeelezwa hapa kwamba, miongoni mwa fedha inayotumika kuendesha mashirika ya umma ni jasho la walipa kodi wa Tanzania. Ili kuona kwamba, fedha hizo zinatumika ipasavyo; je, Serikali sasa ipo tayari kuanzisha Kituo Maalum, ambacho kitakuwa kinafanya wajibu wa investment appraisal kwa mashirika hayo ili kuiwezesha Serikali kufanya vipaumbele sahihi katika kuipatia fedha miradi hiyo?

La pili, kwa kuwa mfumo wa uendeshaji wa Mashirika ya Umma uliopo hivi sasa hautoi fursa nzuri ya kufanyia tathmini utendaji wake; je, Serikali itakubaliana nami kwamba ipo haja kwa Bodi za Wakurugenzi za Mashirika hayo kuingia Mkataba na Watendaji wa kufanya performance contracts na management ili hatimaye iwe ni rahisi kufanya uhakiki wa kiutendaji ya management ya Bodi hizo?

NAIBU SPIKA: Naibu Waziri, naomba ujibu kwa kifupi tu.

30 NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. JEREMIAH S. SUMARI): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, kila Shirika ama Taasisi, ina madhumuni iliyoanzishwa nayo na tunatarajia kwamba, itakuwa katika utekelezaji wa madhumuni hayo. Pale inapodhihirika kwamba, kuna jambo maalum ambalo kwa mfano, linahitaji kikosi kazi ama Tume yoyote ile ambayo itasaidia utekelezaji wa yale madhumuni yake, basi hiyo huwa inafanyika.

La pili, kuhusu tathmini na ushauri wa Bodi na Management kuingia katika Mkataba, tayari kwa misingi ya Utawala Bora wa Mashirika na Makampuni, hilo linafanyika. Katika utawala wa Shirika lolote au Taasisi, Bodi ndiyo msimamizi mkuu wa lile Shirika, halafu management inawajibika kwa Bodi na wafanyakazi wanawajibika kwa management. Kwa hiyo, tayari kuna mkataba ambao unatarajiwa kwamba, utakuwa unafanya kazi. Kwa hiyo, pamoja na ushauri mzuri sana sidhani kwamba, jinsi Mashirika yalivyo na jinsi Utawala Bora wa Mashirika ulivyo, kunakuwa na ulazima wa kuingia kwenye Mikataba Maalum ya Uendeshaji wa Mashirika haya.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali yamekwisha na muda wa maswali umekwisha. Sasa wageni; ninao wageni waliopelekwa ofisini, ninao wageni wenye vikaratasi na miandiko mingine siwezi kuisoma. Kwa hiyo, kuna uwezekano kabisa wageni wengine wasitajwe au watajwe vinginevyo.

Waheshimiwa Wabunge, tuna utaratibu wa kupeleka majina ya wageni ofisini yanachapishwa, halafu yanatajwa vizuri. Wageni waliopo Bungeni asubuhi hii:-

Kwanza, kuna wageni wa Mheshimiwa Mwantumu Mahiza, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, watoka nchi ya Oman, nafikiri ndiyo hao hao ni wataalam ambao Mheshimiwa ana uhusiano nao. Hawa ni wataalam wa kuzalisha umeme kwa kutumia taka ngumu, naomba pale walipo wasimame, hawapo. Nadhani hata kesho wakija tungependa kuwaona, maana inaonekana ni watu muhimu sana.

Tuna mgeni wa Mheshimiwa Prof. Raphael Mwalyosi, ambaye ni Brigita Haule, Mheshimiwa Diwani wa Viti Maalum, Kata ya Mawingi, Wilaya ya Ludewa. Mheshimiwa Diwani, karibu maana wewe upo jirani yangu pale.

Tuna mgeni wa Mheshimiwa Monica Mbega, ambaye ni Ndugu Butinini M. Butinini, mkereketwa wa CCM na mshauri wa SACCOS ya Vijana wa CCM kutoka Iringa Mjini; yuko wapi mkereketwa huyo? Ahsante, karibu.

Tuna mgeni wa Mheshimiwa , ambaye ni Mwalimu William Mkoswe, ahsante. Karibuni sana mwalimu.

Tuna wageni wa Mheshimiwa Christopher Ole-Sendeka, ambao ni Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mererani; Awadhi Omar Yussuf na Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mererani, Bwana Herbert Ngala; karibuni sana.

31 Tuna wageni wa Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Tabora, ambao ni waimbaji wa Tumwinue Bwana Group kutoka Tabora; naomba wote pale walipo wasimame. Ahsante, karibuni sana. (Makofi)

Tunao wanafunzi na walimu kutoka Central High School Dodoma, naomba pale walipo wasimame. Karibuni sana, Bunge lipo kwenu ni vizuri mkawa mnashiriki kama hivi. Ahsanteni.

Tunao wageni 20 wa Ofisi ya Bunge, hao ni wasanii wa Kikundi cha Kaole Sanaa Group, ambao wamealikwa kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya wa 2009, itakayofanyika kesho. Wanaongozwa na Simon Simalenga, Katibu Mkuu wa Kikundi hicho. Naomba wasimame wasanii wote. Ahsanteni karibuni sana.

Sasa kuna mgeni wa Mheshimiwa , Elifadhili Ngelesa, naomba asimame, ahsante.

Nina wageni wa Waheshimiwa Wabunge wa Singida; Mheshimiwa Juma Killimbah na Mheshimiwa Diana Chilolo, ambao ni Hassan Matoto, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Kata ya Shelui, Jimbo la Iramba. Naomba asimame huyo Katibu. Ahsante.

Nina wageni wa Waziri wa Mambo ya Ndani nadhani, hawa ni Wakurugenzi wa Shirika la Blue Finance Services, ambao ni Christocloper, Regional Director na Riwiti, Country Director. Mnakumbuka tuliwahi kupata maelezo kidogo kuhusu Blue Financing Service, sijui kama miaka miwili imepita? Nafikiri wamekuja sijui wataonana na nani? Kwa hiyo, ni vizuri Mheshimiwa Waziri aliyewaleta hapa, basi Waheshimiwa Wabunge, wanaweza kuwasikiliza. You are welcome.

Kwa hiyo, ningependa pia niwatambue wale wageni wanaotoka Oman, wenye utaalam wa kutengeneza umeme kutokana na taka ngumu, naona kama wameingia; karibuni sana. Tumefurahi kuwaona na hayo mema mliyokuja nayo, tungependa hata sisi tuyafahamu na yatusaidie, kwa sababu nadhani ni jambo muhimu sana. (Makofi)

Matangazo ya kazi; Waheshimiwa Viongozi wa makundi yanayohusika; na ninyi mmeanza uvivu ni lazima mlete kwenye minute siyo karatasi zilizochapwa kwenye madaftari zinaletwa kutangaza hapa, yanaweza yakakataliwa.

Kwa hiyo, naanza na matangazo yaliyoandika kwenye minutes. Mheshimiwa Wilson Masilingi, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba, leo tarehe 6 Februari, 2009 saa tano asubuhi katika Chumba Namba 231, ghorofa ya pili, watakuwa na mkutano.

Mheshimiwa Kabwe Zubeir Zitto, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, anapenda niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba, leo

32 tarehe 6 Februari, 2009, saa tano asubuhi, kutakuwa na mkutano wa Wajumbe hao katika Chumba Namba 219.

Nina tangazo la Mheshimiwa Dkt. , Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati hiyo kwamba, leo tarehe 6 Februari, 2009 kutakuwa na kikao cha Kamati hiyo saa 7.30 mchana. Kikao kitafanyika katika Ukumbi wa .

Mheshimiwa Gideon Cheyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati hiyo kwamba, leo tarehe 6 Februari, 2009 watakuwa na kikao katika Chumba Namba 133, kikao kitafanyika saa 5.30.

Mwenyekiti wa Tawi la CPA la Tanzania (Commonwealth Parliamentary Association Tanzania Branch), Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Tawi hili kwamba, kutakuwa na Kikao cha Kamati ya Utendaji leo tarehe 6 Februari, 2009 saa 7.00 mchana katika Chumba Namba 227.

Sasa nije kwenye vile vikaratasi vinavyoandikwa andikwa hivi. Nafikiri Mheshimiwa Halima Mdee, anaomba niwatangazie Kambi yote ya Upinzani kwamba, watakuwa na kikao katika Ukumbi wa Kasusura saa 7.00 mchana.

Mwenyekiti wa Mtandao nafikiri ni Mheshimiwa Prof. Mwalyosi huyu, anasema naomba unisaidie kutoa tangazo hapa Bungeni, Waheshimiwa Wabunge ambao Wajumbe wa Mtandao wa Mazingira, wahudhurie kikao leo saa 5.00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Jengo hili la Bunge.

Waheshimiwa Wabunge, kawaida vile vikao ambavyo si vya Kamati za Kudumu za Bunge, vinaanza saa 7.00 mchana. Vikao ambavyo ni vya Kamati za Kudumu za Bunge, vinaweza kufanyika wakati Bunge linaendelea. Wanamtandao wa Mazingira, naomba mkutane saa 7.00 mchana katika Jengo hili la Bunge.

Tangazo la Ofisi, Waheshimiwa Wabunge wote, kesho tarehe 7 Februari, 2009 kutakuwa na tafrija ya kujipongeza kwa kuanza mwaka mpya wa 2009 na kumuaga aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bwana Damian Foka, katika eneo la Bunge. Kadi za mwaliko zitagawiwa, lakini Waheshimiwa Wabunge wote mnakaribishwa, usije ukakosa kadi ukasema hujaalikwa. Kesho kutakuwa na tafrija hiyo saa 1.00 usiku.

Baada ya matangazo hayo, naomba nieleze kwamba, Mheshimiwa Spika, yupo Dar es Salaam, kushiriki kwenye Siku ya Sheria, ambayo inafanyika leo, lakini kesho tutakuwa naye.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na shughuli nyingine. Katibu.

MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI

33

Muswada wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2008 (The Political Parties (Amendment) Bill, 2008)

(Kusomwa Mara ya Pili)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile ni mara yangu ya kwanza kwa mwaka huu wa 2009, kusimama na kuwasilisha hoja katika Bunge letu, napenda kutoa salamu za kheri na nafaka tele kwa Waheshimiwa Wabunge wote. Napenda kutoa salamu hizo kwa kipekee kabisa, kwa Wananchi wa Mbulu, ambao ninawawakilisha hapa Bungeni. Kipekee, kwao nasema kwamba, tuendelee na desturi yetu ya kushirikiana ili kuiendeleza Wilaya yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia nichukue fursa hii, kuwapa pole nyingi, Waheshimiwa Wabunge waliondokewa na ndugu, wenziwao na hasa Wananchi wa Mbeya Vijijini, kwa kifo cha aliyekuwa Mbunge wao, Hayati Richard Nyaulawa. Kama ilivyo desturi, uchaguzi umefanyika na Wananchi wa Mbeya Vijijini, wamepata Mbunge mpya, Mheshimiwa Mchungaji Luckson Mwanjale, naye nampongeza sana na ninamkaribisha kwenye nyumba hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kutoa hoja kwamba, Muswada wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2008 (The Political Parties (Amendment) Bill, 2008) kama ulivyorekebishwa kwa mujibu wa majedwali mawili ya marekebisho, sasa usomwe kwa mara ya pili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada huu umefikia hatua hii baada ya michango, mawazo na maoni kutoka kwa wadau mbalimbali. Naomba nichukue fursa hii, kuwashukuru sana Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Tume ya Kurekebisha Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar, Tume ya Uchaguzi Zanzibar na Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa kudumu, kwa michango ya awali katika maandalizi ya Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, shukrani nyingine pia ziwaendee watumishi wa ofisi yako na hasa wewe na Mheshimiwa Spika, kwa kunipa muda huu ili niweze kutoa hoja hii muhimu kwa maslahi ya Vyama vyetu vya Siasa na maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika ile ibara ya 3(1) inasema, Tanzania ni nchi ya kijamaa yenye Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa. Ibara ya 3(2) inaeleza kwamba, uendeshaji wa Vyama vya Siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, shughuli za uandikishaji na usimamizi wa Vyama vya Siasa, hufanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa, chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992. Muswada huo unatoa mapendekezo ya kutunga sheria ya marekebisho.

34

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirejee hapo, Muswada ulio mbele yetu, unatoa mapendekezo ya kutunga Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Namba Tano ya mwaka 1992, kwa lengo la kuondoa kasoro na dosari zilizojitokeza katika utekelezaji wa sheria hiyo, kwa muda huu uliopita. Madhumuni ya kuondoa kasoro hizo ni kudumisha demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa nchini kwetu. Aidha, marekebisho yanayopendekezwa yanakusudia kuboresha utaratibu na utendaji katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kumwongezea madaraka ya kiutendaji ya kufanya maamuzi ambayo hayahitaji ridhaa ya Waziri mwenye dhamana ya Vyama vya Siasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada umegawanyika katika sehemu mbili muhimu: Sehemu ya kwanza ni ile inayohusu jina la sheria inayopendekezwa; na sehemu ya pili, inapendekeza marekebisho mbalimbali katika Sheria ya Vyama vya Siasa. Maeneo yanayohusika hasa katika ile Sheria ya 1992 ni vifungu vya 3, 4, 9, 10, 14, 19 na kifungu cha 22. Aidha, vifungu vifuatavyo vimeongezwa; kifungu cha 8(a) na (b); 10(a); 11(a),(b) na (c); 12(a) na (b); 18(a); 21(a) na (b).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muhtasari, Muswada huu unalenga yafuatayo:-

Kwanza, kuifanya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kuwa asasi huru chini ya Waziri mwenye dhamana ya Vyama vya Siasa.

Pili, kumpa uwezo Msajili wa Vyama vya Siasa, kusajili Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa vilivyosajiliwa katika Daftari Maalum na pia kufanya usajili upya endapo vyama vitakuwa vimeungana na kuwa Chama kimoja.

Tatu, kuchunguza na kudhibiti maadili na vitendo ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi yetu.

Nne, kukataza Usajili wa Chama cha Siasa, ambacho kinaruhusu wanachama au viongozi wake, kutumia lugha ya matusi au udhalilishaji dhidi ya Chama kingine.

Tano, kuzuia mwanachama kuwa na uanachama katika vyama viwili au zaidi, pamoja na kuweka vigezo vya uongozi katika Vyama vya Siasa kama vilivyo kwa mtu anayetaka kuwa Mbunge, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977 ile ibara ya 67.

Sita, kuruhusu Vyama vya Siasa kuungana wakati wowote na nyadhifa za viongozi wa vyama vilivyoungana, kukomaa baada ya kuungana. (Makofi)

Saba, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, atakuwa sasa amepewa uwezo wa kukagua Hesabu za Vyama vya Siasa, badala ya wakaguzi binafsi waliokuwa wanateuliwa na Vyama vyenyewe kama ilivyo sasa. (Makofi)

35 Nane, katika mabadiliko ya ibara ya 11(c), Muswada huu unatoa haki kwa Vyama vya Siasa kuwa na Bendera na kuzitumia kama itakavyofafanuliwa katika kanuni zitakazowekwa kwa mujibu wa Sheria hii. Tisa, Ibara mpya ya 21(b) inapendekeza kuwa na Baraza la Vyama vya Siasa ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania na Wajumbe wake watakuwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vilivyosajiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza hapo awali, iwapo Muswada huu wa Sheria utapitishwa na Bunge lako Tukufu kuwa Sheria, utasaidia sana. Kwanza, kuondoa kasoro zinazojitokeza katika utekelezaji wa Sheria Namba Tano ya Mwaka 1992. Pili, kuboresha utaratibu wa utendaji katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Tatu, kudumisha Demokrasia ya Vyama Vingi katika siasa za nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo mafupi, nawaomba Waheshimiwa Wabunge, waujadili Muswada huu na baadaye nitaomba Bunge liweze kuupitisha ili hatimaye kwa kadiri itakavyokuwa imependekezwa, Mheshimiwa Rais, aweke saini na uwe sheria kamili.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

NAIBU SPIKA: Muswada umeungwa mkono. Sasa nitamwita Mjumbe wa Kamati iliyopitia Muswada huu, Mheshimiwa Stephen Galinoma.

MHE. STEPHEN J. GALINOMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kwa Muswada wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2008 (The Political Parties (Amendment) Act, 2008).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, kifungu cha 86(5), Toleo la Mwaka 2007, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uanzishwaji wa Vyama vya Siasa wa Mwaka 2008 (The Political Parties (Amendment) Act, 2008).

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Utaratibu na Bunge, Mheshimiwa Philip Marmo, kwa uwasilishaji wake mzuri wa sababu na madhumuni ya Muswada huu, alioufanya mbele

36 ya Kamati yangu, Siku ya Ijumaa tarehe 17 Oktoba, 2008, Ofisi Ndogo ya Bunge Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Waziri kuwasilisha Muswada huu, Kamati ilitoa fursa ya kusikiliza maoni na ushauri wa wadau wanaoguswa na utekelezaji wa Sheria hii. Wadau wote walioshiriki na kuomba kutoa maoni na ushauri wao, walipatiwa fursa hiyo na Kamati yangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya wadau walioshiriki kutoa maoni na ushauri wao mbele ya Kamati hii ni Mashirika yasiyo ya Kiserikali, ambayo ni National Organization for Legal Assistance, Legal and Human Right Centre, Vyama vya Siasa ambavyo ni SAO, UPDP, CUF, CHADEMA, TLP na wengine wengi walileta maoni yao kwa maandishi, kwa mfano, Chama cha TADEA.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninawashukuru wadau wote walioshiriki na kutoa maoni yao, ambayo yamezingatiwa katika mabadiliko ya Muswada huu. Mengine yameahidiwa kuwa yatazingatiwa katika utayarishaji wa kanuni ya sheria itakayotokana na Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla, Kamati imeridhishwa na maudhui na madhumuni ya Muswada huu, ambao una lengo la kurekebisha upungufu uliomo katika Sheria Mama ya Uanzishwaji wa Vyama vya Siasa Namba Tano ya Mwaka 1992, ili iweze kuboreshwa na kuimarisha Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa uliopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada huu vilevile unalenga kuondoa migogoro, kukuza demokrasia, kuimarisha maadili katika utendaji wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, pamoja na kujaribu kuondoa na kutatua baadhi ya upungufu wa uendeshaji wa Vyama vya Siasa, ulioonekana katika uzoefu wa takriban miaka 16 tangu kuanzishwa kwake.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuunga mkono Muswada huu, Kamati ilitoa maoni ya mabadiliko katika baadhi ya vifungu vya Muswada na kuunga mkono baadhi ya maoni ya wadau na kumshauri Mheshimiwa Waziri ayazingatie.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafurahi kulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba, maoni ya Kamati pamoja na yale ya wadau, yamezingatiwa katika mabadiliko ya Muswada huu uliowasilisha na Mheshimiwa Waziri katika Orodha ya Shughuli za leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko hayo ambayo Kamati ilitoa ushauri na mapendekezo katika Muswada huu ni kama ifuatavyo:-

(a) Kifungu cha pili cha Muswada kifanyiwe mabadiliko kwa kufafanua zaidi maana ya maneno National Leader, kuongezewa mwishoni maneno as prescribed in Constitution of the Political Party na Administrative Committee, nacho kiongezwe maneno kama ya hapo juu.

37 (b) Kifungu cha tatu cha Muswada katika section (b)(i), kifanyiwe marekebisho ya kiuandishi (recasting) na sentensi hiyo ianze na maneno yafuatayo: “There shall be an office of the Registrar of the Political Parties.”

(c) Kamati imeshauri pia katika kifungu kipya (8)(a)(i) liondolewe neno shall be required to apply to the Registrar, badala yake iwe shall fill a special form; ili kuepusha kiongozi aliyechaguliwa na wanachama wake kukataliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

(d) Kiongezwe kifungu 8(b) katika Sheria Mama kitakachoonyesha wapi Register ya Vyama vya Siasa itakapokuwa inakaa.

(e) Katika cha 9(f) Kamati imeona ili lugha ikae vizuri, neno defamation liwe defematory.

(f) Kifungu cha 7 cha Muswada katika kifungu cha 10(a) cha Sheria Mama kiongezwe kifungu (d) kitakachosomeka kuwa, muhusika atakuwa off sound mind. Katika kifungu cha nane cha Muswada, Kamati imependekeza kifungu cha 11(c) kilichopendekezwa kifutwe na kifungu cha 11(d) sehemu ya tatu kiandikwe upya na badala ya kuonyeshwa kuwa a Member or a Leader of a registered political party, sasa kioneshe ni any person.

Katika kifungu cha 12 cha Muswada, Kamati imependekeza kuwa, kifungu cha 21(b) kinachopendekezwa kiwepo katika sheria mama, kifutwe kabisa na kiandikwe upya. Katika kufanya hivyo, Msajili na Naibu Msajili, wasiwekwe kuwa ni Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa. Kamati imependekeza kuwa, Ofisi ya Msajili iwe ni Sekretarieti ya Baraza hilo na Mwenyekiti, pamoja na Makamu wake, wachaguliwe kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza hilo. Sehemu ya pili, kifungu cha 21(c), Kamati imependekeza kifanyiwe marekebisho ya uandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nachukua fursa hii, kuwashukuru Wajumbe wa Kamati hii, kwa kazi nzuri ya kujadili na kuchambua Muswada huu, ambao umuhimu wake kwa ujenzi wa demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, unaeleweka na kila mwananchi wa Taifa letu.

Umahiri na uzoefu wa muda mrefu wa mambo mbalimbali ya kisiasa na kijamii wa Wajumbe hao, ndio uliofanikisha kazi hii. Kwa heshima na taadhima, naomba niwatambue kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa George Malimba Lubeleje, Mwenyekiti, Mheshimiwa Ramadhani Maneno, Mheshimiwa Yusuf Makamba, Mheshimiwa Kingunge Ngombale-Mwiru, Mheshimiwa Stephen Galinoma, Mheshimiwa Fatma Maghimbi, Mheshimiwa Pindi Chana, Mheshimiwa Shoka Khamis Juma, Mheshimiwa , Mheshimiwa Rajabu Hamad Juma, Mheshimiwa Abubakar Khamis Bakar, Mheshimiwa John Lwanji, Mheshimiwa Salim Yussuf Mohamed, Mheshimiwa Riziki Omar Juma, Mheshimiwa Abbas Mtemvu na Mheshimiwa Benedict Ngalama Ole- Nangoro. (Makofi)

38

Aidha, napenda kumshukuru Dkt. Thomas Kashililah, Katibu wa Bunge na Watendaji wote wa Ofisi ya Bunge, kwa kufanikisha shughuli za Kamati. Bila ya kuwasahau Makatibu wa Kamati hii; Ndugu Charles Mloka, Ndugu Ramadhani Abdallah na Ndugu Elihaika Mtui, kwa kuratibu shughuli zote za Kamati na kuhakikisha kuwa, maoni ya Kamati yanakamilika kwa wakati uliopangwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja na naomba kuwasilisha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante msemaji kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati. Sasa nitamwita Msemaji kutoka Kambi ya Upinzani ili aweze kutoa maoni ya Kambi ya Upinzani.

MHE. HALIMA J. MDEE – MSEMAJI MKUU WA UPINZANI KWA OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, ningependa kutumia fursa hii, kukushukuru kwa kunipatia nafasi ya kutoa maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 86(6), Toleo la 2007.

Mheshimiwa Naibu Spika, madhumuni na sababu ya uwepo wa Muswada huu, kama ilivyoainishwa na sheria husika ni kuondoa kasoro zinazojitokeza katika utekelezaji wa sheria iliyopo sasa ili kudumisha Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Nchini. Hali kadhalika, kuboresha utaratibu na utendaji katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kuifanya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kuwa asasi huru, ikiwemo kumwongezea madaraka ya kuitendaji ya kufanya maamuzi ambayo hayahitaji ridhaa ya Waziri mwenye dhamana ya vyama vya siasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi ya Upinzani, haipingani na dhana nzima ya Muswada, kwa kuwa tunaamini kwamba, kuwepo kwa uhuru katika Ofisi ya Msajili, kuna nafasi kubwa sana katika mchakato wa demokrasia katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kukubaliana na dhana husika, bado kuna masuala kadhaa kwenye sheria hii yenye utata, ambayo Kambi ya Upinzani inahitaji kupatiwa ufumbuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya masuala muhimu kabisa yaliyoibuka katika Muswada huu ni dhana nzima ya uwezekano wa kuungana kwa Vyama vya Siasa vyenye usajili. Hii ni kufuatia kuongezwa kwa kifungu cha 11A(2). Suala hili lina uzito sana, hasa ukizingatia hata Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, iliyokaa jana tarehe 5 Februari, 2009 ilishindwa kukubaliana, kulikopelekea Muswada kuletwa mbele ya Bunge lako Tukufu na kipengele husika kukosa muafaka. Kipengele husika kinasema hivi, naomba kunukuu: “Subject to the Provisions of section 11A, President, Members of Parliament, Councilors or such other leaders, elected or appointed through either of the merged parties shall cease to hold office.”

39 Mheshimiwa Naibu Spika, kwa tafsiri ya kawaida, literal interpretation ya kipengele hiki, mabadiliko haya yanatamka bayana kwamba, pale Vyama vya Siasa vinapoamua kuungana, iwapo vyama husika vina Rais, Wabunge, Madiwani au Viongozi wengine wa kuchaguliwa ama kuteuliwa, basi Urais, Ubunge, Udiwani ama Uongozi mwingine wowote wa kuchaguliwa ama kuteuliwa unakoma papo hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele hiki kinaonyesha jinsi ambavyo hakuna dhamira ya dhati ya kupanua demokrasia ya vyama vingi, itakuwa ni ndoto kwa Vyama vya Siasa kuungana na hata vikiungana, kuungana huko kutavigharimu sana vyama husika, hali kadhalika Serikali. Ni muhimu tukajiuliza, hivi kweli Serikali itakuwa tayari kuachia uwazi utakaoweza kusababisha chaguzi ndogo ndogo za kila mara vyama vinapoamua kuungana? Hii inatokana na ukweli kwamba, vyama vikiamua kuungana wakati wowote, hata mwaka mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu, Serikali italazimika kufanya uchaguzi upya ili kuweza kujaza nafasi za Urais, Wabunge, Madiwani, Wajumbe wa Serikali za Mitaa/Vijiji na Vitongoji!

Mheshimiwa Naibu Spika, matatizo yote haya, yanatokana na uwoga usiokuwa na mantiki wa kubadilisha Katiba yetu, ambayo kimsingi vipengele vyake vingi vimepitwa na wakati na haiendani na changamoto za siasa za kizazi hiki. Ikumbukwe kwamba, kipengele cha awali, 11B(2), ambacho kimsingi ndicho kilichopelekea Muswada huu kutokuletwa katika Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge, kilikuwa kinatoa muda wa mpito (transition period), kwa viongozi ambao vyama vyao vimeungana, kuendelea na nafasi zao mpaka uchaguzi mpya utakapoitishwa ndipo watagombea kupitia Chama kipya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika kwamba, kipengele namba 11B(2), kingebaki kama kilivyo kingekuwa kinakiuka Ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambayo inatamka bayana kwamba, Ubunge utakoma iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama wa Chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge. Katiba hii hii ambayo ipo kimya kabisa kuhusiana na nafasi ya Rais, Madiwani ama Viongozi wengine wowote wa kisiasa wa kuchaguliwa ama kuteuliwa, kupoteza nafasi zao pale wanapohama vyama. Kwa Mfano, matakwa ya Kikatiba, ibara ya 39(2), kwa mgombea Urais ni kuwa mwanachama wa Chama cha Siasa. Hata hivyo, kuhama chama cha siasa/kuacha kuwa mwanachama wa chama cha siasa sio moja ya sifa za kukoma kuwa Rais, kama ilivyoainishwa na ibara ya 42(3) ya Katiba hiyo hiyo.

Kwa mantiki hiyo, kumbe basi kikwazo cha kikatiba kipo kwenye nafasi ya Ubunge tu na sio nafasi nyingine za kisiasa. Hivyo, ingewezekana kabisa kipengele tajwa cha Katiba, kufanyiwa mabadiliko, pamoja na vipengele vingine vinavyopigiwa kelele kila siku, ili kuwezesha kuwepo na sheria imara na zenye kukidhi matakwa ya kidemokrasia ya wakati huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ingewezekana kabisa, sheria kutambua mahusiano mengine ya kivyama badala ya kulazimisha vyama kuungana. Ingewezekana kabisa sheria kutambua ushirikiano wa vyama rasmi (alliance au coalition), pasipo vyama hivyo

40 kupoteza uhalali wao wa kuwepo. Hii ingeviwezesha vyama kuwa na ushirikiano katika misingi ambayo vinakubaliana na vyenyewe kuendelea kuwepo. Ni muhimu ikaeleweka, kila chama kina sera na itikadi zake, hivyo basi, sio sahihi kwa sheria kulazimisha ushirikiano wa aina moja, yaani kuungana.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko haya pia yameongeza kifungu kipya cha 18(A), kinachoviagiza Vyama vya Siasa kuwasilisha taarifa ya fedha kwenye Ofisi ya Msajili. Kifungu hiki kinaboresha kifungu cha 18, ambacho kinazungumzia zaidi ya matumizi ya fedha za ruzuku, kwa kuvitaka Vyama vya Siasa kupeleka taarifa ya fedha iliyofanyiwa ukaguzi, ikionyesha vyanzo vingine vya fedha na mchanganuo wa namna fedha husika zilivyotumika. Kifungu hiki ni muhimu sana.

Kambi ya Upinzani inapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa, awe anatangaza mapato na matumizi kila baada ya miezi minne na taarifa hizi zitangazwe kwenye vyombo vya habari vya ndani na sio kwenye Gazeti la Serikali, kama ilivyo hivi sasa ili kuweza kuhakikisha kuwa vyama vinaweka wazi jinsi vinavyotumia fedha za walipa kodi na hasa ambazo zinatokana na ruzuku za vyama ambazo ni fedha za walipa kodi, hali kadhalika matumizi ya vyanzo vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo mengine yanayotakiwa kuangaliwa kwa umakini ni kifungu cha 8(A)(3); kinachomzungumzia mtu ambaye sio Kiongozi wa Kitaifa wa Chama hicho, lakini anajitambulisha kama kiongozi na kufanya shughuli za siasa kupitia chama ambacho yeye sio kiongozi.

Adhabu iliyotolewa chini ya kifungu 8(A)(3) ni ndogo, kutokana na ukweli kuwa, mtu anaweza kujipachika uongozi wa chama na akatumia nafasi hiyo kujinufaisha na hata kama atapatikana na hatia, anaweza kulipa faini hiyo kirahisi. Mapendekezo yetu ni kuwa, kifungu hiki kieleze kuwa kifungo kisichopungua miezi sita au faini isiyopungua shilingi milioni moja ili kumpa wigo mpana wa kuamua kutokana na uzito wa shauri lenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi ya Upinzani, inaunga mkono nyongeza ya Kifungu 12(A)(1), kinachokataza chama kufanya shughuli zake kwenye nyumba za ibada, kwenye taasisi za umma ama majengo ya Serikali. Ni muhimu sana kifungu hiki kikatiliwa mkazo na Ofisi ya Msajili ili kutenganisha shughuli za chama na zile za kidini, hasa ukizingatia kwamba, huko vijijini tumekuwa tukishuhudia ofisi za baadhi ya vyama, zikiwa kwenye majengo ya Serikali, hasa Ofisi za Serikali za Mitaa. Hali kadhalika, imekuwa ni jambo la kawaida, magari ya Serikali kutumika katika shughuli za siasa; jambo ambalo linatakiwa kusitishwa mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi ya Upinzani, inatofautiana na kifungu cha 10(A)(a) kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992, ambayo inatamka kuwa ili Kiongozi wa Chama cha Siasa aweze kuchaguliwa, kitakachozingatiwa ni uwezo wake wa kusoma na kuandika. Ni muhimu ikaeleweka kwamba, Tanzania ya leo ambayo ipo kwenye ulimwengu wa utandawazi, sifa ya Kiongozi wa Kisiasa mwenye kujua kuandika na kusoma pekee, haitoshi kukabiliana na mabadiliko ya ulimwengu wa sasa.

41 Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na viwango tofauti vya elimu, kutegemeana na ngazi ya uongozi. Ni muhimu sana hili likazingatiwa kwenye kanuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, schedule of amendments zimegawiwa; ipo hii ya Serikali na ipo nyingine ya Mheshimiwa Shellukindo. Kwa hiyo, mnapojadili mzingatie hizo schedule of amendments.

Sasa nina wachangiaji kadhaa, nitakaoanza nao ni Mheshimiwa Kabwe Zitto, atafuatiwa na Mheshimiwa Juma Killimbah, Mheshimiwa Shellukindo na wengine nitaendelea kuwataja baadae.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Muswada huu wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, pamoja na mapendekezo ya mabadiliko mbalimbali, ambayo yameletwa. Napenda nimfahamishe Mheshimiwa Naibu Spika kwamba, pamoja na schedule of amendments za Mheshimiwa Shellukindo na Mheshimiwa Waziri Marmo na mimi pia nimeleta schedule of amendments nadhani itakuwa inagawiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina maeneo matatu ambayo nataka kuyazungumzia. Eneo la kwanza ni la National Consensus (Muafaka wa Kitaifa). Licha ya kwamba, tuko watu wa vyama tofauti, lakini bado tunaunganishwa na Tanzania. Kuna masuala ambayo yanapaswa kuwa ni ya Kitaifa, lakini toka Mfumo wa Vyama Vingi umeanza, hatujawahi kukaa kama Taifa na kusema mambo haya ni tunu za Taifa. Vyama vyote vya siasa, vitafanya yote vinavyoyafanya lakini haya ni mambo ya Kitaifa. Suala kama hili halipo na Muswada huu haujajaribu kufikia mahali hapo.

Leo asubuhi nimefurahishwa na schedule of amendments, ambayo Mheshimiwa Shellukindo ameileta katika lile eneo la Halmashauri (Member of a Council) ya Vyama vya Siasa, ambapo pamoja na Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Vyama, ameweka pia watu wengine kama Marais Wastaafu kama watu muhimu katika Taifa, Wawakilishi wa Asasi zile za Kiserikali na watu wa kutoka yeye amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini na Vyuo Vikuu vingine. Hii inaweza ikasaidia, kwa kutumia Halmashauri hii kuweza angalau kwa mwaka au miaka miwili kama Taifa kuli-retreat na kukaa na kuangalia as a Nation ni wapi ambapo tunakwenda; ni masuala yepi ambayo yanatuunganisha kama nchi na masuala yepi ambayo yanatugawa kama nchi ili kuweza kuhakikisha kwamba, tunakuwa na Muafaka wa Kitaifa.

Kwa hiyo, nilikuwa napendekeza, mara baada ya shughuli hii ya Muswada na mapendekezo ambayo tumeyaleta yatakapokuwa yamekubalika, tuanze hatua hii ya kukaa kama Taifa na kujadiliana na kuweza kuona jamani mambo yepi ni ya Tanzania, mambo yepi ni ya vyama na hiyo itatusaidia sana kutuunganisha zaidi. Hilo ni suala la kwanza.

42 Kwa maana hiyo ni kwamba, naunga mkono mapendekezo ambayo Mzee Shellukindo ameyaleta, kwa sababu yanatupeleka hatua moja mbele katika kuhakikisha kwamba, tunakuwa na National Consensus ambayo hatuna, Mataifa mengine yana National Consensus. Ukienda Marekani, sera ya mambo ya nje ni ile ile aidha ni democracy au republican. Ukienda Ujerumani, kuhusiana na Hitler, aidha ni CDU, SPD au FDP, wote msimamo wao ni mmoja kwa sababu ni mambo ambayo wamekubaliana kama tunu za Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni hili suala ambalo lina sehemu kubwa ya huu Muswada, kipengele cha 11(A) kuhusiana na Muungano wa Vyama. Ninakubaliana kabisa na maoni ambayo Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani ameyatoa, kuhusiana na suala hili la Muungano wa Vyama.

Jana nilipata bahati ya kuhudhuria Kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, kulikuwa na mjadala mkali sana kuhusu suala zima la iwapo vyama vikiungana watu ambao wamechaguliwa nafasi za Kiserikali kama Wenyeviti wa Vitongoji, Wajumbe wa Serikali za Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji na Madiwani, Wabunge na Rais na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, kama nao pia watakuwa wanapoteza nafasi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa pia Mheshimiwa Marmo ameleta schedule of amendments kuhusiana na suala hilo leo asubuhi ambayo …

NAIBU SPIKA: Waziri wa Nchi.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Waziri wa Nchi, ameleta schedule of amendments leo asubuhi ambayo inarekebisha kile kipengele. Nilikuwa napenda nipate ufafanuzi, maana yake Waziri sasa ameondoa ile Wabunge, Madiwani, Rais kupoteza nafasi zao, lakini amesema all Political Leaders elected, appointed or nominated before the merger shall vacate their positions; nini definition ya Political Leaders; ni pamoja na Wabunge, Madiwani, Rais, Wawakilishi na Wenyeviti au ni ambao ni appointed na elected ndani ya Vyama?

Kwa hiyo, tulikuwa tunapata kwa sababu ile schedule aliyoileta jana na ambayo tuliijadili katika Kamati, ilikuwa wazi kabisa ametaja Rais, Wabunge na Madiwani, watapoteza nafasi zao. Hii ya sasa wamebumba ndani Political Leaders. Kwa hiyo, tulikwa tunahitaji tupate definition ya Political Leaders katika eneo la interpretation kwamba, hapa tuna maana all Political Leaders Elected, Appointed or Nominated within the Party na sio wale ambao wanashika nafasi za Kidola kama Wabunge, Madiwani na hawa ambao nimewataja. Vinginevyo, huu Muswada hautakuwa na maana yoyote, kwa sababu itakuwa ni sawasawa na kusema msiungane.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa napenda niseme kitu kimoja kwamba, suala hili halihusu Vyama vya Upinzani. Muswada huu hatuutungi kwa ajili ya Vyama vya Upinzani. Muswada huu unaweza ukakihusu hata Chama kinachoongoza hivi sasa, kwa sababu siasa inabadilika sana. Kesho na keshokutwa mmeparaganyika, watu wa Chama Tawala, watu watahitaji kupata new political alliances; kwa nini itumie demokrasia ya

43 nchi hii, kwa nini tuue legacy ya Head of State wa sasa kuhusiana na kupanua demokrasia?

Mimi nilikuwa nadhani Mheshimiwa Waziri, pamoja na maelezo mazuri sana ambayo Msemaji wa Upinzani Bungeni ameyaeleza, kuhusiana na eneo hilo na constitutional implications za eneo hilo, akubaliane nasi kwamba, eneo hili iwapo vyama vitakuwa vimeungana wakati wowote, kwa mujibu wa makubaliano wa vile vyama kuungana, watu ambao wamechaguliwa kwenye nafasi za kidola, wasipoteze nafasi zao. Hii ni kwa sababu hawa wamechaguliwa na wananchi ambao wengine hawana vyama, wengine ni wa chama hiki wamemchagua Mbunge wa chama kingine, kama ilivyotokea kwa watu mbalimbali ambao wamechaguliwa.

Kwa hiyo, tusipoteze na wala nchi haitaweza kubeba gharama. Kwa mfano, leo tuamue CHADEMA, UDP na CUF vinakuwa chama kimoja; by-elections ngapi nchi itakwenda kuzifanya? Hili ni suala tu la kukaa na kufikiria na kuweza kuona ni hatua gani ambayo tunakwenda nayo. Sisi tungependekeza na tungemwomba sana Waziri wa Nchi na Serikali wakubaliane na hili kwamba, hakuna sababu ya kuweka limitations. Kwa hiyo, tupate definition ya Political Leaders elected, appointed na nominated kwenye interpretation ili kuondoa matatizo yoyote ambayo yanaweza yakatokea na options mbalimbali. Jana kwenye Kamati ya Katiba na Sheria, tulimpatia Waziri wa Nchi ili aweze kufanyia marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu na la mwisho, naipongeza hatua sasa ambayo tumeifikia ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kukagua hesabu za vyama. Toka Mfumo wa Vyama Vingi umeanza, Wakaguzi wakishazikagua hesabu za Vyama vya Siasa, zinapelekwa kwa Msajili, Msajili anazihifadhi. Hakuna ukaguzi unaofanywa wa fedha za walipa kodi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kitu ambacho ni kinyume na Katiba, vilevile ni kinyume na Public Finance, lakini ndio kitu ambacho kinasababisha vyama vinapata fedha maeneo ambayo hayajulikani kwa ajili ya uchaguzi. Wakipata dola, wanatumia nafasi hizo kuweza kuwaridhisha wale ambao wamewachangia fedha. Kwa hiyo, hatua hii ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, itatusaidia sana kuweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Vyama vya Siasa.

Mdhibiti pia atajua vyanzo wa hizi fedha ni wapi na kwa nini watu wanatumia fedha nyingi sana kwenye uchaguzi. Chama ambacho kinajulikana kinatumia fedha nyingi sana katika uchaguzi kinajulikana ni chama gani na watu hawaelezi hizo fedha wamezitoa wapi. Ipo siku tutakuja kuwekewa Serikali hapa na mamluki ambao wana interest tofauti na Taifa letu. Hatua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu, kukagua hesabu za vyama vyote na kutoa taarifa ni ya kupongeza sana. Sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuum inamtaka taarifa yake iwe submitted Bungeni. Taarifa hiyo itakuwa submitted Bungeni, Watanzania watajua kodi zao zinatumika namna gani na Vyama vya Siasa. (Makofi)

La pili, kanuni ya ugawaji ruzuku. Sheria mama, section 17, ibara ya 17(1) na (2) zinaelezea kanuni. Kanuni hii nilikuwa naomba na Mheshimiwa Waziri wa Nchi, aweze

44 kukubaliana nami, turejeshe umuhimu wa kura ambazo vyama vinapata katika ugawaji wa ruzuku. Sasa hivi tumeweka uwiano sawa sawa, ruzuku inagawiwa kwa mujibu wa idadi ya Wabunge na kwa mujibu wa idadi ya kura za Wabunge. Nchi ambayo kila chama kimepata na sio kura za Rais ni kura za Wabunge nchi nzima. Nilikuwa napendekeza kwamba, tutoe weight kubwa zaidi kwenye idadi ya kura ambazo kila chama kimepata ili kuhakikisha ya kwamba, kura zinakuwa na thamani. Kwa sababu kuna watu ambao wanapiga kura zinapotea kwa sababu hazihesabiwi. Chama kile kinaendeshwa namna gani na ruzuku inayoendesha vyama hivi leo Serikali ikiiondoa kuna vyama vingine kama chama kinachotawala, sijui kitaendesha namna gani maana wana mlolongo mkubwa wa bureaucracy?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba Waziri wa Nchi, akubaliane nami kwamba, tufanye mabadiliko haya ya kukokotoa ruzuku ili kuhakikisha ruzuku hii inakokotolewa kwa mujibu wa kura ambazo vyama vimepata. La pili, sheria inatamka wazi kwamba, sehemu ya ruzuku ile pia itumike for Parliamentary activities of the Party. Sasa hili nadhani inabidi Msajili aangalie jinsi ya kuweka regulations, maana Bunge la Tanzania sasa lina Kambi mbili; Kambi ya Upinzani na Kambi ya Chama kinachotawala. Lakini ile Parliamentary activities kwa fedha za ruzuku, kwa kweli sijaona jinsi gani ambavyo zinaweza kutumika na kusaidia Wabunge katika shughuli zao mbalimbali za Miswada na kadhalika. Nilikuwa naomba labda hili Msajili anaweza akaliangalia na Waziri katika eneo la regulations.

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya hapo, nilikuwa napenda tupate mabadiliko hayo ya eneo la Wabunge na Madiwani kupoteza nafasi zao, lakini pia eneo la ruzuku. Nikubaliane kabisa na schedule of amendments, ambayo Mheshimiwa Shellukindo ameileta hapa kwa ajili ya kui-widen ile Council ya Vyama vya Siasa, ili itusaidie kuweza kuwa na National Consensus na kukubaliana mambo gani ambayo tunakubaliana kama Taifa. Zaidi ya hapo, nakushukuru sana ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante, nimepokea schedule of amendment iliyoletwa na Mheshimiwa Zitto. Nawatangazieni hivyo, kwa sababu kutakuwepo na kazi juu ya hizi; msifike watu mkasema ndio ndio kumbe hamjaziona. Kwa hiyo, tunaendelea na Mheshimiwa Juma Killimbah, Mheshimiwa Shellukindo na Mheshimiwa John Cheyo wajiandae.

MHE. JUMA H. KILLIMBAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nami nipate fursa ya kuchangia Muswada huu ulioletwa mbele yetu, unaohusiana na Marekebisho ya Vyama vya Siasa wa 2008.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, namshukuru sana Waziri Marmo, kwa kuleta Muswada huu. Pia nachukua fursa hii, kumpongeza Msajili John Tendwa, kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya hasa kwa usimamizi na uwezo wa kuweza kuvisimamia Vyama vya Siasa, kwa kipindi hiki mpaka tunafikia hatua hii na hatua zote alizoshiriki za kuandaa marekebisho ya sheria hii.

45 Mheshimiwa Naibu Spika, Vyama vya Siasa, ndivyo tunavyovitegemea kuunda Serikali. Vyama vya Siasa ni muhimu sana, kwa sura ya kimaadili ya nchi yetu. Tunategemea kuwa, Vyama vya Siasa ndivyo vinavyoweza vikatoa picha kuonyesha kwamba, Serikali inaweza ikawa iko vipi. Kwa hiyo, sheria hii iliyoletwa ni muhimu sana kuweza kuweka udhibiti ili tuwe na viongozi ambao pengine watakuwa wanaozingatia maadili yanayoendana na utaifa wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatutegemei kwamba, katika jamii ambayo ni jamii ya Kitanzania, iliyojengeka katika maadili mema, sasa tufikie mahali Vyama vya Kisiasa kutokana na tofauti ya kiitikadi, viwe ni vyama vya kufarakanisha jamii na kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi, jambo ambalo sisi Watanzania hatupo tayari kabisa. Nchi yetu ni ya kiungwana na napenda kusema kwamba, suala la utaifa linatokana na Vyama vya Siasa jinsi vinavyofanya kazi zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba, nimefurahi sana baada ya Sheria hii kuja, kwa sababu sasa itampa meno Msajili wa Vyama. Atakuwa na uwezo wa kuvidhibiti hivi vyama, ambavyo vimekuwa na tabia ya kuvunja maadili na kuweza kuharibu hali ya amani na utulivu wa nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatutegemei kuwa na vyama ambavyo vinazungumza uongo, vinachafua watu au vyama ambavyo vinaleta chuki miongoni mwa watu. Tunategemea tuwe na vyama ambavyo vitazungumzia Watanzania wanahitaji maendeleo kwa ajili ya taifa lao na si vyama ambavyo vinazungumzia kuwagawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwenye hili suala la kimaadili ni kwamba, lazima sasa Sheria hii na hasa tunapozungumzia suala la kimaadili, Msajili apewe uwezo na nguvu za kisheria. Pale anapoweza kugundua kwamba, kipo chama cha siasa kinatoka katika misingi ya kimaadili na hasa cha kuweza kuzungumza uongo, kuweza kuzua mambo ambayo hayana uhakika, Sheria itumike na kichukuliwe hatua na ikiwezekana kipelekwe Mahakamani kama ilivyo kwa Sheria nyingine zinazofanya kazi .

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye kipengele cha 18(a), ambacho kinazungumzia suala la fedha za shughuli za uendeshaji wa vyama. Ni dhahiri kwamba, tunahitaji fedha zote zinazotaka kuendesha hivi vyama zijulikane na zisipojulikana tunaweza tukapata mgogoro ambao kila mmoja atahitaji kusema, kile ambacho yule aliyempa fedha akafanyia kazi ile anayoitaka. Nafurahi sana hizi fedha lazima Mkaguzi Mkuu wa Serikali awe anazikagua na ijulikane zimetumika kwa kiwango gani. Lazima ijulikane pesa hizi za nje ambazo zinaingia kuja kusaidia vyama, zina malengo gani na ziwekwe wazi, wala hakuna haja ya kuficha. Kama zina nia njema zijulikane.

Bahati nzuri tunasema Marekani wana utaratibu, fedha zote za uchaguzi zinajulikana na zinaelezwa. Hata kama mtu anataka kuchangia kuhusiana na shughuli za uchaguzi, lazima aeleze na ajulikane, vyanzo vya kuchangia hizi fedha vitatoka wapi. Kwa hiyo, hapa utaratibu lazima fedha zote za uchaguzi au fedha zinazohusiana na uendeshaji wa vyama zijulikane ili tuweze kuwa na vyama vyenye maadili na

46 vinavyoweza vikawa na vyama vya utaifa na sio vyama ambavyo vinaweza vikawagawa Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria hii ni sawa na kama tunavyosema kwamba, mapato ya kujua chama kinapataje pesa si kosa. Sawa na mfanyabiashara anapokwenda kukadiriwa mapato na TRA kwamba, wewe biashara yako ya mwaka ina kiasi gani na utapata kiwango gani kutokana na biashara hii ambayo tumekupa leseni. Kwa hiyo, nayo kuweza kutangaza au kujua wafadhili wanaokifadhili hiki chama si vibaya kwa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye upande wa hili Baraza ambalo litaundwa na Msajili wa Baraza, kupitia section 21(b) ambalo litakuwa chini ya Msajili. Nakubaliana kabisa kwamba, pamoja schedule of amendments iliyoletwa na Mheshimiwa Shellukindo, ambayo naikubali, lakini lazima tuwe na limit. Tujue idadi ya Wajumbe, watakaongia katika hilo Baraza, lakini pia idadi hii iendane na uwakilishi; ni chama gani ambacho kina-dominate kwenye uwakilishi wa vyombo vya dola. Chama kinachokuwa na Wabunge wengi, basi lazima kiwe na nafasi kubwa katika lile Baraza. Chama ambacho kina idadi kubwa ya uwakilishi wa Madiwani wengi, lazima pia kiwe na nafasi kubwa. Haiwezekani ukawa na chama chenye Wabunge 250, lakini ukaja ukakilinganisha na chama ambacho kina Mbunge mmoja au kina Wabunge watano au wanne. Lazima Sheria igawanye ili chama ambacho kina uwakilishi mkubwa, kiwe kina Wajumbe wengi katika hiyo Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ile ile section inayozungumzia kuhusu Msajili kwamba, ndiyo atakaye-establish ile Sekretarieti, sio vibaya ila mimi nasema kwa chama ambacho kina eneo kubwa la utawala, nacho kikashirikishwa kwa kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama kikapewa nafasi ili kiweze kuingia kwenye Sekretarieti ili yale mawazo si vibaya, kwa sababu ndiyo kinachoongoza Serikali kwa wakati huo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba, nimezungumzia suala la fedha zinazopatikana kuendesha vyama, lakini pia nimezungumzia suala la Baraza. Napenda nisisitize kwamba, suala la Sheria hii ni muhimu sana kwa hali tuliyonayo hivi sasa. Ni muhimu sana na lazima Sheria hii ikipita, ifanye kazi. Ninaamini maadili ya nchi yetu, yanaweza yakarekebishika, kwa kupitia hivi vyama kwa sababu vyama vyenyewe vina nafasi kubwa ya kuweza kuwafikia wananchi na vinaaminika kwa wananchi, kwa sababu vimekuwa vikizungumza nao muda wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nashukuru sana. Naunga mkono marekebisho. (Makofi)

MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi nitoe mchango wangu kidogo. Awali ya yote, napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu na Msaidizi wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kuleta marekebisho haya. Labda si vibaya tukaweka historia kidogo, bahati nzuri wakati tunaanza Mfumo wa Vyama Vingi, nilikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, mwaka 1991 - 1995. Kwa hiyo, mimi ni mmojawapo wa watu

47 ambao tulianza kuitekeleza Sheria hii na mimi ndiyo nilikuwa nalipa vyama vya siasa, pamoja na Chama changu cha CCM.

Kwa hiyo, kuna baadhi ya mambo ambayo nimeyaona, pengine mtanisamehe, sina budi nitumie uzoefu huo ili kujenga taasisi yetu hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa, iweze kufanya kazi yake vizuri zaidi. Maana unaweza ukatunga Sheria ya kuongoza, lakini kuna vitu vingine ambavyo kama hukuviweka wazi, vinaweza kuleta mkanganyiko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, napenda kuunga mkono marekebisho haya yaliyoletwa na Serikali. Nilichofanya hapa ni kuyaboresha na pengine kuwa na uwazi zaidi, ili kazi ziweze kufanyika vizuri sana. Nina maeneo mawili ya kuchangia kuongeza msisitizo tu:-

Kifungu cha tatu kinazungumzia uhuru wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (Autonomy). Mimi nadhani autonomy lazima iongozwe, vinginevyo unaweza kumkwaza yule mtekelezaji na wale wengine ambao wanadhani mambo yanakiukwa, kumbe ni kwa kutoweka mipaka. Ofisi ya Usajili wa Vyama vya Siasa ni ya Kitaifa, kwa hiyo, ifanye kazi zake vizuri zaidi, iwekewe taratibu ambazo haziikwazi ofisi hiyo.

Kwa hiyo, nilichofanya hapa nikasema yale maeneo ambayo ni muhimu, yafanyiwe mashauriano. Nimeyaorodhesha ili kusiwe na wasiwasi wa mtu kusema mbona hiki hukuni-consult, lakini haina maana kwamba ni haya tu, kuna matukio mengine yanaweza kujitokeza, lakini siyo ya kudumu. Kwa hiyo, hapa nilitaka tu kuweka msisitizo kwamba ni vizuri tukaweka wazi zaidi, watu wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na uwajibikaji kwa yule mwenyewe mwenye ofisi na kwenye taasisi nyingine ambazo zina madaraka hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingine ambayo nimeitazama kwa undani zaidi ni Baraza; kwanza, napenda kuishukuru sana Serikali kwa kuja na wazo hili la kuwa na Baraza la Vyama vya Siasa. Hakuna kitu ambacho baadhi yetu kinatuumiza, nchi yetu tumepata uhuru kwa kuzungumza, kwa muafaka mzuri tu, halafu tunapata matatizo. Matatizo mengine madogo madogo haya, taasisi kutoka nje zinakuja kutushughulisha; inaumiza kweli. Mimi nadhani hapa ndio mahali ambapo tungejenga, hili Baraza liwe ndio mahali pa kuweka mshikamano hapo wa Taifa na kusaidia nchi yetu kuweza kuona ni wapi tunaenda kisiasa. Hili kwa kweli ni la kupongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyoona mimi, hata wenzetu wengine wanangojea mpaka Tanzania tufanye vitu, ndio wao waseme na sisi tunafuata hivyo hivyo. Ninakumbuka jambo moja tu ambalo lilitushangaza; wakati mwalimu anastaafu bahati nzuri mimi nilikuwa Ikulu pale na nilihusika katika kusimamia shughuli za kustaafu kwake, hatukujua astaafu vipi na tumpe stahili gani. Kwa hiyo, tulikaa tukabuni, tuliangalia Afrika ni wapi ambapo Rais ameondoka kwa ustaarabu na amefanyiwa nini hakuna. Kwa hiyo, ikabidi tubuni. Sasa vitu hivyo vinatakiwa viboreshwe kama sheria hii ilikuwa haipo, kwa hiyo, imebuniwa pale. Kwa hiyo, hapana budi sisi wenyewe

48 tuitazame ili tuiweke vizuri. Hili la Baraza nakiri litafurahisha watu wengi, hata nchi nyingine ambazo zinapata matatizo zitaiga mfano huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa upande wangu, niliangalia nini kazi za Baraza, hapa tupo kwenye vyama lakini mwananchi tunayemwongoza ni yule mmoja; sasa kunapotokea migogoro basi tukae na Baraza hili ndio mahali pa kutazama reference point. Hapa kuna wazee, nimeona nilipanue tusiliache tu likawa wazi. Ule wasiwasi kwamba, uwakilishi uwe na wingi wa wanachama au Wabunge; mimi nadhani hebu tulijenge hili kwa sababu tunaenda kuzungumza pale, wakati mwingine chama na chama kina mgogoro, lakini kwa chama chochote tawala kina nafasi kubwa zaidi. Kwa sababu kuna Marais hawa Wastaafu, kama wakiingia mle ndani, kwa kweli busara kubwa sana itaingia kule. Kuna watu wengine wanatoka nje kuja kutazama haya marumbano yanatokana na nini, chanzo chake ni nini watusaidie. Yupo mwenzangu aliuliza kwa nini iwe Dar es Salaam hiyo faculty ya political science; nataka tu kumsaidia kwamba, mimi nina uhakika ndio ina political science, hizo nyingine sijajua. Kwa hiyo, sikuweza kuziacha wazi. Kwa kuwa mimi nimeleta wazo hili, linaweza kuboreshwa na nitakubali kuboresha.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ya kwangu machache ni hayo tu, isipokuwa kwenye jedwali la marekebisho kuna masahihisho ya uchapaji, kama mtakubaliana nami nitumie muda wangu huu ili wakati wa kupitisha kwenye Kamati ya Bunge Zima, tusiwe na muda wa kusahihisha hayo. Nendeni ukurasa wa pili kwenye Kifungu (d), kuna mahali ambapo pameandikwa one eminent person; how had a distinguish service in any multi-national organisation. Halafu kile kifungu cha tatu, kuna mchanganyiko pale kwamba, the council shall elect Chairperson and Vice Chairperson badala ya Chairman.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niishie hapo. Naomba mchango wa wenzangu katika marekebisho hayo ambayo niliona tumsaidie kuboresha Muswada huu. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza kabisa na mimi nataka kujiunga na wasemaji wa mwanzo, kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri, kwa kufanya kazi nzuri na kuleta Muswada huu mbele yetu. Pia namshukuru Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kujitahidi kutufikisha ambapo tumefuka hivi sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni mmojawapo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa na Chama changu ni United Democratic Party (UDP), ambapo mimi ni Mwenyekiti. Kwa hiyo, nitakayoyazungumza labda mengi yatakuwa na uhusiano kwamba, nimekuwa mmojawapo wa Viongozi kwa muda mrefu sasa. Nataka kutumia nafasi hii, kuwashukuru wanachama wote wa UDP, kwa kuendelea kuniamini katika kuendesha chama chetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tangu tumegeuza mfumo kutoka chama kimoja kwenda kwa mfumo wa vyama vingi, kuna kitu kimoja ambacho Watanzania tupende tusipende, lazima tukubali kwamba nchi yetu sasa hivi inaendelea vizuri zaidi kuliko pale ilipokuwa na chama kimoja. Tutumie nafasi hii pia, kuwapongeza Watanzania kwa

49 kuupokea huu mfumo wa Vyama Vingi. Mfumo huu umeleta vifo vingi sana Afrika. Watanzania pamoja na matatizo ndani ya Katiba, upungufu wa Sheria mbalimbali, pamoja na Sheria za uchaguzi, lakini bado tumeuendesha mfumo huu na tukaweza kuwa nchi ambayo ina amani. Hili ni jambo ambalo Watanzania tunapaswa kujivunia sana.

Ninapenda kutumia nafasi hii, kusisitiza kwamba, Demokrasia ndiyo kitu ambacho tunaweza tukakitumia katika kuhakikisha kwamba, tunakuwa na maendeleo. Demokrasia ya Vyama Vingi ndiyo imetuwezesha kufanya maamuzi makubwa sana katika Bunge hili na zaidi katika Bunge hili la Awamu ya Nne. Mambo ambayo yametokea katika Bunge hili, hayajawahi kutokea tangu nchi hii iundwe. Hii imetokana na kuwepo vyama mbalimbali ndani ya Bunge hili. Mambo ya kujificha kwenye kichaka cha chama sasa yamekwisha. Ukifanya madudu huko kwenye chama chako au kwenye Serikali, unajua yatafumuliwa tu kwa upande mwingine. Kwa hiyo, hii kwa kweli imeleta afya njema katika maamuzi yetu ya kisiasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini bado tuna matatizo na tatizo la kwanza ambalo nataka kutumia nafasi hii kuomba Wazungu wanasema change of attitude, change of mindset; hebu tugeuze mtazamo wetu juu ya mambo haya ya siasa. Kwanza, tukubali kabisa mfumo huu wa Vyama Vingi unatufaa Tanzania; uwe chama tawala au chama cha upinzani. Tukubali hilo kwa dhati kabisa kwamba, mfumo huu ndiyo unaotufaa Watanzania and never again tutarudi kwenye chama kimoja. Tukikubali hilo, mazingira ambayo tunaweza kuweka zaidi kwa vyama ambavyo ni vya Upinzani, yatakuwa ni mazuri zaidi. Bado sasa vyama vya Upinzani vinashindwa kuendelea, kwa sababu ya vikwazo vingi mno katika Taifa hili na zaidi ambavyo vinaletwa na Watendaji wa Serikali.

Mimi ninafikiri kuunganisha mtu ambaye ni District Commissioner, Regional Commissioner, kuwa mwanasiasa na upande huo huo yeye ndiyo Mtendaji na leo hii tumeambiwa anaweza akaamua kumuweka mtu ndani kwa saa 48; mimi naona hili ni kosa. DCs wanatumia uwezo wao waliopewa, kugandamiza vyama vya siasa na zaidi kule chini. Hapa juu naona tumeanza kuelewana na zaidi kwa sababu wengi ndiyo tunakaa katika Vikao vya Tanzania Centre for Democracy, ambako mimi ni Mwenyekiti, tunaelewana; lakini kule chini DC anajiona kwamba, akipoteza vijiji vyote kwa Vyama vya Upinzani, ana hakika kwamba cheo chake hataendelea kuwa nacho. Kwa hiyo, anatumia kila njia, hata Sheria za Uchaguzi hazifuatwi.

Tumeona katika sehemu mbalimbali na mimi ni shahidi, kule Bariadi na sehemu nyingine. Kila wakati DCs wanajaribu kutafuta njia ya kutumia, muda mwingine hata vyombo vya Dola kama Polisi vinatumika. Wengine wanathubutu hata kuvunja Sheria, kwa kuwaita Mahakimu na kuwaambia yule anayeja mbele yako ni UDP, hakikisha kwamba, harudi anaenda kulala mahabusu. Huku ni kuvunja Sheria, nazungumza hivi kwa sababu mfumo huu ni mzuri kwetu sote. Sasa wewe umepewa nafasi ya kuendesha Wilaya kwa nini uugandamize mfumo huu? Wewe unataka watu hawa waingie ndani, wapoteze mali zao na waogope kujiunga na vyama vya siasa. (Makofi)

50 Mheshimiwa Naibu Spika, natoa wito wa dhati kwamba, Mfumo wa Vyama Vingi ni mzuri sana kwa wote. Ninyi Chama Tawala, mngekuwa mmelelala usingizi kwa miaka mingi, tusingefika hapa kimaendeleo kama tusingekuwa na watu. Ingawa sisi tuko wachache, lakini tunawachokonoa chokonoa kidogo na kuwaamsha, tumeweza kufanya maamuzi ambayo ni mazuri kwa ajili ya taifa hili. Kwa hiyo, nasema tuunge mkono kwa dhati kabisa, Mfumo huu.

Ninaomba tufungue jamani vyama hivi vya siasa, humu ndani ya Bunge utapata wapi watu wa kuja hapa? Kwanza, wengi unashangaa, kuna cheo kimoja ndani ya CCM labda Mbunge mmoja wanakuwa 25,000 watu wa aina mbalimbali, Maprofesa na kadhalika. Muda mwingine Maprofesa wananishangaza, wakikaa wanasema sijui CCM hivi, lakini siku ya uchaguzi unaona na wao wanatufa humo humo mahali ambapo wanasema pabaya, hapafai huku kuna makosa haya na wanarundikana ishirini. Acheni kurundikana kule, njooni kwenye vyama hivi ambavyo havitafuti Uraisi, tunataka Wabunge waliosoma, ambao wana uwezo na watu ambao wanaweza wakasaidia Mfumo huu wa Vyama Vingi.

Mimi siku moja nilisikitika sana, nilikuwa natafuta Mbunge Chuo Kikuu…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cheyo, unajadili hoja hii au unapiga siasa ndani ya Bunge?

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wewe ni Mwanachama wa CCM, hutaelewa ninachotaka kusema. Ninachotaka kusema …

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cheyo, naomba u-withdraw maneno hayo, kwa sababu hayana maana yoyote. Ninachosema, tunapojadili Muswada unajadili yaliyomo kwenye Muswada. Sasa unaweza kupamba, lakini kama unaendelea na hotuba hiyo, hujasaidia ku-amend huu Muswada.

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Naibu Spika, naendelea kwa kusema kwamba, tusaidie huu Muswada kwa kukubali mfumo wa demokrasia na kwa hiyo tukubali watu waende kwenye vyama mbalimbali. La sivyo, tutakuwa na Muswada wa Vyama vya Siasa ambao upande mmoja ndiyo wako wengi na wana uwezo, lakini upande mwingine hawana hata watu ambao wanaweza kuwachagua kama candidates. Kwa hiyo, hilo ni angalizo zuri na ndiyo maana natumia nafasi hii kusisitiza vitu kama hivi.

Jambo la pili, nimeona hapa amendment ya Mheshimiwa Waziri, lakini kitu ambacho kimewapa tabu sana ni wakati gani kutakuwa na ukomo kwa watu ambao wamechaguliwa kama vyama viwili vitaamua kuungana? Tuangalie historia, tulipoanza mfumo wa vyama vingi, kulikuwa na provision ndani ya Sheria kwamba, utakapoanza huu mfumo, kitakuwa assumed au kitakuwa kimejukikana kwamba kilikuwepo pale ambapo mfumo huu unaanza. Hii ilikuwa ni mantiki, kwa sababu wewe kama kwenye Katiba unasema ni lazima uwe mwachama wa chama cha siasa, kwa hiyo, kisipo-exist ndiyo kusema wakati huo hauna Rais, hakuna Bunge na vitu

51 kama hivyo. Tuliweka provision kama hiyo; sioni kwa nini Mheshimiwa Waziri asiongeze hapa provision kwamba, kama vyama viwili vikiamua kuungana, basi wale wote ambao wamo ndani ya vyama hivyo vilivyoungana, wanakuwa assumed immediately kuwa ni wanachama wa chama kipya kilichoundwa.

Kufanya hivyo, kutaondosha huu mpito sijui nini na mtu mwingine anaweza kuondoka na vitu kama hivyo. Najua hili ndugu zangu wa CCM ndiyo maana walikuwa wanaliogopa, maana walifikiri miezi sita hawatakuwa na Wabunge tena, watahamia katika Vyama vya Upinzani. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa kulisisitiza ni la maadili na nafasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Mimi naona Muswada huu, haujampa meno Msajili, japo upande mwingine nisingependa awe na meno makubwa sana, kwa sababu with a pressure ya kwamba, bado wengine wanaweza kutumia nafasi kugandamiza Vyama vya Upinzani. Muswada haujaweka utaratibu; ni vipi mtu ambaye anakosa maadili au anavunja maadili ataweza kushughulikiwa?

Napenda hili liwe wazi zaidi, kwa sababu kama litakuwa wazi zaidi katika taratibu basi labda itaweza kutusaidia. Inanisikitisha sana, tunakaa kwenye Tanzania Centre for Democracy, tumekubaliana maadili sisi sote lakini pakiwa na uchaguzi ni kama vile yale maadili tunayachukua tunayaweka mfukoni tunayakanyaga kabisa, hatuyaoni na tunafanya mambo ya ajabu; matusi, mapanga, kutumia dola, kutumia fedha. Yote hayo tumeyazungumza kwenye maadili, lakini watu hawatufuati na Chama Tawala ndiyo kabisa, wakishafika kule kwenye chaguzi ndogo, ndiyo wanasahau kwamba tulishakubaliana tuhakikishe hatutumii Polisi kupata vyeo. Kwa hiyo, napenda maadili yaangaliwe vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono kuwepo na Baraza la Taifa. Vilevile ilivyopangwa ni vizuri, tutaangalia marekebisho ambayo yamefanywa na Mheshimiwa Shellukindo ili tuweze kulipanua vizuri zaidi.

Mwisho, nasema huu Muswada ungekuwa umekuja karibu zaidi na Miswada mingine miwili; kwanza, kuzungumzia juu ya political funding wakati wa uchaguzi, lakini pia na Sheria ya namna tunavyochaguana. Mimi nafikiri tuna haja ya kuondokana na uchaguzi wa Kiingereza ili twende kwenye propotional representation.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)

MHE. RUTH B. MSAFIRI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi, niweze kuchangia hoja hii iliyo mbele yetu. Kwanza, napenda niipongeze Serikali kwa uamuzi wake wa kuleta Muswada. Muswada huu ni ukombozi kwa uendeshaji wa Siasa za Vyama Vingi nchini na kimsingi huu haulengi chama chochote.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nizungumzie Muswada kuhusu Vyama vya Siasa kuleta mahesabu yao katika ukaguzi wa kiserikali, suala ambalo halikuwepo. Naunga mkono mabadiliko haya, kwa sababu kutakuwa na uwazi katika chama kupata

52 mapato yake na katika kutumia pesa zake. Kwa maana hiyo, hakutakuwa na nafasi ya chama kutumia fedha ambazo hazijulikani mahali zilipotoka na hata mipangilio yake ya kujenga chama chenyewe itakuwa wazi, kwa sababu zile pesa kila mmoja atakuwa anafahamu zimepatikana vipi na wamekusudia kufanya kitu gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napendekeza kwamba, uwepo utaratibu wa kudhibiti fedha zinazotumiwa na wagombea ndani ya vyama. Matumizi ya wagombea katika vyama yanakuwa hayaeleweki na si kipindi cha kugombea tu, iangaliwe hata kipindi cha kujiandaa kutaka kugombea uongozi. Mimi ninayo mifano ya watu ambao wanawania uongozi, lakini kwa kipindi hiki kuna mambo mabaya wanayayafanya. Kwa mfano, watu wanaamua kwenda kuanzisha mashina ama matawi, lakini katika uanzishaji wao huo, wanatoa fedha na kuahidi kufanya vitu vingi ambavyo kimsingi mimi nadhani si sahihi kuvifanya na vinaachiwa kwa sababu hakuna sheria yoyote ambayo inavisimamia.

Watu wanatengeneza kalenda na kuzisambaza kwa maneno pale yanayoonyesha kwamba, wanawania hizi nafasi. Sasa kutengeneza kalenda, kila mmoja anafahamu gharama yake, haiwezekani mtu anayewania tu nafasi akaamua kufanya kitu hicho kama ndani yake ana fedha anazozipata kihalali. Akiamua kufanya hivyo, ajitangaze mapema ili aweze kubanwa na taratibu hizi. Kama atakuwa amejificha, akijitokeza mambo yote haya yaweze kuhesabika kwamba ni matumizi mabaya ya fedha, ambazo zingefanya kazi za umma ama za familia yake ama za kujenga nchi, kwa sababu kwa kipindi hicho lile eneo anakuwepo kiongozi anayeweza akayafanya mambo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naunga mkono vyama vikaguliwe, lakini na wagombea wanaowania ama ambao wamefika wakati kwamba sasa wameteuliwa, lazima wadhibitiwe matumizi ya fedha zao kwa kipindi chote ili kuweza kujenga hali ya usawa katika kugombea. Watu wote wawe na kiasi walichoambiwa wakitumie, kwa sababu mambo mengi yanasimamiwa na Chama na Serikali. Hakuna sababu yoyote ya mgombea mmoja mmoja, kutumia pesa nyingi; kama lengo ni kutafuta kukubalika kwa wapiga kura kuweza kupigiwa kura na kuweza kutekeleza Ilani ya chama chake.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo napenda kuliunga mkono ni hili ambalo vyama vikiungana, basi wale viongozi wao wa kisiasa, wapoteze nafasi. Kwa nini nasema hivyo? Tunapokaribia wakati wa kwenda kupigiwa kura ama wakati wa kwenda kuomba uongozi, maana yake kipindi cha uchaguzi kinapofika, yeyote ambaye ana nia ya moyoni ya kuona kwamba anapenda sasa kuwania nafasi katika kile chama cha siasa, awe na maamuzi makini toka ndani ya akili yake. Kama anahakikisha kwamba hiki chama anachotaka kujiunga nacho ni kwa sababu tu kitamuwezesha kwenda kupata ile nafasi ili akishafika pale basi, a-mobilise wenzake wakikatae kile chama, mtu huyu hana makusudio ya kuwa kiongozi katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, unapojiunga na chama, unakuwa umekubali malengo yake, madhumuni na katiba ya kile chama. Unapoomba kupewa nafasi ya kuchaguliwa, unakwenda kwa wenzako au kwa Watanzania, kuwaomba wakupe ridhaa. Maana yake ni kwamba, umekubali kuitangaza Ilani ya chama chako. Sasa baada ya kuchaguliwa

53 unaikataa ile Ilani; wewe hufai, unatakiwa uhakikishe kwamba, umeondolewa na umekwenda nje na chama chako ulichojiunga nacho upya, kiende sasa katika usajiri na pia ukawanie nafasi nyingine kwenye chama kingine, itikadi nyingine na ilani nyingine ambayo sasa unaiamini tofauti na ile iliyokuchagua.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naliunga mkono.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo nasema ni ukombozi mkubwa ni hili la kukomesha matusi na ulaghibishaji. Mimi naweza kusema hili ni ukombozi mkubwa, hasa kwa sisi wagombea wanawake. Wagombea wanawake, inapofika kipindi cha kwenda kuwania uongozi wa kuchaguliwa, hasa niseme katika Jimbo ambalo mimi nipo, kama hauna kifua, kama hauna uwezo wa kuvumilia matusi ya nguoni na udhalilishaji kwa watu unaotegemea kuwaomba wakuunge mkono uwe kiongozi wao, hakika hutaweza kuendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili limechukua muda mrefu sana, tumekuwa viongozi wa ndani ya Bunge hili, lakini moyoni tunasononeka jinsi tulivyodhalilishwa mbele ya watu wetu. Kwa msingi huu sasa, ninaamini kabisa kwamba, wanawake ambao wana nia ya kutaka kugombea hawataogopa tena udhalilishwaji, matusi ya nguoni hayatakuwepo tena, wala mambo mengine ambayo wapiga kura wanapotoshwa ili wamkatae mgombea mwanamke hayatakuwepo tena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanawake tumethubutu hata kukemewa kwa nini tunazaa! Hivi mwanamke ukiwa Mbunge unakatazwa kuzaa? Tumekatazwa kubeba mimba tukiwa Bungeni, lakini inaonekana ni tusi, mwanamke akiwa Mbunge anaambiwa asibebe mimba! Tumeambiwa mambo mengi ya ajabu na ya kutisha, kwa sababu hakukuwa na sheria inayosema hizi ni sifa za mgombea. Tumeambiwa mambo mengi na mengine sina haja ya kuyasema, kwa sababu wote ni mashahidi wa yote yanayofanyika huko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefurahi sana kwa hoja hii na hakika naunga mkono. Naomba udhalilishaji usionekane tu dhidi ya chama na chama, ninaomba pia dhidi ya mgombea na mgombea ili inapotokea jambo hili, hata kama uchaguzi unaendelea, hatua zichukuliwe na kesi ifanyike bila kusubiri uchaguzi uishe. Hii ni kwa sababu, uharibifu wa nia ya yule anayekuwa anagombea, unafanyika wakati kampeni zinaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba suala hili litiliwe mkazo. Mimi naamini kwamba, litatusaidia na litasaidia wanawake wengi kuwania hizi nafasi. Tutawapata wanawake wengi ambao wanapenda nafasi hii, kuliko tulionao leo; leo tunao wachache. Ninaamini kundi la wanawake wengi, linabaki nyuma likiwa lina uwoga wa kuona kuna matusi na udhalilishaji mkubwa juu ya nafasi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, ninalopenda kulizungumzia, nimefurahi sana nilipopokea amendment ya Mheshimiwa Shellukindo, inayorekebisha kifungu cha 12(b), kuhusu Uanzishwaji wa Baraza la Vyama vya Siasa. Sikufurahi kuona Wajumbe

54 wawe ni wale tu ambao ni Wenyeviti wa Vyama vya Siasa vyenye usajili wa kudumu. Nilikuwa nimeona ule ujumbe ni kidogo. Kwa maana hiyo, bila kupoteza wakati, naomba niseme kwamba, naunga mkono marekebisho haya. Naomba yakubaliwe na kuwa kifungu halali cha 12(b); kwamba, wajumbe waliopo hapa waweze kukubaliwa kuwa ni Wajumbe wa hili Baraza la Vyama vya Siasa. Isipokuwa kipengele cha 12(b)(3), kinasema kwamba, Mwenyekiti atakuwa ni Msajili wa Vyama.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili kama ambavyo amependekeza, nilikuwa naona kwamba lipo sawa. Isipokuwa mimi ushauri niliokuwa nao, ukitazama yale majukumu; jukumu la kwanza, majukumu ya Baraza yatakuwa ni pamoja na kumshauri Msajili katika migogoro mbalimbali inayoweza kuzuka ndani ya vyama.

Mimi nikizingatia hilo la kwanza, ninaona kama Uenyekiti na Umakamu, utatokana na Wajumbe ambao ni Wenyeviti au Makamu Wenyeviti na kwa kubadilishana, kukiwa kuna migogoro ndani mwao, ninahisi watashindwa kuelewena. Kwa hiyo, pengine nikiwa nina fikra kwamba, niombe tu kupendekeza kwamba, pengine tunao watu ambao wanaaminika, ambao wamefanya kazi hizi kwa muda, kwa mfano, wapo majaji wengi wastaafu, mimi nikafikiri kwamba pengine Mwenyekiti au Makamu angetokana na majaji wengine ambao ni wastaafu, ili kama kunatokea jambo, hawa waweze kusaidia, kwa sababu litakuwa ni suala la kisheria. Hawa ni watu ambao wamezoea kwa muda mrefu, kusimamia masuala ya kutoa haki pasipo kupendelea upande wowote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama itatokana na Wenyeviti, Makamu wao kwa kubadilishana, kuna wakati huyu aliyepata nafasi hawakumkubali. Kwa hiyo, kama kutatokea mambo ya kutaka kusuluhishana wao kwa wao, likawa ni tatizo, nikafikiria kwamba, pengine hata miongoni mwa hawa ambao wamependekezwa kwa mujibu wa mapendekezo ya Mheshimiwa Shellukindo, ingelitufaa vilevile wakatoka miongoni mwao. Lakini isije kuwa kwamba, pengine wataona Marais waliostaafu wametokana na Chama Tawala, hawa hawatawapenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tunao majaji, nilikuwa na pendekezo hilo kwamba, majaji waliostaafu wakubaliwe kuwa ndio wawe Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, kuweza kuhakikisha kwamba, hizi functions zilizo ndani ya kipengele cha 12(c) ziweze kufanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa naamini kwamba, kila mmoja anao Muswada huu, atakuwa anafahamu majukumu wanayotakiwa kuwa nayo Baraza.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuyasema hayo, naomba nichukue nafasi kusema kwamba, nilisimama kuunga mkono hoja na narudia kusema kwamba naiunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Umenikumbusha vidonda vilivyonipata wakati nagombea Ubunge mwaka 1995; matusi! (Kicheko/Makofi)

55

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, nami nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia hoja iliyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi napenda kuunga mkono hoja hii kwa hatua zote, kwa sababu Muswada huu umekuja katika muda ambao tunauhitaji sana, kwa kuzingatia kwamba, Jamii ya Watanzania kila kukicha inazidi kubadilika na sasa tunahitaji kuwa na Muswada au sheria ambayo itaturatibu vizuri zaidi na kuondokana na vitu ambavyo havijengi tabia na utamaduni wa Mtanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, kweli ukiangalia viongozi wotw ndani ya Bunge hili tumechaguliwa. Haiingii akilini kwamba, wewe ulisimama kwa itikadi yako, ukasema mimi naomba nafasi fulani ili niongoze wananchi na wananchi wakakupigia kura kwa kutumia itikadi ambayo umewaambia mbele yao na ukaithibitisha kwao. Leo baada ya siku mbili, tatu, useme kwamba, hiyo itikadi haikufai, sasa unataka uondoke uende mahali pengine! Kweli kupitia Muswada huu ni vyema kama mtu unaamua ku-cross the floor, unataka kuhama ama vyama kuungana, basi nafasi za viongozi wao vilevile ziweze kukoma kwa wakati huo huo. Haiwezekani leo hii ukasema mimi nina imani na Chama cha Mapinduzi, halafu kesho ukasema sina imani na Chama hicho au ukasema mimi nina imani na CHADEMA, kesho ukasema sina imani tena. Nadhani wewe sio kiongozi, hufai!

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzangu wamesema, hivi Watanzania tutafikia lini na sisi tubadilike? Kiongozi unathubutu kupanda kwenye jukwaa na kuanza kutukana wenzake, huo ni ustaarabu gani? Mimi nafikiri Watanzania tufike mahali tubadilike, hata kama unataka kuomba kura, huombi kura kwa kumtukana mwenzako ili uweze kushinda. Hata wanaokuchagua, watasema huna sifa za kugombea nafasi hiyo. Sasa wenzetu wa Upinzani, wao wakisema wanaona wanapaka mafuta, wakiguswa kidogo wanalalamika. Kwa mfano, jana Waziri Mkuu amesema jamani Wapinzani nafasi ya kuchukua dola bado, labda mtapata mbele ya safari, wanalalamika. Wao wanazunguka nchi nzima wanasema eti Operation Sangara; hivi wananchi ndio Sangara? Mnawadhalilisha wananchi kuwaita Sangara, siyo samaki mnawatukana, kitu ambacho siyo kizuri. Sasa mambo kama haya kupitia Muswada huu, ninapenda kabisa suala la lugha za matusi si ustaarabu kwa Mtanzania na naomba tubadilike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la ukaguzi wa mahesabu ya vyama ni kitu muhimu sana. Leo wengine wananyoosha kidole, unajua ninyi mnapata pesa za uchaguzi; hivi ninyi tukiwauliza mnatoa wapi za kwenu mbona hamsemi! Mnapata misaada kutoka nje, hamsemi! Mnahujumu nchi, hamsemi! Tukisema sisi wengine, mnasema hapana, ninyi mnatoa wapi fedha za uchaguzi! Sasa mimi nafikiri Watanzania tuwe na moyo wa kuijenga nchi yetu. Hii ni nchi yetu sote na naomba viongozi wote wa kisiasa, tuwe na majukumu sahihi ya kuilinda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani kitendo cha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kupitia mahesabu, kitatusaidia sana kwa sababu kuna viongozi wengine wamefanya vyama ni mali yao. Toka chama kianzishwe, yeye ni Mwenyekiti wa chama

56 sijui mpaka lini? Uongozi maana yake ni kubadilishana, haiwezekani chama kikawa na Mwenyekiti huyo huyo toka kimeanzishwa mpaka leo! Mgombea huyo huyo, nafasi ya kugombea ni yeye tu! Unakuta Mwenyekiti wa Chama ni yeye, mke wake ndio Makamu Mwenyekiti, mdogo wake sijui Katibu Mkuu wa Chama. Chama gani hiki, halafu unasema eti naendesha chama cha siasa; hii ni kampuni au ni chama cha siasa?

Leo unaamua kufukuza Wabunge wako, unasema wewe out, kwa sababu huna maslahi nao! Jamani tufike mahali, tunaposema tunaunda vyama vya siasa, viwe vyama ambavyo vinaweza kuwakilisha wananchi, siyo familia au ukoo; it’s not a company, is a political party! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, unajua wakati mwingine, nawaona ndugu zangu nawacheka sana. Siwaelewi, kwa sababu vyama vingine vimeundwa kwa nasaba ambazo hazileti maadili ya Kitaifa. Kwa hiyo, nilikuwa nashauri kwamba, kupitia Muswada huu, tuweke kanuni kabisa kwamba, chaguzi ndani ya vyama ziweze kuratibiwa. Haiwezekani mtu akawa mgombea miaka yote, lazima kanuni ifanye namna hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile wanasiasa wenzetu kila mmoja anakuwa anataka kupendezesha mambo yake. Tunasema kwamba, tunaunda Baraza la Vyama vya Siasa, haiwezekani kwenye Baraza hili eti kila chama kiwe na uwiano sawa wa nafasi. Haiwezekani yule ambaye ana nafasi kubwa zaidi, apewe nafasi ya uwiano ulio sawa na nafasi aliyonayo. Huwezi ukaunganisha chama ambacho kina Mwenyekiti huyo huyo mmoja, Katibu Mkuu mke wake, naye apate uwakilishi kwenye Baraza hili, haiwezekani! Twende kwa demokrasia, ndio iweze kuchuja uwakilishi ndani ya Baraza hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kasoro kama hizi ningependa sana ziwekwe vizuri kwenye kanuni za kuendesha vyama vyetu vya siasa, kwa sababu tusipoweka kanuni zetu sahihi, tutapata mvurugano.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia siasa za chuki na matusi, zimekuwa kila mwaka zinaongezeka. Mzee wangu Ndesa, hivi nikisimama kwenye jukwaa nikaanza kukutukana kwamba Mzee Ndesa hafai, hana nini, halali nyumbani kwake, hana kitanda; nitakuwa sijakutendea haki. Kwa sababu ya siasa, mtu anaamua kuzusha kitu. Mheshimiwa Ruth Msafiri, kasema hapa, akina mama wanatukanwa wasigombee nafasi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nikimwona mwanamke mjamzito, nakuwa na matumaini kwamba ana mimba ambayo baada ya miezi tisa atajifungua; ni akili ya kawaida ya binadamu. Nikiona baba ana tumbo linazidi kukua, nitashindwa kuelewa hivi ana mimba ana kitambi au ana ugonjwa, kwa sababu sitegemei kuona mwanadamu wa jinsia ya kiume anapata mimba halafu tuseme kwamba atazaa. Sasa wenzetu hawa wanataka wamwone hata baba anapata mimba, wategemee mtoto, haiwezekani!

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napenda kusema kwamba, sote ni wanasiasa, hebu tuwe katika misingi ya wanasiasa; tufanye siasa zilizo sawa, jinadi kwa sera za chama chako na uweze kupata ushindi bila kuwa na tatizo. Ukianza kusema

57 kwamba, mimi nataka nijinadi kwa sera hii, halafu baadae tena huiamini, haina maana. Mimi nafikiri hili ni sahihi kabisa kwamba, if you cross the flow, una-lose.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii haina mjadala, tujenge nidhamu ya watu kama kweli wana nia ya kuitumikia nchi, tusifanye nchi hii kama majaribio. Hatutaki umalaya wa kisiasa, tunataka watu ambao ni wanasiasa na wenye nia thabiti ya kuitumikia nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tunakutana hapa ili tuweze kujadili mambo mbalimbali ya mustakabali wa kitaifa, sasa wewe leo hii mara huku kesho kule, basi hufai kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina mfano, kaka yangu alikuwa anaongea hapa, Mheshimiwa John Cheyo, nilikuwa namwangalia sana, kwa sababu chama chake yeye ndiye Mwenyekiti, sijui Katibu Mkuu ni nani na kadhalika. Amesema nay eye ana haki sawa ya kuwa na chama ambacho kina uwakilishi katika ngazi zote. Tunaomba mifano kama hii, tuitumie sasa kuuboresha Muswada huu, vyama vya siasa viwe vinazingatia maslahi ya wananchi au wanachama wake. Tusiangalie maslahi binafsi, kwa sababu tukiwa na maslahi binafsi then tunakuwa tunakiuka na kupotosha dhana nzima ya Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kwa kuzungumzia suala la fedha za uchaguzi. Hili bado ni tatizo na naomba nikiri kwamba, si kwa vyama bali hata kwa wagombea vilevile. Watu wengi wanajaribu kutafuta fedha chafu katika kushiriki mambo ya uchaguzi na hata vyama vingine leo hii tunasikia kwamba, vina mikakati ya kupata fedha kutoka sehemu mbalimbali kwa wahisani na kutoka nje ili tu waweze kushika dola. Dola inaweza ikawekwa na mamluki ambao hawana sifa za kuendesha nchi!

Tunaomba kupitia Muswada huu, tuweze kuratibu vizuri sana fedha zote za mambo ya uchaguzi si kwa wagombea na si kwa vyama vya siasa. Ninaamini kwamba, kila chama kama kina wanachama wake, kitaweza kukusanya mapato yake na kupata ruzuku. Kama kina ruzuku, kitumie vizuri mapato haya kwa ajili ya vyama vinavyohusika. Tunaomba kwa Msajili wa Vyama, ofisi yake iboreshwe na aongezewe meno ya kuvisimamia vyama vya siasa. Ninaamini yeye atakuwa ni changamoto kubwa sana, kazi anayofanya sasa hivi ni nzuri, lakini tuiboreshe zaidi ili aweze kusimamia vizuri, kwa sababu kadiri siku zinavyokwenda ndio mambo yanavyozidi kubadilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii. Naomba basi nirudie kusema kwamba, ninaunga mkono hoja hii. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. ROSEMARY K. KIRIGINI: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nianze kwa kukushukuru, kwa kunipatia nafasi hii adimu, ili niweze kuchangia katika mada iliyoko mbele yetu.

58 Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda nimpongeze Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kutuletea marekebisho haya mapya ya sheria, ambayo nina imani kabisa, sheria hizi mpya zitatusaidia kuweza kurekebisha hali iliyoko sasa, maana tunatoka katika hali halisi ya amani ya nchi yetu na tunaelekea kwenye hali tofauti kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuanza kwa kutoa maoni yangu katika ukurasa wa tano, kuhusu vigezo vya uongozi. Binafsi, licha ya kwamba mgombea anatakiwa ajue kusoma na kuandika, lakini vilevile ninaomba level ya elimu iwe specified, maana ninaamini katika dunia ya leo ya utandawazi, kujua kusoma peke yake na kuandika, sidhani kama ni kigezo muhimu kwa kiongozi. Vilevile kiongozi kuwa Mtanzania, mimi ninaomba watu wote wanaotaka kuwa viongozi lazima wapeleke vyeti vya kuzaliwa, kwa sababu tumeona watu ambao si Watanzania halisi wanakuwa. Mtu tu amekaa tu Mkoani Mara kwa muda mrefu, basi yeye anasema amekaa Tanzania muda mrefu, anageuka anasema yeye ni Mtanzania. Kwa hiyo, hapa sheria hizi zingeelekeza kwamba, mbali na form zote ambazo kiongozi anatakiwa kujaza, lakini vilevile apeleke cheti cha kuzaliwa ili kutambulika uzalendo wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa pia kuzungumzia ukurasa wa nne, ambao unazungumzia mtindo wa watu wengi kujiingiza kwenye siasa kiholela. Tumeshuhudia wakati wa uchaguzi, watu wengi wamekuwa wakijihusisha sana na shughuli za kisiasa kiholela. Mtu hana chama, lakini anapanda jukwaani na kukisemea chama fulani. Mtindo huu umekuwa ni kero sana na unapoteza amani ya nchi yetu. Adhabu iliyopendekezwa, kwangu mimi naona ni ndogo sana. Kwa hiyo, mtu yeyote atakayebainika hana chama na anapanda jukwani na kukisema chama chochote ambacho yeye si mwanachama halisi wa chama hicho, basi adhabu hiyo iongezwe kuwa miaka miwili mpaka mitatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika Muswada huu ukurasa wa saba, naunga mkono maoni ya Kamati kwamba, kifungu kiandikwe upya. Lile neno linalosema “a member or a leader of registered political party” liondolewe na badala yake liwekwe neno “any person,” hii itasaidia. Vilevile upatikane ufafanuzi zaidi juu ya vipeperushi, kwa sababu tumeona katika chaguzi nyingi, watu wanaibuka, wanachoma vitu kama t- shirts au vilemba ambavyo vinakuwa na nembo ya chama, ambayo inabeba bendera. Kwa hiyo, ningependa hapa kuwe na ufafanuzi, isiwe mtu ata-abuse bendera, lakini hata lile vazi la chama ambalo lina nembo ya bendera, mtu huyo achukuliwe hatua kali.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kuongelea lugha chafu ya matusi. Msemaji aliyepita ameongelea, lakini na mimi napenda kutilia mkazo. Kwa kweli imezuka tabia mbaya, ninavyoelewa kwenye uchaguzi, vyama mbalimbali vinakuwa na itikadi. Kwa hiyo, unachotakiwa pale ni kunadi itikadi yako kwa wale wanachama au wale wananchi walioko kwenye lile eneo. Umezuka mtindo wa watu kupanda jukwaani na kuanza kutukana chama kingine. Wengine wanafikia hatua ya kumtukana mpaka Rais wa nchi. Kwa hiyo, sheria hii naomba ichukue mkondo wake na watu hawa washughulikiwe ipasavyo, bila kuona aibu kama aliyepanda hapo jukwaani ni Mwenyekiti wa chama husika au ni Mbunge, achukuliwe hatua za kinidhamu. (Makofi)

59 Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, ningependa kuongelea ukurasa wa nane, suala la mapato na matumizi katika vyama vyetu. Imegundulika kwamba, pamoja na nchi yetu kuwa ya amani na nchi nyingi zimekuwa zikija katika nchi yetu kujifunza amani, lakini vilevile kuna nchi nyingine ambazo haziitakii mema nchi yetu, wamekuwa wakija nchini kuvuruga amani. Njia kubwa ambayo wanatumia ni kupitia vyama na hasa vyama vya wenzetu Wapinzani; wanatumika sana katika njia hii na ndio maana katika sheria hii inasema, lazima vyanzo vyote vya mapato vijulikane. Kuna nchi zimekuwa ziki-pump in fedha nyingi sana kwenye hivi vyama, kwa ajili ya kuondoa amani iliyopo. Kwa hiyo, jambo hili ni zuri sana katika kundeleza amani ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine amelisemea Mheshimiwa Chegeni, lakini na mimi napenda kutoa msisitizo; ni kuhusu vyama kupata ruzuku, lakini ruzuku hii inaishia mikononi mwa watu wachache, watu wengine katika chama hawafaidiki. Ruzuku hii haifiki kwenye Mikoa. Kwa hiyo, ingawa wenzetu wanaiona sheria hii siyo nzuri sana, lakini itasaidia kwa wale wanachama wenzao wanaopiga kelele kila siku kwamba, hawaoni pesa za ruzuku. Vilevile hata kwa chama chetu tawala, wanachama na wananchi kwa ujumla, itaondoa haya malalamiko yaliyopo hivi sasa kwamba, chama tawala kinatumia fedha nyingi sana. Tukiweka haya mambo wazi, malalamiko kama hayo hayatakuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naunga mkono kwa dhati kabisa, sheria hizi mpya ambazo zinawekwa, zitatusaidia kutupeleka salama huko tunakoelekea.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi. (Makofi)

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kanuni ya 64(1)(a) inasema mambo yafuatayo: “Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, Mbunge hatatoa ndani ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli.”

Mheshimiwa Naibu Spika, mchangiaji aliyepita wakati anatoa maoni yake, amesema wazi kwamba, Vyama vya Upinzani vinatumiwa na watu wa nje ili kuvuruga amani. Sasa mimi ninaomba ama afute kauli yake au alete ushahidi kuthibitisha kwamba, kuna chama kingine chochote kinachotumiwa na watu wa nje kuvuruga amani. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Aliyesema nani Kirigini? Eti ulisemaje?

MHE. ROSEMARY K. KIRIGINI: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Mdee, kwa kutoa comments zake. Ninafikiri hakusikia vizuri, nimesema “inajionyesha”; inajionyesha kuna vyama ambavyo vinatumika na kuna nchi ambayo inatumika na haijatajwa hapa kama ni Upinzani au ni Chama Tawala. (Makofi)

60 NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hapa tunajaribu kutunga sheria ya kuboesha mwenendo mzima wa siasa ndani ya Bunge. Hisia nyingi zimetolewa hapa, mimi nimeamua kunyamaza, kwa sababu mwisho wa siku tunataka sheria iweze kutusaidia kujenga uwepo wa vyama vyetu vya siasa. Sasa hizi hisia na kutaka kunyoosheana vidole hapa, hamuwezi kufika, maana nimesikia nikaona niache tu. Tunaendelea.

MHE. PONSIANO D. NYAMI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba nitoe masahihisho jina langu ni Ponsiano na sio Ponsiana, Ponsiana ni mwanamke na Ponsiano ni mwanaume. Nashukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, napongeza kwa kuletwa Muswada huu na Mheshimiwa Waziri ninampongeza sana kwa marekebisho haya mazuri. Pili, naomba kuipongeza Kamati yenyewe, ambayo nayo imejaribu kupendekeza mambo mengi ambayo ni mazuri na Wabunge wote wawili ambao wameleta schedule of amendments; Mheshimiwa Shellukindo na Mheshimiwa Kabwe Zitto, wamejitahidi kuleta marekebisho ambayo ni mazuri kwa ajili ya kuboresha hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitapitia kwa ufupi tu maeneo mawili, matatu. Kwanza kuhusu vyama vinapokuwa vimeungana, nashukuru kwa marekebisho ambayo yamefanyika hapo, naomba kusisitiza tu kwamba, vyeo ndani ya vyama vyenyewe vilivyoungana, ndiyo viweze kukoma, halafu waweze kufanya uchaguzi kwa maana ya kukitambua chama hicho. Kwa upande wa Wabunge, Madiwani na Rais, wao wanaweza wakaendelea na nyadhifa hizo hadi kipindi chao kitakapokwisha. Huu mtindo wa vyama labda vinaungana na pengine vinapoungana katika kipindi cha mpito, wanakuwa na bendera mbili au wanapokuwa na shughuli za uchaguzi wanapeperusha bendera mbili, moja inapanda juu zaidi na nyingine inateremka chini, naona siyo mzuri, wanatakiwa waamue kutumia bendera moja badala ya kutumia zote mbili.

Jambo lingine ni kiongozi wa kisiasa unaposema awe anajua Kiswahili ama Kiingereza, kwa maana ya kusoma na kuandika. Mimi sioni mantiki, mtu ambaye amesoma kisomo cha watu wazima, akajua kuandika Kiswahili halafu huyo ndiyo unamwambia aje agombee Udiwani au Ubunge, siyo sahihi hata kama mngesema sijui kuna haki za binadamu kikatiba la hasha, sivyo!

Mheshimiwa Naibu Spika, Diwani anatakiwa awe mwelewa mno; yeye ndiye kiongozi katika Halmashauri. Watendaji wake kwa mfano, ukienda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Mipango wale wa Fedha, Maafisa Elimu, Kilimo, DMO na wenzake, wana shahada na Diploma mbalimbali. Wale ni wataalamu hasa, lakini wenye maamuzi ni Madiwani, wanaojua kusoma na kuandika tu. Hivi mambo yakiharibika pale unamlaumu nani; na je, wale ambao ni wataalamu wa kiasi hicho hawawezi kuwaburuza?

Mheshimiwa Naibu Spika, si suala la kusema kiongozi wa kisiasa awe anajua kusoma na kuandika tu, ni lazima tuweke levels katika nafasi zile za kugombea. Haiwezekani unamleta mtu ambaye anasoma na kuandika tu Mbunge, atakaa miaka mitano bila kuongea neno na atashindwa kujenga hoja; iwe kutetea Chama chake au

61 kutetea Sera na masuala mengine ya maendeleo ya wananchi wake, kwa sababu na yeye ni mbumbumbu. Kwa hiyo ni lazima hapa tunaposema kiongozi wa kisiasa, tuseme ni wa ngazi gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa upande wa Chama cha Mapinduzi kwamba, kiongozi wa kisiasa ambaye anagombea Urais ni lazima angalau awe na digrii ya kwanza; hiyo ni sawa. Kwa hiyo, nilikuwa naomba kwa upande wa Serikali wajaribu kuona ni jinsi gani wanaweza wakarekebisha hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii kuna mambo ya internet, kama mimi najua kusoma na kuandika tu, mambo haya nitayajuaje ili niweze kusoma mambo ya kimataifa? Bado itakuwa ni ngumu.

Mhehsimiwa Naibu Spika, pia nilikuwa naomba kingeingizwa kifungu fulani kwenye sheria hii, pale Diwani au Mbunge anapokuwa amefariki au kuna sifa fulani amekosa wa chama hicho, katika kipindi kinachoendelea pale badala ya Serikali kuendelea kutumia pesa nyingi, vyama vyenyewe kutumia pesa nyingi na kupoteza muda; kwa nini kifungu kisingeingizwa kwamba, kwa chama kile kile kilichokuwa na mwakilishi kama ni Mbunge au Diwani, aweze kuteuliwa au wao wenyewe aingie kumalizia kipindi cha miaka mitano au miaka ile iliyobakia, badala ya Serikali kuingia gharama ya mamilioni ya mamia katika Jimbo au Kata na kadhalika? Tunapoteza pesa nyingi, ambayo ingeweza kutumika kwa maendeleo mengine ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kiingizwe kifungu kinachosema, endapo itatokea hivyo, kwa mujibu wa Katiba hiyo basi, huyu Diwani au Mbunge ambaye amepoteza labda maisha yake au vyovyote itakavyokuwa, kutoka kwenye chama hicho hicho achaguliwe mwingine kama ilivyo kwa Viti Maalum. Mbunge wa Viti Maalum ikitokea bahati mbaya labda amefariki, kama ambavyo pia imetokea katika Bunge hili, walioteuliwa ni wa kutoka katika chama hicho hicho ambacho Mheshimiwa Mbunge huyo amepoteza maisha. Uchaguzi haufanyiki hata kwa upande wa Waheshimiwa Madiwani wa Viti Maalum.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naomba busara itumike pia kifungu hicho kiingizwe ili pesa nyingi zisiendelee kupotea na usumbufu mwingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Chama cha Siasa, tusifananishe tu na NGOs ambazo leo zinaibuka na kesho zinakufa. Nchi zilizoendelea, hazipotezi muda sana katika masuala haya ya kisiasa; zina vyama vichache, Uingereza wana vyama vitatu, Marekani nadhani viwili. Mimi naona huu ndiyo ushindani mzuri wa kisiasa, lakini mnapokuwa na utitiri wa vyama, sasa hivi Tanzania tuna vyama sijui 18 kama sijakosea; ni vingi mno na vinaweza vikaendelea na kufikia hata 50 na kadhalika. Sasa vingine vinakuwa havina mwelekeo kabisa. Nilikuwa naomba kiwepo kifungu kinachoelezea kwamba, uhai wa chama ni ndani ya miaka kumi na baada ya hapo vitathminiwe tena; vyama ambavyo siyo active vifutiwe usajili huo, kuliko kuendelea kujulikana kwamba vipo. Kuna vyama tangu vilipoundwa hata sivifahamu, hata kwenye uchaguzi havijawahi kuingia, lakini

62 vipo tu vinapoteza muda; ndani ya miaka kumi kama vinaonekana vinasua sua basi vifutwe. Kifungu hicho nilikuwa naomba kiwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba niunge mkono Muswada huu, pamoja na marekebisho ambayo yameletwa na yale ambayo nimependekeza hapa. Ninajua Serikali itayaingiza na itayaleta jioni. Mapendekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Shellukindo, nayaunga mkono pia. Nashukuru sana. (Makofi)

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada huu ni muhimu kwa Taifa letu. Ni Muswada unaohusu vyama vyote vya siasa nchini.

Napongeza uwepo wa Kifungu Na.18 ambacho kinalenga au kinahusu ukaguzi wa fedha za ruzuku na vyanzo vingine vya fedha ndani ya vyama vya siasa, kwani sasa Watanzania watajua kila chama kina pesa kiasi gani na kimezipataje na matumizi yake yakoje.

Hili ni jambo la kupongezwa sana kwani Ofisi ya Mkaguzi wa Serikali itafanya kazi yake hadi katika Vyama vya Siasa tofauti na awali kwani nazo ni pesa za walipa kodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napendekeza Kifungu 10 (A) (a) kwenye sheria ya zamani ya 1992, kuwa, kiongozi wa siasa lazima ajue kusoma na kuandika tu kuwa ndio sifa ya kupata nafasi ya kugombea nafasi ya kisiasa wakiwemo Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, elimu ni muhimu, lazima viwango virekebishwe kwani dunia ya sasa inahitaji wasomi zaidi katika nafasi za uongozi kwani kuna mambo mengi ya kitaalam na hoja nyingine (technical) zahitaji taaluma au elimu ya zaidi ya kufahamu kusoma na kuandika tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile napenda kushauri sheria hii itambue umuhimu wa mahusiano mengine ya kinyama badala ya kulazimisha vyama kuungana. Lakini sheria hii imeonyesha Serikali inaogopa na sijui uwoga wa nini, maana huu sio Muswada wa Vyama vya Upinzani tu. Ni wa vyama vyote nchini kwani sheria hii haikutoa kibali cha vyama kuungana kwani vijana vikiungana vinapoteza uhalali wa kuwepo. Serikali itupe maelezo kwa nini iwe hivyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tukubali kila chama kina sera na itikadi zake. Hivyo basi, sio sahihi kwa sheria kulazimisha ushirikiano wa aina moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono kifungu kipya cha 12 (a)(1) kinachokataza chama/vyama kufanyia shughuli zake kwenye nyumba za ibada, (misikiti, makanisani) na ndani ya majengo ya Serikali. Tabia hii ilionekana wazi na ninapongeza kuwepo kifungu cha kisheria kinachokataza hayo, lakini sheria imeacha kuainisha

63 mambo mengine yakiwemo matumizi ya vyombo vya Serikali yakiwemo magari, matumizi ya vyombo vya dola hasa maeneo yenye upinzani mkubwa au pale ambapo chama cha upinzani kinakuwa na wafuasi wengi. Tumeshuhudia matumizi ya vyombo vya dola kama Polisi na Mahakama, havitumiki vizuri, vinatumiwa hasa na chama tawala.

MHE. SIRAJU J. KABOYONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake kwa matayarisho mazuri ya Muswada.

Mheshimiwa Naibu Spika, napendekeza marekebisho au/na nyongeza zifuatavyo; section 10 A (a) kwa nini umri usiwe miaka 18 badala ya miaka 21? Section 11 (a)(2) ‘third line as may be prescribed …’ iwekwe wazi nani atakaye-prescribe manner ya agreement, section 11 B (4) yatumike maneno ‘assets’ and liabilities badala ya the properties and assets. Kwani properties ni sawa na assets, section 12 (a)(2) ruhusa inayotolewa hapa isijumlishe maeneo ya ibada hata kwa kibali; section 18 (a) ipanuliwe kwa kuongeza ukubwa wa michango/misaada inayotolewa kwa vyama na aina ya matumizi yanayoruhusiwa, section 21 (b)(2) members of the council shall be national leaders….’ Napendekeza baada ya maneno ‘National Leaders’ yaongezwe maneno au ‘wawakilishi wao’.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. FATMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaunga mkono Muswada huu na ninaupongeza kwa kufanyika marekebisho na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kufanya marekebisho ukizingatia kuwa mwaka huu kuna chaguzi za vitongoji, mitaa na vijiji na pia 2010 mwakani kuna chaguzi za Diwani, Wabunge na Rais. Kwa hiyo, marekebisho ni muafaka na Baraza ni muhimu ili kuweza kusuluhisha migogoro. Kutokana na uzoefu wa chaguzi zinavyofanywa, ugomvi mbalimbali huwa vinatokea. Kwa hiyo ni muhimu kuwa na Baraza ili kuweza kusuluhisha ugomvi kwani zamani waliachiwa Tume ya Uchaguzi au Serikali za Mitaa au DED au DC. Hii haitoshi Baraza pekee litafanya suluhishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu demokrasia, utawala wa demokrasia ndio utawala bora duniani kwani ni utawala wa ushirikishwaji na unaleta usawa, uwazi, uwajibikaji, udhibiti wa matumizi mabaya ya madaraka kwani kuna uchaguzi huru na wa haki na hufanyika kwa muda wa miaka mitano. Atakayeshinda ndiye atakayetawala. “Wengi wape.”

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya kuwa na vyama vingi ni kushindana katika maendeleo na sio kushindana katika kubishana au kubughudhiana, wananchi ndio wateja wetu. Sasa hivi tuna vyama vingi vya kisiasa takriban vyama zaidi ya 18 na vingine vinaendelea kusajiliwa na vingine vinazidi kuomba kusajili. Lakini vyama maarufu ni CCM, TLP, NCCR – Mageuzi, CUF, UDP, CHADEMA, NRA, PONA, DP, NLD na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba karatasi ya majina ya vyama tafadhali.

64

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vyama hivi vinachukua muda mrefu kubishana badala ya kufanya maendeleo. Hii siyo nia ya mfumo wa demokrasia. Kwa sheria hii utazingatia suala zima la kuzima ubabe, kashfa, matusi, kebehi zinazofanywa na baadhi ya vyama.

Kwa siku za nyuma katika miaka ya sitini tulikuwa na vyama, kwa mfano Chama cha Congress cha Halifa Chipaka, PDP cha Kasanga Tume, UTP cha Zuberi Mtevu, Chama cha UMUNT cha mashehe wa Dar es Salaam, vyama hivi vilijifuta kutokana na Tanzania wakati ule kutokuwa na sheria maalum na usimamizi maalum. Kwa hiyo, suala la kuwa na sheria maalum na kuwa na Serikali ya demokrasia, ninaafiki kwamba ni njia pekee ya kuimarisha demokrasia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Tanzania ni demokrasia pekee ndio tutaiweza. Aina nyingine ya utawala sisi hatutaweza kwa mfano; Tanzania hatutoweza utawala wa kifalme, utawala wa ukoo kama Uarabuni, utawala huo hakuna uchaguzi, sisi hatuwezi, utawala wa U-dictator, utawala wa imla ambapo msemaji ni mmoja mtoaji amri, hii Tanzania hatuwezi kama Uganda Iddi Amini, Udini; kuna Serikali nyingine za udini, yaani watakaotawala lazima wawe ni dini fulani.

Hii sisi hatuiwezi, Serikali ya Mapinduzi, maumau, kupigana kwanza na mwenye nguvu ndie atawale, kama Rwanda, Burundi, hii pia Tanzania hatuwezi. Tumezoea amani na utulivu, demokrasia ya wengi wape, kufanya uchaguzi, atakayeshinda atatawala, hii ndio sahihi kabisa kwa Tanzania. Tunaipongeza Tanzania kwa kuchagua mfumo wa utawala wa demokrasia, utawala wa ushirikishwaji, usawa, uwazi, uwajibikaji na udhibiti wa matumizi mabaya ya madaraka na kila baada ya miaka mitano ni uchaguzi. Ninaafiki Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, muungano wa vyama ni sawa kwani ni hiari ya chama kuungana, sio lazima kama wengine wanavyofikiri chama kina hiari kuungana na chama kingine au kukaa pekee sio lazima.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. SAVELINA S. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mengi ya maudhi sana kwa wananchi pamoja na viongozi kipindi cha chaguzi, nitapenda wazi wakati Mheshimiwa Waziri anajibu nipate majibu mazuri. Suala la utawala bora, katika kipindi cha chaguzi mambo mengi sana yanakiukwa na haki za binadamu. Haya yote: Je, sheria hii itasaidia au vipi? Nina uhakika hata juzi chaguzi hizi za Mbeya makanisa, ofisi za chama kufanyia maafa mengi sana, hata vituo vya kupiga kura, kununua shahada za kupigia kura kipindi cha chaguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatumia pesa za walipa kodi kwenye uandikishaji, wananchi wanajitokeza sana baadhi ya watu kipindi cha chaguzi wanavinunuaje? Muswada huu unasaidia na hili la Wabunge na Madiwani kupoteza nafasi zao. Nitaomba haya yote nipatiwe majibu mazuri.

65

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, pesa tunaomba tujue hata kwenye vyama vyetu tujue ni shilingi ngapi, siyo zitoke kwa siri zisiwe zinaleta migogoro. Naomba baraza litakaloundwa lichanganye vyama vyote viwemo sio chama kimoja tu kuweka haki sawa kwa watu wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaomba haya yote niliyoweka nipatiwe majibu.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kinachoagiza vyama vya siasa kuwasilisha taarifa ya fedha na matumizi kwenye ofisi ya msajili.

Hili ni jambo litakalosaidia kuzuia ile tabia ya baadhi ya vyama kutoa zawadi nyingi kama T-shirt, kofia, sukari na kadhalika ambazo zinawarubuni baadhi ya wapiga kura kwa sababu ya umaskini wetu badala ya kumchagua mtu anayeweza kuwaongoza kimaendeleo wanaishia tu kuchagua mtu sababu ya zawadi na hili liende mpaka kwenye ugombea wa ngazi zote mpaka Mwenyekiti wa Kijiji lazima waeleze wanapata wapi fedha za kufanyia kampeni zaidi ya walizopewa na vyama vyao kwa ajili ya kufanyia kampeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kifungu 12 (a)(1) nakiunga mkono kabisa kutenganisha siasa na dini na hii iende zaidi pia kuzuia chama ambacho kipo madarakani wakati zikifanya ziara za kiserikali kutumia fedha za walipa kodi kutumia magari, Jeshi la Polisi, kufanyia shughuli za chama kwa kufanya mikutano ya hadhara ya chama husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya lugha ya matusi; nalaani kabisa mtindo wa wanasiasa kutukanana kwenye majukwaa ya siasa pasipo na sababu, wanasiasa wanadi sera zao na watueleze mikakati gani wanayo kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

MHE. ALOYCE B. KIMARO: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza msajili wa vyama, naunga mkono hoja, naunga mkono schedule of amendment ya Mheshimiwa Shellukindo, naunga mkono vyama vya siasa kuwa na maadili na kuacha matusi na kupandikiza chuki ndani ya jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, vyama vya siasa ambavyo nia yake ni kupata madaraka kwa njia ya kuzua mambo ya uongo na ya uchochezi hasa mashuleni viongozi wa siasa wanajua wanafunzi wanapaswa kusoma wala siyo kufanya siasa mashuleni. Viongozi wa siasa hawalitendei haki Taifa hili kwa kuwachochea wanafunzi wagombane na Serikali yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, vyama vya siasa vinapaswa kuwa na walezi wa watoto kwa kuacha kuwatumia kisiasa. Migomo ya vyuo vikuu ina harufu kabisa ya siasa ndani. Naomba hili likome kabisa, wanafunzi waachwe wasome, baadaye wafanye siasa tu wakitaka wanapomaliza chuo.

66 MHE. AMEIR ALI AMEIR: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu na pili, namshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Mheshimiwa Philip Marmo na msajili wa vyama kwa kuleta Muswada huu mbele ya Bunge letu Tukufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeridhika na maudhui na madhumuni ya Muswada huu ambao una lengo la kurekebisha mapungufu yaliyoko katika uendeshaji wa shughuli za vyama vyetu pamoja na kuondoa migogoro.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitishwa kwa Muswada huu kutaleta heshima kwa nchi, chama na chama, mtu kwa mtu hasa kwa vile vyama ambavyo mara kwa mara vinavunja sheria ya nchi kama vitashitakiwa pindi vikifanya makosa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na uundwaji wa Baraza la Vyama na sina wasiwasi na wajumbe wa Baraza. Lakini naomba chama chenye Wabunge wengi kipewe nafasi kubwa ya wajumbe ambao watachagua wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba msajili awe makini kusimamia sheria hii. Zitakapopitishwa aache uwoga kwa chama chochote kitakachokwenda kinyume, asisite kukichukulia hatua zinazofaa ili kulenga demokrasia ya kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono vifungu vyote vilivyomo katika Muswada huu.

MHE. CHARLES N. MWERA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Waziri Mkuu kwa Muswada huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuwepo na Baraza la Vyama ni jambo la muhimu ili Baraza hili liwe la usuluhisho, ambalo pengine litakuwa na wanasheria ndani yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema viongozi kama Rais, Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa/Vitongoji waendelee kuwa na vyeo vyao pale vyama vinapoungana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye nafasi ya Rais, napendekeza kuwa ili uwe Rais ni lazima uwe Mbunge. Hii itawapa nafasi viongozi (wagombea Urais) kuweza kuwa Wabunge kama hawakupata nafasi na kuwa Rais.

Mheshimiwa Naibu Spika, mapato na matumizi kwa vyama ni muhimu sana ili kila chama kiweze kukaguliwa mahesabu yake ili wananchi waweze kufahamu jinsi kodi yao inavyotumika.

Mheshimiwa Naibu Spika, viongozi wa Wilaya (DC’S) na Mikoa wasiwe makada wa vyama vya siasa wachaguliwe kufuata sifa (CV).

Mheshimiwa Naibu Spika, elimu ya viongozi katika ngazi zote Mwenyekiti, Madiwani, Wabunge, Rais ifahamike.

67

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la Muswada huu ni kuboresha demokrasia ya kweli. Ndani ya siasa umekuwa unadumazwa kwa sababu ya kuwekwa vipingamizi mbalimbali. Viongozi walipewa dhamana ya kusimamia wananchi, mfano wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Vituo vya Polisi wanatumia nafasi zao kukandamiza/kuonea wananchi wa vyama vya upinzani. Viongozi watendaji waache kushabikia siasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya vyombo vya dola kwenye chaguzi zetu nalo ni tatizo. Serikali kutumia vyombo vya moto, maji ya uchungu na kutumia polisi kuzunguka na bendera nyekundu mitaani kunajenga hofu kwa wananchi, wengine wanajificha/wanaogopa kupiga kura.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele kinachosema vyama vikiungana viongozi wake wanapoteza nafasi zao, hii ina nia ya kuondoa fursa kwa vyama vya upinzani kuungana pale wanapoona inafaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vyama vya siasa unaweza kuona umuhimu wa wao kuungana na hata kuunda chama kimoja kikubwa kwa lengo la kuwahudumia wananchi kwa karibu zaidi na watafanya hivyo kwa makubaliano ya wanachama wao. Ni kwa nini wapoteze nafasi zao za Ubunge, Udiwani, Urais wakati waliowachagua ndio wamewapa ridhaa ya kuungana? Huu ni uwoga kwamba vyama vya siasa vikiungana vitaweza kuangusha Chama Tawala, hiyo sheria/Muswada huu uondoe urasimu huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sheria iweke wazi kuwa viongozi wa Serikali wanahudumia wananchi wote na siyo wanachama wa chama Fulani, wasibague wananchi kwa itikadi za vyama vyao, kama wanashindwa kutimiza wajibu huo, basi waache kazi zao na waingie kwenye jukwaa la siasa.

MHE. RAJAB H. JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) kwa Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali kwa marekebisho haya ya sheria ya vyama vya siasa na hasa katika vifungu vifuatavyo; Kifungu cha 11(A)(1) ambacho kitaruhusu vyama vya siasa kuweza kuungana wakati wowote. Kwa mawazo yangu, marekebisho ya sheria hiyo yataongeza nguvu za vyama na hatimaye kuongeza upinzani. Aidha, kwa mabadiliko hayo kutaongeza upendo kati ya vyama vya siasa kuliko ule upendo uliopo sasa. Nakiunga mkono kifungu hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 11(b)(2) ambacho kitaweka sharti kwamba vyama vikiungana ni lazima viongozi wake wapoteze nyadhifa zao za vyama vikongwe. Umuhimu wa sharti la kifungu hicho ni kuondosa vurugu kwa kuungana ovyo ovyo bila ya nidhamu. Kama vyama vya siasa vitaungana bila ya sharti hilo, basi vyama vitaungana kiholela na sio kwa dhati.

68 Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ENG. STELLA MANYANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, napenda kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Philip S. Marmo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Uratibu na Bunge) kwa kuleta Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naungana nawe katika kuona umuhimu wa kurekebisha/kuongeza kifungu cha nne kwani hali ya kuungana na kuendelea kushika uongozi katika Bunge ni kuleta vurugu kwani ninashuhudia mambo yaliyojitokeza katika nchi za jirani zetu, mfano Malawi ambako Rais wake alivuka na kuhamia chama kingine pia Wabunge walikuwa wakinunuliwa na kuvuka kuhamia maeneo mengine (vyama vingine). Hilo ni tatizo kubwa, kwani ilisababisha hata usumbufu katika kupitisha bajeti ya Malawi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimeshuhudia tatizo hilo katika uchaguzi wa Lesotho jinsi Waziri alivyoamua kuvuka kipindi kifupi kabla ya uchaguzi, bahati nzuri kwa kuwa Katiba yao iliruhusu kuwa na uchaguzi wa kushtukiza, waliamua kufanya uchaguzi. Hali hiyo sio ya afya katika amani ya nchi.

Mheshimimiwa Naibu Spika, nakubaliana na kupangwa mahesabu ya vyama kwa kumtumia mkaguzi wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba, tumeshuhudia sasa hivi pesa za wahisani zote zinawekwa kwenye mfuko wa pamoja, inakuwaje vyama vingine vinapata msaada wa moja kwa moja tofauti ya takwimu na hiyo ya kutoka nje ni nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la umuhimu wa kuwa na elimu ya kutosha angalau elimu ya msingi ni muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muswada huu ni mdogo tu, basi uwekwe pia kwa Kiswahili ili watu wengi waweze kutumia sheria hii.

MHE. BUJIKU P. SAKILA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa niaba ya Serikali kuleta Muswada huu Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la msingi la Muswada huu ni kuanzisha ofisi huru ya msajili wa vyama vya siasa. Jambo hili ni muhimu sana kwa vile vyama vya siasa ni kama timu ambayo ina sea yake. Kwa vile timu hizi ni nyingi, ili ziweze kufanya shughuli zake bila vurugu, basi mratibu huru wa timu hizi ni muhimu, hapa ndipo umuhimu sasa wa ofisi hii ya mratibu/msajili wa vyama inapohitajika. Hatua ya wazo hili ninaipongeza sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninayo machache ya kuzungumzia; uhuru wa ofisi. Ninachoomba, mipaka ya ofisi hii na Wizara iwe wazi na muhimu ajulikane nani

69 mwenye uamuzi wa mwisho msajili na Waziri mwenye dhamana na ofisi hii wasipoelewa kutokana na mvuto wa kisiasa! Katika utekelezaji wa ofisi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele cha saba cha Muswada kuhusiana na 10 (a) ni vyema sasa tuwe jasiri katika maamuzi. Uongozi ni dhamana kubwa. Hivi sasa tumeanzisha shule za sekondari kila kata! Za nini? Tunaanzisha shule za sekondari kwa kata tano mpaka sita kwa kila tarafa, za nini? Ni vyema tuseme na kuamua kwa dhati kuwa uongozi ngazi za kitongoji na vijiji unaweza kuombwa na waliohitimu elimu ya msingi; ngazi za Kata elimu isiyo chini ya kiwango cha elimu vya kidato cha nne na ngazi za Tarafa Chuo Kikuu au angalau stashahada fulani. Tusioneane aibu, tutaliangamiza Taifa. Kusoma, kuandika na kuongea Kiswahili havitoshi kabisa kwa sasa. Uhalali wa wagombea kuwapa kitambulisho, cheti cha kuzaliwa au pasipoti viongezwe katika vigezo vya waombaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kifungu 8 11 D 1 – 3, Tanzania hii tunayo heshima kubwa inayotokana na upendo na kuheshimiana kati ya mtu na mtu. Vipengele hivyo navipongeza sana. Tukiheshimiana na Mwenyezi Mungu ataendelea kutubariki sisi watoto wetu na nchi yetu. Hivyo matusi na maneno machafu yasizuiwe tu kwa bendera ya vyama na mimi ninaunga mkono. Kingine, sheria na adhabu ziwe kali na za kuchukuliwa kwa muda mfupi kwa atendaye makosa hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kifungu cha 9, 12 b(2) matumizi ya strike off, strike off na strike off from yanaweza kuwa na athari zipi kimantiki za kisheria katika sehemu hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, ukaguzi wa fedha za chama kukaguliwa na Mdhibiti wa Serikali, naipongeza sana. Fedha hii ni mali ya umma. Mapato na Matumizi yakidhibitiwa vizuri, matumizi yatakuwa ni kwa maendeleo ya vyama husika na wanachama wake na nchi kwa jumla. Aidha, matumizi ya fedha kupitia ofisi ya chama cha siasa yangeimarishwa na kuungwa mkono zaidi kuliko kumwachia mgombea kutumia fedha zake bila udhibiti wowote wakati wa uchaguzi. Hii ni kwa sababu jambo hili linaimarisha rushwa zaidi ndani na nje ya chama wakati na kabla ya kampeni! Kuunganisha vyama, taratibu zinazowekwa ni muhimu na binafsi ninaziunga mkono.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Baraza, ni jambo jema sana kukawa na Baraza linalokusudiwa, haja yangu ni moja tu, Baraza hili ili lisifungane na upande wa chama kimoja cha siasa ni nani atakayeliondoa katika matatizo hayo? Hivyo, jopo la usuluhishi nje ya Baraza linahitaji kuanzishwa pia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na ninaunga mkono hoja.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, walioomba kuchangia Muswada huu, wote wameshachangia. Kama nilivyosema. Hapa kuna amendments tatu za Wabunge; zipo mbili zilizoletwa kwa maandishi kwa mujibu wa taratibu zetu na ipo ya Serikali. Kwa hiyo, tutakapofika mchana wakati wa Bunge kukaa kama Kamati ya Bunge Zima, Mbunge anayehusika na hoja hii atasimama na kuwasilisha mabadiliko anayotaka

70 kufanya. Atapewa dakika tano, kufanya kazi ya kuwasilisha mabadiliko yake kwa maelezo. Ataungwa mkono na watu kwa kusimama kama kumi hivi, wanaweza pia kusaidia kujadili ile hoja aliyoileta ya mabadiliko, watapata dakika tatu kila mmoja. Tutapiga kura kama tunakubaliana na mabadiliko hayo, kama kura hiyo itakubali mabadiliko basi hoja ya Serikali pale inakufa.

Kwa hiyo, badala yake, inakuwa hoja ya yule Mheshimiwa aliyeleta, kama tutapiga kura ikaonekana kwamba sisi hatujakubali mabadiliko aliyoyaleta Mbunge mwenzetu hapa, basi ile ya kwake inatupwa, tunaendelea na ile iliyokuwa ya Serikali. Kwa hiyo, napenda kila makundi yajiandae kujaribu kutushawishi sisi tukubaliane na wao kwa hoja, siyo kwa ushabiki au kwa kitu kingine chochote ili maandalizi yawe mazuri.

Waheshimiwa Wabunge, hapa Mezani sina kazi nyingine kwa sasa na muda uliobaki ni mzuri kwa upande wa Serikali kwenda kupitia mabadiliko yote yaliyoletwa na Wabunge na yale ya Serikali yenyewe. Kwa kuwa Serikali yenyewe itapata muda pia wa kutoa maelezo kwa ile hoja ya mabadiliko ya Mbunge aliyeleta, kwa hiyo, tutapiga kura na tutaamua. Naomba Serikali mkajiandae na wanaohusika wajiandae.

Waheshimiwa Wabunge, nasitisha Shughuli za Bunge mpaka saa kumi na moja jioni.

(Saa 06.40 mchana Bunge lilifungwa Mpaka saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mara nyingine naomba nikushukuru tena kwa kunipa fursa hii ili niweze kuhitimisha hoja iliyo mbele yetu. Kabla ya kufanya hivyo, napenda kuwashukuru Wabunge 10 waliochangia kwa kuzungumza hapa Bungeni na Wabunge 12 waliochangia hoja yetu kwa maandishi.

Naanza kwa kuwatambua wale ambao walichangia kwa kuzungumza. Kwanza ni Mheshimiwa Steven Galinoma – kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Halima Mdee - Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Zitto Kabwe - Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mheshimiwa Juma Killimbah - Mbunge wa Iramba Magharibi, Mheshimiwa William Shellukindo - Mbunge wa Bumbuli, Mheshimiwa John M. Cheyo - Mbunge wa Bariadi Magharibi, Mheshimiwa Ruth Msafiri - Mbunge Muleba Kaskazini, Mheshimiwa Raphael Masunga Chegeni - Mbunge wa Busega, Mheshimiwa Rosemary Kirigini - Mbunge Viti Maalum na Mbunge Ponsiano D. Nyami - Mbunge wa Nkasi. (Makofi)

Wabunge waliochangia kwa maandishi ni wafuatao:- kwanza ni Mheshimiwa Fatma Mikidadi - Viti Maalum, Mheshimiwa Alyoce Kimaro - Mbunge wa Vunjo, Mheshimiwa Siraju J. Kaboyonga - Mbunge wa Tabora, Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya - Viti Maalum, Mheshimiwa Savelina Mwijage - Viti Maalum, Mheshimiwa

71 Bujiku Sakila - Mbunge wa Kwimba, Mheshimiwa Ali Ameir Ali - Mbunge wa Fuoni, Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya - Mbunge viti Maalum, Mheshimiwa Charles Mwera - Mbunge wa Tarime, Mheshimiwa Magdalena Sakaya - Mbunge Viti Maalum, Mheshimiwa Rajab Hamad Juma - Mbunge wa Tumbatu na Mheshimiwa Lucy F. Owenya - Viti Maalum. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijatoa ufafanuzi kuhusu hoja nyingi za Wabunge hawa waliochangia kwa kuongea na wengine kwa kuandika, naomba unipe fursa ya kusema machache kuhusu sheria hii hasa baada ya kusikia hotuba za kutia uchungu zilizotolewa na baadhi ya Wabunge, hasa Wabunge wanawake na hasa Mheshimiwa Ruth Msafiri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ikumbukwe kwamba wakati tunatunga sheria hii mwaka 1992 hakuna aliyekuwa akitabiri tabia ya wanasiasa wa Kitanzania kuwa itabadilika sana kwa kiwango ambacho tunakiona sasa. Utakumbuka mwenyewe kwamba wakati ule tulipokuwa tunasimama mbele ya wananchi kuomba kura, unamalizia kwa kusema kwamba ndugu wananchi mkiniona mimi ninafaa naomba mnichague, iwapo mtaona mwenzangu anafaa tafadhali nawaomba mchagueni. Ndiyo ilivyokuwa.

Wakati tukitunga sheria, tulidhani kwamba tabia hiyo nzuri ya kuomba mamlaka kutoka kwa wananchi ingeendelea. Baada ya vyama vingi kuanza na kuona kwamba kuna mwanya katika sheria ndiyo hii hali ya lugha chafu ilianza kutumika hadi ilifika mwaka wa 2004 Tume ya Uchaguzi ilipowaita Makatibu wa vyama vyote ili wakubaliane juu ya maadili mema ya uendeshaji wa uchaguzi.

Maadili yale yaliandikwa na vyama vyote vikaridhia wakaviwekea sahihi, lakini kwa bahati mbaya kwa asilimia kubwa kanuni hizo za maadili hazikuzingatiwa katika chaguzi zilizofuatia.

Ndiyo maana ilipofika mwaka 2007, Serikali iliona pengine kanuni za maadili za hiari sasa zingeandikwa katika Gazeti la Serikali ili kuongeza kidogo nguvu lakini bila kuwa na adhabu, tukidhani kwamba viongozi hawa wanaogombea ni watu wazima na wanakuwa waangalifu katika kuchagua lugha wakati wa kuomba kura. Ningependa kukumbusha, kwa sababu hata baada ya kanuni hizi kuchapishwa katika gazeti la Serikali na kukawa na chaguzi kama kule Tarime na Mbeya Vijijini bado hali haikuwa inaridhisha. (Makofi)

Madhumuni ya kuwa na sheria hii sasa ni kufanya kanuni hizi ambazo zilikuwa kanuni ya maadili ya hiari sasa iwe na nguvu za kisheria. Kwa manufaa ya Waheshimiwa Wabunge, naomba niwasomee sehemu chache tu ya kanuni hizi ambazo zilikuwa za hiari na sasa zitakuwa na nguvu za kisheria.

Ni kwamba kila Chama kitaelezea maadili kwa wanachama wake ili kuongeza uadilifu wa kisiasa ndani na nje ya chama cha siasa; pili, kulaani, kuepuka na kuchukua hatua zitazofaa ili kuzuia au kuepuka vitendo vya vurugu, uvunjaji wa amani au ukandamizaji wa aina yoyote; kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni ya uongo

72 kuhusu mtu yeyote ama chama cha siasa chochote; kulaani na kupinga kabisa vitendo vyenye kuashiria ukandamizaji, matumizi ya lugha ya matusi, vitendo vya kibabe na vurugu, matumizi ya nguvu ili kujipatia umaarufu wa chama au sababu yoyote ile; kuepuka kushawishi kwa kutoa rushwa kama cheo ili kupata upendeleo au heshima kwa nia ya kufanikisha malengo, kuepuka kutumia mamlaka, rasilimali za Serikali, vyombo vya dola na wadhifa wa Serikali, kisiasa au ufadhili wa nje ama wa ndani kwa namna yoyote ili kukandamiza chama kingine wakati wa uchaguzi; kuepuka vitendo vya ubaguzi wa rika, kabila, jinsia, dini na mahali alipozaliwa mtu yeyote ikiwa ni jamii au asili fulani kwa kufanikisha malengo ya kisiasa wakati wa uchaguzi. Mwisho, kuheshimu maamuzi halali yaliyofanywa kwa pamoja na vyama vyote.

Sasa kama nilivyosema pale awali, kanuni hizi zilibuniwa na vyama vya siasa vyote vilivyosajiliwa rasmi, vyama vyote vikakubaliana kwamba wagombea wao watazingatia kanuni hizi, lakini haikuwa hivyo na ndiyo maana tumeleta Muswada huu. Kwa maana hiyo, kwa kweli huu ni Muswada mzuri sana ambao utasaidia kurejesha heshima katika kuendesha shughuli za siasa katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hivyo niende kwenye michango ya Waheshimiwa Wabunge. Michango yote iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge, ni mizuri sana na imeunga mkono hoja na nina imani kwamba itaidia sana kuboresha Muswada ulio mbele yetu. Hata hivyo napenda kutoa maelezo ya ufafanuzi kwa hoja mbalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge, kama ifuatavyo:-

Kwanza, Mheshimiwa Steven Galinoma Mbunge, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ametoa mapendekezo kadhaa ya marekebisho katika Muswada huu. Napenda kuliarifu Bunge hili kwamba hoja zote za mapendekezo zimepokelewa na kuzingatiwa katika jedwali la ziada la marekebisho lililosambazwa kwa Waheshimiwa Wabunge; pili, maelezo ya baadhi ya Wabunge ambao wametoa hoja kwa kuungana kwa vyama, haina mantiki kwani itagharimu sana vyama vinavyohusika na Serikali.

Napenda kutoa maelezo hapa pendekezo hili la vyama kuungana wakati wowote kwa kweli lina manufaa makubwa kwani vyama vitaweza kufanya maandalizi iwapo vitapenda kujiunga na vitamwezesha Mkurugenzi wa Uchaguzi kuandaa nyaraka zinazohitajika. Aidha, itawezesha vyama husika kufanya vikao mbalimbali vya chama na hata wanachama katika maamuzi ya kuunganisha vyama vyao. Tukumbuke kwamba vyama hivi sio mali ya viongozi, vyama ni mali ya wanachama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vyama vinapoungana, ina maana kuwa kila kimoja kimekufa na hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2005 Ibara ya 71(f) inayoelekeza kuwa kiongozi wa kisiasa atapatikana kupitia chama cha siasa. Aidha, sheria ya Uchaguzi pia inatoa masharti ya viongozi hao kutoendelea kuwa viongozi kwa kuwa vyama vyao vimekufa. Hoja ya kutangaza mapato na matumizi kila baada miezi minne kwenye vyombo vya habari vya ndani, sio kwenye gazeti la Serikali imepokelewa na inafanyiwa kazi.

73 Adhabu iliyopendekezwa kwa mtu anayejitambulisha kama kiongozi wa chama na kufanya shughuli za chama ni kosa kubwa. Lengo la Muswada huu limelenga katika kurekebisha tabia ya watu na siyo kuadhibu, kwa kuwa kosa hili kwa taathiri yake sio kosa la jinai hasa. Hoja ya sifa ya kiongozi wa kisiasa kujua kusoma na kuandika kuwa haitoshi ni ya kweli. Hata hivyo, hoja hii inahusisha masharti yaliyomo kwenye katiba ya nchi yetu kwa vile Katiba haijabadilishwa siyo muafaka kwa sasa kuongelea marekebisho yake.

Hoja ya Baraza la Ushauri la Vyama vya Siasa kuwa na idadi ya uwiano wa wajumbe kuhusu utaratibu wa kumpata Mwenyekiti wakati hayupo na Makamu pia hayupo mapendekezo ya Muswada yanaelekeza kuwepo kanuni zitakazoeleza jinsi wajumbe watakavyomteua Mwenyekiti wa muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya matumizi ya lugha chafu na zisizofaa katika siasa imeungwa mkono na Waheshimiwa Wabunge wengi na kama nilivyosema, zamani tulikuwa na maadili ya hiari, baadaye tukaandika kwenye Gazeti la Serikali, lakini bado lugha inatumika. Tunashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa kulaani sana tabia hii. Kwa ujumla hoja zote zinazohusu utalaam wa kisheria zimepokelewa na zinafanyiwa kazi na Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Mheshimiwa Kabwe Zitto, ametoa hoja ya msingi ya mgawanyo wa fedha za ruzuku. Kimsingi wazo lake ni zuri tumelipokea, lakini kwa vile hoja hii inaelekea kwenye sera zaidi, basi atupe muda tuifanyie kazi. (Makofi)

Mwisho, samahani, nilikuwa nimesahau kumtaja Mheshimiwa Profesa Raphael Mwalyosi, naye alikuwa amechangia hoja yetu hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kutoa maelezo hayo, sasa naomba kutoa hoja. Ahsante.

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Muswada wa Sheria ya Serikali Ulisomwa Mara ya Pili)

KAMATI YA BUNGE YA ZIMA

Muswada wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2008 [The Political Parties (Amendment) Bill, 2008]

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama nilivyowakumbusha asubuhi, tumepata faida ya kuwa na amendments za Serikali halafu na amendments za

74 Waheshimiwa Wabunge. Kwa hiyo, amendments za Waheshimiwa Wabunge ziko za aina mbili.

Kwa hiyo, tutakapofika kifungu ambacho Mbunge amefanya amendment nitamwita yule Mbunge ambaye ameleta amendments, atasimama kwa muda wa dakika tano, ataeleza yale anayofikiria, anapenda tufanye amendment kwenye vifungu vile vilivyotolewa. Ataungwa mkono kwa kusimama Wabunge wasiopungua 10, baada ya hapo akishatoa hiyo amendment ataungwa mkono na wale Wabunge 10, halafu wale wanaweza kujadili mtu. Mbunge mwingine anaweza kujadili ile amendment ya Mheshimiwa Mbunge na muda wake ni dakika tatu.

Mwenye hoja atapewa dakika tano, wengine watakaomuunga mkono au kumpinga watapewa dakika tatu. Watachangia wote wanaotaka kuchangia hiyo hoja kwa kuunga au kwa kupinga hoja zile halafu anaachiwa, anaitwa mtoa hoja ambaye ni Waziri wa Serikali, naye atatoa ufafanuzi kwa yale yote yaliyotokea, halafu inarudi tena kwa yule aliyetoa hoja. Nadhani tuko wote.

Narudia tena kwamba, tutakapofika kifungu kile cha amendment Mbunge atasimama na kusema naomba kutoa hoja kuhusu kitu kama hicho na atajielekeza. Atakapojieleza ataungwa kwa kusimama Wabunge. Halafu yeye anatumia dakika tano, wale watakaotaka kuchangia ile amendment ya Mheshimiwa Mbunge, watapewa dakika tatu, halafu Waziri aliyetoa hoja atajibu zile hoja. Akishajibu tunamrudisha mwenye hoja ambaye ni Mbunge ndiyo anayemaliza mazungumzo. Sasa ikibidi kama yule mtoa hoja amekubaliana na maelezo ya Serikali, atasema basi naondoa hoja yangu. Kama haondoi, basi itabidi niwahoji. Ikiwezekana kuwahoji ikaonekana hoja ya Mbunge imeshinda, basi kifungu kile cha Serikali kinatoka. Kama itakuwa hoja ya Mbunge imeshindwa, basi ile ya Serikali inaendelea. Kwa hiyo, naomba mzingatie hilo.

Ibara ya 1

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 2

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 3

MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri, tumefanya mawasiliano ku-harmonize na Waziri na inaelekea yale marekebisho niliyotaka kuyaweka katika ile sub-section one yamekubalika pale kwa kuweka ile office of the registrar to have political parties badala ya political parties.

75 Sasa kuna lile suala la autonomy. Nilipendekeza kuwa na kifungu kidogo cha 2(2) ambacho inaweka mwongozo wa kutumia ile autonomy na nikaorodhesha maeneo ambayo hapana budi registrar afanye consultation na Waziri anayehusika na kuondoa lile neno la kusema which institution under the minister responsible for political parties.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo tu katika section hii ndiyo ambayo nilikuwa napenda tuyatazame, yale maeneo ya consultations autonomy inakuwepo, lakini ile ya kusema under the minister iondoke ili tubakie na yale majukumu ambayo lazima yafanyiwe consultations.

MWENYEKITI: Huyu hakutoa hoja hapa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, wazo la Mheshimiwa Mbunge ni zuri, lakini kwa maoni yetu, tofauti ni lugha tu. Katika hali halisi ndivyo hali ilivyo. Tunaona construction hii ni bora zaidi kwa sababu katika hali halisi, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni autonomous, ni ofisi huru. Kama utakumbuka, hata fedha zake Waziri anakuja kuziomba tu hapa wala haipitii katika Ofisi ya Waziri Mkuu, inakwenda moja kwa moja.

Busara ni kwamba ofisi hii inahudumia vyama vyote na isiegemee upande wowote na ndiyo maana tumetumia lugha hii. Lugha ya Mheshimiwa Mbunge, inatupa shida kidogo kwa sababu ni kama kuegemea kunaongezeka wakati hakuna kuegemeana katika utendaji wa kazi wa kila siku ukiacha kuleta maombi ya fedha hapa na kutengeneza regulations.

Kwa hiyo, tungeomba sana Mheshimiwa Mbunge, atuelewe hivyo. Malengo yanafanana, ni kama lugha inatofautiana. Malengo ya Ofisi ya Msajili kuwa autonomous tunakubaliana wote ni suala la lugha na kwa upande wa kuchagua lugha sisi tumechagua lugha hii zaidi tukidhani inatekeleza malengo yetu.

MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, asubuhi nilisema, mimi niliwahi kufanya hii wakati ofisi haijafunguliwa. Niliona umuhimu wa kuweka baadhi ya mambo wazi kwa mfano katika suala la kufuta chama cha siasa, hivi Waziri anayesimamia suala hilo angeona kwamba ni vizuri wakafanya consultation pengine kuna suala kuliko kuliacha wazi ile autonomy, maana autonomy ukiacha pale juu haina mahali ambapo imeongozwa , hilo ni moja.

Lingine, hata mabadiliko katika political leadership hii consultation ni kwamba at least Waziri awe na nafasi ya kuelewa ni nini kinafanyika. Haiwezi kuwa chini yake, maana yake ni katika masuala haya makubwa tu kwa mfano budget framework, halafu changes katika subsides kama zimeongezeka na kufuta vitu kama hivyo. Sasa mimi nimeona labda itazamwe vizuri, wakati mwingine Serikali ikubali baadhi ya maendeleo haya kama ni improvement kuliko kubaki hii sheria ilivyokuwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nasema, nilihusika kwenye sheria, wakati ule hatuna experience. Kwa hiyo, umeacha tu. Kuna baadhi ya mambo ambayo yalikuwa

76 yanaleta matatizo, mimi nilikuwa pale toka mwaka 1992 mpaka 1995 wakati tumekwenda kwenye uchaguzi na kuunda ofisi ya registrar. Lakini kama wenyewe wanaona inaweza kufanya kukaa hivyo, basi mimi sina hoja. Lakini nilikuwa nimetoa hoja hii kwa Waheshimiwa wenzangu Wabunge, labda wana mchango nao wangeweza kuchangia katika hiyo.

MWENYEKITI: Lakini hujaleta hoja ni ufafanuzi tu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa kabisa. Kama nilivyosema awali, tunakubaliana na Mheshimiwa Mbunge. Haya anayosema sisi tuliyaona mapema sana na ndiyo maana tumeona sasa tuunde chombo kinachoitwa Political Parties Council.

Kazi anayosema Mheshimiwa Mbunge, inaweza ikafanywa kwa sehemu kubwa na Political Parties Council kwa maoni yetu. Lakini kama anadhani pia haitoshelezi hivyo kwa sababu Political Parties Council baadaye maoni yake yakiratibiwa na Msajili, kwa vyovyote vile yatamfikia Waziri. Waziri atakuwa na uhakika kwamba haya sasa ni maoni ya vyama vyote.

Kwa hiyo, atakuwa akitekeleza majukumu yake tu ya kawaida ya kisheria kama kuna by laws zinataka kutengenezwa au kama kuna mahitaji ya fedha zaidi haya ndiyo mambo mawili hasa ambayo yanatakiwa yatekelezwe na Waziri. Lakini haya mambo mengine anayosemea Mheshimiwa Shellukindo nadhani yangekuwa taken care na hii ibara mpya ya 21 (b) ambayo kwa sasa inaunda Baraza la Vyama vya Siasa.

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 4 Ibara ya 5

(Ibara zilizotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 6

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 7

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na marekebisho yake)

Ibara ya 8

77 MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunachangia kuhusiana na kifungu hiki na hasa schedule of amendment ambayo Serikali imeileta niliomba Serikali itoe tafsiri ya political leaders kwenye Muswada huu. Lakini bahati mbaya labda Mheshimiwa Waziri ameelezea, ningependa nipate maana sijaona schedule of amendment mpya kama ina definition ya what do you mean by having these words all political leaders.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Tulikubaliana na pendekezo lake, ni bahati mbaya tu Mwandishi Mkuu wa Sheria ndiyo anaandaa tafsiri hiyo anayosema Mheshimiwa Mbunge. Badiliko hili limeanza kufanyiwa kazi baada ya Mheshimiwa Zitto kuongea hapa Bungeni na baada ya watalaam wetu kukaa chini na kuliafiki. Kwa sasa hivi linaandaliwa pengine wakati wowote kuanzia sasa Waheshimiwa Wabunge wanaweza wakapata nakala ya tafsiri ya political leader.

MWENYEKITI: Kwa hiyo, kwa msingi mnakubaliana na mawazo aliyotoa Mheshimiwa Zitto wakati wa hoja yake.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, Hansard pia ni maelekezo kwa drafters, Mheshimiwa Waziri aseme hiyo tafsiri ili iwe recorded kwamba tafsiri ni hii. Kwa sababu nilichokiomba mimi ni tafsiri, sasa akisema tu kwamba amekubali, lakini hajaisema hiyo tafsiri itatuletea matatizo sana hapo baadaye tutakapoipitisha hii sheria.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, UTARATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri mimi ni mwandishi wa sheria kwa profession na nimeandika sheria kwa miaka nane na nimekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 20, lakini siwezi kuwa na construction ya hapa moja kwa moja, isipokuwa kwa lugha ya kawaida viongozi wanaanza kwenye ngazi ya chini kwa upande wa vyama.

Kwa mfano kama ni CCM, kuanzia Balozi, Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kata, Mwenyekiti wa Wilaya na Mwenyekiti wa Taifa. Kwa upande wa Serikali; Mwenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Kijiji mpaka wakuu wa nchi, lakini lugha ya kuweka pendekezo hili itakuwa ni lugha ya kisheria, inafanyiwa kazi na Mwandishi wa sheria. (Makofi)

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa msingi huo hakuna sababu ya kwanini ile application ya walivyokuwa wamesema mwanzoni kwamba viongozi hawa na wenyewe wata-cease isi-apply kama definition ni pana kiasi ambacho Mheshimiwa Waziri anafikiria. Ndio maana wakati tunazungumza hilo, nilisema kuwa labda kama njia ya ku-cure hii ambiguity ingesemwa wazi kabisa kwamba wanachama wale ambao wamo katika vyama ambavyo vinaungana watakuwa assumed immediately, hiyo signature ikiwekwa kwamba wanakuwa wanachama wa kile chama kipya bila kupoteza uanachama wao. Hili lilifanyika wakati tulipoanza vyama vya siasa kwamba tungesema CCM nayo iandikishwe upya, ndio kusema lisingekuwepo Bunge na pasingekuwa na Rais kama unafuata Katiba iliyopo kwa sasa. Kwa hiyo, ile definition

78 yake ilinipa wasiwasi na kama tukipitisha huu Muswada, kusema kweli tutakuwa tumerudi tu kwenye original. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa, tunacho-debate hapa ni ambiguity labda inayosemekana katika amendment ya Serikali ile (b)(1). The Political Parties merged in accordance with the provision of Section 11 (a )”… shall with effect from the date of registration of new Political Party cease to exist and all Political Leaders elected, appointed or nominated before the merger of such Political Parties shall vacate their positions. Alichouliza huyu ni Political Leader.” What is the ambiguity? Mheshimiwa Waziri, tunaweza kuimaliza hiyo kwa haraka sana!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – SERA, UTARATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema sasa tumekubali kuwa na tafsiri mpya ya Political Leader.

MWENYEKITI: Sio mpya, yaani katika hapa, sio mpya.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – SERA, UTARATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, itaingia katika schedule of amendments baadaye na hii itakuwa kwenye Hansard. Lakini kwa kutoa maelezo zaidi kuhusu suala hili, vyama viwili vimeungana, vilikuwa na viongozi; tuseme CCM imeungana na CUF, huyu alikuwa ni kiongozi wa Tawi la CUF na tawi hilo hilo CCM, sasa itakuwaje? Si lazima kuwe na uchaguzi? Kwa sababu chama hiki kilichoundwa ni kipya, kwa hiyo, ni lazima kuwa na viongozi wapya na kutakuwa na wanachama wenye kadi mpya. (Makofi)

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kuna masuala mawili. Kuna suala la viongozi wa ndani ya chama kwa mfano, Tawi la Mwandiga Mwenyekiti wa CHADEMA na Mwenyekiti wa CUF. CHADEMA na CUF zimeungana hawa automatically nafasi zao wanazipoteza kwa sababu ni lazima kile chama kichague viongozi wapya.

Hoja tunayoizungumza sisi ni katika Kijiji cha Mwandiga kuna Mwenyekiti wa Kijiji. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji kile ni wa CHADEMA. Sasa CHADEMA na CUF wameungana, huyu Mwenyekiti wa hiki Kijiji au Diwani wa Kata hiyo ya Mwandiga au Mbunge wa Kigoma Kaskazini sababu amechaguliwa na watu tofauti asipoteze na ndio kama jinsi alivyosema Mzee Cheyo, kwamba ndio maana wakati tunatunga Sheria ya Vyama vya Siasa tuliweka special provision kwamba Chama Cha Mapinduzi kisiandikishwe upya kwa sababu kingeandikishwa upya tungepoteza Bunge, tungepoteza Rais, tungepoteza everything kwa sababu ingewataka CCM waanze process upya kama Chama kingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana kwenye Kamati, nimemwambia Mheshimiwa Waziri, mwaka 1977 wakati Chama cha Mapinduzi kinazaliwa, wakati ASP na TANU zinaungana, Wabunge waliokuwepo kwenye Bunge hawakupoteza nafasi zao wakati Chama kipya kiliundwa.

79 Sasa tunakuwa na standard za namna gani? Tunakuwa na standard za miaka ile kwa ajili ya kui-favour CCM na standard za sasa kwa ajili ya kuwa, this is the point. Kwa hiyo, tunaomba tafsiri itakayoonyesha kwamba Political Leaders ni wale viongozi wa ndani ya Chama, haihusishi Viongozi wa Dola. (Makofi)

MWENYEKITI: Lakini mfano wa mwaka 1977, wewe huoni kama sio wenyewe kabisa! (Makofi/Kicheko)

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi inaongozwa kwa historia yake. Tunajifunza kutokana na historia ya nchi na kitendo kile cha ASP na TANU kuungana ni kitendo kizuri kwenye historia yetu, kiliimarisha muungano. Kwa hiyo, tunajifunza kutokana na hicho na tunaomba sasa busara ile ile iliyotumika itumike na sasa. (Makofi)

MWENYEKITI: Hakuna busara. Mheshimiwa Waziri na Waheshimiwa Wabunge, hakuna hoja hapa, ni debate tu.

Haya Mheshimiwa Lucy unataka kusemaje? Samahani Mheshimiwa Lucy, nilikwishamwita Mheshimiwa Cheyo, nimesahau. Mheshimiwa Cheyo, tafadhali.

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo sio debate, tunachotaka ni nia na makusudi mazima. Ni kwamba, Vyama vyovyote vile na wala sio Vyama vya Upinzani, vikiamua ku-merge, sheria hii inasema nini kwa viongozi wa kisiasa ambao ni Madiwani, Wenyeviti, Wabunge na Rais?

Sisi tunasema sheria inaweza tu ikamaliza hili jambo kama ikitoa tafsiri ya Political Leaders. Tujue limitation yake mpaka hapa, ikiwepo pale moja kwa moja basi utaona kwamba kwa mfano, inawezekana Political Leaders ni wale tu ambao wamechaguliwa ndani ya Chama au Vyama mbalimbali ndio maana yake hapa. Fine, itakuwa imewa-exclude na sheria inaweza kuendelea ikasema excluding the leaders ambao wamechaguliwa kwa utaratibu wa uchaguzi wa dola, ambao ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uchaguzi wa Bunge na uchaguzi wa Rais. Something like that inakuwa clear, kila mmoja anapiga kura kwamba tumetunga sheria ambayo inasaidia hivi vyama kuweza ku-merge. (Makofi)

MWENYEKITI: Naomba nimwite Mheshimiwa Waziri, kwa sababu hakuna hoja iliyotolewa, ni ufafanuzi tu. Haya tuendelee Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – SERA, UTARATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, laiti ubishi huu ungelikuwa unahusu sera, lakini kwa bahati mbaya sana ubishi huu hauhusu sera ni sheria ambazo tumezipitisha katika Bunge hili.

Nianze na Mbunge. Katiba wala sio ambiguous, iko wazi. Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafutayo, (a), (b), (c), (d), unafika (f). Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama wa Chama

80 alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge; ubishi uko wapi hapo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Uchaguzi kwa upande wa Serikali za Mitaa nayo inasema hivi hivi. Ndio maana nilikuwa nasema, laiti ubishi ungelikuwa ni wa Sera, ubishi huu ni sheria na sheria iko wazi na hatuwezi tukabadilisha Katiba kwa kutumia sheria hii. Wenzangu kama hawataki hali hii ya sasa waanzishe mchakato wa kubadilisha Katiba ili mawazo yao yawe accommodated. Kwa sasa sisi tunaongozwa na Katiba hii na tumeapa Katiba hii na ndio maana tuko hapa. (Makofi)

MWENYEKITI: Hamna hoja yoyote iliyoletwa kwa suala hili, ilikuwa ni majadiliano na ufafanuzi umetolewa na ufafanuzi wa Katiba umetolewa. Kwa hiyo, nawaombeni tusiendelee na ubishi katika hili, mngeleta hoja tungepiga kura, hamkuleta hoja kwa hili. Kifungu hiki kinaafikiwa? (Makofi)

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 9

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 10

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeleta schedule of amendments kuhusiana na utaratibu wa ugawaji wa ruzuku ambao Mheshimiwa Waziri, amekubali kwamba ni wazo zuri, lakini tu amesema ni wazo la kisera. Tunafahamu implications za mawazo ya kisera, kwa hiyo, nilikuwa naomba tu commitment ya Mheshimiwa Waziri kwamba wazo hili litafanyiwa utekelezaji kwa time frame ipi?

MWENYEKITI: Halafu Mheshimiwa Zitto, umeleta karatasi mbili. Ni ipi unataka tuitumie sisi?

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapana nadhani hiyo nyingine imekuja kimakosa, hii ndio ambayo imefanyiwa kazi na Ofisi ya Sheria ya Bunge.

(Hapa Mheshimiwa Kabwe Z. Zitto, Alionyesha Karatasi)

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ambayo ilikuja asubuhi ambayo ni ndefu. Hii nyingine mimi mwenyewe nimeshangaa imefikaje kwa sababu tuliifanyia marekebisho kwa Ofisi ya Mwanasheria wa Bunge.

MWENYEKITI: Kwa hiyo, Mheshimiwa Zitto hujatoa hoja unataka maelezo tu.

81

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa nimeomba commitment ya Mheshimiwa Waziri, kuhusiana na hili. Kufuatana na maelezo yake ndio tutaona kama nitatoa hoja ama sitatoa hoja.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, UTARATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri tu ni kwamba sisi Watanzania tunaheshimiana sana na ni waungwana kwelikweli.

Katika hali halisi Muswada wa Fedha, maswali yote yanayohusu fedha hayaletwi kwa utaratibu wa hoja binafsi. Lakini kwasababu ni jambo zuri, tulishaeleza kwamba tumelichukua na tutalifanyia kazi Serikalini. Nami ninaahidi kwamba tutalifanyia kazi Serikalini. Lakini kama ni utaratibu wa Kawaida mpaka kufikia kupiga kura isingewezekana kwasababu hili ni suala linalohusu fedha.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni sawa.

(Ibara iliyotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake) Ibara ya 11

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

Ibara ya 12

MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumewasiliana na Mheshimiwa Waziri, nimeridhika kwamba wamechukua maoni yangu, lakini wameandika kwa lugha tofauti. Hicho ndicho kitu ambacho tunatofautiana na kwa kuwa lugha ni ya kwao; kwasababu mimi niliona kuacha jumla tu bila kusema ni viongozi wangapi, niliandika Chairmen na National Secretary. Wao wamesema two National Members halafu kwenye U-Chairmen tumesema wachague Chairmen from among the National Leaders walioko pale.

Hapa vilevile wameichukua isipokuwa wameiacha tu wazi, nadhani labda itazingatiwa kwenye kanuni kwamba ni kwa muda gani. Mimi kule nilisema ni yearly rotation basis kwahiyo, sina hoja zaidi ya hili; yamezingatiwa.

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)

Ibara ya 13

(Ibara iliyotajwa hapo juu ilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)

82

Ibara ya 14

(Ibara ziliyotajwa hapo juu zilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

Muswada wa Sheria ya Kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2008 (The Political Parties (Amendment) Bill, 2008)

(Kusomwa Mara ya Tatu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, UTARATIBU NA BUNGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kutoa taarifa kwamba Kamati ya Bunge Zima imepitia Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama Vya Siasa ya Mwaka 2008, yaani The Political Parties Amendment Act, 2008 pamoja na marekebisho yake yote kifungu kwa kifungu na kukubaliwa.

Hivyo basi, naomba kutoa hoja kwamba Muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2008, yaani The Political Parties Amendments Act, 2008 sasa ukubaliwe rasmi. Naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kura zihesabiwe.

NAIBU SPIKA: Ni sawa, ameungwa mkono. Katibu piga kengele.

(Hapa kengele ilipigwa ili Wheshimiwa Wabungewaliopo nje waingie ndani ya Ukumbi wa Bunge)

(Hapa Waheshimiwa Wabunge walipiga kura)

Mhe. Samuel J. Sitta Hakuwepo Mhe. Anne S. Makinda Mhe. Jenista J. Mhagama Ndiyo Mhe. Job Y. Ndugai Hakuwepo

83 NAIBU SPIKA: Naomba tuanze tena. Mimi kwa kuwa sasa nimekalia Kiti, siwezi kupiga kura; mpaka zifungane ndiyo nitakwenda ninakotaka. Kwa sasa siwezi kupiga kura kwa hiyo anzia kwa Waziri Mkuu.

Mhe. Mizengo K. P. Pinda Hakuwepo Mhe. Jenista J. Mhagama Hakuwepo Mhe. Philip S. Marmo Ndiyo Mhe. Ndiyo Mhe. Prof. Juma A. Kapuya Ndiyo Mhe. Dkt. Mary M. Nagu Hakuwepo Mhe. John P. J. Magufuli Hakuwepo Mhe. Prof. Mark J. Mwandosya Hakuwepo Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Hakuwepo Mhe. Capt. John Z. Chiligati Hakuwepo Mhe. Margaret S. Sitta Ndiyo Mhe. Prof. Peter M. Msolla Hakuwepo Mhe. Stephen M. Wassira Ndiyo Mhe. Prof. D. H. Mwakyusa Hakuwepo Mhe. Prof. Jumanne A. Maghembe Ndiyo Mhe. Dkt. Shukuru J. Kawambwa Hakuwepo Mhe. Hawa A. Ghasia Ndiyo Mhe. Sophia M. Simba Hakuwepo Mhe. Dkt. Batilda S. Burian Hakuwepo Mhe. Bernard K. Membe Ndiyo Mhe.Mathias M. Chikawe Hakuwepo Mhe. Dkt. Diodorus B. Kamala Ndiyo Mhe. Shamsa S. Mwangunga Ndiyo Mhe. Mustafa H. Mkulo Ndiyo Mhe. Lawrence K. Masha Ndiyo Mhe. William M. Ngeleja Hakuwepo Mhe. Capt. George H. Mkuchika Hakuwepo Mhe. Celina O. Kombani Hakuwepo Mhe. Johnson P. M. Mwanyika Hakuwepo Mhe. Dkt. Maua A. Daftari Hakuwepo Mhe. Hezekiah N. Chibulunje Ndiyo Mhe. Balozi S. A. Iddi Hakuwepo Mhe. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi Ndiyo Mhe. Mwantumu B. Mahiza Ndiyo Mhe. Dkt. Cyril A. Chami Hakuwepo Mhe. Dkt. Milton M. Mahanga Hakuwepo Mhe. Dkt. Aisha O. Kigoda Ndiyo Mhe. Joel N. Bendera Hakuwepo Mhe. Dkt. David M. David Hakuwepo Mhe. Christopher K. Chiza Hakuwepo Mhe. Gaudentia M. Kabaka Ndiyo Mhe. Jeremiah S. Sumari Ndiyo

84 Mhe. Mohamed Aboud Mohamed Hakuwepo Mhe. Omar Yussuf Mzee Hakuwepo Mhe. Balozi H. S. Kagasheki Hakuwepo Mhe. Dkt. Lucy S. Nkya Hakuwepo Mhe. Dkt. James M. Wanyancha Ndiyo Mhe. Ezekiel M. Maige Hakuwepo Mhe. Adam K. A. Malima Hakuwepo Mhe. Aggrey D. J. Mwanri Hakuwepo Mhe. Dkt. Abdallah O. Kigoda Hakuwepo Mhe. George M. Lubeleje Hakuwepo Mhe. Wilson M. Masilingi Hakuwepo Mhe. Anne K. Malecela Ndiyo Mhe. John M. Cheyo Hapana Mhe. Dkt. Wilbrod P. Slaa Hakuwepo Mhe. Kabwe Z. Zitto Hapana Mhe. George B. Simbachawene Ndiyo Mhe. Lediana M. Mng’ong’o Hakuwepo Mhe. Abdisalaam Issa Khatib Hakuwepo Mhe. Omar S. Kwaangw’ Hakuwepo Mhe. Gideon A. Cheyo Hakuwepo Mhe. William H. Shellukindo Hakuwepo Mhe. Hamad Rashid Mohamed Hakuwepo Mhe. Halima J. Mdee Hapana Mhe. Shoka Khamis Juma Hakuwepo Mhe. Grace S. Kiwelu Hakuwepo Mhe. Riziki Omar Juma Hapana Mhe. Dkt. Ali Tarab Ali Hapana Mhe. Susan A. J. Lyimo Hapana Mhe. Said A. Arfi Hakuwepo Mhe. Mwanawetu S. Zarafi Hapana Mhe. Salim Abdallah khalfani Hapana Mhe. Mhonga S. Ruhwanya Hapana Mhe. Salim Hemed Khamis Hakuwepo Mhe. Anna Maulidah Komu Hapana Mhe. Mwadini Abbas Jecha Hapana Mhe. Magdalena H. Sakaya Hapana Mhe. Ibrahim Mohamed Sanya Hakuwepo Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa Hakuwepo Mhe. Mohamed H. J. Mnyaa Hapana Mhe. Fatma Mussa Maghimbi Hakuwepo Mhe. Masoud Abdallah Salim Hapana Mhe. Abubakar Khamis Bakary Hapana Mhe. Lucy F. Owenya Hapana Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji Hapana Mhe. Ania Said Chaurembo Hapana Mhe. Omar Ali Mzee Hapana

85 Mhe. Ali Said Salim Hakuwepo Mhe. Nuru Awadhi Bafadhili Hakuwepo Mhe. Bakari Khamis Faki Hapana Mhe. Mohamed Ali Said Hapana Mhe. Mkiwa A. Kimwanga Hapana Mhe. Juma Said Omar Hapana Mhe. Ali Khamis Seif Hapana Mhe. Savelina S. Mwijage Hapana Mhe. Khadija S. Ally Al-Qassmy Hakuwepo Mhe. Mgeni Jadi Kadika Hapana Mhe. Anna M. Abdallah Ndiyo Mhe. Maida Hamad Abdallah Ndiyo Mhe. Mohamed Rished Abdallah Hakuwepo Mhe. Mohammed Abdi Abdulaziz Hakuwepo Mhe. Bahati Ali Abeid Hakuwepo Mhe. Ali Haji Ali Ndiyo Mhe. Fatma Othman Ali Hakuwepo Mhe. Aziza Sleyum Ally Hakuwepo Mhe. Ame Pandu Ame Ndiyo Mhe. Kheri Khatib Ameir Hakuwepo Mhe. Ameir Ali Ameir Ndiyo Mhe. Idd M. Azzan Ndiyo Mhe. Rostam A. Azizi Hakuwepo Mhe. Faida Mohamed Bakar Ndiyo Mhe. Prof. Feetlham F. Banyikwa Ndiyo Mhe. Elizabeth N. Batenga Ndiyo Mhe. Gosbert B. Blandes Hakuwepo Mhe. Felister A. Bura Ndiyo Mhe. Pindi H. Chana Hakuwepo Mhe. Dkt. Raphael M. Chegeni Hakuwepo Mhe. Andrew John Chenge Hakuwepo Mhe. Diana Mkumbo Chilolo, Hakuwepo Mhe. Samweli Mchele Chitalilo, Hakuwepo Mhe. Mohamed Amour Chombo Hakuwepo Mhe. Pascal C. Degera Ndiyo Mhe. Hasnain G. Dewji Ndiyo Mhe. Antony M. Diallo Ndiyo Mhe. Mercy M. Emmanuel Ndiyo Mhe. Col. Saleh Ali Farrah Hakuwepo Mhe. Stephen J. Galinoma Hakuwepo Mhe. Dkt. Zainabu A. Gama Hakuwepo Mhe. Josephine J. Genzabuke Ndiyo Mhe. Ali Juma Haji Hakuwepo Mhe. Dkt. Haji Mwita Haji Hakuwepo Mhe. Zuleikha Yunus Haji Hakuwepo Mhe. Hemed Mohamed Hemed Hakuwepo

86 Mhe. Maria I. Hewa Hakuwepo Mhe. Parmukh Singh Hoogan Hakuwepo Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma Hakuwepo Mhe. Issa Kasim Issa Ndiyo Mhe. Yahaya Kasim Issa Ndiyo Mhe. Othman S. Janguo Hakuwepo Mhe. Asha Mshimba Jecha Ndiyo Mhe. Rajab Hamad Juma Hakuwepo Mhe. Siraju J. Kaboyonga Ndiyo Mhe. Janeth B. Kahama Hakuwepo Mhe. Nazir M. Karamagi Ndiyo Mhe. Teddy L. Kasella-Bantu Ndiyo Mhe. Mariam R. Kasembe Ndiyo Mhe. Eustace O. Katagira Ndiyo Mhe. Vita R. Kawawa Ndiyo Mhe. Gaudence C. Kayombo Hakuwepo Mhe. Charles N. Keenja Hakuwepo Mhe. Yono S. Kevela Hakuwepo Mhe. Vua Abdallah Khamis Ndiyo Mhe. Mwajuma Hassan Khamis Hakuwepo Mhe. Hassan Rajab Khatib Hakuwepo Mhe. Hassan C. Kigwalilo Ndiyo Mhe. Felix N. Kijiko Ndiyo Mhe. Estherina J. Kilasi Ndiyo Mhe. Juma H. Killimbah Ndiyo Mhe. Aloyce B. Kimaro Ndiyo Mhe. Halima Omar Kimbau Hakuwepo Mhe. Fuya G. Kimbita Ndiyo Mhe. Paul P. Kimiti Hakuwepo Mhe. Rosemary K. Kirigini Ndiyo Mhe. Capt. John D. Komba Hakuwepo Mhe. Suleiman O. Kumchaya Ndiyo Mhe. William J. Kusila Ndiyo Mhe. Al-Shymaa J. Kwegyir Ndiyo Mhe. Florence E. Kyendesya Ndiyo Mhe. Michael L. Laizer Ndiyo Mhe. James D. Lembeli Hakuwepo Mhe. Castor R. Ligallam Ndiyo Mhe. Devota M. Likokola Ndiyo Mhe. Dkt. Festus B. Limbu Hakuwepo Mhe. Sameer I. Lotto Hakuwepo Mhe. Edwar N. Lowassa Hakuwepo Mhe. Emmanuel J. Luhahula Hakuwepo Mhe. William V. Lukuvi Ndiyo Mhe. Riziki S. Lulinda Hakuwepo Mhe. Anna R. Lupembe Ndiyo

87 Mhe. John P. Lwanji Hakuwepo Mhe. Clemence B. Lyamba Ndiyo Mhe. Ernest G. Mabina Hakuwepo Mhe. Joyce N. Machimu Hakuwepo Mhe. Ephrain N. Madeje Ndiyo Mhe. Dkt. Binilith S. Mahenge Ndiyo Mhe. Yusuf R. Makamba Hakuwepo Mhe. Jackson M. Makweta Ndiyo Mhe. Benito W. Malangalila Hakuwepo Mhe. John S. Malecela Hakuwepo Mhe. Halma M. Mamuya Hakuwepo Mhe. Ramadhan A. Maneno Hakuwepo Mhe. Eng. Stella M. Manyanya Ndiyo Mhe. Vedastus M. Manyinyi Ndiyo Mhe. Abdul J. Marombwa Ndiyo Mhe. Masolwa Cosmas Masolwa Ndiyo Mhe. Haroub Said Masoud Ndiyo Mhe. Janeth M. Massaburi Ndiyo Mhe. Joyce M. Masunga Hakuwepo Mhe. Lucy T. Mayenga Hakuwepo Mhe. Kiumbwa Makame Mbaraka Ndiyo Mhe. Monica N. Mbega Ndiyo Mhe. Mwanne I. Mchemba Ndiyo Mhe. Zakia H. Meghji Hakuwepo Mhe. Maria S. Mfaki Ndiyo Mhe. Feteh Saad Mgeni Ndiyo Mhe. Laus O. Mhina Hakuwepo Mhe. Zabein M. Mhita Ndiyo Mhe. Fatma A. Mikidadi Ndiyo Mhe. Margreth A. Mkanga Ndiyo Mhe. Dunstan D. Mkapa Hakuwepo Mhe. Nimrod E. Mkono Hakuwepo Mhe. Rita L. Mlaki Hakuwepo Mhe. Martha M. Mlata Ndiyo Mhe. Dkt. Charles O. Mlingwa Hakuwepo Mhe. Herbert J. Mntangi Hakuwepo Mhe. Ali Ameir Mohamed Ndiyo Mhe. Salim Yussuf Mohamed Hapana Mhe. Elisa D. Mollel Ndiyo Mhe. Balozi Dkt. Getrude I. Mongella Ndiyo Mhe. Dkt. Samson Ferdinand Mpanda Ndiyo Mhe. Benson M. Mpesya Ndiyo Mhe. Luhaga J. Mpina Hakuwepo Mhe. Kilontsi M. Mporogomyi Hakuwepo Mhe. Basil P. Mramba Ndiyo Mhe. Felix C. Mrema Ndiyo

88 Mhe. Raynald A. Mrope Hakuwepo Mhe. Dkt. Ibrahim S. Msabaha Hakuwepo Mhe. Ruth B. Msafiri Ndiyo Mhe. Manju S. O. Msambya Ndiyo Mhe. Dkt. James A. Msekela Hakuwepo Mhe. Balozi Abdi H. Mshangama Ndiyo Mhe. Mgana I. Msindai Hakuwepo Mhe. Mwinchoum A. Msomi Ndiyo Mhe. Abbas Z. Mtemvu Hakuwepo Mhe. Prof. Idris A. Mtulia Ndiyo Mhe. Mtutura A. Mtutura Ndiyo Mhe. Mudhihir M. Mudhihir Ndiyo Mhe. Joseph J. Mungai Hakuwepo Mhe. James P. Musalika Hakuwepo Mhe. Omar Sheha Mussa Hakuwepo Mhe. Mossy Suleiman Mussa Ndiyo Mhe. Bernadeta K. Mushashu Ndiyo Mhe. Dorah H. Mushi Hakuwepo Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe Ndiyo Mhe. Prof. Raphael B. Mwalyosi Ndiyo Mhe. Victor K. Mwambalaswa Ndiyo Mhe. Ludovick J. Mwanazila Ndiyo Mhe. Mbaruk K. Mwandoro Ndiyo Mhe. Thomas A. Mwang’onda Hakuwepo Mhe. Mch. Luckson Mwanjale Ndiyo Mhe. Harith B. Mwapachu Hakuwepo Mhe. Hamza A. Mwenegoha Hakuwepo Mhe. Charles N. Mwera Hapana Mhe. Dkt. Chrisant M. Mzindakaya Hakuwepo Mhe. Damas P. Nakei Ndiyo Mhe. Benedic N. Ole-Nangoro Ndiyo Mhe. Richard M. Ndassa Hakuwepo Mhe. Philemon Ndesamburo Hakuwepo Mhe. Dkt. Juma A. Ngasongwa Ndiyo Mhe. Sigifrid S. Ng’itu Hakuwepo Mhe. Kingunge Ngombale-Mwiru Ndiyo Mhe. Cynthia H. Ngoye Ndiyo Mhe. Hadija Saleh Ngozi Ndiyo Mhe. Brg. Gen. Hassan A. Ngwilizi Ndiyo Mhe. Juma Suleiman N’hunga Ndiyo Mhe. Juma A. Njwayo Ndiyo Mhe. Dkt. Omar M. Nibuka Ndiyo Mhe. Sijapata F. Nkayamba Ndiyo Mhe. Said J. Nkumba Hakuwepo Mhe. Danie N. Nsanzugwako Hakuwepo Mhe. Tatu M. Ntimizi Ndiyo

89 Mhe. Lazaro S. Nyalandu Hakuwepo Mhe. Ponsiano D. Nyami Hakuwepo Mhe. Esther K. Nyawazwa Ndiyo Mhe. Ussi Ame Pandu Ndiyo Mhe. Mwaka Abdulrahaman Ramadhan Ndiyo Mhe. Shally J. Raymond Ndiyo Mhe. Mch. Dkt. Getrude P. Rwakatare Hakuwepo Mhe. Kabuzi F. Rwilomba Hakuwepo Mhe. Suleiman A. Saddiq Hakuwepo Mhe. Mwanakahamis Kassim Said Ndiyo Mhe. Bujiku P. Sakila Ndiyo Mhe. Kidawa Hamid Salehe Hakuwepo Mhe. Ahmed A. Salum Hakuwepo Mhe. Salum K. Salum Hakuwepo Mhe. Prof. Philemon M. Sarungi Ndiyo Mhe. Lucas L. Selelii Hakuwepo Mhe. Christopher O. Ole-Sendeka Ndiyo Mhe. Haji Juma Sereweji Ndiyo Mhe. Peter J. Serukamba Hakuwepo Mhe. Ahmed M. Shabiby Hakuwepo Mhe. Abdulkarim Esmail Hassan Shah Hakuwepo Mhe. Beatrice M. Shellukindo Hakuwepo Mhe. Jacob D. Shibiliti Hakuwepo Mhe. Magalle J. Shibuda Hakuwepo Mhe. Dkt. Guido G. Sigonda Ndiyo Mhe. Mohamed S. Sinani Hakuwepo Mhe. Dkt. Luka J. Siyame Ndiyo Mhe. Mohamed Rajab Soud Ndiyo Mhe. Ali Haroon Suleiman Ndiyo Mhe. Abdallah S. Sumry Hakuwepo Mhe. Elietta N. Switi Ndiyo Mhe. Hafidh Ali Tahir Hakuwepo Mhe. Fatma Abdalla Tamim Ndiyo Mhe. Kaika S. Telele Ndiyo Mhe. Fred M. Tungu Ndiyo Mhe. Martha J. Umbulla Hakuwepo Mhe. Zayna M. Vulu Hakuwepo Mhe. Anastazia J. Wambura Ndiyo Mhe. Godfrey W. Zambi Ndiyo Mhe. Mzee Ngwali Zubeir Hakuwepo Mhe. Mussa A. Zungu Ndiyo

MJUMBE FULANI: Huyu hatukuwa tumemtaja.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sasa kuna wengine wameingia ningeomba walioingia column hii wasimame na wataje majina yao na wapige kura.

90 Column hii kwanza mkono wangu wa kushoto, kama hayupo column ya pili mkono wa kushoto na wataje majina yao na wapige kura.

(Hapa ambao hawakupiga kura waliingia Ukumbini kupiga kura)

Mhe. Benito W. Malangalila Ndiyo Mhe. Halima M. Mamuya Ndiyo Mhe. Ali Juma Haji Ndiyo Mhe. Abdallah O. Kigoda Ndiyo Mhe. Maria I. Hewa Ndiyo Mhe. Joyce N. Machimu Ndiyo Mhe. Raphael M. Chegeni Ndiyo Mhe. Mohamed Amour Chomboh Ndiyo Mhe. William M. Ngeleja Ndiyo Mhe. Aggrey D. J. Mwanri Ndiyo

NAIBU SPIKA: Kwa hiyo, wote sasa tunafunga kura. Kwa hiyo, tunataka kuhesabu, tunaanza kazi. Sekretarieti wahesabu wangapi wamesema ndiyo na wangapi wamesema hapana.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, democracy ndiyo inavyotaka hata ikitaka kwenda mwendo mrefu ndiyo hivyo hivyo hata ikiwa na gharama kubwa ndiyo hivyo democracy inavyotaka. Kwa hiyo, wale waliosema hapana ni 32, waliosema ndiyo ni 146. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Shame! Wamezoea kusutwa, CCM hoyeeeeeeee!

WABUNGE: Hoyeeee!

MBUNGE FULANI: Haoooooo!

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, sasa napenda kusema kwamba Muswada ule umepita kwa walio wengi.

WABUNGE FULANI: Haoooooooooo! Shame!

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Muswada wa Sheria ya Serikali Ulisomwa Mara ya Tatu na Kupitishwa)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Muswada umepita hatua zake zote, kwa maana ya hapa Bunge umemaliza safari yake, sasa utasubiri Mheshimiwa Rais kuweka mkono wake ili uweze kuwa sheria ya vyama vya siasa. (Makofi)

Baada ya hapo, napenda kutangaza kwamba kesho saa 1.30 tutakuwa na hafla ya kuupokea mwaka 2009 na kumuaga aliyekuwa Katibu wa Bunge Bwana Damian Foka

91 saa 1.30 usiku, msije mkaja asubuhi mtakuta hamna itakuwa kama wale wanaokuja kujiandikisha majina ili waweze kusema kwa Waziri Mkuu. Kwa hiyo, ni usiku kesho saa 1.30.

Waheshimiwa Wabunge, ni vizuri wote mkahudhuria, maana sherehe ukishapanga wenzako wasipohudhuria inakuwa sio sherehe.

Kwa hiyo, mnakaribishwa na mgeni wetu rasmi atakuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Baada ya kusema hayo, naomba niwatakie heri ya wikiendi na asante sana kwa kazi mliyofanya wiki hii na wote mmefanya kazi vizuri, kesho hamna semina wala mkutano kwa sababu tulishafanya mkutano. Kwa wale wanaopenda matembezi na mshikamano, yapo nadhani nimeshatangaza kwa matembezi ya mshikamano kesho kwa Mkoa wa Dodoma, sijui saa ngapi na wapi. Saa tatu Kikombo.

Naomba niahirishe shughuli za Bunge mpaka siku ya Jumatatu, saa tatu.

(Saa 12.20 jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumatatu, Tarehe 9 Februari, 2009 Saa Tatu Asubuhi)

92