Dodoma Aprili, 2019
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHESHIMIWA MHANDISI ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 DODOMA APRILI, 2019 HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHESHIMIWA MHANDISI ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuweka mezani Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai na kutuwezesha kukutana tena leo kujadili maendeleo ya shughuli zinazosimamiwa na sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa 1 hii kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Alli Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wao thabiti ambao umewezesha kutekelezwa kwa mafanikio makubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, ahadi za Viongozi pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi. Hakika Watanzania tunajivunia uongozi huu unaoacha alama kwa Taifa na tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuwajalia afya njema Viongozi hawa ili waendelee kutuongoza kuelekea kwenye Tanzania mpya ya uchumi wa kati na hali bora zaidi ya maisha kwa kila mwananchi. 4. Mheshimiwa Spika, kipekee namshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniamini na kuniteua kuongoza Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano. Jukumu hili ni kubwa, hivyo naamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali nitaweza kulitekeleza kikamilifu. Nichukue fursa hii kurejea ahadi 2 yangu kwa Mheshimiwa Rais na Watanzania wenzangu kuwa nitaendelea kutumia uwezo na maarifa kutekeleza majukumu yangu kwa weledi na uadilifu ili kuhakikisha kuwa Wizara yangu inatoa mchango unaotarajiwa katika kuiwezesha nchi yetu kuingia kwenye uchumi wa kati. 5. Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza na kumshukuru Waziri mwenzangu aliyenitangulia kuongoza Wizara hii, Mheshimiwa Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb) kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika sekta ninazozisimamia. Aidha, nawapongeza Waheshimiwa Wabunge wafuatao waliochaguliwa katika chaguzi ndogo zilizofanyika nchini katika mwaka 2018/19. Wabunge hao ni: Mheshimiwa Timotheo Paul Mzava, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini; Mheshimiwa Eng. Christopher Kajoro Chizza, Mbunge wa Jimbo la Buyungu; Mheshimiwa Pauline Phillipo Gekul, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini; Mheshimiwa James Kinyasi Milya, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro; Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Jimbo la Ukerewe; Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, Mbunge wa Jimbo la Serengeti; Mheshimiwa Abdallah Ally Mtolea, Mbunge wa Jimbo la Temeke; Mheshimiwa Mwita Mwikabe Waitara, Mbunge wa Jimbo 3 la Ukonga; Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka, Mbunge wa Jimbo la Liwale Mjini na Mheshimiwa Julius Kalanga Laizer, Mbunge wa Jimbo la Monduli. Ushindi walioupata umeonyesha imani kubwa waliyonayo wananchi wa majimbo hayo kwa Chama Cha Mapinduzi. Wizara yangu inawaahidi ushirikiano na kuwatakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yao. 6. Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kutoa pole kwako binafsi pamoja na Bunge lako tukufu kwa kuondokewa na aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini marehemu Stephen Hilary Ngonyani. Tunaendelea kuwaombea subira familia, wananchi wa Jimbo la Korogwe Vijijini pamoja na wote walioguswa na msiba huu. 7. Mheshimiwa Spika, vilevile, nitoe pole kwa wananchi walioathirika kwa kupoteza ndugu, mali au kupata majeraha kutokana na ajali za vyombo vya usafiri nchini. Kipekee natoa pole kwa waathirika wa ajali ya kivuko MV Nyerere iliyotokea katika Kisiwa cha Ukara, Wilaya ya Ukerewe siku ya Alhamisi tarehe 20 Septemba 2018. Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kudhibiti ajali za vyombo vya usafiri nchini ikiwa ni pamoja na kuandaa kanuni maalum kwa 4 ajili ya kuhakikisha usalama wa huduma za vivuko. Aidha, ili kuhakikisha kuwa huduma za vivuko katika visiwa hivyo inaendelea kutolewa, Wizara imepeleka kivuko mbadala wa MV Nyerere ambacho kinatoa huduma kwa sasa. Pia, Wizara kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme inaendelea na manunuzi ya kivuko kipya kitakachohudumia visiwa vya Bugolora na Ukara ili kuboresha huduma ya usafiri katika visiwa hivyo. 8. Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii adhimu kukupongeze wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika na Naibu Spika kwa kuliongoza Bunge hili Tukufu kwa hekima na busara. Uongozi wenu umewezesha Bunge kutimiza kikamilifu jukumu lake la kuisimamia na kuishauri Serikali. 9. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, lakini si kwa umuhimu, naomba kuwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Moshi Seleman Kakoso (Mb.) na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma (Mb.) kwa ushirikiano na ushauri waliotupa katika kuboresha utendaji wa Wizara yangu. Aidha, ninawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Miundombinu kwa kupitia Mpango na Makadirio ya 5 Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na kutoa ushauri na mapendekezo yaliyoniwezesha kuwasilisha Hoja hii mbele ya Bunge lako Tukufu. 10. Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea kuelezea kuhusu Wizara ninayoisimamia, nitoe pongezi zangu kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwa hotuba yake ambayo imefafanua kwa kina utekelezaji wa mipango na mikakati ya Serikali ya kuimarisha na kuboresha huduma za jamii kwa lengo la kupunguza kero za wananchi zinazotokana na umaskini, ujinga na maradhi. Aidha, nampongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa hotuba ya ujumla iliyofafanua utekelezaji wa sera na malengo ya uchumi na fedha, uimarishaji wa huduma za kijamii na kutoa malengo kwa mwaka 2019/2020. Naomba pia kuwapongeza Mawaziri wote waliotangulia kuwasilisha Hotuba zao hapa Bungeni. 11. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Wizara yangu, napenda kumpongeza Dkt. Agnes Lawrence Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa mjumbe wa kamati ya 6 Umoja wa Mataifa yenye wajumbe 10 itakayotoa ushauri wa masuala ya teknolojia (Technology Facilitation Mechanism - TFM) kwa Umoja huo. Kamati hiyo itasaidia pia katika masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika mchakato wa kufikia malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals – SDGs) ifikapo 2030. Uteuzi huu umeleta heshima kubwa kwa Taifa letu. Nimtakie kila la kheri katika kutekeleza majukumu yake na awe balozi mzuri wa nchi yetu katika ngazi hiyo ya Umoja wa Mataifa. Aidha, napenda kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Bwana Hamza Said Johari ambaye amechaguliwa bila kupingwa kuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Utoaji Huduma za Usafiri wa Anga na Uongozaji Ndege katika kanda ya Afrika. Hatua hii imeifanya Tanzania kuingia kwenye Kamati Kuu ya Shirikisho hilo ili kushiriki katika uandaaji wa sera na sheria mbalimbali zinazohusu usafiri wa anga. MAJUKUMU YA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO 12. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inajumuisha sekta kuu tatu ambazo ni Sekta ya Ujenzi, Sekta ya Uchukuzi na Sekta ya 7 Mawasiliano. 13. Mheshimiwa Spika, majukumu ya msingi ya Sekta ya Ujenzi ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Ujenzi (2003) pamoja na Sera ya Taifa ya Usalama Barabarani (2009); ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara, madaraja na vivuko; ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege; ujenzi na ukarabati wa nyumba na majengo ya Serikali; usimamizi wa masuala ya ufundi na umeme; usimamizi wa shughuli za ukandarasi, uhandisi, ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi; usimamizi wa maabara na vifaa vya ujenzi; usimamizi wa masuala ya usalama na mazingira katika Sekta; uboreshaji utendaji na uendelezaji wa watumishi wa Sekta na usimamizi wa majukumu ya taasisi zilizo chini ya Sekta. 14. Mheshimiwa Spika, Sekta ya Uchukuzi ina majukumu ya kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uchukuzi ya mwaka 2003; ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya reli na bandari; usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga, reli na bandari; utoaji wa leseni za usafirishaji; usalama katika usafirishaji; usimamizi wa huduma za hali ya hewa; kuendeleza rasilimali watu na kusimamia Taasisi na Mashirika ya Umma yaliyo chini ya Sekta ya Uchukuzi. 8 15. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Sekta ya Mawasiliano, majukumu yake ni pamoja na kusimamia Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003; na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016 na utekelezaji wake. Aidha, Sekta ya Mawasiliano ina dhamana ya kuhakikisha kuwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inachangia katika maendeleo ya nchi yetu, pamoja na usimamizi wa majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Mawasiliano. 16. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, naomba sasa kuwasilisha hotuba yangu ambayo imejikita