1588591331-HOTUBA YA BAJETI 4 MEI.Pdf

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

1588591331-HOTUBA YA BAJETI 4 MEI.Pdf JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, MHESHIMIWA ENG. ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 DODOMA MEI, 2020 HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, MHESHIMIWA ENG. ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa humu Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ninaomba kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/20. Aidha, kwa mara nyingine ninaomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2020/21. 2. Mheshimiwa Spika, sisi sote kwa ujumla wetu, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutujalia uhai na afya njema na hivyo kutuwezesha kukutana leo kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano huu wa 19 na wa mwisho wa Bunge la 11, ili kujadili utekelezaji wa majukumu ya Sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/20 pamoja na kujadili Mipango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Sekta hizo kwa mwaka wa fedha 2020/21. Aidha, ninamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutupatia ulinzi wake dhidi ya janga linaloisumbua dunia kwa sasa la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID -19). 3. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/20, Bunge lako Tukufu lilipatwa na simanzi kubwa kufuatia vifo vya wapendwa wetu ambao ni Mhe. Rashid Ajali Ahkbar aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Newala Vijijini, Richard Mganga Ndassa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sumve na Mhe. Mchungaji Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare, Mbunge wa Viti Maalum. Ninachukua fursa hii kutoa pole kwako wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika, Familia za Marehemu hao, Bunge lako Tukufu, Wananchi wa Jimbo la Newala Vijijini na Watanzania kwa ujumla kwa kuondokewa na wanasiasa hao wakongwe na mahiri. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu hao mahali pema peponi. Amina. 4. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwapa pole ndugu wa marehemu na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa 2 msiba mkubwa wa wafanyakazi watano (5) waliopoteza maisha na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Mwakinyumbi na Gendagenda ambapo treni iligongana na kiberenge, wananchi 104 waliopoteza maisha kutokana na moto uliosababishwa na lori la mafuta mjini Morogoro, ajali ya lori kugongana na basi la abiria eneo la Mkuranga - Pwani ambapo abiria 20 walipoteza maisha na 15 kujeruhiwa. Aidha, ninawapa pole wote waliofikwa na majanga ya kupoteza ndugu zao kufuatia mvua zilizonyesha kupita kiwango katika maeneo mbalimbali nchini. Mwenyezi Mungu awape nafuu ya haraka majeruhi wote na aziweke roho za marehemu hao mahali pema peponi. Amina. 5. Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima ninaomba uniruhusu kutumia fursa hii kumpongeza Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kwa umakini mkubwa na hivyo kuendelea kuiongoza nchi yetu kwa amani na utulivu. Aidha, ninampongeza Mhe. Rais kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na kuiongoza vyema Jumuiya hiyo hususan katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID -19). Vilevile, ninawapongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wao thabiti. 6. Mheshimiwa Spika, ninaomba nikupongeze wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Katibu wa Bunge, Watendaji wa Ofisi ya Bunge pamoja na Bunge lako Tukufu kwa ushirikiano ninaoendelea kuupata wakati wote ninapotekeleza majukumu yangu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa mbalimbali kuhusu sekta ninazozisimamia. Ninapenda kuwahakikishia kuwa, Wizara yangu itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kufikia malengo ya Kisekta na Kitaifa kwa ujumla. Vilevile, kwa namna ya pekee ninaomba kuishukuru familia yangu na wapiga kura wa Jimbo langu la Uchaguzi la Katavi kwa kuendelea kunipa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yangu kwa Watanzania. 7. Mheshimiwa Spika, nitumie pia fursa hii kuwapongeza Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais 3 (Muungano na Mazingira) na Mhe. George Boniface Taguluvala Simbachawene (Mb), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuteuliwa kuwa Mawaziri. Aidha, ninapenda kutoa pongezi kwa Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Mhe. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa kuchaguliwa kuwa Wabunge katika chaguzi ndogo zilizofanyika nchini katika mwaka wa fedha 2019/20. Ushindi wao wa kishindo ni kielelezo tosha cha kuonyesha namna Chama cha Mapinduzi kinavyoendelea kuaminika na kupendwa na Watanzania. Vilevile, ninampongeza Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano. 8. Mheshimiwa Spika, mwisho lakini siyo kwa umuhimu, ninapenda kuchukua fursa hii kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inayoongozwa na Mhe. Seleman Moshi Kakoso (Mb), Mbunge wa Mpanda Vijijini na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Hawa Mchafu Chakoma (Mb). Nakiri kuwa Wizara imenufaika sana na umahiri, umakini na ushirikiano wa Kamati hiyo katika kuchambua, kushauri na kufuatilia maendeleo ya Sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba maoni, ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati yamezingatiwa katika Bajeti hii. 9. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuwasilisha Hotuba hii, ninapenda kuwashukuru Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango kwa hotuba zao zilizotangulia. Hotuba hizo zimeeleza kwa ujumla maendeleo ya sekta za Kijamii na Kiuchumi kwa mwaka 2019/20 na mwelekeo kwa mwaka 2020/21. Ninawashukuru na kuwapongeza pia Mawaziri wote waliowasilisha hotuba zao. 10. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ninaomba sasa kuwasilisha hotuba yangu ambayo imejikita katika Utekelezaji wa Mipango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/20 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2020/21. Aidha, kabla ya kuelezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, ninapenda nitoe kwa muhtasari taarifa ya utekelezaji wa Ilani 4 ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015` kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano. B. UTEKELEZAJI WA MALENGO YALIYOAINISHWA KATIKA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2015 KWA KIPINDI CHA MWAKA 2016/17 – 2019/20 B-1 SEKTA YA UJENZI 11. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, Serikali kupitia Wizara yangu imepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja kwa kuzingatia vipaumbele ambavyo ni; Kujenga barabara zetu zinazounganisha nchi yetu na nchi jirani, kujenga barabara zinazounganisha mikoa kwa kiwango cha lami na kujenga barabara zinazokwenda kwenye maeneo yenye fursa za kiuchumi. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,624.27 zimejengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami. Aidha, jumla ya kilometa 82.6 za barabara za kupunguza msongamano wa magari katika miji zimejengwa kwa kiwango cha lami na barabara kuu zenye urefu wa kilometa 1,298.44 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami. Vilevile, ukarabati wa barabara kuu zenye urefu wa kilometa 300.9 umekamilika. 12. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, jumla ya madaraja makubwa 13 yalikuwa katika hatua mbali mbali za utekelezaji. Kati ya hayo, madaraja makubwa nane (8) yamekamilika, ambayo ni Daraja la Magufuli, Magara, Mlalakuwa, Momba, Lukuledi II, Mara, Sibiti na Daraja la Nyerere (Kigamboni). Aidha, madaraja makubwa matano (5) yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ambayo ni Daraja Jipya la Selander, Msingi, Wami, Kitengule na Ruhuhu. Madaraja makubwa nane (8) ya Kigongo – Busisi, Sukuma, Simiyu, Mkenda, Mtera, Godegode, Malagarasi Chini na Ugalla yako kwenye hatua mbalimbali za maandalizi ya kazi za ujenzi. 13. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa kilometa 4,856 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara kuu na za mikoa pamoja na madaraja mapya 12. Aidha, upembuzi yakinifu wa kilometa 452.3 kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu na za mikoa kwa kiwango cha lami ulikamilika. Vilevile kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa 5 jumla ya kilometa 3,653.13 upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. 14. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege nchini. Viwanja vya ndege vilivyokamilika ni: Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) pamoja na ukarabati na uboreshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza. Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato upo katika hatua ya maandalizi ya kuanza utekelezaji. Aidha, Viwanja vya Ndege vya Songea, Kigoma, Shinyanga, Sumbawanga, Tabora, Iringa na Musoma vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Vilevile, kati ya viwanja kumi na
Recommended publications
  • Hotuba Ya Waziri Wa Uchukuzi, Mhe. Dkt
    HOTUBA YA WAZIRI WA UCHUKUZI, MHE. DKT. HARRISON G. MWAKYEMBE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2013/2014 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyochambua bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kuweka mezani taarifa ya Kamati mbele ya Bunge lako Tukufu, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2013/2014. 2. Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai na kutuwezesha kukutana tena leo kujadili maendeleo ya Sekta ya Uchukuzi, Hali ya Hewa na Taifa letu kwa ujumla. 3. Mheshimiwa Spika, napenda vilevile nimpongeze kwa namna ya pekee Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Mwenyekiti wa Chama 1 cha Mapinduzi. Kuchaguliwa kwake, tena kwa kishindo, ni ushahidi tosha wa imani kubwa waliyonayo wana CCM kwake kutokana na kazi nzuri aliyoifanya miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake. Aidha, nawapongeza Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Mhe. Philip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara) na Mhe. Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Binafsi nina imani kubwa kuwa safu hii mpya ya uongozi yenye rekodi ndefu ya utendaji uliotukuka nje na ndani ya Chama cha Mapinduzi itatusogeza karibu zaidi na malengo tuliyojiwekea kama Taifa ya kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. 4. Mheshimiwa Spika, niruhusu vilevile nitumie fursa hii kuwashukuru Mhe.
    [Show full text]
  • List of Rivers of Tanzania
    Sl.No Name Draining Into 1 Bubu River Endorheic basins 2 Deho River East Coast 3 Great Ruaha River East Coast 4 Ifume River Congo Basin 5 Ipera River East Coast 6 Isanga River Nile basin 7 Jipe Ruvu River East Coast 8 Kagera River Nile basin 9 Kalambo River Congo Basin 10 Kavuu River Endorheic basins 11 Kihansi East Coast 12 Kikafu River East Coast 13 Kikuletwa River East Coast 14 Kimani River East Coast 15 Kimbi River East Coast 16 Kiseru River East Coast 17 Kizigo River East Coast 18 Kolungazao River East Coast 19 Lake Burunge Endorheic basins 20 Lake Eyasi Endorheic basins 21 Lake Jipe East Coast 22 Lake Malawi Zambezi basin 23 Lake Manyara Endorheic basins 24 Lake Natron Endorheic basins 25 Lake Rukwa Endorheic basins 26 Lake Tanganyika Congo Basin 27 Lake Victoria Nile basin 28 Little Ruaha River East Coast 29 Loasi River Congo Basin 30 Luamfi River Congo Basin 31 Luega River Congo Basin 32 Luegele River Congo Basin 33 Luengera River East Coast 34 Luhombero River East Coast 35 Lukigura River East Coast 36 Lukosi River East Coast 37 Lukuledi River East Coast 38 Lukumbule River East Coast 39 Lukwika River East Coast 40 Lungonya River East Coast 41 Luwegu River East Coast 42 Malagarasi River Congo Basin 43 Mara River Nile basin 44 Matandu River East Coast 45 Mavuji River East Coast 46 Mbarali River East Coast 47 Mbiki River East Coast 48 Mbungu River East Coast 49 Mbwemkuru River East Coast www.downloadexcelfiles.com 50 Mgeta River East Coast 51 Migasi River East Coast 52 Miyombo River East Coast 53 Mkata River East Coast 54 Mkomazi
    [Show full text]
  • Groundwater Resources in the East African Rift Valley: Understanding the Geogenic Contamination and Water Quality Challenges in Tanzania
    Scientific African 13 (2021) e00831 Contents lists available at ScienceDirect Scientific African journal homepage: www.elsevier.com/locate/sciaf Groundwater resources in the East African Rift Valley: Understanding the geogenic contamination and water quality challenges in Tanzania ∗ Fanuel Ligate a,b,c, , Julian Ijumulana a,b, Arslan Ahmad a,d,f, Vivian Kimambo a,b, Regina Irunde a,b,e, Joseph O. Mtamba b, Felix Mtalo b, Prosun Bhattacharya a a KTH-International Groundwater Arsenic Research Group, Department of Sustainable Development, Environmental Science and Engineering, KTH Royal Institute of Technology, Teknikringen 10B, SE-100 44 Stockholm Sweden b Department of Water Resources Engineering, College of Engineering and Technology, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania c Department of Chemistry, Mkwawa College of Education, University of Dar es Salaam, Tanzania d KWR Watercycle Research Institute, Groningenhaven 7 3433 PE, Nieuwegein, The Netherlands e Department of Chemistry, College of Natural and Applied Sciences, University of Dar es Salaam, Tanzania f Department of Environmental Technology, Wageningen University and Research (WUR), Droevendaalsesteeg 4, 6708 PB Wageningen, The Netherlands a r t i c l e i n f o a b s t r a c t Article history: Over the years, groundwater has been used as a means of adaptation to the seasonal and Received 26 May 2020 perennial scarcity of surface water. Groundwater provides water for households, livestock, Revised 17 April 2021 and irrigation in semi-arid areas of Tanzania. It is acknowledged that groundwater is sus- Accepted 27 June 2021 ceptible to chemical and other mineral contamination which not only poses a threat to the health of human beings and livestock but also agriculture.
    [Show full text]
  • Dodoma Aprili, 2019
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHESHIMIWA MHANDISI ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 DODOMA APRILI, 2019 HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHESHIMIWA MHANDISI ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuweka mezani Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai na kutuwezesha kukutana tena leo kujadili maendeleo ya shughuli zinazosimamiwa na sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa 1 hii kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Alli Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wao thabiti ambao umewezesha kutekelezwa kwa mafanikio makubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, ahadi za Viongozi pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
    [Show full text]
  • Vulnerability and Impact Assessment Ecosystem-Based Adaptation for Rural Resilience (Ebarr) in Tanzania
    © Malcolm Cerfonteyn, Flickr Vulnerability and Impact Assessment Ecosystem-based Adaptation for Rural Resilience (EbARR) in Tanzania Final Report Vulnerability and Impact Assessment Ecosystem-based Adaptation for Rural Resilience (EbARR) in Tanzania Final Report Client Vice President’s Office, Tanzania Authors Paul Manning (Independent Consultant, Team Leader) Dr. Jochen Statz (UNIQUE forestry and land use, Germany) Renuka Srinivasan (UNIQUE forestry and land use, Germany) Dr. Gordon Stanger (Independent Consultant) Demetrius Kweka (Independent Consultant) Abdallah Henku (Independent Consultant) Dr. Japhet Kashaigili (Independent Consultant) Date: 14.04.2020 UNIQUE | EbARR – Vulnerability Impact Assessment Final Report 2 TABLE OF CONTENTS List of tables ........................................................................................................................ 4 List of figures ....................................................................................................................... 5 List of abbreviations ............................................................................................................ 7 Executive Summary ............................................................................................................. 9 Background .............................................................................................................................. 9 Summary of climate projections and impacts ....................................................................... 10 Recommended EbA
    [Show full text]
  • A Checklist of the Land Mammals Tanganyika Territory Zanzibar
    274 G. H. SWYNNERTON,F.Z.S., Checklist oj Land Mammals VOL. XX A Checklist of the Land Mammals OF mE Tanganyika Territory AND mE Zanzibar Protectorate By G. H. SWYNNERTON, F.Z.S., Game Warde:z, Game Preservation Department, Tanganyika Territory, and R. W. HAYMAN, F.Z.S., Senior Experimental Officer, Department of Zoology, British Museum (Natural History) 277278·.25111917122896 .· · 4 . (1)(3)(-)(2)(5)(9)(3)(4)280290281283286289295288291 280. .. CONTENTS· · · No. OF FORMS* 1. FOREWORDINSECTIVORA ErinaceidaM:,gadermatidaEmballonuridaSoricidt:eMacroscelididaMarossidaNycteridaHipposideridaRhinolophidaVespertilionida(Shrews)(Free-tailed(Hollow-faced(Hedgehogs)(Horseshoe(Leaf-nosed(Sheath-tailed(Elephant(Simple-nosed(Big-earedBats)Bats)Shrews)BatsBats)Bats) Pteropodida (Fruit-eating Bats) 2.3. INTRODUCTIONSYSTEMATICLIST OF SPECIESAND SUBSPECIES: PAGE CHIROPTERA Chrysochlorida (Golden" Moles to) ···302306191210.3521. ·2387 . · 6 · IAN. (1)(2)1951(-)(4)(21)(1)(6)(14)(6)(5),(7)(8)333310302304306332298305309303297337324325336337339211327 . SWYNNERTON,. P.Z.S.,·· ·Checklist··· of·Land 3293Mammals52 275 PItIMATES G. It. RhinocerotidaPelidaEchimyidaHyanidaPongidaCercopithecidaHystricidaMuridaHominidaAnomaluridaPedetidaCaviidaMustelidaGliridaSciuridaViverrida(Cats,(Mice,(Dormice)(Guinea-pigs)(Apes)(Squirrels)(Spring(Hyaenas,(Genets,(Man)(Polecats,(Cane(porcupines)(Flying(Rhinoceroses)Leopards,(Monkeys,Rats,Haas)Rats)Civets,Arad-wolf).Weasels,Squirrels)Gerbils,Lions,Baboons)Mongooses)Ratels,etc.)•Cheetahs)..Otters) ProcaviidaCanidaLeporidaElephantidaLorisidaOrycteropodidaEquidaBathyergidaManida
    [Show full text]
  • Birdlife Naturekenya INTERNATIONAL the East Africa Natural Hlslory Society Scopus 30, October 2010 Contents
    TOS 4-OI 8 ISSN 0250-4162 SCOPUS ^ z FEB j 2014 I A publication of the Bird Committee of the East Africa Natural History Society Edited by Mwangi Githiru Volume 30, October 2010 BirdLife NatureKenya INTERNATIONAL The East Africa Natural Hlslory Society Scopus 30, October 2010 Contents Maurice O. Ogoma, Broder Breckling, Hauke Reuter, Muchai Muchane and Mwangi Githiru. The birds of Gongoni Forest Reserve, South Coast, Kenya 1 Wanyoike Wamiti. Philista Malaki, Kamau Kimani, Nicodemus Nalianya, Chege Kariuki and Lawrence Wagura. The birds of Uaso Narok Forest Reserve, Central Kenya 12 Richard Ssemmanda and Derek Pomeroy. Scavenging birds of Kampala: 1973-2009 26 Jon Smallie and Munir Z. Virani. A preliminary assessment of the potential risks from electrical infrastructure to large birds in Kenya 32 Fred B. Munyekenye and Mwangi Githiru. A survey of the birds of Ol Donyo Sabuk National Park, Kenya 40 Short communications Donald A. TUrner. The status and habitats of two closely related and sympatric greenbuls: Ansorge's Andropadus ansorgei and Little Grey Andropadus gracilis 50 Donald A. Turner. Comments concerning Ostrich Struthio camelus populations in Kenya 52 Donald A. Turner. Comments concerning the status of the White-bellied Bustard race Eupodotis senegalensis erlangeri 54 Tiziano Londei. Typical Little Egrets Egretta garzetta mix with Dimorphic Egrets Egretta dimorpha on open coast in Tanzania 56 Donald A. Turner. The Egretta garzetta complex in East Africa: A case for one, two or three species 59 Donald a. Turner and Dale a. Zimmerman. Quailfinches Ortygospiza spp. in East Africa 63 Neil E. Baker. Recommendation to remove the Somali Bee-eater Merops revoilii from the Tanzania list 65 Neil E.
    [Show full text]
  • Eac Regional Transport Strategy March 2011
    East African Community Secretariat THE EAST AFRICAN TRADE AND TRANSPORT FACILITATION PROJECT EAST AFRICAN TRANSPORT STRATEGY AND REGIONAL ROAD SECTOR DEVELOPMENT PROGRAM FINAL REPORT PART II: EAC REGIONAL TRANSPORT STRATEGY MARCH 2011 Prepared By: Africon Ltd EAC Transport Strategy and Regional Roads Sector Development Program STRUCTURE OF DOCUMENT This report is made up of four parts: Part I provides the general background to the study. It reports on the analyses that are common to and form the foundation of the Transport Strategy and Roads Development Program, including the regional corridors, the economy and demography of the region, transport demand and transport modelling, and the principles for project identification and prioritisation. Part II (this document) is the Transport Strategy. It covers the policy/institutional arrangements in the transport sector in the EAC and its member countries. It then provides an overview of regional issues and identifies regional interventions in each of the transport modes, i.e. roads, rail, ports, pipelines, airports and border posts. It concludes by presenting the prioritised interventions together with an implementation approach. Part III is the Roads Development Program. It covers the regional roads network, and analyses roads needs from capacity and condition perspectives. It also develops some cross-cutting themes (regional roads classification system, regional roads management system and regional overload control). Regional roads projects are identified and described. Part IV is the list of transport projects, together with short profiles for the priority projects. Parts II and III are drafted so that they can be read stand-alone, i.e. in isolation of the other three parts.
    [Show full text]
  • Hotuba Ya Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi Na Mawasiliano Mheshimiwa Prof
    HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHESHIMIWA PROF. MAKAME M. MBARAWA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyochambua Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuweka mezani Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018. 2. Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai na kutuwezesha sote kukutana tena leo kujadili maendeleo ya sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 3. Mheshimiwa Spika, kipekee naomba kuwapongeza sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, 1 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiongoza vema nchi yetu. 4. Mheshimiwa Spika, napenda nimpongeze kwa namna ya pekee Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuiongoza nchi yetu kwa umahiri mkubwa na kudumisha umoja, amani na utulivu. Mheshimiwa Rais ameendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na kutekeleza kwa kiwango kikubwa ahadi za Serikali kwa wananchi. Ama kwa hakika uongozi wake mahiri umekuwa dira sahihi katika kuleta mabadiliko ya kweli ambayo Watanzania wameyasubiri kwa muda mrefu.
    [Show full text]
  • 4.5 Tanzania Airport Company Contact List
    4.5 Tanzania Airport Company Contact List Airport Company Street / Physical Address Name Title Email Phone Phone Fax Website Number Number Number (office) (mobile) Julius Nyerere Tanzania Airport Ilala jnia@airport +255 22 http://www. International Airport Authority s.go.tz 2844324 jnia.go.tz (JNIA) Dar es Salaam +255 22 P. O. Box 18032 2844373 Tanzania Songwe International Tanzania Airport P. O Box 249, Hamisi Airport +255 25 http://www. Airport Authority Amiri Manager 250 4274 taa.go.tz/# Songwe-Mbeya Abeid Amani Karume Zanzibar Airport Abeid Amani Karume Zaina. +255 24 http://www. International Airport - Authorities International Airport, PO Box commandent 2233979 zaa.go.tz Zanzibar 1254, Zanzibar @zaa.go.tz /#tab-id-4 Kilimanjaro International Tanzania Airport KADCO, info@kadco. +255 (27) +255 (27) Airport Authority and co.tz 255 4252, 255 4312 P.O. BOX 10 KIA, Kilimanjaro Airports Development Company Kilimanjaro,Tanzania (KADCO) Kigoma Airport Tanzania Airport P.O Box 764, Kigoma. +255 28 +255 767 36 Authority 280 2857/8 3386/ +255 713 363 384 Dodoma Airport Tanzania Airport P.O. Box 1025, +255 26 Authority 235 4833/ Dodoma. +255 26 235 2179 Manyara Airport Tanzania Airport P.O Box 06, Authority Mto wa Mbu - ARUSHA Mafia Tanzania Airport P. O Box 21, +255 23 Authority 2011309 Airport Mafia Shinyanga Airport Tanzania Airport P.O Box 837, Authority Shinyanga Tabora Airport Tanzania Airport P.O Box 11, +255 26 Authority 2604133 Tabora. Tanga Airport Tanzania Airport P.O Box 851, +255 27 Authority 2644175 Tabora. Morogoro Airport Tanzania Airport P.O Box 89, Authority Morogoro.
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Wizara Ya Ujenzi Na Uchukuzi
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI, MHESHIMIWA MHANDISI DKT. LEONARD MADARAKA CHAMURIHO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/22 DODOMA MEI, 2021 HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI, MHESHIMIWA MHANDISI DKT. LEONARD MADARAKA CHAMURIHO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/22 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuchambua Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2020/21. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22. 2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa unyenyekevu mkubwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa afya njema na uzima aliotujaalia. 3. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii, kwa masikitiko makubwa, kuungana na Waheshimiwa Wabunge waliotangulia kutoa pole kwako wewe binafsi, Bunge lako Tukufu na watanzania wote kwa ujumla kufuatia kifo cha mpendwa wetu Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea tarehe 17 Machi, 2021. Hakika tutamkumbuka shujaa huyu wa Afrika kwa uzalendo, ujasiri, vita dhidi ya ufisadi na uongozi 3 wake mahiri ulioacha alama kubwa kwa Taifa letu na Afrika kwa ujumla.
    [Show full text]
  • Vote 04 Records and Archives Management Department
    VOTE 04 RECORDS AND ARCHIVES MANAGEMENT DEPARTMENT 1 Vote 04 Records and Archives Management Department A. ESTIMATE of the amount required in the year ending 30th June, 2016, for the development projects in the Records and Archives Management Department Two hundred fifty million (Shs.250,000,000) B. Projects under which this Vote will be accounted for by the Director General , are set out in the details below. 2013/2014 2014/2015 2015/2016 Item Description Loan/ Actual Expenditure Approved Estimates Estimates Grant Total Local Forex Local Forex Local Forex C/R/D Donor Shs Shs Shs Shs Sub Vote 1001 ADMINISTRATION AND HR MANAGEMENT 6284 Public Service Reform 0 0 0 0 250,000,000 0 250,000,000 Programme II Total of Subvote 0 0 0 0 250,000,000 0 250,000,000 Total of Vote 0 0 0 0 250,000,000 0 250,000,000 2 VOTE 05 NATIONAL IRRIGATION COMM BOARD 3 Vote 05 National Irrigation Comm Board A. ESTIMATE of the amount required in the year ending 30th June, 2016, for the development projects in the National Irrigation Comm Board Fifty-three billion three hundred ninety-four million five hundred seventy-four thousand (Shs.53,394,574,000) B. Projects under which this Vote will be accounted for by the Chairperson, National Irrigation Comm Board , are set out in the details below. 2013/2014 2014/2015 2015/2016 Item Description Loan/ Actual Expenditure Approved Estimates Estimates Grant Total Local Forex Local Forex Local Forex C/R/D Donor Shs Shs Shs Shs Sub Vote 1002 FINANCE AND ACCOUNTS 4486 Agricultural 0 0 100,990,000 0 0 0 0 Development Programme
    [Show full text]